Riwaya: Siri

SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 7
Geti la kambi ya kikosi
cha operesheni maalum
likafunguliwa na gari la
akina Mathew
likapita.Tayari walikwisha
wasiliana na Austin na
kumjulisha kuwa
wanakwenda kuanza
mahojiano na Edger
Kaka.Wote wakazima simu
zao kwani ukiwa ndani ya
kambi ile huruhusiwi
kutumia simu ya mkononi
bali zipo simu maalum
unazoweza kutumia
kupiga.Walifika hadi katika
jengo la utawala
wakapokewa na kuongozwa
moja kwa moja hadi katika
ofisi ya Austin
“Karibuni tena ndugu
zangu”akasema Austin
“Ahsante
Austin.Utatuwia radhi kwani
tutaendelea kuwa wageni
wako na tutafika hapa mara
kwa mara kila pale
tutakapokuwa na uhitaji na
mtu wetu”
“Mathew msijali
tafadhali kuweni na
amani.Hili ni suala la kitaifa
hivyo basi lazima
tuhakikishe linakamilika”
“Ahsante sana
Austin.Tumelazimika
kurejea tena kuja kuanza
kumuhoji Edger.Usiku wa
kuamkia leo watu wa IS
wamevamia na kuteka
wasichana sitini na sita
katika shule ya sekondari ya
St Getrude na lengo kubwa
la kuwateka wasichana hao
ni kumshinikiza Rais aweze
kumuachia Edger Kaka”
akasema Mathew
“Wana uhakika kama
Rais anafahamu mahala
alipo Edger? Akauliza Austin
“Hawajui chochote
kuhusu Edger Kaka kama
alitekwa na Mossad na
alikuwa Nairobi,wao
wanaamini yuko hai na
mchezo ule ulifanywa na
serikali ya Tanzania ndiyo
maana wanatumia kila njia
kushinikiza Rais aweze
kumuachia mtu wao”akajibu
Mathew
“Saa mbili kamili za
asubuhi watampigia simu
Rais kujua kama tayari
amekwisha muandaa Edger
na kama hatatekeleza hilo
basi wataanza kuwaua wale
wasichana.Tumelazimika
kuja tena hapa kumuhoji
Edger Kaka atusaidie
kufahamu mtandao wao
hapa nchini ili tuweze
kuwaokoa wale wanafunzi
pamoja na mtoto wa Rais”
akasema Mathew
“Sawa Mathew
nimekuelewa hapa tuna
chumba maalum kwa ajili ya
mahojiano mtakitumia
chumba hicho kumuhoji
Edger na kama mkihitaji
kuingia katika hatua
nyingine zaidi ya kutumia
nguvu kipo chumba maalum
kwa ajili hiyo na wapo
wataalamu wa kuifanya hiyo
kazi” akasema Austin huku
akiinuka
“Tunaye mtaalamu wetu
wa kutesa ambaye ni Gosu
Gosu.Hakuna aliyewahi
kuingia katika mikono yake
akashindwa kufungua
mdomo wake lakini kwa afya
ya Edger Kaka tunataka
kwanza kumuhoji bila
kutumia nguvu” akasema
Mathew wakatoka mle ofisini
na Austin akawaongoza hadi
katika chumba cha
mahojiano kulimokuwa na
meza na viti viwili.Mathew
akaingia mle ndani na baada
ya dakika tatu Edger Kaka
akiwa amefungwa pingu
mkononi akaingizwa ndani
ya kile chumba akiwa
anasukumwa katika basikeli
ya magurudumu kwani bado
hakuwa na uwezo wa
kutembea.Mathew akaamuru
afunguliwe mikono abaki
huru na watu wote watoke
nje akabaki na Edger,
akamtazama kwa sekunde
kadhaa halafu akasema
“Edger Kaka pole sana
kwa masahibu yote
yaliyokupata kwa muda wa
miaka mitatu.Lakini yote
hayo yamekwisha sasa
umerejea
nyumbani.Unajisikiaje
kurejea tena nyumbani?
Akauliza Mathew.Edger
akajaribu kuzungumza lakini
sauti ikamkwama Mathew
akaomba kuletewa maji
Edger akanywa
“Sasa niambie Edger
unajisikiaje kurejea
nyumbani ? Akauliza
Mathew
“Unataka nikwambie
nina furahi?I’m not happy at
all.Mlikosea sana
msingesumbuka kuja
kunikomboa na kunirejesha
tena Tanzania” akasema
Edger kaka
“Kwa nini unasema hivyo
Edger? Hupendi
Tanzania?Hupendi kurejea
nyumbani? Akauliza Mathew
“Because I’m dead
already.Nimeonyeshwa video
ya mazishi yangu namna
watu walivyonililia wakijua
nimefariki dunia wengine
wakipoteza fahamu baada ya
kupita katika jeneza ambalo
waliamini kuna maiti yangu
lakini kumbe ulikuwa ni
mchezo
umetengenezwa.Imeniumiza
sana baada ya kulifahamu
hilo jambo na siwafichi
ninatamani hata sasa
mnipige risasi nife niondoke
kabisa katika dunia hii”
akasema Edger
“Edger waliofanya tuko
lile si Tanzania bali ni Israel
wakitumia shirika lao la
ujasusi la Mossad na ndiyo
maana baada ya kufahamu
kwamba uko hai tukafanya
kila lililo ndani ya uwezo
wetu kukukomboa na
kukurejesha
nyumbani.Tumetengeneza
mgogoro mkubwa sana wa
kidiplomasia kati yetu na
Israel kwani tumelazimika
kuua watu wao wengine wa
muhimu kabisa ili tuweze
kukukomboa.Naweza
kusema kwamba serikali ya
Tanzania kwa kukuthamini
imetumia gharama kubwa
kukukomboa na kukurejesha
nyumbani.Unapaswa
kufurahi”akasema Mathew
“Ninashukuru kwa
kunitoa katika nyumba ile ya
mateso lakini haikuwa na
ulazima wowote wa kutumia
gharama kubwa
kunikomboa”akasema Edger
“Edger wewe ni
mtanzania na ilikuwa lazima
kwa gharama zozote zile
tukurejeshe
nyumbani”akasema Mathew
na kumtazama Edger kwa
sekude kadhaa halafu
akasema
“Edger unaweza
ukatueleza sababu za Israel
kutumia gharama kubwa
kutengeneza kifo chako
wakati bado uko
hai?akauliza Mathew na
Edger akabaki kimya
“Nijibu Edger swali
nililokuuliza”
“Sifahamu chochote”
akasema Edger
“Edger jina langu
ninaitwa Mathew Mulumbi
ndiye niliyeongoza
operesheni ya kuja
kukukomboa na kukurejesha
nyumbani.Hapa uko sehemu
salama na mateso yote
uliyoyapata kwa miaka
mitatu yamekwisha.Hapa
ndipo patakuwa chimbuko la
maisha yako
mapya.Mheshimiwa Rais
anafahamu kuwa uko hapa
na ndiye aliyetoa kibali cha
kufanya operesheni ile ya siri
ya kukukomboa na yuko
tayari kukufanyia kitu
chochote unachokihitaji ili
uanze maisha yako upya
lakini amenituma hapa
kwako nije kuzungumza
nawe ili tuufahamu ukweli
wote kwa nini ulitekwa na
Israel?Usihofu hapa uko
sehemu salama na hakuna
anayefahamu kama uko hapa
hivyo kuwa huru”akasema
Mathew na Edger
akainamisha kichwa
akazama mawazoni
“Edger please usiipoteze
hii nafasi uliyoipata.Hii ni
tiketi ya kuelekea maisha
mapya hivyo itumie
kikamilifu” akasema Mathew
“Sifahamu chochote kwa
nini waliniteka nyara na
kunipa mateso yale makali
kwa miaka mitatu.Watu
wale ni wanyama mno!
Akasema Edger na sura ya
Mathew ikaanza kubadilika
“Who is Habiba Jawad?
Akauliza Mathew na Edger
akastuka
“Umesema nani?
“Habiba Jawad ni nani?
“Si..simfahamu” akajibu
Edger.Mathew akamtazama
kwa macho makali
“Edger Kaka narudia
tena kauli yangu kwamba
hapa panaweza kuwa
chimbuko la maisha yako
mapya au panaweza kuwa ni
mwisho wa maisha yako
hivyo ni jukumu lako
kuchagua nini unakitaka
kuishi au kufa.Mimi
ninayezungumza nawe hapa
ninamuwakilisha Rais hivyo
sihitaji mzaha.Ninapokuuliza
nataka unipe majibu ya
kweli kama ukitaka kuwa
kiburi nakuhakikishia
hautafika kokote
Edger.Mateso uliyoyapata
nchini Kenya kwa miaka
mitatu yanatosha sana
hatutaki kuendelea kukutesa
hata hapa nyumbani hivyo
funguka,kuwa mkweli
tueleze nini kilitokea na sisi
tutajua namna ya
kukusaidia.We need
information from you”
akasema Mathew
“Mathew
Mulumbi,right?akauliza
Edger
“Ndiyo”akajibu Mathew
“Nakwambia kweli
kabisa kwamba sifahamu
sababu ya kutekwa na
kupelekwa mafichoni kwa
miaka mitatu.Kama kuna
taarifa zozote mlizopewa
kuhusu mimi si taarifa za
kweli hata kidogo”akasema
Edger
“Mzaha umeisha ngoja
nikueleze ukweli.Edger wewe
unashirikiana na kikundi
cha kigaidi cha IS.Ukiwa
katika matibabu nchini
Israel ulitembelewa na watu
wawili ambao ni wafadhili
wakuu wa kundi hili na
mengine mengi ya kigaidi
ambao ni Habiba Jawad na
Sayid Omar na hapo ndipo
Israel walipoanza
kukufuatilia na hatimaye
kukuteka wakaenda
kukuficha jijini Nairobi
katika ubalozi wao wakitaka
kupata taarifa za mahala
walipo Habiba Jawad na
wenzake wanaofadhili
ugaidi” akasema Mathew na
jasho likaonekana usoni kwa
Edger
“Taarifa zinaonyesha
kwamba chanzo cha ugonjwa
wako uliosababisha upelekwe
nchini Israel ni sumu Dr
Olivia Themba aliyapigania
maisha yako hadi
ukapona,aliweka rehani
maisha yake kwa ajili yako
lakini umemuingiza katika
mtandao wa IS.Haya ndiyo
malipo kwa mtu kama huyu
ambaye alipambana kuokoa
maisha yako? Akauliza
Mathew kwa ukali
“Sikuwahi kumuingiza
Olivia katika IS” akajibu
Edger Kaka
“Kama si wewe nani
aliyemuunganisha Olivia na
kundi la IS?
“Olivia hayupo katika
kundi la IS” akajibu Edger
“Umejuaje kama Olivia si
mfuasi wa IS?akauliza
Mathew na Edger akabaki
kimya.Mathew akapiga meza
kwa nguvu
“Answer me Edger !!
“Olivia is not IS !
akasema Edger kwa sauti ya
juu halafu akainamisha
kichwa chini kwa sekunde
kadhaa na kusema
“Look guys Olivia ni mtu
muhimu mno kwangu.She
saved my life.Kama si yeye
kupigania maisha yangu hivi
sasa wala msingekuwa
mnanihoji ningekwisha kufa
zamani sana.Hakuna kiasi
chochote cha pesa
kinachoweza kufikia thamani
ya Olivia kwangu.Thamani
yake ni kubwa kuliko tani ya
dhahabu,almasi na kila kito
cha thamani
unachokifahamu.Zaidi ya
yote kuna kitu ambacho
hamkifahamu.Mimi na
Olivia tulikuwa tunaelekea
kuwa wapenzi.Ni mwanamke
pekee ambaye moyo wangu
umemuangukia na
kumpenda hata yeye pia
alikwisha tokea kunipenda”
akasema Edger
“Muongo mkubwa we
!Ungekuwa unampenda
Olivia usingemuingiza katika
kundi lenu la
kigaidi.Umeyaharibu maisha
yake.Olivia wa sasa si Olivia
Yule unayemfahamu
wewe.Amekuwa muuaji hana
huruma hata chembe kutoa
roho ya mtu.Kwa
kushirikiana na IS
ametengeneza kirusi cha
maangamizi ambacho
wanataka kukitumia
kufanya mashambulio yao ya
kigaidi.Kwa nini ukakubali
mwanamke unayempenda
ageuke kuwa mkatili namna
hii? Akauliza Mathew
“Mimi sijamuingiza
Olivia IS na siwezi kufanya
kitu kama hicho.Mara ya
mwisho kuonana na Olivia ni
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere tulipotoka
Israel.Tuliagana kwa miadi
ya kuonana kesho yake
lakini huo ukawa ni mwisho
wa kuonana naye kwani hiyo
kesho haikunikuta Tanzania
tayari nilikuwa nimetekwa
na sifahamu chochote
kilichokuwa kinaendelea
wakati nikiwa nimeshikiliwa
na Mossad.Taarifa za
kwamba mimi ndiye
niliyemuingiza Olivia IS si za
kweli.Kwanza Olivia
hafahamu chochote kuhusu
IS” akasema Edger.Mathew
akamtazama kwa macho
yaliyojaa hasira halafu
akasema
“Walipokuja wale
majasusi wa Mossad
kukuhoji uliwaambia
wakusaidie kumtafuta Olivia
na utawaeleza kila kitu
wanachokitaka.Hapo
ulionyesha kweli unampenda
Olivia na uko tayari kufanya
kitu chochote ili
kumpata.Nataka kufahamu
kama unaendelea kusimama
katika kauli yako kwamba
ukimpata Olivia utakuwa
tayari kufunguka”akasema
Mathew
“Olivia ninampenda
kuliko kitu chochote na
sintoacha kumpenda ndiyo
maana niliwaamba wale
watu wa Mossad waniletee
Olivia mwanamke
ninayempenda nami
nitawaeleza kile
wanachotafuta kwangu.Niko
tayari kufanya chochote kwa
ajili yake”
“Ahsante kwa kuweka
wazi namna unavyompenda
Olivia.Lakini kuna tatizo
katika kumpata.Olivia yuko
katika mikono ya IS hivi
sasa”
“Mikono ya IS
kivipi?akauliza Edger
“Ngoja nitumie dakika
chache kukupa maelezo
kidogo.Idara ya usalama wa
taifa ya jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo
walipata taarifa kwamba
mmoja wa watu wa IS
anaitwa Seif Almuhsin
anatembelea nchini kwao
hivyo wakaanza kujiandaa
kumfuatilia.Alipofika
Kinshasa wakaanza
kumfuatilia na wakagundua
kwamba alikutana na
mwanamke mmoja wa
kitanzania ndipo taarifa
zilipotumwa huku Tanzania
na akagundulikwa kwamba
ni Olivia Themba.Ililazimu
idara zinazihusika na
usalama wa nchi kumteka
Olivia mara tu aliporejea
kutokea Kinshasa na lengo
likiwa ni kutaka kujua
mahusiano yake na watu wa
IS.Kuthibitisha kwamba
Olivia ni mtu wao IS
walishambulia hospitali ya
Mtodora wakaua watu na
kumteka mtoto wa Rais
wakimshinikiza Rais
awakabidhi Olivia na Rais
katika jitihada za kutaka
kumkomboa mwanae
akalazimika kuwapa Olivia
na mpaka sasa hatujui yuko
wapi ndiyo maana tunahitaji
sana msaada wako tuweze
kumpata ili utueleze kile
tunachotaka kukisikia
kuhusu IS.Edger machoni pa
watu tayari umekwisha kufa
na kusahaulika hata IS
hawajui kama uko hai hivyo
basi ni wakati wako wa
kuachana nao na kuishi
maisha mapya.Rais yuko
tayari kukusaidia kuanza
maisha mapya kwa
kukutafutia nchi ambako
utakwenda kujificha huko
ukiwa na Olivia.Huo ndio
msaada pekee ambao Rais
wa Tanzania yuko tayari
kukusaidia kama nawe
utakuwa tayari kutusaidia”
akasema Mathew na Edger
akainamisha kichwa
“Edger tafadhali tusaidie
tukusaidie.IS wana mipango
miovu sana dhidi ya nchi
yetu.Usiku wa kuamkia leo
wamevamia shule ya
sekondari ya wasichana na
kuteka wasichana sitini na
sita ambao mpaka sasa
hawajulikani walipo.Edger
umekuwa mbunge wa bunge
la jamhuri ya muungano na
ulijizolea sifa nyingi sana
kutokana na utendaji wako
wa kazi hasa katika kupiga
vita ufisadi.Una mapenzi
makubwa na nchi hii na
siamini kama uko tayari
kuona IS wakihatarisha
amani na usalama wa nchi
yetu.Watu wanaishi kwa
hofu hivi sasa kwani IS
wametishia kufanya
mashambulizi mengi hapa
nchini.Kama uliona video ya
mazishi yako ya bandia
utakuwa umeona namna
watu walivyokuwa na
mapenzi makubwa
nawe,wengi walipoteza
fahamu kukulilia.Edger
upendo ule ni mkubwa na
ninaamini hauko tayari
kuwaona watu wale ambao
walikupenda na wakawa na
matumaini makubwa kwako
wakiishi kwa mashaka na
kukosa amani.Tusaidie
kuufahamu mtandao wa IS
hapa nchini na sisi
tutakupatia kila
unachokihitaji ili kuyaanza
maisha mapya.Mwanamke
unayempenda yuko katika
mikono ya IS,wasichana
sitini na sita wasio na hatia
wanashikiliwa mateka na
wanaweza wakapoteza
maisha kama juhudi za
haraka za kuwatafuta
hazitafanywa.Tunakutegeme
a sana Edger tafadhali
tusaidie” akasema
Mathew.Edger akafikiri
kidogo na kusema
“Hili jambo la Olivia
kujiunga na IS
linanishangaza
sana.Limetokeaje?
“Edger muda unakwenda
mbio sana kama una nia ya
dhati ya kutusaidia kumpata
Olivia muda ni huu”akasema
Mathew lakini bado Edger
Kaka aliendelea kuinamisha
kichwa.
“Edger unaufahamu
vyema mtandao wa IS hapa
nchini nataka kujua ni wapi
unahisi amefichwa Olivia?
Tafadhali…” akasema
Mathew
“Sifahamu chochote
nimekuwa mateka kwa
miaka mitatu na sijui
kinachoendelea hapa nchini”
akasema Edger
“Tupe majina ya viongozi
wa IS hapa Tanzania”
akasema Mathew na Edger
akamtazama na kusema
“I’m not IS”
Kauli ile ilimkasirisha
sana Mathew akasimama
“Edger we don’t want to
destroy you.We want to help
you.Ili tukusaidie lazima na
wewe utusaidie kuutambua
mtandao wa IS hapa
Tanzania na kuwakomboa
watu wanaowashikilia
mateka”
“Guys I’m not
IS.Siufahamu mtandao
wowote wa IS hapa
Tanzania” akasema Edger na
Mathew akaendelea
kumtazama kwa jicho kali
“Kitu gani ulitaka
kuwaeleza Mossad? Akauliza
Mathew Edger akawa
kimya.Mathew akapiga meza
kwa hasira
“Answer me Edger !!
“Sifahamu chochote !
akajibu Edger.Mathew
akamtazama na kusema
“Ninakupa dakika kumi
nitakaporejea nitahitaji
kupata taarifa za mtandao
wote wa IS hapa nchini ama
sivyo tutafungua ukurasa
mpya” akasema Mathew na
kutoka ndani ya kile chumba
akaingia katika chumba
kingine ambacho
Austin,Gosu Gosu na
Devotha walikuwa
wanafuatilia mahojiano yale.
“Bastard ! akasema
Mathew kwa hasira akiwa
ameshika kiuno
“Natamani kumuharibu
haribu Yule mtu lakini
ninasita kwanza afya yake
mbovu na vile vile bado
tunamuhitaji sana”akasema
Mathew
“Usijali Mathew ni
mwanzo
mzuri.Ulimchanganya kwa
maswali na mwenyewe
akajikuta akikiri kuwa ni
IS.Ninaamini katika awamu
ya pili tunaweza kupata
jambo toka kwake” akasema
Austin
“Akiendelea kujifanya
kiburi nipe dakika tano tu
nicheze naye atasema kila
kitu” akasema Gosu Gosu
“Usihofu Gosu Gosu
atafunguka tu” akasema
Mathew na kumgeukia
Austin
“Austin I need to call
president” akasema Mathew
na Austin akamchukua
wakaelekea katika ofisi yake
akampatia simu ili aweze
kuzugumza na Rais
“Mathew ahsante kwa
kupiga.Hapa nilipo
nimechanganyikiwa na sijui
nifanye nini.Nimekutafuta
katika simu yako
haupatikani”akasema
DrEvans
“Niko hapa katika kambi
ya kikosi maalum na simu
zetu tumezima.Nini
kinaendelea huko?Saa mbili
kamili imekwisha pita wale
jamaa wamepiga simu?
“Ndiyo Mathew
wamepiga simu na wamenipa
hadi saa tatu za asubuhi
niwe nimewapa Edger Kaka
ama sivyo wataanza
kuwachinja wale wasichana
waliowateka.Mmekwisha
anza kumuhoji
Edger?akauliza
“Ndiyo mheshimiwa
Rais,tumekwisha anza
kumuhoji lakini tunakwenda
naye taratibu na atafunguka”
“Mathew tafadhali fanya
haraka kupata taarifa
kutoka kwa huyo mtu kwani
inakaribia saa tatu na wale
jamaa wameahidi mpaka
kufikia saa tatu kama
sijawatimizia wanachokitaka
wataanza kuua watoto.Fanya
kile unachoweza kuhakikisha
unapata taarifa muhimu
kabla ya muda huo” akasema
Dr Evans
“Mheshimiwa Rais kwa
hali ya Edger Kaka ilivyo
hatuwezi kutumia nguvu
afya yake ni dhaifu sana
ndiyo maana tunajaribu
kutumia njia ya ushawishi ili
aweze kukubali kufunguka
na tuna uhakika huo
kwamba atafunguka”
“Mathew zimebaki
dakika chache kufika saa
tatu kamili muda ambao
wale jamaa wametoa
unadhani kuna chochote
ambacho tutakuwa
tumekipata hadi kufikia
muda huo?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa Rais siwezi
kukuahidi chochote kwa
muda huu mfupi lakini kama
wakipiga tena hiyo saa tatu
kamili kama
walivyoahidi,buy time”
akasema Mathew
“Mathew I don’t know
what to do.Tegemeo langu
lote ni kwako.Niko katika
kikao cha baraza la usalama
la taifa na nimejitahidi
kufanya kama
ulivyonielekeza kuendelea
kuliweka siri hili suala lakini
nina wasi wasi yawezekana
ukafika muda nikashindwa
kuendelea kuliweka siri hili
jambo pale watakapoanza
kufanya mauaji ya watoto na
mimi sina njia nyingine ya
kufanya” akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais kwa
namna yoyote ile hakikisha
huliweki wazi hili
jambo.Ninakuahidi kufanya
kila linalowezekana
kuwakomboa hao wasichana
na wengine wote
wanaoshikikliwa na IS lakini
usijaribu kabisa kufunguka
suala hili mbele ya viongozi
tutaharibu kila kitu.Siwezi
kukuahidi chochote kwa sasa
mheshimiwa Rais lakini nina
imani kubwa tutawakomboa
hao wasichana wote
waliotekwa nyara” akasema
Mathew
“Mathew nina kuamini
sana lakini tatizo ni muda
ambao tutautumia
kuwakomboa hao mateka
kabla magaidi hawajaanza
kuwaua.Hapa nilipo katika
kikao viongozi wote wana
hasira kali na wanataka
itumike nguvu kubwa
kuwasaka magaidi na
kuwakomboa
watoto.Ninasita kuruhusu
nguvu kubwa itumike kwa
sasa kuogopa kumpoteza
kabisa mwanangu.Hapo
ndipo akili yangu
inapokwamia” akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa Rais
relax.Umetupa kazi ya
kuwakomboa watoto hivyo
usiwe na wasiwasi tutaifanya
hiyo kazi.Ninachokuomba tu
kama wale jamaa watapiga
muda huo wa saa tatu
jitahidi kuvuta muda wakati
sisi tukiendelea utafuta
mbinu za kuwasaka hao
magaidi”
“Sawa nitafanya hivyo
Mathew lakini naomba
ufahamu hili suala linazidi
kuwa zito kwangu na kama
usipopatikana msaada wa
haraka basi litanishinda
nguvu.Tutawasiliana tena
baadae ninakwenda
kuendelea na kikao kusubiri
ifike saa tatu kamili”
akasema Dr Evans na
kukata simu.
“Saa tatu kamili magaidi
wameahidi uanza kuua
watoto kama Rais hatauwa
ametekeleza ombi
lao.Tunapaswa kujitahidi
sana tumfungue Edger kwa
haraka” akasema Mathew
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 7
Geti la kambi ya kikosi
cha operesheni maalum
likafunguliwa na gari la
akina Mathew
likapita.Tayari walikwisha
wasiliana na Austin na
kumjulisha kuwa
wanakwenda kuanza
mahojiano na Edger
Kaka.Wote wakazima simu
zao kwani ukiwa ndani ya
kambi ile huruhusiwi
kutumia simu ya mkononi
bali zipo simu maalum
unazoweza kutumia
kupiga.Walifika hadi katika
jengo la utawala
wakapokewa na kuongozwa
moja kwa moja hadi katika
ofisi ya Austin
“Karibuni tena ndugu
zangu”akasema Austin
“Ahsante
Austin.Utatuwia radhi kwani
tutaendelea kuwa wageni
wako na tutafika hapa mara
kwa mara kila pale
tutakapokuwa na uhitaji na
mtu wetu”
“Mathew msijali
tafadhali kuweni na
amani.Hili ni suala la kitaifa
hivyo basi lazima
tuhakikishe linakamilika”
“Ahsante sana
Austin.Tumelazimika
kurejea tena kuja kuanza
kumuhoji Edger.Usiku wa
kuamkia leo watu wa IS
wamevamia na kuteka
wasichana sitini na sita
katika shule ya sekondari ya
St Getrude na lengo kubwa
la kuwateka wasichana hao
ni kumshinikiza Rais aweze
kumuachia Edger Kaka”
akasema Mathew
“Wana uhakika kama
Rais anafahamu mahala
alipo Edger? Akauliza Austin
“Hawajui chochote
kuhusu Edger Kaka kama
alitekwa na Mossad na
alikuwa Nairobi,wao
wanaamini yuko hai na
mchezo ule ulifanywa na
serikali ya Tanzania ndiyo
maana wanatumia kila njia
kushinikiza Rais aweze
kumuachia mtu wao”akajibu
Mathew
“Saa mbili kamili za
asubuhi watampigia simu
Rais kujua kama tayari
amekwisha muandaa Edger
na kama hatatekeleza hilo
basi wataanza kuwaua wale
wasichana.Tumelazimika
kuja tena hapa kumuhoji
Edger Kaka atusaidie
kufahamu mtandao wao
hapa nchini ili tuweze
kuwaokoa wale wanafunzi
pamoja na mtoto wa Rais”
akasema Mathew
“Sawa Mathew
nimekuelewa hapa tuna
chumba maalum kwa ajili ya
mahojiano mtakitumia
chumba hicho kumuhoji
Edger na kama mkihitaji
kuingia katika hatua
nyingine zaidi ya kutumia
nguvu kipo chumba maalum
kwa ajili hiyo na wapo
wataalamu wa kuifanya hiyo
kazi” akasema Austin huku
akiinuka
“Tunaye mtaalamu wetu
wa kutesa ambaye ni Gosu
Gosu.Hakuna aliyewahi
kuingia katika mikono yake
akashindwa kufungua
mdomo wake lakini kwa afya
ya Edger Kaka tunataka
kwanza kumuhoji bila
kutumia nguvu” akasema
Mathew wakatoka mle ofisini
na Austin akawaongoza hadi
katika chumba cha
mahojiano kulimokuwa na
meza na viti viwili.Mathew
akaingia mle ndani na baada
ya dakika tatu Edger Kaka
akiwa amefungwa pingu
mkononi akaingizwa ndani
ya kile chumba akiwa
anasukumwa katika basikeli
ya magurudumu kwani bado
hakuwa na uwezo wa
kutembea.Mathew akaamuru
afunguliwe mikono abaki
huru na watu wote watoke
nje akabaki na Edger,
akamtazama kwa sekunde
kadhaa halafu akasema
“Edger Kaka pole sana
kwa masahibu yote
yaliyokupata kwa muda wa
miaka mitatu.Lakini yote
hayo yamekwisha sasa
umerejea
nyumbani.Unajisikiaje
kurejea tena nyumbani?
Akauliza Mathew.Edger
akajaribu kuzungumza lakini
sauti ikamkwama Mathew
akaomba kuletewa maji
Edger akanywa
“Sasa niambie Edger
unajisikiaje kurejea
nyumbani ? Akauliza
Mathew
“Unataka nikwambie
nina furahi?I’m not happy at
all.Mlikosea sana
msingesumbuka kuja
kunikomboa na kunirejesha
tena Tanzania” akasema
Edger kaka
“Kwa nini unasema hivyo
Edger? Hupendi
Tanzania?Hupendi kurejea
nyumbani? Akauliza Mathew
“Because I’m dead
already.Nimeonyeshwa video
ya mazishi yangu namna
watu walivyonililia wakijua
nimefariki dunia wengine
wakipoteza fahamu baada ya
kupita katika jeneza ambalo
waliamini kuna maiti yangu
lakini kumbe ulikuwa ni
mchezo
umetengenezwa.Imeniumiza
sana baada ya kulifahamu
hilo jambo na siwafichi
ninatamani hata sasa
mnipige risasi nife niondoke
kabisa katika dunia hii”
akasema Edger
“Edger waliofanya tuko
lile si Tanzania bali ni Israel
wakitumia shirika lao la
ujasusi la Mossad na ndiyo
maana baada ya kufahamu
kwamba uko hai tukafanya
kila lililo ndani ya uwezo
wetu kukukomboa na
kukurejesha
nyumbani.Tumetengeneza
mgogoro mkubwa sana wa
kidiplomasia kati yetu na
Israel kwani tumelazimika
kuua watu wao wengine wa
muhimu kabisa ili tuweze
kukukomboa.Naweza
kusema kwamba serikali ya
Tanzania kwa kukuthamini
imetumia gharama kubwa
kukukomboa na kukurejesha
nyumbani.Unapaswa
kufurahi”akasema Mathew
“Ninashukuru kwa
kunitoa katika nyumba ile ya
mateso lakini haikuwa na
ulazima wowote wa kutumia
gharama kubwa
kunikomboa”akasema Edger
“Edger wewe ni
mtanzania na ilikuwa lazima
kwa gharama zozote zile
tukurejeshe
nyumbani”akasema Mathew
na kumtazama Edger kwa
sekude kadhaa halafu
akasema
“Edger unaweza
ukatueleza sababu za Israel
kutumia gharama kubwa
kutengeneza kifo chako
wakati bado uko
hai?akauliza Mathew na
Edger akabaki kimya
“Nijibu Edger swali
nililokuuliza”
“Sifahamu chochote”
akasema Edger
“Edger jina langu
ninaitwa Mathew Mulumbi
ndiye niliyeongoza
operesheni ya kuja
kukukomboa na kukurejesha
nyumbani.Hapa uko sehemu
salama na mateso yote
uliyoyapata kwa miaka
mitatu yamekwisha.Hapa
ndipo patakuwa chimbuko la
maisha yako
mapya.Mheshimiwa Rais
anafahamu kuwa uko hapa
na ndiye aliyetoa kibali cha
kufanya operesheni ile ya siri
ya kukukomboa na yuko
tayari kukufanyia kitu
chochote unachokihitaji ili
uanze maisha yako upya
lakini amenituma hapa
kwako nije kuzungumza
nawe ili tuufahamu ukweli
wote kwa nini ulitekwa na
Israel?Usihofu hapa uko
sehemu salama na hakuna
anayefahamu kama uko hapa
hivyo kuwa huru”akasema
Mathew na Edger
akainamisha kichwa
akazama mawazoni
“Edger please usiipoteze
hii nafasi uliyoipata.Hii ni
tiketi ya kuelekea maisha
mapya hivyo itumie
kikamilifu” akasema Mathew
“Sifahamu chochote kwa
nini waliniteka nyara na
kunipa mateso yale makali
kwa miaka mitatu.Watu
wale ni wanyama mno!
Akasema Edger na sura ya
Mathew ikaanza kubadilika
“Who is Habiba Jawad?
Akauliza Mathew na Edger
akastuka
“Umesema nani?
“Habiba Jawad ni nani?
“Si..simfahamu” akajibu
Edger.Mathew akamtazama
kwa macho makali
“Edger Kaka narudia
tena kauli yangu kwamba
hapa panaweza kuwa
chimbuko la maisha yako
mapya au panaweza kuwa ni
mwisho wa maisha yako
hivyo ni jukumu lako
kuchagua nini unakitaka
kuishi au kufa.Mimi
ninayezungumza nawe hapa
ninamuwakilisha Rais hivyo
sihitaji mzaha.Ninapokuuliza
nataka unipe majibu ya
kweli kama ukitaka kuwa
kiburi nakuhakikishia
hautafika kokote
Edger.Mateso uliyoyapata
nchini Kenya kwa miaka
mitatu yanatosha sana
hatutaki kuendelea kukutesa
hata hapa nyumbani hivyo
funguka,kuwa mkweli
tueleze nini kilitokea na sisi
tutajua namna ya
kukusaidia.We need
information from you”
akasema Mathew
“Mathew
Mulumbi,right?akauliza
Edger
“Ndiyo”akajibu Mathew
“Nakwambia kweli
kabisa kwamba sifahamu
sababu ya kutekwa na
kupelekwa mafichoni kwa
miaka mitatu.Kama kuna
taarifa zozote mlizopewa
kuhusu mimi si taarifa za
kweli hata kidogo”akasema
Edger
“Mzaha umeisha ngoja
nikueleze ukweli.Edger wewe
unashirikiana na kikundi
cha kigaidi cha IS.Ukiwa
katika matibabu nchini
Israel ulitembelewa na watu
wawili ambao ni wafadhili
wakuu wa kundi hili na
mengine mengi ya kigaidi
ambao ni Habiba Jawad na
Sayid Omar na hapo ndipo
Israel walipoanza
kukufuatilia na hatimaye
kukuteka wakaenda
kukuficha jijini Nairobi
katika ubalozi wao wakitaka
kupata taarifa za mahala
walipo Habiba Jawad na
wenzake wanaofadhili
ugaidi” akasema Mathew na
jasho likaonekana usoni kwa
Edger
“Taarifa zinaonyesha
kwamba chanzo cha ugonjwa
wako uliosababisha upelekwe
nchini Israel ni sumu Dr
Olivia Themba aliyapigania
maisha yako hadi
ukapona,aliweka rehani
maisha yake kwa ajili yako
lakini umemuingiza katika
mtandao wa IS.Haya ndiyo
malipo kwa mtu kama huyu
ambaye alipambana kuokoa
maisha yako? Akauliza
Mathew kwa ukali
“Sikuwahi kumuingiza
Olivia katika IS” akajibu
Edger Kaka
“Kama si wewe nani
aliyemuunganisha Olivia na
kundi la IS?
“Olivia hayupo katika
kundi la IS” akajibu Edger
“Umejuaje kama Olivia si
mfuasi wa IS?akauliza
Mathew na Edger akabaki
kimya.Mathew akapiga meza
kwa nguvu
“Answer me Edger !!
“Olivia is not IS !
akasema Edger kwa sauti ya
juu halafu akainamisha
kichwa chini kwa sekunde
kadhaa na kusema
“Look guys Olivia ni mtu
muhimu mno kwangu.She
saved my life.Kama si yeye
kupigania maisha yangu hivi
sasa wala msingekuwa
mnanihoji ningekwisha kufa
zamani sana.Hakuna kiasi
chochote cha pesa
kinachoweza kufikia thamani
ya Olivia kwangu.Thamani
yake ni kubwa kuliko tani ya
dhahabu,almasi na kila kito
cha thamani
unachokifahamu.Zaidi ya
yote kuna kitu ambacho
hamkifahamu.Mimi na
Olivia tulikuwa tunaelekea
kuwa wapenzi.Ni mwanamke
pekee ambaye moyo wangu
umemuangukia na
kumpenda hata yeye pia
alikwisha tokea kunipenda”
akasema Edger
“Muongo mkubwa we
!Ungekuwa unampenda
Olivia usingemuingiza katika
kundi lenu la
kigaidi.Umeyaharibu maisha
yake.Olivia wa sasa si Olivia
Yule unayemfahamu
wewe.Amekuwa muuaji hana
huruma hata chembe kutoa
roho ya mtu.Kwa
kushirikiana na IS
ametengeneza kirusi cha
maangamizi ambacho
wanataka kukitumia
kufanya mashambulio yao ya
kigaidi.Kwa nini ukakubali
mwanamke unayempenda
ageuke kuwa mkatili namna
hii? Akauliza Mathew
“Mimi sijamuingiza
Olivia IS na siwezi kufanya
kitu kama hicho.Mara ya
mwisho kuonana na Olivia ni
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere tulipotoka
Israel.Tuliagana kwa miadi
ya kuonana kesho yake
lakini huo ukawa ni mwisho
wa kuonana naye kwani hiyo
kesho haikunikuta Tanzania
tayari nilikuwa nimetekwa
na sifahamu chochote
kilichokuwa kinaendelea
wakati nikiwa nimeshikiliwa
na Mossad.Taarifa za
kwamba mimi ndiye
niliyemuingiza Olivia IS si za
kweli.Kwanza Olivia
hafahamu chochote kuhusu
IS” akasema Edger.Mathew
akamtazama kwa macho
yaliyojaa hasira halafu
akasema
“Walipokuja wale
majasusi wa Mossad
kukuhoji uliwaambia
wakusaidie kumtafuta Olivia
na utawaeleza kila kitu
wanachokitaka.Hapo
ulionyesha kweli unampenda
Olivia na uko tayari kufanya
kitu chochote ili
kumpata.Nataka kufahamu
kama unaendelea kusimama
katika kauli yako kwamba
ukimpata Olivia utakuwa
tayari kufunguka”akasema
Mathew
“Olivia ninampenda
kuliko kitu chochote na
sintoacha kumpenda ndiyo
maana niliwaamba wale
watu wa Mossad waniletee
Olivia mwanamke
ninayempenda nami
nitawaeleza kile
wanachotafuta kwangu.Niko
tayari kufanya chochote kwa
ajili yake”
“Ahsante kwa kuweka
wazi namna unavyompenda
Olivia.Lakini kuna tatizo
katika kumpata.Olivia yuko
katika mikono ya IS hivi
sasa”
“Mikono ya IS
kivipi?akauliza Edger
“Ngoja nitumie dakika
chache kukupa maelezo
kidogo.Idara ya usalama wa
taifa ya jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo
walipata taarifa kwamba
mmoja wa watu wa IS
anaitwa Seif Almuhsin
anatembelea nchini kwao
hivyo wakaanza kujiandaa
kumfuatilia.Alipofika
Kinshasa wakaanza
kumfuatilia na wakagundua
kwamba alikutana na
mwanamke mmoja wa
kitanzania ndipo taarifa
zilipotumwa huku Tanzania
na akagundulikwa kwamba
ni Olivia Themba.Ililazimu
idara zinazihusika na
usalama wa nchi kumteka
Olivia mara tu aliporejea
kutokea Kinshasa na lengo
likiwa ni kutaka kujua
mahusiano yake na watu wa
IS.Kuthibitisha kwamba
Olivia ni mtu wao IS
walishambulia hospitali ya
Mtodora wakaua watu na
kumteka mtoto wa Rais
wakimshinikiza Rais
awakabidhi Olivia na Rais
katika jitihada za kutaka
kumkomboa mwanae
akalazimika kuwapa Olivia
na mpaka sasa hatujui yuko
wapi ndiyo maana tunahitaji
sana msaada wako tuweze
kumpata ili utueleze kile
tunachotaka kukisikia
kuhusu IS.Edger machoni pa
watu tayari umekwisha kufa
na kusahaulika hata IS
hawajui kama uko hai hivyo
basi ni wakati wako wa
kuachana nao na kuishi
maisha mapya.Rais yuko
tayari kukusaidia kuanza
maisha mapya kwa
kukutafutia nchi ambako
utakwenda kujificha huko
ukiwa na Olivia.Huo ndio
msaada pekee ambao Rais
wa Tanzania yuko tayari
kukusaidia kama nawe
utakuwa tayari kutusaidia”
akasema Mathew na Edger
akainamisha kichwa
“Edger tafadhali tusaidie
tukusaidie.IS wana mipango
miovu sana dhidi ya nchi
yetu.Usiku wa kuamkia leo
wamevamia shule ya
sekondari ya wasichana na
kuteka wasichana sitini na
sita ambao mpaka sasa
hawajulikani walipo.Edger
umekuwa mbunge wa bunge
la jamhuri ya muungano na
ulijizolea sifa nyingi sana
kutokana na utendaji wako
wa kazi hasa katika kupiga
vita ufisadi.Una mapenzi
makubwa na nchi hii na
siamini kama uko tayari
kuona IS wakihatarisha
amani na usalama wa nchi
yetu.Watu wanaishi kwa
hofu hivi sasa kwani IS
wametishia kufanya
mashambulizi mengi hapa
nchini.Kama uliona video ya
mazishi yako ya bandia
utakuwa umeona namna
watu walivyokuwa na
mapenzi makubwa
nawe,wengi walipoteza
fahamu kukulilia.Edger
upendo ule ni mkubwa na
ninaamini hauko tayari
kuwaona watu wale ambao
walikupenda na wakawa na
matumaini makubwa kwako
wakiishi kwa mashaka na
kukosa amani.Tusaidie
kuufahamu mtandao wa IS
hapa nchini na sisi
tutakupatia kila
unachokihitaji ili kuyaanza
maisha mapya.Mwanamke
unayempenda yuko katika
mikono ya IS,wasichana
sitini na sita wasio na hatia
wanashikiliwa mateka na
wanaweza wakapoteza
maisha kama juhudi za
haraka za kuwatafuta
hazitafanywa.Tunakutegeme
a sana Edger tafadhali
tusaidie” akasema
Mathew.Edger akafikiri
kidogo na kusema
“Hili jambo la Olivia
kujiunga na IS
linanishangaza
sana.Limetokeaje?
“Edger muda unakwenda
mbio sana kama una nia ya
dhati ya kutusaidia kumpata
Olivia muda ni huu”akasema
Mathew lakini bado Edger
Kaka aliendelea kuinamisha
kichwa.
“Edger unaufahamu
vyema mtandao wa IS hapa
nchini nataka kujua ni wapi
unahisi amefichwa Olivia?
Tafadhali…” akasema
Mathew
“Sifahamu chochote
nimekuwa mateka kwa
miaka mitatu na sijui
kinachoendelea hapa nchini”
akasema Edger
“Tupe majina ya viongozi
wa IS hapa Tanzania”
akasema Mathew na Edger
akamtazama na kusema
“I’m not IS”
Kauli ile ilimkasirisha
sana Mathew akasimama
“Edger we don’t want to
destroy you.We want to help
you.Ili tukusaidie lazima na
wewe utusaidie kuutambua
mtandao wa IS hapa
Tanzania na kuwakomboa
watu wanaowashikilia
mateka”
“Guys I’m not
IS.Siufahamu mtandao
wowote wa IS hapa
Tanzania” akasema Edger na
Mathew akaendelea
kumtazama kwa jicho kali
“Kitu gani ulitaka
kuwaeleza Mossad? Akauliza
Mathew Edger akawa
kimya.Mathew akapiga meza
kwa hasira
“Answer me Edger !!
“Sifahamu chochote !
akajibu Edger.Mathew
akamtazama na kusema
“Ninakupa dakika kumi
nitakaporejea nitahitaji
kupata taarifa za mtandao
wote wa IS hapa nchini ama
sivyo tutafungua ukurasa
mpya” akasema Mathew na
kutoka ndani ya kile chumba
akaingia katika chumba
kingine ambacho
Austin,Gosu Gosu na
Devotha walikuwa
wanafuatilia mahojiano yale.
“Bastard ! akasema
Mathew kwa hasira akiwa
ameshika kiuno
“Natamani kumuharibu
haribu Yule mtu lakini
ninasita kwanza afya yake
mbovu na vile vile bado
tunamuhitaji sana”akasema
Mathew
“Usijali Mathew ni
mwanzo
mzuri.Ulimchanganya kwa
maswali na mwenyewe
akajikuta akikiri kuwa ni
IS.Ninaamini katika awamu
ya pili tunaweza kupata
jambo toka kwake” akasema
Austin
“Akiendelea kujifanya
kiburi nipe dakika tano tu
nicheze naye atasema kila
kitu” akasema Gosu Gosu
“Usihofu Gosu Gosu
atafunguka tu” akasema
Mathew na kumgeukia
Austin
“Austin I need to call
president” akasema Mathew
na Austin akamchukua
wakaelekea katika ofisi yake
akampatia simu ili aweze
kuzugumza na Rais
“Mathew ahsante kwa
kupiga.Hapa nilipo
nimechanganyikiwa na sijui
nifanye nini.Nimekutafuta
katika simu yako
haupatikani”akasema
DrEvans
“Niko hapa katika kambi
ya kikosi maalum na simu
zetu tumezima.Nini
kinaendelea huko?Saa mbili
kamili imekwisha pita wale
jamaa wamepiga simu?
“Ndiyo Mathew
wamepiga simu na wamenipa
hadi saa tatu za asubuhi
niwe nimewapa Edger Kaka
ama sivyo wataanza
kuwachinja wale wasichana
waliowateka.Mmekwisha
anza kumuhoji
Edger?akauliza
“Ndiyo mheshimiwa
Rais,tumekwisha anza
kumuhoji lakini tunakwenda
naye taratibu na atafunguka”
“Mathew tafadhali fanya
haraka kupata taarifa
kutoka kwa huyo mtu kwani
inakaribia saa tatu na wale
jamaa wameahidi mpaka
kufikia saa tatu kama
sijawatimizia wanachokitaka
wataanza kuua watoto.Fanya
kile unachoweza kuhakikisha
unapata taarifa muhimu
kabla ya muda huo” akasema
Dr Evans
“Mheshimiwa Rais kwa
hali ya Edger Kaka ilivyo
hatuwezi kutumia nguvu
afya yake ni dhaifu sana
ndiyo maana tunajaribu
kutumia njia ya ushawishi ili
aweze kukubali kufunguka
na tuna uhakika huo
kwamba atafunguka”
“Mathew zimebaki
dakika chache kufika saa
tatu kamili muda ambao
wale jamaa wametoa
unadhani kuna chochote
ambacho tutakuwa
tumekipata hadi kufikia
muda huo?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa Rais siwezi
kukuahidi chochote kwa
muda huu mfupi lakini kama
wakipiga tena hiyo saa tatu
kamili kama
walivyoahidi,buy time”
akasema Mathew
“Mathew I don’t know
what to do.Tegemeo langu
lote ni kwako.Niko katika
kikao cha baraza la usalama
la taifa na nimejitahidi
kufanya kama
ulivyonielekeza kuendelea
kuliweka siri hili suala lakini
nina wasi wasi yawezekana
ukafika muda nikashindwa
kuendelea kuliweka siri hili
jambo pale watakapoanza
kufanya mauaji ya watoto na
mimi sina njia nyingine ya
kufanya” akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais kwa
namna yoyote ile hakikisha
huliweki wazi hili
jambo.Ninakuahidi kufanya
kila linalowezekana
kuwakomboa hao wasichana
na wengine wote
wanaoshikikliwa na IS lakini
usijaribu kabisa kufunguka
suala hili mbele ya viongozi
tutaharibu kila kitu.Siwezi
kukuahidi chochote kwa sasa
mheshimiwa Rais lakini nina
imani kubwa tutawakomboa
hao wasichana wote
waliotekwa nyara” akasema
Mathew
“Mathew nina kuamini
sana lakini tatizo ni muda
ambao tutautumia
kuwakomboa hao mateka
kabla magaidi hawajaanza
kuwaua.Hapa nilipo katika
kikao viongozi wote wana
hasira kali na wanataka
itumike nguvu kubwa
kuwasaka magaidi na
kuwakomboa
watoto.Ninasita kuruhusu
nguvu kubwa itumike kwa
sasa kuogopa kumpoteza
kabisa mwanangu.Hapo
ndipo akili yangu
inapokwamia” akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa Rais
relax.Umetupa kazi ya
kuwakomboa watoto hivyo
usiwe na wasiwasi tutaifanya
hiyo kazi.Ninachokuomba tu
kama wale jamaa watapiga
muda huo wa saa tatu
jitahidi kuvuta muda wakati
sisi tukiendelea utafuta
mbinu za kuwasaka hao
magaidi”
“Sawa nitafanya hivyo
Mathew lakini naomba
ufahamu hili suala linazidi
kuwa zito kwangu na kama
usipopatikana msaada wa
haraka basi litanishinda
nguvu.Tutawasiliana tena
baadae ninakwenda
kuendelea na kikao kusubiri
ifike saa tatu kamili”
akasema Dr Evans na
kukata simu.
“Saa tatu kamili magaidi
wameahidi uanza kuua
watoto kama Rais hatauwa
ametekeleza ombi
lao.Tunapaswa kujitahidi
sana tumfungue Edger kwa
haraka” akasema Mathew
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 8
Tayari chumba ambacho
Fahad na kundi lake
wangekitumia kwa ajili ya
kurusha moja kwa moja
tukio la mauaji kwa
wasichana waliowateka ili
kumshinikiza Rais
awakabidhi mtu wao Edger
Kaka,kilikwisha
andaliwa.Macho ya Fahad
yalikuwa katika saa ya
mkononi akisubiri ufike
muda wa kumpigia simu
Rais ili kujua kama
ametekeleza takwa
lao.Mshale ulipogonga saa
tatu kamili akawasha simu
yake na kumpigia Rais.Simu
ikaita bila kupokelewa
akapiga tena ikaita na
kukatika bila
kupokelewa.Akapiga mara ya
tatu simu haikupokelewa.
“Hataki kupokea
simu.Huyu Rais bado
hajatufahamu
vizuri.Tunatakiwa
kumuonyesha kwamba
tunamaanisha kila
tunachokisema.Tuendelee na
zoezi letu.Kila kitu kiwekwe
tayari” akasema Fahad na
kuchukua kofia ya kufunika
uso akavaa akabaki
anaonekana macho.Kamera
ikawashwa kisha akapewa
ishara kwamba aanze
kuzungumza
“Ndugu watanzania mimi
ni kiongozi wa kikundi cha
Islamic state hapa Tanzania
ambao tumekuwa
tukiendesha mfululizo wa
matukio.Ni sisi tuliofanya
shambulio katika hospitali
ya Mtodora na usiku wa
kuamkia leo tumevamia
shule ya sekondari ya St
Getrude na kuteka
wanafunzi sitini na sita na
walimu wao watatu.Tunayo
madai yetu kwa Rais wa nchi
na amekuwa akiyapuuza
hivyo basi kumuonyesha
kwamba hatutanii kwa kile
tunachokisema tutaua
msichana mmoja baada ya
mwingine miongoni mwa
hawa tuliowateka kila baada
ya nusu saa.Tutaendelea
kumwaga damu nchini
Tanzania hadi pale Rais
wenu atakapotupatia kile
tunachokihitaji.Tutaendelea
na zoezi hili la kuua
wanafunzi hawa hadi
watakapomalizika na kama
hatakuwa ametekeleza kile
tunachokitaka tutafanya
tukio lingine kubwa zaidi ya
hili” akasema Fahad na
kutoa ishara mwanafunzi
mmoja akaletwa mbele ya
kamera na mtu aliyejifunika
sura yake.Mwanafunzi Yule
aliyekuwa katika mavazi ya
kulalia akapigishwa magoti
mbele ya kamera.Macho yake
yalikuwa mekundu na
yamevimba kwa kulia.
“Binti unaitwa nani?
Akauliza Fahad
“Naitwa Lucy Nswami”
“Lucy una miaka
mingapi?
“Nina miaka kumi na
tano.Tafadhali naomba
msituue.Ongeeni na baba
yangu ni tajiri anafanya
biashara ya madini atawapa
kiasi chochote cha pesa
mnachohitaji.Tafadhali
naomba msituue….”akasema
Lucy na Fahad akasema
“Lucy angalia ile kamera
na umuombe Rais wako
awaokoe kwa kutupa kile
tunachomdai” Huku uso
wake umefunikwa na
machozi Lucy akaiangalia
kamera na kusema
“Mheshimiwa Rais baba
yetu, tunaomba
utuokoe.Tumetekwa na
tunahitaji msaada
wako.Tumeambiwa kwamba
usipowapatia wanachohitaji
watatuua wote. Tunakuomba
Rais tuokoe tusiuawe.Sisi
bado ni wasichana wadogo
na tuna malengo mengi ya
maisha.Tuokoe
mheshim……..” akashindwa
kuendelea akaangua kilio.
“Ndugu
watanzania,wasichana hawa
wanakwenda kupoteza uhai
wao angali wadogo kwa
sababu ya ukaidi wa Rais
wenu.Narudia tena kila
baada ya dakika thelathini
mwanafunzi mmoja
atapoteza uhai” Akasema
Fahad na kumpa ishara
Fulani Yule mtu aliyekuwa
amesimama karibu na Yule
binti.Akaenda katika meza
akachukua kamba
akamfuata Lucy na
kumfunga mikono akaikaza
barabara na kumfunga
kitambaa cheusi usoni halafu
akachukua panga kali
akamsogelea na kuliinua
juu.Panga liliposhuka chini
kichwa cha Lucy
kikatengana na kiwiliwili.
“Huyu ni wa kwanza
.Tutaendelea kuua kila
baada ya dakika thelathini”
akasema Fahad na kamera
ikazimwa.
“Fanyeni usafi na
muuhifadhi huu mwili.Zoezi
hili ni endelevu hadi pale
Rais atakapotekeleza ombi
letu” akasema Fahad na
kuvua ile kofia akatoka
ndani ya kile chumba
IKULU – DAR ES SALAAM
Wakati kikao cha baraza
la usalama la taifa
kikiendelea katika ikulu Dar
es salaam,mmoja wa
wasaidizi wa Rais akaingia
na kumnong’onza kitu Rais
sikioni halafu akatoka
“Nimetaarifiwa kuna
video imeanza kusambaa
mtandaoni ambayo
inasemekana inatoka kwa
watekaji” akasema Dr Evans
na kuwasha runinga
iliyokuwa ukutani na video
ile ikaanza
kuonekana.Chumba cha
mikutano kilibaki kimya na
watu wote mle ndani wakiwa
katika taharuki kubwa
sana.Hawakutegemea kabisa
kama wangeona ukatili
mkubwa kama ule.Dr Evans
kama ilivyo kawaida yake
awapo katika mstuko
midomo ilikuwa
inamtetemeka hakujua
aseme nini.
“Oh my God I can’t
believe this ! akasema waziri
mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania
Evarist Mlukola.Minong’ono
ya chini chini ikaanza na
Elizabeth wimara
mkurugenzi msaidizi wa
idara ya kudhibiti na
kupambana na ugaidi
alishindwa kujizuia
kudondosha machozi.
“Mr President can you
say anything about this
video?akauliza waziri mkuu
ambaye uso wake ulikuwa
umejikunja kwa hasira
“Niseme nini
mheshimiwa waziri mkuu?
Sote tumeshuhudia video hii
na tumeona
kilichotokea.Tumeona
unyama uliofanywa na hawa
magaidi.Kinachotakiwa
kufanyika sasa hivi ni
kufanya kila juhudi
kuhakikisha watekaji hawa
wanapatikana na vile vile
kuwakomboa wasichana
waliotekwa”akasema Dr
Evans
“With all due respect Mr
President you must have to
explain something to us.Sote
tumesikia alichokisema huyu
kiongozi wa magaidi ambaye
ameelekeza lawama zote
kwako kwamba wewe ndiye
sababu ya wao kufanya
mashambulizi kadhaa
likiwamo lile la Mtodora na
kama haitoshi wamewateka
wasichana usiku wa leo na
wameanza kuwachinja kama
kuku kukushinikiza
uwapatie kile ambacho
wanakitaka.Mheshimiwa
Rais katika hili tunahitaji
maelezo ya kina ! Kwa nini
wasimtaje mtu mwingine na
wajielekeze moja kwa moja
kwako?Wanataka nini?
Umekuwa na mawasiliano
nao? Akauliza waziri mkuu
akiwa amekasirika
“Guys nawaombeni
mtulie.Tulikuwa
tunakwenda vyema na kikao
chetu video hii isije
kutuvuruga.Hii ni vita na
hawa magaidi wanatumia
kigezo hicho cha kuelekeza
lawama kwangu moja kwa
moja ili kutuvuruga lakini
ukweli ni kwamba sifahamu
chochote.Sina mawasiliano
nao na sifahamu wanataka
nini”
“Mr president please if
you know something please
tell us so we can save the
innocent children.Watoto
wale wanachinjwa kama
kuku hawana kosa lolote !
akasema waziri mkuu
akionekana kupandisha
jazba
“Mheshimiwa waziri
mkuu naomba utulize jazba
kwani jambo hili linatakiwa
lijadiliwe kwa umakini
mkubwa.Ninafahamu wasi
wasi wako kwani mtoto wako
ni mmoja wa mateka
wanaoshikiliwa,lakini
tunatakiwa kujadili jambo
hili kwa busara na kufikia
maamuzi ya namna bora ya
kukabiliana na watu
hawa.Tukienda kwa papara
tutawapoteza watoto wetu na
watu wengi watakufa.”
Akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais muda
hausimami.Muda mfupi ujao
wasichana wengine
watauawa.We need to act
faster.Kama unalo la
kutuambia mheshimiwa Rais
this is the time.Kama kuna
kitu wanakihitaji hawa
magaidi tuweke wazi ili
tuweze kujadili namna ya
kufanya” Akasema waziri
mkuu kwa jazba.Tayari
alikwisha pandwa na
hasira.Dr Evans naye
alionekana kukerwa na
maneno ya waziri mkuu
“Ndugu waziri mkuu,nchi
haiendeshwi namna
hiyo.Janga hili ni kubwa na
lazima itumike busara na
mbinu kubwa katika
kulishughulikia.Nimekwisha
sema kwamba magaidi hawa
lengo lao ni kutuvuruga kwa
kutunga uongo na ninaanza
kulichukulia jambo hili kama
mbinu ya kunichafua mimi
kisiasa.Yawezekana
wanatumiwa na watu wa
ndani na wa nje kwa
madhumuni yao ya kisiasa
lakini mimi sifahamu
chochote.Siwafahamu watu
hawa na wala sifahamu
wanachokitaka.Suala
kwamba ninajua
wanachokitaka ni uongo
mkubwa.Ninachowaomba
ndugu zangu kitu kikubwa
kwa sasa ni kuviachia
vyombo vya usalama
vilishughulikie hili suala na
kuwakomboa wasichana
wetu”
“Mheshimiwa Rais
watoto wetu wanachinjwa
kama kuku lakini huonekani
kuguswa kabisa!!.Please Mr
president wake up.Act like a
president…!! akasema kwa
ukali waziri mkuu.Dr Evans
naye akafura kwa hasira na
kumtaka waziri mkuu
watoke wakaongee nje.
“Mheshimiwa waziri
mkuu sintavumilia tena
kitendo chako cha dharau
mbele ya
wajumbe.Umenionyesha
dharau kubwa sana.Mimi
ndiye Rais na ndiye mwenye
maamuzi ya nini
kifanyike.Kama una njia
bora ya kuweza
kulishughulikia suala hili
tueleze tukusikie.Tuko
katika kipindi kigumu
tunatakiwa
tushikamane,tuwe kitu
kimoja ,tukianza kuvurugana
sisi viongozi hatutaweza
kukabiliana na suala hili.Hii
ni vita na hawa jamaa
wamedhamiria kutuvuruga
kwanza ili waweze kutupiga
vizuri”akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais
samahani sana kwa kile
kilichotokea mle ndani ya
kikao nadhani unafahamu
namna nilivyo mtiifu
kwako,sijawahi kupingana
nawe hata mara moja,nakiri
nilichokifanya ni utovu wa
nidhamu kwa kiongozi
wangu mkuu naomba
msamaha sana lakini sikuwa
nimekusudia kubishana
nawe mheshimiwa Rais ni
kutokana na hasira na
uchungu nilio nao kujua
kwamba mwanangu ni
mmoja wa watoto walio
mikononi mwa magaidi na
muda wowote anaweza
akachinjwa.Naamini hata
wewe kama mwanao
angekuwa mikononi mwa
magaidi hawa wasio na hata
chembe ya huruma ungejua
nini ninakimaanisha
mheshimiwa Rais ndiyo
maana ninakuomba kama
kuna kitu hawa magaidi
wanakitaka angalia namna
ya kuwapatia ili tuweze
kuwakomboa hawa watoto
wasio na hatia wanaochinjwa
kama ndege.Mheshimiwa
Rais wewe unafahamika ni
Rais mwenye msimamo na
watu wanakupenda sana
unadhani nini kitatokea
baada ya sakata
hili?Litakuwa ni anguko
kubwa la kisiasa na si kwako
tu bali kwetu sote na chama
chetu pia hivyo basi wewe
pekee ndiye unayeangaliwa
na kila mtu hivi sasa.Tukio
hili linaweza kukujenga zaidi
kisiasa au kukubomoa
kabisa” akasema waziri
mkuu na kuanza kupiga
hatua kuondoka Dr Evans
naye akamfuata ndani ya
kile chumba cha mikutano.
“Guys we need a
break.Waziri mkuu
nakuhitaji ofisini
yangu.Baada ya dakika
ishirini turejee tena hapa
tumalizie kikao chetu”
akasema Dr Evans na
kuongozana na waziri mkuu
kuelekea ofisini wakaketi
sofani
“Nakusikiliza
mheshimiwa Rais”akasema
waziri mkuu baada ya
kumuona Dr Evans akiwa
ameinamisha kichwa katika
kiti chake toka walipoingia
mle ofisini
“Mr Evarist sijui nianzie
wapi lakini naomba kile
nitakachokueleza hapa
kibaki kuwa siri yetu na
nimeamua kukueleza kwa
sababu ninakuamini”
“Usihofu mheshimiwa
Rais.Unanifahamu vyema
namna nilivyo mtiifu
kwako,nieleze chochote na
kitabaki ndani ya kuta za
chumba hiki” akasema waziri
mkuu
Dr Evans akavuta pumzi
ndefu na kusema
“Unachokipitia waziri
mkuu na mimi ndicho
ninachokipitia”akasema
DrEvans
“Sijakuelewa una
maanisha nini mheshimiwa
Rais”
“Mwanangu Coletha pia
ametekwa na hao magaidi”
“Coletha..!
Ametekwa..aagh I don’t
understand..how ?Waziri
mkuu akapatwa na
mshangao
“Ni hadithi ndefu lakini
shambulio la juzi katika
hospitali ya Mtodora
lilimlenga mwanangu na
walifanikiwa kumteka na
hadi hivi sasa tunavyoongea
wako naye na yuko katika
hatari ya kuuawa kama
wengine” akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais
sijaelewa sababu ya Coletha
kutekwa nyara na magaidi”
akasema waziri mkuu
“Kuna kitu ambacho
hawa magaidi wanakitaka”
akanyamaza tena kwa
sekunde chache akasema
“Wanamtaka Edger
Kaka”
“Edger kaka? Akauliza
waziri mkuu na kutoa
kicheko kidogo
“Ndiyo wanamtaka Edger
Kaka”
“Huo ni
upuuzi.Wanamtaka
marehemu? Hawajui kama
Edger kaka amekwisha fariki
miaka mitatu iliyopita?
“Edger kaka is not dead”
akasema Dr Evans
“What? Waziri mkuu
akashangaa
“Ni kweli.Edger Kaka
hajafariki yuko hai” akasema
Dr Evans na waziri mkuu
akasimama akamtazama Dr
Evans kwa mshangao
mkubwa
“Mheshimiwa Rais
najaribu kutaka kuamini kile
unachonieleza lakini
ninashindwa kwa sababu
sote tulihudhuria msiba wa
Edger Kaka na tukamzika
sasa unaponiambia kwamba
Edger yuko hai ni kitu cha
ajabu sana.Hicho ni kitu cha
kufikirika.Yuko hai kimwili
au umeonekana mzimu
wake?akauliza waziri mkuu
“Edger Kaka ni mzima
kabisa hakufa katika ile ajali
kama wengi
tunavyoamini.Naomba ukae
nikueleze japo kwa ufupi”
akasema Dr Evans na waziri
mkuu akaketi.
“Siku chache zilizopita
kupitia vyanzo vyangu
nilipata taarifa za Edger
Kaka kuwa hai.Nilianza
kuzifuatilia taarifa hizi kujua
ukweli wake na
nikathibitisha kwamba kweli
Edger Kaka yuko hai.Ajali ile
ambayo ilichukua uhai wake
ilikuwa ya kutengenezwa”
“Ajali ile
ilitengenezwa?akauliza
waziri mkuu
“Ndiyo ilikuwa ajali ya
kutengenezwa”
“Nani walioteneneza ajali
ile na kwa nini?akauliza
waziri mkuu
“Israel”
“Israel?!! Waziri mkuu
akazidi kushangaa
“Ndiyo.Israel kupitia
shirika lao la ujasusi la
Mossad ndio waliotengenezea
ajali ile.Sababu kubwa ya
kutengeneza ajali ile ni ili
kumpata Edger Kaka
ambaye waligundua ana
mahusiano na wafadhili
wakuu wa kikundi cha kigadi
cha IS ambao wanaendesha
mashambulizi ndani ya
Israel.Hiyo ndiyo sababu ya
wao kutengeneza ajali ile
wakafanikiwa kumpata
Edger Kaka na kumpeleka
mafichoni”
“Mheshimiwa Rais
unazidi
kunichanganya.Edger kaka
ana mahusiano na kikundi
cha IS? Akauliza waziri
mkuu
“Ndiyo.Ana mahusiano
na kikundi cha IS”akajibu Dr
Evans
“Haya ni maajabu.Edger
Kaka ni IS?Alikuwa ni
mmoja wa wabunge wenye
kuaminiwa sana hapa
nchini,alisimama kidete na
kupigana vita dhidi ya
ufisadi na kutokana na
juhudi zake wengi
tulimtabiria kufika mbali
kisiasa taarifa za kwamba
ana mahusiano na kikundi
cha IS zimenistua mno”
akasema waziri mkuu
“Nilipigiwa simu na
kiongozi wa kikundi cha IS
akanifahamisha kwamba
wamemteka mwanangu na
wakanipa maelekezo
kwamba kama ninamtaka
mwanangu akiwa hai basi
nisimueleze mtu yeyoite
jambo hili la mwanangu
kutekwa ndiyo maana mpaka
leo sijamweleza mtu yeyote
kama mwanangu katekwa
kila mtu ninamwambia
kwamba mwanangu yuko
sehemu anapumzika lakini
ukweli ni kwamba ametekwa
na magaidi.Pili magaidi hao
wakanitaka nimuachie Edger
Kaka.Magaidi hao
wanafahamu kwamba Edger
Kaka yuko hai lakini hawajui
yuko wapi na wanaamini
kwamba serikali ya Tanzania
ndio tuliotengeneza ajali ile
na kwamba tunafahamu
mahala alipo Edger.Jana
walinipigia simu na kunitaka
leo saa mbili za asubuhi niwe
nimemuandaa Edger Kaka
na watanipa maelekezo
sehemu ya kumpeleka lakini
niliwaonya kwamba
nitawasaka kwa nguvu
zangu zote hadi nihakikishe
nimewafyekelea mbali na
hapo ndipo vita ilipopamba
moto na wakavamia shule ya
sekondari wakateka
wasichana na sasa
wameanza kuwaua.Kauli ya
kwamba kuna kitu
wanakidai kutoka kwangu ni
huyo Edger kaka” akasema
Dr Evans
“Jesus Christ ! akasema
waziri mkuu.
“Mheshimiwa Rais
ulipaswa kuliweka wazi
suala hili ili lishughulikiwe
na vyombo husika kabla
jambo hili halijawa kubwa
kama lilivyo
sasa.Hukupaswa kulifanya
jambo hili kuwa
siri.Tumefika hapa tulipofika
kwa sabab……….” Akasema
waziri mkuu lakini Dr Evans
akamkatisha
“Jambo hili ni kubwa
zaidi ya unavyofikiri.Si
kwamba sikuwa na uwezo wa
kutumia vyombo vya ulinzi
na usalama kuwatafuta
magaidi hawa lakini
nililazimika kulifanya siri
kwa sababu maalum”
“Mheshimiwa Rais hili si
suala la kufanya
siri.”akasema waziri mkuu
“Ni suala la siri !
akasema Dr Evans
“Kuna sababu gani ya
kulifanya suala hili kuwa siri
na kuwaacha magaidi
wafanye watakacho ndani ya
ardhi yetu? Wameteka watu
na wanaanza kuwaua.Hii
haikubaliki kabisa
mheshimiwa Rais.Tusiwape
nafasi magaidi ya kufanya
wakitakacho.Tanzania
hatuwezi kuwaogopa magaidi
! akasema waziri mkuu.
