KERO Huruma Hospital ya Rombo inatumia wanafunzi wasio na uzoefu

KERO Huruma Hospital ya Rombo inatumia wanafunzi wasio na uzoefu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa ROMBO MKUU naomba kuelezea kero ya hospitali ya HURUMA. Hospitali hii imekuwa ikiajiri wanafunzi waliohitimu masomo ya vyuoni ambao hawana experience ya kutosha katika kufanya kazi za wodini.

Kitu ambacho kimekuwa kikisababisha vifo vya Mara kwa Mara kutokea katika Hospitali hii. Hospitali hii ina ma Clinical Officers wanafunzi ambao hawana uwezo mzuri wa kumuhudumia mgonjwa vizuri. Inapenda kuwaajiri watu kama hawa kwa sababu ni rahisi kuwarubuni na sh 100k mpaka 200k. ( Mshahara wa chini).

Vilevile haina wafanyakazi wa kutosha unakuta Leba nesi yupo mmoja kwenye shifti nzima kitendo ambacho kinamlazimu kufanya majukumu mengi kwa wakati mmoja.

Pendekezo langu kwa Hospitali hii kuajiri watu wenye viwango na pia kuajiri wahudumu wa afya wengi wenye ubora katika fani ya afya ilikupunguza vifo ambavyo vimekuwa vikitokea mara na kutuliza wana ROMBO kila siku
 
Hilo ni janga kubwa na sio kwa hiyo hospitali pekee
Ma Intern wamekuwa wana achiwa kila kitu bila msaada wa kutosha kutoka kwa madactari
Hospitali nyingi hata hizi kubwa unaweza kuta hazina mfumo ulio rasmi wa kudeal na intern; kila hospitali inajiamulia itakavyo ona inafaa.....
Nilikuwa na mgonjwa kwenye moja ya Hospitali ya rufaa, nilishangaa kuona kinacho endelea...Intern anapambana kwa uwezo wake wote (try and error) niliandikiwa dawa ya aina moja na Intern kwa kiasi kikubwa hadi pharmacy wanakataa kuniuzia kuwa sio kawaida!. Yaani dawa hairespond, anaongeza tu dozi badala ya kufikiri linaweza kuwa tatizo tofauti hivyo assugest vipimo zaidi.
Dactari alikuwa anapita x 2 kwa siku na kila session ikichukua dkk 5 shukuru Mungu.... na hata kuwapangia zamu ma intern....yaani kila siku ya pili wanabadilishwa wakati hata tatizo la mgonjwa halijaajulikana
Yaani wanatoka pale sifuri kabisa au niseme, wanatoka pale na kile kile walichotoka nacho chuoni...
 
Makosa ndo yanawafanya wawe bora zaidi siku za usoni, tuendelee kuwapa nafasi madaktari wetu bingwa 😂

Tuendelee kuumwa

Ndio wafanye try and error kwenye mwili wa mtu unafikiri ni panya wa majaribio???
 
Madatari wa sasa hata wenye experience bado hawana kitu kichwani. Sio ajabu daktari akakwambia huumwi lakini kumbe unahitaji matibabu makubwa. Kwa level tuliyofikia tunategemea maombi tu uombe Mungu usiumwe ukiumwa habari unayo utasumbuka kila hospital hutapata wakukutatulia tatizo lako
 
Mimi ni mkazi wa ROMBO MKUU naomba kuelezea kero ya hospitali ya HURUMA. Hospitali hii imekuwa ikiajiri wanafunzi waliohitimu masomo ya vyuoni ambao hawana experience ya kutosha katika kufanya kazi za wodini.

Kitu ambacho kimekuwa kikisababisha vifo vya Mara kwa Mara kutokea katika Hospitali hii. Hospitali hii ina ma Clinical Officers wanafunzi ambao hawana uwezo mzuri wa kumuhudumia mgonjwa vizuri. Inapenda kuwaajiri watu kama hawa kwa sababu ni rahisi kuwarubuni na sh 100k mpaka 200k. ( Mshahara wa chini).

Vilevile haina wafanyakazi wa kutosha unakuta Leba nesi yupo mmoja kwenye shifti nzima kitendo ambacho kinamlazimu kufanya majukumu mengi kwa wakati mmoja.

Pendekezo langu kwa Hospitali hii kuajiri watu wenye viwango na pia kuajiri wahudumu wa afya wengi wenye ubora katika fani ya afya ilikupunguza vifo ambavyo vimekuwa vikitokea mara na kutuliza wana ROMBO kila siku
Ufanyike mpango wa lazima maana kuna wahudumu wapo vizuri zaidi ila wanagomea kutoka katika hospitality za mikoa kwakukwepa kuja wilayani njia pekee serikali itenge bajeti nzuri ya kuweza kuwashawishi hawa wauguzi na madoctor waweke kambi zaidi katika hospital za wilaya ili kuwanoa ata hawa wanaoanza kazi
 
Back
Top Bottom