Roman Abramovich: Utajiri wa Damu, Risasi na Umafia

Habibu B. Anga

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined
May 7, 2013
Messages
6,375
Points
2,000
Habibu B. Anga

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined May 7, 2013
6,375 2,000
SEHEMU YA TANONifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij addenbwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush mossad 03 white wizard xtaper Mzigua90 Ollachuga Oc Gidbang Mateja M.G Yango jipu abaa4all DIBAJI Agenda1 Grahnman The MaskmaN Slim5 Xubzero agprogrammer JoJiPoJi Architectus blance86 Mamtolo monde arabe Ngao Ya Imani stardust JK naiman64 Dharra seledunga ABB SHAMMA Richard Waziri wa Kaskazini Mwinjuma1 Kanungila Karim baracuda Mwamba028 besaro Pyepyepye Bilionea Asigwa ibn Kiti Chema Tugas Royal Warrior mederii mmangO manzi james LIKUD adrenaline Royal Son Mhadzabe salaniatz Natasha Ismail jiwe jeusi chibalangunamchezo
John Mloy conjuget Van Pauser great G Mtoto wa nzi Zeus1 hindustan Sci-Fi MAN OF PEACE kashata emnly danny baraka bb MTOTELA kbosho TEMLO DA VINCA
 
Niccolo Machiavelli

Niccolo Machiavelli

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2017
Messages
1,364
Points
2,000
Niccolo Machiavelli

Niccolo Machiavelli

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2017
1,364 2,000
yani kwenye uandishi wako umeutukuza huo uyahudi utadhani dunia nzima top 50 ya matajiri ni wayaudi tu,kwanza kiuhalisia huyo abramovich hana uyaudi wowote ukianza kufatilia uzazi wake sema tu umekuzwa kutokana na uhasama uliopo kati ya USA na RUSSIA kuonesha kuwa mzungu wa kawaida asingeweza kumteka rais yeltsin kirahisi.Ndipo hapo neno uyaudi likakuzwa kwa Abra
img_2461-jpg.1181607
 
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Messages
4,680
Points
2,000
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2015
4,680 2,000
Jamani Maorich wenzangu ngoja nilale japo stori imeishia sehemu tamu
 
monde arabe

monde arabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2017
Messages
4,675
Points
2,000
monde arabe

monde arabe

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2017
4,675 2,000
ROMAN ABRAMOVICH: UTAJIRI WA DAMU, RISASI NA UMAFIA

SEHEMU YA TANOMara ya mwisho nilieleza kuhusu mwendesha mashtaka mkuu wa serikali Bw. Yuri Skuratov akijitapa kuwa ana ushahidi wa kutosha kumfungulia mashtaka oligarch Roman Abramovich na ameweka nia kumburuza mahakamani siku si nyingi.Kuna suala moja la msingi sana… katika nchi za Ulaya mashariki pamoja na nchi za ulimwengu wa tatu, ukiona mtu amechuma utajiri mkubwa wa kutisha basi ufahamu kuwa si mtu wa ‘mchezo mchezo’. Kwa namna ambavyo serikali zetu na biashara zetu zinaendeshwa katika nchi za ulimwengu wa tatu namna pekee unaweza kuushinda ‘uhuni’ ni kwa kuwa ‘muhuni’ wewe mwenyewe pia. Mambo kwenye nchi hizi hayaendeshwi kwa kanuni za ustaarabu kama kwenye ulimwengu wa kwanza… kwa hiyo ni eidha ujifunze kula nyama za watu au usubiri wewe ufanywe kitoweo.Ndio maana utaona kuna mjasiriamali maarufu na mwenye mafanikio makubwa sana hapa nchini, tumuhifadhi jina maana ni marehemu kwa sasa amefariki kama miezi mitatu iliyopita… alikuwa yuko vizuri haswa na kitengo chake binafsi cha ulinzi na ‘intelijensia’. Kuna watu watashangaa, ati yule mzee mwenye media house kubwa nchini ana kitengo binafsi cha intelijensia? Naam, na kiko vizuri haswa… well, si kitengo kikubwa haswa kufananisha na jamaa zetu wa Oysterbay au makumbusho, bali ni kitengo cha ulinzi haswa lakini kiko very well equipped kufanya ushushushu wa kibiashara na hata mwenendo wa nchi na viongozi wake.

