KWELI Roque Jose Florencio alikuwa Mtumwa aliyetumika kama dume la mbegu kuzalisha watumwa wenye nguvu

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Inadaiwa huyu jamaa bhana enzi za utumwa, alitumika na masta wake kama mbegu ya kuzalisha watumwa wenye nguvu. Inadaiwa kutokana na kuwa na nguvu, umbo maridadi na urefu wa futi 7 hivyo masta wake alimpa upendeleo wa kipekee wa kumpunguzia majukumu mengi huku kazi yake kubwa ilikiwa ni kulala na kuwapa mimba wanawake mbalimbali ili waweze kumzalia masta wao watoto wenye nguvu ambao wangetumika katika shughuli za kitumwa.

maxresdefault-11.jpg


Roque Jose Florêncio aliacha idadi kubwa sana ya watoto.
 
Tunachokijua
Roque José Florêncio au kwa jina la utani la Pata Seca aliyeishi viunga vya jiji la São Carlos, ndani ya São Paulo, alizaliwa katika nusu ya kwanza ya karne ya 19 mnamo mwaka 1828.

Maisha ya Pata Seca yanatumika kama ukumbusho wenye kuhuzunisha wa mateso makubwa waliyovumilia Waafrika waliokuwa watumwa nchini Brazili.

Historia ya kuwa Mtumwa
Florêncio ilinunuliwa na Francisco da Cunha Bueno, mmojawapo wa watu wanaomiliki mashamba makubwa kwenye sherehe mojawapo ya maonyesho ya ndani. Alikuwa mtumwa mwenye nguvu na mrefu, akifikia zaidi ya futi 7.

Kwa sababu ya saizi yake ya mwili na imani ya wakati huo, Roque José Florêncio alitangazwa kuwa "Mtumwa wa kuzalisha".

Wakati huo, kulikuwa na imani kwamba wanaume warefu na wenye mwili mkubwa walikuwa na tabia ya kuwa na nafasi kubwa ya kuzalisha watoto wa kiume. Kwa hivyo, kumtumia mtu wa aina hii kuwapa wanawake ujauzito kungezalisha kizazi chenye wanaume wenye nguvu, ambacho kingetoa nguvu kazi ya kutosha kuhudumia mashamba utumwani.

Akiwa mtumwa, alilazimishwa kufanya ngono na wanawake watumwa ili kupata watoto zaidi utumwani. Kwa mujibu wa Free Press Journal, alizaa watoto 249 na wanawake kadhaa hivyo kumfanya kuwa babu wa moja kwa moja wa karibu 30% ya wakazi wa Santa Eudóxia, São Carlos.

Mbali na sifa za kimwili zilizotajwa tayari, anatajwa pia kuwa na mikono mirefu, myembamba, ambayo ambayo ilimpa jina la utani la Pata-Seca. Jambo lingine la kustaajabisha kuhusu mtumwa huyo ni kwamba hakufanya kazi shambani wala hakuishi katika makao ya watumwa. Kinyume chake kabisa, hadhi yake kama “Mtumwa wa kuzalisha” ilimpa manufaa fulani.

f9cb9f86-28f0-4e70-8252-1cd290bb6597.jpg

Roque José Florêncio (Picha ya Talk Africana)
Florêncio pia alikuwa na uhusiano mzuri na Cunha Bueno na hivyo kuwa na jukumu la kutunza wanyama wa usafiri wa shamba hilo. Zaidi ya hayo, alipewa jukumu la kusafiri zaidi ya kilomita 30 kwa farasi kila siku ili kukusanya barua za bwana wake.

Kwa hakika, ilikuwa ni kupitia huduma hii ya ujumbe ambapo alikutana na Palmira , msichana kutoka mjini ambaye alimuoa na pamoja walibahatika kupata watoto tisa.

Seca alikua mtu huru baada ya kushuhudia kukomeshwa kwa utumwa huko Brazil mnamo 1888.

Maisha baada ya utumwa na kifo
Roque alijihusisha sana na kilimo na ufugaji akiwa na familia yake.

Lakini kwa bahati mbaya, alipatwa na jeraha lililomfanya apate maambukizi ya pepopunda (tetenasi), na licha ya kupata huduma ya kwanza kutoka kwa mganga wa kienyeji, hali yake ilidhoofika haraka.

Baadae alipata maambukizi kwenye moyo (Endocarditis) kwa hivyo kutokana na umri wale pia kuwa mkubwa sana, aliaga dunia mnamo Februari 17, 1958 akiwa na umri wa miaka 130, miezi mitatu tu baada ya kushiriki gwaride la siku ya kuzaliwa kwa jiji kama mwanamume mzee zaidi katika kaunti hiyo.

img_0119-compressed.png

Cheti cha kifo cha Roque José Florêncio au kwa jina la utani la Pata Seca
Habari hizi kuhusu Roque José Florêncio zinathibitishwa na Mjukuu wake aliyefanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari katika nyakati kadhaa.

Mathalani, kwa mujibu wa gazeti Black Brazil Today, mjukuu wake anayeitwa Celso Tassim aliwahi kusema hawana cheti cha kuzaliwa cha babu yao, lakini huwatafuta ndugu zao waliosambaa maeneno mengi ya Brazil kupitia kitandao ya kijamii.

15082016085259f01-1.jpg

Mjukuu wa Roque José Florêncio anayefahamika kwa jina la Maria Magdalena Florencio Florentino akiwa na Cheti cha kifo cha babu yake

3-11.jpg

Maria Magdalena Florencio Florentino akiwa na picha ya babu yake
Kwa mujibu wa Maria Magdalena, babu yake aliishi kwa muda mrefu kwa sababu tofauti na watumwa wengine, aliishi katika Casa Grande (Nyumba Kubwa) na alikula vizuri zaidi. Aidha, bado anafanya utafiti juu ya historia yake na kabla ya kufa anakusudia kutoa kumbukumbu kwenye jumba la makumbusho ya kihistoria.

"Nina furaha sana, najivunia kusimulia hadithi ya babu yangu." alisema Maria Magdalena.

Kupitia machapisho mbalimbali ya kuaminika pamoja na nyaraka maalumu za kihistoria, JamiiCheck imebaini kuwa habari zinazomhusu Roque José Florêncio zina ukweli.

Roque José Florêncio anabaki kuwa mtu muhimu sana kwenye historia ya watu weusi, mateso yao na biashara ya utumwa iliyodumu kwa karne nyingi huku ikiacha maumivu makubwa hasa kwa bara la Afrika kwa kupoteza nguvu kazi kubwa na kurudishwa nyuma kwenye nyanja mbalimbali za maisha.
Nafikilia kwa ulimwengu huu tulio nao,kijana wa hovyo atumike km mbegu,angezaa Mara mbili ya idadi ya huyu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom