Mambo ya Ajabu Yaliyompata Allan Quatermain na Wenzake.
Leo nitadonoa kidogo Hadithi ya Allan Quatermain, Simulizi za Sir H. Rider Haggard kwenye moja ya simulizi zake zinazo elezea visa vya mwindaji Tembo hodari Bwana Allan Quatermain.
allan Quatermain (Makumazan or Macumazahn)... Na msaidizi wake Msolopagazi (Umslopogaas) na shoka lake Inkosi kazi (Inkosi-kaas)... Bwana Henry Curtis, na rafikie Siri Good, (Bwana Mzuri).
Kwenye riwaya hii ndipo pia lilipo patikana jina Gagula... Kibibi kilichokuwa kichawi (Kigagula).
Vitabu hivi ni miongoni mwa vitabu ambavyo vinaonyesha au kusimulia ujasiri na ushujaa wa hali ya juu sana... Soma pia riwaya ya Machimbo ya Mfalme Suleiman na nchi ya Wakukuana... Na vitabu vyake vingine ambavyo havikuwahi kutafsiriwa kwa kiswahili kama vile SHE, Ayesha, The Virgin of the Sun na Vingine vingi. Gonga HAPA kupata orodha ya vitabu vyake.
Wale waliowai kusoma Hadithi ya Allan Quatermain watamkumbuka sana Bwana Mslopagazi (Umslopogaas), na majigambo yake a.k.a Mikwara mizito aliyokuwa akiwatishia maadui zake...!
Basi tega sikio, nikumegee japo kidogo.
Mkuu nalijua ilo la bibi Kigagula kuwemo kwenye simulizi ya Machimbo ya Mfalme suleiman, hapo nilitaka kuandika kwa ujumla yaani "riwaya hizi" na ndipo vidole vikasahau kuchapa vema, ah ah ah ah.Kibibi Gagula yupo kwenye King Solomon mines (machimbo ya mfalme Suleiman).
Thanks kwa kunikumbusha stori hizi. Nakumbuka kwenye hii ya umsolopagaas, alipomwona Makumazha, aliongea risala fulani "mkuu, mkuu, mkuu, Makumazhan.... unakumbuka ...ilivyoua tembo..." Hapa ilikuwa kabla hawajaanza safari ya kuingia bara ambako ndiko walikutana na wajivuni, baadaye kupotea kwa kuchukuliwa na mto hadi kuingia nchi ya wazuvendi.
Zilikuwa stori nzuri kuliko hizi za kwenye globalpublishers.
Mkuu nalijua ilo la bibi Kigagula kuwemo kwenye simulizi ya Machimbo ya Mfalme suleiman, hapo nilitaka kuandika kwa ujumla yaani "riwaya hizi" na ndipo vidole vikasahau kuchapa vema, ah ah ah ah.
Enzi hizo wale jamaa waliokuwa wanajifanya wao bab'kubwa tukiwaita kwa majina mbali mbali, mojawapo ni ili kutoka simulizi ya Allan Quertamain... "Mpaya paya"
Ah ah ah ah, mkuu, unanichekesha, wasome vitabu na muda wa kucheza video game wamuachie nani, yaani wasome vitabu wapitwe na tamthilia za Eastender, Rebeka, shades of Sin, don't Mess with an Angel na Isidingo!?Poa mkuu.
Tupo pamoja.
Hivi umegundua vijana siku hizi hawasomi vitabu?
Tunatakiwa kufanya juhudi za makusudi ili kuwahamasisha wasome hadithi kama hizi na zingine. Vitabu vinafundisha ujanja, na vinaboresha lugha.
Anyway, thanks again for the thread.
jamani nakala ya kitabu hiki inapatikana?