Kuhusu Ugonjwa wa Kujikojolea kitandani

Kuhusu Ugonjwa wa Kujikojolea kitandani

KingGenerous

New Member
Joined
May 27, 2026
Posts
1
Reaction score
0
Habari za wakati huu wana Jamiiforum, mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 26, nimeishi na tatizo la kujikojolea kitandani tangu utotoni hadi hivi sasa ambapo bado sijapona kwa 100% ila namshukuru Mungu nimeanza kupata nafuu kidogo na pia nimefahamu vingi vingi sana kuhusu tatizo hili na nimeona nisaidie wengine kwa namna moja ama nyingine

Najua uliposoma hapo ina sound kama nataka kufanya biashara ya kuuza dawa za kutibu kujikojole kitandni Lakini nikwambie sito kuuzia chochote na sipo hapa kufanya hivyo na kama nitakuja kukuuzia dawa yoyote ile njoo hapa uniripoti kwa utapeli. Kwanza 80% ya dawa zinazo uzwa ambazo ndio tunaambiwa ni kutibu kujikojolea kitandani huwa hazitibu tatizo hilo kabisa, nitaeleza yote

Nitaandika hapa na nitasaidia watu kwa namna ambayo Mungu ataniwezwsha kwani naona ni kusudi la Mungu kunipitisha katika hali hii na kunifanya niwe msaada kwa wengine.

Wazee kijana wa miaka 26 kujikojolea kitandani sio jambo dogo, sio jambo la kujifanyisha yani sio uzembe...
.
Kiufupi ni jambo zito zito zaidi ya unavyo fikiri
.
Niseme tu Mungu aniongoze na anipe Nguvu nisikate tamaa katika kusaidia watu katika jambo hili
 
Back
Top Bottom