Na ndio maana pia Askofu maarufu sana hapa nchini ambaye hakauki kutoa matamko yenye utata unaweza kujiuliza anawezaje ‘ku-survive’ na hata muda mwingine vyombo vya usalama kupigwa chenga… jawabu ni hilo hilo, ana kitengo maridhawa mno cha ulinzi na usalama ambao pia wako vyema mno kwenye kufanya ushushushu. Tena huyu askofu nimeshuhudia kwa macho yangu na naweza kusema kabisa kwamba ni kitengo chake cha usalama kiko mbali zaidi kushinda hata wafanyabiashara wengi hapa nchi… kiko very sophisticated.Kwa nini nasema haya? Ni kwa sababu sisi wafanyabiashara wetu wanayafanya haya leo hii, Roman Abramovich alikuwa ameshaanza kukifanya kitu hiki tangu miaka ya mwanzoni mwa tisini na alikuwa anakifanya kwa ufanisi mkubwa haswa.

Ndani ya kampuni ya Sibneft alikuwa ameunda kitengo maalumu cha ulinzi na usalama. Kazi ya kitengo hiki, Mosi, kilihusika na ulinzi wa kawaida wa mali za kampuni. Lakini pia ndani yake kulikuwa na idara maalumu ya siri ambayo Abramovich mwenyewe aliita SUR ambayo ilikuwa inahusika na ukusanyaji wa intelijensia juu ya washindani wao wa kibiashara pamoja na viongozi wa serikali na hapa hasa ndiko ninapotaka kupaongelea.Kitengo hiki cha SUR kama ambavyo Abramovich mwenyewe alipendelea kukiita walikuwa na intelijensia ya kutosha juu ya viongozi wengi wa serikali na mmojawapo akiwa ni mwendesha mashtaka mkuu wa serikali Bw. Yuri Skuratov.Wanasema kila binadamu chini ya jua kuna ‘mafuvu’ ameyaficha kabatini. Kila mtu ana siri ambayo anatamani afe nayo. Siku ambayo adui zako wakigugundua siri hiyo ndio inakuwa kiama chako kama ambavyo ilimtokea mwendesha mashtaka Skuratov.Baada ya joto la mwendesha mashtaka wa serikali kutaka kumshtaki Abramovich kupanda, Oligarch Berezovsky alikaa na Abramovich kumuuliza ana mpango gani na hicho ambacho kinaelekea kutokea. Abramovich akamuondoa wasiwasi, akamwambia tu anahitaji msaada mmoja kutoka kwake.“Anything you want.!” Berezovsky akamjibu .Abramovich akamuomba Berezovsky ampatie nusu saa tu katika televisheni yake muda wa usiku, kiandaliwe kipindi maalumu kwa ajili yake. Nilieleza kwamba kwa kipindi hicho Berezovsky alikuwa anamiliki kituo cha televisheni ambacho ndicho kilikuwa kinatazamwa zaidi nchini Russia. Berezovsky bila kusita akawasiliana na meneja wa kituo chake cha televisheni na kumueleza kwamba atenge muda huo wa nusu saa majira ya usiku ndani ya siku mbili zijazo kwa ajili ya Oligarch Abramovich kuongea.Muda ukapangwa na siku ya Abramovich kuongea ikawekwa kwenye ratiba.

Ikapigwa ‘promo’ ya kutosha kutangaza siku hiyo husika na muda husika ambao Oligarch Roman Abramovich ataongea kupitia televisheni kujibu shutuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake kuhujumu uchumi wa nchi. Ajabu ni kwamba muda huu ambao ulitangazwa Abramovich ataongea ilikuwa ni saa tano usiku na kuna angalizo lilitolewa kwamba wazazi wahakikishe asiangalie mtoto mwenye umri chini ya miaka 18.