“Si kwamba kulifanya
suala hili liwe siri ni kuwapa
nafasi magaidi
watambe.Kuna operesheni ya
chini kwa chini inayoendelea
kuwatafuta magaidi hawa
mahala walipo na
kuwakomboa watoto wote
waliotekwa” akasema
DrEvans
“Nani wanafanya hiyo
operesheni?
“Nina kikosi cha
majasusi mahiri ambao
wanalioshughulikia hili
suala na wako katika hatua
nzuri hivi sasa” akasema Dr
Evans
“Ni akina nani hao?
“I’m sorry I can’t tell you
right now ni akina nani
wanaolishughulikia hili
jambo”
“Mheshimiwa Rais
unanishangaza sana kwa
namna jambo hili
unavyolifanya kuwa
siri.Kuna kitu gani hapa
ambacho hutaki kukiweka
wazi?Ninashindwa
kukuelewa mheshimiwa
Rais”
“I have my reasons!
Akasema Dr Evans
“Ni sababu zipi hizo
ambazo zinakusababisha
kutolifikisha suala hili kwa
vyombo husika?Umekuwa
unawalaumu wakuu wa
vyombo vya usalama
kwamba hawafanyi kazi zao
vyema wakati kumbe unazo
taarifa zote za magaidi hawa
lakini uko
kimya.Mheshimwa Rais
….”akasema waziri mkuu
Rais akamkatisha
“Waziri mkuu nimesema
kwamba suala hili
ninalishughulikia kwa
namna ninavyojua mimi na
ninakuomba yale
niliyokueleza yawe siri yako
sitaki jambo hili
livuje.Umenielewa? akauliza
Dr Evans akionekana
kukasirika
“Mheshimiwa Rais
mwanangu anashikiliwa na
magaidi na hatujui
yawezekana yeye akawa ni
wa pili kuchinjwa unadhani
nitakuelewa vipi
unaposhindwa kuchukua
hatua madhubuti za
kupambana na magaidi
hawa?
“Si mwanao tu ambaye
anashikiliwa na magaidi
hawa.Hata mimi pia nina
uchungu pia kwani sijui hali
ya mwanangu
ikoje.Sifahamu kama ni
mzima au wamekwisha
muua lakini pamoja na
uchungu huo ninalichukulia
suala hili kwa umakini
mkubwa sana na ndiyo
maana sijataka suala hili
lijulikane kwa sababu
inaonekana huu ni mtandao
mkubwa na wengine
wamepandikiwa katika
vyombo vyetu vya ulinzi na
usalama.Edger Kaka hakuwa
peke yake lazima wapo watu
aliokuwa anashirikiana nao
hivyo basi kuliweka wazi hili
jambo taarifa zitawafikia
magaidi na mipango yetu
yote itajulikana ndiyo maana
ninalishughulikia kimya
kimya” akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais
utaniona mtovu wa nidhamu
lakini hapa tunazungumzia
maisha ya watoto wasio na
hatia wanaoendelea
kuuawa.Wananchi
hawatatuelewa kama
hatutachukua hatua za
haraka kuwazuia magaidi
hawa wasiendelee kufanya
mauaji ya watoto
wetu.Lazima tuwadhibiti
haraka sana kwa kila namna
tuwezavyo” akasema waziri
mkuu.
“Magaidi watadhibitiwa
lakini si kwa haraka kama
unavyotaka
wewe.Tunakwenda taratibu”
akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais suala
hili si la kwenda nalo
taratibu.Magaidi wameahidi
kuua watoto wetu kila baada
ya nusu saa hatupaswi
kulichukulia rahisi hili
jambo.Nchi iko katika
taharuki wananchi hawana
uhakika na usalama wao
macho yao yote yako kwetu
sisi lazima tuchukue
maamuzi magumu ya
kulimaliza hili jambo na
kuwakomboa watoto wetu
wanaoshikiliwa na magaidi”
akasema waziri mkuu.Dr
Evans akafikiri kidogo na
kusema
“Kwa mtazamo wako
unashauri nini
kifanyike?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa Rais
kwanza nataka kufahamu
Edger Kaka yuko wapi?Je
umejiridhisha ni kweli yuko
hai?akauliza waziri mkuu
“Ni kweli Edger Kaka
yuko hai nimejiridhisha kwa
hilo na tayari kikosi
kinachoshughulika na suala
hili kimefanikiwa
kumkomboa kutoka mahala
alikokuwa amefichwa na
serikali ya Israel na yuko
hapa nchini.Hivi
tunavyoongea anafanyiwa
mahojiano”
“Pongezi kubwa kwa hilo
mheshimiwa Rais lakini
mimi ushauri wangu ni
huu.Taifa liko katika
taharuki kubwa
sana.Kitendo walichokifanya
magaidi hawa cha
kuwachinja kama kuku
wanafunzi waliowateka
hakijawahi kuonekana hapa
nchini na kimeleta hofu
kubwa mno.Ili kuirejesha
nchi katika hali ya kawaida
ninashauri kwamba
tukubaliane na hawa
magaidi tuwapatie kile
wanachokitaka”akasema
waziri mkuu na Dr Evans
akasimama
“Mheshimiwa waziri
mkuu niambie haumaanishi
hicho unachokisema”
akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais
ninamaanisha.Hatuna ujanja
hawa jamaa tayari
wamekwisha tubana katika
kona na lazima tukubaliane
nao ili tuwaokoe wasichana
wetu.Timu inayoshughulikia
hili suala hatuna uhakika
kama itafanikiwa kuwapata
magaidi hawa
leo.Mheshimiwa Rais watu
hawa kabla ya kufanya
shambulizi lolote lile
wanakuwa tayari
wamekwisha jipanga vya
kutosha kukabiliana na
nguvu yoyote itakayotumika
kuwatafuta.Ninaamini hadi
kikosi hicho unachokitumia
kifanikiwe kuwapata mahala
walipo tayari idadi kubwa ya
watoto wetu kama si wote
watakuwa wamechinjwa
ndiyo maana nashauri
kwamba tuwape hicho
wanachokitaka halafu
tujipange upya namna ya
kuwakabili.Kuwapa kile
wanachokitaka kwa ajili ya
kuwakomboa watoto wetu si
kushindwa vita ni jambo la
kawaida.Edger Kaka hana
msaada wowote kwetu kwa
muda ambao tulijua
amefariki dunia hakuna
shughuli yoyote iliyosimama
hapa nchini hivyo hakuna
kitu
tutakachopungukiwa.Watu
wote hapa nchini wanajua
Edger amefarki dunia na
hata tukiwapa magaidi mtu
wao hakuna atakayejua bado
jambo hili litaendelea kuwa
siri kama unavyotaka na
watoto wetu watakombolewa
na baada ya hapo tutaanza
kufanya uchunguzi kuubaini
mtandao huu hapa nchini”
akasema waziri mkuu na
kumfanya DrEvans azame
mawazoni.
“Mheshimiwa Rais muda
unakwenda mbio.Muda si
mrefu kutoka sasa magaidi
hawa watarusha tena video
ya pili wakimchinja mtoto
mwingine kama ndege.Siri
hii tutaifahamu sisi watu
wachache.Kama Edger kaka
atakuwa na umuhimu
mkubwa bado tutaendelea
kumsaka na kumtia
mikononi kwa kutumia
vyombo vyetu” akasema
waziri mkuu.Baada ya
tafakari ya dakika tatu Dr
Evans akasema
“Mawazo yako si mabaya
mheshimiwa waziri
mkuu.Kuna kitu cha msingi
nimekiona ndani
yake.Nadhani tukubaliane
na hawa jamaa na tuwape
kile wanachokitaka ili
tuweze kuwakomboa watoto
wetu na nchi itulie” akasema
Dr Evans
“Mheshimiwa Rais hayo
ndiyo maamuzi kama Rais.Si
kila wakati tutashinda kuna
nyakati tutashindwa na
katika hili si kwamba
tumeshindwa bali
tumekubali yaishe lakini
tutajipanga tena upya
kuwakabili vilivyo magaidi
hawa”akasema waziri
mkuu.Dr Evans akachukua
simu na kumpigia Austin
January mkuu wa kikosi cha
jeshi cha operesheni maalum
“Mheshimiwa Rais”
akasema Austin
“Austin nataka kujua
kinachoendelea hapo sasa
hivi kuhusiana na Yule mtu
wetu Edger Kaka”
“Kwa sasa
kinachoendelea ni
mahojiano.Mathew amempa
Edger mapumziko mafupi
kabla ya kurejea tena
kuendelea kumuhoji”
“Kuna mategemeo ya
kupata kitu chochote kutoka
kwake?akauliza Dr Evans
“Mategemeo yapo lakini
si kwa haraka.Inahitaji
subira kidogo kwani kila
mbinu zinatumika” akasema
Austin
“Sawa Austin
nimekuelewa.Nimekupigia
simu ili tuzungumze jambo
moja la muhimu sana”
“Nakusikiliza
mheshimiwa Rais”
“Nadhani tayari unazo
taarifa kwamba usiku wa
kuamkia leo magaidi
walivamia shule moja ya
sekondari wakateka watoto
na tayari wameanza
kuwachinja wakitaka
tumuachie Edger
Kaka.Baada ya tafakari ya
kina nimeona hakuna haja
ya kuendelea kumshikilia
Edger Kaka wakati magaidi
wanaendelea kuua watoto
wetu.Nimeamua kuwapa kile
wanachokitaka yaani Edger
Kaka.Najua ni maamuzi
yatakayowastua sana akina
Mathew hasa baada ya kazi
kubwa na ngumu ya
kumrejesha nyumbani lakini
sina namna ya kufanya kwa
haraka kuzuia watoto wetu
wasiendelee kuuawa.Magaidi
tayari wamemuua binti
mmoja na wameahidi
kuendelea kuua watoto
wengine kila baada ya nusu
saa hivyo nimeamua kuwapa
wakitakacho.Naomba jambo
hili liwe siri yako na
usiwaeleze akina
Mathew.Kuna mtu
ninamtuma sasa hivi
anakuja hapo kambini
kumchukua Edger Kaka”
akasema Dr Evans na katika
line ya simu kukawa na
ukimya mkubwa
“Austin are you
there?akauliza Dr Evans
“Nipo mheshimiwa Rais”
“Good.Umenielewa
nilichokisema?
“Nimekuelewa
mheshimiwa Rais,nitafanya
kama ulivyoelekeza” akajibu
Austin
na DrEvans akakata
simu
“Mheshimiwa Rais
hakuna namna unayoweza
kuwasiliana na hawa jamaa
ukawajulisha kwamba
wasifanye tena mauaji
mengine ya watoto kwani
ombi lao unalifanyia kazi?
Akauliza waziri mkuu
“Wao ndio hupiga simu
pale wanapohitaji
kuzungumza nami.Naamini
kabla ya kufanya mauaji
mengine lazima watanipigia
simu” akasema Dr Evans na
kumuita mmoja wa wasaidizi
wake akampa maelekezo ya
kwenda katika kambi ya
kikosi cha operesheni
maalum akamchukue Edger
Kaka na kisha asubiri
maelekezo
“Ni namna gani
tutafanya makabidhiano na
hao jamaa? Tutakuwa na
uhakika gani kama tukiwapa
mtu wao watarejesha watoto
wetu?akauliza waziri mkuu
“Shida yao ni kumpata
Edger Kaka pekee hivyo
watakapompata hawatakuwa
na sababu ya kuendelea
kuwashikilia watoto wetu”
akanyamaza Dr Evans baada
ya simu yake
kuita.Akazitazama mpigaji
halafu akamtazama waziri
mkuu
“Wenyewe wanapiga”
akasema Dr Evans na
kutazama saa
“Why don’t we trace that
call na kufahamu mahala
walipo?
“They are not
stupid.They are very smart
people.This phone is
untraceable! Akasema Dr
Evans
“Sawa waambie wasiue
tena watoto tunawapa mtu
wao” akasema waziri mkuu
na Dr Evans akapokea simu
“Mheshimiwa Rais sina
maneno mengi nadhani
salamu zetu tayari
umekwisha zipata.Zoezi
tulilolianza linaendelea
nimekupigia kukujulisha
kwamba ndani ya dakika
chache zijazo tutaondoa
shingo ya mwanafunzi
mwingine.Ninataka
kufahamu kuna mabadiliko
yoyote au bado msimamo
wako ni ule ule?
“Tafadhali msiue tena
mwanafunzi mwingine.Ninyi
ni watu makatili sana
mmetoa uhai wa mwanafunzi
asiye na hatia ! akafoka Dr
Evans
“Damu ya mwanafunzi
Yule na wote tutakaoendelea
kuwatoa uhai iko juu yako
mheshimiwa Rais.Wewe ni
sababu ya watoto hawa wasio
na hatia kuuawa.Kama
unataka kuokoa maisha yao
tekeleza kile tunachokitaka
na wataendelea kuwa salama
lakini ukitaka kushindana
nasi utawapoteza wote.Sisi
hatuogopi kufa mheshimiwa
Rais hapa tulipo tumevaa
mabomu tayari kujilipua na
watoto hawa pale
itakapolazimu kufanya
hivyo”
“Tafadhali msiue tena
mtoto mwingine.Nitawapa
kile mnachokitaka.Nitawapa
Edger Kaka.Ninaomba
mnipe muda zaidi ili niweze
kumuandaa kwa ajili ya
kuwakabidhi ila naomba
mtakapompata mtu wenu
msiendelee tena na mauaji
ya watu wasio na hatia”
“Mheshimiwa Rais tupe
mtu wetu na sisi tutasitisha
mauaji na hautasikia tena
kuna mtu ameuawa na IS
hapa nchini kwako.Kwa
kuwa umekubali kuimaliza
hii vita nitakupigia baada ya
nusu saa na kama utakuwa
unanidanganya nitawakata
vichwa wanafunzi saba.!
Akasema na kukata simu.
“Wameongeza tena nusu
saa.Kama hatutakuwa
tumewakabidhi mtu wao
wataua wanafunzi saba”
“Mheshimiwa Rais hawa
jamaa hawatanii kabisa.Ni
watu wenye roho za kikatili
mno” akasema waziri mkuu
“Ndani ya muda huo
tayari Edger atakuwa
amepatikana na tutasubiri
maelekezo yao mahala pa
kumpeleka na mahala
tutakapowapata watoto
wetu” akasema Dr Evans
“Nimewahi kufanya kazi
na Edger Kaka bungeni
alikuwa mmoja wa wabunge
mahiri mno katika
kuchangia mambo mbali
mbali.Kila aliposimama
bunge lilikaa kimya
kumsikiliza.Bado
ninatafakari taarifa hizi
kwamba ana mahusiano na
kikundi cha IS” akasema
waziri mkuu.
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 9
Austin January
aliegemea meza ya ofisi yake
baada ya kumaliza
kuzungumza na
Rais.Alikuwa katika mawazo
mengi.
“Nini kimetokea hadi
Rais anataka kumkabidhi
Edger Kaka kwa magaidi
ambao wanafanya mauaji
ndani ya ardhi yetu?Hapa
Rais amekosea.Nilikula
kiapo cha kumtii Rais lakini
kwa hiki anachotaka
kukifanya niko tayari
kuvunja kiapo changu.Edger
ni mshirika wa magaidi na
kamwe hawezi kukabidhiwa
kwa magaidi.Hatuwezi
kusalimu amri kwa magaidi
hata siku moja.Lazima nikiri
hapa Rais ameonyesha
udhaifu mkubwa.Ana
uhakika gani kama akiwapa
wanachokitaka watawaachia
watoto wanaowashikilia?Ni
vipi kama akiwapa mtu wao
na wasiwaachie watoto na
wakaanzisha tena madai
mengine? Wanaweza
wakasema hivyo kwani
tayari wamekwisha muona
ana udhaifu” akawaza Austin
na kutoka haraka ofisini
kwake akaelekea katika
chumba cha mahojiano
akawakuta Gosu Gosu na
Devotha wakifuatilia
mahojiano ya Mathew na
Edger
“Kuna chochote
kimepatikana?akauliza
“Mathew ameingia muda
mfupi uliopita kuendelea
kumuhoji Edger”akajibu
Gosu Gosu na Austin
akafungua mlango akaingia
ndani ya kile chumba cha
mahojiano
“Mathew excuse me can I
talk to you for a second?
akasema na Mathew akatoka
“Mathew we need to get
out of here now !
“Nini
kimetokea?akauliza Mathew
kwa mshangao
“Listen to me Mathew
we’re leaving this place now !
“I don’t understand you
Austin.Nini
kimetokea?Tunakwenda
wapi?Vipi kuhusu mahojiano
na Edger?akauliza Mathew
“Tunamchukua
tutakwenda kuendelea na
mahojiano naye huko mbele
ya safari.We need to
hurry.Tusaidiane tumbebe
tuondoke! Akasema Austin
na Mathew akamuita Gosu
Gosu wakasaidiana
wakambeba Edger Kaka
wakamfuata Austin hadi
katika gari la Mathew aina
ya land cruiser v8 rangi
nyeusi wakamuingiza Edger
sehemu ya nyuma na
kumlaza Gosu Gosu akapewa
kazi ya kumchunga na
Austin akaondoa gari.
“Austin what happened?
Akauliza Mathew baada ya
kulivuka geti.
“Something happened
nitawaeleza mbele ya
safari”akasema Austin
“Tunakwenda
wapi?akauliza Mathew
ambaye alistushwa sana na
mabadiliko yale ya Austin
“Somewhere safe”akajibu
Austin huku akiwa makini
kufuatilia kama kuna gari
yoyote inawafuata.
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 10
Kitendo cha magaidi
kurusha mtandaoni video
wakimchinja mmoja wa
wanafunzi waliomteka
kiliamsha hasira kali kwa
wazazi wa wanafunzi
waliokuwa wamekusanyika
katika shule ya sekondari ya
St.Getrude ambako
wanafunzi waliotekwa
walikuwa wanasoma.Umati
mkubwa wa wazazi na watu
wengine ulikuwa
umekusanyika katika shule
hii kupata taarifa za
kilichotokea na kujua hatima
ya watoto wao.Mkuu wa
polisi wa kituo kilichokaribu
na shule ile ambaye
alikuwepo pale shuleni na
timu ya makachero
wakiendelea na uchunguzi
wa tukio lile aliwasihi
wananchi wale wawe
watulivu kwani suala lile
linashughulikiwa na jeshi la
polisi pamoja na vyombo
vingine vya ulinzi na
usalama.
Video ya mwanafunzi
akichinjwa mabayo ilisambaa
mtandaoni kwa kasi kubwa
iliamsha hasira kali kwa
wananchi wale na vilio
vikasikika.Illazimu kuongeza
askari polisi zaidi eneo lile
kwani tayari kulikwisha
anza kuonekana viashiria
vya kuvunjika amani.Askari
polisi baada ya kuona hali
imebadilika na hasira
miongoni mwa wananchi
wale imepanda wakawataka
wazazi wale kutawanyika
eneo lile kwani suala la
watoto wao kutekwa
linashughulikiwa na
watapewa taarifa.Kutoka
ndani ya gari moja jeupe
ambalo lilikuwa limeegeshwa
pembeni kabisa ya shule
akashuka mtu mmoja akiwa
na kipaza sauti akapanda
juu ya gari na kuanza
kutangaza.
“Jamani watoto wetu
wametekwa,wanauawa na
hatupati jibu lenye uhakika
kuhusu juhudi za
kuwatafuta.Tukiendelea
kukaa hapa hatutawapata
watoto wetu.Twendeni
tuanze maandamano
kuelekea ikulu kwa Rais
kushinikiza juhudi za
kuwatafuta watoto wetu.Bila
kutoa shinikizo kwa serikali
watoto wetu
hawatapatikana.Twendeni
ikulu hatuogopi
mabomu,tunaandamana wa
amani kushinikiza serikali
iwatafute watoto wetu.Tuko
pamoja jamani? akauliza
Yule jamaa na wananchi
wote wakamuunga mkono na
maandamano yakaanza
kutoka pale shuleni
wakitembea kwa mguu
kuelekea ikulu.Waliingia
katika barabara kuu na
kulazimisha magari
kusimama kwa muda
kuwapisha wapite.Kadiri
walivyozidi kusonga mbele
ndivyo taarifa zilizvyozidi
kusambaa na idadi ya watu
kuzidi kuongezeka.Jeshi la
polisi lililazimika kuchukua
hatua za kuyatawanya
maandamano yale
yasiyokuwa na kibali ambayo
yalianza kugeuka kero kwa
watu waliokuwa wakiendelea
na shughuli zao kwani kila
walikopita ililazimu shughuli
zote kusimama kwa muda.
Gesi ya kutoamachozi na
maji ya kuwasha vilitumika
katika kuwatawanya
waandamanaji wale na
kusababisha mtafaruku
mkubwa.Mtifuano ule kati ya
polisi na waandamanaji
ulikuwa ni kama kuongeza
mafuta katika moto kwani
idadi ya watu ilizidi
kuongezeka,biashara
kufungwa shughuli
zikasimama na wengi
wakajiunga katika
maandamano yale ya
kuishinikiza serikali iweze
kupambana na magaidi wale
na kuwakomboa watoto
waliotekwa.
Taarifa za maandamano
yale makubwa zilifika ikulu
katika chumba ambamo
mkutano wa dharura wa
baraza la usalama la taifa
ulikuwa unaendelea na
kumlazimu Rais kuahirisha
kwa muda kikao kile hadi
jioni ili waweze
kushughulikia lile suala
lililojitokeza.Yeye na waziri
mkuu wakaelekea ofisini
“Mheshimiwa Rais
nadhani sasa umeamini
maneno yangu
niliyokwambia kwamba
suala hili litakuwa kubwa
sana na tayari moto umeanza
kuwaka.Wananchi wana
hasira kali ndiyo maana
wameingia barabarani
wakiandamana kushinikiza
serikali kufanya juhudi za
kuwakomboa watoto wao
waliotekwa na
magaidi”akasema waziri
mkuu
“Ulikuwa sahihi
kabisa.Hakuna tena haja ya
kuendelea kupambana na
hawa jamaa tuwape kile
wanachokitaka na tuwapate
watoto wetu” akasema Dr
Evans na kuchukua simu
akampigia Austin lakini
simu ikaita bila
kupokelewa.Akapiga tena
bado simu iliendelea kuita
bila kupokelewa.
“Kwa nini Austin hapokei
simu?akajiuliza Dr Evans na
kumpigia simu mtu
aliyemtuma kwenda
kumchukua Edger kaka
“Mheshimiwa Rais”
akasema Yule jamaa baada
ya kupokea simu
“Ben umefika wapi?
“Mheshimiwa Rais tayari
nimefika hapa mahala
uliponituma lakini kuna
tatizo nimelikuta hapa na
nilikuwa katika harakati za
kukupigia simu kukujulisha”
“Kuna tatizo gani?
akauliza
“Austin hayupo hapa
kambini na kwa taarifa
nilizopewa ameondoka hapa
kambini kama dakika kumi
na tano
zilizopita.Nimepelekwa kwa
msaidizi wake nikampa
maagizo uliyonipana
akaniambia kwamba mtu
niliyetumwa kuja
kumchukua Edger Kaka
ambaye ameletwa kutoka
Nairobi alfajiri ya leo
amechukuliwa na akina
Austin na hajui
wamempeleka wapi”
“What ? That can’t
be.Nimezungumza na Austin
na kumpa maagizo kwamba
nitatuma mtu kwenda
kumchukua Edger kaka sasa
iweze aondoke naye?Hebu
mpe simu huyo msaidizi
wake nizungumze naye !
akasema Dr Evans kwa ukali
“Mheshimiwa Rais”
ikasema sauti ya upande wa
pili
“Derick nataka
kufahamu Austin
amekwenda wapi?
“Hakuna anayejua
amekwenda wapi
mheshimiwa
Rais,ameondoka hapa bila
kumjulisha mtu yeyote
mahala anakoenda”
“Alikuwa ameongozana
na nani?
“Kwa mujibu wa
waliomuona wakati
akiondoka alikuwa
ameongozana na wale jamaa
aliokuwa nao katika
operesheni ya Nairobi jana
usiku,Mathew Mulumbi na
wenzake vile vile
walimchukua Edger Yule
mtu waliyekwenda
kumkomboa Nairobi na
hakuna anayejua
wamekwenda wapi” akasema
Derick
“Bastard ! akasema
DrEvans na kugonga meza
kwa hasira
“Derick hakuna namna
mnayoweza kumfuatilia
Austin kufahamu mahala
alipo?
“Mheshimiwa Rais
haitakuwa rahisi kwa kuwa
hawajumia gari la kikosi
wametumia gari walilokuja
nalo akina Mathew
Mulumbi.Magari yetu ya
kikosi ingekuwa rahisi
kufuatilia kwa sababu yote
yana mfumo ambao
unatuwezesha kufahamu
mahala yalipo”
“Oh my God ! Kwa nini
Austin amenifanyia
hivi?akauliza Dr Evans na
ukimya mfupi ukapita halafu
akasema
“Derick ninakupa kazi ya
kumtafuta Austin.Tumia njia
zozote unazozijua kumtafuta
na ukifanikiwa kujua mahala
alipo nijulishe haraka
sana.Ninakuahidi zawadi
kubwa mno kama
ukilifanikisha hilo.Nitakupa
hata uwaziri kama
utafanikiwa kumpata
Austin.Derick ninamaanisha
ninachokisema kwani suala
hili ni muhimu mno kwa
taifa.Austin amefanya kosa
kubwa sana.Umenielewa
Derick?
“Nimekuelewa
mheshimiwa Rais”
“Good.Tumia kila aina ya
uwezo mlio nao hapo kikosini
kumtafuta Austin mahala
alikoelekea.Watumie
wataalamu wote mlio nao
hapo na kama mkifanikisha
kumpata nitawazawadia
shilingi bilioni moja
mgawane na ahadi yangu ya
kuupa nafasi kubwa ndani ya
serikali iko pale pale.Derick
umenielewa
ninachokimaanisha?
“Nimekuelewa
mheshimiwa Rais na
ninakwenda kuianza kazi
hiyo sasa hivi”
“Good.Nijulishe ukipata
chochote” akasema Dr Evans
na kuiweka simu mezani
“Nini kimetokea
mheshimiwa Rais?akauliza
waziri mkuu
“That bastard Austin is
gone.Edger Kaka is gone!
“Sijakuelewa
mheshimiwa Rais
ametoweka vipi?
“Give me a second”
akasema Dr Evans na
kumpigia simu Kaiza
“Mheshmiwa Rais
shikamoo mzee” akasema
Kaiza
“Kaiza nataka nikupe
kazi ambayo ukiifanya
kikamilifu nitakupa zawadi
kubwa ambayo hukuwahi
kuitegemea.Safari hii sitaki
mzaha” akasema DrEvans
“Niko tayari mheshimiwa
Rais kwa kazi yoyote”
“Good.Nataka utumie
kila aina ya uwezo ulio nao
kumtafuta
Devotha.Ninamuhitaji sana
tena kwa haraka.Ukifahamu
mahala alipo nijulishe
haraka sana.Nakuahidi
Kaiza kama uifanikiwa
kumpata Devotha nitakupa
nafasi kubwa sana ambayo
hukuwa umeitarajia”
“Mheshimiwa Rais
ahsante kwa jukumu hilo
naomba unipe muda
nilifanyie kazi kwa kutumia
kila uwezo nilio nao”
akasema Kaiza na Dr Evans
akakata simu
“Mheshimiwa Rais nini
kinaendelea?Nini
kimetokea?Hao uliokuwa
unazungumza nao ni akina
nani?akauliza waziri mkuu
“Edger is gone.Siamini
kama Austin amenifanyia
kitu kama hiki.oh my God !
“Who is Austin?
“Ni mkuu wa kikosi
nilichokituma kwenda
kumchukua Edger kaka
mahala alikokuwa
amefichwa.Baada ya
kufanikiwa kumrejesha
Edger kaka nyumbani
nilielekeza ahifadhiwe
mahala salama kitu cha
kushangaza baada tu ya
kumwambia kwamba
ninatuma mtu kwenda
kumchukua,Mathew
amemtorosha na
hawajulikani wamekwenda
wapi.I’m sure this was
Mathew’s idea !
“Mathew ! who is he?
Akauliza waziri mkuu
“Mheshimiwa kwa sasa
tujielekeze katika kutafuta
plan B.Tayari kumeanza
kuonekana mkwamo katika
mpango wetu wa kumkabidhi
Edger kaka kwa IS”
“Mheshimiwa Rais
sijakuelewa nini hasa
kimetokea? Kwa nini Edger
asipatikane?akauliza waziri
mkuu
“Waziri mkuu hili
limekuwa ni tatizo kubwa
kwa sasa tujaribu kubuni
namna nyingine ya
kulishughulikia hili suala
wakati jitihada za kuwasaka
hao jamaa waliomtorosha
Edger zinaendelea”
“Mheshimiwa Rais hao
watu kwa nini
wamemtorosha Edger?
“Siwezi
kufahamu.Naomba
tusipoteze muda
mheshimiwa waziri mkuu
tujitahidi kutafuta namna ya
kukabiliana na hili
suala.Kumbuka wale jamaa
wameahidi kuua wasichana
saba kama hatutawapatia
Edger katika muda huo
walioutoa”
“Nimechanganyikiwa
mheshimiwa Rais na sijui
nifanye nini” akasema waziri
mkuu na kuzama katika
tafakari ya muda mfupi
halafu akasimama
“Mheshimiwa Rais sasa
nimekuelewa lakini naomba
nikufahamishe kitu kimoja
kwamba mimi si mtoto
mdogo unayeweza kucheza
na akili yangu.Nafahamu
yote hii ni michezo yako
unataka kunichezea lakini
nakuhakikishia kwamba
haitafanikiwa kamwe.Mpaka
sasa sijafahamu kitu gani
ambacho unakificha na
hutaki kuliweka wazi hili
suala kwa vyombo husika
vilifanyie kazi.Sitaki tena
kupoteza muda kujua kitu
gani unakificha lakini siwezi
kamwe kuendelea kukaa
hapa kupoteza muda wakati
watoto wetu wakiendelea
kuchinjwa kama kuku !
akasema kwa ukali waziri
mkuu na kugeuka akaanza
kupiga hatua kuelekea
mlangoni Dr Evans akabaki
amepigwa na butwaa
“Mheshimiwa waziri
mkuu !! akaita Dr Evans
lakini waziri mkuu
hakugeuka akaufungua
mlango na kutoka
hakupoteza muda akachukua
simu na kumpigia kamanda
wa polisi kanda maalum ya
Dar es salaam na kumtaka
asiwatawanye waandamanaji
bali awaache wakusanyike
yeye anakwenda mahala
hapo.Baada ya kuzungumza
na kamanda wa polisi waziri
mkuu akainga katika gari na
msafara wake ukaondoka
ikulu.Akiwa garini
akaamuandikia mtu Fulani
ujumbe mfupi
“Our plan is
working.Ninaelekea kwenye
maandamano.Tukutane
hapo”
Kamanda wa polisi
kanda maalum ya Dar es
salaam alifika sehemu
ambako maandamano ya
wananchi waliokuwa
wanakwenda ikulu kutaka
kumshinikiza Rais kufanya
juhudi za kuwakomboa
wasichana waliotekwa
yalizuiliwa.Kwa kutumia
kipaaza sauti aliwatangazia
waandamanaji warejee
sehemu ile na wawe watulivu
wamsubiri waziri mkuu
ambaye alikuwa njiani
akielekea mahala pale
kuzungumza nao.Polisi wote
waliondolewa na kuingia
katika magari yao ili
kuondoa hofu kwa
waandamanaji
Dakika kumi na saba
msafara wa waziri mkuu wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania ukawasili eneo
ambalo maandamano
yalizuiliwa.Watu walikuwa
wamekusanyika tena baada
ya tamko lile la kamanda wa
polisi wa kanda maalum ya
Dar es salaam.Baada ya
kufika eneo la tukio waziri
mkuu akazungumza na
kamanda wa kanda maalum
halafu akajitokeza juu ya
gari lake akapewa kipaza
sauti
“Habari za asubuhi
ndugu zangu” akawasalimu
watu wale waliokuwa
wamekusanyika.Watu
wengine waliokuwa
wametawanyika na kujificha
wakiogopa askari polisi
wakajtokeza na kuanza
kurejea baada ya kumuona
waziri mkuu.
“Kwanza kabisa
nachukua nafasi hii
kuwapeni pole sana kwa kile
kilichotokea usiku wa
kuamkia leo baada ya
magaidi kuwateka watoto
wetu sitini na sita.Kama
haitoshi wamefanya unyama
mwingine mkubwa kwa
kuanza kuwaua watoto
wetu.Huu ni ukatili
uliopitiliza na hauvumiliki.
Ndugu zangu nimekuja
hapa kama mzazi kwani na
mimi pia mwanangu ni
mmoja wa watoto
waliotekwa.Nimekuja
kuungana nanyi katika
kuishinikiza serikali iweze
kufanya kila iwezalo
kuhakikisha watoto wetu
wanakombolewa”akasema
waziri mkuu na watu
wakashangilia
“Najua wengi
mtashangaa sana kwa nini
nije kuungana nanyi wakati
mimi ni sehemu ya serikali
ambayo inatakiwa
kuhakikisha inafanya kila
juhudi za kuwakomboa
watoto wetu lakini hapa sipo
kama waziri mkuu
ninaungana nanyi kama
mzazi na tutaandamana wote
kwa pamoja kwa amani huku
tukishindikizwa na polisi
tukielekea ikulu
kumshinikiza Rais aweze
kutumia nguvu yake
kuwakomboa watoto
wetu.Rais anao uwezo wa
kuwakomboa watoto wetu na
kuzuia wasiuawe na magaidi
hivyo tunakwenda ikulu na
hatutaondoka pale hadi
tutakapohakikisha watoto
wetu
wamekombolewa.Msiogope
ndugu zangu lazima
tushikamane imara
kuhakikisha watoto wetu
wanarejeshwa” akasema
waziri mkuu huku
akishangiliwa akashuka
garini na kwenda kuungana
na waandamani
wakashikana mikono na
safari ya kuelekea ikulu
ikaanza.Maandamano yale
ambayo sasa yaliongozwa na
waziri mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania
yaliendelea kuzoa idadi
kubwa ya watu na kulifanya
jiji la Dar es salaam
kusimama kwa muda.
