Riwaya: UCHU

Riwaya: UCHU

Sikiliza Gamba 1 nimetafuta hiki kitabu nimekosa hebu nielekeze kinapatikana wapi?
 
Nipo dar nahangaikia hicho kitabu

Mkuu ni vigunu sana kupata hivyo vitabu (almost impossible) tuendelee kuwapigia magoti hawa akina Willy Gamba 1, kidi kudi, mareche, m2n washushe hapa hapa jamvini.
 
Mkuu ni vigunu sana kupata hivyo vitabu (almost impossible) tuendelee kuwapigia magoti hawa akina Willy Gamba 1, kidi kudi, mareche, m2n washushe hapa hapa jamvini.

Inauma sana
 
Imeisha!Musiba sijui kwa nini hakuendelea na hii story
 


KASHESHE
III


Willy aliangaliana na Bibiane. "Unasemaje
tuwasaidie hawa ama vipi?", Bibiane
aliuliza.
"Hapana tuendelee na mipango yetu. Hii
imekuwa bahati nzuri kwetu, naamini
Meja Kasubuga ana uwezo wa kuukabiri
uvamizi huu, na nahisi walengwa wa
uvamizi huu ni sisi tunatafutwa, huenda
kikosi cha Col. Gatabazi kimesikia ama
kuhisi kuwa tuko hapa. Wakati wao
wanatusaka hii itatupa nafasi nzuri,
kwanza kumtoroka Meja Kasubuga na pili
kuendelea na mipango yetu. Panda gari
twende zetu Kibumba tukawasake hawa
majahiri", Willy alieleza huku wakipanda
gari na kuondoka kwa kasi kuelekea
Kibumba.

