Rose Mhando: Nilitekwa msituni nifanyiwe ngono

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
2,009
2,000
Stori: Erick Evarist na Imelda Mtema

NYOTA wa Nyimbo za Injili Bongo, Rose Mhando (pichani)amefungukia eneo fupi la maisha yake magumu ambapo alisema amewahi kutekwa kwa bastola na mwanaume mmoja, akampeleka msituni ambako alimlazimisha kuwa naye kimapenzi lakini akadunda.

MSIKIE MWENYEWE

"Dunia ina mambo mengi sana ndugu zanguni, wengine wema, wengine waovu. Mimi nakumbuka siku moja kuna mwanaume ambaye nilikuwa na ukaribu naye."Huyu bwana, ana jina kubwa sana Dodoma. Alinichukua kwenye gari kwa ajili ya kunisaidia mambo fulani maana alikuwa ananisaidia katika kazi zangu.

"Nilishangaa kumuona anapeleka gari nje ya mji, nikamuuliza tunakwenda wapi, akasema tulia utajua. "Sikuwa nimemuwazia ubaya, hivyo nilitulia lakini matokeo yake akanipeleka hadi porini ambako alikutana na watu wengine, naamini walikuwa wasaidizi wake.

"Naamini ulikuwa mpango kabambe. Wale watu wakaniweka chini ya ulinzi na kunifunga kamba kisha wakanioneshea mtutu wa bastola," alisema Rose huku akisisitiza ni tukio ambalo hawezi kulisahau.

AMBIWA KISA
Rose aliendelea kudai kuwa, mpaka hapo hakuwa amejua kisa lakini akiwa amekutana macho na mdomo wa bastola. Ndipo akaambiwa kuwa, anatakiwa kuwa chini ya himaya ya kimapenzi ya mwanaume huyo la sivyo siku zake zilikuwa zinahesabika."

Niliona ni jambo la ajabu, kwani mwanaume kumtaka mwanamke ni mpaka silaha na kutishia kuua?" alihoji staa huyo mkubwa wa gospo.

AKUBALI YAISHE
Rose aliendelea: "Kwa pale nilikubali kwamba niko tayari kuwa mtu wake lakini nikamwambia tukirudi mjini tukae tuongee kwa kirefu, akakubali."

Tulifika mjini nikiwa najisikia kuumwa sana maana wale wasaizidi wake walikuwa wakinisulubu kwa kunipigapiga pia ile kamba niliyofungwa ilichangia kunipa maumivu makali."

AKACHA KUKUTANA
Rose alisema walipofika mjini walipanga kukutana baadaye ili wayaongee lakini yeye akakacha kutokea kwenye kikao, hivyo akaenda polisi (hakutaja kituo) ambako alifungua jalada la uchunguzi."

Nimekuwa nikisita kumwanika kwa jina huyo mwanaume kwani yupo na ni adui yangu mkubwa. Naishi kwa tahadhari kubwa sana, naamini siku nikimtaja ataniua.

"Mbaya zaidi najua mambo yake mengi, mabaya kwa mazuri lakini mabaya ni mengi sana kwani hata wakati ananisaidia kuhusu kazi zangu alinitenda maovu mengi, nimemwachia Mungu."

KWA NINI AMEAMUA KUSEMA?
"Nimeamua kusema ili moyo wangu uwe mweupe, nimekuwa nikiwaza siku hadi siku kuhusu lile tukio, ni kumbukumbu mbaya sana kwangu, lakini kwa kukiri kwangu huku sasa nitakuwa na amani."
Amani: "Polisi walichukua uamuzi gani?"

Rose: "Walisema wanafanya uchunguzi wa kina lakini sijawahi kuambiwa walifikia wapi!"
Amani: "Baada ya kuingia mitini jamaa hajawahi kukutumia meseji ya kukutishia maisha?"
Rose: "Hapana, alijua nimekwenda polisi."

Amani: "Unadhani ni kwa nini alikuteka hadi msituni, kwa nini asikwambie tu kawaida mjini?"
Rose: "Alishawahi kuanza hizo dalili za kunitaka nikamwonesha sitaki, nilimwambia nataka kazi kwake na si mapenzi. Mimi najua fedha ndiyo jeuri yake."

Amani: "Ana familia?"

Rose: "Ana mke na watoto."
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alipotafutwa hakuweza kupatikana kuzungumzia ishu hiyo.

SOURCE: globalpublishers.info
 

belie

JF-Expert Member
Sep 19, 2014
387
195
mmmh! wanatakana hao, si bure! kwann asimtaje.... mfyuuuu
 

belie

JF-Expert Member
Sep 19, 2014
387
195
Huyo mwanaume atakua mchaga tu,zama za kutumie bunduk kupata Papuchi sio za sasa

hakuna mwanaume anaejua kubembeleza kama mchaga, wakat anakutaka, ila ukimkubalia sasa afu umletee ushenz ndo mnashikiana visu na mtutu!
 

MFUKUZI

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
934
1,000
Hana lolote,, anatafuta huruma juu ya kashfa ya uteja.. Huyu dada madawa yatamuumbua vibaya, anamchezea Mungu!!!
 

yaliyomoyamo

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
516
500
aiseee! kule porini alinusurika kweli..?! asione aibu aseme tu kama jamaa alishapita mbona mambo yakawaida tu?! teh! teh
 

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
2,009
2,000
NI MWANAUME GANI HUYO? amtaje, labda tuangalie ni wanaume wepi waliofanya kazi na Rose anaosema walikuwa wanamsaidia, tukipata list ya waliokuwa wanafanya naye kazi ndio tutascreen na kupata uyo mwanaume ni yupi...rose anasema anaogopa kumtaja atamuua ila kesi alisharipoti polisi dodoma.polisi dodoma wanalijua jina la huyo mtu.baya lolote likimpata rose, mwanauem huyo wanaye...
 

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,629
2,000
Lazima mtu hapo alilamba tu, haiwezekani kabisaaaaaa labda story isiwe ya ukweli
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom