Rombo kama Loliondo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rombo kama Loliondo!

Discussion in 'JF Doctor' started by mlaizer, Mar 18, 2011.

 1. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  17 March 2011
  Daniel Mjema, Moshi

  Ni siku za mwisho? Hili ndilo swali lililoanza kuumiza vichwa vya watu baada ya kijana mmoja kuibuka wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro na kudai ameoteshwa dawa ya ajabu na Bikira Maria inayotibu magonjwa sugu ukiwamo Ukimwi.

  Kama ilivyo kwa mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambikile Mwasapile wa Loliondo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, kijana huyo naye amekuwa akitoa tiba kwa sh500.

  Kwa imani ya waumini wa Kanisa Katoliki Duniani, Bikira Maria ni mama wa Yesu ambaye anaaminiwa na waumini wa Kanisa hilo na hata katika sala jina lake ndilo linalotumika zaidi huku wakiamini kuwa Yesu ni mtoto wa Mungu.

  Habari za uhakika kutoka eneo la Customs katika mji mdogo wa Tarakea, mpakani mwa Kenya na Tanzania, zilimtaja kijana huyo ambaye sasa anajiita Nabii, kuwa ni Hilary James Kitwai (28), kutoka wilayani Babati.


  Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kutoka Tarakea, Kitwai alisisitiza kuwa dawa hiyo ameoteshwa na Bikira Maria na Yesu na kwamba inatibu Ukimwi, Saratani, Kisukari, Shinikizo la Damu, Figo, Pumu na maradhi ya maumivu.


  "Walinitokea kwenye ndoto wakanionyesha huo mti na waliniambia kwa sasa tuko wawili tu Tanzania, lakini huyo mwenzangu simfahamu. Mimi natoza Sh500 lakini katika hiyo pesa yangu na familia yangu ni Sh300 tu,"alidai.

  Kitwai ambaye amekuwa gumzo katika mji wa Tarakea, alisema anakabiliwa na changamoto kubwa katika kuwahudumia wenye mahitaji kwa kuwa hana msaada na kuomba serikali imsaidie kumpatia wahudumu.


  Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka wilayani Rombo, tayari vyombo vya ulinzi na usalama vimemzuia kwa muda, kijana huyo kutoa tiba inayofanana na ya mchungaji Mwasapile na kuitisha sampuli za mizizi anayoitumia.


  Kijana huyo ambaye ni fundi baiskeli kwa miaka mingi katika eneo hilo, aliibuka Jumatatu wiki hii na kuanza kutoa tiba kwa kutumia kikombe na tayari watu takribani 100 kutoka Kenya na Tanzania wamekunywa dawa yake.


  "Anadai kuwa ameoteshwa na Bikira Maria na alielekezwa huo mti ambao una utomvu na kuanzia juzi (Jumatatu),watu kama 100 hivi walishakunywa dawa hiyo ambayo wenyeji wanadai mti wake ni sumu,"kilidai chanzo chetu.

  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Tarakea, Motamburu, Kimario, alilithibitishia Mwananchi kuwapo kwa kijana huyo.


  Kimario alisema yeye binafsi, Ofisa Afya na Ofisa Usalama wa Taifa, walifika nyumbani kwa kijana huyo juzi na kumfanyia mahojiano.

  "Tulimhoji akasema alitokewa na Bikira Maria na Yesu ambao walimwonyesha mti huo ambao upo katika Mto Tarakea na walimwambia yupo mmoja tayari anayetibu maradhi sugu na kwamba yeye atakuwa wa pili," alisema mtendaji.


  Kwa mujibu wa mtendaji huyo, kijana huyo aliwaeleza kuwa baada ya Babu wa Loliondo na Yeye, bado atatokea mtu wa tatu ambaye naye ataoteshwa dawa za kutibu maradhi hayo na baada ya hapo Yesu mwenyewe atakuja duniani.


  "Tulimuuliza kama ameshatoa dawa hiyo kwa watu mbalimbali akasema alianza kutoa Jumapili na watu kama 20 hivi walikunywa na alitupa vipande vya miti viwili vya dawa hiyo na tumevikabidhi kwa uongozi wa juu,"alisema Kimario.


  Kwa mujibu wa Kimario aliyekuwa akimkariri kijana huyo, alisema 'nabii' huyo ameamua kutoendelea kutoa tiba hiyo hadi hapo serikali itakaporidhia na kwamba kwa sasa anamuomba Mungu ampe maono zaidi juu ya dawa hiyo.


  Wananchi walioongea na Mwananchi baada ya kuzagaa kwa taarifa hizo, wameitahadharisha serikali kuwa makini na watu wanaojiita ni manabii vinginevyo wananchi wanaweza kukumbwa na maafa ya kunywa sumu bila kujua.


  Wananchi hao wameitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwajibika kikamilifu kwa kuzuia matumizi ya dawa ambazo hazijathibitishwa kutokuwa na madhara.