IV
Wakati kikosi cha Nkubana kikisonga
mbele kuelekea hoteli Meridien-Izuda
kilishitukiwa na askari mmoja wa doria
ambaye baada ya kusikia nyayo za watu
zisizo za kawaida akapanda juu ya mti na
kuchungulia chini ya kjinjia kilichotelemka
kutoka mlimani kuelekea hotelini.
Akisaidiwa na mbalamwezi askari hjuyu
aliweza kukiona kikundi cha askari
kadhaa kikielekea hotelini hapo, baada ya
kuthibitisha kuwa walikuwa askari wa
adui na jinsi walivyokuwa wakisonga
mbele kwa tahadhari kubwa huku silaha
zao zikiwa zimewekwa tayari kwa
mashambulizi.
Huyu askari wa doria alitelemka kwenye
mti haraka haraka na kimya ili
asiwagutue wale wavamizi waliokuwa
hatua kumi tu karibu na ule mti na kwa
kutumia uzoefu wa sehemu ile alikimbia
kwa kutumia njia za mkato na kwenda
kutoa taarifa kwa kikosi kilichokuwa
kwenye maandalizi ya kuondoka kuelekea
mpakani kisiondoke kwani kulikuwa na
uvamizi.
"Kuna kikosi cha adui kinaweza
kutushambulia sasa hivi, kimetumia
kichochoro namba tatu na kitafika hapa
sasa hivi, askari huyo alimweleza Mkuu
wa kikosi hicho Sajenti Ibrahim.
"Oke, wewe kimbia kwa Afande Kasubuga
umweleze wakati sisi tunaelekea huko
kuwasimamisha mpaka tupate msaada",
Sajenti Ibrahim aliamru na palepale
akawaamru askari wake waweke silaha
zao tayari na kusonga mbele kuelekea
kichochoro namba tatu. Njia zote
zilizokuwa zinaelekea kwenye hoteli hii
zilipewa namba ili iwe rahisi kuzitambua
kwani zilikuwa nyingi. Yule askari wa
doria alikimbia mpaka ofisini kwa Meja
Kasubuga lakini hakumkuta, kwani ndio
wakati Meja Kasubuga alikuwa
amewasimamisha Willy na Bibiane
wasiondoke, na kabla hajajuwa ampate
wapi na yeye alisikia milio ya bunduki
akajuwa tayari mapambano yameanza.
Sajenti Ibrahim na kikosi chake
walifanikiwa kuwaona wale askari
wavamizi wakisonga mbele kuelekea
hotelini na kwa vile hakujuwa walikuwa
na nguvu kiasi gani aliamru askari wake
waanze kushambulia hata bila kulenga
shabaha kwa uhakika ili kuwatia kiwewe.
Na kweli hii ilimshitua Nkubana kwani
hakutegemea kukutana na upinzani
haraka kiasi hicho kutokana na maelezo
ya yule askari muasi.
"Luteni Nyamboma", Nkubana alimwita
msaidizi wake, "Wewe endelea kukabiliana
na hawa adui zetu ili mimi na askari
watano tuweze kupata mwanya wa
kwenda kumkamata Willy. Fanya
mashambulizi makubwa ili askari wote
wafikiri kuwa wanashambuliwa na kikosi
kikubwa ili wote waje upande huu na sisi
tupate urahisi pale Willy alipo".
"Sawa, nimekusoma Kamanda",
Nyamboma alijibu.
Nkubana aliwachagua askari watano
wazuri pamoja na yule kikaragosi wao.
"Wewe tupeleke chumba cha yule mtu,
tumia uzoefu wako wa hapa".
"Sawa afande, yule askari alijibu huku
akitetemeka maana alistaajabu namna
walivyokuwa wamebainika na kuonekana
kwa adui mapema namna ile.
Mapigano makali yalianza na, kama
Nkubana alivyotaka, askari wengi wa
kambi ile walielekea upande wa mapigano
kuongeza nguvu wakiongozwa na
kiongozi wao Meja Kasubuga. Nkubana
na askari wake hawakupata kikwazo
mpaka walipofika kwenye chumba
alichopangiwa Willy.
Baada ya Nkubana kushuhudia umahiri
wa Willy Kigali, hakutaka kufanya makosa
tena. Aliwapanga askari wake vizuri na
kwa hadhari kubwa, walipofika kwenye
chumba cha Willy na kwa amri moja
wakaupiga mlango kwa nguvu zao zote
na askari wawili wakaingia na mlango
ndani ya kile chumba. Chumbani
hawakumkuta mtu isipokuwa mikoba
miwili iliyokuwa na nguo, Nkubana
akautambua mkoba mmoja kuwa ulikuwa
wa Bibiane, maana alipata kuuona pale
sebuleni kwa Bibiane mjini Kigali.
"Watakuwa wapi hawa?", Nkubana alihoji,
kisha akaendelea. "Wanaweza kuwa
wamejiunga na askari wa hapa
wanaopigana na kikosi chetu au
wamevuka mpaka".
Yule askari kikaragosi alikuwa ametoka
nje na akarudi na kusema. "Gari lao
halipo, nafikiri wamekimbia mapigano".
Nkubana aliposikia hivyo woga
ulimwingia kwani alijua mtu huyu
amevuka mpaka. "Itatubini na sisi tuvuke
mpaka sasa hivi. Wao wameondoka na
gari sisi itabidi twende kwa miguu sasa",
Nkubana aliamru huku ule upande wa
mapigano makali yalikuwa yakiendelea.
"Itabidi turudi kuongeza nguvu", askari
mmoja alishauri.
"Hapana, Luteni Nyambona ana ujuzi wa
kutosha, akiona amezidiwa atarudi nyuma
na kukimbilia mpakani. Huu ni wakati
mzuri kwetu kuondoka kuwafuata hawa
washenzi", Nkubana alijibu huku
wakiondoka kuelekea mpakani.

V
Usiku ule Willy na Bibiane walipokuwa
wakielekea kwenye mpaka wa Rwanda na
Zaire, mbalamwezi iling'aa sana na
kuyaonyesha mandhari safi ya milima ya
Volkano ya Virunga.
Milima hii ilijulikana toka zama za kale,
ambapo hata Wagiliki wa zamani
waliizungumzia sana milima hii wakiita
milima ya mwezi. "Sasa wewe mwenyewe
unaweza kuona kwanini waliita hivyo",
Willy alimsimulia Bibiane.
"Inaonekana wewe umesoma sana
historia", Bibiane alieleza.
"Unajuwa kitu chochote hakiwezi kuwa
kitu bila historia. Ili uijue dunia hii lazima
ujue historia. Hata binadamu hawezi kuwa
binadamu kama hana historia. Ndio
maana mimi nikikwambia naitwa Willy,
lazima utaniuliza Willy nani, nitakujibu
Willy Gamba. Halafu utataka kujuwa baba
yangu anatoka wapi halafu nitakwambia.
Hii yote ni kutaka kujua historia yangu ili
uweze kujua namna utakavyoniweka.
Hata nchi. Nchi isiyokuwa na historia si
nchi. Haiwezi kuwa na maendeleo. Sijui
kama umenielewa vizuri mpaka hapo?",
Willy alijibu na kuhoji.
"Nimekuelewa vizuri sana Willy. Kwa
muda huu mfupi nitakaokuwa na wewe
hakika nitajifunza mambo mengi", Bibiane
alimwambia Willy.
"Sasa walikuwa wanakaribia sana
mpakani, na Bibiane akasema.
"Tukivuka mpaka tu, lazima tutakutana na
kikosi cha jeshi la Zaire, Unasemaje?".
"Unazijuwa njia nyingine tunazoweza
kukwepa mambo ya mpakani?", Willy
aliuliza.
"Ndiyo Willy, na ndio sababu nimesema
hivyo, hapo mbele utakata kulia
nitakuonyesha njia ya siri wanayotumia
wapelelezi wa Akazu, lakini tuwe na
tahadhari kubwa. Willy akakata kulia
baada ya mwendo wa dakika kadhaa
mara njia iliisha. Kukawa na njia ya
majani tu. "Endelea tu. Ukikata tena
kushoto. Tutakuwa tayari tuko Zaire. ni
kilomita kama moja tu kutoka hapa",
Bibiane alimwambia Willy, baada ya
kutembea mwendo wa kilomita moja na
baada ya kupita sehemu ya miti mingi
walitokea mahali pa wazi na upande wa
kushoto wakaona taa zinawaka.
"Pale ndio mpakani upande wa Zaire na
ile ni kambi ya jeshi la Zaire", Bibiane
alieleza.
"Tunaweza kupata magari ya jeshi pale?",
Willy alimuuliza Bibiabe.
"Lazima. Unataka tukaibe gari moja la
jeshi?", Bibiane alihoji.
"Unasoma sana mawazo yangu. Tusiibe,
tukachukue tu?", Willy alijibu na
kuendelea. "Ili tusije tukatia shirika la
Msalaba Mwekundu dosari, yafaa tusiwe
na gari lao kwenye uwanja wa
mapambano. Hapa tutapata mahali pazuri
pa kulificha halafu tukachukue gari la
jeshi la Zaire. Itakuwa vilevile vigumu
kusimamishwa na askari hovyohovyo".
"Je kuhusu nguo itakuwaje?", Bibiane
alihoji tena kwa shauku.
"Kuhusu nguo tutawavua askari walioko
mpakani". Willy alisema huku Bibiane
akicheka sana.
"Wewe una mambo. Mbona naanza
kusikia raha, usiku huu naona itakuwa
kasheshe tupu", Bibiane alinena.
Walitafuta sehemu iliyokuwa na msitu
wakalificha gari la Msalaba Mwekundu na
kuitoa mizigo yao. Gari lilifichika vizuri
sana kiasi kwamba ingekuwa vigumu mtu
kuligundua mara moja.
"Tutalipitia kabla jua halijachomoza", Willy
alinena.
"Kama tukiwa hai", Bibiane alijibu.
"Ili uweze kubaki hai fikiri kuwa utakuwa
hai. Na ukiwa hai ukifikiri utakufa. Utakufa
tu", Willy alifafanua.
"Sawa bosi. Tutarudi hapa kwenye gari
letu tukiwa hai", Bibiane alisema.
"Mawazo safi kabisa", Willy aliongeza.
Wakiwa wamebeba silaha zao na kila kitu
walichohitaji kwa mapambano usiku ule
walianza kuinyemelea ile kambi ya jeshi
mpakani Zaire. Walipofika pale kituoni
waliyaona magari matatu ya jeshi aina ya
Landrover ya wazi nyuma yakiwa
yameegeshwa. Walipoangalia vizuri
waliwaona askari watatu. Kila mmoja
akiwa ameegemea kwenye gari lake.
"Hao watakuwa madereva wa hayo
magari", Bibiane alibobota kwa sauti ya
chini.
"Hata mimi nafikiri hivyo, nahisi yalikuwa
yamewachukua wale askari
walioshambulia kule Meridiane hoteli,
maana inaonekana hawa askari
wanaosubiri watu", Willy alijibu.
Kwa vile yale magari yalikuwa karibu na
ua wa michongoma na pale mahali. Willy
alifikiri namna ya kuwashambulia bila ya
kuwagutusha watu wengine pale kikosini.
Mara akawaona askari wote wanakuja
kuzungumza na yule askari aliyekuwa
kwenye gari la mwisho karibu kabisa na
ua.
"Bibiane kazi kwako, hapohapo wewe
mshambulie yule wa kushoto. Mimi
nitamalizana na wale wawili. Wa kati na
kulia", Willy aliagiza huku hawa askari
wakiwa sasa wameegemea kwenye
magari yao huku wameipa visogo sehemu
ile waliyokuwa wamejibanza akina Willy.
"Wale tutumie bastola zenye kizibo
tusipoteze muda", Bibiane alishauri.
"Hapata, tunahitaji kila risasi tuliyonayo
isipotee bure, pale ambapo tunaweza
kulinda risasi nashauri tutumie njia
nyingine, au unaogopa hutaweza
kumkaba sawasawa?", Willy alimuuliza
Bibiane.
"La, hasha! naweza sana Willy na wewe
mwenyewe utanishuhudia leo; haya
twende", Bibiane aliamru.
Huku wakitambaa chini kama nyoka,
waliwanyemelea wale askari. walipofika
usawa wa gari la kwanza Willy alisema.
"Sasa", wote wawaili walirukia na bila
kuwapa nafasi hata ya kushituka, Willy
aliwapiga wawili karate kwenye vichwa
akitumia mikono yake miwili na kupasua
vichwa vyao palepale. Bibiane alimrukia
yule wa kushoto na kumbana shingo na
kisha kuikata kwa mikono yake. Hawa
askari waliuawa kama kondoo.
Hawakutoa upinzani wa aina yoyote,
huenda kwa vile hawakutegemea
kushambuliwa kama lile mahali pale.
Kisha walizivuta maiti zao mpaka nyuma
ya ua, wakawavua zile sare za jeshi na
kuzivaa haraka haraka. Bibiane
alichekelea sana maana zilikuwa kubwa.
Hata hivyo akazifungafunga zikamwenea
hivyohivyo.
"Utaweza kukimbia ama kupigana na adui
ukiwa na magwanda haya?", Willy
alimuuliza Bibiane huku akicheka.
"Tena ndio mazuri zaidi hasa kwa judo na
karate", Bibiane alijibu.
Willy na Bibiane walibeba mizigo yao na
kisha wakachungulia ndani ya magari na
kukuta la gari la katikati likiwa na funguo.
Waliweka mizigo yao ndani na kuliwasha
na kisha kuondoka. Walipoangalia saa
ilikuwa yapata saa nne na nusu usiku.
Waliondoka bila mtu yeyote pale kuhisi
kitu. "Moja kwa moja Kibumba", Bibiane
alisema.

ITAENDELEA
 
shukran kidikudi mdogo mdogo tutafika safari ni hatua
 
duh kidi kudi, kila ninaposoma episode hizi roho hunienda mbio. Tafadhalializa kitu hii
 
Back
Top Bottom