Riwaya: UCHU

"Pepe mpenzi".
"Uko wapi", Pepe aliuliza.
""Niko Kampala narudi kesho".
"Ooh Mungu wangu, toka umeondoka
sijapata usingizi. Njoo mume wangu
nina
hamu sana na wewe, nakupenda sana".
"Na mimi zaidi, kesho mama, kwaheri",
Willy akakata simu.
Bibiane alikuwa akisikia lakini alijifanya
kama hamsikii alimgeukia Willy na
kusema. "Uko wapi Willy?, njoo ulale,
najua siku yangu ni leo tu, hivyo lazima
niitumie siku hii kikamilifu".
"Katika nafsi yangu hupenda mtu
anayeelewa mambo kama wewe", Willy
alijibu huku akirudi ndani ya shuka na
kumkumbatia Bibiane.

KWELI NDOA NI JINA TU UKIWA NA MUME HAPO UBAVUNI MWAKO
 
hope uchu umewaisha sasa. nawashukuru kwa uvumilivu wenu tangu mwanzo mpaka hapa tulipofikia. waliokwazika poleni sana tusameheane tusonge mbele naimani mambo mazuri mengi yanakuja.

ukweli ni kwamba ulituboa, hasira zikapanda, ndita zikatanda kwenye nyuso zetu. nilipogundua siwezi kukufanya lolote, nikawa mdogo kama piliton, nikakubali uniendeshe utakavyo, maana mwisho wa siku ni hisani tu.

Mungu akubariki. usituchoke ndugu yangu. naisubiri kikosi cha kisasi au tutarudi na roho zetu mkuu
 
Hongera ndg kidikudi
japo ulikuwa ukiondoka unachelewa kurudi
Nasi kukusubiri hatukuwa na budi
kwa sababu uchu ulikuwa umetuzidi
ugonjwa wetu ni zaidi ya homa za vipindi
hata mua ukianza kuulia chini jua kuna tindi
Ulitingwa na mambo hukufanya makusudi
Ulitupa kitu kwa uhakika hukufanya ilimradi
wacha nimalizie pongezi mkuu kidikudi.
 
kidikudi nakupongeza sana kwani vitabu ivi adimu sana kama una riwaya "tutarudi na roho zetu"tupia mkuu
 
Riwaya hizi ni moto wa kuotea mbali. Weka mbali na wanafunzi kupindi cha mitihani. Vinginevyo kufeli ni njenje.
 
Back
Top Bottom