Genius ni mtu ambaye mwili wake unakaliwa na roho ya mtu msomi iliyotoroka kutoka mbinguni?

Big Shaman

Member
Dec 22, 2014
22
73
Yesu kristo alitoka mbinguni kama roho akaibukia duniani kupitia mimba ya bikra maria, nadhani mnajua mambo makubwa aliyo yafanya.

Roho + mwili = binadamu. Chukulia mfano roho ya marehemu mwenye PhD imerudi duniani kupitia kichanga kilichozaliwa leo unadhani huyo mtoto shuleni atakuaje?

Je, umewahi kusoma na mtu ambaye yeye haingii darasani mara kwa mara na usomaji wake ni wa kulipua lipua tu yeye muda mwingi anakula bata au kuzurula ovyo ovyo ila ukija mtihani anawaacha mdomo wazi kwa kupata alama za juu zaidi.

Je, unadhani ni kawaida kwa mtoto wa darasa la pili kusolve hesabu za form two? au kijana wa form four kupiga pepa la form six PCB akatoka na division one kali?

Tukisema genius ni mtu ambae ana roho ya marehemu msomi iliyochomoka kwa bahati mbaya kutoka mbinguni tutakua tunakosea?

Una maoni gani?
 
Roho ni Roho tu.si lazima iwe ya marehemu.kwanini haujanyoosha maelezo KUSEMA ni mtu mwenye Roho ya maarifa zaidi??

Kutoka 31:2-5
[2]
Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda;
[3]
nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,
[4]
ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba,
[5]
na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom