Roho ni nini na ipo sehemu gani ya mwili?

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
935
Neno roho kwa wote sio geni sana. Kwa wanaojua wasaidie kujibu maswali, wasitumie imani za dini.

1: Roho ni nini?

2: Roho inapatikana wapi katika sehemu ya mwili?

3: Nani amewahi kuiona roho na inafananaje?

4: Moyo ndio kiungo kikuu Cha binadamu, binadamu akifariki tunasema roho imemtoka na sio moyo umesimama. Kwa Nini? Na roho ikimtoka binadamu inaenda?

5: Roho Safi ikoje na roho chafu zikoje?

6: Kama binadamu anaishi kwa kutegemea hewa Aina ya oxygen, kwanini binadamu roho ikimtoka ndio hufa? Na bado hewa ya oxygen inakuwepo bado.
 
Maswali magumu hayo! Wanatheolojia na wabobez wa philosophy watujuze.
SIMPLe,roho ni uhai,uhai wa roho haushikiki,hauonekani, haufi ni wa milele.uhai wa mwili unaonekana ni wa damu na oxygen ,hufa ni wa muda.muhimu malaika wote wana uhai wa roho hawana wa mwili,wanyama,ndege najamii ya saamaki wana uhai wa mwili hawana uhai wa roho.in mwanadamu peke yake mwenye uhai was mwili na uhai wa roho,eemwanadamu jua kuna moto wa milele na kuna mbingu ya milele..nakusihi tenda mema ungali na uhai was muda wa uhaimwili.
 
Huwezi kuiona roho yako kwa macho kwa kuwa si mwili. Nikuulize kidogo ili uweze kunielewa: Je, umewahi kuuona upepo kwa macho? Hata kama hujawahi kuuona lakini sauti yake, matokeo au madhara yake, unayasikia na kuyaona kwa hakika.

Kwahiyo, uwepo wa kitu fulani si lazima ukione kwa macho. Hata sauti hujawahi kuziona lakini unazisikia kwa hakika!

Roho yako ndiyo wewe mwenyewe. Mwili ni koti tu lililoivaa roho, ikitoka unakuwa umekufa. Pia una nafsi (soul) ambayo hujumuisha akili (mind), hisia (emotions) na maamuzi (decisions). Nafsi hubeba utashi (conscience) ambao wanao watu tu, si wanyama.

Unafanya jambo lolote kwa utashi wako, kwa maamuzi yako na mtazamo au mapenzi yako. Tunu hiyo haipo kwa wanyama. Hata mnyama anapokunya hafikirii chochote - kunya kunamtokea tu popote!

Je, umewahi kutokewa ambapo unabishana na wewe mwenyewe? Akili yako inaamua kwenda mahali fulani, lakini ndani yako unasikia sauti ya chini inakukataza usiende! Ukiamua kwenda bila kuitii hiyo sauti ndani yako halafu ukapata shida huko uendako, utaanza kusema roho yangu ilinikataza! Roho yangu ilisita! Roho iligoma kwenda!

Kwahiyo, kila mtu ana sehemu tatu: Roho (spirit), Nafsi (soul) na Mwili wa damu, nyama, mifupa, nk (flesh). Kama hujanielewa nitafute ili nikupe ufafanuzi zaidi kadri Mungu atakavyonijaalia. Pia waweza kusoma 1 Thesalonike 5:23
 
Huwezi kuiona roho yako kwa macho kwa kuwa si mwili. Nikuulize kidogo ili uweze kunielewa: Je, umewahi kuuona upepo kwa macho? Hata kama hujawahi kuuona lakini sauti yake, matokeo au madhara yake, unayasikia na kuyaona kwa hakika.

Kwahiyo, uwepo wa kitu fulani si lazima ukione kwa macho. Hata sauti hujawahi kuziona lakini unazisikia kwa hakika!

Roho yako ndiyo wewe mwenyewe. Mwili ni koti tu lililoivaa roho, ikitoka unakuwa umekufa. Pia una nafsi (soul) ambayo hujumuisha akili (mind), hisia (emotions) na maamuzi (decisions). Nafsi hubeba utashi (conscience) ambao wanao watu tu, si wanyama.

Unafanya jambo lolote kwa utashi wako, kwa maamuzi yako na mtazamo au mapenzi yako. Tunu hiyo haipo kwa wanyama. Hata mnyama anapokunya hafikirii chochote - kunya kunamtokea tu popote!

Je, umewahi kutokewa ambapo unabishana na wewe mwenyewe? Akili yako inaamua kwenda mahali fulani, lakini ndani yako unasikia sauti ya chini inakukataza usiende! Ukiamua kwenda bila kuitii hiyo sauti ndani yako halafu ukapata shida huko uendako, utaanza kusema roho yangu ilinikataza! Roho yangu ilisita! Roho iligoma kwenda!

Kwahiyo, kila mtu ana sehemu tatu: Roho (spirit), Nafsi (soul) na Mwili wa damu, nyama, mifupa, nk (flesh). Kama hujanielewa nitafute ili nikupe ufafanuzi zaidi kadri Mungu atakavyonijaalia. Pia waweze kusoma 1 Thesalonike 5:23

Ili kutambua uwepo wa vitu Kama vipo ni aidha viwe vimepita katika sensual organs ( touch, hear, see, sens and smell). Mfano wa upepo hata Kama usipouona utasikia kwa masikio. Kuna vitu unavisikia ila huvioni, Kuna vitu unaviona ila hunisikii na vice versa yake.... Mfano wa upepo na roho ni tofauti huwezi isikia roho Wala iona Wala ishika Wala kuihisi....

ila upepo unausikia kwa upepo tu, na huwezi ku-uona...

Roho unasikia watu wanaizungumza, ukiwauliza wamewahi kuona hamna jibu wanaleta imani za kidini.
 
Soma vizuri nilichoandika kuhusu roho (moyo) kisha jihoji mwenyewe kama unayo au la. Nazungumzia moyo usio wa nyama na damu! Mtu akisema moyo uliuma au uliugua haaminishi moyo kiungo cha mwili wa damu na nyama kila mara, bali pia humaanisha roho. Roho iliuma au iliugua!
Ili kutambua uwepo wa vitu Kama vipo ni aidha viwe vimepita katika sensual organs ( touch, hear, see, sens and smell). Mfano wa upepo hata Kama usipouona utasikia kwa masikio. Kuna vitu unavisikia ila huvioni, Kuna vitu unaviona ila hunisikii na vice versa yake.... Mfano wa upepo na roho ni tofauti huwezi isikia roho Wala iona Wala ishika Wala kuihisi....

ila upepo unausikia kwa upepo tu, na huwezi ku-uona...

Roho unasikia watu wanaizungumza, ukiwauliza wamewahi kuona hamna jibu wanaleta imani za kidini.
 
Swali lako ni zuri sana, lakini umeruhusu uwigo mdogo katika kulijibu. Ungeruhusu watu wajibu katika mazingira yote mawili; yaani kiulimwengu huu tulionao na ulimwengu wa kiroho, hapo ndipo ungejuwa roho ni nini. Kwa mtazamo wangu swali lako linajibiwa vizuri kiulimwengu wa roho (imani), lakini kwa bahati mbaya huko wewe hutaki!
 
Hilo swali aliulizwa Mtume Muhammad (S.A.W) miaka kalibu 1600 iliyopita jibu lake liko ndani ya Quruani Tukufu,Mungu anamwambia wambie hiyo Elimu Mimi sina anayejua ni Mwenyezi Mungu.haina tofauti na kuuliza Mungu mambo ya Mungu mfano kabla yake kulikuwa na nini,hiyo Elimu mwanadamu hajapewa, Asalam alekum
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom