Rostam Aziz aandaa timu ya watetezi wa Dowans

EL+RA=UFISADI

Member
Jul 4, 2010
56
6
Nimepata taarifa leo kutoka kwa mtu aliye karibu na Rostam Aziz kuwa fisadi huyu aliyechonga dili zima la Richmond/Dowans sasa ameandaa timu ya viongozi mbali mbali wenye ushawishi kwenye jamii ambao wataibuka kwenye vyombo vya habari kuishinikiza serikali iwalipe Dowans.

Atatumia vyombo hivi kueneza propaganda yake: Tanzania Daima, Clouds FM, TBC1, Channel Ten, Mtanzania/Rai, Jambo Leo, Daily News, Habari Leo, Sauti Huru, etc.

Watu hawa wataibuka kuwapinga vikali Samuel Sitta na Harisson Mwakyembe na kutaka wafukuzwe kwenye uwaziri.

Pia wataitisha serikali kwa vitisho vya uwongo kuwa iwalipe Dowans haraka ama sivyo mali za Tanzania nje zitakamatwa, riba itaongezeka, eti Tanzania kamwe haiwezi kukwepa kuwalipa Dowans, wakati Mahakama Kuu ina uwezo kutupilia mbali hukumu ya ICC.

Wahariri wa vyombo hivyo tajwa vya habari wameshaandaliwa kutoa taarifa hizo prominently kwenye ukurasa wa mbele au kwenye vipindi maalumu vya TV na redio.

Watu hao mashuhuri wastaafu na wa sasa ni pamoja na wanasiasa, wanasheria, viongozi wa dini, waandishi wa habari, etc.

Tayari AG wa zamani, Jaji Mark Bomani, kashapewa mlungula na kuropoka hadharani kuunga mkono malipo haramu kwa Dowans.

Bomani has already been compromised na mafisadi. Wamemuweka pale Serengeti Breweries Limited kama mwenyekiti wa bodi na kumlipa senti zinazomfanya apoteze maadili. Serengeti Breweries inamilikiwa na mafisadi wa kihindi kina Mehta na wengine ambao waliiba pesa nyingi za Watanzania kupitia Benki Kuu (BoT).

Bomani kapewa rushwa na Rostam Aziz ili aibuke kutetea malipo kwa Dowans. Rostam sasa hivi anatoa pesa kwa watu ambao wanaonekana na influence kwenye jamii kushinikiza Dowans walipwe. Yupo radhi kutumia shilingi milioni 500 kugawa rushwa kwa viongozi hawa ili apate malipo ya shilingi bilioni 100.

Bado wataibuka viongozi wengine mashuhuri muda wowote sasa kuunga mkono malipo kwa Dowans ili kujaribu kuwachanganya wananchi.

Kuna jitihada kuwaweka sawa kina Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF, Hamad Rashid wa CUF, Zitto Kabwe wa Chadema (kashanunuliwa siku nyingi na Rostam), John Shibuda wa Chadema, James Mbatia wa NCCR Mageuzi, John Cheyo wa UDP, Augustino Mrema wa TLP na Christopher Mtikila wa DP watoke hadharani kuunga mkono malipo kwa Dowans.

Hapo tutajionea wazi jinsi viongozi wetu wanavyonunulika kirahisi kutokana na njaa kubwa waliyokuwa nayo na kukosa uzalendo kwa nchi yao wenyewe.

Stay tuned.... The Dowans circus is about to begin!
 
hii cinema sintataka inipite, hata umeme wa mgao nitanunua generator. Kwetu kijijini tutaandamana
 
wakiwa katikati ya safari (kutetea huu upuuzi) itisheni maandamano nchi nzima nipo tayari muda wowote hata kama nitaamshwa saa nane usiku nipo tayari jamani some people must be killed period ...
 
Hawezi kutumia Tanzania Daima, na wala wananchi hawatakubali huo ujinga waTZ washaelimishwa na Chadema vyakutosha.
 
MWEEEE NIMECHOKA NA HAYA MADUDU YA HAWA WATU MIMI!
kweli pesa ni sabuni ya roho.
 
Hivi kweli hii sio "opinionated opinion"? Inawezekana kweli mtoa hoja kaambiwa kwamba Rostam anapanga kuunda timu ya kutetea DOWANS lakini sidhani kaambiwa ni watu na vyombo gani atavitumia kufanya shuguli hii. Mtoa hoja kutaja majina ni kwenda mbali. Hii waadishi wanaita opinionated opinion.
 
Huyo Rostam amedekezwa sana na vibaraka hapa Tanzania wakati si Mtanzania.
Enough is enough..huyu inatakiwa apotezwe katika ramani ya Tanzania.. thro any means available under the sun!!
 
safi sana!!! nadhani hapo ndiyo tutawajua waukweli!!! Sitta, mwakyembe! rukeni nje njooni chadema tubadili upepo nchi!

kweli Mungui akiishakiri amechoka basi ndio siku ya anguko! STAY TUNED!
 
Tanzania Daima?
A typo or what?

It could be true. Tanzania Daima imekuwa ikitumiwa sana kuwakosha kina Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge na kuwaandika vibaya kina Samuel Sitta na Harisson Mwakyembe. Hii inatokana na ukweli kuwa mhariri wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, yuko kwenye payroll ya Edward Lowassa na Rostam Aziz.
 
Rostam hata amshushe Yesu kumtetea watanzania hawatakubali. Amejaribu advocate wake kachemsha, amejaribu ngeleja somo halijaeleweka ndio kwanza moto ukashika kasi, kaja bomani kushusha hadhi yake watanzania kupitia askofu mkuu wa moravian wakaponda, sasa sijui aseme nani -watanzania tutaingia mtaani kuwafukuza rostam na mafisadi wenzake kuikimbia nchi kama tunisia.

Kwa hali hii ngumu itatokea tuu ya Tunisia subiri uone na hii style mpya ya polisi kuua kwa kuilinda serikali subiri utaona moto wake. Hata ashuke nani - hakuna mtu wa kufumbia macho shetani fisadi ra na kundi lake enough is enough
 
eeeh!!!! Hizi habari za kiintelijensia zimfikie IGP mapema ili atume vijana wazuie hiyo timu ya watetezi kuibuka, maana watasababisha uvunjifu wa amani.
 
Ebu aje anigawie na mimi hizo fedha nianze kazi ya kumtetea... tumbaf kabisa.
yaani tunafanywa kama wanasesere vile, kana kwamba hatuna akili
 
Kwamba, litatokea jaribio la kulazimisha au kuhalalisha malipo ya Dowans tena kwa nguvu hilo halina shaka. Nadhani sehemu imesahauliwa ni Ikulu.

Kwa sababu, hivi vingine ni kama vikasuku; Ikulu wakishasema "hatuwezi kukwepa kulipa, Watanzania tuheshimu sheria za kimataifa" ndio mchezo kwishnei hao wengine wote (sijui kama ni wote kihivyo) watajipanga mstari kuimba wimbo wa "tuwalipe Dowans, yoyo mama!! tuwalipe haraka papapapappapa"!

Si mnakumbuka Ikulu walivyogeuza na kusema "Tunataka Katiba Mpya na sisi" na mara moja wote wakageuka na kusema "serikali inasikiliza"?
 
Yaani kumbe sinema ndo kwanza imeanza!!!

These guys are capable of anything to achieve what they want.
Ila safari hii tunao hata wakilipana hawatakula kwa furaha, kilio cha watz hakitawaacha wakae na amani
 
Back
Top Bottom