Roho ni nini na ipo sehemu gani ya mwili?

Huwezi kuiona roho yako kwa macho kwa kuwa si mwili. Nikuulize kidogo ili uweze kunielewa: Je, umewahi kuuona upepo kwa macho? Hata kama hujawahi kuuona lakini sauti yake, matokeo au madhara yake, unayasikia na kuyaona kwa hakika.

Kwahiyo, uwepo wa kitu fulani si lazima ukione kwa macho. Hata sauti hujawahi kuziona lakini unazisikia kwa hakika!

Roho yako ndiyo wewe mwenyewe. Mwili ni koti tu lililoivaa roho, ikitoka unakuwa umekufa. Pia una nafsi (soul) ambayo hujumuisha akili (mind), hisia (emotions) na maamuzi (decisions). Nafsi hubeba utashi (conscience) ambao wanao watu tu, si wanyama.

Unafanya jambo lolote kwa utashi wako, kwa maamuzi yako na mtazamo au mapenzi yako. Tunu hiyo haipo kwa wanyama. Hata mnyama anapokunya hafikirii chochote - kunya kunamtokea tu popote!

Je, umewahi kutokewa ambapo unabishana na wewe mwenyewe? Akili yako inaamua kwenda mahali fulani, lakini ndani yako unasikia sauti ya chini inakukataza usiende! Ukiamua kwenda bila kuitii hiyo sauti ndani yako halafu ukapata shida huko uendako, utaanza kusema roho yangu ilinikataza! Roho yangu ilisita! Roho iligoma kwenda!

Kwahiyo, kila mtu ana sehemu tatu: Roho (spirit), Nafsi (soul) na Mwili wa damu, nyama, mifupa, nk (flesh). Kama hujanielewa nitafute ili nikupe ufafanuzi zaidi kadri Mungu atakavyonijaalia. Pia waweza kusoma 1 Thesalonike 5:23
Je nikisema kuna jambo nataka nifanye lakini nafsi inakataa nakosea?
 
Naomba nijibu la swali # 1, 2, 3, 4 kwa pamoja

Roho ni umbile la pekee lisiloonekana ambalo linasadikiwa kuwemo pamoja na mwili katika binadamu na kuunda hasa malaika (ambao kati yao wale wabaya wanaitwa ma shetani ).
Katika lugha mbalimbali umbile hilo linafananishwa na upepo au pumzi .
Mungu mwenyewe anasadikiwa kuwa roho bora. Kwa namna ya pekee Ukristo unasadiki moja ya nafsi za Kimungu ndani ya Utatu inayoitwa Roho Mtakatifu.
Pengine roho inafikiriwa kueleza tofauti kubwa mno ambayo inajitokeza kati ya binadamu na sokwe na wanyama wengine wote upande wa akili na utendaji, pamoja na ambayo haielezwi vya kutosha na tofauti katika DNA zao.
Inasadikiwa kuwa roho ndiyo sehemu bora zaidi ya mwanadamu na husadikiwa kuwa haifi bali hudumu milele. Roho humuunganisha mtu na ulimwengu wa kiroho ambao aghalabu huwa ni ulimwengu usioonekana na macho ya kawaida, yaani ya mwili.

Waandishi wa Biblia walitumia neno la Kiebrania
ruʹach au neno la Kigiriki, pneuʹma waliporejelea “roho.” Maandiko yenyewe yanaonyesha maana ya maneno hayo. Kwa mfano, andiko la Zaburi 104:29 linasema: “[Yehova] ukiiondoa roho [ ruʹach ] yao, wanakata pumzi, na kurudi katika mavumbi yao.” Andiko la Yakobo 2:26 linasema kwamba “mwili bila roho [ pneuʹma ] umekufa.” Katika andiko hilo “roho” inamaanisha kile ambacho huupa mwili uhai. Bila roho, mwili umekufa. Kwa hiyo, katika Biblia neno ruʹach
halitafsiriwi tu “roho” bali pia “nguvu” au kani ya uhai. Kwa mfano, Mungu alisema hivi kuhusu Mafuriko ya siku ya Noa: “Ninaleta gharika ya maji duniani ili kuharibu kutoka chini ya mbingu wote wenye mwili walio na nguvu [ ruʹach ] za uhai ndani yao.” ( Mwanzo 6:17; 7:15, 22) Hivyo, “roho” inarejelea nguvu isiyoonekana, inayotendesha viumbe vyote vilivyo hai.
Nafsi na roho hutofautiana. Mwili unahitaji roho kama vile redio inavyohitaji umeme ili kufanya kazi. Kwa mfano, unapotia betri katika redio na kuiwasha, nguvu zilizo katika betri huiwezesha redio kufanya kazi. Hata hivyo, redio haiwezi kufanya kazi bila betri. Hali kadhalika, redio ambayo imeondolewa kwenye umeme haiwezi kufanya kazi. Vivyo hivyo, roho ni nguvu ambayo hutendesha mwili wetu. Kama umeme, roho haiwezi kuhisi wala kufikiri. Ni nguvu isiyo na utu. Lakini bila roho au kani ya uhai, “tunakata pumzi na kurudi kwenye udongo,” kama mtunga-zaburi alivyosema.
Andiko la Mhubiri 12:7 linasema hivi linapozungumzia kifo cha mwanadamu: “Mavumbi [mwili wake] huirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho yenyewe humrudia Mungu wa kweli aliyeitoa.” Roho au kani ya uhai inapoondoka mwilini, mwili hufa na kurudi ulipotoka, yaani, kwenye udongo. Vivyo hivyo, nguvu ya uhai hurudi ilipotoka, yaani, kwa Mungu. ( Ayubu 34:14, 15; Zaburi 36:9 ) Hiyo haimaanishi kwamba nguvu ya uhai huenda mbinguni kihalisi. Badala yake, inamaanisha kwamba mtu akifa, tumaini lolote la kuishi tena linamtegemea Yehova Mungu. Ni kana kwamba uhai wake uko mikononi mwa Mungu. Ni kupitia nguvu za Mungu tu ndipo roho au nguvu ya uhai inaweza kurudishwa ili mtu aweze kuishi tena.
Inafariji kama nini kujua kwamba hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya kwa wote wanaopumzika ndani ya “makaburi ya ukumbusho!” ( Yohana 5:28, 29) Wakati wa ufufuo, Yehova atamfanyizia mwili mpya yule anayelala katika kifo na kuuhuisha kwa kutia roho, au nguvu ya uhai ndani yake.
 
Nilisema kuwa Kuna kitabu Cha Freemasonry nilisoma, Sasa naki-quote katika kujibu swali la mleta mada, nita-quote maelezo marefu kidogo, ila najua wengi watayapenda.

Here We go.

"The lodge is more than an assembly of individuals. When properly formed, it is an object lesson in the knowledge of yourself. The true work of the craft—disciplining and perfecting yourself— cannot be entered upon without first understanding the details of the many parts which make up yourself. The lodge provides a model to help you understand."

Naendelea ku-quote

"You're a threefold being. You have an outside personality, which functions in the world. This is temporal, mutable, and fall far short of expressing your real nature" (Body???)

"You also have an inside personality: a large psychological field called the mind. Your mind actuates the outside self, but is more subtle and complex. ......... The secret science of the craft is directed towards developing your mind, and the lodge is formed with the purpose of serving as a model of that sphere of psychical faculties and tendencies which We call intellect. We can change from a rough ashlar to a perfect cube and be carried from natural darkness into supernatural light.

Sasa swali la mleta mada lime-base hapa..check Freemasonry inavyosema kuhusu roho...

"But there is a third factor, beyond your outward person. The factor which joins you to the source of all being. This is your spirit, your real self, your centre, which We sometimes call your soul. This spirit has it's mysteries which can never be know until the teaching of the craft has been assimilated both In theory and personal experience. The spirit indwells the mind, just as the mind suffuses the body.."

Wakuu nimemaliza ku-quote kitabu Cha Freemasonry
 
Roho ni nafsi kamili ambayo huwezi kuishika wa kuiona...kwann binadamu anakufa nafsi zetu hazikamilika kwaiyo inafika mwisho ndio unakufaa...kwa mfano binadamu wote tungekuwa tuna nafsi kamili dhambi wala vifo visingetokea...

Ili ujue nafsi yako ndio roho yako inapotokaa na kuacha mwili kwenye hii dunia....mengine huwezi jua mpaka roho yako itokee...
 
1. Roho ni pumzi au uhai kwenye
mwili.

2: Roho inapatikana sehemu zote za
mwili, kwa kuwa roho ni uhai.

3: Hakuna aliyewahi kuona roho kwa
kuwa haonekani. Ndiyo maana
unaweza kuona mtu hai lakini
huwezi kuona uhai.

4: Hata Moyo pia hufanya kazi kama
kuna roho(uhai) katika mwili. Ndio
maana uhai ukitoweka na moyo pia
unaacha kufanya kazi.

5: Roho Safi ni ile inayowezesesha
matendo yenye mapokeo, na roho
chafu hutenda kinyume chake.

6: Binadamu anapotokwa na roho
hufa kwa sababu roho ndiyo uhai
wenyewe. Hata oxygen pia
hutegemewa kama kuna uhai
mwilini.
 
Kula likes nyingi sana ndg
Huwezi kuiona roho yako kwa macho kwa kuwa si mwili. Nikuulize kidogo ili uweze kunielewa: Je, umewahi kuuona upepo kwa macho? Hata kama hujawahi kuuona lakini sauti yake, matokeo au madhara yake, unayasikia na kuyaona kwa hakika.

Kwahiyo, uwepo wa kitu fulani si lazima ukione kwa macho. Hata sauti hujawahi kuziona lakini unazisikia kwa hakika!

Roho yako ndiyo wewe mwenyewe. Mwili ni koti tu lililoivaa roho, ikitoka unakuwa umekufa. Pia una nafsi (soul) ambayo hujumuisha akili (mind), hisia (emotions) na maamuzi (decisions). Nafsi hubeba utashi (conscience) ambao wanao watu tu, si wanyama.

Unafanya jambo lolote kwa utashi wako, kwa maamuzi yako na mtazamo au mapenzi yako. Tunu hiyo haipo kwa wanyama. Hata mnyama anapokunya hafikirii chochote - kunya kunamtokea tu popote!

Je, umewahi kutokewa ambapo unabishana na wewe mwenyewe? Akili yako inaamua kwenda mahali fulani, lakini ndani yako unasikia sauti ya chini inakukataza usiende! Ukiamua kwenda bila kuitii hiyo sauti ndani yako halafu ukapata shida huko uendako, utaanza kusema roho yangu ilinikataza! Roho yangu ilisita! Roho iligoma kwenda!

Kwahiyo, kila mtu ana sehemu tatu: Roho (spirit), Nafsi (soul) na Mwili wa damu, nyama, mifupa, nk (flesh). Kama hujanielewa nitafute ili nikupe ufafanuzi zaidi kadri Mungu atakavyonijaalia. Pia waweza kusoma 1 Thesalonike 5:23
 
Nafsi na roho ni tofauti kama ulivyo mwili na nafsi

Back
Top Bottom