Roho ni nini na ipo sehemu gani ya mwili?

Moyo una maana mbili tofauti kama ambavyo neno "ua" lina maana tatu tofauti. Kuna ua mmea, ua nyuma ya nyumba, na ua likimaanisha kutoa uhai. Itoshe kusema si kila neno lina maana moja!

Kuna moyo (heart) ambao ni kiungo cha mwili chenye nyama, damu na mishipa. Kuna moyo (heart or spirit) wenye maana ya roho (subconscious being)
Moyo ni nyama...

Roho ipo kihisia zaidi, roho huambatana na nafsi... nafasi huvaa mwili...


Cc: mahondaw
 
Huwezi kuiona roho yako kwa macho kwa kuwa si mwili. Nikuulize kidogo ili uweze kunielewa: Je, umewahi kuuona upepo kwa macho? Hata kama hujawahi kuuona lakini sauti yake, matokeo au madhara yake, unayasikia na kuyaona kwa hakika.

Kwahiyo, uwepo wa kitu fulani si lazima ukione kwa macho. Hata sauti hujawahi kuziona lakini unazisikia kwa hakika!

Roho yako ndiyo wewe mwenyewe. Mwili ni koti tu lililoivaa roho, ikitoka unakuwa umekufa. Pia una nafsi (soul) ambayo hujumuisha akili (mind), hisia (emotions) na maamuzi (decisions). Nafsi hubeba utashi (conscience) ambao wanao watu tu, si wanyama.

Unafanya jambo lolote kwa utashi wako, kwa maamuzi yako na mtazamo au mapenzi yako. Tunu hiyo haipo kwa wanyama. Hata mnyama anapokunya hafikirii chochote - kunya kunamtokea tu popote!

Je, umewahi kutokewa ambapo unabishana na wewe mwenyewe? Akili yako inaamua kwenda mahali fulani, lakini ndani yako unasikia sauti ya chini inakukataza usiende! Ukiamua kwenda bila kuitii hiyo sauti ndani yako halafu ukapata shida huko uendako, utaanza kusema roho yangu ilinikataza! Roho yangu ilisita! Roho iligoma kwenda!

Kwahiyo, kila mtu ana sehemu tatu: Roho (spirit), Nafsi (soul) na Mwili wa damu, nyama, mifupa, nk (flesh). Kama hujanielewa nitafute ili nikupe ufafanuzi zaidi kadri Mungu atakavyonijaalia. Pia waweza kusoma 1 Thesalonike 5:23



Nitakuja kuhoji.
 
Roho huweza kuona ambavyo macho ya mwili hayawezi kuona, hasa jambo au kitu kitakachotokea baadaye. Usishangae kuwa litakalotokea kesho roho yako inalijua leo!

Hata mke wa kuoa au mume wa kuolewa naye, unaweza kumfurahia kwa macho na kuvutiwa na kila kitu leo, lakini roho yako ikamkataa kabisa, na pengine kwa kuugua na kuumia sana jinsi unavyompenda wewe na akili yako, pasina kujua lolote.

Unaweza kushupaza shingo, lakini moto utakapoanza kuwaka ndani ya nyumba baada ya miaka kadhaa ya uvumilivu, utakumbuka na kuanza kusema: ndio maana roho ilisita, iligoma, iliuma, iliogopa, nk.; Inabaki kuwa majuto ni mjukuu!
Na ni kwanini ukifanywa kitu usichopenda roho inauma
 
Umeeleza vizuri sana!
Naomba nijibu la swali # 1, 2, 3, 4 kwa pamoja

Roho ni umbile la pekee lisiloonekana ambalo linasadikiwa kuwemo pamoja na mwili katika binadamu na kuunda hasa malaika (ambao kati yao wale wabaya wanaitwa ma shetani ).
Katika lugha mbalimbali umbile hilo linafananishwa na upepo au pumzi .
Mungu mwenyewe anasadikiwa kuwa roho bora. Kwa namna ya pekee Ukristo unasadiki moja ya nafsi za Kimungu ndani ya Utatu inayoitwa Roho Mtakatifu.
Pengine roho inafikiriwa kueleza tofauti kubwa mno ambayo inajitokeza kati ya binadamu na sokwe na wanyama wengine wote upande wa akili na utendaji, pamoja na ambayo haielezwi vya kutosha na tofauti katika DNA zao.
Inasadikiwa kuwa roho ndiyo sehemu bora zaidi ya mwanadamu na husadikiwa kuwa haifi bali hudumu milele. Roho humuunganisha mtu na ulimwengu wa kiroho ambao aghalabu huwa ni ulimwengu usioonekana na macho ya kawaida, yaani ya mwili.


