RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu

SEHEMU YA 14


ILIPOISHIA...

Tuliona Mkuki na Mei Lee wamefukuzwa nyumbani kwa Meja, wakiwa njiani Mkuki anamuokoa bibi mmoja wasiyemfahamu katika ajali ya ajali. Bibi anawaomba kuishi nao pamoja.

SOMA KILICHOJIRI...

Ni kama kile alichokizungumza kilikuwa na barafu kali, kilimgandisha Mkuki na kumfanya sasa afikirie kwamba inawezekana hiyo ikawa ni fursa pekee ya kumuacha Mei Lee pale na kumfuata jioni akiwa ameshafikiria ni wapi watakwenda. Lakini nafsi yake ilikinzana yenyewe ndani kwa ndani, alifikiria kumuacha Mei Lee pale, tena bila ya kukubaliana ama kumuuliza kwamba hilo litampendeza ilikuwa ni sawa na nusu ya kumtelekeza.



“Usijali bibi, tutakuja siku nyingine.” Akaamua Mkuki.
“Sawa. Nawashakuru sana kwa kunisaidia. Kwa sasa sina cha kuwapa lakini nawaahidi nitawaandalia kitu kizuri mtakapokuja hiyo siku nyingine.” Akasema Bibi, na baada ya hapo Mkuki na Mei Lee wakatoka wakimuacha bibi akifunga mlango na kurudi kuketi kwenye kiti chake akipendacho zaidi mle ndani.
Punde mlango ulibishwa hodi, bibi aliinuka kwenda kufungua na hapo akakutana na Mkuki na Mei Lee—waliamua kurudi baada ya kukubaliana kwamba ni vyema Mei Lee akabaki pale hadi jioni.
“Bibi, naomba mwenzangu abaki hapa. Nitamfuata jioni.” Akasema Mkuki na hilo halikuwa ombi kwa bibi, bali ni zawadi kubwa na ya muhimu sana ya kumuondolea ile hali ya upweke, hali ya kuwa mwenyewe kwa siku nzima.
Yeye alikuwa akiitwa Pin Ping, bibi kikongwe wa miaka takriban 80. Alikuwa akiishi peke yake kwa sababu kuu moja ambayo mwenyewe aliifanya kama siri.
Awali alikuwa akiishi Guanzouh na si hapa Hong Kong alipo leo, bali alikimbilia huko baada ya mwanae kumpelekea akaishi katika nyumba ya kulelea wazee. Hakuwa akiyataka maisha ya huko lakini hakutaka kuwakwaza wanawe na maamuzi yao. Alichoamua ni kutoroka akiwa huko kituoni, na akatumia pesa zake alizozihifadhi kwa siri kuhama Hong Kong, kupanga nyumba na kuanzisha maisha kwa kujificha ingawa alifahamu fika kwamba maisha ya aina hiyo yana ukingo wake.
“Sawa. Anaweza kubaki hapa.” Akasema bibi Pin Ping, hapo Mei Lee akamuaga Mkuki na kuingia ndani, kisha mwanaume akaondoka mbio mbio hadi mgahawani.
Alichelewa mno, na siku hiyo ilikuwa ni manusura afukuzwe kazi isipokuwa Meja alimtetea kwamba alikuwa na matatizo ya kiafya na ilibidi apite hospitali kwanza.
Kisha baada ya hapo Meja akamuita pembeni Mkuki na kumuomba msamaha zaidi wa kile kilichotokea. Hakika kilimuumiza lakini hakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima aegemee upande wa familia yake, upande wa mke wake.
Hata hivyo Mkuki sasa alimuelewa, hakuwa na kinyongo naye wala chuki dhidi yake, alijtahidi kusahau kila kilichotokea, na kuamua kuangalia mbele tu.
******************************
Jioni Mkuki alirudi kwa bibi Pin Pong, alibisha hodi na mlango ulifunguliwa na Mei Lee.
“Karibu.” Akasema Mei Lee. Mkuki akapita ndani, akaketi kwenye kiti.
“Bibi yuko wapi?” Mkuki akauliza.
“Kalala.” Akajibu Mei Lee.
“Muamushe umuage tuondoke.” Akasema Mkuki, alikuwa amepanga kwenda kulala na Mei Lee kwenye hoteli ndogo, alikuwa amepata vipesa kidogo siku hiyo.
“Mkuki, nimezungumza vitu vingi sana na bibi, nimemueleza kila kitu kuhusu maisha yetu, kasema tunaweza kuishi naye hapa.” Akaeleza Mei Lee huku akimtazama Mkuki machoni.
Mkuki alimtazama kana kwamba hakuelewa kile kilichosemwa; lakini ukweli ni kwamba alikipenda ingawa aliogopa kwa kiasi fulani kutokana na kwamba hawakuwa wakimfahamu uzuri yule bibi.
Lakini Mkuki hakuona sababu ya kupinga ofa ile hasa ukizingatia kwamba ilionekana hata bibi alikuwa anawahitaji, yaani kila mmoja alikuwa na umuhimu kwa mwenzake; bibi alichoka maisha ya upweke na Mkuki na Mei Lee hawakua na pahala pa kuishi.
********************************
Mkuki, Mei Lee na bibi Pin Ping walitengeneza familia bora sana yenye furaha hata kila mmoja akasahau mahangaiko aliyopitia. Na hivi ndivyo Mungu alivyo, mara zote hufanya njia pale pasipotarajiwa ili kuthibitisha uwepo na uwezo wake mkubwa wakufanya kile atakacho ndani ya nukta moja tu
Mkuki sasa akawa ndiye mleta huduma wa familia kama ambavyo alikuwa kwenye familia ya mzee Wong na hilo lilizidisha umuhimu wake katika familia hii.
Walikaa na bibi Pin Ping kwa miezi miwili; na kwa wiki ya kwanza ya kipindi chote hicho bibi Pin alipata kugundua kipaji kikubwa cha kuimba alichokuwa nacho Mei Lee. Mara kadhaa alimsifia na kuonesha hisia zake za wazi za jinsi ambavyo anafurahishwa na uimbaji wa msichana huyo, hata ukajengekea utamaduni wa kwamba kabla ya kulala ilibidi aimbiwe, aisikie sauti ya Mei Lee masikioni mwake ndipio usingizi uje.
Siku moja, baada ya miezi miwili ya kuishi kama familia , bibi Pin Ping alimuuliza Mei Lee jambo kuhusiana na muziki wake.
“Unajua kupiga chombo gani?” aliuliza bibi.
“Chombo cha muziki?”
“Ndiyo.”
“Hapana. Sijui kupiga chochote.”
“Mh! Kwanini? Hupendi?”
“Hapana. Napenda. Sikupata nafasi ya kujifunza tu.”
“Basi ngoja.” Akasema bibi Pin Ping, kisha akainuka kuelekea chumbani kwake akimuacha Mei Lee pale sebuleni walipokuwa. Punde alirejea akiwa na kitu fulani mkononi, ala ya muziki ambayo ilikuwa ni miongoni mwa ndoto za Mei Lee kwamba siku moja aimiliki na ajue kuitumia.
Lilikuwa ni gitaa, ala maarufu yenye kutengeneza muziki kwa kuvutwa nyuzi zake. Hili alilokuja nalo bibi Pin Ping lilikuwa ni gitaa lisilotumia umeme, lenyewe lilikuwa limetengenezwa kwa mbao nyepesi na kunakishiwa kwa rangi nyeusi, huku likiwa na vumbi kiasi kana kwamba lilihifadhiwa mahala kwa muda mrefu bila kutumika.
“Shika,” bibi akasema huku akimkabidhi Mei Lee lile gita. “Nenda kalisafishe, lifute vumbi kisha uje nalo.” Akamuelekeza.
Mei Lee akapokea, akainuka nalo na kwenda chumbani kwake akimucha bibi mwenyewe pale sebuleni. Alirudi sekunde chache baadae akiwa na gitaa lisilokuwa na vumbi sasa, alikwenda huko ndani kwa ajili ya kuchukua kitambaa kikubwa na kulisafisha.
“Tayari.” Akasema Mei Lee huku akimkabidhi bibi lile gitaa. Bibi akapoke taratibu, akalipaka kwenye mapaja yake akilitazama kwa makini kana kwamba lilimkumbusha jambo fulani murua lenye kusisimua lililopata kutokea katika maisha yake. Akafumba na macho kama mtu anayevuta hisia tamu, na hapo kiganja chake cha mkono kilipapasa gitaa lile.
Sekunde chache baadae akashusha pumzi ndefu, akafumbua macho, akamtazama Mei Lee.
“Hili gitaa linaitwa Caihong (Upinde wa Mvua),” akazungumza polepole na kwa hisia kali bibi Pin Ping na kuendelea. “kwangu ni kitu cha thamani zaidi kilichobaki kwenye uso wa dunia. Nilipewa kama zawadi na mume wangu, alinunua Uingereza alipokwenda kusoma. Sijui alifikiria nini hata akaamua kuniletea zawadi ya aina hii kwa sababu mimi na yeye, sote hatukuwahi kuwa wanamuziki; lakini niliipenda.
Basi nilitafuta mwalimu, akanifundisha jinsi ya kulitumia kwa usahihi na nilipohitimu tu nikawa nikitengeneza melodi nzuri kwa ajili ya kumliwaza mume wangu kila usiku.
Alifurahia sana, hata aliandika kwenye wosia wake kwamba akifa kabla yangu nimpigie melodi kadhaa kwenye mazishi yake.” alisimulia bibi Pin Ping na hadi kufikia hapa hisia zilimzidi. Akashindwa kujizuia, akajikuta akitokwa machozi.
Kile alichokisimulia kilimkumbusha mbali sana, kilimpa kumbukumbu za kusisimua za mapenzi. Alimkumbuka Lau, mwanaume aliyemuoa kwa ndao halali, ndoa iliyochochewa na upendo wa dhati wa kila mmoja kwa mwenzake. Alifariki kipindi ambacho bibi Pin Ping bado alikuwa ni mwanamke mwenye nguvu, hivyo baada ya pale alipata kuwa na wanamume wengine na hata kuolewa pia lakini bado nafasi ya Lau ilibaki kama ilivyo; hakuna shababi aliyefanikiwa kumfunika mwanaume huyo.
Bibi aliendelea kulia kwa machozi, Mei Lee alikuwa pale lakini hakuthubutu kusema neno, alielewa wakati mgumu namna ile aliokuwa akipitia bibi yake, hivyo aliamua kumpa uhuru wa kufanya vile alivyoamua, kutoa sumu za kumbukumbu zote za raha alizowahi kupewa na mumewe kipenzi Lau.
Baadae bibi alitulia mwenyewe, hapa sasa Mei Lee akapata nguvu ya kumsemesha na bibi akamuunga mkono kwa kumjibu na kisha mazungumzo mengine yakashika hatamu ambayo yalikuwa na sentensi mbili tu za kati kabla ya bibi kufikia kuelezea kwanini alikuja na lile gitaa.
“Ninataka nikufundishe kupigia gitaa.” Akasema bibi Pin Ping na hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Bibi Pin Ping alimfunza barabara Mei Lee jinsi ya kutumia gitaa, na ndani ya wiki nne tu binti akawa tayari na uwezo wa kuchezesha vizuri vidole vyake na kutengeneza muziki mzuri. Alilielewa kwa muda mfupi sana hasa ukilinganisha na watu wengine jinsi ambavyo huchukua kipindi kirefu cha kujifunza matumizi ya dubwana hilo; lakini bila shaka yeye alifanikiwa kutokana na kiu aliyokuwa nayo.
Sasa ikawa kila jioni, baada ya chakula Mei Lee aliwaimbia Mkuki na bibi Pin Ping huku akipiga gitaa. Alifanya hivyo kwa ustadi mkubwa sana na hakika kila mmoja alifarikija kusikiliza nyimbo zake.
****************************************
Mei Lee alikuwa akilala chumba kimoja na bibi Pin Ping; na huko kikongwe huyo aligundua kitu nyeti kuhusu mjuu wake huyu ambacho ni zaidi ya sauti nzuri na kipaji kikubwa alichokuwa nacho.
Aligindua kwamba Mei Lee alikuwa na mapenzi makubwa mno na Mkuki, na si mapenzi ya kawaida, mapenzi ya kaka na dada, bali mapenzi ya Adam na Hawa; mapenzi yaliyopelekea leo hii dunia kuwa na idadi kubwa mno ya watu.
Hili halikuwekwa wazi na Mei Lee mwenyewe, isipokuwa bibi Pin Ping alikuwa shuhuda wa kuweweseka kwa Mei Lee na ndoto zake za kila siku usiku alizokuwa akiota na huku akimtaja Mkuki.