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 11
Baada ya kutoka katika
kambi yao,Austin
aliwapeleka akina Mathew
hadi katika nyumba Fulani
iliyokuwa na ukuta wa
mawe.Haikuwa nyumba
kubwa sana ilikuwa na
vyumba vitatu vya kulala
sebule jiko chumba kidogo
cha kupumzika na chumba
cha kusomea.
“Karibuni ndani jamani”
akasema Austin na
kumsaidia Gosu Gosu
kumbeba Edger na
kumuingiza ndani
wakampeleka katika moja
wapo ya chumba na
kumfunga pingu mkononi
katika dirisha lililokuwa
karibu na kitanda
alicholazwa.
“Whats’s going on
Austin?akauliza Mathew
“Wakati ukiendelea
kumuhoji Edger nilipokea
simu kutoka kwa Rais
akanieleza kwamba anatuma
mtu kuja kumchukua Edger
Kaka kwani amefanya
maamuzi ya kumkabidhi kwa
magaidi.Alinielekeza
kwamba nisiwataarifu
kuhusu jambo hili.Baada ya
simu ile nilitafakari nikaona
haitakuwa sawa.Huyu mtu
amewahi kuwa kiongozi na
ana mahusiano na magaidi
yawezekana akawa ni
pandikizi na alikuwa
anatumiwa kuwapa magaidi
siri za nchi.Kuna mambo
mengi ambayo
hatuyafahamu kuhusu Edger
kaka hivyo nikaamua
kupingana na Rais na
kumchukua Edger kumleta
hapa.Naamini baada ya
kugundua kwamba
nimemtorosha Edger Rais
atakasirika sana na mpaka
sasa nimekwisha poteza kazi
yangu na tayari nimeingia
katika mgogoro mkubwa na
mkuu wa nchi lakini hilo si
tatizo kwangu kwani
nilichoamua kukifanya ni
kwa manufaa ya
taifa.Maamuzi ya Rais ni
maamuzi ya uoga na yanafaa
kupuuzwa.Ni maamuzi ya
kutatua tatizo kwa muda
mfupi bila kufahamu kama
kuna mtandao mkubwa wa
IS hapa nchini.Kuanzia sasa
mimi ni mwenzenu
tutashirikiana pamoja katika
kupambana na hawa magaidi
wanaotishia amani na
usalama wa nchi yetu”
akasema Austin
“Dah ! akasema Mathew
akiwa katika mshangao
“Nimekosa neno la
kusema kwa hiki alichotaka
kukifanya Rais.Austin una
hakika kweli ni Rais ndiye
aliyekupa maelekezo hayo na
si mtu mwingine aliyetumia
simu ya Rais?akauliza
Mathew
“Ni Rais.Nimekuwa
nazungumza na Rais mara
kwa mara na kama
angekuwa ni mtu mwingine
ametumia simu yake
ningegundua lakini
aliyenipigia simu na kunipa
maelekezo yale ni Rais Dr
Evans” akasema Austin
“Oh my God ! ni akili
yake kweli au kuna mtu
kamshauri afanye
hivi?Tumeyaweka maisha
yetu rehani kwa ajili ya
kwenda kumkomboa Edger
Kaka nchini Kenya lakini
kumbe alikuwa na mipango
yake,amenisikitisha sana
sikutegemea kabisa kama
angeweza kutufanyia kitu
kama hiki.Ahsante sana
Austin kwa hiki
ulichokifanya,usijali kuhusu
kazi hapa tunalitanguliza
taifa kwanza.Kuanzia sasa
tutambue kwamba
operesheni hii tuko peke yetu
na hatuna tena msaada wa
Rais” akasema Mathew
“Kwa namna
ninavyomfahamu Dr Evans
akigundua kwamba
tumemtorosha Edger tayari
tutakuwa maadui zake na
atatumia nguvu kubwa
kutusaka.We must prepare
ourselves for that” akasema
Devotha.
“Vipi kuhusu Ruby na
Yule mke wa balozi?
Akauliza Gosu Gosu
“We must go get
her.Ruby ni muhimu sana
katika operesheni hii.”
akasema Mathew
“So what’s the
plan?akauliza Austin
“Plan ya kwanza ni
kuwakomboa watoto
waliotekwa ambao tayari IS
ameanza kuwaua.Naamini
Rais amewaahidi kuwa
atawapa mtu wao lakini
baada ya kumkosa hali
itakuwa mbaya lazima
watawachinja watoto kwa
hasira.Tunatakiwa
tusimamishe mauaji hayo na
kuwakomboa
watoto”akasema Mathew
“How are we going to do
it?akauliza Devotha
“We have Edger
kaka.Huyu atatusaidia sana
kuweza kuufahamu mtandao
wao” akasema Mathew
“Mathew unadhani
anaweza akafunguka kwa
haraka na tukazuia mauaji
yale ya watoto
yasiendelee?Tayari wameua
mmoja na wametishia
kuendelea kuua kila baada
ya muda Fulani”akasema
Austin
“Let me try once
again.Lazima kila mbinu
itumike kuhakikisha Edger
anaongea.Guys let’s not
waste time.Gosu Gosu na
Devotha mnakwenda
kuwachukua Ruby na mke
wa balozi mimi na Austin
tutaendelea hapa” akasema
Mathew
“Mathew I don’t think
that’s a good idea.Laiti kama
ungekuwepo ingesaidia
lakini nikienda peke yangu
na Gosu Gosu anything can
happen.Ruby bado ana
hasira na mimi”akasema
Devotha
“I’ll go.Nitakwenda
badala ya Devotha” akasema
Austin na Mathew hakuwa
na kipingamizi wakaondoka
akabaki na Devotha.Mathew
akamuacha Devotha
akichunga usalama yeye
akaingia katika chumba
alimo Edger Kaka
“Edger kaka
tumelazimika kukuhamisha
na kukuleta hapa kwa
sababu maalum.Israel tayari
wamekwishafahamu
kwamba ni sisi tuliokuteka
nyara na hivi tunavyoongea
umeibuka mzozo mkubwa
sana kati yao na sisi ndiyo
maana Rais akaelekeza
tukuondoe pale haraka
sana.Wewe ni Raia wa
Tanzania na hatuwezi
kukukabidhi kwa Israel
kwani watakuua.Rais ana
mpango mzuri sana juu yako
Edger anataka kukusaidia ili
uweze kuishi maisha mazuri
yenye amani ukiwa na
mwanamke umpendaye
Olivia.Lakini ili tukusaidie
nawe pia hauna budi
kutusaidia kufahamu
mtandao wa IS hapa
Tanzania na kuwapata
Olivia pamoja na watoto
waliotekwa usiku wa
leo.Edger wasichana wale
hawana hatia yoyote na
tayari IS wamekwisha anza
kuua mtoto mmoja baada
mwingine kwa kuwakata
vichwa.Huu ni ukatili
mkubwa sana na
usiovumilika.Wasichana
wale hawafahamu chochote
na hawastahili kutendewa
ukatili wa namna
hii.Wasichana sitini na sita
wote watauawa kama
hatutafanya juhudi za
kuwakomboa” akasema
Mathew na Edger
akaendelea kumtazama bila
kusema chochote.Mathew
akasema
“Edger nataka kujua kitu
kimoja toka
kwako.Uliendesha harakati
kubwa sana hapa nchini za
kufichua ufisadi uliokuwa
unafanywa na watu mbali
mbali serikalini ukajenga
jina kubwa na wananchi
wakakuamini.Nataka
kufahamu je mambo yale
uliyokuwa unayafanya ni
kweli uliyafanya kwa
dhamira ya dhati ya
kupambana na kufichua
ufisadi au ilikuwa ni moja ya
njia zako ya kutafuta
umaarufu ili kuficha maovu
yako?
Bado Edger Kaka
alikuwa kimya
“Edger please.Muda
unakimbia nijibu swali langu
ni kweli ulikuwa na dhamira
ya dhati ya kupambana na
ufisadi au ilikuwa ni moja ya
mipango yako kujenga
taswira nzuri mbele ya jamii
ili kuficha mambo yako
unayoyafanya? akasema
Mathew na kumtazama
Edger machoni
“Don’t say it.Tayari
nimepata jibu.It was all
lies.Mapambano yale
yalikuwa ni kiini macho
kuwalaghai
wananchi,kujenga jina lako
katika jamii.Nini hasa
lilikuwa lengo lako au lengo
lenu?Naamini haukuwa peke
yako katika hili.Mlikuwa na
mipango gani?akauliza
Mathew Edger aliendelea
kuwa kimya
“Nani ni kiongozi wa
mtandao wenu hapa
Tanzania? Naamini si wewe
bali yupo mkubwa wako na
wewe ulikuwa unatumika
tu.Nani kiongozi
wako?akauliza Mathew
lakini bado Edger aliendelea
kuwa kimya akimtazama
Mathew
“Edger unaniudhi sana
ninapokuuliza unakaa
kimya.Ninao uwezo wa
kukuharibu hapa hapa lakini
ninayaheshimu maelekezo ya
Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania
ambaye ana malengo mazuri
ya kukusaidia ili
ukaishimaisha mazuri
mahala ambako hakuna
atakayekugundua.Nataka
unisaidie tuweze
kuwakomboa wale wasichana
ambao wanakatwa shingo
kikatili huku watu
wakishuhudia mtandaoni.Ni
kitendo cha kikatili sana
walichokifanya.Watoto wale
wanaouawa wana ndoto zao
ambazo wanataka kuzitimiza
katika maisha yao lakini
wanakatishwa ndoto zao
kikatili.Edger your not a
killer.You are not like
them.Macho yako
yanaonyesha haujawahi
kutoa roho ya mtu hivyo basi
waonee huruma watoto wale
wanaouawa bila kuwa na
kosa lolote.Naomba utusaidie
tuwapate wale watoto”
akasema Mathew.Edger
akainamisha kichwa
akaonekana kuzama
mawazoni
“Edger hakuna tena kitu
cha kuficha kuhusu
IS.Hawana msaada tena
kwako.Kwao umekwisha
fariki na hauna thamani tena
hivyo ni wewe na sisi
tu.Tusaidie na sisi tukusaidie
ili uishi maisha yenye raha
mustarehe mahala ambako
hakuna atakayekufahamu
ukiwa na mwanamke Yule
umpendaye” akasema
Mathew na baada ya dakika
mbili Edger akainua kichwa
akaonekana kusikitika na
kusema
“Fine,let’s end
this.Nitawaeleza kile
ninachokifahamu lakini
ninataka kuzungumza na
rais ili nipate uhakika
kutoka kwake kwamba
baada ya kuwapa kile
mnachokitaka nitapatiwa
kile ninachokitaka” akasema
Edger
“Baada ya kitisho cha
magaidi ulinzi wa Rais
umeongezeka na hivi
tunavyozungumza Rais yuko
mahala pa siri na hakuna
namna utakayoweza
kuzungumza naye kwa
sasa.Niko hapa kwa niaba
yake hivyo utazungumza na
mimi.Rais tayari amekwisha
weka wazi kuwa anataka
kukusaidia.Zungumza nami
nieleze chochote
unachokitaka na utakipata”
akasema Mathew.
“I need a new passport
with new name,I need a
house.Si nyumba tu mradi
nyumba nataka nyumba
nzuri ya ghorofa yenye hadhi
huko Uswisi.I need two
cars,luxury ones.Nahitaji
mtaji mkubwa
utakaoniwezesha kuwekeza
katika kilimo,mwisho
namuhitaji
Olivia.Mkinihakishia
kwamba nitapata hivyo vyote
niko tayari kuwasaidia
kuwapa taarifa”akasema
Edger
“Edger,Rais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania
yuko tayari kufanya chochote
kile utakachokihitaji ili
uweze kutupa taarifa
muhimu.Hesabu kwamba
haya yote umeyapata”
akasema Mathew
“Not so simple
Mr…what’s your name
again?akauliza Edger
“Mathew ..Mathew
Mulumbi”
“Mr Mathew Mulumbi
mambo hayaendi kirahisi
namna hiyo.Nahitaji uhakika
kutoka kwa Rais pekee na si
mtu mwingine” akasema
Edger
“Kama nilivyokwambia
kwamba Rais haitawezekana
kuzungumza naye kwa sasa
kutokana na kupelekwa
sehemu salama kufuatia
vitisho vya mashambulio ya
kigaidi na badala yake nipo
mimi.Usihofu mambo yako
yote yatatekelezwa.Lakini
wakati hayo yakitekelezwa
kwa nini tusianze kwanza
kumtafuta Olivia? Kila
unachokitaka kitapatikana
lakini kitakosekana kimoja
tu,Olivia Themba.Nipe
taarifa ambazo zitatusaidia
kumuokoa
Olivia.Ninakuhakikishia kila
kile unachokihitaji
kitapatikana.I give you my
word” akasema Mathew
“Mathew wewe
mwenyewe unafahamu
namna mambo haya
yanavyokwenda ninahitaji
uhakika kwamba kweli yale
ninayoyataka yanakwenda
kutekelezwa.Convince me!
Akasema Edger
Kaka.Mathew akamtazama
usoni kwa makini halafu
akasema
“Unataka kutumia jina
gani jipya?
Edger akafikiri kidogo na
kusema
“Nickson Robert”
“Sawa nisubiri
nitarejea”akasema Mathew
na kutoka
“Bastard ! akasema
Mathew kwa ukali.
“Nini
kimetokea?akauliza Devotha
“Edger yuko tayari
kufunguka lakini kuna
masharti ametoa” akasema
Mathew
“Ametoa sharti gani?
“Anataka nyumba ya
kifahari Uswisi,anataka
magari mawili ya kifahari
anataka mtaji wa kuwekeza
katika kilimo na anataka
hati mpya ya kusafiria yenye
jina jipya na mwisho kabisa
anataka kuondoka na Olivia
Themba.Tukimtekelezea
hayo yote yuko tayari kutupa
maelezo ya kutusaidia
kuwakomboa watoto pamoja
na Olivia”
“Vitu alivyovitaka ni
vikubwa mno viko nje ya
uwezo wetu.Tutafanya nini
kuvipata na mahusiano yetu
na Rais yamevunjika?Kama
bado tungekuwa na
mahusiano naye,Rais anao
uwezo wa kutekeleza hayo
yote”akasema Devotha
“Forget about
president.We’ll move on
without him.Edger anahitaji
kitu cha kumridhisha
kwamba maombi yake
yanafanyiwa kazi”
“What are we going to do
Mathew?
“I need to call my wife in
Paris”
“Your wife? Akauliza
Devotha
“Ndiyo”
“Mkeo anaingiaje katika
sakata hili?
“Ni bilionea
mkubwa.Anafahamiana na
matajiri wakubwa sehemu
mbali mbali duniani,nataka
anisaidie kupata nyumba ya
kununua nchini Uswisi
ambayo itanunuliwa kwa
jina la Nickson Robert
ambalo amechagua Edger”
“Mathew kwa nini
unataka kuingia hasara?
“I don’t care
ninachohitaji ni kupata
taarifa za kutuwezesha
kuwakomboa Olivia,Coletha
na watoto
waliotekwa.Tuwasubiri
akina Gosu Gosu warejee na
vifaa ili niweze kupiga simu
kwa mke wangu.Tukinunua
nyumba hiyo ataridhika na
atatueleza kila kitu”
akasema Mathew
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 12
Waziri mkuu wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania
aliendelea kuongoza
maandamano ya wananchi
kuelekea ikulu kumshinikiza
Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania
kutumia nguvu kuwakomboa
watoto waliotekwa nyara
ambao walianza kuuawa na
magaidi.
Akiwa ofisini kwake Dr
Evans alipewa taarifa ya
waziri mkuu kuungana na
wananchi katika
maandamano ya kuelekea
ikulu kushinikiza
kuwakomboa watoto
waliotekwa.Zilikuwa ni
taarifa zilizomstua sana Dr
Evans.
“Traitor ! akasema kwa
ukali huku akitazama
maandamano yale
yaliyokuwa yanarushwa
mubashara runingani
“Nilifanya kosa kubwa
sana kumuamini waziri
mkuu na kumpa siri za kile
kinachoendelea.Bahati nzuri
sikumpa siri zote hasa
kuhusiana na ile idara ya siri
wala kutekwa kwa akina
Olivia.Sikujua kama
angeweza kunigeuka namna
hii na sasa ameamua
kulifanya jambo hili kama
mtaji wake wa kisiasa.Kwa
nini nikakubali kumsikiliza
na kufuata ushauri wake? Ni
kwa sababu yake
nimewapoteza akina Mathew
hadi Austin January ambaye
siku zote amekuwa mtiifu
mno kwangu.Wote
wameniona mimi ni mpuuzi
kwa sababu waliyaweka
rehani maisha yao kwa ajili
ya kwenda kumkomboa
Edger Kaka na kumleta
nyumbani lakini mimi
nimetaka kuwageuka na
kumkabidhi kwa
magaidi.Nimerud…………….
” akastuka baada ya simu
yake kuita akahisi mikono
inamtetemeka akaitazama
simu ile ikiita akaogopa
kuipokea.Simu ikakatika na
kuanza kuita tena akaamua
kuipokea
“Hallo” akasema
“Mheshimiwa Rais nusu
saa tuliyokuongezea
imemalizika nataka
kufahamu kama tayari
unaye Edger Kaka” ikasema
sauti ya upande wa pili
“Kitendo mlichokifanya
cha kumuua mmoja wa
wanafunzi mliowateka
kimeleta matatizo makubwa
sana.Maandamano makubwa
yanafanyika hivi sasa watu
wanaandamana kuja ikulu
na hadi viongozi wa serikali
wamejiunga na maandamano
hayo
makubwa.Mmesababisha
mtikisiko mkubwa sana
k……” Dr Evans
akakatishwa
“Mheshimiwa Rais yote
haya umeyataka wewe
mwenyewe kama ungetupa
kile tunachokihitaji kwa
amani tusingefika hapa
tulipofika.Sasa nataka
kufahamu tayari umekwisha
muandaa Edger Kaka?
“Kumuandaa Edger Kaka
si kitu chepesi inahitaji
taratibu zifanyike kumtoa
mahala alipo.Nimewatuma
wasaidizi wangu huko na
wanaendelea
kulishughulikia.Tafadhali
nahitaji muda zaidi niweze
kuwakamilisha kile
mnachokitaka”
“Mheshimiwa Rais bado
unaonekana hujali na una
moyo mgumu kama
Farao.Kutokana na
kuendelea kutudharau
hakutakuwa na majadiliano
tena na kila baada ya nusu
saa tutaua watoto wawili
hadi pale utakapokuwa
umekamilisha hitaji
letu.Itakapofika saa nane na
haujatupatia mzigo wetu
tutaongeza idadi ya watoto
na kuwa watano ambao
watachinjwa kila baada ya
nusu saa.Ikifika saa kumi na
mbili za jioni bado
hujatupatia mzigo wetu
tutaongeza tena idadi
tunataka hadi itakapofika
saa sita za usiku wa leo tuwe
tumewamaliza wasichana
wote.Nitawasiliana nawe
tena baada ya nusu saa”
“Tafadhali msiue tena
watoto nitawapatia kile
mn……….”akasema Dr
Evans lakini tayari simu
ilikwisha katwa.
“Sijawahi kukutana na
mtihani mkubwa kama huu
katika maisha yangu.Hawa
makatili wanakwenda
kumuua mtoto mwingine”
akawaza na kuchukua simu
akampigia mkuu wa jeshi la
polisi akazungumza naye
lakini hakukuwa na taarifa
zozote zenye kuleta
matumaini ya kuwapata
watekaji.Dr Evans akazidi
kuchanganyikiwa.
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 13
Austin na Gosu Gosu
walirejea wakiwa na Ruby na
mke wa balozi ambaye
alikuwa amefungwa
kitambaa usoni wakaingizwa
ndani.
“Samahani sana Ruby
kwa usumbufu huu”
akasema Mathew huu
akimsaidia Ruby kuketi
sofani
“It’s okay Mathew.What’s
going on? Wametuchukua
bila kutueleza nini
kinaen…..” akasema Ruby
mara akatokea Devotha wote
wakabaki kimya
wakitazamana kwa jicho la
chuki.
“Look ladies” akasema
Mathew na kuwatazama kwa
zamu
“Najua nyote
hamtazamani usoni
kutokana na kile kilichotokea
lakini kwa wakati huu tuko
katika dharura kubwa sana
tunahitaji ushirikiano
mkubwa ili kuweza
kufanikisha misheni yetu
hivyo basi ninawaomba ninyi
wawili ambao wote ni
muhimu sana katika misheni
hii muweke kando tofauti
zenu na mfanye kazi kwa
pamoja.I know it’s hard but
do it for the country.Do it for
the girls we’re trying to
rescue.Are we clear ?!
akauliza Mathew
“Yes we’re clear ! akajibu
Devotha Ruby akabaki kimya
“Ruby are we clear ?!
akauliza Mathew
“Yes we’re clear” akajibu
Ruby
“Good.Kwa ufupi sana
Ruby nataka nikupe taarifa
ya kile kilichotokea.Ni
kwamba Rais ametugeuka na
amekusudia kumkabidhi
Edger Kaka kwa magaidi
kwa lengo la kuwakomboa
mateka
wanaowashikilia.Hiyo ndiyo
sababu tuko hapa.Hatuko
tayari Edger Kaka
akabidhiwe kwa magaidi”
akasema Mathew
“Is he crazy? How could
he do that? Akauliza
Ruby.Austin na Gosu Gosu
nao wakaingia pale sebuleni.
“Ahsanteni sana Austin
na Gosu Gosu kwa
kufanikiwa kuwaleta Ruby
na mke wa balozi.Naamini
mmechukua kila kifaa
muhimu tunachokihitaji”
akasema Mathew
“Tumekuja na kila kitu
muhimu” akasema Ruby
na kuomba apewe
kompyuta yake.
“Nilifanya mahojiano
tena na Edger Kaka na safari
hii amekubali kutoa
ushirikiano lakini ametoa
masharti ambayo ni
kupatiwa hati mpya ya
kusafiria,kutafutiwa nyumba
Uswisi,Kutafutiwa gari la
kifahari na mtaji wa
kuwekeza katika
kilimo.Kama mnavyoona
mambo haya anayoyataka
Edger ni makubwa sana na
yanahitaji fedha
nyingi.Kama tungeendelea
kuwa na ukaribu na Rais
ingekuwa rahisi kwetu
kuweza kuyatimiza hayo
lakini kwa sasa hii ni
misheni yetu wenyewe bila
kumshirikisha Rais hivyo
inatulazimu kutafuta namna
ya kumfanya Edger aweze
kufunguka.Nimefikiria
kufanya jambo
hili.Nitampigia simu mke
wangu aliyeko Paris
Ufaransa.Ni bilionea na
anafahamiana na wafanya
biashara wengi wakubwa
duniani kote.Nataka anunue
nyumba nchini Uswisi kwa
jina la Nickson Robert
ambalo amelichagua Edger
ili kumpa moyo kwamba
maombi yake yanafanyiwa
kazi.Ni gharama kubwa sana
lakini hakuna namna we
have to do everything we can
to save the girls” akasema
Mathew
“Kwa upande wangu sina
tatizo na hilo kwani
tunachohitaji ni taarifa
zitakazotusaidia kufahamu
mahala wasichana walipo na
kuufahamu mtandao wa IS
hapa nchini” akasema Gosu
Gosu.
“Kuna yeyote mwenye
wazo mbadala?akauliza
Mathew na wote wakabaki
kimya
“Inaonekana wote
tumekubaliana na hiki
ninachotaka kukifanya.Ruby
nahitaji kompyuta yako
nizugumze na mke wangu”
akasema Mathew na
kuchukua kompyuta ya Ruby
akaingia mtandaoni na
kumtafuta mke wake
akampigia simu ikapokelewa
“Hello sweetheart I had a
very bad dream about
you.Are you okay my
love?akauliza Peniela mke
wa Mathew
“C’mon my Peny I’m
more than fine.watoto
wanaendeleaje?Miss you
guys so much” akasema
Mathew
“We miss you too
darling.When are you coming
home?akauliza
“Soon.Very soon” akajibu
Mathew
“Ouh Mathew It’s hard
without you.I love you more
than I can say.Please come
very soon.Missed your
kisses,the way you hold me
in your strong arms,they way
you take me to the moon,the
way you…ouh gosh !
akasema Peniela na
kunyamaza
“Just say it” akasema
Mathew huku akitabasamu
“Forget it.How you doing
out there?akauliza Peniela
na Mathew akageuza shingo
kamtazama Ruby
“Uko na
nani?Unaangalia nini huko
pembeni? Akauliza Peniela
“Niko mwenyewe usihofu
darling”
“Mathew please don’t you
ever try cheat on
me.Nikigundua uko na
mwanamke mwingine huko
Tanzania I swear I’ll kill
myself.Mathew you are mine
and mine alone”
“Usihofu darling you
know me I can’t do that.You
are my one and only angel”
akasema Mathew na uso wa
Peniela ukatakata kwa
tabasamu kubwa
“Darling nimekupigia
ninahitaji unisaidie kitu
kimoja”
“Unataka nini Mathew?
“Nataka kununua
nyumba Uswisi.It’s very
urgent”
“Uswisi?! Peniela
akashangaa
“Ndiyo.Nataka nyumba
Uswisi.A luxury one”
“Luxury house?What
for?akauliza Peniela
“I’ll explain later darling
just find me a
house.Nitafutie nyumba tatu
nzuri za kifahari zinazouzwa
unitumie nichague moja
itakayonifaa” akasema
Mathew
“Mathew what’s going
on? Are you buying this for
someone?A woman?
“C’mon Peniela just do as
I say.I’ll explain to you later”
akasema Mathew
“Sawa Mathew.Let me
make some calls.Nitakupigia
baada ya muda mfupi”
akasema Peniela na kukata
simu
“Ruby kwa nini usiende
kupumzika pale
tutakapokuhitaji
tutakujulisha.Let me take
you to the room” akasema
Mathew na kumshika mkono
Ruby wakaelekea chumbani
“She don’t know what
you are doing out here”
akasema Ruby wakati
wanaelekea chumbani
“Tayari ameukana uraia
wa Tanzania na kuchukua
uraia wa nchi nyingine kitu
ambacho mimi siwezi
kukifanya ndiyo maana
muda mwingi ninakuwa
hapa Tanzania.I was born
here and I will die here.I love
this beautiful country.I’m a
man and I have needs and
she knows that.Do you
understand me?akauliza
Mathew
“I understand you
Mathew but you must be
very carefull.Akifahamu…...”
“I’m not a saint.I need
love,Ineed someone when
she’s not here but she’s still
my wife and I love her so
much”
“I’m here Mathew to give
you love,to take her place
when she’s not around.Niko
tayari kuishi Tanzania au
sehemu yoyote ile ulipo”
akasema Ruby
“Thank you
Ruby.Pumzika kwa sasa”
akasema Mathew na
kumbusu Ruby shavuni
akatoka akarejea sebuleni.
“What happened out
there?akauliza Mathew
“Haikuwa rahisi
kuwachukua lakini
imetulazimu kutumia
nguvu”akasema Austin
“You didn’t kill those
guys,right?akauliza Mathew
“No we didn’t”
“Mathew kuna kitu
kinaendelea huko nje
ambacho si cha kawaida”
akasema Gosu Gosu
“Nini
kinaendelea?akauliza
Mathew
“Kuna maandamano
makubwa ya wananchi
yanafanyika kuelekea ikulu
kumshinikiza Rais atumie
nguvu katika kupambana na
magaidi ili kuwakomboa
watoto waliotekwa
wasiendelee kuuawa”
akasema Gosu Gosu
“Wanaelekea
ikulu?Mathew akashangaa
“Ni maandamano
makubwa sana ya watu
barabara nyingi zimefungwa
na kikubwa zaidi waziri
mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania
ndiye anayeongoza
maandamano hayo”
“Waziri mkuu?!
“Ndiyo.Ni tukio la
kushangaza sana.Inadaiwa
kwamba mwanae ni mmoja
wa mabinti waliotekwa na
magaidi ndiyo maana
ameamua kuungana na
wananchi kuandamana
kuelekea ikulu kuishinikiza
serikali kutumia nguvu
kubwa kuwakomboa watoto”
akasema Gosu Gosu
“It doesn’t make sense to
me.Waziri mkuu ni mtu
mkubwa serikalini na hata
kama mwanae ametekwa
nyara alipaswa kushirikiana
na viongozi wenzake
serikalin….” Mathew
akakatisha mazungumzo
baada ya simu katika
kompyuta kuita
“It’s her.Peniela”
akasema na kuipokea
“Mathew nimefanya
mawasiliano ya haraka kuna
nyumba tatu nimepata
ambazo ninakutumia picha
na maelezo yake sasa hivi ili
uchague ipi unaitaka”
“Thank you
Peny.Nitumie sasa hivi”
akasema Mathew na simu
ikakatwa
“Tayari amepata
nyumba” akasema huku
akifungua akaunti yake ya
barua pepe akakuta picha za
nyumba ambazo ametumiwa
na Peniela.
“Twendeni kwa Edger
akachague nyumba ipi
anaitaka” akasema Mathew
na kuchukua kompyuta ile
wakaenda katika chumba
alimo Edger Kaka.
“Hallow Edger I’m
back.Nataka kukuthibitishia
kwamba tunaamisha kile
tunachokisema.Nimekuletea
nyumba tatu uchague moja
utakayoipenda” akasema
Mathew na kumsogezea
Edger kompyuta akaanza
kumuonyesha zile
nyumba.Zilikuwa ni nyumba
za kifahari haswa.
“Is this real or is your
game ?akauliza Edger
“Edger hatufanyi mchezo
hapa.Kila kitu ni
halisi.Chagua nyumba
unayoipenda na itanunuliwa
hapa hapa
ukishuhudia.Chagua
nyumba” akasema Mathew
na Edger akachagua nyumba
anayoitaka.Mathew
akampigia simu Peniela na
kumpa maelekezo ya
kuinunua nyumba ile.Baada
ya dakika kumi Peniela
akampigia simu na
kumjulisha kwamba tayari
malipo yamekwisha fanyika
na nyumba ile imekwisha
nunuliwa.Mathew akapiga
simu katika kampuni ile
ambayo waliuza nyumba na
kuthibitishiwa kwamba
nyumba ile imenunuliwa na
Nickson Robert
mfanyabiashara kutoka
Tanzania.
“Done.Umehakikisha
wewe mwenyewe.Mambo
yameanza kushughulikiwa
nyumba tayari umepata
mengine yanafuata.It’s your
turn.Give me information”
akasema Mathew na Edger
akatazama chini halafu
akainua kichwa na kusema
“I don’t know his name”
“You don’t know what?
Akauliza Gosu Gosu kwa
ukali huku akimsogelea
Edger
“Gosu Gosu please”
akasema Mathew
“Nimesema sifahamu
jina lake.Ni mtu mmoja ana
asili ya kiarabu lakini
anazungumza Kiswahili safi
na anaishi hapa Dar es
salaam ila sifahamu wapi”
“C’mon Edger we’re using
billions of money that’s not
the information I want!
Akafoka Mathew
“I real don’t know his
name lakini huyo ndiye
ambaye hunipa maelekezo na
taarifa mbali mbali.Ufisadi
wote niliokuwa naufichua
taarifa na nyaraka zote
nilipata kutoka kwa huyo
jamaa ambaye sikupaswa
kumuuliza jina lake wala
kufahamu taarifa zake”
“Mlikuwa
mnawasilianaje? Akauliza
Austin
“Nilikuwa napokea
ujumbe katika simu yangu
unaosema LUNCH.Kila
nilipopokea ujumbe ule
nilijua maana yake na
nilikwenda Masjid Hidaya
kuonana na huyo jamaa
ambaye husali hapo kila
siku.Baada ya swala hunipa
kama ana ujumbe wowote”
akasema Edger
“Unaweza ukazikumbuka
namba zake za simu
alizokuwa anazitumia
kuwasiliana nawe?Mathew
akauliza
“Hapana sizikumbuki”
akasema Edger
“Remember the number
dammit ! akafoka Gosu Gosu
na kurusha kofi zito Mathew
akamdaka mkono
“Easy gentlemen”
akasema Mathew na kutuliza
jazba iliyoanza kupanda mle
ndani
“Edger I’m going to ask
you one more question”
akasema Mathew na
kunyamaza kidogo
“Huyu mtu ambaye
humfahamu jina lake
unaweza ukanieleza
muonekano wake?akauliza
Mathew
“Ndiyo” akajibu Edger na
Mathew akaomba aletewe
kalamu ya risasi na
karatasi.Edger akaanza
kumuelezea mwonekano wa
Yule jamaa huku Mathew
akifuata maelezo yale
kuchora picha.Alipomaliza
kuchora akamuonyesha
Edger
“Wow ! This is
amazing.Haya ni
maajabu.Nilikuwa nasikia
kwamba wapo watu wana
uwezo wa kumchora mtu
kwa kufuata maelezo
nilidhani ni uongo kumbe ni
kitu cha kweli kabisa.Huyo
mtu yuko hivyo hivyo
ulivyomchora” akasema
Edger
“Thank you Edger
pumzika tutakuja
kuzungumza tena baadae”
akasema Mathew wakatoka
mle ndani
“Mathew huyu jamaa
anacheza na akili
zetu.Nyumba ile ina thamani
zaidi ya milioni mia moja na
hailingani kabisa na taarifa
hii aliyotupa !! akasema Gosu
Gosu
“Gosu Gosu asili yako
wewe ni mpiganaji hivyo
unapaswa kujifunza mambo
haya ya kipelelezi.Katika
kazi hii taarifa ndogo sana
inaweza ikanunuliwa kwa
gharama kubwa na ikawa na
msaada mkubwa mno ndiyo
maana hainiumizi kutumia
kiasi kikubwa cha pesa kwa
taarifa ile aliyotupa
Edger.Kwa sasa tunatakiwa
kwanza kumfahamu mtu
huyu ni nani.Muite Ruby”
akasema Mathew na Ruby
akaitwa
“Ruby tunataka
kumfahamu mtu huyu ni
nani.Huyu ndiye ambaye
alikuwa anawasiliana na
Edger Kaka” akasema
Mathew na kumpatia Ruby
ile karatasi.Ruby akaichukua
ile picha akaiingiza katika
kompyuta yake na kuanza
kumtafuta mtu Yule ni
nani.Picha zilipita haraka
haraka katika kompyuta na
mara program ikasimama.
