Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 31,870
- 33,285
Dah huyu jamaa hapa round about (Lake Oil) nami kaniambia nikienda kituoni na kupata hizo stika atanirudishia buku 5 na elfu 2 za usumbufu. Huu ni mradi wa wakubwa.
Inasiktisha sana
Dah huyu jamaa hapa round about (Lake Oil) nami kaniambia nikienda kituoni na kupata hizo stika atanirudishia buku 5 na elfu 2 za usumbufu. Huu ni mradi wa wakubwa.
Mimi niko ofisi Moja hapa Posta nimeshangaa Sana kumuona Dada mmoja anapita maofisini anapita.... TZ NI N NOMA.Nimekutana na mtu mmoja katika kituo cha kujaza mafuta pale round about ya stand ya daladala Morogoro mjini anauza sticker za wiki ya nenda kwa usalama kwai Tshs 5,000 huku zikiwa zimeandikwa kiasi cha Tshs 3,000, nilipomwuliza kwanini unaziuza wewe raia wakati zilitakiwa zitolewe na kikosi cha usalama barabarani baada ya kufanya ukaguzi wa gari, akanambia hao usalama barabarani ndiyo wameniuzia zote nilizonazo mkononi.
Nimejiuliza swali huu utaratibu wa raia kuuza sticker umelipeleka jeshi la polisi hususani kikosi cha usalama barabarani likizo?
Kuna sababu gani kuuza stucker kama ukaguzi wa magari haufanyiki kama sheria inavyotaka?
Huyo kiongozi wa kikosi cha usalama barabarani aliyempa raia burungutu la sticker aziuze anatambua madhara yake?
Huyo kiongozi anayepaswa kuzitoa sticker hizo kwa magari yaliyo kaguliwa anafanya kazi gani kama kazi yake imekabidhiwa kwa raia?
Mimi niko ofisi Moja hapa Posta nimeshangaa Sana kumuona Dada mmoja anapita maofisini anapita.... TZ NI N NOMA.
Wewe umeiba vingapi!? Mbona hakuna aliyekuletea ukuda.! Take care utapotea.
Ficha upumbavu wako.
Ninaandika barua ya wazi kwa Afande MPINGA Mkuu wa Usalama Barabarani kwa wizi na uonevu unaofanywa na Maaskari wa Usalama Barabarani kituo cha Mpakani mwa Mkoa wa Simiyu na Mkoa wa Mara.
Nilikuwa naenda kuhudhuria mazishi ya Ndugu yangu tarehe 28.2.2015 kule Tarime na nilikuwa na gari dogo la RAVA4. Nilipofika mpakani mwa Simiyu na Mara nikakaguliwa na askari namba G.9368 wa Usalama Barabarani.
Baada ya ukaguzi akanieleza kuwa sina STIKA na mimi nikakubali. Nikamweleza kagua gari na nilipie stika. Nikamuuliza kuwa stika ni shillingi ngapi?.
Akanieleza kuwa stika ni tshs.10,000 mimi nikamueleza kuwa mbona stika ni shs.2,000 na ukichelewa kama mimi inaweza kuwa tshs.5,000.
Yeye akanieleza kuwa nitoe tshs.10,000 ndipo anipe stika. Mimi nikagoma na baadaye akasema sasa ninakulipisha faini ya tshs.30,000 kwa kukosa stika.
Nikakubali sawa lakini nipe risiti. Yeye akanieleza kuwa hana risiti ila nitoe tshs.30,000. Nikamuuliza je faini si fedha za Serikali?. Akashindwa la kusema.
Baadaye nikaandikiwa kosa kwa ahadi ya kuchukua risiti kesho yake. Kesho yake nikafuatilia risiti kwa binde ndipo nikaipata.
Maaskari wa Usalama Barabarani wa kituo cha NASA na mpaka wa Simiyu na Mara wanaiibia Serikali sana kwa sababu hawatoi risiti pindi mwenye gari anapopatikana na kosa na fedha wanaweka mfukoni.
Nakushauri Afande MPINGA maaskari wote kwenye vituo nilivyovitaja wavuliwe vyeo mara moja na kuwa Maaskari wa kawaida.
Kwanza wanatesa sana wasafiri na siyo waaminifu mbele ya umma. Hasa Askari namba G.9368 wa kituo cha Wilaya ya Busega afukuzwe kazi mara moja.
Nimeamua kuchagua upumbavu..!
Hakika hii nchi ina wapuuzi. Kosa la nani? Babu au baba?