*****************************
 
SEHEMU YA 15



ILIPOISHIA...
Tuliona Mkuki na Mei Lee wamepata hifadhi kwa bibi wa kichina baada ya kufukuzwa kama mbwa nyumbani kwa Meja. Lakini sasa bibi huyu amegundua kitu kuhusu Mei Lee.
SHUKA NAYO....
Hilo halikuwa jambo geni kumtokea Mei Lee, isipokuwa bibi Pin Ping aliligundua mara walipoanza kuwa wanalala pamoja, lakini ukweli ni kwamba Mei Lee alianza kuchanganyikiwa juu ya Mkuki tangu alipozungumza naye kwa kirefu kwa mara ya kwanza; ile siku alipomuonesha sura yake na Mkuki akampatia zawadi ya cheni. Tangu hapo moyo wake ulimuangukia mtoto wa kiume, alihisi kumpenda sana kiasi kwamba alishafunga naye ndoa, wakaanzisha familia na kuzaa watoto lukuki huko huko ndotoni.
Mkuki yeye hakuwa na mawazo hayo kabisa, alimchukulia Mei Lee kama dada yake kwa jinsi ambavyo alikuwa akimuheshimu sana marehemu mzee Wong na ule msaada aliompa.
Sasa bibi Pin Ping aliona kuna kila sababu ya kumsaidia mjukuu wake wa kike. Yeye aliyaelewa mapenzi sanjari na hisia za kumpenda mtu ambaye haonekani kuwa na dalili za kukufikiria kwa namna hiyo; hivyo mara moja akaanza kuandaa mipango ya kuhakikisha Mei Lee anafanikiwa, lakini alifanya hivi kimya kimya.
**************************************
Jiono moja Mkuki alirudi nyumbani na taarifa nzito, taarifa kwa ajili ya kubadilisha maisha ya Mei Lee sambamba na yeye pia.
Alirudi akiwa na karatasi ndogo ya rangi ya manjano mkononi, ilikuwa ni kipeperushi chenye kutangaza shindano kubwa la kusaka vipaji vipya vya waimbaji wa aina zote za muziki. Shindano lilikuwa likiitwa 'Chinese Singers Search', na lilikuwa likifanyika jijini Beijing.
“Inabidi twende Mei Lee. Ni lazima ushinde hili shindano.” Alimwambia lakini jibu alilolitoa Mei Lee lilimchosha.
“Hapana. Siwezi kwenda.”
“Kwanini? Hii ni nafasi yako Mei Lee, fursa kubwa ya kutimiza ndoto zako za na kubadilisha maisha pia.”
“Hapana. Siwezi.” Akasisitiza binti asieleze sababu za kukataa, lakini ukweli ni kuwa si kwamba hakuwa akipenda kushiriki shindano hilo, bali alikuwa akifikiria jinsi ambavyo atasimama mbele ya kundi kubwa la watu akiimba huku ile sura yake anayoichukia yenye makunyazi ikitazamwa na kila mmoja. Alijiona akikumbwa na fedhea kubwa kama atathubutu kufanya hivyo; hakika alijithibitishia kwamba hakuwa na ujasiri wa kiasi hicho.
Lakini Mkuki hakukata tamaa, alimbembeza na kumlazimisha kwenda kwa sababu aliamini kama Mei Lee atashinda shidano hilo watakuwa matajiri wakubwa kwa sababu mshindi wa kwanza wa shindano huogeshwa pesa si mchezo. Hata hivyo aligundua kuwa peke yake asingeweza, hapa akaamua kumshirikisha na bibi Pin Ping ambaye kimsingi ndiye aliyeweka nguvu kubwa na hata mwishowe Mei Lee alikubali kwenda ingawa kwa shingo upande.
Pia kukubali kwa Mei Lee ilikuwa na maana ya kwamba Mkuki aache kazi, na kwa pamoja, yeye na Mei Lee waongozane kutoka hapo Hong Kong hadi Beijing lilipokuwa likifanyia shindano hilo, kwa ajili ya kuweka kambi huko kipindi chote cha miezi miwili hadi litakapomalizika shidano; hivyo watamuacha na bibi Pin Ping mwenyewe pia.
Hakika suala la kaucha kazi kwa Mkuki lilikuwa ni gumu sana kwa kufukirika kwa akili ya kawaida, lakini kwa sababu ya kuthamini ndoto za Mei Lee na lile donge nono kama zawadi kwa mshindi vilimjaza matuamini na hakuogopa kupoteza kibarua chake-- alikuwa na imani kubwa na kipaji cha Mei Lee.
**********************************
Basi siku ya safari iliwadia, hakika ilikuwa ni siku chungu kuliko zote alziowahi kuishi bibi Pin Ping, ukiondoa ile siku aliyompeoteza mume wake kipenzi. Alikuwa amewazoea sana Mkuki na Mei Lee, kuondoka kwao ilikuwa ni kama kuchomolewa kiungo muhimu mwilini mwake.
Alishindwa kujizuia kulia bibi huyo wakati Mkuki na Mei Lee wanamuaga kwa mara ya mwisho, wanachukua mabegi yao na kuondoka—tena si kulia tu, bali aliangusha kilio kikubwa mno kilichoanzia moyoni.
Kubwa lililomliza ni jinsi ambavyo Mei Lee na Mkuki walishi naye kwa kumjali kana kwamba walikuwa ni familia moja yenye uhusiano wa kibailojia kabisa. Mei Lee na Mkuki walimuonesha upendo mkubwa bibi Pin Ping zaidi ya ambavyo mwanae wa kumzaa ambaye mara baada ya mama yake kuzeeka alimsukumia kwenye kituo cha kulelea wazee akaishi huko; hivyo maisha yake bila Mkuki na Mei Lee yasingekuwa na sababu ya msingi sana ya kuendelea kuwepo, bibi alitamani kutomokea mbali na dunia kuanzia siku ile.
Ili kuonesha upendo na thamani kubwa kwa yale waliyomfanyia kwa kipindi chote walichoishi pamoja alimuachia Mei Lee lile gita, alimpa kama zawadi akaitumie huko aendeko na hakika jambo hilo lilikuwa na maana kubwa kwa wote wawili hasa ukizingatia thamani ya lile gitaa analoliita ‘Caihong’ katika maisha ya Pin Ping.
Basi walifanikiwa kutoka nje ya Hong Kong na wakafika Beijing kwa gari. Huku walichukua chumba kimoja kwenye hoteli ya hadhi ya kawaida na kukilipia kwa siku saba—Mkuki alikuwa na pesa ya kutosha ya kumudu maisha ya kawaida kwa kipindi chote cha wao kuwa huko Beijing.
Usaili wa kwanza wa shindano ulikuwa ukifanyika kesho ya siku waliyofika, hivyo iliwalazimu waamke asubuhi kwa ajili ya kuelekea aneo ambalo zoezi zima lilikuwa likifanyika.
Usiku Mei lee hakutaka hata kufanya mazoezi, akili yake ilikuwa haifanyi kazi, alikuwa akifikiria jinsi ambavyo atasimama mbele ya kundi la watu huku uso wake ukiwa wazi—mashaka yake makubwa yaliishi katika hili.
********************************
Asubuhi ilifika, baada ya kupata kifungua kinywa Mkuki aliongozana na Mei Lee kuelekea lilipokuwa likifanyika shindano; hapakuwa mbali na hoteli waliyokodi hivyo walitumia miguu kufika huko.
Lilikuwa ni shindano kubwa na la aina yake, lilikuwa na mtindo tofauti na mashindano mengi ya aina hiyo hiyo. Wenyewe walikuwa wakifanya usaili mbele ya macho ya dunia nzima, yaani walirusha zoezi hilo 'mubashara' kwenye televisheni lakini pia kundi kubwa la hadhira huruhusiwa kuhudhuria ukumbini kutazama hatua ya awali kabisa ya upatiakanaji wa washiriki wa shindano.
Walifika ukumbini, lilikuwa ni shindano kubwa kweli kweli. Washiriki lukuki walijazana kwenye mstari baada ya kujaza fomu za ushiriki wakisubiri kupanda jukwaani ili kuonesha walichokuwa nacho.
Mkuki alimsindikiza Mei Lee kwenye kuchukua fomu ya ushiriki na akajaza; baada ya hapo wakaachaana—Mkuki alikwenda kuketi kwa mashabiki wakati Mei Lee alikwenda kupanga foleni ya washiriki wanatakiwa kupanda jukwaani, kuimba.
Namba yake ilikuwa ni 69, hiyo ni sawa na kusema kwamba yeye alikuwa ni mshiriki wa sitini na tisa kupanda jukwaani na hadi kufikia wakati huo tayafi washiriki arobaini walishaimba na saba tu kati yao walifuzu kwa kupata kura za ndio kutoka kwa majaji wote watatu waliobobea kwenye suala zima la muziki.
Sasa alipanda mtu wa arobaini na moja, aliposhuka akaja anauemfuatia, akaja mwingine na mwingine. Kadri zamu ya Mei Lee ilivyokaribia ndivyo ambavyo alizidi kuchanganyikiwa. Alihisi joto lisilosemekana akiwa pale mstarini na gitaa lake. Tena ili kuficha fedhea juu ya uso wake aliufunika kwa nywele jambo ambalo Mkuki alimkataza sana kulifanya.
Mungu si Athumani zamu yake ikafika, mshehereshaji wa shindano akataja namba yake pamoja na jina na uraia kwa sababu shindano hilo hurusu watu kutoka Thaiwan na nchi nyingine za jirani pia. Akatoka kuelekea jukwaani taratibu huku akitetemeka si mchezo. Mapigo ya moyo yalimwenda kasi kana kwamba alimeza injini ya treni ya umeme, kile alichokiwa anakwenda kukifanya kilikuwa ni kizuri kwa maisha yake lakini kilihitaji kujiamini zaidi ya alivyokuwa yeye.
Akafika jukwaani akiwa na gita lake, hapo Mkuki akamuona kutokea kule alipoketi, akawa anamuomba Mungu amjaze ujasiri Mei Lee na kujiamini pia ili aweze kuunoesha uwezi mkubwa aliokuwa nao.
“Mei Lee. Karibu?” Jaji mkuu wa shindano akamkaribisha—mwanamume wa makamo, chotara wa kichina na Kimarekani, mrefu, mnene kidogo, mwenye nywele zilizonyolewa ungaunga (kawaida), aitwaye Will Chan; na alimuita jina kwa sababu majaji walikuwa na nakala ya fomu ya kila mshiriki aliyepanda jukwaani, kwahiyo alisoma jina lake huko.
“Asante.” Mei Lee akaitikitia lakini ni kwa sauti ya chini sana kiasi kwamba hata kuna wengine hawakusikia ingawa sauti ilipenya kwenye kipaza sauti kilichosimamishwa jukwaani, mbele ya kiti cha mguu mmoja maalum kwa ajili ya washiriki wanaopenda kuimba wakiwa wameketi.
“Utatuimbia nini leo?” Akauliza jaji Will Chan lakini kabla ya Mei Lee kuendelea jaji mwingine wa kiume pia aitwaye Zoe Zhing akaingilia mazungumzo yao.
“Kabla hatujajua atakachoomba tungependa tuione sura yake.” Akasema Jaji Zoe Zhing kwa sababu Mei Lee alikuwa amefunika uso wake kwa nywele; jambo ambalo Mkuki alishamkataza kubisa kulifanya.
 
SEHEMU YA 16


ILIPOISHIA...
Tuliona Mkuki na Mei Lee wamekwenda Beijing kwenye shindano la muziki; Mei lee amepanda jukwaani kuimba lakini anakutana na changamoto baada ya kuambiwa aachiwe wazi uso wake alioufunika kwa nywele.
SHUKA NAYO....
“Sawa. Mei Lee tungependa utuimbie huku tukikuufahamu kwa sura.” Akasema Jaji Will Chan kwa mtindo wa kumbembeleza. Lakini Mei Lee hakujibu chochote juu ya suala hilo, badala yake alikuwa kimya kama bubu huku akiinamnisha kichwa chini mithili ya kondoo.

“Hei! Vipi? Kama unaona aibu toka hapo mbele waje wenzako. Shindano si kwa ajili mtu mmoja. Usitupotezee muda.” Akabatwa jaji Zoe Zhing lakini Will Chan akamtuliza kiutuzima; yeye alikuwa na mtazamo tofauti juu ya kile alichokuwa anaendelea kukiona kwa Mei Lee; alishaanza kufikiria kwamba huenda kulikuwa na tatizo linalomfanya yule msichana awe vile, hivyo ni lazima angehitaji msaada badala ya kupelekwa kijeshi kama ambavyo jaji Zoe Zhing alifanya.
“Mei Lee, umekuja na mtu yeyote hapa?” akauliza jaji Mkuu, Will Chan.
“Ndiyo.” Akajibu Mei Lee kwa sauti ya upole.
“Anaitwa nani?”
“Mkuki.”
“Ni nani yako?”
Mei Lee akapiga kimya, swali hilo lilikuwa gumu sana kwake, hakuwa akijua amtambulishe vipi Mkuki.
“Will huyu anatupotezea muda, tuna washiriki lukuki huko nje wanasubiri jukwaa hili hili. Atoke waje wengine.” Akasema jaji Zoe Zhing lakini kabla hata ya neno lingine la ziada halijazungumzwa kutoka kwake Mkuki alifika karibu na jukwaani, akaonana na mshereheshaji na kumuomba apate nafasi ya kuzungumza na msichana huyo kwa maana ni ndugu yake na ana matatizo fulani ya akili—alidanganya.
Mshehereshaji akaingilia kati.
“Majaji, mtu aliyekuja na Mei Lee yuko hapa, anaomba kusogea jukwaani azungumze naye, anasema ana matatizo.”
“Mruhusu aje.” Akasema jaji Will Chan, jambo ambalo lilimboa sana Zoe Zhing na wakaanza kuzozana wenyewe kwa wenyewe hata jaji Zoe akafikia hatua ya kusiamama na kutoka kwenye kiti cha ujaji kwa hasira, akaenda kukaa huko nyuma ya jukwaa akiahidi kurudi baada ya jaji mkuu kumaliza kumpendelea Mei Lee kwa kumpa fursa ya kupoteza muda namna ile.
Mkuki akapita akiwa na kipaza sauti mkononi, akasogea na kwenda kusimama karibu na Mei Lee.
“Wewe ndiye umekuja na Mei Lee.” Jaji Will akauliza swali ambalo tayari alikuwa na jibu lake—alitaka kuthibitisha tu.
“Ndiyo.” Mkuki akajibu.
“Ni nani yako.” Akauliza jaji.
“NI MPENZI WANGU.” Akajibu Mkuki tena kwa kujiamini mno kana kwamba yeye na Mei Lee walikuwa na uhusiano wa aina hiyo kwa miaka kumi sasa.
Jibu lake lilimshitua sana Mei Lee mwenyewe hata ilibaki kidogo aanguke na azirai kwa kile alichokisikia. Kwa taarifa yako tu mi kwamba kilimfurahisha mno, alihisi mashamushamu na raha tele moyoni mwake. Hakuwahi kuitwa mpenzi na mwanaume yeyote tangu kuzaliwa kwake; lakini leo Mkuki Salumu Goigoi amefanya hivyo tena mbele ya dunia nzima, hakika alijihisi ni malaika, asijue Mkuki alifikiria nini hata kutamka maneno yale.
“Sawa. Zungumza naye aonyeshe sura na aanze kuimba. Ana dakika moja tu kuanzia sasa.” Akasema jaji Mkuu, wakati wote huo mashabiki walikuwa wakitamani kuona tamati ya ile filamu fupi isiyokuwa na ‘script’ inayochezeka pale jukwaani.
Basi Mkuki akamsogelea karibu zaidi Mei Lee, akasimama mbele yake, akanyanyua mkono wake mmoja na kumshika kidevuni, akamuinua uso ili wawe kama wanatazama, alifanya hivyo bila kumfunua nywele.
“Nakupenda Mei Lee. Nakupenda sana.” Akamwambia, tena kila mtu alisikia kwa sababu sauti yake ilipenya kwenye kipaza sauti alichoshika.
Kisha baada ya hapo Mkuki akafunua mywele za Mei Lee taratibu na kuzirudisha nyuma, halafu akasogeza mdomo wake polepole karibu na mdomo wa msichana huyo na bila dada mwenyewe kutarajia alinyonywa mate mbele ya hadhara kwa sekunde kadhaa.
Hakikuwa ni kitendo chenye maadili kwa nchi kama China lakini niamini mimi kwamba kilifanya kila mtu pale ukumbini ampende Mkuki na kumuona ni mwanaume timilifu hasa baada ya kumuachia, na uso wa Mei Lee kumulikwa na kamera na kufanya wote wagundue sababu ya binti huyo kukataa kuachia nywele zake—watu walijiuliza na hawakupata jibu la Mkuki alimpendaje, na huko kutokuwa na majawabu ndiko kulipelekea wamuone Mkuki ni shujaa haswa?
Baada ya pale Mkuki aliteremka jukwani akiwa amemuachia Mei Lee ujasiri mkubwa mno; lile busu mubashara alilopewa lilikuwa ni tiba haswaa; lilikuwa ni busu lake la kwanza la mdomo kwa mdomo tangu aumbwe na Mungu Mwenyezi.
Mkuki alifanya vile kwa sababu kuu moja; bibi Pin Ping alikwishamueleza kila kitu kitu kuhusu upendo wa Mei Lee juu yake; hivyo Mkuki alikuwa anafahamu yote, anafahamu kiu ya kupendwa aliyokuwa nayo Mei Lee na ndiyo maana alifanya vile ili kumpa ujasiri.
Binti akaketi kwenye kiti akielekea kipaza sauti, akapiga gitaa kidogo, kisha akafungua kinywa na kuimba. Ni nani kati ya waliomsikia alikuwa na kiburi kiasi kwamba angepinga ubora wa binti huyo kwenye kuimba na ule utamu wa sauti yake—hakuwepo hakika, wote walimuelewa sana, alipigiwa shangwe za ‘kufa mtu’ zilizoufunika ukumbi mzima.
Siku ile aliimba wimbo wake mwenyewe uitwao RANGI YA HUBA. Wimbo alioundika akiwa na ndoto za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mkuki, na mashahiri yake yaliendana kabisa na lile tukio lililotokea siku ile.
“Umeimba vizuri sana. Una pointi tatu kutoka kwangu.” Alisema jaji Mkuu na mtazamo wake ulikuwa sawa na jaji namba tatu ambaye alikuwa ni mwanamke; na ili kufuzu usaili huo mshiriki yeyote alihitaji jumla ya pointi sita huku kila jaji akiwa na uwezo wa kutoa pointi zisizozidi tatu tu, hiyo ilikuwa ni sawa na kusema kwamba ingawa maamuzi ya Mei Lee yalitoka kwa majaji wawili, lakini alifuzu kutokana na kwamba majaji wote wawili walimpa pointi tatu kila mmoja.
Baada ya pale Mei Lee aliteremka jukwaani akisindikizwa na makofu ya pongezi kutoka kwa hadhara waliohudhuria tukio lile; na ratiba ilikuwa ni kwamba baada ya hapo washiriki wote watakaofuzu watafanyiwa semina kabla ya kitumbukizwa kwenye shindano rasmi ambapo sasa raia watapewa ruhusa ya kupiga kura kwa njia ya simu za mkononi.
Aliposhuka chini Mei Lee alikutana na Mkuki, hapa Mei Lee alishindwa kujizuia kumkimbilia, kumkumbatia na kumpiga busu refu la mate kwa mate kwa mara nyingine—alikuwa ni kama amewehuka.

“Nakupenda Mkuki. Nakupenda sana.” Alimwambia baada ya kujichomoa kutoka kwenye lile kumbatio, kisha akamkumbatia na kumbusu tena.
Walipotoka nje ya ukumbi ilikuwa ni kasheshe, walikutana na kundi kubwa la waandishi wa habari wanaotaka kuzungunza na Mei Lee, si kwa sababu aliimba vizuri bali ni kutoka na ile hitulafu iliyo usoni mwake—waliamini habari iko hapo.
Hata hivyo mwenyewe hakuwa tayari kuzungunza lolote na kwa msaada wa Mkuki walifanikiwa kuwachenga waandishi wote na wakarejea hotelini.
Walifika hotelini huku mioyo yao ikiwa imejaa furaha na raha lakini zaidi ilikuwa ni kwa Mei Lee. Yeye aligubikwa na lindi zito la huba kwa kiasi kwamba nishati iliyotokana na hali penzi iliyozalishwa na moyo wake ingeweza hata kufanyiza umeme kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Walipoingia ndani tu Mkuki alimkamata Mei Lee, akambeba na kwenda kumuanguashia kitandani. Kisha naye akaja juu yake, akaanza kumpiga denda huku akimpapasa taratibu kwenye maeneo mengine ya mwili wa binti huyo.
Binti alihisi raha iliyoje, raha isiyosimulika, raha ambayo bado haijapata msamiati wa kuidadavua kwa uzuri zaidi.
Mtoto wa kiume akaendelea na mashambulizi, na sasa wakafikia hatua ya kuchojoana nguo kabisa. Mkuki alipukitisha kiwalo kimoja baada ya kingine cha Mei Lee kana kwamba alikuwa akimchuna ngozi na tamati binti alibaki mtupu kama alivyozaliwa.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Mkuki kushuhudia tupu ya Mei Lee, mtu ambaye awali alikuwa akimtazama kama dada yake. Mtoto wa kike alikuwa na mwili mzuri kweli kweli, ngozi laini kama hariri, kama aliyekoga mafuta ya jibini.
Basi Mkuki hakutaka kupepesa katika hili, alikwenda moja kwa moja kifuani, eneo ambalo lilikuwa na matiti saa sita yenye chuchu zilizosimama kama ncha ya msumari. Hapo akazinyonya taratibu kwa mahaba huku akitega sikio lake kusikiliza mrejesho wa jinsi ambavyo Mei Lee alikuwa akiugulia.
Ilikuwa ni raha tu, na utamu ulikamalika baada ya Mkuki kuingiza roketi yake pangoni mwa binti, na tangu hapo historia ikaandikwa kuwa ilikuwa ni mara ya kwanza kwa msichana huyo kuonja utamu wa ‘tunda la edeni’.
Tangu siku ile maisha yalibadilika sana hasa kwa Mei Lee, sasa alikuwa akijiona ni binadamu kamili, mwanamke asiye na kasoro. Mkuki alijitahidi sana kuwa mwanaume muungwana kwake na alifanya hivyo akisukumwa na upendo wa dhati ulioibuka ghaflla juu ya Mei Lee.
 
SEHEMU YA 17


ILIPOISHIA...

Ilikuwa ni raha tu, na utamu ulikamalika baada ya Mkuki kuingiza roketi yake pangoni mwa binti, na tangu hapo historia ikaandikwa kuwa ilikuwa ni mara ya kwanza kwa msichana huyo kuonja utamu wa ‘tunda la edeni’.
Tangu siku ile maisha yalibadilika sana hasa kwa Mei Lee, sasa alikuwa akijiona ni binadamu kamili, mwanamke asiye na kasoro. Mkuki alijitahidi sana kuwa mwanaume muungwana kwake na alifanya hivyo akisukumwa na upendo wa dhati ulioibuka ghaflla juu ya Mei Lee.


ENDELEA...
Siku ya semina kwa ajili ya wa washiriki wote waliofuzu ilifika; washiriki wapatao thelethini wa shindano lile walihidhuria akiwemo Mei Lee. Yeye alisindikizwa na Mkuki kama kawaida na alikuwa nje ya ukumbi wa semina akimsubiri.
Baada ya semina washiriki waliruhusiwa kuondoka huku sasa wakifahamu kwamba shindano litaanza kurindima wiki moja baadae.
Wiki haikuwa mbali namna hiyo; iliwadia na shindano lilianza mara moja, tena lilianza moto kweli kweli. Washiriki wote thelathini walikuwa na vipaji vikubwa lakini amini kwamba kwa Mei Lee wote walikuwa ni cha mtoto tu.
Mei Lee aliimba vizuri mno, sauti yake na ujuzi wa kupiga gita vizuri kulimfanya awe wa pekee sana kulinganisha na wenzie
Shindano lilikatiza wiki nne, na sasa walisalia washiriki 18 kwa sababu kila wiki moja walikuwa wakitoka washiriki watatu wenye kura chache zaidi za mashabiki.
Hata hivyo dalili zilioneyesha wazi kwamba Mei Lee alikuwa anakwenda kuwa mshindi kwa sababu yeye alikuwa na kura nyingi sana ukilinganisha na washiriki wengine.
Baada ya wiki nane walisalia washiriki sita tu akiwemo Mei Lee ambao hao wangeimba kwenye onesho la nusu fainali na angetoka mshiriki mmoja na watano watakaosalia watakwenda moja kwa moja fainali.
Kabla ya nusu fainali Mei Lee alipata ofa kubwa ambayo ilikuwa ni kama ngekewa ya kubadilisha maisha yake. Ilikuwa ni kitu ambacho pengine alitamani kiwezekane kwa muda mrefu lakini alishindwa kukimudu kutokana na gharama.
Ilikuwa ni ofa kutoka hospitali ya YUN; hospitali ambayo ilikuwa imeshehenei madaktari bingwa hasa waliobobea katika suala zima la kufanya upasuaji.
Walimpa ofa ya kimsaidia kufanya uchunguzi wa tatizo alilonalo usoni na kama watagundua kuwa linaweza kutibika basi watampa matibabu na kuhakikisha anapona kabisa na walimchagua yeye kwa sababu waliamini kama atashinda atakuwa ni msanii mkubwa kwa hivyo anaweza kuwa balozi wao nambari moja.
Alimpa taarifa hiyo mpenzi wa maisha yake, Mkuki Salumu Goigoi ambaye naye alikubali bila shida huku akiomba Mungu tatizo la Mei Lee lipate matibabu ili naye apate kuona urembo halisi wa msichana huyo uliofichwa nyuma ya makunyanzi yake.
Basi Mkuki alimsindikiza hospitalini siku ya vipimo, binti akaingia chumba cha dakatari na baada ya mazungumzo ya hapa na pale alichukuliwa na kupelekwa chumba cha vipimo. Huko madaktari walifanya wanachofanya na tamati walikuja na jibu kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kupona kabisa kupitia upasuaji watakaomfanyia ambao kimsingi ulikuwa ni upasuaji wa gharama kubwa mno.
Aliambiwa tatizo lilikuwa kwenye leya ya ndani ya ngozi, iliathiriwa na sumu ya Holocen ambayo hupatikana kwenye seli za viumbe wa baharini hasa samaki na kupitia hilo daktari alithibitishia kwamba huenda Mei Lee alipata tatizo baada ya kula samaki mwenye sumu hiyo.
Baada ya pale alipangiwa siku ya zoezi lenyewe la upasuaji na ilikuwa ni kesho kutwa ya siku hiyo ambayo itakuwa ni siku nne kabla ya nusu fainali ya shindano kufanyika; hivyo madaktari walimuhakikishia kwamba upasuaji hautaathiri uwezo wake wa kuimba.
Basi tangu pale waliona ni kama muda haukwendi, umesimama. Si yeye Mei Lee si mpenzi wake Mkuki, waliona siku ya upasuaji ni kama ilipangwa miaka miwili mbele. Lakini huo ulikuwa ni mtazamo wao, muda ulikwenda kama kawaida na hatimaye siku ikafika.
Mkuki alismindikiza tena mpenzi wake hadi hospitalini; huko Mei Lee akakutana na wale madaktari, wakamchuka hadi kwenye chumba cha upasuaji na shughuli ikaanza mara moja. Ulikuwa ni upasuaji mkubwa, uligharimu zaidi ya saa tatu hadi kukamilika na baada ya hapo Mei lee alifunikwa na kitu kama bandeji nyeupe usoni na kuingizwa kwenye mashine fulani ambayo hii ilikuwapo maalum kwa ajili ya kukamilisha matibabu.
Alitakiwa kukaa katika mashine hiyo kwa dakika thelathini na baada ya hapo angetoka akiwa Mei Lee mpya, Mei Lee halisi.
Basi hizo dakika thelathini zilikuwa ni kama miaka mia nane kwa Mkuki. Alikuwa na hamu ya kumuona Mei Lee baada ya matibabu, aliwashwa sana na mashumumashamu ya kuiona sura halisi ya msichana huyo—unajua hakuwahi kumuona hata kwenye picha.
Dakika thelathini nazo hazikuwa kitu, zilikatika na sasa ukawa ni muda muafaka kwa binti kutolewa kwenye ile mashine, kuvuliwa ile bandeji na kuwa yeye kama yeye.
Daktari aliyekuwa akimshuhulikia Mei Lee aliingia kule alipokuwa mgonjwa, akabofya kitufe na mashine ikafunguka, na taratibu akaanza kuondoa ile bandeji usoni mwa Mei Lee.
Zoezi lilikamlika, dokta akamuomba Mei Lee asimame taratibu, asogee mbele ya kioo na ajitazame kuona jinsi alivyokuwa.
Mei Lee akafanya hivyo, akashuka kitandani na kwenda kusimama mbele ya kioo kikubwa. Alitulia wa sekunde kadhaa akijitazama lakini ghafla alianza kulia kilio kikubwa mno, kilio cha furaha, kilo ambacho kilitafisri shukrani aliyokuwa nayo kwa Mungu na wale madktari waliofankisha zoezi la matibabu yake—hakuwahi kutarajia kwamba kuna siku tatizo lake litapata kikomo.
Baada ya hapo aliombwa kutoka nje, kwenye kordo ambapo Mkuki alikuwa akimsubiri.
Basi Mkuki akiwa hapo akaona mlango ukifunguliwa, akatoka msichana ambaye Mkuki alijithibitishia kabisa kwamba ni Mei Lee wake. Hakika alihisi furaha moyoni kumtazama, hakuwahi kufikiria hata siku moja kwamba Mei Lee atakuwa ni msichana mrembo namna ile hasa ukizingatia kwamba si wasichana wengi wa kichina na hata Thaiwan ambao waliwahi kumvutia machoni. Mei Lee alikuwa na sura murua, ndogo ndogo ya duara, yenye kipua , vimacho, na vidomo viduchu-duchu.
Mkuki alisamama wakati Mei Lee akimfuata taratibu. Akamfika, akasimama mbele yake akimtazma bila aibu yoyote lakini ghafla alimvamia na wakakumbatiana.
“Nakupenda Mkuki. Nakupenda sana. Yote haya ni kwa sababu yako.” Alisema Mei Lee huku akilia kilio cha furaha mno. Yeye aliamini kwamba bila Mkuki kila kitu kisingekuwa kama kilivyo, asingefanikiwa kwa kiasi kile.
Hakika ile ilikuwa ni siku ya maana kubwa kwa wote wawili, siku ya kujitambua na kujifahamu, siku ambayo kila mmoja aligundua waziwazi sababu ya yeye kuwepo duniani.

**********************************
Siku ya nusu fainali iliwadia, watu walijazana ukimbini kama ilivyo kawaida na walianza kupata burudani taratibu kutoka kwa washiriki wa shindano lile.
Washiriki wote walipanda jukwaani na kuimba na Mei Lee akawa wa mwisho. Walifanya hivyo kwa sababu walitaka kuwashamgaza mashabiki kwa kile kilichotokea kwa kuwa hakuna mtu yeyote aliyefahamu kama anakwenda kufanya upasuaji wa kurekebishwa sura yake.
Basi alivyopanda jukwaani ziliibuka shangwe za kufa mtu, huku wengine hasa wanawake wakishindwa kuzuia hisia zao kiasi kwamba walilia mno kana kwamba walikuwa na undugu wa damu na Mei Lee. Walikuwa wakimpenda sana, walikuwa wakipenda anavyoimba, walipenda anavyopiga gita lakini pia walipenda haiba yake, na sasa wakajikuta wanaongezewa kitu kingine cha kupenda toka kwake—ile sura yake nzuri ya kitoto.
Niamini mimi kwamba baada ya hapo Mei Lee alikuwa na aslimia mia moja za kuwa mshindi wa shindano lile, hakukuwa na cha kumzuia asilani, aliwaongoza wenzake kwa kila kitu.
Baada ya mtanange wa nusu fainali kwisha na Mei kuwa ni miongoni mwa washiriki watakaokwenda fainali alitoka na Mkuki mpaka nje ya ukumbi ambapo huko Mei alivamiwa na kundi kubwa la mashabiki wakiomba kupiga naye picha na kupata saini yake kwenye nguo zao.
Kundi la mashabiki lilikuwa ni kubwa mno kiasi kwamba wasingeweza kuwamudu kwa namna yoyote ile; yaani kwa Mei Lee kukubali kupiga nao picha au labda kuwakimbia.
Hapo ilibidi wapate msaada kutoka kwa walinzi wa ukumbi lilipokuwa likifanyika shindano, lakini pia hawakufanikiwa kitu; watu waliendelea kumzonga Mei Lee pamoja na Mkuki pia.
‘Paaa’ mara mlio wa risasi ukasikika, risasi ambayo ilipigwa na askari mlinzi aliyeoona kuwa labda hiyo ndiyo njia pekee ya kuwasaidia kina Mei Lee. Ghafla watu wakaonekana kuchanganyana huko na huko jambo ambalo kidogo lilifanya Kina Mei Lee wawe huru.
Papo hapo akatokea mwanaume mmoja, akamkamata mkono Mei Lee na kuanza kumvuta kwa kuelekea eneo ambalo halikuwa na mashabiki.
“Twendeni huku.” Akasema mwanaume huyo akimwambia Mkuki pamoja na Mei Lee, nao wakamfuata bila kujua wapi wanapelekwa na ni nani huyo aliyewaongoza.
Kwa msaada wa mwanaume yule walifanikiwa kuwatoka mashabiki na wakaifikia gari ya kisasa aina ya Rolls Royce yenye rangi nyeusi, jamaa akafungua mlango wa nyuma na kuwataka Mkuki na Mei Lee waingie kisha na yeye akaingia akiwa wa mwisho—upande huo wa nyuma ulikuwa na viti wiwili vinavyotazama huku kila kiti kikitosha kukaliwa na watu wawili.
Yule mwanamume akaketi upande ambao alikuwa akiwatazama kina Mkuki uso kwa uso kisha papo hapo akamuamrisha dereva aendeshe gari na mambo yakawa hivyo, safari ya kusipojulikana ikaanza.
Kimya kifupi kilitawala mle ndani, jamaa alitazama na kina Mkuki kana kwamba walikuwa wakipanga mipango ya kukamilisha biashara fulani ya haramu.
Alikuwa ni mwanamume wa kichina mwenye umri unaocheza katikati ya miaka 25 hadi 30, mrefu ukimlinganisha na wachina wengi lakini mfupi kwa Mkuki. Alikuwa amevalia suruali ya jinzi, raba miguuni na shati la mikono mirefu alilolivaa ndani ya koti la suti la rangi nyeusi. Nywele zake hazikuwa za kawaida, zilikuwa na mtindo wa ajabu kana kwamba alikuwa ni msanii wa muziki, pia alikuwa na hereni ndogo kwenye sikio lake la kushoto, cheni kubwa shingoni, pete kidoleni na makorokoro mengi ya kufanana na bangili mikononi.
“Unajisikiaje? Umaarufu ni mtamu?” Akaamua kufuta ukimya jamaa huyo kwa kumuuliza Mei Lee.
Mei Lee hakumjibu, alitabasamu.
“Samahani; umetusaidia lakini hatujui tukushuru kama nani, tunaweza kutambuana?” Akasema Mkuki. Hapa alikuwa akitaka kumfahamu mtu huyo baada ya ile sintofahamu iliyokuwemo baina yao hasa ukizingatia kwamba aliwaokoa kwa kutumia njia ya hatari sana ambayo hata hivyo hurusiwa kutumika zinapotokea hali za namna ile.
“Naitwa Leehom; bila shaka si jina linalohitaji ufafanuzi zaidi.” Akasema mwanaume huyo huku muda wote akionesha uso wa tabasamu—alikuwa na sura ya kuvutia pia.
“Sio vibaya ukitufafanulia.” akasema Mkuki; alikuwa akijiamini kweli kweli.
“Sawa. Nitafanya kama mnavyotaka.” Akasema jamaa huyo aliyejitambulsiha kwa jina la Leehom na kuendelea. “Leehom ni moja ya nembo za taifa hili, sina tofauti na bendera yetu au labda ukuta mkuu wa Uchina. Kazi yangu ninnanyoifanya ni lulu masikioni mwa watu wengi, na kuna watu nje ya ardhi hii wananifahamu mimi zaidi ya wanavyoijua China.” Akasema Leehom; alitumia mtindo wa kona kona katika kujitambulisha.
“Kama nimekuelewa basi unamaanisha wewe ni mwanamuziki, sio?” Mkuki akauliza.
“Bila shaka jibu ni ndiyo. Mimi ni mwanamuziki.” Akasema.
“Sawa. Kwahiyo utatupeleka hadi wapi? Kwa maana sisi tunaishi katika hoteli ya Nei Pei, ni karibu na pale ukumbini.”
“Najua. Najua kila kitu kuhusu nyinyi wawili. Najua pia hamtakuwa na pingamizi endapo nitawaomba kwamba kituo cha safari hii kiwe ni nyumbani kwangu, tupate mvinyo laini na chakula cha jioni kisha nitawariduisha hotelini kwenu.” Akasema Leehom.
********************************
 
SEHEMU YA 18

ILIPOISHIA....
Tuliona Mkuki na Mei Lee wamezongwa na mashabiki, ghafla akatokea mtu mmoja na kuwasaidia; akawaingiza kwenye gari yake. Na sasa mtu huyo akawaomba kuwapeleka nyumbani kwake.
SHUKA NAYO....

“Hilo niombi?”
“Ndiyo ni ombi; na itapendeza kama jibu litakuwa ni ndiyo.” Akasema Leehom.

Mkuki alitazamana na Mei Lee kana kwamba walikuwa wakiulizana kuhusu kukubali ombi la jamaa huyo; na kupitia macho yao wakaonekana kukubaliana jambo ambalo ni wenyewe tu walielewa—hata hivyo walikubali ombi la Leehom.
Leehom alikuwa ni msanii wa muziki mkubwa zaidi nchini China, amabye pia alikuwa ni maarufu hata nje ya taifa hilo. Tayari alishawahi kufanya kazi na wasanii wakubwa wa muziki hasa kutoka Marekani; amewahi kufanya kazi na mtu kama marehemu Michael Jackson na wengine wengi. Yeye alipendezwa sana na jinsi ambavyo Mei Lee alikuwa akiimba lakini zaidi alijikuta anatamani kuwa karibu naye mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa kusafisha uso. Alivutiwa sana na jinsi ambavyo uso wa Mei Lee unaonekana bila yale makunyanzi; hivyo alikuwa na mpango wa wa hata kufanya naye kazi pamoja.
Yote hayo Leehom alikwenda kuyazungumza walipofika kwenye kasri lake, wakiwa wanapata chakula cha jioni.
“Nataka shindano likiisha nifanye kitu kikubwa na wewe, nataka nikutangaze duniani.” Alimwambia na alifafanua zaidi.
Hiyo ilikuwa ni kama ngekewa kwa Mei Lee, msichana ambaye kwa kipindi chote alikuwa akiota kuwa msanii mkubwa, kuzungumza na dunia kupitia sauti yake aitosayo ndani ya mashahiri matamu ayaundayo kwa kutumia akili yake ya kawaida lakini ya pekee. Alitamani hata shindano liishe leo, sasa hivi, ili apate nafasi ya kufanya kazi na Leehom na amtangaze duniani kote kama ambavyo yeye alikuwa akifahamika.
Kwa upande wa Mkuki pia aliona hiyo ni heri na neema inazidi kuja upande wake kwa sababu kama Mei Lee atafanikiwa kwa kiasi kikubwa namna hiyo basi ni wazi kwamba yeye atakuwa mtu wa kwanza kufaidi matunda ya mafanikio hayo.
Basi baada ya chakula Leehom aliwachuka hadi kwenye maegesho ya magari ya nyumbani kwake, huko kulikuwa na magari yapatayo sita ya kifahari lakini alichagua moja ambalo alipanga kulitumia kuwarejesha nyumbani kina Mei Lee kwa kuwaendesha yeye mwenyewe.
Ilikuwa hivyo, aliwarudisha huku safari nzima wakizungumza na kucheka; walizoena naye mapema sana kwa sababu Leehom alikuwa ni mzungumzaji sana na mcheshi.
Aliwafikisha hotelini, akaawaacha hapo na yeye akarejea nyumbani huku akimtaka Mei Lee anapopata muda awe anamtafuta kwa ajili ya kumnoa na kumfua zaidi kama sehemu ya maandilizi ya fainali ya mashindano yale.


**********************************
Mei Lee na Mkuki walikuwa ndani ya chumba cha hoteli walimopanga, punde walisikia hodi mlangoni, Mkuki akasimama kwenda kufungua. Alikutana na mgeni, mwanamke wa kichinia ambaye hakuwa akimfahamu.
“Karibu.” Alisema Mkuki.
“Asante. Naitwa Yin, ni afisa mratibu matangazo wa kampuni ya fenicha ya Beijing, nina shida na Mei Lee. Naweza kumuona.” Akajitambulisha mwanamke huyo na kuweka wazi adhma ya ujio wake.
“Ndiyo. Karibu ndani.” Akasema Mkuki huku akimpisha. Yule mwanamke akaingia na hapo Mkuki akafunga mlango.
Dada huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Yin alimuona Mei Lee mara tu baada ya kuingia ndani, akamsogelea na kumsalimu kwa kumpa mkono kisha akaelekezwa akateti kwenye kiti; akafanya hivyo.
“Karibu.” Mei Lee akasema, kwa wakati huo Mkuki alikiwa ameshakuja, ameketi pembeni yake.
“Asante Mei Lee,” akasema yule msichana na kujitambulisha zaidi kama alivyofanya kwa Mkuki na akaendelea. “Kampuni yetu inataka kufanya tangazo kwa ajili ya mtindo mpya wa fenicha zetu, kwahiyo tulimtafuta Leehom ili tumtumie katika tangazo hili lakini yeye alikataa na akapendekeza tukutumie wewe; na kimsingi vigezo unavyo; kwahiyo nimekuja hapa ili tufikie makubaliano ya awali, tujue kama na wewe unapenda kufanya kazi na sisi kama ambavyo sisi tunapenda kufanya na wewe. Na kama jibu litakuwa ndio, basi tunaweza kutoka sote, mimi na wewe, twende ofisini tukaweke sawa baadhi ya mambo kisha tupange ni lini tutafanya hilo tangazo kabla ya siku ya fainali ya shindano lako.” Akasema Yin.
Mei Lee na Mkuki wakatizamana kana kwamba walikuwa wakiulizana kitu kuhusu taarifa ile na kupitia ishara za macho Mkuki akamshauri Mei Lee akubali.
“Sawa. Hakuna shida.”
“Kwahiyo tunaweza kwenda?” akauliza Yin kuthibitisha.
“Sawa.”Akajibu Mei Lee kisha akamgeukia Mkuki na kumuuliza na kumuuliza kama watakwenda pamoja na Mkuki akajibu ndiyo.
“Samahani Mei Lee. Hili jambo ni la kiofisi zaidi, kwahiyo ni vyema kama tutaenda na wewe peke yako.” Ghafla Yin akaingilia mazungumzo yao kina Mei Lee na kutoa taarifa ya namna hiyo.
“Kwanini!? Hapana haiwezekani. Kwani tunakwenda kujadili nini ambacho mpenzi wangu hastahili kukisikia?” akahoji Mei Lee na swali lake lilionesha kumkata maini Yin ingawa bado hakuonekana kuridhishwa na kwamba waondoke pamoja na Mkuki.
Mtoto wa kiume aligundua hilo, akapiga mahesabu ya haraka, akagundua kwamba hata kama Mei Lee atakwenda peke yake pesa atakayolipwa kwa ajili ya kufanya tangazo hilo haitapungua; kwahiyo kimantikki yeye hakuwa wa muhimu sana kwenye suala zima la maslahi. Haraka akatumia akili hiyo, akamtaka Mei Lee akubali bila kinyongo huku akimuhakikisha kwamba hakuna kitakachoharibika, na kwa sababu binti alikuwa akimsikiliza sana Mkuki hakuweka kipingamizi katika hilo, alifanya kama alivyoelekezwa.
Basi baada ya pale Yin akamchukua Mei Lee mpaka nje ya hoteli yao ya gharama za chini waliyokuwa wakiishi. Huko kulikuwa na gari safi ya kifahari sana ikiwasubiri kwa ajili ya safari. Walipoifikia wakaingia na safari ya kuelekea zilipo ofisi za kampuni ya fenicha inyomuhitaji Mei Lee katika tangazo lao ikaanza.
Ilikuwa ni safari iliyogharimu robo saa tu, walipofika wakashuka garini na Yin akamuongoza Mei Lee ndani ya jengo ambalo bila shaka ndilo lilikuwa na ofisi za kampuni yao. Alimpeleka hadi ndani ya ofisi moja kubwa ya kisasa, na mara tu baada ya wao kuingia humo Mei Lee alimuona Leehom kwenye moja ya picha kubwa zilizobandikwa ukutani; jambo hilo lilimshangaza lakini alijitahidi kujiaminisha kwamba huenda picha zile zilikuwa pale kwa sababu Leehom alikuwa ni msanii mkubwa na maarufu hivyo mtu yeyote aliweza kuweka picha yake ofisini.
“Karibu.” Alisema Yin huku akimuelekeza Mei Lee aketi kwenye kochi; binti akafanya hivyo.
“Naomba dakika moja nakuja.” Akaomba Yin kisha akatoka nje akimuacha Mei Lee peke yake pale kwenye kochi, mle ofisini.
Punde mlango ilifunguliwa, akaingia Yin, lakini hakuwa mwenyewe safari hii, alikuja na mtu mwingine—alikuwa amekuja sambamba na Leehom. Mei Lee akamtazama, wakatazama, Leehom akatabasamu kidogo huku akimsogelea binti pale kwenye kochi na alipomfikia akampa mkono wa salamu.
“Karibu.” Akasema Leehom huku akiendeleza lile tabasamu lake, binti akampa mkono pia kama ishara ya kuipokea karibu yake huku na yeye akionesha tabasamu kwa mbali.
“Nawaacha.” Mara Yin akawaaga, kisha akatoka ofisini humo na kumuacha Mei Lee na Leehom, huku Mei Lee asielewe nini kinachoendelea, kwa sababu aliambiwa anapelekwa kwenye makubaliano ya kufanya tangazo na sio hiki anachokiona—lakini alijitahidi kuwa mpole kusubiria matokeo ya kile kinachoendelea.
Leehom akamuachia mkono Mei Lee baada ya kumganda kwa sekunde kadhaa, kisha akazunguka na kwenda kuketi kwenye kiti kukubwa cha kibosi kilichopo nyuma ya meza ya kisasa ya ofisi hiyo ambayo juu yake ilikuwa na kompyuta na makabrasha mengi.
“Karibu Mei Lee. Hapa ni ofisini kwangu pia.” Akasema Leehom, jambo hilo lilitabiriwa na Mei Lee lakini aliigiza kushangaa ili aonekane kwamba hakutarajia kupelekwa hapo na hata alipolekwa hakugundua kwamba kuna uhusiano wa aina yoyote na Leehom.
“Asante.” Akajibu Mei Lee.
“Najua labda unaona kila kitu hakifanani na jinsi ambavyo Yin amekueleza. Lakini ilivyo ni kwamba mimi ndiye mmiliki wa Beijing Furniter na nimependa kufanya kazi na wewe; ningependa utokee kwenye tangazo la fanicha za mtindo mpya ambazo tutaziingiza sokoni hivi karibuni.” Akafafanua kwa uzuri Leehom huku akijizungusha-zungusha kwenye kiti chake cha kunesanesa.
Kampuni ya Beijing Furniter ilikuwa chini yake, yeye ndiye alikuwa mmiliki mkuu na ndiye aliyekuwa na mamlaka ya kufanya vyovyote atakavyo, na ndiyo maana hata alikuwa na nguvu ya kumchagua Mei Lee katika tangazo hilo bila kupingwa na mtendaji yeyote aliyemuajiri.
Hata hivyo kumchagua Mei Lee hakukuwa ni bure-bure tu, isipokuwa moyo wa Leehom ulikuwa ukifurukutwa ndani kwa ndani na jambo fulani la kiutu uzima zaidi, jambo zito mno. Hata hivyo hakutaka kuruka hatua hata moja katika kulifanikisha, kwahiyo ili kuhakikisha ujumbe unafika mahala pake kwa utulivu na usahihi aliamua kuanzia mbali namna hiyo.
*****************************
 