“Hakuna picha
inayofanana na hii” akasema
Ruby.
“That can’t be.Search
again” akasema Mathew na
kuchukua ile picha akaenda
kwa Edger
“Edger huu si mchezo wa
kuigiza.Nataka uniambie
picha hii inafanana kweli na
mtu ambaye ulikuwa
unawasiliana naye?
“Ndiyo.Ni yeye
mwenyewe”
“Tumejaribu kumtafuta
hakuna picha inayofanana
na hii”
“Mathew nilichokwambia
ni kitu cha kweli kabisa.Find
that man.” akasema Edger
Mathew akatoka na
kuwafuata wenzake
“Mmepata chochote?
“Hakuna picha
inayofanana na hiyo”
akasema Ruby
“Keep on searching.Mimi
na Austin tunakwenda
Masjid Hidaya ambako
Edger anadai ndiko
amekuwa akikutana na huyo
jamaa.Gosu Gosu na Devotha
mtabaki hapa mkilinda
usalama.Tunaye mtu
muhimu mno hapa ndani
hivyo unahitajika ulinzi wa
kutosha” akasema Mathew
na kumuita pembeni Gosu
Gosu
“I don’t trust Devotha
keep an eye on her.Usimpe
nafasi asije akafanya kama
alivyomfanyia Ruby”
akasema Mathew
hawakupoteza muda
wakaingia garini na
kuondoka.
“Mathew inawezekanaje
Edger asilifahamu jina la
mtu ambaye wamekuwa
wakiwasiliana naye? Una
hakika anasema kweli?
Akauliza Austin
“I believe him.Edger
alikuwa anatumika kwa ajili
ya misheni maalum ndiyo
maana hawakutaka afahamu
jina la Yule aliyekuwa
anawasiliana
naye.Tutamfahamu tu
usijali” akasema Mathew.
Kulikuwa na heka heka
nyingi mitaani.Barabara
zilijaa magari kufuatia
baadhi ya barabara
kufungwa kutokana na
maandamano ya wananchi
kushinikiza serikali
iwakomboe wasichana
waliotekwa
“Kuna kitu mliniambia
kilinishangaza kidogo.Waziri
mkuu kuamua kuungana na
wananchi kuandamana hiki
ni kitu cha ajabu sijawahi
kukishuhudia.Waziri mkuu
ni mtu mkubwa hata kama
mwanae ni mmoja wa
waliotekwa hauapswa
kufanya alivyofanya
alipaswa kushirikiana na
viongozi wenzake serikalini
kuhakikisha watoto
wanapatikana” akasema
Mathew
“Ni kweli inashangaza
sana” akajibu Austin ambaye
tayari alikwisha vua sare za
kijeshi na kuvaa mavazi ya
kawaida
Austin na Mathew
walifika Mikunguzi na
kuitafuta Masjid
Hidaya.Ulikuwa ni msikiti
mzuri sana na magari
kadhaa yaliegeshwa nje.Pale
nje walinunua kofia na
kuvaa
“Sijawahi kuingia
msikitini” akasema Austin
“Nimeishi nchi za
kiarabu nifuate ninavyofanya
tukifanikiwa kuingia ndani
tujitahidi kuangaza kila kona
kumtafuta huyu jamaa”
akasema Mathew na
kuelekea sehemu ya kufanya
maandalizi kabla ya kuingia
katika swala.Austin
akamfuatisha Mathew
anavyofanya kisha
wakaingia ndani ambako
tayari swala ilikuwa
inaendelea.Macho ya
Mathew na Austin
hayakutulia sehemu moja
yalizunguka kama kinyonga
kumtafuta Yule jamaa bila
mafanikio.Wengi wa
waliokuwamo ndani ya
msikiti walikuwa ni watu
wenye asili ya arabuni
Swala ilimalizika na
watu wakaanza
kutoka.Mathew ambaye
alikaa karibu na mlango
alizungusha macho kuangaza
lakini hakumuona mtu Yule
na mwisho Austin naye
akatoka
“Nothing.Hayupo huyu
mtu.Sina hakika kama Edger
ametuambia kitu cha kweli”
akasema Austin
“Wait for me here”
akasema Mathew na
kumfuata Imamu wa msikiti
“As salamu alaykum”
Mathew akamsalimu
“Wa Alaikum Salaam”
akajibu Imam
“U mgeni hapa,umetokea
wapi?akauliza Imamu
“Ni kweli mimi ni mgeni
nina shida nawe Imamu”
akasema Mathew na Imamu
akamchukua hadi pembeni
kidogo ya msikiti
“Nikusaidie nini ndugu
yangu?akauliza Imamu Yule
mwenye ndevu
nyingi.Mathew akatoa
karatasi mfukoni na
kuikunjua
“Unamfahamu huyu
mtu?Umewahi kumuona
hapa msikitini?
Imamu Yule akaitazama
picha ile na kusema
“Hapana simfahamu”
“Imamu tazama vizuri
hiyo picha.Mtu huyu husali
hapa masjid Hidaya
unamfahamu?
“Hapana
simfahamu.Ninashindwa
kumtambua katika picha ya
kuchora.Huna picha yake
halisi?
“Imamu jaribu kutazama
vizuri hii picha unaweza
kuwa unamfahamu mtu
huyu” akasema Mathew na
Yule imamu akaitazama
picha kwa mara nyingine
“Sina kumbu kumbu
kama nimewahi kumuona
mtu mwenye sura hii hapa
katika mskikiti
huu.Tunaosali hapa si watu
wengi na tunafahamiana
ndiyo maana ilikuwa rahisi
mimi kukutambua wewe
kuwa ni mgeni hapa”
akasema Imamu na
kumtazama Mathew kish
akauliza
“Wewe ni askari?
“Hapana mimi si askari”
“Kwa nini basi
unamtafuta huyu mtu kama
si askari?
“Huyu ni mtu muhimu
kwangu.Nisaidie tafadhali
kujua mahala alipo” akasema
Mathew lakini Yule imamu
akamrejeshea picha yake
“Picha yako hii huyu mtu
simfahamu na
sijawahikumuona
hapa.Jaribu labda misikiti
mingine” akasema Imamu na
kuanza kuondoka Mathew
akamfuata
“Mzee naomba
unisikilize.Mimi natoka
katika idara ya kupambana
na ugaidi”akasema Mathew
na imamu yule akastuka
“Nilihisi kitu kama
hicho.Kwa nini kila
mnapofanya misako yenu ya
kuwatafuta magaidi huwa
mnakimbilia katika nyumba
zetu za ibada kana kwamba
sisi ndio huwaficha watu
hao?akauliza Imamu
akionekana kukereka
Mathew hakumjali
“Huyu mtu ambaye
ninataka unisaidie
kumtambua ana mahusiano
na kikundi cha magaidi
ambao wamefanya shambulio
la bomu katika hospitali ya
Mtodora na kuua watu wasio
na hatia na kama haitoshi
wamewateka tena wanafunzi
na wameanza kuwaua
kikatili kwa kuwachinja
kama kuku”
“Kwa kweli kitendo kile
nimekiona na kimeniumiza
sana.Hata sisi mchana huu
tumefanya dua maalum ili
watu hao wanyama waweze
kupatikana” akasema Imamu
“Huyu tunayemtafuta
ana mahusiano na watu
hao.Tafadhali tusaidie
tuweze kumtambua”
akasema Mathew na Imamu
Yule akaiomba tena ile picha
akaitazama vizuri.
“Imamu huyu mtu
amekuwa akisali katika
msikiti huu na kama
ulivyosema kwamba watu
wote wanaosali katika huu
msikiti mnafahamiana
lazima utakuwa
unamfahamu.Huyu ni mtu
hatari sana na kama
hautatusaidia kumfahamau
utatufanya tuamini kwamba
mnawahifadhi magaidi
katika msikiti huu..”
“Hapo unakosea ndugu
yangu.Uislamu ni dini safi
na isihusishwe na
ugaidi.Kamwe uislamu
haujawahi kushabikia
ugaidi.Hii ni dini inayohubiri
amani ndiyo maana salamu
yetu inasema As salamu
alaykum maana yake amani
iwe kwako.Muislamu yeyote
analazimika kusambaza na
kutangaza amani kwa
muislamu mwenzake na
asiye muislamu hivyo basi
itendo chochote cha
kumnyima mtu yeyote amani
hakikubaliki ndani ya
uislamu.Magaidi ni watu
wanaotumia nguvu
kulazimisha matakwa yao
yafanikiwe aidha kiimani au
kisiasa.Mwenyezi Mungu
Subhaanahuu wataala
kupitia Quran tukufu Surah
An-Nisa 4 aya ya 93
anakemea mauaji
“walakun klu min yaqtul
mwmnaan ean eamad –
falmukafa’at hi
aljahim,hayth
Yuthbit ‘iilaa al’abad,waqad
ghadib allah ealayh
washatamah wa’aeada lah
eqabaan
Kbyraan…..Tafsiri ya
Kiswahili inasema “Lakini
yeyote anayemuua mwamini
kwa makusudi malipo yake
ni Jahannamu ambako
atakaa milele na Mwenyezi
Mungu amekasirika naye na
amemlaani na
amemtayarishia adhabu
kubwa” akasema Imamu na
kumtazama Mathew
Aya hiyo na nyingine
kadhaa zinatufundisha
ubaya wa kuua nafsi iso na
hatia na hata kujiua
mwenyewe.Kuna somo refu
hapa ambalo linafundisha
namna uislamu
usivyofungamana na ugaidi
lakini muda wangu
hauruhusu ila nimekupa
hayo machache
kukuthibitishia kwamba
uislamu haukumbatii
ugaidi.Katika matendo hayo
ya kigaidi wanaoathirika pia
wamo waislamu.Katika
wasichana waliotekwa wamo
pia waislamu hivyo basi
itoshe tu kusema kwamba
Uislamu si dini ya kigaidi
kama inavyoendelea
kujengeka kwa wengi”
“Nimekuelewa Imam
hata mimi nimewahi kuishi
katika nchi za kiarabu
ninaifahamu dini ya kiislamu
vizuri na hata kiarabu
ninakizungumza
vyema.Turejee katika suala
letu.Huyu mtu ni muhimu
sana naomba tafadhali
unisaidie kupata taarifa
zake” akasema Mathew.
“Nasema ukweli na
Mwenyezi Mungu
Subhaanahuu wataala
ananisikia,huyu mtu mimi
simfahamu kwa sababu nina
miezi minne tu toka
nimehamia katika msikiti
huu.Yupo imamu wa zamani
kwa sasa anasumbuliwana
maradhi labda tukifanikiwa
kumpata huyo anaweza
akawa anamfahamu”
“Unafahamu mahala
anapoishi huyo imamu wa
zamani?akauliza Mathew
“Ndiyo ninapafahamu.Si
mbali sana na hapa”
akasema Imamu na bila
kupoteza muda wakaingia
katika gari na kuondoka
kuelekea kwa imamu wa
zamani wa Masjid Hidaya.
“Nimestuka sana kusikia
kwamba katika msikiti
wangu anasali mtu ambaye
anajihusiana na vitendo vya
kigaidi.Mambo haya
tumekuwa tunayapinga kwa
nguvu kubwa”akasema
Imamu
“Magaidi hawana alama
ni watu tunaoishi nao katika
jamii na kushiriki nao
mambo mbalimabli hata
ibada”akasema Austin
Walifika katika nyumba
ya imamu wa zamani
ambaye alikuwa
anasumbuliwa na ugonjwa
wa kuvimba
miguu,wakamkuta amekaa
nje akipunga upepo
wakamsalimu na bila
kupoteza muda wakamueleza
kile kilichowapeleka
pale.Imamu Sadiq
akaitazama ile picha kwa
makini sana na kusema
“Ni kweli huyu mtu
alikuwa anasali katika
msikiti wetu na alipenda
sana kuhudhuria Swalat
Dhuhri.Hakuwa mtu wa
kuchangama sana na
wenzake aliondoka baada ya
swala kumalizika.Mara
chache alikuja kunisalimu na
alikuwa mchangiaji mzuri
sana kila pale kulipohitajika
michango
mbalimbali.Nimestuka
kusikia kwamba
anahusishwa na matendo ya
kigaidi yanayoendelea
kutokea hapa nchini”
akasema Imamu Sadiq
“Mzee tunahitaji
utusaidie namna ya kumpata
huyu mtu.Unafahamu
mahala anapoishi?akauliza
Mathew
“Huyu mtu simfahamu
vyema zaidi ya kumuona
msikitini,sifahamu anaishi
wapi wala kazi
yake..”akasema Imam Sadiq
na kunyamaza
“Lakini kuna kitu
nimekikumbuka.Kuna
wakati aliwahi kumtuma
mwanamama mmoja anaitwa
Zulfa aniletee mchango wake
wa ujenzi wa choo cha
madrasa.Naamini huyo Zulfa
anaweza akawa
anamfahamu vyema huyu
jamaa” akasema Imam
Sadiq.
“Zulfa yupi
mzee?akauliza Imam Shafii.
“Zulfa mtoto wa Ustaadh
Shabani ana duka lake la
kuuza vitambaa mtaa wa
Mkongoro” akasema Imam
Sadiq na kuwaelekeza akina
Mathew lilipo duka la Zulfa
wakamuaga mzee Yule na
Mathew akamuachia shilingi
lakini tatu kwa ajili ya
kumsaidia katika matibabu
wakaondoka.
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 14
“Mathew alikuita nje
akaenda kukueleza
nini?Devotha akamuuliza
Gosu Gosu wakiwa sebuleni
wakipumzika baada ya akina
Mathew kuondoka
“Kwa nini unataka
kujua?akauliza Gosu Gosu
“Alikwambia
unichunge.Bado haniamini
hata kidogo” akasema
Devotha huku akitabasamu
“Hapana hakusema hivyo
kuna maelekezo mengine
alinipa”
“Gosu Gosu yawezekana
bado hunifahamu
vyema.Mimi ninao uwezo
mkubwa sana wa kusikia
kuliko kawaida.Ninao uwezo
wa kusikia hata sisimizi
akipita mbele yangu”
“That’s impossible !
akasema Gosu Gosu
“It’s true.Huifahamu
historia yangu ndiyo maana
unadhani haiwezekani.Kwa
ufupi tu ni kwamba niliwahi
kulipukiwa na bomu nikiwa
bado msichana mdogo
nikapelekwa Marekani kwa
matibabu nimefanyiwa
operesheni nyingi
kuutengeneza mwili wangu
huu unaoniona leo na katika
operesheni hizo ndipo
nilipooongezewa uwezo wa
kusikia.Sifahamu
walifanyaje lakini uwezo
wangu ni mkubwa mno na
niliwasikia mkinong’onezana
na Mathew akikutaka
unichunge nisije nikageuka
na kufanya kama
nilivyofanya kwa Ruby”
akasema Devotha na Gosu
Gosu akabaki kimya
“Nakubali nilifanya kosa
na inaniumiza mno.Nilikuwa
katika harakati za kuutafuta
ukweli huu ambao
tunautafuta sasa.Naomba
mniamini mimi si msaliti na
siwezi tena kufanya hivyo”
akasema Devotha
“I trust you Devotha”
“Kitu gani kinakufanya
uniamini?
“Macho yako yananifanya
nikuamini” akasema Gosu
Gosu na Devotha akatoa
kicheko.
“Nina jicho moja tu hili
lingine ni bandia”
“I don’t care but I do
trust you” akasema Gosu
Gosu
“Papii nakiri sijawahi
kukutana na katili kama
wewe.Nilishuhudia namna
ulivyowakata kata watu kule
Nairobi lakini unapokuwa
nami ukatili ule
unapotea,unaongea
vizuri,unasimama
kunitetea,kwa nini?
“Imenitokea
hivyo.Ninapokuwa karibu
nawe nahisi tofaut…..”
“Wait ! akasema Devotha
na kuongeza sauti ya
runinga
“Ndugu watazamaji wetu
sasa tunawaunganisha na
waandishi wetu walioko
katika maandamano
makubwa ya wananchi
yanaoelekea ikulu hivi sasa”
akasema mtangazaji na
kujiunga na waandishi wao
walikuwa wakifuatilia
maandamano yale makubwa
yaliyoongozwa na waziri
mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania.
“Hii haijawahi
kutokea.Waziri mkuu aliyeko
madarakani kuungana na
wananchi kuandamana
kuishinikiza serikali ambayo
na yeye ni sehemu yake !
akasema Devotha
“Inasemekana yeye pia
mwanae ni mmoja wa
wasichana waliotekwa ndiyo
maana ameungana na
wananchi kuishinikiza
serikali kufanya juhudi za
kuwakomboa
watoto”akasema Gosu Gosu
“Vipi kuhusu nafasi yake
ya uwaziri mkuu?Ataendelea
nayo baada ya hiki
alichokifa………..”Devotha
akanyamaza baada ya
kutokea vikosi vya askari
polisi wa kutulia ghasia
wakiwa wamejihami kwa
silaha na vifaa tayari
kuyazuia maandamano yale
yasiendelee kuelekea
ikulu.Waziri mkuu
aliyekuwa kiongozi wa
maandamano yale
akasimamana watu wote
wakasimama.Amri ikatolewa
na mkuu wa kikosi kile cha
kutuliza ghasia kwamba
maandamano yale si halali
na kuwataka wananchi
watawanyike ama sivyo jeshi
litalazimika kutumia nguvu
Waziri mkuu aliyekuwa
kiongozi akaomba kipaza
sauti na kupewa
“Jeshi la
polisi,ninayezungumza hapa
ni waziri mkuu wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania
na maandamano haya ni ya
amani ndiyo maana
nimeungana na wananchi
kuwaonyesha kwamba tuko
pamoja nao.Naomba
mturuhusu tafadhali tuweze
kuendelea na maandamano
yetu hadi ikulu,wananchi
hawa wanaandamana kwa
amani bila vurugu zozote”
akasema Waziri mkuu na
kushangiliwa na watu
“Mheshimiwa waziri
mkuu,umeongoza wananchi
kuvunja sheria ya
kuandamana bila kibali
naomba uwatake wananchi
watawanyike tafadhali ama
sivyo jeshi la polisi litatumia
nguvu”
“Kamanda
nakuhakikishia kwamba
kama mwananchi yeyote
atapigwa kuuawa au
kuumizwa wewe na kikosi
chako chote mkatafute kazi
nyingine za kufanya”
akasema waziri mkuu
“Mheshimiwa waziri
mkuu hakuna aliye juu ya
sheria na sisi tuko hapa kwa
mujibu wa sheria.Tafadhali
nawaomba wananchi
mtawanyike haraka sana
maandamano haya hayana
kibali hivyo si
halali.Mkikaidi tutatumia
nguvu” akasema mkuu wa
kikosi kile lakini bado watu
waliendelea kushikana
mikono kuonyesha
mshikamano huku wakiimba
kwa nguvu wakitaka serikali
iwakomboe watoto wao.
Jeshi la polisi walifuata
taratibu za kuwataka watu
watawanyike na walipokaidi
wakaanza kuwatawanya kwa
gesi ya kutoa machozi na
maji ya kuwasha.Mvurugano
mkubwa ukatokea.Devotha
akasimama na kusogelea
runinga zaidi kuna kitu
alikiona katika runinga
kikamstua
“Papii we need to get this
video.Kuna kitu nimekiona
kimenisua sana”
“Umeona nini katika
mvurugano huu mkubwa?
“Muite Ruby” akasema
Devotha na Gosu Gosu
akamuita Ruby lakini Ruby
akagoma akadai hajisikii
vyema
“Kuna kitu nimekiona
hapa muhimu sana
kukifuatilia.” akasema
Devotha
“Umeona nini?
“Siwezi kukwambia kwa
sasa lakini lazima tuipate
video ile.Tuwasubiri akina
Mathew warejee kwani ni
yeye pekee anayeweza
kumpa kazi Ruby akaifanya”
akasema Devotha
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 15
Akina Mathew walifika
mtaa wa Mkongoro
wakalitafuta duka
waliloelekezwa na Imam
Sadiq
wakalipata.Wakashuka
garini na kuingia ndani mara
tu walipoingia Imam Shafii
akasalimiwa na sauti ya
mwanamke
“As salamu alaykum”
Imam Shafii akageuka
na kutazamana na
mwanamke aliyevaa gauni
refu jeusi
“Wa Alaikum
Salaam.Wajionaje hali”
akajibu Imam
“Mimi mzima
sana.Karibu sana Imam
Shafii leo umekuja dukani
kwetu kumchukulia bi
Khadija kitambaa?akauliza
Yule mwanamke Imam shafii
akatoa kicheko
kidogo.Hakuna anamfahamu
lakini Yule mwanamke
alikuwa anamfahamu
“Ni kweli nimekuja
kumtafutia bi Khadija
kitambaa kizuri lakini vile
vile nimekuja kuonana na bi
Zulfa.Natumai ndiye wewe”
akasema Imam Shafii
“Hapana mimi ni mdogo
wake naitwa Zaituni”
“Ouh Zaituni.Mmefanana
sana.Huyu mama Zulfa yeye
yuko wapi?akauliza Imam
Shafii
“Ametoka amekwenda
katika mizunguko yake
nimwambiaje
akifika”akauliza Zaituni
“Naomba unipatie namba
yake nitazungumza naye
kuna mchango wa
kuwapeleka watoto wetu wa
madrasa ziara jijini Arusha
na tunataka watembelee pia
mbuga za wanyama ndiyo
maana ninazunguka
kutafuta michango kwa
wafadhili mbali
mbali.Nimeambiwa dada
yako ni mchangiaji mzuri
sana wa maendeleo ya
msikiti wetu” akasema Imam
Shafii na kuchukua namba
za simu za Zulfa kisha
akachagua kitambaa kimoja
kikubwa na kuwaonyesha
akina Mathew
“Unaonaje hiki si
kitampendeza bi
Khadija:?akauliza na
Mathew akatoa fedha
akakilipia kile kitambaa
wakaondoka
“Mambo haya magumu
nusura ningeharibu kwani
mtu mwenyewe
tunayemtafuta simfahamu
lakini wao wananifahamu”
akasema Imam Shafii
“Usijali ulifanya vizuri
hujakosea”
“Nini kinandelea baada
ya hapa?akauliza Shafii.
“Imam Shafii sisi
tunakushukuru sana kwa
ushirikiano mkubwa
uliotupa.Kwa sasa kazi yako
imemalizika na kama
tukihitaji tena msaada
tutakuja
kukuona.Tutakuacha hapo
mbele utachukua taksi kwani
hatutaweza kukurejesha
nyumbani” akasema Mathew
“Jamani hata mimi
nawashukuruni sana kwa
kazi kubwa mnayoifanya ya
kupambana kuwakomboa
watoto wetu.Naombeni
msikate tamaa na muda
wowote mkihitaji kitu
chochote kutoka kwangu
nitafuteni
nitawasaidia.Kabla sijashuka
nataka niwaombee dua
Mwenyezi Mungu
awatangulie katika kazi hii
na mfanikiwe kuwakomboa
wote waliotekwa na kuwatia
nguvuni magaidi hawa”
akasema Imamu Shafii na
kuwaombea dua halafu
Mathew akampatia shilling
laki mbili kama ahsante kwa
ushirikiano aliowapa
wakamuacha katika kituo
cha taksi wakaendelea na
safari.
Baada ya kumshusha
Imam Shafii,Mathew
akampigia simu Ruby kwa
kutumia simu mpya
walizonunua na kumtaka
aifuatilie namba
atakayoipigia kufahamu
mahala mtu anayempigia
alipo.Ruby akaweka sawa
program zake na kumjulisha
Mathew kila kitu tayari na
Mathew akaipiga ile namba
ya Zulfa simu ikaanza kuita
“Hallow”ikasema sauti
laini ya mwanamke
“As salamu alaykum bi
Zulfa” akasema Mathew
“Wa Alaikum
Salaam.Nani mwenzangu?
Akauliza Zulfa
“Naitwa Hassan ninasali
Masjid Hidaya.Nilikuwa na
Imam Shafii ndiye aliyenipa
namba zako nikupigie
nikujulishe kwamba kuna
mchango unafanyika ili
kuwapeleka watoto wetu wa
madrasa waende ziara jijini
Arusha na kuzungukia
vivutio mbali mbali vya
kitalii.Mchango huu ni wa
hiyari na unatoa kile
ulichonacho.Kwa kuwa wewe
umekuwa mchangiaji
mkubwa wa miradi mingi
tumeona tukujulishe na
kama hali itaruhusu badi
unaweza ukatuchangia
chochote.”
“Nashukuru sana kwa
taarifa hiyo.Hilo ni jambo
jema sana Inshallah
tukijaaliwa nitachangia”
“ahsante sana bi Zulfa
unaweza ukatuelekeza
mahala ulipo hivi sasa
tukufuate tuchukue mchango
huo?
“Kwa sasa niko katika
mizunguko yangu ila
mwambie Imam Shafii
nitamfikisha mchango wangu
jioni au kesho asubuhi”
“Ahsante sana
nashukuru bi Zulfa.Uwe na
siku njema”
“Amina” akasema Zulfa
na kukata simu Mathew
akampigia Ruby
“Umefanikiwa kupata
mahala alipo? akauliza
Mathew
“Give me a second”
akasema Ruby na baada ya
dakika kama mbili akapiga
“Mathew nimefanikiwa
kupata mahala alipo huyo
mtu
uliyempigia.Ninakutumia
sasa hivi katika simu yako
ramani ya mahala hapo”
akasema Ruby na baada ya
dakika moja ujumbe
ukaingia katika simu ya
Mathew akaufungua ilikuwa
ni ramani aliyotumiwa na
Ruby ikionyesha mahala
alipo Zulfa .Mathew na
Austin wakaitazama ramani
ile kisha Mathew akasema
“Huu ni mtaa wa Saada
Thabit.Huu ni mtaa maarufu
kwa kuwa na maduka mengi
ya vifaa vya
elekroniki.Ramani
inaonyesha Zulfa yuko katika
moja wapo ya jengo katika
mtaa huu.Tuelekee huko”
akasema Mathew Austin
aliyekuwa katika usukani
akawasha gari wakaingia
barabarani wakaendelea na
safari.
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 16
“Ruby tayari umepata
satellite? Tumekaribia kufika
mtaa wa Saada Thabit”
Mathew akamwambia Ruby
“Yes I have it.Baada ya
muda mfupi nitaanza
kupokea picha za mahala
mlipo” akasema Ruby
“Thank you.Tujulishe
pale utakapokuwa tayari”
akasema Mathew na kukata
simu.
Mwendo ulikuwa wa
taratibu katika mtaa huu
wenye pilika pilika
nyingi.Simu ya Mathew
ikaita alikuwa ni Ruby
“Mathew tayari kila kitu
kimekaa sawa nimeanza
kupokea picha.Mtu wetu
yupo katika jengo lililo
pembeni ya jengo refu lenye
rangi ya dhambarau
“Ni Savanna hotel”
akasema Mathew
“Basi jengo la pembeni
yake ndimo alimo mtu wetu
uliyempigia simu” akasema
Ruby
“Good Job Ruby tutafika
hapo baada ya muda mfupi”
akasema Mathew
Austin aliendesha gari
taratibu hadi walipofika
Savanna hotel wakaipita
hoteli ile kubwa na pembeni
yake kulikuwa na jengo la
ghorofa moja.
“Nafikiri tumefika
mahala hapo” akasema
Mathew na kumpigia simu
Ruby
“Ruby tayari tumefika
mahala hapo.Tupe mrejesho
mtu wetu bado yumo ndani
ya jengo hili?akauliza
“Ndiyo.Bado hajatoka
ndani ya hilo jengo”
“Good.We’re going in”
akasema Mathew
Wakaegesha gari mbele
ya jengo lile lenye maduka
matano makubwa
yaliyokuwa upande wa chini
na upande wa juu kulikuwa
na maduka mawili na saluni
kubwa ya wanawake.
“Austin pitia maduka ya
chini kagua mimi naelekea
juu.Naamini lazima huyo
Zulfa atakuwa anafanana na
Yule mdogo wake
tuliyemkuta kwenye lile
duka la vitambaa” akasema
Mathew na kupanda ngazi
zilizokuwa pembeni ya jengo
lile kuelekea juu huku Austin
akianza kukagua maduka
yaliyokuwa chini.Mathew
alitembea taratibu hadi
katika mlango wa chumba
cha saluni ile kubwa
akachungulia
ndani.Kulikuwa na
wanawake kadhaa.
“Mathew the target is
moving.She’s talking to
someone on phone” Ruby
akamtaarifu Mathew na
mara mlango ukafunguliwa
wakatoka wanawake wawili
mmoja aliyevaa gauni refu la
rangi nyekundu
akizungumza na simu.
“Thank you Ruby.Tayari
nimemuona” akasema
Mathew na kuanza
kutembea taratibu kumfuata
mwanamke Yule.Mathew
akampigia simu Austin
akamtaka aelekee garini
kwani tayari amekwisha
muona mtu waliyekuwa
wanamtafuta.
Mwanamke Yule
alielekea moja kwa moja
katika gari lake aina ya
Mercedece benz rangi nyeusi
akaingia na kuondoka huku
akizungumza na simu.Austin
akakimbia kumfuata
Mathew garini wakaondoka
kumfuata Yule mwanamke.
“Mathew nimefuatilia
simu yake anazungumza na
mtu anaitwa Habib
Hussein.Ninakutumia
ramani ya mahala alipo huyo
Habib” akasema Ruby
“Sawa Ruby endelea
kumfuatilia na sisi tuko gari
tatu nyuma yake” akasema
Mathew na baada ya dakika
moja ukaingia ujumbe katika
simu yake ni ramani
ikionyesha mahala alipo
Habib Hussein ambaye
alikuwa anazungumza na
Zulfa simuni
Waliendelea kumfuatilia
Zulfa akaiacha barabara ya
Mtambikile akaingia katika
mtaa wa misheni.
“Where’s she
going?akauliza Mathew kwa
sauti ndogo akakata kona
kungia katika mtaa alioingia
Zulfa.Kulikuwa na watu
wengi mtaa huu hivyo
mwendo haukuwa
mkali.Ruby akapiga simu
“Mathew inawezekana
huyu mtu wetu anakwenda
kuonana na Habib kwani
inaonyesha anaelekea
uelekeo alipo Habib”
akasema Ruby na Austin
akaitazama ramani
waliyotumiwa na Ruby ni
kweli walikuwa wanaelekea
mahala alipo Habib.
“Ruby is right.Kuna
uwezekano Zulfa anamfuata
Habib” akasema Austin
“Tutaendelea kumfuata
hadi pale tutakapompata ili
atuonyeshe mahala alipo
huyu mtu ambaye alikuwa
na mawasiliano na Edger”
akasema Mathew.
Gari za Zulfa liliwasha
taa kuonyesha ishara ya
kukata kona kuingia upande
wa kushoto.
“Gaming house ! Mathew
akashangaa
“Anakwenda kufanya
nini hapa?akauliza
“Nadhani ndipo alipo
Habib” akajibu Austin.
Gari la Zulfa liliingia
katika jengo lenye bango
kubwa linalosomeka Dar es
salaam gaming house.Hapa
ni mahali ambapo inachezwa
michezo mbali mbali ya
kubahatisha kwa kutumia
mashine mbali mbali.Zulfa
hakwenda katika maegesho
ya kawaida wanakoegesha
watu wengine akaelekea
katika mlango mkubwa
uliokuwa upande wa kushoto
wa jumba lile na lango
likajifungua akaingiza gari
ndani.
“Huyu anaonekana ni
mzoefu sana wa mahala hapa
ndiyo maana amepita moja
kwa moja katika lile lango na
kuingia ndani” akasema
Mathgew
“Tumsubiri akitoka
tumfuate na tukipata nafasi
nzuri tumchukue kwani
hatuwezi kufanya chochote
hapa kuna watu wengi”
akasema Austin
“Austin hatuna muda wa
kusubiri.Magaidi
wanaendelea kuchinja watoto
hivyo lazima tuhakikishe
tunawakomboa watoto
haraka sana.I’m going in
there nataka kuchunguza
kama nitaweza kumuona
Zulfa.Wewe utabaki hapa nje
kwa tahadhari ukilichunguza
jengo hili.Nikikupigia simu
haraka sana uje ndani”
akasema Mathew na kabla
hajashuka garini Ruby
akapiga simu
“Mathew I’ve lost
them.Simu zao zote
zimezimwa”akasema Ruby
“Kwa nini wote wazime
simu kwa wakati
mmoja?akauliza Mathew
“Sifahamu nini
kimetokea hadi wakazima
wote simu kwa wakati
mmoja.Mathew
……”akasema Ruby na
kunyamaza
“Nini Ruby?Mathew
akauliza
“Wameua watoto
wengine wawili muda mfupi
uliopita.Mathew we must
hurry to find the
kids,wanawaua kikatili mno”
akasema Ruby
“Arlight.Ninakwenda mle
ndani kumtafuta
Zulfa.Lazima tuhakikishe
kwa namna yoyote ile
tunampata ili atuelekeze
kwa mtu huyo ambaye
tunaamini anaweza kuwa na
majibu ya mahala walipo
wasichana waliotekwa.Ruby
I promise you,we’ll get the
kids very soon” akasema
Mathew na kukata simu.
“Change of plan,we’re
going in together” akasema
Mathew na kushuka garini
wakatembea kwa tahadhari
kuelekea ndani ambako watu
walikuwa wanacheza
michezo mbali mbali.Mathew
na Austin wakaingia ndani
ya jengo lile wakatawanyika
kile mmoja akaenda upande
wake wakaanza kuchunguza
kama wangeweza kumuona
Zulfa.Kulikuwa na kamera
kadhaa zimefungwa mle
ndani
“Ninaziona kamera humu
ndani lazima kuna chumba
ambacho kinatumika kwa
ajili ya kuangalizia kila
kinachoendelea humu
ndani.Hii ina maanisha
kwamba kuna ofisi ziko
mahala ndani ya jengo hili
yawezekana huko ndiko
alikoenda Zulfa” akawaza
Mathew huku akiendelea
kuchunguza.Wakati
akiendelea kuzunguka
ukaingia ujumbe katika simu
yake ulitoka kwa Austin
“Tukutane maliwato”
Mathew hakupoteza
muda akaelekea iliko
maliwato akamkuta Austin
akinawa mikono.
