Preta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 24,323
- 18,804
Aliyekuwa Mbunge wa Igunga kupitia CCM na baadae kujiuzulu, Rostam Aziz ameishukia vibaya Serikali ya CCM akiitaka iache kukandamiza wananchi na vyombo vya habari.
Bwana Rostam alikuwa akiongea leo Serena Hotel, Dar ambapo wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) waliongea na waandishi kutolea ufafanuzi kasoro walizobaini katika muswada wa Haki ya Kupata Habari (Access to Information Bill)
Rostam ambaye ni mmiliki wa kampuni ya New Habari Corporation amelitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokubali kuujadili muswada huo kwakuwa unaua uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa wananchi kupata habari.
Naye Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi ameungana na Bwana Rostam kuitaka Serikali kuuondoa muswada huo Bungeni ili kwanza wadau wawasilishe mapendekezo ya marekebisho.
Mkurugenzi wa Jamii Media, ambao ni waendeshaji wa JamiiForums ndugu Maxence Melo akiongea katika mkutano huo, amesema Muswada badala ya kutoa haki ya kupata Habari, unageuka kuwa kama kupata Taarifa muhimu toka kwenye taasisi za umma na mamlaka husika ni hisani na si haki ya msingi.

Last edited by a moderator: