Tetesi: Robert Mugabe aanza rudisha mashamba kwa wazungu

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
7,869
16,916
Nimekumbuka jambo hili baada ya kusoma thread hii kwa huyu jamaa ambaye sometime yupo fresh sometime mwezi mchanga. Mh/ Shujaa Kibanga aomba Radhi baada ya Kumpiga Mzungu

inasemekana kutokana na hali ngumu ya kiuchumi zimbabwe rais robert mubabe ameamua kuyarudisha mashamba aliyowapokonya wazungu mikononi mwao. hali imekuwa mbaya kwa mashamba hayo kutokuendelezwa kwa kipindi chote ambacho walinyang'anywa. na hivyo kusababisha baa la njaa kwa nchi hiyo iliyo kusini mwa afrika.

mzee mubabe(mugabe) baada ya kutafakari ameona suluhisho pekee ni kurudisha mashamba hayo kwa wazungu ambao waliweza kuyashughulikia vizuri sana.
 
Maamuzi yanayoongozwa na chuki, visasi au kutafuta umaarufu wa kisiasa bila hesabu za kisayansi ni mauti!. Kama ni kweli naona mzee anaanza kuzaliwa upya kwa maisha mapya!
 
Maamuzi yanayoongozwa na chuki, visasi au kutafuta umaarufu wa kisiasa bila hesabu za kisayansi ni mauti!. Kama ni kweli naona mzee anaanza kuzaliwa upya kwa maisha mapya!
maamuzi ya Mugabe yalikuwa na nia njema tu lakini kwakuwa aligusa maslahi ya wazungu basi wamemkomoa kwa kumuwekea vikwazo lukuki,hata kama wazawa wangeweza kuendeleza hayo mashamba wangeuza wapi?wakati wamewekewa vikwazo?nikitafakari jinsi LIBYA ilivyosambaratika naona hakuna nchi ya AFRIKA hata moja itakuja kuwa nchi tajiri na kuwa moja kati ya nchi zilizoendelea hata kuwe na rasilimali za kila aina.
 
Libya ni ushenzi wa Gadafi kung'ang'ania madaraka na wala hakuna uchawi. Hivi kama angelikuwa anatawala Libya kwa ajili ya wananchi, ni kwa nini hakukubali kufanya demokrasia? Kama angelikubali kuongoza nchi kwa utashi wa wananchi wake, kwa maana ya kufanya uchaguzi wananchi wachague raisi wanayemtaka kwa wakati walipotaka, nayeye akabaki na heshima ya uraisi mstaafu akishuhudia na kushauri mwendelezo wa Libya, yangemkuta yaliyomfika? Walibya Wangeuana? Alidhani ataishi milele? Lazima kufa angelikufa kwa namna yoyote. Je baada ya kufa kwake, Waliby awasingegombana kama ilivyoleo? Kiongozi mzuri ni yule anayetawala na kuliangalia taifa kwa vizazi vijavyo na hivyo kuandaa mfumo sahihi wa maendeleo ya uma na si yale ya faimilia au kundi dogo analotaka yeye kinyume na wenye nchi.

Ni ujinga wa viongozi kudhani uraisi ni utemi.

Mugabe alipashwa kuzijua hizo hesabu kabla hajatwanga maji. . Mugabe siyo Zimbabwe. Kama maamuzi yake yalikuw ani kwa ajili ya Wazimbabwe, kwa nini kung'anng'ani madaraka na kuua watu kwa sana eti wanampiga?

Leo hii Zanzibar watu wakianza kufa na njaa mtalaumu Wazungu? Kila maamuzi yanagharama. Zingatia uwezo wa kufika bei kabla hujatoa order. Makeke bila nguvu ni upumbavu na fedheha!. Sasa yako wapi?

Zilikuwapo njia nyingi sana za kufanya uchumi shirikishi Zimbabwe ambazo kila upande ungenufaika na hatimaye kujenga uwezo mkubwa kwa wazawa zaidi ya ubabe wa kijinga ambao haujalipeleka taifa mahala popote. Na ndiyo sababu haka kazee hakataki kuachia nchi kwa hofu ya hasira za Wazimbabwe kalikowaua kwa kisingizio cha kuwalinda.
 
Hiyo, haiwezi tokea mkuu, yule mzee ana pride na ego kubwa sana ambayo inawa cost sana wananchi wake
 
mugabe apumzike sasa loh au ndo ukurunzinza hivi hao jamaa wanapiga kura ama ndo mpaka huyu yamaa arudi mavumbini afrika hii damnnnnnnnnn
 
Na bado ! huyu mzee chuki zake za kishamba zimesababisha zimbabwe irudi nyuma zaidi ya marehemu , maandiko matakatifu yanasema iko siku tutakuja kuonana na marehemu wetu .
 
IMG-20160110-WA0026.jpg
 
Libya ni ushenzi wa Gadafi kung'ang'ania madaraka na wala siyo suala la nini. Ni ujinga wa viongozi kudhani uraisi ni utemi.

Mugabe alipashwa kuzijua hizo hesabu kabla hajatwanga maji. Leo hii Zanzibar watu wakianza kufa na njaa mtalaumu Wazungu? Kila maamuzi yanagharama. Zingatia uwezo wa kufika bei kabla hujatoa order.
Wazungu wanaendelea kututawala kwa kigezo cha demokrasia,demokrasia siku zote inawagawa watu,siku zote kwenye demokrasia watu hawawi wamoja.Gadafi alikuwa na ubaya wake lakini kungangania madaraka haikuwa tatizo,tatizo alikuwa anatishia maslahi ya wazungu kwa kutaka AFRIKA iungane kuwe na kitu kama UNITED STATE OF AFRICA hiyo ajenda ndio iliomuua sio kitu kingine.
 
Libya ni ushenzi wa Gadafi kung'ang'ania madaraka na wala hakuna uchawi. Hivi kama angelikuwa anatawala Libya kwa ajili ya wananchi, ni kwa nini hakukubali kufanya demokrasia? Kama angelikubali kuongoza nchi kwa utashi wa wananchi wake, kwa maana ya kufanya uchaguzi wananchi wachague raisi wanayemtaka kwa wakati walipotaka, nayeye akabaki na heshima ya uraisi mstaafu akishuhudia na kushauri mwendelezo wa Libya, yangemkuta yaliyomfika? Walibya Wangeuana? Alidhani ataishi milele? Lazima kufa angelikufa kwa namna yoyote. Je baada ya kufa kwake, Waliby awasingegombana kama ilivyoleo? Kiongozi mzuri ni yule anayetawala na kuliangalia taifa kwa vizazi vijavyo na hivyo kuandaa mfumo sahihi wa maendeleo ya uma na si yale ya faimilia au kundi dogo analotaka yeye kinyume na wenye nchi.

Ni ujinga wa viongozi kudhani uraisi ni utemi.

Mugabe alipashwa kuzijua hizo hesabu kabla hajatwanga maji. . Mugabe siyo Zimbabwe. Kama maamuzi yake yalikuw ani kwa ajili ya Wazimbabwe, kwa nini kung'anng'ani madaraka na kuua watu kwa sana eti wanampiga?

Leo hii Zanzibar watu wakianza kufa na njaa mtalaumu Wazungu? Kila maamuzi yanagharama. Zingatia uwezo wa kufika bei kabla hujatoa order. Makeke bila nguvu ni upumbavu na fedheha!. Sasa yako wapi?

Zilikuwapo njia nyingi sana za kufanya uchumi shirikishi Zimbabwe ambazo kila upande ungenufaika na hatimaye kujenga uwezo mkubwa kwa wazawa zaidi ya ubabe wa kijinga ambao haujalipeleka taifa mahala popote. Na ndiyo sababu haka kazee hakataki kuachia nchi kwa hofu ya hasira za Wazimbabwe kalikowaua kwa kisingizio cha kuwalinda.

Ulivyo na akili fupi mbona museven hawamtoi? Mda mwingine weka chuki zako pembeni ueleze ukweli
 
Ulivyo na akili fupi mbona museven hawamtoi? Mda mwingine weka chuki zako pembeni ueleze ukweli

Kila mmoja hutoka kwa muda wake. Angalia mishenzi kama sadam, gadafi, Samwel Do, n.k. Ilitoka siku moja? Kila nchi na kikombe chao. Kinapofurika, ndipo hapo. Siku ya kikombe cha waganda kufurika, utaona ya mseveni. Siku ya kikombe cha Tanzania kufurika, utaona ya ccm, mugabe n.k, Ukombozi hauji siku moja kwa mara moja mahala pote.

Hakuna akili kamilifu inaweza kukimbilia kwenye chuki badala ya kuongelea hoja. Ninaona tatizo,
 
Na bado ! huyu mzee chuki zake za kishamba zimesababisha zimbabwe irudi nyuma zaidi ya marehemu , maandiko matakatifu yanasema iko siku tutakuja kuonana na marehemu wetu .
ukiiangalia ZIMBABWE hata leo hii pamoja na vikwazo vyote walivyowekewa huwezi kuifananisha na Tanzania,sisi tuna hali duni zaidi kuliko ZIMBABWE.
 
Hahahaha poor Mugabe.....bado na Shein atawapigia magoti ngoja wakaze kamba kidogo tu utaona anavyohemea kooni
 
Hii inanikumbusha Nyerere alipojaribu kumtaifisha Tiny Rowland (LONRHO) alipoambiwa hapo ulipopachezea sipo, akasema hatogeuka nyuma kurudisha mali za Tiny akigeuka atakuwa jiwe. Mziki wa Tiny aliokumbana nao baada ya hapo, mwenyewe akasalim amri na kurudisha mali zote za Tiny kimya kimya na fidia juu na hatukuona akigeuka jiwe.

Mugabe nae anaonesha kabana weee sasa mwenyewe anaachia.
 
Wazungu wameifanya afrika kama shamba la kupata malighafi,na kwakuwa waafrika hatujielewi hatutakuja kujikomboa kamwe,umaskini hautakwisha kamwe ili iwe sababu ya sisi kuombaomba ili watuwekee masharti ya kuchukua rasilimali zetu.niambie ni nchi gani ya afrika ina maendeleo na wananchi wake wana maisha mazuri?utakuta ni nchi chache sana na ndogo ambazo hazina malighafi(rasilimali)wazitakazo wazungu,nimesema mwanzo kwamba hakuna nchi ya afrika itakujakuwa katika listi ya nchi zilizoendelea NEVEr.

Nchi za Afrika zenye utajiri wa rasilimali zote zina matatizo na wananchi wake wala hawanufaiki na huo utajiri wa nchi zao.kama hujamuelewa MUGABE wala hujamuelewa GADDAFI na wengine wengi wa aina hiyo,basi wewe hujajielewa kama muafrika,upo upo tu.
 
Back
Top Bottom