“Nini
umegundua?akauliza
Mathew
“Kuna kamera
zimefungwa katika kila
chumba na kuna watu
wanaofuatilia kila
kinachoendelea humu
ndani.Wakati nikiwa
ninachunguza kuna mlango
mmoja karibu na block F
ulifunguliwa akatoka jamaa
mmoja ambaye alikuja
kutazama mashine moja
ambayo haikuwa ikifanya
kazi vizuri akatoa maelekezo
isitumike hadi
itakapotengenezwa kisha
akareja tena ndani.Kuna
ofisi zipo katika jengo hili
nahisi ndiko alikoenda Zulfa”
“Nimekuelewa
Austin.Kuna kitu kingine pia
nimkigundua katika jengo
hili kuna vifaa vya kuhisi
hatari ya moto kabla
haujatokea.Katika gari letu
tunayo makopo yale ya kutoa
moshi na kwa kawaida vifaa
hivi huweza kupiga kelele
pale vinapohisi moshi
mwingi.Utakwenda katika
gari utachukua kopo moja
kisha utakuja nalo huku
chooni na kulifungua.Moshi
utaanza kutoka na vifaa vile
vitapiga kelele na itatokea
taharuki humu ndani.Mimi
nitakuwa karibu na mlango
ule na utakapofunguliwa tu
nitazama ndani kumtafuta
Zulfa wewe utakwenda
kunisubiri katika gari”
akasema Mathew
“Looks like a good plan”
akasema Austin na
kutangulia kutoka mle
maliwato baada ya dakika
tatu Mathew naye akatoka
akaenda block F akauona ule
mlango aliousema Austin na
ili kupoteza muda
akalazimika kucheza katika
moja wapo ya mashine
iliyokuwa karibu na ule
mlango.Wakati akiendelea
kucheza akamuona Austin
akielekea chooni na baada ya
dakika moja akatoka
Mathew akaanza kujiweka
tayari.Dakika moja na nusu
toka Austin atoke mle chooni
moshi mzito ukaanza kutoka
kupitia chini ya mlango na
kuzua taharuki kubwa kwa
watu waliokuwa wakicheza
mle ndani wakaanza
kuulizana chanzo cha ule
moshi na mara kengele za
tahadhari ya moto zikaanza
kulia.Walinzi wakaingia
ndani na kuanza kuwatoa
watu nje ya jengo.Kulikuwa
na taharuki kubwa.Kama
alivyokuwa ametazamia
Mathew mlango ule aliokuwa
amesimama pembeni yake
ulifunguliwa na watu wawili
waliotoka kwa haraka sana
kuja kushuhudia
kilichokuwa kimetokea na
Mathew akapata upenyo
akaingia ndani.Hakuna
aliyekuwa anamfuatilia
kwani watu walikuwa katika
heka heka za
kujiokoa.Alipoingia upande
huu wa pili Mathew
akakutana na meza mbili
zilizokuwa na kompyuta
mbili ambazo hazikuwa na
watu.Akakipita chumba kile
na kukutana na korido
ambako aliona watu
wakitoka katika ofisi zao
wote wakijiuliza
kilichotokea.Akalifuata
korodo lile na kumkuta
mwanadada mmoja aliyevaa
shati jeupe na sketi fupi ya
kijivu akitoka ndani ya ofisi
moja Mathew akamgonga
akaanguka akamshika
mkono akamuinua..
“Samahani,kuna dada
mmoja ameingia huku
amevaa gauni refu
jekundu la kung’aa.Mimi ni
dereva wake aliniacha nje
nimsubiri baada ya kengele
ya tahadhari ya moto kuita
nimelazimika kuja
kumtafuta.Kama unafahamu
alipon ielekeze tafadhali”
akasema Mathew
“Yule ni mchumba wa
Habib.Mfuate katika ofisi ya
Habib nyoosha halafu pinda
kushoto mlango wa pili
ndimo ofisi ya Habib”
akasema Yule mwanadada
na kuanza kukimbia.Mathew
naye akakimbia kuelekea
katika ofisi ya Habib kama
alivyoelekezwa.Akaitoa
bastora yake akakinyonga
kitasa lakini mlango ulikuwa
wazi akaingia ndani chumba
kilikuwa kitupu hakukuwa
na mtu yeyote akachukua
simu akampigia Austin
“Austin nimeipata ofisi
ya Habib lakini hayuko
humu chumba ni kitupu.Kaa
macho huko nje kama
anatoka” akasema Mathew
na kuelekea mezani akaanza
kupekua makaratasi na
mafaili aliyoyakuta pale juu
kuangalia kama anaweza
akapata kitu cha kumsaidia
lakini hakupata chochote
akaenda katika kabati
kubwa akavunja kioo na
kuanza kupekua mafaili
mara akastuliwa na sauti
kali
“Taratibu sana inua
mikono yako juu” ikasema
sauti ya mwanaume.
“Taratibu geuka
nitazame” akasema Yule
jamaa na Mathew akageuka
taratibu akajikuta akitazama
na bastora mbili na
kilichomstua zaidi ni kumuoa
mtu aliyekuwa akimtafuta
Zulfa akiwa na bastora
pi.Zulfa na Yule jamaa
walionekana kushangaa
hawakumfahamu Mathew
“Who are you?akauliza
Yule jamaa
“Habib Hussein”
akasema Mathew na Yule
jamaa akastuka sana na
kutazamana na Zulfa
“Slowly drop down your
gun” akasema Habib na
Mathew akatii taratibu
akaichomoa bastora yake
akaiweka chini huku mkono
mmoja akiwa ameuinua.
“Nini unakitafuta katika
ofisi yangu?Nimekuona
kupitia simu yangu ukiingia
katika ofisi yangu nikarudi
haraka.Nakuuliza tena wewe
ni nani?Unatafuta nini
humu? Akauliza Habib
“Listen to me guys.Kuna
bomu ndani ya nyumba hii
na muda si mrefu
litalipuka.Let’s talk outside !
akasema Mathew Habib
akastuka akageuka
kumtazama Zulfa aliyekuwa
mlangoni.Ni fursa hiyo
ambayo Mathew alikuwa
anaitafuta.Kwa kasi ya
umeme akairukia bastora
yake iliyokuwa sakafuni
“Habib !! akapiga ukelele
Zulfa kumstua Habib
ambaye aligeuka ghafla na
kutaka kuizinga bastora
yake lakini Mathew
aliyekuwa mwepesi kama
kima tayari alikwisha
inyakua bastora yake
akaizinga na kuachia risasi
tatu zilizompata Habib
kifuani akaanguka
chini.Baada ya Habib
kuanguka chini Zulfa
akageuka haraka na kuachia
risasi mbili kumlenga
Mathew aliyekuwa chini
lakini jicho la Mathew
lililozunguka kama kinyonga
lilikwishaona uelekeo ambao
Zulfa alikuwa ameulenga
hivyo akajirusha pembeni
haraka na kufumba na
kufumbua Zulfa alikuwa
amepotea.Mathew akainuka
na kwenda mlangoni
akachungulia lakini
hakumuna Zulfa alikwisha
toweka
“She’s gone” akasema
Mathew na kuchukua simu
akampigia Autin huku
akikimbia.
“Austin kuwa makini
huko nje Zulfa ametoweka
huku ndani.Angalia ule
mlango
alikoingilia”akaelekeza
Mathew na mara akajikuta
amepigwa na kitu usoni
akaanguka chini.Kabla
hajajua kilichompiga
akapigwa teke kali la tumbo
akatoa mgumo wa
maumivu.Mathew alihisi
maumivu makali sana ya
kichwa lakini akajitahidi
kufumbua macho na kitu cha
kwanza alichokishuhudia ni
mwanamke aliyevaa suruali
nyeusi na gauni jekundu
akiwa amelipandisha na
kulifungia kiunoni.
“Zulf..” akapigwa teke
kali la usoni damu ikaanza
kumtoka mdomoni
“Huyu mwanamke
anaonekana ni hatari sana
katika kupigana natakiwa
kumdhibiti haraka
sana.Mathew akajifanya
akigugumia kwa maumvu
makali na Zulfa akiwa na
bastora mbili akaanza
kumsogelea.
“Who are you son of
b…………” hakumaliza
alichotaka kukisema Mathew
akajigeuza kwa kasi ya ajabu
na kumkata mtama
akaanguka chini lakini kwa
umahiri mkubwa
akajibiringisha na kusimama
tena lakini kabla hajafanya
chochote Mathew naye
alikwisha simama Zulfa
akazunguka mateke mawili
Mathew akayaona na
kukwepa halafu
akamtandika teke zito
lililompeleka ukutani na
kutoa mguno wa
kuumia.Ghafla Zulfa
akachomoa bastora nyingine
Mathew akarukia nyuma ya
mtungi mkubwa wa maua
risasi zikapiga mtungi ule na
kuupasua kisha Zulfa
akatoka mbio.Mathew
akaokota simu yake na
bastora zile mbili alioziacha
Zulfa na kuanza
kumfuatilia.Akasikia mlango
ukibamizwa na piki piki
ikiwashwa.Akawahi mlango
ule lakini ulikuwa
umefungwa kwa ndani
.Akaruka teke zito na
kuuvunja lakini alichelewa
tayari Zulfa alikuwa
ameondoka na pikipiki
kubwa akielekea katika
mlango mkubwa wa kutokea
nje.Mathew akaanza kuachia
risasi lakini Zulfa alikuwa
makini akashika usukukani
kwa mkono mmoja akageuka
na kuanza kuachia risasi
ikamlazimu Mathew
kujificha Zulfa akasimama
katika mlango mkubwa
akisubiri ufunguke huku
akiachia risasi kumzuia
Mathew asimsogelee.Mathew
akampigia simu Austin
“She’s coming out.Yuko
na piki piki ! akasema
Mathew mlango ukafunguka
Zulfa akatoka
“Tayari
nimemuona.What do you
suggest I take her down or
we follow her?
“Take her down we don’t
have much time” akasema
Mathew.Austin ambaye
alikuwa karibu na lango lile
alilotokea Zulfa akajiweka
tayari na mara tu lango
lilipofunguliwa Zulfa akatoka
akiwa katika mwendo mkali
Austin bila kujali watu wengi
waliokuwepo pale nje
akaachia risasi kadhaa na
piki piki ile ikaanguka
chini.Zulfa alirushwa na
kuanguka mbali lakini kwa
umahiri wake akatua chini
kifundi hivyo hakuumia
lakini hakuweza kutembea
kwani risasi mbili kati ya zile
alizoachia Austin zilimpata
mguuni.Bila kupoteza muda
Austin akamfuata
akamfunga pingu haraka
haraka akamuinua na
kumkimbiza hadi katika gari
lao akamuweka kiti cha
nyuma na kumpigia simu
Mathew
“Mathew tayari
nimempata.Come quick”
“Good job
Austin.Nilikuwa napekua
gari lake kuna vitu
nimevipata.I’ll be there in a
second” akasema Mathew na
kukata simu.
Watu waliokuwapo pale
nje walishuhudia kile
alichokifanya Austin na kwa
haraka walinzi wawili
waliokuwa na silaha
wakaanza kulisogelea gari
lake
“C’mon guys don’t do this
!akasema Austin kwa sauti
ndogo mara wote wawili
wakaanguka chini.Mathew
Mulumbi aliyetokea ndani
aliwaona na kuwamaliza
wote kwa bastora yake yenye
kiwambo cha sauti kisha
akakimbia hadi katika gari
akaurushia mkoba aliokuwa
nao garini akarukia katika
usukani na kuwasha gari
kisha wakaondoka kwa kasi
kubwa huku Austin akiwa
dirishani na bastora
akiendelea kuachia risasi na
kulifanya eneo lote liwe jeupe
kabisa.Walitoka mtaa wa
misheni wakaingia barabara
ya Mtambikile kisha
wakakunja kulia na kuingia
barabara ya Fidel ambayo
haikuwa na magari mengi na
hapo mwendo ukawa mkali
wakakata kulia na kuingia
barabara ya Ngorongoro
“Austin Make sure no
body is following us”
akasema Mathew
“Hakuna anayetufuatilia
Mathew.Just drive ! akasema
Austin.Jeraha la Zulfa
lilikuwa linatoa damu nyingi
“Una boksi la huduma ya
kwanza humu?akauliza
Austin na Mathew
akamuelekeza lilipo Austin
akachukua pamba na
kuigandamiza katika jeraha
la Zulfa ambaye alikuwa
anagugumia kwa maumivu
makali.
“I’ll kill you bastard !!
akalia Zulfa akihisi maumivu
makali.
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 17
Austin na Mathew
waliwasili katika makazi
yao,haraka Zulfa
akashushwa garini na
kuingizwa ndani.
“Mathew tunahitaji
kuziondoa risasi katika
mguu wa Zulfa amepoteza
damu nyingi” akashauri
Austin
“I need to call a doctor”
akasema Mathew
“There is no need.Hatuna
muda wa kumsubiri hadi
daktari afike hapa.I’ll do it”
“Can you remove the
bullets?
“That’s why we’re special
unit.Tunafundishwa kila kitu
ili hata tukiwa katika
misheni Fulani na mmoja
wetu akapigwa risasi
tunamuhudumia sisi
wenyewe” akasema Austin
“Good.Let’s do it”
akasema Mathew na Zulfa
akaingizwa katika chumba
alimo mke wa balozi
kulimokuwa na meza.Austin
akaenda kuchukua sanduku
lake dogo la vifaa na kulileta
mle chumbani.Mathew
akawaacha Austin na Gosu
Gosu akamfuata Ruby
“Ruby you did a great job
thank you”
“You’re welcome” akajibu
Ruby huku akitabasamu
Mathew akampatia
kompyuta aliyoitoa katika
gari la Zulfa ili aichuguze
kama kuna kitu anaweza
akakipata.
“Gosu Gosu mshike
mikono mzuie kwa nguvu
kwani hatuna sindano ya
ganzi wala usingizi hivyo
nitamuwekea dawa Fulani
katika jeraha kisha nitazitoa
risasi.Atapiga ukulele kwani
dawa inauma sana” akasema
Austin na Gosu Gosu
akamshika Zulfa mabegani.
“Hey ! listen to me
lady.I’m going to remove the
bullets.It’s goin to hurt lakini
nakupa hii uma na meno”
Austin akamwambia Zulfa
na kumpa kitu Fulani aweke
mdomoni
“You go to he……..aaghh”
Zulfa akapiga ukelele
mkubwa wa maumivu baada
ya Austin kumwagia dawa
katika jeraha.
“Easy gentlemen..easy !!
akasema mke wa balozi
aliyekuwamo mle chumbani
akainuka na kusogelea pale
mezani
“Please stay away maam”
akasema Gosu Gosu
“I can help.I’m a doctor”
akasema Yule mama Austin
akageuka na kumtazama
“Are you sure?akauliza
“Yes”akajibu na kisha
akaanza kusaidia na Austin
kutoa risasi katika mguu wa
Zulfa
“Mimi na Yonathan
tulikutana jeshini”akasema
Yule mke wa balozi
“Sote tulikuwa
tunahudumia askari
walioumia katika mapigano
na wapalestina”akaendelea
kuwapa historia yake namna
alivyokutana na balozi
Yonathan Cohen wakawa
wapenzi na hatimaye
wakafunga ndoa
Walifanikiwa kutoa
risasi mbili katika mguu wa
Zulfa,wakayafunga
majeraha.Zulfa alikwisha
poteza fahamu
“You need to take her to
hospital ! akasema mke wa
balozi Austin hakumjibu
kitu akafanya usafi na kisha
wakambeba Zulfa na
kumpeleka katika chumba
kidogo ambacho alikitumia
kama stoo ambamo kulikuwa
na kitanda kidogo
wakamlaza
Wakati Ruby akiendelea
na jitihada za kuipekua
kompyuta ya Zulfa Mathew
akaelekea katika chumba
alimo Edger
“Hallow Edger” akasema
Mathew
“Mmefanikiwa kumpata
Yule jamaa?akauliza Edger
“Bado hatujafanikiwa
kumpata lakini tumempata
mtu ambaye anaweza
akatufikisha
kwake.Umewahi kumuona
au kumsikia mwanamke
mmoja anaitwa Zulfa?
“Zulfa?
“Ndiyo.Ni mtu wa karibu
na jamaa tunayemtafuta”
akasema Mathew
“Hapana simfahamu
huyo Zulfa na sijawahi
kumuona”
“Una hakika hajawahi
kutumwa kwako hata mara
moja kukuletea ujumbe
wowote?akauliza Mathew
“Kama nilivyokwambia
kwamba mimi nilikuwa
nawasiliana na Yule jamaa
pekee na hajawahi kumtuma
mtu mwingine yeyote
kuniletea ujumbe”
“Are you sure?
“yes I’m sure” akajibu
Edger
“Good.Nitakujulisha pale
tutakapokuwa tumempata”
akasema Mathew na kuanza
kutoka mle chumbani
alipofika mlangoni akageuka.
“Magaidi tayari
wamechinja watoto wanne na
wanaendelea kuchinja
zaidi.Kuna chochote ambacho
unaweza ukaniambia
kinachoweza kusaidia
kuwapata watoto wale zaidi
ya huyu jamaa?
“Hakuna chochote
ninachokifahamu
kinachoweza kusaidia zaidi
ya taarifa hiyo niliyokupa
Mathew.Find that man !
akasema Edger na Mathew
akatoka na kuwakuta aina
Austin tayari wamemaliza
kumtoa Zulfa
risasi.Wakamjulisha kuwa
mke wa balozi ni daktari na
ametoa msaada katika
kumtibu Zulfa.
“Good job to you
all.Hatimaye tumempata
mtu ambaye tuna hakika
anaweza akatufikisha kwa
mtu ambaye alikuwa
anawasiliana na Edger
Kaka.Mwanamke huyu ni
hatari sana ana uwezo
mkubwa wa kupigana bila
kutumia silaha na akiishika
silaha ni mtumiaji mzuri
pia.Sikuwa nimetegemea
kabisa kama angeweza kuwa
hatari namna ile.Haikuwa
rahisi kumpata”Akasema
Mathew na kuwataka
wenzake wapumzike wakati
wakiendelea kumsubiri Zulfa
azinduke na papo hapo
kusubiri kama Ruby
anaweza akapata kitu katika
kompyuta ya Zulfa.
“Kuna chochote
umekipata Ruby?akauliza
Mathew
“Still searching” akajibu
Ruby na Mathew akasimama
nyuma yake akiangalia
namna Ruby alivyokuwa
akiifanya kazi yake mara
akafuatwa na Gosu Gosu
“Mathew can we talk for
a second” akasema Gosu
Gosu wakatoka ndani ya kile
chumba
“Mlipoondoka mimi na
Ruby tulikuwa tunatazama
runinga namna maandamano
yalivyokuwa
yanaendelea.Maandamano
hayo yalisimamishwa na
askari wa kutuliza ghasia
kwa hayakuwa halali na
waliyatawanya.Mimi sikuwa
nimetilia maanani sana
kutazama kilichokuwa
kinaendelea lakini Devotha
aliyekuwa makini kufuatilia
kuna kitu alikiona ambacho
alisema si cha kawaida na
akataka kuipata video ile ya
namna maandamano
yalivyotawanywa na
askari.Tulimuomba Ruby
atusaidie kuipata video hiyo
ili Devotha aweze
kuchunguza zaidi hicho
alichokisema hakikuwa cha
kawaida lakini kwa kuwa
Ruby na Devotha bado
hawajakaa sawa ilikuwa
vigumu kwa Ruby
kukubali.Nimeona bora
nikueleze jambo hili
ulifahamu ili tujue kitu gani
ambacho Devotha
alikiona”akasema Gosu Gosu
“Hakukueleza nini
aliona?akauliza Mathew
“Hapana
hakunieleza”akasema Gosu
Gosu wakatoka kwenda nje
kuonana na Devotha
“Gosu Gosu ameniambia
kwamba kuna kitu Fulani
ulikiona wakati askari wa
kutuliza ghasia wakitawanya
maandamano.Can you tell
me what you saw?Mathew
akamuuliza Devotha
“Ni kweli kuna kitu
nilikiona ambacho
kilinishangaza kidogo ndiyo
maana nikataka kupata
kipande kile cha video ya
askari wakitawanya
waandamanaji ili nijiridhishe
na kile nilichokiona ni kitu
cha kweli”
“Uliona nini?akauliza
Mathew
“Wakati maandamano
yamesimamishwa na
polisi,kulitokea majibizano
kati ya kamanda wa polisi na
waziri mkuu.Wakati
majibizano hayo yakiendelea
I saw someone”akasema na
kunyamaza kidogo
“Ulimuona nani?
“Nyuma ya waziri mkuu
kulikuwa na mwanamke
mmoja aliyevaa suti ya
suruali rangi ya kijivu na
pembeni ya huyo
mwanamama kulikuwa na
mtu mmoja amevaa miwani
myeusi na suti
nyeusi.Nilipomuona huyo
mtu nikastuka na
kumuelekezea macho
nikamuona akizungumza na
simu halafu akampatia simu
mwanamama ambaye
alikuwa nyuma ya waziri
mkuu aliyekuwa
akizungumza katika kipaza
sauti wakati
huo.Alipomaliza,yule
mwanamama akamsogelea
waziri mkuu na
kumnong’oneza kitu
sikioni.Kamera ilihama na
sekunde chache baadae gesi
ya machozi ikaanza
kurushwa waandamanaji
wakatawanyika.Nilitaka
kupata kipande kile
nijiridhishe kama mtu
niliyemuona kweli ni
mwenyewe au wamefanana”
“Mtu huyu uliyemuon….”
Akasema Gosu Gosu lakini
Devotha akamkatisha
“Sijamaliza bado”
“Go ahead” akasema
Mathew
“This man I saw…”
akasita kidogo halafu
akasema
“Wakati idara yetu
inaanzishwa jukumu letu la
kwanza lilikuwa ni
kuvitafuta na kuvisafisha
vikundi vya kigaidi
vilivyoanza kuchipuka na
kutishia hali ya amani.Kuna
kikundi kimoja ambacho
kiongozi wake alijulikana
kama Nazil Jalib kiliwahi
kuvamia kijiji, kuiba mali na
kuua watu
hamsini.Tulifanikiwa
kukiondoa kikosi hicho
hatari na nyumba ya
kiongozi wake Nazil
iliteketezwa kwa bomu na
tuliamini kwamba amefariki
lakini mtu niliyemuona leo
katika maandamano yale
anafanana vile vile na
Nazil.Ninataka kuipata video
ile ili kujiridhisha kama
kweli mtu Yule ni Nazil
kama ni yeye basi mtu huyu
ni hatari sana na kama ni
yeye ana ukaribu gani na
waziri mkuu?akauliza
Devotha
“Usihofu D……” akasema
Mathew na Austin akatokea
“Guys Ruby ana jambo
amelipata anataka
kutueleza.Am I missing
something here?akauliza
“Kuna jambo Fulani
Devotha alikuwa ananieleza”
akasema Mathew
wakaelekea ndani
“Ruby umepata
nini?akauliza Mathew.
“Kuna kitu ambacho
kimenishangaza
kidogo”akanyamaza na
kuvuta pumzi
“Nimeipekua kompyuta
hii ya Zulfa haina kitu
chochote cha maana zipo
program za kawaida za
kuiwezesha kompyuta
kufanya kazi.Kompyuta hii
haitumiki kwa mawasiliano
yoyote ya barua pepe au
mitandao yoyote ya kijamii”
akasema Ruby
“Kompyuta hii nimeikuta
katika mkoba uliokuwamo
katika gari lake pamoja na
vifaa vyake vingine vidogo
vidogo nikajua ndiyo
kompyuta yenye taarifa zake
zote.Haiingii akilini atembee
na kompyuta ambayo
haitumii katika shughuli
zake.Haitumii kwa
mawasiliano au hata kwa
program za kiofisi.Una
hakika hakuna mafaili
ameyafuta?
“Kama kuna mafaili
ameyafuta ningejua lakini
hakuna kilichofutwa”
akasema Ruby
“Austin unadhani Zulfa
ataamka saa ngapi?
“Sina hakika lakini
hatachukua muda mrefu”
“Tunahitaji kumfanya
mahojiano haraka.Magaidi
wanaendelea kuua watoto
kila baada ya muda”
akasema Mathew na Ruby
akasema
“Sijamaliza bado.”
Akasema Ruby na kufumba
macho akionekana kuwa
katika maumivu
“Ruby are you
oay?akauliza Mathew
“Yeah I’m fine” akajibu
Ruby
“Wakati naendelea
kuipekua hii kompyuta
kuna ujumbe ulijitokeza
ghafla.Nikaufungua
ujumbe ule ulikuwa ni
mchezo wa
kompyuta.Ulisomeka hivi
“Hello Zay come online
let’s play” akasema Ruby
“A computer game!
Mathew akashangaa
“Yes a computer game”
akasema Ruby
“Let me see it” akasema
Mathew
“Unahitaji namba za siri
za kufungulia huo mchezo ili
uweze kucheza” akasema
Ruby.Mathew akafikiri
kidogo na kusema
“Ruby unaweza kuitafuta
namba ya siri anayotumia
Zulfa kufungulia mchezo
huu?akauliza Mathew
“Yes I can” akajibu Ruby
“Good.Find it” akasema
Mathew.
“Wakati Ruby anatumia
program yake ya kutafuta
namba za siri za kuufungulia
mchezo huu Devotha endelea
na lile suala ulilokuwa
unatueleza” akasema
Mathew
“Niliwaeleza kuwa Nazil
Jalib ni mtu hatari sana
ambaye tuliamini amekufa
katika mlipuko wa bomu
pamoja na watu wengine
saba waliokuwemo katika
nyumba mlipuko ulipotokea
lakini kumuona mtu kama
Yule pale leo tena karibu na
waziri mkuu nimestuka
sana.Ni mtu hatari na kama
yuko hai anapaswa
kutafutwa”
“Mtu huyu ni nani hasa?
“Anajiita invisible.Ni mtu
ambaye hatukuwahi
kufanikiwa kupata taarifa
zake za kutosha.Nahitaji
kupata kile kipande cha
video ili kujiridhisha kama
kweli ni yeye ama vipi.Kuna
jambo lingine vile vile
ambalo sina hakika
mtalipokeaje lakini kama
tukithibitisha kweli ni Nazil
italazimu kumshirikisha
Kaiza” akasema Devotha
‘That bastard works for
president !! akafoka Mathew
“Ili kujiridhisha kwamba
huyu niliyemuona leo katika
maandamano ni Nazil Jalib
italazimu kumtafuta Kaiza
kwani kwa sasa yeye ndiye
kiongozi wa idara niliyokuwa
ninaiongoza na kumbu
kumbu zote za Nazil ziko
pale”
“Fine.We’ll see what we
can do” akasema Mathew na
kumfuata Ruby
“Kuna chochote
umekipata?akauliza Mathew
“Program still searching”
akasema Ruby
“How long it’ll take”
“It depends.Let’s wait for
program to finish” akasema
Ruby.Mathew akatoka na
kuingia katika chumba
alimokuwamo mke wa balozi
ambaye alistuka sana na
kuanza kuogopa,Mathew
akamsogelea
“Unajisikiaje?akauliza
‘Naendelea vizuri.Lini
nitakuwa huru?akauliza
“Nimeambiwa
ulichokifanya muda mfupi
uliopita.Tunashukuru sana
kwa msaada uliotoa kwa
mgonjwa tuliyemleta hapa”
akasema Mathew
“Taaluma yangu ni
daktari ndiyo maana
nikawasaidia”
“Mama kwanza kabisa
naomba ufahamu kwamba
sisi si watu wabaya.Sisi siyo
wakatili kama unavyodhani
na usiwe na hofu yoyote
ukiniona mimi au
mwenzangu yeyote ameingia
humu ndani.Tuko katika
kutekeleza kazi moja nzito
sana kwa ajili ya usalama wa
taifa.Magaidi wamevamia
shule na kuteka watoto sitini
na sita na hivi
tuzungumzavyo tayari
wamekwisha anza
kuwachinja mmoja baada ya
mwingine na tunafanya
jitihada za kuwakomboa”
“Mimi na mume wangu
tunahusika nini na hao
magaidi?akauliza mke wa
balozi
“Jioni ya leo utarejea
nyumbani kwako,hatuna
tena sababu ya kuendelea
kukuweka hapa na yeyote
atakayekuuliza mahala
ulipokuwa utamueleza
ulipata safari ya
dharura.Ningekupeleka
nyumbani kwako muda huu
lakini tunayo shughuli nzito
ya kuwakomboa watoto
waliotekwa na magaidi”
akasema Mathew na mlango
ukafunguliwa Gosu Gosu
akaingia
“Mathew program
imekubali” akasema Gosu
Gosu na Mathew akatoka
akamfuata Ruby
“Nimefanikiwa kuzipata
namba za siri za kuingia
katika mchezo huu” akasema
Ruby na kuufungua mchezo
ule Mathew akautazama
kisha akasema
“Oh thank you Heaven
Father” akasema Mathew na
kuwatazama wengine
“This is how terrorist
communicates.Wanafahamu
kwamba wanafuatiliwa sana
katika simu na mitandaoni
hivyo siku hizi wanatumia
michezo kama hii kwa
mawasiliano kitu ambacho si
rahisi kwa mtu kuweza
kutilia shaka” akasema
Mathew na kuanza
kuwaelezea wenzake namna
magaidi wanavyowasiliana
kwa kutumia michezo.
“Mkitaka kuamini
ninachokisema ngoja
tujaribu” akasema Mathew
na kuanza kucheza
“Nimeanzisha mchezo ili
kuwapa taarifa kwamba niko
hewani” akasema Mathew
Baada ya muda mtu
mwingine akacheza na kisha
ujumbe ukajitokeza chini
“uko wapi?Tunakutafuta
sana.Kwa nini umezima
simu siku kama ya
leo?akauliza Yule mtu wa
upande wa pili
“Mmeona namna
wanavyowasiliana?akauliza
Mathew na kucheza tena
halafu akaandika ujumbe
chini
“Kulifanyika uvamizi
Habib ameuawa mimi
nimefanikiwa kutoka salama
na kukimbia.Msihofu ni wezi
walitaka kupora fedha”
Baada ya muda ujumbe
ukajibiwa
“Z kuna mabadiliko ya
dharura yamefanyika
naamini bado hujapata
taarifa.Hatutakutana kwa
Zahara kama ilivyokuwa
imepangwa bali tutakutana
Mellisa hotel ukumbi no
5.Utamkuta Zeno
atakupokea” akasema Yule
jamaa mwingine
“Nini sababu ya
mabadiliko? Mathew
akauliza
“Kuna jambo linakwenda
kufanyika hapo fika bila
kukosa.Saa tisa kamili”
akasema Yule jamaa
“Sawa ninakuja” Mathew
akajibu na Yule mtu akatoka
hewani na meseji zote
walizotumiana zikafutika
“Nadhani mmeona
namna wanavyofanya
mawasiliano yao.Si rahisi
kwa mtu mwingine
kugundua kama kuna
mawasiliano
yanafanyika.Wote wana
mchezo huu katika simu au
kompyuta zao na
wameunganishwa na
mtandao wao hivyo basi
kunapokuwa na jambo
hujulishana kwa kupitia njia
hii”
“These people are smart”
akasema Gosu Gosu
“No ! They are stupid !
akajibu Austin
“Tayari tumepata
uhakika kwamba
wanakutana mchana wa leo
Mellisa hotel.Tutakuwa
wageni wao kwani na sisi
tutakwenda kuhudhuria
katika kikao chao kujua
wanachokijadili.Sasa
tumepata uhakika mkubwa
kwamba kweli Zulfa
anashirikiana na magaidi wa
IS ambao tayari wana
mtandao wao mkubwa hapa
nchini.Kitu kikubwa kwa
sasa ni kutafuta namna ya
kuweza kuingia katika hicho
kikao” akasema Mathew
“Ninaamini kikao hicho
kitahudhuriwa na watu
wengi na muhimu wa IS
hapa nchini ambao
tunawatafuta sana so this is
the chance.Hakuna wakati
ambao tutawapata wengi
kwa pamoja kama katika
kikao hiki na ninaamini
kutokea pale tutaweza
kupata taarifa za mahala
walipo watoto waliotekwa
nyara”akasema Austin
“Anachokisema Austin ni
kitu cha msingi sana na
kama tukifanikiwa kuingia
katika kikao hicho tutakuwa
tumepiga hatua kubwa
sana.Guys we’re so close to
know where the kids
are”akasema Mathew
“Nina wazo” akasema
Devotha
“Mellisa hoteli ni moja ya
hoteli kubwa hapa
nchini.Viongozi wengi wa
kimataifa wanapokuja nchini
hufikia pale kutokana na
hadhi yake.Ni hoteli yenye
ulinzi mkubwa.Nimefika pale
mara nyingi katika shughuli
zangu hivyo ninapafahamu
vyema.Kumbi zake za
mikutano zinaaminika sana
na hata vikao vingi vya siri
hufanyika pale ndiyo maana
kupata ukumbi pale kwa
mikutano ni shida kwa kuwa
kila siku kumbi zake
zimejaa.Tunatakiwa
kutafuta namna ya kuweza
kuwapata ambayo kwanza
haitawafanya wastuke na
waahirishe kikao,pili
kuwachukua bila kutumia
nguvu”
“Nini ushauri
wako?akauliza Mathew
“Maya B virus”akasema
Devotha
“Whats that? Akauliza
Mathew
“It’s a sleeping Virus.Hiki
ni kirusi ambacho
kinasambaa kwa njia ya
hewa na mtu yeyote akivuta
hewa yenye kirusi hiki basi
hupatwa na usingizi wa
ghafla na kulala.Tukiwa na
kirusi hiki tutatumia mfumo
wa usambazaji hewa wa pale
hotelini na hewa yenye kirusi
hicho itambaa hoteli nzima
na watu wote hotelini mle
watalala usingizi.Baada ya
kuwalaza tutaleta gari la
wagonjwa na kuwapakia
watu wetu na kuondoka
nao”akasema Devotha
“Hii ni njia nzuri
sana.Nataka kufahamu zaidi
kuhusu hicho kirusi,mtu
akivuta hewa yenye kirusi
hicho inamchukua muda gani
kulala na inachukua muda
gani kuamka? Hakuna
madhara yoyote ya kiafya
kwa mtu aliyevuta hewa
yenye kirusi hicho?Mathew
akauliza
“Inamchukua mtu dakika
tano hadi kumi kulala
usingizi toka avute hewa
yenye kirusi Maya naakisha
lala inamchukua dakika
thelathini ndipo
anaamka.Kuhusu madhara
hakuna madhara
yoyote.Kirusi hiki
kimetengenezwa maalum
kwa ajili ya kumfanya mtu
alale.Hiki ni kirusi kipya
kabisa ambacho
kimetengenezwa na jeshi la
Marekani na kinatumika
kama silaha.Wanapokuwa
katika mapambano dhidi ya
vikosi mbali mbali vya
kigaidi hutumia teknolojia ya
ndege ndogo zisizo na rubani
kwenda kusambaza kirusi
hiki mahala walipo magaidi
ambao hulala na kujikuta
wamevamiwa.Mtu akiamka
baada ya dakika mbili
atakuwa mzima tena na
hakuna madhara mengine
msihofu” akasema Devotha
“Nadhani njia hii
aliyoipendekeza Devotha ni
njia nzuri sana labda kama
kuna mtu ana wazo
mbadala”akasema Mathew
na wote wakakubaliana na
wazo lile la Devotha la
kutumia kirusi Maya B
“Okay sote
tumekubaliana kutumia
kirusi hicho.Swali ni wapi
tutakipata hicho kirusi?
Mathew akauliza
“Ninacho nyumbani
kwangu”akajibu Devotha
“Good.Kama kirusi kipo
tayari tujadili namna ya
kwenda kukiingiza katika
mfumo wa hewa wa pale
hotelini”
“I’ll do it.Nimefika katika
ile hoteli mara nyingi na
ninaifahamu vyema kila
sehemu.Nitachukua kirusi
na kwenda kukiingiza katika
mfumo wa hewa safi.Kabla
sijaingiza kirusi hicho katika
mfumo wa hewa nataka gari
la wagonwa liwe
limeandaliwa na kuwepo
karibu na nitakapojulishwa
kuwa kila kitu tayari basi
nitaingiza kirusi na baada ya
dakika tano kupita
mnatakiwa kufika haraka
sana na kuwachukua watu
tunaowahitaji”
“Good plan.mambo
yatakwenda namna
hii.Devotha na Austin ninyi
mtakwenda hotelini.Austin
utamlinda Devotha hadi
uhakikishe amefanikisha
kuingiza kirusi hicho katika
mfumo wa hewa kisha
mtanijulisha.Mimi
ninakwenda kufanya mpango
wa gari la wagonjwa na
baada tu ya kupewa taarifa
nitafika hapo mara moja na
wote tutasaidiana kuweza
kuwabeba watu wetu na
kuwapakia garini.Gosu Gosu
wewe utabaki hapa kulinda
usalama tunao watu wawili
hatari humu ndani.Kuna
yeyote mwenye wazo
mbadala kabla
hatujatawanyika kwenda
kujiandaa kwa kazi
hii?akauliza Mathew
hakukuwa na mwenye wazo
mbadala bila kupoteza muda
Austin akaingia chumbani
kwake akavaa suti nzuri
nyeusi kisha wakaingia
katika gari la Mathew
wakaondoka hadi nyumbani
kwa Devotha Mathew
akawaacha pale yeye
akaondoka kwenda kuonana
na Dr Hiran.
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 18
Devotha na Austin
waliwasili hoteli Mellisa
wakiwa katika gari la
kifahari aina ya Rolls Royce
phantom rangi ya fedha mali
ya Devotha.Ukimya ulikuwa
mkubwa sana katika hoteli
hii iliyokuwa imezungukwa
na msitu wa miti ya
kivuli.Sauti za ndege mbali
mbali ndizo
zilizosikika.Ulinzi katik
ahoteli hii ulikuwa wa
kielektroniki.Gari linapofika
getini tayari linakuwa
limeonekana na kukaguliwa
kama lina silaha
ndani,mlipuko au kitu
kingine chochote cha hatari
na baadaya ukaguzi geti
hifunguliwa na gari huingia
ndani.Endapo gari litakutwa
na tatizo lolote geti
halitafunguka na kengele
maalum hulia kuwapa
taarifa kikosi cha walinzi
ambao wana sehemu yao
maalum ndani ya hoteli.
Baada ya kufika getini
walitumia dakika moja gari
likakagulia kisha geti
likafunguliwa wakaingia
ndani moja kwa moja
wakaelekea katika
maegesho.Devotha
akafungua sehemu ya siri
ndani ya gari lake
anakohifadhi silaha na
ambapo si rahisi kuonekana
katika mitambo ya usalama
akatoa bastora mbili
zilizofungwa viwambo vya
sauti akampatia moja
Austin.Akachukua vifaa
vingine pamoja na kirusi kile
kilichokuwa katika chupa
ndogo inayofanana na chupa
za uturi akaviweka katika
mkoba wake
“Sasa tuelekee
ndani.Ninaifahamu hoteli hii
vyema na hata badhi ya
wafanyakazi wa hapa wengi
wananifahamu kutokana na
kuja mara kwa mara.Kabla
ya kuachia kirusi nitakupigia
simu halafu utaelekea
maliwato kule utavaa maski
kujikinga na hewa yenye
kirusi hicho”akasema
Devotha wakashuka na
kuelekea ndani ya hoteli.
Mara tu walipoingia
ndani ya hoteli Devotha
akasalimiwa na baadhi ya
wafanyakazi waliomfahamu
kisha wakaenda kuchukua
meza wakakaa na kuagiza
chakula.Watu walikuwa
wachache ndani ya hoteli hii
ni kutokana n gharama za
juu sana za hoteli hii ndiyo
maana inajulikana kama
hoteli ya mabilionea.Chakula
kililetwa wakaanza kula
wakivuta muda kusubiri
muda wa kuanza kikao
ufike.Wakati wakiendelea na
chakula simu ya Devotha
ikaita alikuwa ni Mathew
“Tayari nimekwisha
andaa gari kubwa la
wagonjwa ninawasubiri
ninyi” akasema Mathew
“Sisi tayari tunasubiri
muda wa kuanza kikao ufike
na kwa mujibu wa saa yangu
zimebaki dakika
chache.Nitajulisha kila kitu
kitakapokuwa tayari”
akasema Devotha na kukata
simu akaitazama yake
Muda ule alioambiwa
Zulfa wa kuanza kikao
ulipofika Devotha akachukua
mkoba wake na kuinuka pale
mezani kama vile anaelekea
upande wa pili lakini
akakunja kona na kufuata
ujia uliokuwa upande wa
kulia akakutana na mlango
wa kioo na ndani yake
kulikuwa na mtu mmoja
akipata chakula huku
akiyaelekeza macho katika
kompyuta yake.Devotha
akagonga mlango na Yule
jamaa akainuka haraka
akamfuata
“Nikusaidie nini
mama?akauliza Yule jamaa
aliyevaa suruali nyeusi na
shati zito jeupe lenye nembo
ya Mellisa group.
“Samahani nimepotea na
kujikuta nimefika
hapa.Natafuta njia ya
kwenda juu sitaki kutumia
lifti
“Rudi ulikotoka
utakutana na kibao
kimeelekez…………..” kabla
hajamaliza maelekezo yake
Devotha alichomoa bastora
kutoka katika koti lake na
kumtandika risasi mbili Yule
jamaa akaangukia
ndani.Devotha akageuka
kutazama kama kuna mtu
lakini alikuwa peke yake
haraka haraka akaingia
ndani na kumvuta Yule
jamaa akamficha chini ya
meza halafu akachukua simu
na kumpigia Austin
akamtaka aelekee maliwato
kwani muda wowote
angeweza kuingiza kirusi
kile katika hewa.Bila
kupoteza muda akaufungua
mlango mwingine wa
chumba na kuingia katika
mashine ya kuzalisha hewa
safi na kuisambaza katika
hoteli.Akatafuta sehemu
nzuri akavaa mask na
kumpigia simu Austin kuwa
avae mask halafu akatoa kile
kichupa chenye kirusi
akang’oa kifuniko na kirusi
kile kikaanza kutoka ndani
ya chupa kwa kasi na
kuingia katika
hewa.Alipomaliza akaelekeza
macho katika saa akihesabu
dakika baada ya dakika tano
akampigia simu Mathew
“Tayari tumemaliza kazi
unaweza ukaja” akasema
Devotha kisha akazima
mtambo ule wa kupeleka
hewa ili kuacha hewa ile
yenye kirusi isambae
akatoka mle ndani akaelekea
katika ukumbi wa
chakula.Yalikuwa ni mambo
ya kushangaza sana kwani
watu wachache waliokuwemo
mle ukumbini walikuwa
wamelalia meza zao kana
kwamba wamekufa lakini hii
ni baada ya kuvuta hewa
yenye kirusi.Moja kwa moja
akaelekea jikoni ambako
alikuta hali ile ile akazima
majiko ili kuzuia ajali ya
moto isitokee..
Devotha akamjulisha
Austin kila kitu
tayari,Austin akatoka
maliwato akamfuata
“I’ve never seen
something like this.Hoteli
yote wamelala usingizi ndani
ya kipindi hiki kifupi?Austin
akashangaa
“C’mon Austin we have
job to do.Follow me! Akasema
Devotha wakakimbia
kuelekea ulipo ukumbi
ambao Zulfa alielekezwa.Nje
ya ukumbi ule walikuta
walinzi wawili wakiwa
wamekaa chini wamepitiwa
na usingizi.Kwa haraka
haraka ungeweza kudhani
watu wale wamekufa lakini
walikuwa wamelala
“Ni hapa” akasema
Devotha na kukiminya kitasa
cha mlango ulikuwa
umefungwa kwa
ndani.Austin akaurukia teke
mlango ukafunguka
wakaingia ndani ya chumba
kile ambamo kulikuwa na
watu kumi na tano na wote
walikuwa wamelala usingizi.
“Hurry up.We have to
collect
everything.Kompyuta,simu
na kila walichonacho
ambacho kinaweza kusaidia”
akasema Devotha wakaanza
mara moja zoezi la
kukusanya kila kitu
kilichokuwa mezani mara
Devotha akastuka baada ya
kumuinua kichwa mmoja wa
watu waliokuwa wamelalia
meza
“This is unbelievable !!
akasema kwa sauti na
kumstua Austin ambaye
naye akainua kichwa
kutazama kilichomstua
Devotha naye akajikuta
akiupatw ana mshangao
mkubwa
“Waziri mkuu!! Ni yeye
kweli au ni mtu aliyefanana
naye?akauliza Austin
“Ni yeye mwenyewe”
akasema Devotha huku
akimpekua na kuchukua
simu yake akaitenga tofauti
na zile za wengine
Haraka haraka Devotha
akampigia simu Mathew
“Mathew umefika wapi?
“Tayari ninapita hapa
getini wewe uko
wapi?akauliza Mathew na
Devotha akampa maelekezo
mahala walipo.Mathew na
Dr Hiran wakiwa wamevaa
makoti meupe pamoja na
vifaa vya kujikinga na hewa
ile yenye kirusi wakashuka
garini wakiwa na machela na
kukimbia kuelekea mahala
waliko akina Devotha
wakaingia ndani
“Devotha haya ni
maajabu ya karne.Are you
sure they’ll be fine?Mathew
akauliza
“They’re fine.Wote
wataamka” akasema
Devotha na kumfanyia
ishara Mathew atazame
katika kiti na Mathew
akapatwa na mshangao
mkubwa
“Waziri mkuu ?! What is
he doing here?akauliza
“Tumemkuta humu
anaonekana ndiye aliyekuwa
mwenyekiti wa kikao
hiki,atatueleza alichokuwa
anakifanya humu ndani ni
kitu gani atakapoamka”
akasema Devotha na kazi ya
kuwaondoa wale watu mle
ndani ikaanza mara
moja.Mathew akamuinua
waziri mkuu akamuweka
katika kitanda cha
magurudumu Dr Hiran na
Devotha wakasukuma
kitanda kile kumtoa
nje.Mathew akamuinua mtu
mwingine akamuweka
begani Austin naye akafanya
hivyo hivyo na kuelekea
kwenye lifti wakashuka chini
na kuwapakia watu wale
ndani ya gari.Devotha na Dr
Hiran wakabaki wakiwalinda
watu wale wakati Mathew na
Austin wakiendelea na zoezi
la kuwatoa wengine ndani ya
kile chumba.Walitumia
dakika ishirini kumaliza
zoezi la kuwaondoa watu
wale kumi na tano
waliokuwemo mle ndani ya
chumba na kuchukua kila
kitu walichokuwa nacho na
bila kupoteza muda
wakaondoka kwa kasi kubwa
huku gari lile likipiga
king’ora na kuachiwa njia
barabarani.Austin
aliwafuata nyuma akiwa na
gari la Devotha
“Simu ya waziri mkuu hii
hapa” Devotha akamkabidhi
Mathew
“Devotha kitu
ulichokifanya leo sijawahi
kukiona sehemu yoyote hata
katika filamu.Bado najiuliza
ni kweli kile
nilichokishuhudia ama ni
mazingaombwe? Akauliza
Mathew na Devotha
akatabasamu
“Hiki ni kirusi kipya
kimetengenezwa na
kinatumika kama silaha japo
kwa siri mno.Kirusi kama
hiki hakiwezi kutangazwa
wala kuruhusiwa kutumika
kwani kinaweza kusababisha
maafa makubwa
duniani.Kinaweza kutumika
katika uhalifu mkubwa na
hata mauaji ndiyo maana ni
moja kati ya vitu vya siri
kubwa katika jeshi la
Marekani.Wamekuwa
wanatumia kirusi hiki katika
kuwatafuta magaidi ambao
wamekuwa wakijificha
milimani”
“Wewe ulikipata vipi?
Mathew akauliza
“Niliwahi kufanya kazi
katika idara ya kupambana
na ugaidi ya Marekani na
ndiko nilikopata kirusi hiki
na ni siri yangu
kubwa.Hawataki
teknolojiayao
ijulikane”akasema Devotha
na Mathew akayaelekeza
macho yake kwa waziri
mkuu.
“Ulikuwa sahihi
ulipoingiwa na shaka
kuhusiana na waziri
mkuu.Bado siamini kama
kiongozi mkubwa kama huyu
ana mahusiano na
magaidi.Kumbe Edger Kaka
hakuwa peke yake,mtandao
wao ni mpana sana na ndiyo
maana hawakutaka Edger
aufahamu.”akasema Mathew
“Mathew mimi tayari
nilikwisha ingiwa na wasi
wasi kwanza kwa kitendo
chake cha kuamua kuungana
na wananchi katika
maandamano.Ni kitendo cha
kushangaza sana.Pili
nilistuka baada ya kumuona
akiwa karibu na Yule mtu
ambaye nina uhakika ni
Nazil jalib ambaye ni gaidi
na muuaji mkubwa.Baada ya
kumkuta huku katika kikao
na watu wa IS sina shaka
kabisa kuwa waziri mkuu wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania anashirikiana na
magaidi.Kwa nini kiongozi
mkubwa kama huyu
aliyebeba dhamana kubwa
kabisa akafanya hivi?Nini
anakitafuta? Au alitumwa na
Rais kuja kufanya
majadiliano na hawa magaidi
namna ya kufanya
makabidhiano? kauliza
Devotha ambaye alikuwa
anaendelea na zoezi la
kuwafunga watu wale
mikono kwa pingu za plastiki
“Tayari nimefahamu
anachokitafuta.Ni
madaraka.Ameisaliti serikali
na kujiunga na wananchi
kwa lengo la kutafuta
umaarufu.Anachochea
wananchi waichukie serikali
yao na yeye aonekane shujaa
kwa kushiriki nao katika
maandamano.Kwa kitendo
hicho anajitengenezea
mazingira ya kuwania nafasi
ya urais na kama akishinda
huo utakuwa ni ushindi kwa
IS.Katika kutafuta
madaraka wanasiasa wako
tayari kufanya jambo lolote
lile ili waweze kutimiza
malengo yao.Wapo vibaraka
wa mabeberu ambao wako
tayari kuweka rehani nchi na
rasilimali zake kwa
mabeberu ili wasaidiwe
kupata madaraka
makubwa.Lakini mwisho
wake umefika na mipango
yake haitaweza
kufaniki………..”akanyamaza
Mathew baada ya simu ya
waziri mkuu aliyokuwa
ameiweka mfukoni
kutetema.Mathew akaitoa
mfukoni na kutazama
mpigaji jina liliandika Nazil.
“Nazil ?!! Mathew
akashangaa na kuipokea ile
simu akaiweka sikioni
“Mheshimiwa tayari
nimefika na nimetoa
maelekezo kwa Fahad.Mtoto
atakayefuata ni mwanao
lakini itakuwa ni kwa
kutishia tu hatauawa hivyo
usiwe na wasi wasi.Fahad
yuko mtandaoni kwa
sasa”akasema Nazil na
Mathew akakata simu halafu
akamuandikia ujumbe mfupi
“Kila kitu kiende kama
kilivyopangwa mimi niko
kwenye kikao”akautuma
ujumbe ule halafu
akamgeukia Devotha
“Devotha we have the
kids vile vile sina shaka tena
waziri mkuu anashirikiana
na magaidi” akasema
Mathew
“Mtu aliyempigia simu
waziri mkuu sasa hivi jina
lake limeandikwa Nazil jina
ambalo linafanana na yule
mtu ambaye ulimuona katika
maandamano akiwa karibu
na waziri mkuu.Nazil
alikuwa anamjulisha waziri
mkuu kwamba tayari
amefikisha ujumbe kwa
Fahad.Inaonekana huyu
Fahad ndiye ambaye
anafanya mauaji ya watoto
waliowateka.Kwa mujibu wa
maelezo yake inaonekana
waziri mkuu alimtuma
kupeleka ujumbe kwa Fahad
akimtaka atishie kumuua
mtoto wake ambaye ni
mmoja wa mabinti
waliotekwa.Nadhani hii ni
kutaka kumpa shinikizo
zaidi Rais kwani hawezi
kukubali kuona mtoto wa
waziri mkuu wake
akichinjwa hivyo atafanya
kila awezalo kuhakikisha
anamuokoa.Nadhani lengo la
kumtumia mwanae ni hilo”
akasema Mathew.Devotha
kwa kutumia simu yake
alitazama mtandaoni
ambako kulirushwa video
ambayo watekaji wa watoto
walitishia kumuua mtoto wa
waziri mkuu.
“Ni kweli.Imerushwa
video nyingine wakitishia
kuua mtoto wa waziri
mkuu.Kumbe suala zima la
kuteka watoto wale wa shule
limeratibiwa na waziri
mkuu.Anathubutuje
kumfanyai mwanae kitu
kama hiki? akasema Devotha
na mara mtu wa kwanza
akapiga chafya na kufumbua
macho
“Wameanza
kuamka”akasema Mathew
“I told you” akasema
Devotha akitabasamu.
Ndani ya dakika tano
tayari wote walikuwa
wameamka na walishangaa
baada ya kujikuta wakiwa
wamefungwa mikono na
wakiwa wameelekezewa
bastora
“Who are you
people?akauliza waziri mkuu
baada ya kuzinduka na
kutoka usingizini.Alijaribu
kujitikisa lakini alikuwa
amefungwa mikono kwa
nyuma
“Nifungueni mikono
yangu ng’ombe nyie.!!
akafoka waziri mkuu.
“Mimi ni waziri mkuu wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania hiki
mnachokifanya ni kosa
kubwa mno na ninawaambia
wazi kwamba adhabu yake ni
kubwa mno.This is a kidnap!!
Akaendelea kufoka waziri
mkuu lakini
hakujibiwa.Devotha
akachukua gundi ya nailoni
na kuanza kuwabandika
midomoni ili wasiweze
kupiga kelele
Walichukua muda mfupi
kufika katika makazi yao
kwani gari lile la wagonjwa
liliachiwa njia ya kupita
barabarani.Baada ya
kuwasili wote wakashushwa
wakaingizwa ndani na
kujazwa katika chumba
kimoja
“Guys natamani
niwashukuru kwa kazi hii
kubwa lakini bado tunayo
kazi ya kufanya mbele
yetu.We need to find the
girsl” akasema Mathew na
kuwaeleza kile alichokipata
katika simu ya waziri
mkuu.Akampatia simu ile
Ruby na kumtaka atafute
mahala ambako Nazil
alikuwepo wakati akipiga ile
simu.Haraka haraka Ruby
akaanza kucheza na
kompyuta ili kufahamu
mahala alipo Nazil
“Tukifanikiwa kupata
mahala alipo Nazil hapo
ndipo walipo wasichana
waliotekwa” akasema
Mathew na wote wakawa
kmya wakimsubiri Ruby
awape jibu.Baada ya dakika
tatu Ruby akasema
“Nimempata.Alikuwa
hapa wakati akipiga simu”
akasema Ruby na
kuwaonyesha katika ramani
mahala alipokuwa Nazil
wakati akimpigia simu
waziri mkuu.
“Thank you Ruby.Guys
mahala hapo alipo Naziri
ndipo walipo
watoto.Tunakwenda
kuwaokoa watoto lakini
tutahitaji msaada.Hatuwezi
peke yetu.Hawa watu lazima
watakuwa wamejiandaa
vilivyo kiulinzi kwani
wanajua nguvu kubwa
inatumika kuwasaka watoto
wale.Austin we need your
team” akasema Mathew
“Nakubaliana nawe
Mathew kwamba tunahitaji
msaada lakini kwa sasa
mimi si kiongozi tena wa
kikosi kile baada ya kupuuza
agizo la Rais”
“Usihofu I’m going to talk
to president”
“President?! Devotha
akashangaa
“Yes”
“He betrayed
us.Hatuwezi kumuamini
tena”
“Tunahitaji timu ya watu
kutusaidia kupambana na
magaidi ni yeye mwenye
uwezo wa kutusaidia kupata
timu tunayoihitaji” akasema
Mathew kisha akachukua
simu yake ya zamani
akaiwasha na kumpigia Rais.
“What do you
want?akauliza Dr Evans kwa
ukali baada ya kupokea simu
“Mheshimiwa Rais
nahitaji msaada wako”
“You go to hell Mathew !!
Mambie na Aus………….”
“Mheshimiwa Rais
naomba unisikilize
kwanza.Tayari tumefahamu
mahala walipo watoto
waliotekwa” akasema Austin
na Dr Evans akasikika
akishusha pumzi
“Are you sure?akauliza
Dr Evans
“Ndiyo mheshimiwa Rais
tuna uhakika”
“Ni wapi?
“Mheshimiwa Rais
ninahitaji kikosi cha
operesheni maalum
kitusaidie tuweze
kuwakomboa watoto
hao.Mahala walipo
tunaamini magaidi
watakuwa wamejihami
vilivyo kwa silaha hivyo
tunahitaji nguvu ya kutosha”
“Mathew I don’t kno
what to say …” akasema Dr
Evans na kuvuta pumzi
ndefu
“Mathew niko tayari
kuwasaidia kila
mnachokihitaji.Uko na
Austin hapo karibu?Nipe
nizungumze naye”akasema
Dr Evans na Mathew
akampa Austin simu
“Mheshimiwa Rais”
akasema Austin
“Austin nataka utumie
kikosi chako katika
kuwakomboa wasichana hao
waliotekwa.Tusameheane
katika yale yaliyotokea”
akasema Dr Evans
“Nashukuru mheshimiwa
Rais” akasema Austin na
kumrejeshea simu Mathew
“Mathew nimekwisha
mpa maelekezo Austin
mtatumia kikosi chake na
hakikisheni mmewakomboa
wasichana wote waliotekwa”
akasema Dr Evans
“Sawa mheshimiwa
Rais”akasema Mathew na
kukata simu.Bila kupoteza
muda Austin akapiga simu
kikosini na kutoa maelekezo
wajiandae.Kulitokea
mabishano kidogo kati yake
na msaidizi wake hadi pale
alipomthibitishia kwamba
lile ni agizo la Rais.
Ofisi ya muda ililazimu
kuhama kutoka katika
nyumba ile na kurejea katika
kambi ya kikosi cha
operesheni maalum.Waziri
mkuu na wenzake
wakapaiwa katika gari.Edger
akapakiwa katka buti ya gari
la Devotha kisha mke wa
balozi na Zulfa aliyekuwa
analindwa na Gosu Gosu
wakaingia katika gari la
Devotha wakaondoka mahala
pale kuelekea katika kambi
ya kikosi cha operesheni
maalum.
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 19
“Mike team,Oscar team
tunakaribia kufika sehemu
lengwa.Mmefika wapi ?
Mathew Mulumbi akauliza
wakiwa ndani ya gari
wakikaribia kufika eneo la
magetini wakiifuata nyumba
ambayo wanaamini ndiko
waliko watoto waliotekwa
nyara.Ulikuwa ni msafara
wa gari tatu ambazo ndani
yake zilijaza wanajeshi
kutoka kikosi cha jeshi cha
operesheni maalum
“Oscar team,Mike team
tumekaribia sana kufika
sehemu hiyo ndani ya dakika
chache tutakuwa tumefika
hapo” akasema Austin
ambaye alikuwa anaongoza
kikosi kilichokuwa katika
helkopta
“Main tower what’s your
status?akauliza Mathew
“Kwa kuhesabu
ninawaona watu zaidi ya
kumi wakiwa nje ya nyumba
hiyo wakiwa na
bunduki.Saba wako upande
wa mbele ya nyumba na
wengine wako upande wa
nyuma”akasema kamanda
kutoka katika ofisi kuu ya
kuongozea operesheni ambao
walikuwa wanafuatilia
kinachoendelea kupitia
satelaiti maalum
Ndani ya nyumba ile
katika chumba ambacho
magaidi walikuwa
wanatumia kurushia
matangazo yao mtandaoni
namna wanavyowachinja
wanafunzi
waliowateka,mwanafunzi
mmoja alikuwa amefungwa
mikono kwa nyuma akiwa
wamepigishwa magoti.Fahad
akiwa amevaa kofia ya
kumziba asionekane sura
akajitokeza na kamera
ikawashwa
“Ndugu watanzania
nimekuja tena.Bado Rais
wenu amegoma kutekeleza
matakwa yetu,ameendelea
kuwa na kiburi na sisi
hatuna namna nyingine zaidi
ya kuendelea kuwachinja
watoto tuliowateka.Hapa
ninaye mtoto wa waziri
mkuu ambaye naye
tutamchinja kama
tulivyofanya kwa
wengine.Niliwapa muda Rais
na serikali yake ili
wamuokoe mtoto wa kiongozi
mwenzao lakini wamepuuza
hivyo tunakwenda kuondoa
kichwa cha mtoto
huyu.Baada ya saa moja
tutaongeza idadi hadi kufika
saa sita usiku wa leo lazima
watoto wote tuliowateka
wawe wamemalizika na hapo
tutaufungua ukurasa
mpya.Tayari tumekwisha
jipanga na tutaigeuza
Tanzania nyekundu kwa
damu hadi pal…….”
Akanyamaza baada ya
kusikika mtikisiko kutokana
na milio ya helkopta.
“Nini hicho?akauliza
akiwa na wasiwasi
“Kata kamera!! Akasema
kwa sauti kubwa halafu
akavua kofia
Milio ya risasi ilianza
kusikika nje ya ile nyumba.
Helkopta mbili kutoka
katika kikosi anachokiongoza
Austin zilifika katika
nyumba ile na kuanza
kushambulia kwa risasi
walinzi waliokuwa nje na
silaha wakilinda.Wakati
mashambulizi yakiendelea
wanajeshi wengine walikuwa
wanashuka toka ndani ya
helkopta kwa kamba.Risasi
ya kwanza ilipolia iliwasha
taa ya kijani kwa akina
Mathew wakashuka
magarini na mmoja
akapanda geti hadi ndani
akalifungua wakaingia.
Milio ile ya helkopta
iliwastua waliokuwa ndani
wakaanza kutoka
wakikimbia kuja kushuhudia
kinachoendelea nje lakini
walikutana na timu ya akina
Mathew ambao walikuwa
wanaelekea ndani na
kuwamaliza mmoja mmoja
“Nazil
tumevamiwa.Tayari
wanafahamu mahala
tulipo.You know what to do”
Fahad akamwambia Nazil
aliyeonekana
kuchanganyikiwa.
“Wewe na wewe nendeni
mkawalete watoto wote hapa
we’ll die with them !!
akasema Fahad lakini wale
jamaa aliowatuma
hawakuweza kuinua hata
hatua moja kwani tayari
mvua ya risasi ilianza
kunyesha.Nazil aliyepigwa
risasi ya bega la kushoto
akachomoa bomu kutoka
katika kizibao alichovaa na
kung’oa funguo kisha
akalirusha.
“Gurunetiiiii !! Mathew
akawajulisha wenzake na
kufanya kitendo ambacho
wote
hawakukitarajia.Aliitupa
chini bunduki yake akaruka
kulidaka bomu lile kabla
halijagusa chini kisha
akasimama na kutoka mbio
mle ndani akaenda katika
dirisha akapiga ngumi kioo
na kulitupa bomu lile nje
likalipuka akasimama
akihema huku akivuja jasho
mwili mzima.Kilikuwa ni
kitendo cha hatari sana.
Baada ya kunusurika
kulipukiwa na bomu,Gosu
Gosu akaliendea panga
ambalo magaidi walikuwa
wanalitumia kuwakatia
vichwa wasichana
waliowateka akamfuata
Nazil
“Mliwachinja watoto
wetu kama kuku sasa ni
zamu yenu ! akasema kwa
hasira na kuliinua panga juu
na kulishusha kwa nguvu
akatenganisha kichwa cha
Nazil na kiwili wili.
“Haya ndiyomalipo ya
uovu wenu kenge nyie !!
Mvua ya risasi ilikoma
baada ya magaidi wote
kuanguka chini.Walikuwa
wamechakazwa vibaya sana
kwa risasi.
Tayari nyumba yote
ilikuwa
imedhibitiwa.Mathew akatoa
picha mfukoni akampatia
Gosu Gosu
“Find this man” akasema
Mathew na mara akaingia
mmoja wa makamanda
“Mr Mathew Mulumbi
tumezunguka nyumba yote
na hakuna tena gaidi
mwingine.Wote
wamejeruhiwa au
kuuawa.Habari njema ni
kwamba tayari tumewapata
wasichana wote waliobaki
waliokuwa wanashikiliwa
mateka pamojana walimu
wao”
“Ahsante sana
Kamanda.Good job” akasema
Mathew
“Mike team,this is Oscar
team.Tumefanikiwa
kuwapata wasichana
waliotekwa.Ninarudia
tumewapata wasichana
waliotekwa” akasema
Mathew akiwajulisha akina
Austin halafu akachukua
simu akampigia Rais Dr
Evans
“Mathew nini
kinaendelea?akauliza Dr
Evans akiwa na wasi wasi
“Misheni imekamilika
mheshimiwa Rais na
tumewapata wasichana wote
waliotekwa pamoja na miili
mine ya wale waliouawa”
“Ouh Mungu wangu !
akasema Dr Evans na kukaa
kimya kwa muda
“Mheshimiwa Rais”
akaita Mathew
“Mathew nimeishiwa
maneno.Sijui niseme nini”
“Mheshimiwa Rais
tunawachukua watoto hawa
na kuwapeleka katika kambi
ya kikosi cha operesheni
maalum ambako
watapumzika kabla ya ratiba
nyingine kuendelea.Mr
President I need to see
you.Kuna mambo mazito
ambayo unatakiwa
uyafahamu.Vile vile jeshi la
polisi wanatakiwa kufika
hapa kuchukua miili hii ya
magaidi na kuifanyia
uchunguzi nyumba hii”
akasema Mathew
“Mathew mtakaporejea
kambini nifahamisheni ili
niweze kufika huko mara
moja kuja kuwapa pole
watoto hao.Kwa sasa
natakiwa kulihutubia taifa ili
kuwajulisha kwamba watoto
waliotekwa na magaidi
wamekombolewa ili kutuliza
hali ya wasiwasi mkubwa
iliyotanda” akasema Rais na
kuagana na Mathew.
“Mathew Mulumbi
ahsante sana.Umefanya
kitendo cha kishujaa mno
kudaka bomu lile.Umetuokoa
wote ndani ya chumba
vinginevyo tungekufa wote”
akasema mmoja wa
wanajeshi wa kikosi kile na
kumpa mkono Mathew
kumpongeza.
“Mathew ! akaita Gosu
Gosu
“Nimempata yule mtu
wetu ni huyu hapa lakini
amepigwa risasi amefariki
dunia” akasema Gosu Gosu
na kumpatia Mathew simu
ya Yule jamaa.
“We needed him
alive.Lakini hakuna ubaya
kwani tumefanikiwa
kumfikia na kumuua”
akasema Mathew
“Mathew Yule mtu
aliyerusha bomu ukalidaka
ni Yule ambaye Devotha
alimuona katika
maandamano na akamtilia
shaka.Ni gaidi wa muda
mrefu na kwa mujibu wa
Devotha alikuwa anajiita
mtu asiyeonekana lakini leo
ameonekana na umekuwa ni
mwisho wake”
“Good job Gosu
Gosu”akasema Mathew
Wasichana wale
walipakiwa katika helkopta
na wengine katika magari
kisha wakaondoka kurejea
kambini.
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 20
Matangazo katika
runinga na redio ya taifa
yalikatishwa ghafla na
wimbo wa taifa kupigwa.Rais
wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania akajitokeza
“Ndugu watanzania
wenzangu,nimejitokeza
kwenu muda huu kuwapeni
taarifa kwamba muda mfupi
uliopita,vijana wetu hodari
wakishirikiana na kikosi cha
jeshi cha operesheni maalum
wamefanikiwa kuvamia
nyumba ambayo magaidi
waliitumia kuwaficha
wasichana waliowateka na
kufanya mauaji ya
kikatili.Katika uvamizi huo
vijana wetu shupavu
wamefanikiwa kuwaua
magaidi wote na
kuwakomboa wasichana
sitini na mbili na walimu
wao watatu pia miili minne
ya wasichana wengine
waliouawa na magaidi
imepatikana.Ndugu
watanzania huu ni ushindi
mkubwa tumeupata dhidi ya
magaidi hawa waliojaribu
kutaka kuvuruga amani yetu
Ninawahakikishia
kwamba tutausaka mtandao
wote wa magaidi hapa nchini
na kumkamata hadi gaidi wa
mwisho.Ninawaomba
tuendelee kuwa watulivu
wakati vyombo husika
vikiendelea kutekeleza
majukumu yake.Tutaendelea
kuwajulisha kila
kinachoendelea katika
sakata hili.
Kwa wazazi ambao
watoto wao wamekombolewa
mtajulishwa wakati gani
watoto wenu watarejeshwa
kwenu na kwa wale ambao
watoto wao wameuawa
serikali itagharamia mazishi
yao.Mtaendelea kupewa
taarifa zaidi za kile
kinachoendelea
Mungu ibariki Tanzania
Ahsanteni kwa kunisikiliza
Ilikuwa ni hotuba fupi ya
Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania
akilijulisha taifa kuhusiana
na kukombolewa kwa
wasichana waliotekwa nyara
na magaidi.
“Sijui nitawatazama vipi
vijana wale machoni kwa
jambo nililowafanyia la
kuwageuka na kutaka
kumkabidhi Edger Kaka kwa
magaidi.Sikuwa nimepanga
kufanya hivyo bali yalikuwa
ni mawazo ya waziri mkuu
ambayo niliona ni mazuri na
kuamua kuyafuata.Nilikosea
sana kumshirikisha waziri
mkuu jambo hili kubwa
halafu akanigeuka na
kuungana na
waandamanaji.Mpaka sasa
sifahamu nini hasa ilikuwa
dhamira yake ya kwa kitendo
kile alichokifanya.Kwa
alichokifanya ameonyesha
kutokuiamini serikali
ambayo yeye ni sehemu yake
na amepoteza sifa za kuwa
waziri mkuu.Ngoja kwanza
nikakutane na watoto wale
waliokombolewa nataka
nijue kuhusu Olivia na
Coletha” akawaza Dr Evans
na kuelekeza helkopta ya
Rais iandaliwe
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 21
Kikosi kilichokwenda
kuwakomboa wasichana
waliotekwa kilirejea kambini
na wasichana wote
wakakusanywa katika bwalo
la chakula ambako walianza
kupewa huduma mbali za
matibabu kwa wale
waliokuwa na majeraha na
vile vile wakapewa chakula
chepesi
Wakati wakiendelea
kupongezana kwa ushindi
ule mkubwa helkopta ya Rais
ikaonekana angani na
ikaelekezwa sehemu ya
kutua.Mara tu Rais alipotua
akapokelewa na Austin
January mkuu wa kikosi kile
na kuelekea moja kwa moja
ofisini kwake
“Karibu sana
mheshimiwa Rais” akasema
Austin
“Ahsante sana
Austin.Mathew Mulumbi
yuko wapi?
“Alikuwa anaangaliwa na
daktari amepata majeraha
madogo”
“Please call him.I need to
see you both” akasema Dr
Evans na Austin akapiga
simu katika hospitali ya
kambi na hazikupita dakika
tano Mathew akafika
“Mheshimiwa Rais”
akasema Mathew
“Mathew na Austin sipati
maneno mazuri ya
kuwaambia lakini kabla
sijasema ahsante nataka
niwaombe sana msamaha
kwa yale yote
niliyowatendea.Nitawaeleza
kila kitu pale tutakapokuwa
tumepata muda lakini toka
ndani ya moyo wangu I’m
deeply sorry” akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa Rais yale
yamekwisha pita.Sisi ni
binadamu na wote
tunakosea.Kwa sasa
tutazame ya mbele.Bado
tunayo kazi ya
kufanya.Hatujafika mwisho”
akasema Mathew na
kumueleza Rais namna
operesheni ile ilivyofanyika
hadi wakafanikiwa
kuwakomboa mateka.Austin
na Mathew wakamuongoza
Rais kuelekea katika bwalo
la chakula kuonana na
wasichana wale
waliokombolewa.Baada ya
kuwasalimu akaenda pia
katika chumba cha maiti
pale kambini na kuiona miili
ya wasichana wale
waliouawa na magaidi kisha
akawageukia akina Mathew
“Kazi nzuri sana
vijana.Ahsanteni kwa
kuwafyekelea mbali makatili
hawa ambao wamekatisha
uhai wa wasichana wadogo
wasio na hatia”
“Mheshimiwa Rais kuna
jambo lingine ambalo
unatakiwa ulishuhudie kwa
macho yako” akasema
Mathew na kumuongoza Dr
Evans hadi katika chumba
walimowahifadhi waziri
mkuu na wenzake.
“Huyu ni waziri mkuu wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania.Anafanya nini
hapa? Akauliza Dr Evans
alipatwa na mshangao
mkubwa
“Mheshimiwa Rais nchi
hii imebarikiwa kupata
viongozi wazuri lakini wapo
viongozi wachache ambao
wako tayari kufanya
chochote ili kutimiza
matakwa yao ya
kisiasa.Mbele yako ni waziri
mkuu wa Tanzania ambaye
tumemkuta katika mkutano
na watu wa IS.Mpango huu
wa kuwateka wanafunzi
umepangwa na magaidi
pamoja na huyu waziri mkuu
na tunao ushahidi wote
kupitia simu yake ambayo
amekuwa akiitumia
kuwasiliana na
magaidi.Mmoja wa
mag…………..” Mathew
hakumaliza kutoa maelezo
kwa Rais ghafla Dr Evans
akachomoka na kumfuata
waziri mkuu akaanza
kumporomoshea makonde
mazito.Mathew na Austin
wakamshika
“Sasa nimepata
picha.Huyu mtu ndiye
aliyenipa wazo la
kumkabidhi Edger Kaka kwa
magaidi.Kumbe ni
mwenzao.Kwa nini
sikulitambuahili
mapema?Nimefanya naye
kazi kwa muda mrefu
sikujua kama niko na nyoka
mwenye sumu !! akasema
DrEvans na kutaka
kumfuata tena kwenda
kumuadhibu lakini akina
Mathew wakamzuia
“Imetosha mheshimiwa
Rais ataadhibiwa na sheria”
akasema Mathew
“Kwanza alikuwa Edger
Kaka na sasa ni kiongozi
mkubwa kabisa naye
anashirikiana na
magaidi.Nani nimuamini?
Akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa Rais hawa
wengine wote unaowaona
humu ni washirika wa
mtandao wa IS.Tunaamini
hawa ni baadhi tu lazima
wapo wengine kwani
inaonekana tayari IS
wamekwisha jenga mtandao
mkubwa hapa nchini.Vyombo
vinavyohusika vitachunguza
na kuubaini mtandao wote
wa IS hapa
nchini.Tumechukua simu zao
kompyuta na kila kifaa chao
cha mawasiliano
tutavikabidhi kwa chombo
kitakachokuwa
kinalishughulikia suala hili”
akasema Mathew kisha
akamchukua Rais na
kumpeleka katika chumba
kingine alimokuwamo Edger
Kaka.
“Mhshimiwa Rais huyu
ni Edger Kaka”akasema
Mathew
“Hallow Edger” akasema
Dr Evans
“Hello”
“Nimefurahi kukuona
tena”
“Me too Mr President”
Hakukuwa na maongezi
ndani ya kile chumba
Mathew akamchukua
wakaenda katika hospitali ya
kikosi akamuonyesha Zulfa
ambaye naye ni mfuasi wa IS
halafu akampeleka kwa mke
wa balozi wa Israel
“Mama ahsante kwa
uvumilivu wako kwa muda
wote uliokaa na hawa
vijana.Jioni ya leo
utarejeshwa kwako lakini
kinachotakiwa ni kufuata
masharti utakayopewa”
akasema Dr Evans wakatoka
“Vijana mmefanya kazi
kubwa sana ambayo sijui
niwalipe nini.Hata hivyo
nataka kufahamu mipango
ya kuwatafuta akina Olivia
na Coletha”
“Kuna mtu mmoja
ambaye amekuwa akihusika
na utekaji anaitwa Fahad
ameuawa katika uvamizi na
kama tungeweza kumpata
huyo angetusaidia kufahamu
walipo Olivia na
Coletha.Itatulazimu
kuzungumza tena na Edger
Kaka ili atusaidie kutupa
taarifa zilizosaidia kuwapata
wasichana hawa na
atatusaidia pia kujua mahala
walipo Coletha na Olivia.”
akasema Mathew na
kumueleza Rais kile
ambacho walikuwa
wamekubaliana na Edger
Kaka kisha wakaelekea
katika sehemu ya kupumzika
viongozi na Edger Kaka
akaletwa mbele ya Rais
“Hallow Edger.Karibu
tena Dar es salaam karibu
tena Tanzania.Sikutegemea
kabisa kama tungeweza
kuonana lakini imetokea
tumekutana”
“Ahsante mheshimiwa
Rais” akasema Edger
“Edger tayari
tunafahamu kila kitu kuhusu
wewe na ndiyo maana
tukafanya kila juhudi ili
tuweze kukupata na sasa ni
wakati wa mimi na wewe
kuzungumza” akasema Dr
Evans na kunyamaza kidogo
halafu akaendelea
“Nilimpa ruhusa Mathew
Mulumbi ya kuzungumza
nawe kwa niaba yangu na
umemtajia vitu ambavyo
unavihitaji ili kuweza kutupa
taarifa tunazozihitaji sana
kuhusu mtandao wa kikundi
cha IS hapa
Tanzania.Mathew
amenikabidhi orodha ya vitu
ulivyoviorodhesha tukupatie
na tayari vimekwisha anza
kuvifanyia kazi mfano
nyumba tayari umeipata na
hivi vingine vinaendelea
kufanyiwa kazi na utavipata
vyote.Ninakupa nafasi
nyingine ya kuanza maisha
mapya.Ningeweza
kukufunga mahala katika
shimo ukaishi huko kwa
miaka yako yote au
ningeamua kukuteketeza
kabisa kwani kila mtu
anafahamu umekwisha kufa
lakini sitaki kufanya hivyo
nataka nikupe nafasi
nyingine ya kufurahia
maisha ila fursa hii
haitakuja hivi hivi you’ll
have to pay me
something.Nataka unipe
taarifa za mahala walipo
Coletha na Olivia
Themba.Nataka
kuwakomboa ili nimchukue
mwanangu na wewe
umchukue Olivia mkaishi
maisha mazuri yenye amani
mahala ulikochagua kwenda
kuishi” akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais
ninashukuru kwanza kwa
kuja kuniona na kunipa
nafasi nyingine ya kwenda
kuanza maisha
yangu.Natamani sana
ningekuwa na msaada zaidi
lakini nimekuwa ndani ya
chumba cha giza kwa miaka
mitatu na sijui chochote
kinachoendelea huku
nje.Sifahamu mahala walipo
mwanao na Olivia.I’m sorry
Mr President” akasema
Edger
“Edger hii ni nafasi ya
mwisho ya kutengeneza
maisha yako.Ukishindwa
kuitumia ni hiyari yako
lakini baada ya hapa
hakutakuwa na majadiliano
tena kwani utapelekwa
mahala ambako utateseka
hadi siku yako ya mwisho ya
maisha hapa duniani.Kwa
nini ukubali mateso
Edger?Hutaki kuishi maisha
mazuri sehemu salama
ambako hakuna
anayekufahamu huku ukiwa
na mwanamke unayempenda
Olivia Themba? Watu wako
wa IS hawana kumbu kumbu
tena nawe wamekwisha
kusahau ni wakati wako na
wewe kuwasahau ili
ukaendelee na maisha yako
hawana tena msaada
kwako.Tumia vyema fursa
hii uliyoipata kwani ukiamua
kuiacha utaijutia kwa
maisha yako yote” akasema
Dr Evans
“Edger ulikuwa mbunge
kijana mwenye maisha
marefu sana ya kisiasa na
sote tuliamini kwamba
utakuwa kiongozi mkubwa
mbeleni na wengi walikwisha
anza kukutabiria mambo
makubwa,kwa nini ukaamua
kujiunga na magaidi hao
wasio na huruma hata
chembe? Nini hasa ulikuwa
unakipata kutoka kwao?
Sitaki kulizungumzia sana
hilo ninaliweka pembeni
itabaki kuwa siri yetu sisi
tuliomo humu ndani ya hiki
chumba ninachotaka nisaidie
niweze kuwapata mwanangu
na Olivia Themba” akasema
Dr Evans na Edger
akainamisha kichwa
akafikiri kwa muda halafu
akaomba apewe kalamu na
karatasi akaandika namba
Fulani na kumpa Rais
“Sina hakika kama bado
zinatumika lakini jaribu
kupiga namba
hizo.Ukiulizwa jina watajie
namba W0023S12 kisha
utazungumza na Habiba
Jawad.Yawezekana yeye
anaweza akawa na taarifa za
mahala walipo Coletha na
Olivia”
“Ni nani huyu Habiba
Jawad?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa Rais piga
namba hizo na pengine
unaweza ukafahamu mahala
walpowatu wako.Sina
maelezo zaidi” akasema
Edger
“Mheshimiwa Rais
habiba Jawad ni mfadhili
mkuu wa kikundi cha IS na
ana ukaribu mkubwa na
Edger hata alipokuw
hospitali Israel alikwenda
kumtembelea nay eye ndiye
sababu ya Mossad kumteka
Edger” akasema Mathew
“Austin waambie watu
wako wafuatilie namba hii
aliyotoa Edger tufahamu
mahala alipo huyu
Habiba.”Dr Evans
akamwambia Austin lakini
Edger akaingilia kati
“You can’t trace that
number.Watajua
mnawafuatilia.Wana
teknolojia kubwa ya kuficha
mawasiliano yao.Ukijaribu
kufuatilia hiyo namba
unaweza ukawakosa watu
wako” akasema Edger na Dr
Evans akamtazama Mathew
“Do it Mr President”
akasema Mathew na Dr
Evans akapiga zile namba
simu ikaanza kuita.Kama
alivyokuwa amesema Edger
simu ilipokelewa na Dr
Evans akaulizwa jina lake
akataja namba zile alizopewa
na baada ya muda ikasikika
sauti nyingine ya mwanamke
“Hallow Seif”
“Hallow.Unazungumza
na Dr Evans Rais wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania.Nazungumza na
Habiba Jawad? akauliza Dr
Evans na ukimya ukapita
“Hallow! Akaita DrEvans
“Naamini Edger Kaka
ndiye aliyekupatia namba
hizi unipigie.Ninaomba
umuachie haraka sana ama
sivyo kutatokea umwagikaji
mkubwa sana wa damu hapo
Tanz……..” akasema Habiba
na Dr Evans akamkatisha
“Hakuna mnachoweza
kukifanya tena Habiba
Jawad,sehemu kubwa ya
mtandao wenu
tumewakamata na wengine
wameuawa na tunaendelea
kuwafuatilia wengine
waliosalia.Tunaye hadi
waziri mkuu ambaye
mlikuwa mnashirikiana
naye” akasema DrEvans na
ukimya mfupi ukapita
“Najua hujanipigia simu
kunieleza namna
mlivyofanya mauaji.Unataka
nini?Habiba Jawad akauliza
“Habiba pamoja na haya
yote yaliyotokea lakini bado
mimi na wewe tunaweza
kuzungumza tukafikia
makubaliano”
“Nini unataka
kukubaliana nami?akauliza
Habiba
“Watu wako waliwateka
watu wangu wawili ambao
ninawahitaji”
“Waliwateka watu wako
baada ya wewe kugoma
kutekeleza matakwa yetu ya
kutukabidhi mtu wetu.Je uko
tayari sasa kutukabidhi mtu
wetu na sisi tukukabidhi
watu wako?
“Habiba niko tayari
kuwapa kile mnachokitaka
lakini na mimi mnirejeshee
watu wangu wawili
mnaowashikilia” akasema Dr
Evans na wote mle ndani
wakapatwa na mshangao
“Hatimaye umekubali
kumuachia Edger Kaka !
akasema Habiba
“Tutafanya
mabadilishano.Nitawapa
mtu wenu na ninyi mtanipa
watu wangu.No more
blood.Mko tayari kwa sharti
hilo? Akauliza Dr Evans
“Sina tatizo na hilo.Kama
ungekubali toka mwanzo
kufanya makubaliano nasi
haya yote yaliyotokea kamwe
yasingetokea” akasema
Habiba
“Nataka kujua namna
tutakavyofanya
mabadilishano”
“Ndugu Rais kwanza
naomba ufahamu kwamba
mwanao na Olivia Themba
hawako Tanzania”
“Hawako Tanzania?
DrEvans akastuka
“Ndiyo ndugu
Rais.Hawapo
Tanzania.Baada ya saa moja
nitakupigia kukujulisha
namna tutakavyofanya
mabadilishano na mahala
yatakapofanyika.Maelekezo
yatakayotolewa yafuatwe
tafadhali ama ukijaribu
mchezo wowote wa kijinga
utawakosa watu wako”
akasema Habiba na kukata
simu
“Edger ninakurejesha
kwa watu wako ili niweze
kuwapata watu wangu lakini
yale tuliyokubaliana
yataendelea kubaki vile vile
na utakabidhiwa vitu vingine
vyote vilivyobaki”
“Vipi kuhusu Olivia?
Edger akauliza
“Baada ya kumpata
Olivia tutamrejesha kwanza
nyumbani halafu baadae
atawasiliana nawe mtapanga
namna ya kukutana.Huu ni
wakati wa kutengeneza
amani hatutaki tena damu
imwagike na jambo hili
litabaki kuwa siri yetu sisi
tuliomo humu ila ninakuonya
ukiondoka hapa usithubutu
kukanyaga mguu
Tanzania.Umenielewa?
“Nimekuelewa
mheshimiwa Rais” akasema
Dr Evans na kutoka mle
ndani akiwa ameongozana na
akina Mathew
“Mheshimiwa Rais una
hakika unataka kumrejesha
Edger kwa magaidi?akauliza
Mathew
“Once you get Coletha
and Olivia,make sure you kill
that Zombie.Anzeni
kujiandaa kwa hilo.We can’t
let him go” akasema Dr
Evans
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 22
Saa sita za usiku katika
mpaka wa Tanzania na
Kenya helkopta mbili za
kikosi cha jeshi cha
operesheni maalum zikatua
upande wa Tanzania mita
kadhaa kutoka mahala
ambako mabadilishano
yangefanyika.Ni helkopta
ambazo hazina mlio na
hazionekani katika
rada.Kikosi cha wanajeshi
kumi na mbili waliojihami
kwa silaha wakashuka na
kuanza kutembea kwa miguu
kuelekea eneo ambako
mabadilishano
yangefanyika.Kikosi hiki
kiliongozwa na Austin
January
“Mike team tunatoa
taarifa tumekwisha tua na
sasa tunaelekea eneo la
tukio”Austin akatoa taarifa
kwa ofisi yao Dar es salaam
waliokuwa wanawaongoza
katika operesheni ile
“Tumewapata Mike
team,Oscar team wako njiani
wanaelekea eneo la tukio
ndani ya dakika kumi
watakuwa
wamefika”akasema kamanda
Linus kutoka ofisi kuu Dar
es salaam
Wakati wakikaribia eneo
la tukio wakapokea taarifa
kutoka ofisi kuu
“Mike team kuna gari
tatu zinawasili eneo la tukio”
“Unaweza kuhesabu
kuna watu wangapi?Austin
akauliza
“Hawajashuka katika
magari nitawajulisha
watakapoanza kushuka”
akasema kamanda Linus
kutoka ofisi kuu
Magari matatu yaliwasili
eneo la tukio na baada ya
dakika tatu wakashuka watu
wanne waliojifunga vitambaa
vichwani wakiwa na bunduki
nzito.Wakashuka tena watu
wengine kumi na tano
wakajipanga mstari wakiwa
na bunduki zao za
kivita.Eneo lilikuwa na giza
na mwangaza ulitoka katika
taa za magari yaliyowashwa.
Austin na kikosi chake
walifika eneo la
mabadilishano.Wote
walikuwa wamevaa miwani
ya kuwasaida kuona usiku
hivyo waliweza kuwaona
wale jamaa walivyokuwa
wamejipanga.
“Mike team we’re in
position” akasema Austin
akiwajulisha Dar es salaam
kwamba wako tayari
Dakika chache baadae
helkopta ikasikika ikielekea
eneo lile.
“Mike team,Oscar team
wanakaribia kufika eneo la
tukio” Austin
akajulishwa.Taa kubwa
yenye mwangaza mkali
kutoka katika helkopta
ilimulika chini na
likapatikana eneo zuri la
kutua na helkopta ile ikatua
wakashuka wanajeshi kumi
waliokuwa na silaha nzito
baada ya kushusha katika
helkopta akina Mathew
wakajipanga vizuri kisha
Mathew akiwa na
mwanajeshi mmoja
wakaanza kupiga hatua
taratibu kuwafuata wale
jamaa na walipofika katikati
wakasimama.Watu wawili
kutoka upande wa Kenya
wakaanza kupiga hatua
kuwafuata akina Mathew
“Karibu Kenya Mathew
Mulumbi” akasema kiongozi
wa kile kikundi
“Thank you
Rashid.Nahitaji kuwaona
watu wangu nijiridhishe !
akasema Mathew kwa sauti
kubwa kutokana na
muungurumo wa helkopta
“Only you.”akasema
Rashid
“Fine” akasema Mathew
na Rashid akamuongoza hadi
katika mojawapo ya gari
mlango ukafunguliwa na
tochi ikamulikwa ndani
Mathew akawashuhudia
Coletha na Olivia
wakiwa.Olivia hakuweza
kumtambua Mathew
kutokana na mavazi ya
kijeshi aliyokuwa ameyavaa
“Nataka kumuona wa
kwangu” akasema Rashid na
Mathew akamuongoza hadi
katika helkopta akamuona
Edger Kaka na kuthibitisha
ni yeye.
“Now let’s make the
exchange.Waruhusu watu
wangu watembee na mimi
nitamuachia Edger
Kaka.Hawezi kutembea
hivyo mtu wangu mmoja
atamsukuma katika kiti
kumleta kwenu.Wakati watu
wangu wanakuja na mtu
wako naye atakuwa
analetwa.Umenielewa?akauli
za Mathew
“Nimekuelewa”
“Good.Nitakapopiga
alama nyekundu juu
mabadilishano yaanze
haraka” akasema Mathew na
Rashid akarejea upande
wao.Edger Kaka akatolewa
katika helkopta na kuwekwa
tayari.Taa kubwa ikawashwa
ili kulifanya eneo lile liwe na
mwanga.Baada ya kila kitu
kukamilika Mathew akapiga
alama nyekundu juu
kuashiria mabadilishano
kuanza
“Mike team stand by !
Austin akawajulisha watu
wake.Taratbu Edger Kaka
aliyekuwa katika kiti cha
magurudumu akaanza
kusukumwa na wakati huo
huo Olivia na Coletha
wakaanza kutembea taratibu
kuelekea upande wa
Tanzania waliko akina
Mathew.Sehemu zote mbili
watu walikuwa makini
wamejiandaa kama
kungetokea aina yoyote ya
shambuli😵livia alikutana
kati kati na Edger Kaka
“Olivia ! akasema Edger
kaka na Olivia akastuka
sana akataka kumfuata
Edger lakini Yule
mwanajeshi aliyekuwa
anamsukuma katika kiti
akamzuia.Olivia alikaribia
sana kufika mahala walipo
akina Mathew.
“C’mon Olivia hurry up”
akasema Mathew kwa sauti
ndogo.
Kabla Olivia hajawafikia
akina Mathew ukatokea
mlipuko wa bomu katikati ya
walipokuwa akina Mathew
na wale watu wa IS na kuzua
taharuki kubwa kisha
ikafuata mivumo ya
risasi.Mathew alikimbia na
kuwarukia Olivia na Coletha
akawaangusha chini huku
Risasi nyingi zikipigwa.
“Mike team,Mike team
there is an ambush we need
help !! akasema Mathew
aliyekuwa amelala chini
akiwakinga akina Coletha
“I repeat there is an
ambush we need help !!
akasema na kuwainua akina
Olivia akawashika mikono
wakaanza kukimbia
kuelekea ilipo helkopta
yao.Kabla hawajaifikia
ukatokea mlipuko helkopta
ikasambaratika ililipuliwa
kwa bomu.Ilimlazimu
Mathew kusimama ghafla
baada ya mlipuko ule
kutokea na mara akatoa
mgumo baada ya risasi mbili
kupiga bega lale la
kushoto.Aligeuka ili
kutazama nyuma lakini
akapigwa risasi ya mguu
akaanguka chini
“Olivia take Coletha Run
!! akasema Mathew ambaye
aliiokota bunduki yake
akaanza kupiga risasi
hovyohovyo ili kuwakinga
akina Olivia.
“Aaagghhhhhh ! akapiga
ukelele na kuangusha
bunduki chini baada ya risasi
kupiga mkono aliokuwa
ameshika bunduki.Risasi
ziliendelea kuvuma eneo lile
na mara Mathew
akamulikwa kwa tochi yenye
mwanga mkali sana.Alikuwa
amezungukwa na mitutu
saba ya bunduki kutoka kwa
watu waliofunika nyuso zao
na kuacha macho.Haraka
haraka akafungwa pingu na
kunyanyuliwa akabebwa na
kupelekwa sehemu Fulani
kulikokuwa na pango .Ndani
ya pango hilo kulikuwa na
taa zenye mwanga mkali
kulikuwa pia na vitanda
vinne na vifaa mbalimbali
vya matibabu.Inaonekana
watu wale walikuwa
wamejiandaa kwa ajili ya
matibabu endapo itatokea
watu wao wakapata
majeraha.Haraka haraka
Mathew akaanza
kuhudumiwa ili kuzuia damu
kutoka kwa wingi.Mara
wakaingia tena watu sita
wakiwa wamefunika nyuso
zao na walimbeba mtu
ambaye walimtupa katika
kitanda kilichokuwa karibu
na Mathew.Mathew
akageuza shingo kumtazama
alikuwa ni Edger
Kaka.Mathew akastuka
akataka kumsemesha lakini
akachomwa sindano ya
usingizi taratibu nguvu ya
macho ikaanza kupunguza
“Edger
Kaa..Edger..Edg…E..E…..”
akashindwa kuendelea
kutamka akalala.
Hatimaye milio ya risasi
na milipuko vilivyodumu
kwa dakika kumi na tano
vikakoma.Austin aliyekuwa
amejificha mahala akiwa na
Olivia na Coletha akachukua
redio yake na kuanza kuita
“Mike team please
respond ! akasema
Eneo lote lilikuwa kimya
kabisa.Austin alianza
kuwatafuta watu wake kwa
kutumia redio na akawapata
wote isipokuwa watatu.
“Oscar team please
respond ! akasema lakini
hakupokea taarifa zozote
“I repeat Oscar team
please respond ! akasema
tena lakini hakupokea
taarifa zozote.Akawaita Mike
team wakakusanyika kisha
wakaanza kuwatafuta
wenzao.Timu yote ya
Mathew hakuna aliyebaki
hai wote walikuwa
wamekufa.Miili ya watu wote
waliokuwa wameuawa
ikakusanywa sehemu moja.
“Mathew Mulumbi is
missing ! Lazima tumtafute
tumpate.Hatuwezi kurejea
nyumbani bila yeye.We have
to bring him home dead or
alive,let’s find him !
akasema Austin wakaingia
tena kumtafuta Mathew na
wakalazimika kufika hadi
eneo la upande wa pili la
Kenya walikokuwa IS ndipo
walipogundua kwamba
karibu magaidi wote
walikuwa wameuawa.
“Tumewamaliza wote.!
Akasema mmoja wa Mike
team
“Si wote.Edger Kaka
haoinekani hapa.Wengine
wametoroka naye” akasema
Austin wakaendelea
kumtafuta Mathew
Nje ya pango ambamo
Mathew alikuwa anatibiwa
kulikuwa na watu wawili
wakiwa ndani ya gari
lililofichwa kwa kufunikwa
na matawi ya miti.Hili ni
gari maalum la mawasiliano.
“Sasa tunawarudishia
mawasiliano yao” akasema
mmoja wao na kubonyeza
kitufe Fulani na baada ya
muda mfupi redio ya Austin
ikaanza kuita
“Mike team..Mike?
“Dar es salaam
tunawapata
vizuri.Tumejaribu
kuwatafuta lakini hamkuwa
mkipatikana.Nini
kimetokea?akauliza Austin
“Mawasiliano yalikatika
ghafla na hata sisi
hatukuweza kuwapata.Tuko
hapa na Rais.Nini
kinaendelea huko?
“Kumefanyika shambulio
la kustukiza,tumepoteza
watu kumi na tatu na sisi
tumefanikiwa kuua watu
karibu wote wa IS lakini
kuna wachache wametoweka
na Edger Kaka”
“Austin Rais hapa
ninaongea.Shambulio hilo
limetokeaje?Hamkuwa
mmejiandaa?akauliza Dr
Evans
“Mheshimiwa Rais
shambulio hilo limefanyika
ghafla sana kabla hata
makabidhiano
hayajamalizika”
“Lilikuwa shambulio
kubwa kiasi gani hadi
tukapoteza watu wengi kiasi
hicho?
“Mheshimiwa Rais
lilikuwa shambulio kubwa na
lenye kutumia nguvu
nyingi.Tumepoteza pia
helkpota moja”
“Jesus Christ ! akasema
Dr Evans
“Vipi kuhusu watu wetu
mmefanikiwa kuwaokoa?
“Ndiyo mheshimiwa
Rais,Coletha na Olivia wote
tumewaokoa lakini Mathew
Mulumbi hatujui yuko
wapi.Tumetafua eneo lote
hajapatikana.Tunahisi
yawezekana amejificha au
yuko mahali amepoteza
fahamu tunaendelea
kumtafuta” akasema Austin
“Austin mnatakiwa
haraka sana muondoke eneo
hilo kwani tayari ni
hatarishi.Watu hao
walionusurika yawezekana
wamekwenda kutoa taarifa
kwa wenzao na muda wowote
watarudi tena hapo wakiwa
na nguvu kubwa”
“With all due respect Mr
President we can’t leave
without Mathew.We need to
find him and bring him back
home dead or alive.We don’t
leave anybody behind”
akasema Austin
“Austin you are coming
home that’s an order from
president.The mission is
complete.We’ll find Mathew
but for now I command you
bring my people home!
akasema DrEvans.
“Sawa mheshimiwa
Rais”akasema Austin na
kuwajulisha marubani wa
helkopta zao maalum ambazo
zilikuwa mbali na eneo lile
ambazo zilifika mara
moja.Miili yote ikapakiwa
wakaondoka kurejea
Tanzania.Austin January
alishindwa kujizuia machozi
kumtoka walipoondoka eneo
lile bila ya Mathew
“Ni mara ya kwanza
ninapoteza watu wengi kiasi
hiki.Ni mara ya kwanza vile
vile ninaondoka na
kumuacha mtu
nyuma.Yawezekana Rais
akawa sahihi kwani
kuendelea kukaa pale
kungekuwa ni kuhatarisha
maisha ya hawa
walionusurika na
yawezekana watu wale
wangerejea na nguvu
kubwa.Inaniumiza sana
kumuacha Mathew” akawaza
Austin
“Lakini shambulio lile
limetokeaje? Mbona tulifanya
uhakiki wa eneo lile na
kujiridhisha waliokuwepo ni
wale watu wa
IS?Mawasiliano kati yetuna
ofisi yetu ya Dar es salaam
yalikatika vipi? Akajiuliza
Austin akakosa majibu
“Watanzania
wameondoka.Narudia tena
watanzania
wameondoka.Tumenasa
mawasiliano wakizungumza
na Rais wao akiwataka
kurejea nyumbani haraka”
akasema mmoja wa wale
jamaa waliokuwa katika gari
lenye mitambo ya
mawasiliano akiwajulisha
wenzao waliokuwa ndani ya
pango ambao walianza
kupongezana.Gari tano
zikafika pale pangoni na
watu wale wakaanza kuingia
katika magari wakapakia
kila kitu na kuondoka eneo
lile.
DAR ES SALAAM
Devotha hakuwa na
usingizi usiku huu.Alikuwa
amejilaza katika kitanda
chake kikubwa huku
pembeni yake kukiwa na
chupa ya mvinyo na
glasi.Alikuwa amevaa gauni
fupi la kulalia la rangi
nyeupe.Macho yake
aliyaelekeza katika runinga
kubwa iliyokuwa ukutani
akitazama filamu.
Simu yake ikaita alikuwa
ni Gosu Gosu.
“Gosu Gosu,nilikuwa
nasubiri sana simu yako.Are
you coming? Akauliza
Devotha huku akitabasamu
“Devotha nimepigiwa
simu na Ruby muda mfupi
uliopita amenipa taarifa za
kilichowatokea wenzetu
usiku huu waliokwenda
mpakani kufanya
mabadilishano”
“Nini kimetokea
Papii?akauliza Devotha na
kukaa kitandani
“Kumetokea shambulio la
kustukiza na tumepoteza
watu kumi na tatu.Kibaya
zaidi…” akanyamaza
“Papii !! akaita Devotha
“Mathew is missing.They
left him !
“What ? They left
him?Why? akauliza
“Nimechanganyikiwa
Devotha.Ninasubiri warejee
ili niweze kujua nini
kimetokea” akasema Gosu
Gosu
“Ahsante sana Papii kwa
taarifa hii ya
kusikitisha.Please keep me
posted” akasema Devotha na
kukata simu.Akaichukua
simu yake ambayo huitumia
kuwasiliana na Mossad
akapiga na kutaja namba
yake ya siri
“Devotha nilikuwa
najiandaa kukupigia simu
kukushukuru kwa msaada
wako mkubwa
uliotusaidia.Tumefanikiwa
kumpata tena Edger Kaka na
vile vile Mathew Mulumbi
kiongozi wa kuvamia ubalozi
wetu wa Nairobi na kuua
watu wetu.Watasafirishwa
kwenda Israel ambako
Mathew atapata adhabu
stahiki kwa makosa
aliyoyafanya.Amevamia
balozi zetu akaua watu
wetu,wengine wakiwa ni wa
muhimu sana” akasema
mkurugenzi wa Mossad
“Ninachowaomba
msimuue.Mpeni adhabu
yoyote mnayoona anastahili
lakini msimuue ni mtu
muhimu sana na mwenye
taarifa nyingi za kumuhusu
Edger Kaka.Hata ninyi pia
anaweza akawa na msaada
kwenu” akasema Devotha
“Ni mapema sana
kusema adhabu atakayoipata
Mathew Mulumbi lakini kwa
mauaji aliyoyafanya sina
hakika kama kutakuwa na
msamaha.Nitaendelea
kukujulisha.Jitahidi sana
usigundulike” akasema
mkurugenzi
“Nitajitahidi” akasema
Devotha na kukata simu
“Kazi imemalizika.Kwa
heri Mathew.I’m just doing
my job” akasema Devotha
kwa sauti ndogo na
kumimina mvinyo katika
glasi akanywa wote
“I’m done here.I’m done
with this job.I need new life
somewhere far from
here.Ninacho kiasi cha
kutosha cha fedha ambacho
kinaweza kunitosha
kuyaanza maisha yangu
mapya.Nimeshuhudia mengi
katika sakata hili la akina
Olivia hadi kwa Edger
Kaka,nimeshuhudia mauji ya
kutisha yaliyovuka
ubinadamu.I need to change
my life.Time for me to
disappear ” akawaza Devotha
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…