Watu walikumbwa na butwaa… Abramovich anataka kuongea nini hicho ambacho watoto hawapaswi kukisikia.?Yuri Skuratov mwenyewe alifahamu ni ‘tsunami’ gani ilikuwa inakuja japo hakutaka kuamini.Siku ikawadia, muda ukawadia… saa tano kamili usiku, Abramovich alikuwa mubashara kwenye runinga kujitetea tuhuma zake. Nadhani wengi tunafahamu namna ambavyo Abramovich anaongea, anaongea taratibu mno na kwa sura ya upole haswa. Upole wake anapoongea unaweza kumfananisha na kijana Jared Kushner, mastermind aliyemuingiza Trump whitehouse. Hapa kwetu waweza kumfananisha na marehemu mzee wetu Mengi labda au Ruge Mutahaba… wote hawa mastermind wa masuala mengi ya nchi japo kwa namna wanavyoongea taratibu na kwa upole unaweza kudhani ni magoigoi tu. Lakini waguse uone cha mtema kuni…Kipindi kilipoanza Abramovich akajieleza kwamba anaonewa wivu na wanasiasa kutokana na mafanikio yake ya kibiashara. Abramovich akajitetea kwamba mafanikio yake hayo si kwa ajili yake tu bali pia ni kwa ajili ya familia nyingi masikini ambao nao watanufaika (miaka michache baadae Abramovich alitumia fedha zake binafsi zaidi ya dola bilioni tatu (zaidi ya trilioni 6.7 za Tanzania) kwa ajili miradi ya maendeleo kwenye moja ya majimbo masikini zaidi nchini Russia, nitaeleza).

Akajitetea zaidi kwamba wanasiasa hao wanamtumia mwendesha mashitaka Yuri Skuratov ili amchafue na kumuondolea imani kwa wananchi wenzake. Kisha Abramovich akamalizia kwa kusema kwamba anao ushahidi kuthibitisha kwamba Skuratov ni mtu wa hovyo kabisa ambaye hapaswi kuaminiwa na jamii.Alipomaliza kusema hayo mkanda wa video ukaanza kuchezwa kwenye runinga. Video hiyo ilikuwa inamuonyesha Yuri Skuratov akiwa uchi wa mnyama kwenye chumba cha hoteli akifanya ngono mabinti wadogo wawili waliokadiriwa mmoja kuwa na miaka kumi na mitano na mwingine miaka kumi na sita. Video inamuonyesha binti mmoja akimfanyia kitendo cha ngono kwa kutumia midomo yake na huku mwingine akimpapasa mwilini na kubusiana.(natamani kuiweka hapa video lakini sidhani kama itakuwa sawa kwa sababu za maadili na sidhani kama ni lazima sana kuitazama… nimepiga ‘screenshots’ tu ili walau upate picha wa kilichotokea)Ilkuwa ni tsunami na ambayo haikutegemewa… Abramovich akaongeza kuwa anao ‘ushahidi’ wa wanasiasa wengi wanaompinga kuwa ni watu wa hovyo na mafisadi waliojawa wivu. Kwa maneno mengine alikuwa anatoa ‘warning’ kwa wapinzania wake kwamba anao ushahidi wa mauzauza wanayoyafanya gizani.Nchi ya Urusi ilitetema usiku mzima. Kesho yake asubuhi Skuratov akajaribu kujitetea kwamba mkanda huo wa video ni feki lakini hakuna ambaye alimuamini. Yeye ambaye alikuwa kwenye harakati za kumfungulia kesi Abramovich kibao kiligeuka kwake, akafunguliwa mashataka ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto ambao hawajafikia umri halali kisheria kujihusisha na vitendo vya ngono. Kutokana na kushtakiwa kwa kesi hiyo akashinikizwa pia kujiuzulu wadhifa wa mwendesha mashtaka mkuu wa serikali.Skuratov akapotea kwa namna hiyo na hata tuhuma zake dhidi ya Abramovich zikafa kibudu kwa mtindo huo pamoja naye.Abramovich sasa akawa anaogopwa pale Moscow. Wapinzani wake wakikutana naye walitamani hata wamuamkie japo ni kijana mdogo kwao. Walifahamu kuwa ana ushahidi wa mauzauza yao na anaweza kuyaachia kwa umma muda wowote ule. Hiyo ilikuwa ni kinga tosha kwake Abramovich.. sasa alikuwa ni ‘untouchable’. Hakuna ambaye alikuwa anathubutu kumnyooshea kidole…Hii ilikuwa ni fursa adhimu kwake kutimiza lengo lake la pili kwenye kujilimbikizia mabilioni ya dola. Lengo hili la pili lilikuwa ni kushikilia sekta ya uzalishaji Aluminum. Rusia ni mzalishaji mkuu wa Aluminium duniani na kipindi kile miaka ya tisini asilimia kubwa ya aluminium ambayo ilikuwa inatumika duniani ilikuwa inatoka nchini Rusia. Abramovich alikuwa anataka kuweka mguu wake kwenye sekta hii… mguu mmoja tayari alikuwa ameuweka kwa uthabiti kabisa kwenye sekta ya mafuta na gesi.Lakini kulikuwa na tatizo kubwa zaidi linawakabili ma-oligarch. Na lilikuwa tatizo kubwa zaidi ambalo lilikuwa linatishia utajiri wao kupotea na hata uhai wao… kulikuwa na kila dalili kwamba Rais Boris Yeltsin alikuwa amekumbwa na tatizo la ugonjwa fulani wa akili.Mwanzoni watu walidhani ni ucheshi tu lakini kadiri siku zilivyoenda kulikuwa hakuna ubishi kwamba Yeltsin alikuwa amekumbwa ghafla na tatizo la akili. Kwanza alikuwa amekuwa mlevi kupindukia… alikuwa analewa mpaka muda wa kazi. Kuna siku alikuwa anahutubia taifa akiwa amelewa chakali. Alikuwa anasoma sentesi moja dakika tano nzima. Siku nyingine alihudhuria mazishi ya jenerali wa jeshi akiwa amelewa chakali tena. Hata ulipofika muda wake wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu ambapo unasogelea jeneza na kupiga saluti, Yeltsin aliposogelea jeneza ili apige saluti nusura adondoke kwa kupepesuka. Ilibidi mpaka walinzi wake wamshike kama mtoto ndio asimame sawasawa na kupiga saluti.

