Rostam Aziz aachia ngazi CCM

Hii ya kuachia nyadhifa haitoshi baada ya hapa inabidi akamatwe awekwe ndani na kufunguliwa mashataka mana makosa yake yapo wazi,chama gani hiki kimejaa Mijizi tuu,hivi nyie mnaoshabikia hiki hamuoni haya au tu kwa vile chama cha Magamba kinawaweka mjini? hebu kuweni tujadilipo mambo yenye manufaa kwa waTz
 
Mbona kama vile maskio yangu hayaoni vizuri na macho yangu hayasikii uzuri? hebu naombeni miwani hapo jamani.....hii sura si ipo bungeni leo kweli? Bunge la wanawake na vijanaume wa CCM wasio na fikra pevu..........ushabiki wa kitoto tu.
 
Katua na ndege ya kukodi uwanja wa Lusu, Nzega majira ya saa tano asubuhi.Hayuko bungeni kama mwanajanvi alivosema.
Kaja na waandishi wa habari katika msafara wake. Nawakilisha.
 
Bado haitoshi..achunguzwe akipatikana na wizi wa EPA wa kagoda afilisiwe na afukuzwe arudik wao Irani huyu jamaa mafia sana kaiba mpaka kaona sasa imetosha..yani wewe rostam natamani uje arusha tukukomeshe
 
Wandugu,

Kuna habari nimezipata Hivi sasa kuwa Mh. Rostam Aziz ameachia ngazi CCM pamoja na Ubunge .... Mwenye Taarifa Zaidi atusaidie Jamani!
 
Wanajamvi:

Habari za kuaminika ni kwamba Rostam Azizi asubuhi hii atatangaza kujivua gamba rasmi katika mkutano na waandishi haabari Tabora. Anajiuzulu nyadhifa zote nakubakia na kadi ya CCM tu.

Kwa Kosa Gani?
 
Hii ya kuachia nyadhifa haitoshi baada ya hapa inabidi akamatwe awekwe ndani na kufunguliwa mashataka mana makosa yake yapo wazi,chama gani hiki kimejaa Mijizi tuu,hivi nyie mnaoshabikia hiki hamuoni haya au tu kwa vile chama cha Magamba kinawaweka mjini? hebu kuweni tujadilipo mambo yenye manufaa kwa waTz
Huyu jamaa tumemlea sana, na aombe mungu raia wa tanzania ni wapenda amani na tumemvumilia tumechoka. Sasa kesha taifisha kile alichokitaka sasa anataka kuondoka. Hatuhitaji hata kusikia sauti yake akatangazie kujiuzulu huko kwao uarabuni. Sasa hii fimbo ya huyu jamaa imetushikisha adabu ni afadhali angekuwa mtanzania mwenzetu angesaidia hata watanzania wawili watatu. Jamaa anaondoka na kitita chote alichovuna hapa Tz anakwenda kuwanufaisha waliopo mbali sisi tunabaki tukitupiana maneno ya umasikini bila jibu. Nenda, nenda, nenda baba.....! lakini kumbuka ni mali ya watu masikini. Waliokubeba ni wachache walioamua kuiuza nchi popote utakapo kuwa dhamira itakusuta tu kwa taifa hili masikini.
 
Nyadhifa zipi za Rostam kujivua???....... Labda UBUNGE WA IGUNGA...anything else ni uongo mtupu na hapo ndipo CCM watakuwa wameharibu sana sana sana sana!!!!!
Wanajamvi:

Habari za kuaminika ni kwamba Rostam Azizi asubuhi hii atatangaza kujivua gamba rasmi katika mkutano na waandishi haabari Tabora. Anajiuzulu nyadhifa zote nakubakia na kadi ya CCM tu.
 
Wana member kuna tetesi kuwa R.A kaingia chumba cha habari,HABARI CORP na kutangaza kujivua nyadhifa zake;ubunge na ujumbe Ccm,kuna chanzo kimebainisha.nami naendelea kutafuta ukweli zaidi hasa kwa kuanzia bungen iwapo leo amehudhuria ama la? NB Tetesi ni mwanzo wa kuchimbua habari yenyewe.
 
Makilikili show

images
 
Back
Top Bottom