Rosemary Mwakitwange ampinga Sophia Simba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rosemary Mwakitwange ampinga Sophia Simba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by samirnasri, Mar 15, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Rosemary Mwakitwange amewasihi wanawake kushiriki maandamano ya amani kwa kuwa katiba inaruhusu. Amewaomba wanawake kushiriki katika siasa kwa kuwa maamuzi ya kisiasa yana yanagusa nyanja zote za maisha.

  Zaidi ya hapo amesema wanawake hawapaswi kumsikiliza mtu yeyote awe mwanaume au mwanamke mwenzao atakaye washauri wasishiriki kwenye maandamano au siasa.

  Siku kadhaa zilizopita Sophia Simba alinukuliwa akiwashauri wanawake wasiandamane kwa kuwa wao wana kazi nyingi hivyo wawaachie wanaume ambao hawana kazi nyingi.

  Source: Wanawake live EATV
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  ni sahihi kabisa mama rosemary mwakitwange yuko right, watu wote wanawake, wanaume,vijana, wanayo haki ya kushiriki maandamano na kuhudhuria mikutano ya siasa kadiri utashi wao unavowatuma maadamu tu wasivunje sheria. mama simba sijui marufuku yake kwa akina mama ilimaanisha nn.
   
 3. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,235
  Trophy Points: 280
  Si kushiriki na kudhuria tu bali ikibidi hata kumwajibisha na kusitisha ajira ya yule waliyemwajiri kusimamia rasilimali zao, na ikilazimu hata kabla ya wakati muafaka unaokubalika kikatiba.

  Ikiwa tunataka kubadili sheria ya manunuzi ya umma ili kuibeba Dowans, kwanini tusibadili katiba na sheria za nchi ili kuiokoa nchi!!!!!! Tukishindwa sana tutumia ile hukumu ya umma.......Wananchi wenye hasira kali.....
   
 4. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sofia simba anatakiwa afanyiwe psychotherapy.
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Maneno ya dada rose yanamashiko, yanaelimisha na kuwakumbusha wamama kuondokana na fikra za kupendelewa, wawajibike kwa mujibu wa katiba.
   
 6. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Si khudhuria na kushiriki bali ni lazima wahakikishe maandamano hayo yanafuata taratibu zote za kisheria katika kuitishwa kwake na kusiwepo na chembe chembe za uvunjifu wa amani na katiba ya nchi.
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mtu mmoja aliniambia kwamba sehemu kubwa sana ya wanawake walioolewa wanaongea maneno yenye busara sana, lakini wasioolewa ni chukizo kila wanapokuwapo. Kumbe nikatambua mwanaume ni dawa muhimu sana ya utulivu wa mwanamke. Heri Simba angefanya bidii kupata mume atakayempa dose kila inapohitajika, sio kutegemea dozi ya kuipata kwa kubahatisha.
   
 8. T

  Tata JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 644
  Trophy Points: 280
  Angewashauri pia kuwa waache kupiga kura kwa kuangalia sura ya mgombea baada ya kupokea vijizawadi vya kanga, chumvi, Tshirt na kofia. Angewashauri wajitokeze kupigia kinamama wenzao ili kuwe na wawakilishi wengi wanawake kutoka majimboni. Labda mambo yatabadilika kwani wanaume wameshatekwa na ufisadi na wameshindwa uongozi. Mwisho angewakumbusha kina mama wanaweza bila ya kuwezeshwa kwa sababu huku kuwezeshwa ndio kunawaweka nyuma na kuwafanya watumike kama vyombo vya kuwaweka viongozi mafisadi madarakani.
   
 9. M

  Marytina JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  yes!Rose amesoma na kuelimika.
  Appreciated
   
 10. K

  Kana Amuchi Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  rosemary ni mpiganaji. ana upeo mkubwa ndio maana ana uthubutu wa kuongea haya. na siku zote siyo mtu anaesubiri kubebwa, na huwa hayumbishwi. wale wanaobebwa bebwa usishangae hata wakampinga!!
   
 11. S

  Speedo Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 13
  Sophia Simba huwa simwelewi.
  Katika matukio mengi akiwa anaongea huwezi mtofautisha na mwanamama (baadhi) wa huku uswazi kwetu ambaye elimu yake kuuubwa ni std 7 alafu hana exposure.

  Juma lililopita alikuwa anahojiwa na BBC kuhusu siku ya wanawake....... AIBU TUPU!!!!!!

  Hivi hao wanaomwajiri wanatumia kigezo gani??????????????
  Au mimi nakosea labda utendaji ni mzuri kuliko kuelezea jambo??????

  Nijulisheni wanaJF mnaomfahamu zaidi ili nijiridhishe au nibadili mtazamo wangu kwake kuwa ni "Kilaza" anayebebwa kwa jambo ambalo anafanya au aliwahi kufanya.

  Nawasilisha
   
 12. N

  Ntandalilo Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi ya Tanzania iatjengwa na watanzania wenyewe pasipo kubagua huyu ni mwanamke na huyu ni mwanaume!!! kama maandamano yanahusu kujenga nchi yetu au yana manufaa kwa nchi yetu wote tutasimama........ Sidhani kama zama na nyakati hizi bado kuna wanawake wanamsikiliza Sophia Simba ( mropokaji) tangia nimemfahamu huyu mama sijawahi kusikia pointi iliyoongelewa naye. Nawahurumia sana watoto wake coz siju wanajifunza nini kutoka kwake zaidi ya ushangingi wa mjini!!! ( samahani sana kwa lugha kali) ni uchungu tu.................
   
 13. alberaps

  alberaps JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,450
  Likes Received: 804
  Trophy Points: 280

  amani ipi tuliyonayo............

  Katiba ipi tuliyonayo............
   
 14. M

  Maimai Senior Member

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  babu wa Loliondo kapooza machungu yetu yote ya ukali wa maisha.... du ama kweli bongo.. vyombo vya habari navyo vimeacha kutukumbusha machungu ya kiuchumi na kuhamia Loliondo.. Jamani Jamani jamani.. JK anakula shushu tu nje watu wake tunakufa.. this make no fukin sense......
   
 15. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hiyo hiyo unayoijua wewe na kuifuata hata leo hii inakuongoza.
   
 16. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Crap..Katiba ya ccm..ya chama kimoja.:A S 13::A S 13::A S 13:
   
 17. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndio inayokuongoza na lazima uifuate utake usitake.

  Kinyume chake muulize Godbless Lema wa Arusha atakueleza.
   
 18. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,235
  Trophy Points: 280
  Siku moja yatatokea kwako, kama siyo kwako kwa mkeo, mama au baba yako kisha tutawafuata kuwauliza.

  Kwa haya ya Arusha, hatuna haja ya kumuuliza Lema kwani alishatueleza kwa maandishi kupitia Bungeni
   
 19. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,550
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  Mimi natafuta mke wa pili, ani PM tupange
   
 20. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  samaki mkunje angali mbichi akisha kauka hakunjiki
   
Loading...