Rostam aishukia Serikali, aitaka iache kupitisha sheria kandamizi

Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,323
18,794
Aliyekuwa Mbunge wa Igunga kupitia CCM na baadae kujiuzulu, Rostam Aziz ameishukia vibaya Serikali ya CCM akiitaka iache kukandamiza wananchi na vyombo vya habari.

Bwana Rostam alikuwa akiongea leo Serena Hotel, Dar ambapo wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) waliongea na waandishi kutolea ufafanuzi kasoro walizobaini katika muswada wa Haki ya Kupata Habari (Access to Information Bill)

Rostam ambaye ni mmiliki wa kampuni ya New Habari Corporation amelitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokubali kuujadili muswada huo kwakuwa unaua uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa wananchi kupata habari.

Naye Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi ameungana na Bwana Rostam kuitaka Serikali kuuondoa muswada huo Bungeni ili kwanza wadau wawasilishe mapendekezo ya marekebisho.

Mkurugenzi wa Jamii Media, ambao ni waendeshaji wa JamiiForums ndugu Maxence Melo akiongea katika mkutano huo, amesema Muswada badala ya kutoa haki ya kupata Habari, unageuka kuwa kama kupata Taarifa muhimu toka kwenye taasisi za umma na mamlaka husika ni hisani na si haki ya msingi.

 
Last edited by a moderator:
chombo gani kiliwatia hatiani au wewe ni mshabiki wa timu usiejua wachezaji.
 
Hivi watu wngine ni wajinga sana mtu analeta mada mjinga anaanza kumuingiza lowassa. Mheshimiwa Lowassa anaingiaje. Anawauma sana mtakufa mwaka huu. Kama humtaki lowassa kula vyupa ukufe
 
na ukizingatia vyombo vya habari vimeonyesha rahisi kutumika hususani itv...ina ile sheria ya kujiunga tbc saa mbili usiku ipite kabisa
 
Ukiona hivyo ujue masrahi ya mhusika yameguswa, Rostamu hatetei sheria za wala rushwa ziongezwe ukali na takukuru ipewe meno ila anaona sheria ya vyombo vya habari. Kama anaona masharti ni magumu ruksa ahamishe Mali zake kwasababu mtu mwenyewe hata si ndugu yetu alafu eti atupangie jinsi ya kuendesha nchi yetu, agenda uingereza akaanzishe media huko huko ...mwizi mkubwa huyu.
 
Muswada ukipitishwa basi mimi nitapunzika kidogo hapa jukwaani mpaka uchaguzi upite.
 
Hivi watu wngine ni wajinga sana mtu analeta mada mjinga anaanza kumuingiza lowassa. Mheshimiwa Lowassa anaingiaje. Anawauma sana mtakufa mwaka huu. Kama humtaki lowassa kula vyupa ukufe

Hamna Rostam Hamna Lowassa. Ukisikia Lowassa anatafuta Urais jua anayeutaka Urais huo ni Rostam.
Hawa wawili wameunganishwa na ufisadi. Wakisema Richmond ni Rostam jua ni Lowassa mwenye Richmond.

Wapo pamoja ktk Vodacom nk. Vodacom walau kwa Siku mtu lazima kupitia voda lazima wamkate walau shilingi 50,000/ hizi ni za kampaini ya Lowassa.
 
Muswada huo usipite mpaka wadau wa habari wapekele mapendekezo yao. Wanagusa nyanja muhimu sana ya habari. Watanzania tusiwe wajinga.

Kuna mtu hapo amesema kuwa muswada unataka taarifa ya habari itangaze tbc tu kisha vituo vingine vijiunge saa mbili.

Huo si upuuzi tu. Wanataka wawe wanapiga pesa kwenye taasisi za umma kisha wananchi tusijue.
 
Nimeshangaa kumuona leo anaiponda sheria ya kubana uhuru wa mitandao as if yeye serikali haijua kabisa wala system nzima iliyofikiri hayo haijui.

cha kunishangaza mtu huyu kaibukia nchini mwaka huu wa uchaguzi,kageuka mwanaharakati kutetea watanzania.

kwa nini asingempigia simu mkuu wa nchi na spika ambao ni chama chake wampe sababu za kufika hapa na kama anawazo aliwasilishe tu huko wafikirie upya?

au ndio sasa kawa na uchungu sana na wananchi?
 
Back
Top Bottom