Rostam Aziz aachia ngazi CCM

Rostam Aziz aachia ngazi CCM

makamba alishatangulia kuwaandalia makao...ili atakapokuwa nao wawepo
 
Sizitaki mbichi hizi, Sungura akagumia,
Naona nafanya kazi, bila faida kujua,
Yakamtoka machozi, matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura Nakuambia.

So sweet,umenikumbusha mbali sana,maneno hayo utayapata kupitia msemo huu SIASA UCHWALA [GUTTER POLITICS]

Maana ya kuwa baada ya kuambiwa TUNAOMBA JEZI ZETU,ulipokuwa unazikabidhi na nyuma yake kuna kawimbo kazuri kama JUMA NA ROZA wa zama hizo.
 
Nimekuwa msomaji mzuri wa gazeti la Mwanahalisi kwa kupindi cha miaka miwili sasa hizi, kumbukumbu zangu kama ziko sawa sikumbuki siku ambayo nimenunua gazeti la Mwanahali likakosa habari ya Rostam Aziz. Kila wiki lazima kuna picha au story ya Rostam tena front page, nahakika gazeti hili limechangia kwa kiasi kikubwa Rostam kujivua gamba.
 
ili asiwe mbunge ni lazima arudishe na kada ya chama......jamaa bado mbunge huyu
 
Rosta amesema mengi sana kwa wazee wake wakati akitangaza kuachia nyadhifa zote ndani ya chama hiki kichovu.
Niliona kwenye TV watu (wazee wake) wengine wakilia lada kwa kumuonea huruma.
Napenda niulize hivi hasa ni wanani walikuwa wakilia? Hivi walikuwa wanawakilisha watu wote wa Igunga? Mie naona waliokuwepo ni wale wazee ambao kwa kawaida wana ukaribu fulani na mbunge na wapiga debe, huwa wanaambulia makombo ya hawa mafisadi, sasa wameona makombo yanaondoka wanamwaga machozi. Kama ni jitihada zao na mbunge wao zilizowapa maendeleo kwani mbunge mwingine yeyote atakayekuja hawataweza kuleta maendeleo?
Ati amejenga shule kila kata na vituo bya afya kila kijiji, hivi ni nani anaweza kutuambia alitumia fedha halali za biashara zake au ni fedha haramu za ufisadi zilizotumika kufanya hayo. Kama ni fedha halali si bado ataendelea na bishara zake? Na ataendelea kuwasaidia hata kama si mbunge kwani si anawapenda sana wazee wake wa Igunga? Hivyo waache unafiki wa kulia wachape kazi, wanacholilia si kingine ni mabaki ya Rostam ambayo ataondoka nayo.
Sasa Rostam ashikwe na afikishwe kwenye vyombo vya sheria kwa ufisadi.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"][/TD]
[TD="class: buttonheading"]Igunga yazizima, Rostam kujiuzulu
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Wednesday, 13 July 2011 20:57
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

Baada ya Rostam kumaliza kusoma hotuba, Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nzega, Daudi Ngutu, na Katibu wa Uchumi Kata ya Igoweko, Athuman Kanyama, walizirai na kupandishwa katika gari la Halmashauri ya kupelekwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya.

Wakati Rostam akiwa njiani kuondoka kwenda Dar es Salaam wanachama wengine ambao ni Katibu mwenezi kata ya Chabutwa, Athumani Mihayo, Catherine Mabula na Zainabu Athumani walizirai.

Viongozi wa CCM waliokuwapo
Viongozi wa CCM wengi kutoka wilaya zote za mkoa wa Tabora walihudhuria ambao ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Igunga, Katibu Tawala wa Wilaya, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tabora, wajumbe wa kamati ya siasa wa wilaya na Baraza la Wazee la Wilaya na Mbunge wa Viti Maalumu, Munde Tambwe


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Dah alikuwa na listi ndefu sana ya anaowalipa
 
well well well...............sio mbaya sana...mnajitahidi.......right there..CCM thats ya bargaining chip........However, hatua zaidi zahitajika......
 
Sizitaki mbichi hizi, Sungura akagumia,
Naona nafanya kazi, bila faida kujua,
Yakamtoka machozi, matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura Nakuambia.

karuka tena karuka, matunda akarukia,
mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia,
penye miti akatoka, pembeni akasogea,
pembeni akasogea, sungura nakuambia!
 
Sasa ni wakati mzuri wa kufuatilia tuhuma mbalimbali zinazomhusu, kwani sasa hivi hana kinga iliyokuwa inamsaidia
 
- Next stop kwenye Sheria!, Bravo Nape!

Willie @ NYC, USA.

kaka yangu, unasema bravo nape kwaa kitu gani? tarumbeta na mpuliza tarumbeta nani apewe bravo? in my opinion, simply say bravo JK kwani nape kwa uwezo wake hawezi lolote!
 
bado kuna mengi sana ya kufanya....mengi mno ya kurekebisha. mi bado sijaridhika mpaka kieleweke, kura yangu 2015 inakwenda CHADEMAAAAAAA!!!!!!!!
 
Hao akina baba na kina mama walio kuwa wanalia na kumwaga chozi huyu Rostam alikuwa anawalelea familia zao?
 
Na Kikwete ataachia lini ngazi?Huyu ndiye chanzo cha matatizo yote kwa uchu wake wa kutaka kwenda ikulu.
 
Kwa upande mmoja inaonekana Rostam Aziz ni "sacrificial lamb". Inabidi tufikirie kapata hasara gani kwa kujiuzulu? Bado ni tajiri mkubwa. Bado ana connections za kisiasa na access kwa viongozi wakuu wa nchi. Inawezekana kapewa kitu mpaka aka kubali kujiuzulu. Kapata hasara gani kwa kuachia nyadhifa hizo? Kiukweli ni haja pata hasara yoyote.Kwa upande wa pili hili ni jambo la kihistoria. Tunaweza kusema ni kiongozi wa kwanza kujiuzulu kutokana na public pressure. Nani alitegemea "untouchable" kama Rostam Aziz angejiuzulu? Pia hii ina wapa CCM jeuri ya kuongea. Watasema zile siku 90 zimeisha na magamba yameanza kujivua. CCM itatumia hii kama fursa ya kipropaganda kwamba kweli wapo serious.Ila swali la muhimu zaidi kujiuliza ni je is this too little to late? Je bado wanaweza kuinusuru chama? Kujiuzulu RA kunaisaidia vipi CCM kwa sasa? Time will tell.
Mkuu Rostam hajasema anajivua gamba,bali amechoshwa na 'siasa uchwara' ndani ya CCM!ina maana hapa ukifikiria kwa umakini unaweza kujua moja kwa moja anayesemwa hapa ni Nape + Mkama hasa kwa kupenda siasa za uropokaji!angalia magazeti ya Rostam yanavyomponda vuvuzela Nape siku hizi.
 
Mwalimu alisema kuwa na MALI ilikuwa inamwondolea mtu sifa ya kuwa mgombea wa TANU/CCM. Tukampuuza kama kawaida yetu.
 
kwa wana igunga tunasikitika kuachia ngazi kwa rostam, hatutapata mbunge kama yeye, kaleta maendeleo makubwa sana, hata kama wanasema ni fisadi, ufisadi wake ni mzuri kwetu maana zahanati tunazo, shule, umeme, tutaendelea kumpenda na kumuenzi. Ila hasira kali inamsubiri nape, asithubutu kuja igunga, wananchi tumelia sana sana na kusikitishwa kwa kuachia ubunge, nape hasira zetu zinakusubiri

Mkuu sawa mna zahanati, shule, umeme, mtaendelea kumpenda lakini wana Igunga kumbukeni maendeleo mliyo nayo ni matokeo ya ufisadi katika kagoda, meremeta, richmond, rada, dowans na uchafu mwingine ambao mbunge wenu ameuasisi. Ni kushukuru tu kuwa sehemu ya hizo fedha walizoiba angalao amewagawia kidogo ninyi watanganyika wenzetu wa Igunga lakini maendeleo hayo kiduchu hayalingani na matrilion waliyoiba na kupeleka kwenye account zao huko uingereza, india, switzerland na kwingineko walikoweka vijisenti vyao pamoja na magorofa waliyo nayo Dar. Mahela hayo yangetumika yote hapa nchini yangeleta maendeleo sio Igunga tu bali nchi nzima. Hapo kaachia ngazi mmezimia sijui itakuwaje atakapofikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayomsubiri na hasa pale atakapokwenda jela? Kazi kwenu poleni
 
hawa jamaa hata hatuwaelewi, huyu anamsema huyu, kama vipi watoke tu wote tuitishe uchaguzi upya, darn t
 
Back
Top Bottom