Ninaandika barua ya wazi kwa Afande MPINGA Mkuu wa Usalama Barabarani kwa wizi na uonevu unaofanywa na Maaskari wa Usalama Barabarani kituo cha Mpakani mwa Mkoa wa Simiyu na Mkoa wa Mara.
Nilikuwa naenda kuhudhuria mazishi ya Ndugu yangu tarehe 28.2.2015 kule Tarime na nilikuwa na gari dogo la RAVA4. Nilipofika mpakani mwa Simiyu na Mara nikakaguliwa na askari namba G.9368 wa Usalama Barabarani.
Baada ya ukaguzi akanieleza kuwa sina STIKA na mimi nikakubali. Nikamweleza kagua gari na nilipie stika. Nikamuuliza kuwa stika ni shillingi ngapi?.
Akanieleza kuwa stika ni tshs.10,000 mimi nikamueleza kuwa mbona stika ni shs.2,000 na ukichelewa kama mimi inaweza kuwa tshs.5,000.
Yeye akanieleza kuwa nitoe tshs.10,000 ndipo anipe stika. Mimi nikagoma na baadaye akasema sasa ninakulipisha faini ya tshs.30,000 kwa kukosa stika.
Nikakubali sawa lakini nipe risiti. Yeye akanieleza kuwa hana risiti ila nitoe tshs.30,000. Nikamuuliza je faini si fedha za Serikali?. Akashindwa la kusema.
Baadaye nikaandikiwa kosa kwa ahadi ya kuchukua risiti kesho yake. Kesho yake nikafuatilia risiti kwa binde ndipo nikaipata.
Maaskari wa Usalama Barabarani wa kituo cha NASA na mpaka wa Simiyu na Mara wanaiibia Serikali sana kwa sababu hawatoi risiti pindi mwenye gari anapopatikana na kosa na fedha wanaweka mfukoni.
Nakushauri Afande MPINGA maaskari wote kwenye vituo nilivyovitaja wavuliwe vyeo mara moja na kuwa Maaskari wa kawaida.
Kwanza wanatesa sana wasafiri na siyo waaminifu mbele ya umma. Hasa Askari namba G.9368 wa kituo cha Wilaya ya Busega afukuzwe kazi mara moja.