Waandishi wa Biblia walitumia neno la Kiebrania
ruʹach au neno la Kigiriki, pneuʹma waliporejelea “roho.” Maandiko yenyewe yanaonyesha maana ya maneno hayo. Kwa mfano, andiko la Zaburi 104:29 linasema: “[Yehova] ukiiondoa roho [ ruʹach ] yao, wanakata pumzi, na kurudi katika mavumbi yao.” Andiko la Yakobo 2:26 linasema kwamba “mwili bila roho [ pneuʹma ] umekufa.” Katika andiko hilo “roho” inamaanisha kile ambacho huupa mwili uhai. Bila roho, mwili umekufa. Kwa hiyo, katika Biblia neno ruʹach
halitafsiriwi tu “roho” bali pia “nguvu” au kani ya uhai. Kwa mfano, Mungu alisema hivi kuhusu Mafuriko ya siku ya Noa: “Ninaleta gharika ya maji duniani ili kuharibu kutoka chini ya mbingu wote wenye mwili walio na nguvu [ ruʹach ] za uhai ndani yao.” ( Mwanzo 6:17; 7:15, 22) Hivyo, “roho” inarejelea nguvu isiyoonekana, inayotendesha viumbe vyote vilivyo hai.
Nafsi na roho hutofautiana. Mwili unahitaji roho kama vile redio inavyohitaji umeme ili kufanya kazi. Kwa mfano, unapotia betri katika redio na kuiwasha, nguvu zilizo katika betri huiwezesha redio kufanya kazi. Hata hivyo, redio haiwezi kufanya kazi bila betri. Hali kadhalika, redio ambayo imeondolewa kwenye umeme haiwezi kufanya kazi. Vivyo hivyo, roho ni nguvu ambayo hutendesha mwili wetu. Kama umeme, roho haiwezi kuhisi wala kufikiri. Ni nguvu isiyo na utu. Lakini bila roho au kani ya uhai, “tunakata pumzi na kurudi kwenye udongo,” kama mtunga-zaburi alivyosema.
Andiko la Mhubiri 12:7 linasema hivi linapozungumzia kifo cha mwanadamu: “Mavumbi [mwili wake] huirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho yenyewe humrudia Mungu wa kweli aliyeitoa.” Roho au kani ya uhai inapoondoka mwilini, mwili hufa na kurudi ulipotoka, yaani, kwenye udongo. Vivyo hivyo, nguvu ya uhai hurudi ilipotoka, yaani, kwa Mungu. ( Ayubu 34:14, 15; Zaburi 36:9 ) Hiyo haimaanishi kwamba nguvu ya uhai huenda mbinguni kihalisi. Badala yake, inamaanisha kwamba mtu akifa, tumaini lolote la kuishi tena linamtegemea Yehova Mungu. Ni kana kwamba uhai wake uko mikononi mwa Mungu. Ni kupitia nguvu za Mungu tu ndipo roho au nguvu ya uhai inaweza kurudishwa ili mtu aweze kuishi tena.
Inafariji kama nini kujua kwamba hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya kwa wote wanaopumzika ndani ya “makaburi ya ukumbusho!” ( Yohana 5:28, 29) Wakati wa ufufuo, Yehova atamfanyizia mwili mpya yule anayelala katika kifo na kuuhuisha kwa kutia roho, au nguvu ya uhai ndani yake.
 
Ili kutambua uwepo wa vitu Kama vipo ni aidha viwe vimepita katika sensual organs ( touch, hear, see, sens and smell). Mfano wa upepo hata Kama usipouona utasikia kwa masikio. Kuna vitu unavisikia ila huvioni, Kuna vitu unaviona ila hunisikii na vice versa yake.... Mfano wa upepo na roho ni tofauti huwezi isikia roho Wala iona Wala ishika Wala kuihisi....

ila upepo unausikia kwa upepo tu, na huwezi ku-uona...

Roho unasikia watu wanaizungumza, ukiwauliza wamewahi kuona hamna jibu wanaleta imani za kidini.
Nguvu za uvutano (gravitational force) hujawahi kuziona wala kuzisikia, lakini zipo!!!
 
Back
Top Bottom