  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Anthony Tesha ambaye pamoja na kukiri kusikia habari hizo lakini alisema anaviachia vyombo husika kufuatilia jambo hilo.
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Watazuka wengi tu
   
 3. Ally Msangi

  Ally Msangi Verified User

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Jun 29, 2010
  Messages: 581
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  kweli Tz sasa wa2 wameanza kuibuka, huyu jamaa mie simwamini hvi, au kaskia babu yupo nae akaona atokeze
   
 4. makete

  makete Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa tumwamini yupi maana tiba inaonekana kua ni njia yakujipatia umaarufu na pesa kwa njia rahisi. Jamani tuwe makini na watu wanaozuka nakujitaftia umaarufu maana kama dawa ya nabii ingekua inafanya kazi kati ya hao watu 100 tungukua tumeshapata ushuhuda kamili juu ya tiba yake
   
 5. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Kumeibuka kijana mmoja huko Tarakea, kwa jina la Hilary Katwai fundi baiskeli, akitoa dawa kama Babu wa loliondo kwa kudai naye ameoteshwa na bikira Maria na Yesu awaponye watu kwa kuwapa kikombe kimoja cha dawa hiyo!wenye magonjwa sugu kama Saratani,Ukimwi,Kisukari n.k.Kumekuwa na mkusanyiko mwingi sana huko mpakani na watu mbalimbali wamefurika kupata tiba hiyo!

  chanzo: gazeti la Mwananchi la leo
   
 6. M

  Marytina JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Tuikumbuke pia dowans wakati tukiendelea na vikombe
   
 7. nziriye

  nziriye JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 960
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Nimeanza na swali na kutaka kujua mana biblia yaelezea kuwa siku za mwisho manabii wa uongo watakuja wakidai wametumwa na MUNGU....nadhani wote tumesikia na wengine tumebahatika kwenda huko loliondo kupata tiba ya magonjwa sugu,mchungaji mstaafu hajamaliza kutibu ,kheee !!kaja kijana mwingine toka rombo,tarakea eneo la custom anajiita nabii james kitwai (28)yeye ni fundi baiskeli na anasema BIKIRA MARIA alimjia ktk ndoto akamwambia porini kuna mti ambao unatibu magonjwa sugu ukiwepo na ukimwi,ameanza toa tiba jmosi na watu zaidi ya 100 washakunywa kikombe chake na yeye hana gharama kubwa ni tsh 500 tu,wapendwa hapo nashndwa elewa ina mana twaelekea pata dawa ya magonjwa sugu au ndo dalili za siku za mwisho au ni utapeli mtupu?SOURCE.-Mwananchi newspaper
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni siku za mwisho? Hili ndilo swali lililoanza kuumiza vichwa vya watu baada ya kijana mmoja kuibuka wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro na kudai ameoteshwa dawa ya ajabu na Bikira Maria inayotibu magonjwa sugu ukiwamo Ukimwi.Kama ilivyo kwa mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambikile Mwasapile wa Loliondo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, kijana huyo naye amekuwa akitoa tiba kwa sh500.

  Kwa imani ya waumini wa Kanisa Katoliki Duniani, Bikira Maria ni mama wa Yesu ambaye anaaminiwa na waumini wa Kanisa hilo na hata katika sala jina lake ndilo linalotumika zaidi huku wakiamini kuwa Yesu ni mtoto wa Mungu.Habari za uhakika kutoka eneo la Customs katika mji mdogo wa Tarakea, mpakani mwa Kenya na Tanzania, zilimtaja kijana huyo ambaye sasa anajiita Nabii, kuwa ni Hilary James Kitwai (28), kutoka wilayani Babati.

  Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kutoka Tarakea, Kitwai alisisitiza kuwa dawa hiyo ameoteshwa na Bikira Maria na Yesu na kwamba inatibu Ukimwi, Saratani, Kisukari, Shinikizo la Damu, Figo, Pumu na maradhi ya maumivu.

  "Walinitokea kwenye ndoto wakanionyesha huo mti na waliniambia kwa sasa tuko wawili tu Tanzania, lakini huyo mwenzangu simfahamu. Mimi natoza Sh500 lakini katika hiyo pesa yangu na familia yangu ni Sh300 tu,"alidai.

  Kitwai ambaye amekuwa gumzo katika mji wa Tarakea, alisema anakabiliwa na changamoto kubwa katika kuwahudumia wenye mahitaji kwa kuwa hana msaada na kuomba serikali imsaidie kumpatia wahudumu.

  Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka wilayani Rombo, tayari vyombo vya ulinzi na usalama vimemzuia kwa muda, kijana huyo kutoa tiba inayofanana na ya mchungaji Mwasapile na kuitisha sampuli za mizizi anayoitumia.

  Kijana huyo ambaye ni fundi baiskeli kwa miaka mingi katika eneo hilo, aliibuka Jumatatu wiki hii na kuanza kutoa tiba kwa kutumia kikombe na tayari watu takribani 100 kutoka Kenya na Tanzania wamekunywa dawa yake.

  "Anadai kuwa ameoteshwa na Bikira Maria na alielekezwa huo mti ambao una utomvu na kuanzia juzi (Jumatatu),watu kama 100 hivi walishakunywa dawa hiyo ambayo wenyeji wanadai mti wake ni sumu,"kilidai chanzo chetu.Ofisa Mtendaji wa Kata ya Tarakea, Motamburu, Kimario, alilithibitishia Mwananchi kuwapo kwa kijana huyo.

  Kimario alisema yeye binafsi, Ofisa Afya na Ofisa Usalama wa Taifa, walifika nyumbani kwa kijana huyo juzi na kumfanyia mahojiano."Tulimhoji akasema alitokewa na Bikira Maria na Yesu ambao walimwonyesha mti huo ambao upo katika Mto Tarakea na walimwambia yupo mmoja tayari anayetibu maradhi sugu na kwamba yeye atakuwa wa pili,"alisema mtendaji.

  Kwa mujibu wa mtendaji huyo, kijana huyo aliwaeleza kuwa baada ya Babu wa Loliondo na Yeye, bado atatokea mtu wa tatu ambaye naye ataoteshwa dawa za kutibu maradhi hayo na baada ya hapo Yesu mwenyewe atakuja duniani.

  "Tulimuuliza kama ameshatoa dawa hiyo kwa watu mbalimbali akasema alianza kutoa Jumapili na watu kama 20 hivi walikunywa na alitupa vipande vya miti viwili vya dawa hiyo na tumevikabidhi kwa uongozi wa juu,"alisema Kimario.

  Kwa mujibu wa Kimario aliyekuwa akimkariri kijana huyo, alisema 'nabii' huyo ameamua kutoendelea kutoa tiba hiyo hadi hapo serikali itakaporidhia na kwamba kwa sasa anamuomba Mungu ampe maono zaidi juu ya dawa hiyo.

  Wananchi walioongea na Mwananchi baada ya kuzagaa kwa taarifa hizo, wameitahadharisha serikali kuwa makini na watu wanaojiita ni manabii vinginevyo wananchi wanaweza kukumbwa na maafa ya kunywa sumu bila kujua.

  Wananchi hao wameitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwajibika kikamilifu kwa kuzuia matumizi ya dawa ambazo hazijathibitishwa kutokuwa na madhara.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Anthony Tesha ambaye pamoja na kukiri kusikia habari hizo lakini alisema anaviachia vyombo husika kufuatilia jambo hilo.
   
 9. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  hv bikira maria naye ni mungu?
   
 10. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Duh! Kazi ipo!?
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hapo ndipo wa TZ mnanishangaza mnakivusha kwa muda mfupi na likitoke jingine mnalisahau kabisa mwaka huu ilianza dowans Gombs mabom yalipolika 2kayashkilia sasa la babu limejitokeza tumelishkilia pindi likijitoka jingine tunalishkilia tubadilike tusidandie mambo kiivyo
   
 12. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  tunaiua dowans taratibu
   
 13. nziriye

  nziriye JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 960
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  hapana bwana mchakamchaka,huyu ni mama aliyemzaa MWANA WA MUNGU,Kwa sisi wa-rc tuna imani ya kuwa na MUNGU MMOJA KATIKA NAFSI TATU, yani BABA,MWANA na ROHO MT,sasa huyu mwana ndio alikuja duniani ktk umbo la ubinadamu ili tuonje upendo wa MUNGU kupitia kwa mwanae mpendwa YESU,hoping i conquer u a bit and thank you kwa kuweka habari yote.
   
 14. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mpango mzima wa chama tawala huo kuwapoteza maboya wananchi kuconcetrate kwenye dawa badala ya uchumi kweli kazi ipo miaka 5 inaisha hakuna katiba mpya
   
 15. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wachaga tunawajua bana, mwambie amechelewa sana kuja kutudanganya maana babu hadanganyi:lol::lol::lol::lol:
   
 16. K

  Kivia JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Njaa inaupeleka ukiristo pabaya- kuna. Ukiristo umekuwa tatizo kwani wanatapeli watu kwa mgongo wa maono. Mf. DECI walidai kuoteshwa wakaibia watu. Kina kakobe, mzee wa upako, mwingira wote hawa wanawaibia waumini wao kila siku kwa kisingizio cha unabii/utume. Sasa wamezuka wengine kina babu wa loliondo na sasa nabii james wa rombo. Huu ni msiba mkubwa, wakiristo amkeni na utafuteni ukweli wa dini.
   
 17. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wa tatu anayemsema ni huyu aliyesema"....Njooni kwangu ninyi msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo, nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi"

  waombe Mungu hizo sumu wanazokunywa zisiwe na short or long term side effects.
   
 18. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  huyu jamaa anatokea Babati si mchaga!
   
 19. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  duuuh sijui na mimi ntaoteshwa lini?:A S-coffee:
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Bongo ni shamba la bibi, yaani unaweza ukanya, ukakojoa, ukala, ukalala na hata kuchoma mkaa humohumo
   
Loading...