Riwaya: Scolastica Temu

Riwaya: Scolastica Temu

Kapamba naye kawa kimya sana, watu tunataka kuona makekke yake
 
Kapamba atakuwa anajipigia kvant tu
 
Jameni... Kapamba vipi tena bado tu hafanyi maamuzi, asichelewe sana basi mwisho kindonya atamdhuru binti temu.!
 
SEHEMU YA 52

ILIPOKOMEA...
“Sasa nakwambia hivi, kwa kuwa kanikaa moyoni sina budi kulivalia njuaga suala la kiyalinda maisha yake pia, ua! Nitafanya kila liwezekanalo na kulazima hata lisilowezekana, ili kuhakakisha kuwa SCOLASTICA TEMUI hadhuruki!”
Wanaume hao wakabaki wakitazama, kimya kikatawala kwa muda.
ENDELEA...
“Kwani kuna janga lipi unalodhani linamnyemelea? Kipini alimuuliza.
Ukali wa macho ya Kapamba uliongezeka alipoulizwa swali hilo. “Si ni’shakwambia kuwa kuna jambo ni’logundua?”
“Nakumbuka.”
“Na kwamba katika maelezo ya Ndonya kuna siri aliyoihifadhui moyoni?”
“Ndiyo.”
“Basi, naamini siri aliyotuficha ni ile ambayo alidai eti, tukishampiga mande Scolastica, hatua inayofuata haituhusu mimi na wewe. Ni yeye na Scola baaas!”
Sasa mwendo wao ulikuwa wa kususasua. Wakishavuta hatua tatu, nne wanasimama. Kwa yeyote aliyewaona alibaini kuwa wamezama katika maongezi mazito. Hata wanawake waliokuwa wakirandaranda katika barabara hiyo wakiinadi miili yao, walisita kuwasogelea au kuwapigia miluzi ya wito.
“Kinachonifanya nimtilie shaka Ndonya,” Kapamba aliendelea, “ni ile hatua ya kutumia pesa nyingi sana katika kuhakikisha eti Scola anatoka rumande. Pia, kutojulkikana kuwa katoroshawa au katoroka katika mazingira gani.
“Ndonya anatambua fika kuwa ni Scola huyohuyo aliyemuua Machemba. Nakumbuka siku ile kesi ya Scola ilipotajwa mahakamanui kwa mara ya kwanza, na Scola akaonesha kutabasamu, Ndonya alibadilika ghafla. Hasira zilisomeka wazi usoni pake! Machozi yalilenga machoni!”
Hapo tena walisitisha kutembea. Wakawa wakitazamana, kila mmoja akionekana kutafakari. Mara Kapamba akapiga ngumi kiganja chake cha mkono wa kushoto, akionesha kukerwa na jambo.
Akaendelea, “Kwa vyovyote vile, Ndonya alikuwa na uchungu mkubwa moyoni mwake. Na kwa uchungu huo, leo katuthibitishia kuwa kifo cha kaka yake kimezua donda kubwa analoamini kuwa halitapona hata mwisho wa maisha yake hapa duniani.
“Kwa kauli hiyo, hata mwendawazimu anaweza kukwambia kuwa Scola yuko hatarini. Na zinaweza kupatikana habari mbaya zaidi kuhusu yeye kama ataendelea kuishi na Ndonya hata kwa wiki moja tu zaidi.”
Kipini alitikisa kichwa akionesha ishara ya kuafiki.
“N’nachotaka ujue,” Kapamba aliendelea, “ni kwamba, kesho asubuhi nitampigia simu Ndonya. Akijibu kuwa yuko ofisini, n’tajitia kumuuliza kama dhamira ya mpango wake bado iko palepale. Nadhani atajibu kuwa bado dhamira yake ipo. Ni hapo ndipo nitakapoicheza karata yangu.”
*****
HUU ulikuwa ni usiku wenye sura tofauti na siku nyingine akilini mwa Scolastica Temu. Ilikuwa ni saa tatu u nusu, akiwa subuleni akitazama tamthilia katika runinga. Hakuwa na fikra zozote zilizokisumbua kichwa chake. Ni muda mfupi tu uliopita alikuwa ametoka kupata maakuli.
Wakati akiendelea kuitazama tamthilia hiyo, mara akasikia ngurumo ya gari nje. Muda mfupi baadaye akamwona Ndonya akiingia. Kwa kutazama haraka na kwa chati, Scolastica aliyabaini mabadiliko katika uso wa Ndonya. Huyu hakuwa yule Ndonya wa siku zote, Ndonya ambaye kila alipoingia, usowe ulikuwa na tabasamu japo la mbali.
Huyu alikuwa Ndonya mwingine, Ndonya mwenye uso uliosheheni hasira nyingi zilizojikita moyoni kwa wingi wa tani na hatimaye kwa kutostahimili msongamano, zikajitokeza hadharani.
Binadamu tuna desturi ya kusalimiana pale mkutanapo baada ya saa kadhaa, siku, wiki, miezi hata miaka. Tangu Ndonya alipoondoka asubuhi, usiku huu ndiyo alikuwa amerejea. Na kama kawaida, alimsalimu, lakini hakuujua uwezo wa Scolastica Temu katika kumsoma mtu.
Ni kweli Scolastica hakuwa mungu-mtu kiasi cha kuweza kubaini ni kipi alichokiwaza Ndonya au ni kipi kilichomfanya awe katika hali hiyo isiyoonesha uchangamfu hata wa mbali. Uwezo huo hakuwa nao.
Kipaji pekee alichojaaliwa na Mungu ni kubaini kuwa fulani anacheka kwa uchungu au anatabasamu kwa huzuni. Alihitaji sekunde chache tu kumtazama mtu usoni na kuweza kumsoma.
Hii salamu ‘habari za saa hizi’ aliyopewa na Ndonya, alitambua fika kuwa ilimtoka kwa kuwa ni utaratibu uliokwishazoeleka baina yao au baina ya binadamu wote wenye akili timamu.
Haikuwa salamu ya kutoka moyoni, salamu itokayo kwa mmoja ampendaye mwenzake. Kwa jumla ilikuwa ni salamu iliyotoka katika sauti isiyokuwa hata na chembe ya amani.
Si hilo tu, bali hata alipokaribishwa chakula mezani, alikigusagusa tu kisha akanyanyuka na kutokomea chumbani.
Ilikuwa ni hali iliyoshtua na kumshangaza Scolastica kwa kiasi kikubwa. Lakini, akiwa ni mwanamke aliyejiamini, hakutaka kuhoji chochote.
Alivitoa vyombo mezani kisha akamfuata huko chumbani na kumuuliza, “Vipi huendi kuoga?”
"Aaah….leo nasikia baridi."
"Au unaumwa?"
“Siumwi chochote, basi tu."
“Yaani we’ hulisikii joto hili?"
Ndonya alisonya bila ya kumtazama, kisha kwa sauti ya chini, akiwa amegeukia ukutani hapo kitandani alipojilaza, akasema, “We kaoge.”
“Mi’ ni’shaoga muda tu.”
“Basi.”
Scolastica aliguna. Akarudi sebuleni ambako alizima runinga. Akaenda pia kufunga mlango wa mbele kabla ya kurejea chumbani ambako akiwa vilevile kajilaza kitandani, muda huu akiwa amechojoa nguo nyingine na kubakiwa na boksa pekee.
Scolastica naye akachojoa mavazi yake na kubakiwa na nguo pekee ya ndani. Akapanda kitandani akimvuka Ndonya na kwenda kujilaza jirani na ukuta, kisha akamgeukia na kuamua kumchokonoa akitarajia jibu lolote, baya au zuri.
“Vipi, una nini leo?”
Jibu lolote alilolitarajia, halikupatikana mapema. Na huenda swali hilo ndilo lililomnyanyua Ndonya kitandani na kwenda sebuleni, ambako aliiwasha tena taa.
Kisha akarejea chumbani ambako alitwaa suruali yake na kuingiza mkono mfukoni. Humo alitoa kifurushi kidogo kilichokuwa ndani ya bahasha.
Akatoka tena, akirejea sebuleni. Huko akaifuata kabati kubwa ya vitabu iliyokuwa kando ya runinga. Akainama na kujaribu kufungua moja ya saraka lakini haikufunguka.
Akasonya na kusimama akionekana kufikiri. Kisha akarudi chumbani na kutwaa begi ambako alifungua mfuko mmojawapo na kutoa funguo mbili zilizoambatana.
Akarudi sebuleni na kuifungua ile saraka. Hakutoa chochote humo sarakani bali alikiweka kile kifurushi alichokitoa kwenye suruali. Akafunga saraka hiyo kwa funguo na safari hii hakuzirudisha kule alikozitoa, alizipachika ndani ya mfuko wa boksa aliyovaa.
Mlango wa chumbani haukuwa umefungwa, hivyo kama Ndonya alitarajia kuwa kile alichokifanya kingekuwa ni siri yake, basi haikuwa hivyo. Scolastica Temu hakuwa usingizini. Alishuhudia kila kitu, hatua kwa hatua.
Hata hivyo, hakuweza kubaini kile kilichohifadhiwa sarakani. Kumhoji Ndonya kuhusu hilo, hakuona kuwa ulikuwa wakati mwafaka. Badala yake alilirudia lile swali lake: “Hujanijibu Ndonya, una nini leo?”
“Kwani vipi?” kwa mara ya kwanza baada ya ile salamu sasa sauti ya Ndonya ilisikika. Zaidi, mikunjo ya uso ilijitokeza tena, akimtazama Scolastica kwa namna isiyo na chembe ya furaha.
Scolastica hakubabaishwa na uso huo wala sauti hiyo. Kwa upole akasema, “Hauko katika hali ya kawaida, ujue. Leo ume’change’ kiukweli.”
“Ki-vipi?” Ndonya alimtazama kidogo na kuyaepusha macho haraka.
“Nimekuona tu. Wewe si mgeni kwangu."
"Hisia zako tu. Sina tatizo lolote. Uchovu tu unanitesa."
Scolastica aliguna. Kisha: "Uchovu?!"
"Ndiyo ni uchovu tu," Ndonya alijibu. "Kazi za leo zimenichosha sana."
Kwa mara nyingine Scolastica aliguna, lakini kabla hajatamka lolote akamwona Ndonya akigeukia upande wa pili, akionesha kuwa hahitaji kuendelea kuzungumza.
***ITAENDELEA***

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh.. ni stori nzuri sana na inafundisha. Tunangoja kujua nini kitatokea zaidi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom