Rose Garden: Bar inayopendwa na Majasusi

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Hii Bar ipo Mikocheni B, (sina uhakika sana kwa sababu sina uenyeji na jiji la Dar)

Mara ya kwanza kufika kwenye hiyo bar nilipelekwa na girlfriend wangu siku ya pili baada ya kuwasili kutoka Australia.

Kipindi hicho ilikuwa mida ya jioni na mwenyeji wangu alinionya kuwa mwangalifu sana na kauli siku nikienda hapo peke yangu, nilipomuuliza, niwe mwangalifu kwa kauli zipi? Akanijibu, nisijaribu kuwa na kauli za kuisema vibaya serikali, kwa maana ya kuikosoa,kwa sababu imeshatokea watu kudakwa hapo bar, yaani unatoka kwenda chooni huko huko hurudi tena, wanakuona nyumbani baada ya siku 5 ukiwa umepigika hasa.

Enzi zile ilikuwa ni awamu ya nne,nimekaa nikajiuliza Kama awamu ya nne ilikuwa hivyo, je? Hali ikoje kwa awamu hii ya tano?
Ukienda umeenda jumla, hakuna kurudi.

RIP Ben Saanane
RIP Kanguye
RIP Azori Gwanda
RIP my best friend Eric, ulipotelea Rose Garden baada ya kuanza kukosoa serikali.
 
Mikocheni B na Rose Garden ni vitu tofauti. Ile iko barabara ya kwenda kwa Nyerere. Bora useme iko Mikocheni.
 
Duh hio bar sio kabisa..
Maana bia ya kwanza na pili watu tunaanza kuongea story za kawaida tu

Bia ya tatu na nne lugha inabadilika kidogo kingereza kinachanganywa.

Bia ya tano na sita tunaanza kuongelea siasa nyepesi za jimboni na mikoani.

Bia ya saba na nane tunaanza kuongea siasa konki za kitaifa na uchambuzi wa kiintelijensia (hapa kila mtu anakuwa agent wa kitengo)

Bia ya tisa na kumi ni kuongea siaza za kimataifa...hapa wakina carl max wanachambuliwa kama tunachambua kikosi cha simba na yanga..

Bia ya kumi na moja tunainywa njiani wakati wa kurudi hom.
 
42 Reactions
Reply
Back
Top Bottom