KERO Rombo: Kitengo cha Ustawi kina hali mbaya

KERO Rombo: Kitengo cha Ustawi kina hali mbaya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Maafisa Ustawi Kila siku wanatishiwa kuhamishwa na Katibu wa Idara ya Afya bila sababu za kueleweka.

Sijui yeye ana hayo Mamlaka ya kumhamisha Mtumishi maana hata kwenye Mfumo wa PEPMIS amewapanga vituo vya afya (bila kupewa barua zozote) ambako wanalazimishwa kwenda kukusanya mapato utadhani ndicho wamesomea.

Wanaambiwa wanajazana tu Halmashauri HQ angali Wagonjwa wao huko mahospitalini wanatia hasara tu kwa Misamaha ya Matibabu. Vituoni tayari wapo Maafisa ustawi.

Bajeti yao pia inatumiwa na watu wa Idara ya Afya. Mfano lipo swala la Mtoto alisafirishwa kuja kutumikishwa kazi za nyumbani. Mtoto alitakiwa arudishwe kwao Kagera lakini walipoenda kuomba wawezeshwe kupitia kifungu chao cha Dharura wakajibiwa kishatumika Kwa matumizi mengine.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya aliingilia na Mtoto amesafirishwa. Hilo pia la kudai pesa zao nalo ni mojawapo ya Kwa nini wanatishiwa kuhamishwa kituo chao Cha kazi.

Pia, Idara ya Uhasibu wanachelewesha malipo ya KITENGO cha Ustawi tofauti na Idara zingine ambazo Zinapendelewa kwani malipo yao huchukua wiki Moja tu lakini Malipo ya watu wa Ustawi yanachukua Hadi miezi hayatoki mpaka utokee ugomvi.

Baadhi ya Wahasibu ni miungu watu pale na wanapendeleana wao kwa wao na kuwaacha watumishi wengine wakiishi maisha ya ajabu. Idara hiyo Uhasibu ichunguzwe pia pamoja na Idara ya Afya
 
Back
Top Bottom