Siku nyingine wako kweye halaiki ya kitaifa… wakati wimbo wa taifa unaimbwa Yeltsin akainuka na kwenda kumpokonya kipaza sauti mwendesha shughuli na kuanza yeye kuongoza kuimba wimbo wa taifa huku akiimba hovyo hovyo na kwa sauti ya ulevi.Yeltsin alikuwa na tatizo na alikuwa anatakiwa kuondolewa madarakani haraka iwezekanavyo. Kama wakifanya uzembe na bunge likamuondoa madarakani Yeltsin na kumuweka mtu wao kuna kila dalili kwamba mali zao zote zitataifishwa na hata wao wenyewe kuishia jela maana wanasiasa wengi ndani ya Moscow walikuwa na hasira na namna ambavyo ma-oligarch wanaitafuna nchi kwa kukingiwa kifua na Yeltsin.Lilikuwa linahitajika suluhisho la haraka kabla mambo hayajaaribika. Ma-oligarch wote walimtazama Abramovich, tumaini lao lilikuwa kwake atoe wazo wapate suluhu wa nini kifanyike.

Ma-Oligarch wenzangu mnisamehe bure mkiona niko kimya, kuna muda natamani niweke updates ila nashindwa kutokana na mihangaiko… waweza kuni-support pia kwa kuungana nami Whatsapp.Kesho tutapumzika kidogo, kisha kesho kutwa itaweka seheu ya sita.The Bold – 0718 096 811

To Infinity and Beyond
Daaaahhhhhhh,wewe jamaa ni shida tupu!
Usisahau kuni-tag!
 
kipapi

kipapi

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
627
Points
1,000
kipapi

kipapi

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
627 1,000
Hatari sana..! Utajili huu..! lazma uwe na akili mingi na roho mbaya ndio ufanikiwe
 
