wax
JF-Expert Member
- Jun 14, 2015
- 5,530
- 5,060
Daaah mkuu unashusha nondo hatar yaan unaongea Ukweli wenyewe aise vitu vinatutokea kabsaa roho Huwa Inaumagaa Sana tena inakataa inasema huyu mtu achana nae akili nayo inagoma
Baadae unajutaa na kulia sanaa unasema nlisikia roho ikinikataza
Baadae unajutaa na kulia sanaa unasema nlisikia roho ikinikataza
Roho huweza kuona ambavyo macho ya mwili hayawezi kuona, hasa jambo au kitu kitakachotokea baadaye. Usishangae kuwa litakalotokea kesho roho yako inalijua leo!
Hata mke wa kuoa au mume wa kuolewa naye, unaweza kumfurahia kwa macho na kuvutiwa na kila kitu leo, lakini roho yako ikamkataa kabisa, na pengine kwa kuugua na kuumia sana jinsi unavyompenda wewe na akili yako, pasina kujua lolote.
Unaweza kushupaza shingo, lakini moto utakapoanza kuwaka ndani ya nyumba baada ya miaka kadhaa ya uvumilivu, utakumbuka na kuanza kusema: ndio maana roho ilisita, iligoma, iliuma, iliogopa, nk.; Inabaki kuwa majuto ni mjukuu!