Gien Banks

Gien Banks

Senior Member
Joined
Sep 10, 2018
Messages
103
Points
250
Gien Banks

Gien Banks

Senior Member
Joined Sep 10, 2018
103 250
yani kwenye uandishi wako umeutukuza huo uyahudi utadhani dunia nzima top 50 ya matajiri ni wayaudi tu,kwanza kiuhalisia huyo abramovich hana uyaudi wowote ukianza kufatilia uzazi wake sema tu umekuzwa kutokana na uhasama uliopo kati ya USA na RUSSIA kuonesha kuwa mzungu wa kawaida asingeweza kumteka rais yeltsin kirahisi.Ndipo hapo neno uyaudi likakuzwa kwa Abra
Ulitaka nisifie wanyakyusa ??

F.O.H
 
smarte_r

smarte_r

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2013
Messages
1,005
Points
2,000
smarte_r

smarte_r

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2013
1,005 2,000
Pia wale wote ambao wameomba kuwaongeza kwenye taglist, nafanya hivyo next time mtaona majina yenu nimeongeza kwenye list
kwa hakika hadithi hii ya chanzo cha utajiri wa roman abramovich ina reflect 100% circle ya watz wachache waliotajirika kupitia udhaifu wa serikali ya ccm nyakati za utawala wa mkapa na kikwete. sitakuja kusahau yale maskendo ya upotevu wa mabilioni ya fedha za tz.
 
Khan

Khan

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Messages
5,656
Points
2,000
Khan

Khan

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2012
5,656 2,000
Maisha bwana, kwahiyo Mr A kamsuggest Mr Putin awe Raisi, kwa sasa Mr A ana Usd 12.4B na Putin awe na USD 200B duh Mbona gap kubwa sana??
 
lyasi

lyasi

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Messages
220
Points
250
lyasi

lyasi

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2015
220 250
Wengi tunaakili (na mimi nikiwemo) lkn,tunakosa-connection!
Huna akili huna connection (Sina bahati), Una akili una connection hayo ndiyo matumizi ya akili mkuu.
Hata na wewe ni msukule umejuaje wameshinda wakisubiria hadithi za kutungwa kama wewe hufungui hii thread kila baada ya dk 5 na kusoma comments za wadau kuhusu kusubiria? Na ulijuaje ni hadithi ya kutunga kama hujaisoma?..Kubali tu kuwa na wewe ni sehemu ya misukule kama unavyowaita wenzako...

Akina bashite??Ebu tusaidie angalau kuanzisha vuguvugu la kumng'oa jiwe maana akishaondoka ndo utakuwa mwisho wa bashite...Ebu tusaidie mkuu na sisi tutakuunga mkono maana lazima tuwe na kiongozi..Ongoza hilo vuguvugu hata sisi akina bashite wanatukera sana ila tumekosa tu mtu mwenye uthubutu kama wewe...Tunakuomba uwe MUSA wetu....anza kesho kuita waandishi wa habari na umnyee jiwe na genge lake mwanzo mwisho uone jinsi tutakavyokuunga mkono..
 
de play boy

de play boy

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2017
Messages
769
Points
1,000
de play boy

de play boy

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2017
769 1,000
Shukran boss

nafanyaje kujiunga group lako la watsapp
 
pappilon

pappilon

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2015
Messages
2,771
Points
2,000
pappilon

pappilon

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2015
2,771 2,000
Maisha bwana, kwahiyo Mr A kamsuggest Mr Putin awe Raisi, kwa sasa Mr A ana Usd 12.4B na Putin awe na USD 200B duh Mbona gap kubwa sana??
Unaweza kumfundisha mtu wizi mkuu ila yeye akajiongeza na kuwa jambazi kabisa (hapa nikazie..ujambazi wa mali ya umma)..hiki ndo kilitokea kwa hawa mabwana nadhani....ishitoshe Putin alikuwa jasusi mbobezi na ndo alikuwa/ameshikilia mpini
 

Forum statistics

Threads 1,325,716
Members 509,275
Posts 32,200,578
Top