SEHEMU YA 19



ILIPOISHIA...
Tuliona Mkuki na Mei Lee wamekutana na mtu mpya, anaitwa Leehom ambaye yeye ni mwanamuziki maarufu sana nchini China. Leehom anampenda kimapenzi Mei Lee na sasa anajitahidi kuonesha kumsaidia sana Mei Lee ili kumvutia.
ENDELEA...
Baada ya mazungumzo ya hapa na pale kuhusu lile tangazo Mei Lee alikubaliana na Leehom kwamba atafanya wakati bosi Leehom yeye aliahidi kumwaga pesa nyingi sana kwa mwanadada huyo kama malipo ya kazi hiyo.

Ili kutimiza ahadi, mara tu baada ya mazungumzo Leehom akanyanyua simu ya mezani na kumpigia Yin, akamuomba amuandalie Mei Lee hundi ya malipo ya kiasi kikubwa cha pesa na alipomaliza kutoa maagizo alimrudia Mei Lee.
“Tutatoka hapa nitakupeleka kwa watu watakaokutengezea nguo kwa ajili ya tangazo, na kesho kutwa asubuhi utapigwa picha za video za tangazo.” Akaeleza Leehom huku akionekana kujipa majukumu mengi ambayo hata hakuwahi kuyafanya kwa kazi nyingine za kufanana na hiyo zilizowahi kufanyika kipindi cha nyuma.
Baada ya pale Leehom alimchukua Mei Lee hadi kwenye gari ile ile waliyokuja nayo akiwa na Yin; na walikuwa wao wawili tu pamoja na dereva. Basi mwendo ukaanza kuelekea kwa mbunifu wa mitindo maarufu nchini China aitwaye Hannuo. Huko Mei Lee alifanyiwa vipimo kwa zaidi ya dakika 30 na baada ya hapo kazi ikawa imekamilika kwamba binti angeweza hata kurejea nyumbani.
Lakini Leehom hakutaka kuzitumia vibaya nafasi za kuwa karibu na Mei Lee namna hiyo, alihakikisha anautumia muda wake kwa ufasaha ili ikiwezekana atimize lengo lake ndani ya muda mfupi. Ili kufanikisha hilo alimuomba Mei Lee kwamba kabla hajamrejesha nyumbani ampelekee kwenye mgahawa, wapate mlo wa mchana wa pamoja kisha amrejeshe hotelini kwao; na kwa kuwa binti hakuwa akifahamu chochote, au labda kuhisi ile adhma ya Leehom alimkubalia kwa wepesi sana.
Basi Leehom akamtaka dereva awapeleke kwenye moja ya migahawa mikubwa ya jijini Beijing; mgahawa uitwao ‘Luminax’ ambao wenyewe ulikuwa ukishika nambari mbili kwa kupika vyakula vitamu sana na vya gharama kubwa. Huko Mei Lee alinunuliwa ‘msosi’ wa maana, chakula ambacho dhumuni lake kuu si kushiba tu, bali pia kufanyiza tafrija ndani ya kinywa cha mlaji.
Lakini haikuwa chakula tu, pia Leehom na Mei Lee walizungmza mengi mno, na kwa muda ule mfupi tu walianza kuhisi kuzoena sana hata wakajikuta soga walizokuwa wakipiga zilitawaliwa sana na vicheko vikubwa.
Baada ya yote hayo Leehom alimchukua Mei Lee na kumrejesha nyumabni, hakuwa akiendesha yeye gari hivyo hata njiani pia walipata nafasi ya kuzungumza mengi kwa uhuru pia.
**************************************
Muda uliyoyoma kwa Mkuki, alipigwa na sintofahamu kwa sababu kwa jinsi alivyokuwa akifikiria yeye ni kwamba zoezi lile lingefanyika mara moja kisha Mei Lee angerudishwa nyumbani, lakini mambo yalikuwa kinyume chake.
Wote wawili hawakuwa na simu hivyo haikuwa rahisi kumtafuta; mtoto wa kiume alibaki akiugulia maumivu ya wivu mle chumbani hata asijue nini cha kufanya.
Punde mlango ulifunguliwa, akaingia Mei Lee mwenye furaha kweli kweli. Akapita moja kwa moja hadi kitandani alipokuwa Mkuki, akamrukia na kumkumbatia na kumbusu huku akisema maneno ya kuthibitisha kwamba walikuwa wanaelekea kuachana na umaskini lakini mwenzake hata hakutaka kuwa mshabiki katika jambo hilo—yeye alikuwa akifikiria ni kwanini Mei Lee alichelewa sana kurejea nyumbani.
“Mbona umechelewa?” Akauliza Mkuki.
“Nilikwenda ofisini kwao, kumbe Leehom ndiye bosi wao, basi tukafanya mazungumzo pale, kisha Leehom akanichukua kwenda kupima nguo kwa ajili ya tangazo, halafu tukaenda kula, kisha akanirejesha hapa.” Akaeleza Mei Lee na kuongoza. “Mkuki, Leehom ni mtu safi sana. Nimekaa naye kwa muda mfupi tu lakini nimegundua hilo.” Akasema Mei Lee; yeye hakuwa akiona tatizo lolote juu ya kila kitu kilichokuwa kinaendelea.
Mkuki alibaki kimya huku akitafunwa na hasira ndani kwa ndani; maelezo na sifa alizozitoa Meu Lee juu ya Leehom zilimkera, zilimuumiza na kumfanya ahisi wivu uliopitiliza.
**************************************
Siku ya kutengeneza tangazo iliwadia, Mei Lee akafuatwa asubuhi na hata sik hiyo aliondoka peke yake bila Mkuki. Lakini leo mambo yalikuwa tofauti kwa Mkuki, hakuwa mwenye furaha kama ilivyokuwa siku ya kwanza Mei Lee alipofuatwa na Yin, na yote hiyo ni kwa sababu tayari alianza kuingiwa na uoga, alikuwa na mshaka kwamba huenda kulikuwa na maagano fulani ya siri kati ya mpenzi wake na Leehom.
Basi binti alichukuliwa hadi studio litakapofanyika zoezi za upigaji picha za video za tangazo, huko Leehom alikuwepo kama kawaida. Kazi ya uchukuaji picha hizo iligharimu saa tatu tu na huwezi kuamini kwamba Mei Lee alifanya vizuri mno kama ambavyo muelekezi (Director) alitaka iwe.
Baada ya pale Leehom alimchukua Mei Lee lakini kwa hiari; alimuomba kwa siku hiyo akamtembelee kwake, kwenye jumba lake jipya, si lile ambalo walikwenda akiwa na Mkuki; na kisha atamrejesha nyumbani.
Mei Lee hakuwa na tatizo juu ya hilo, kwa mtazamo wake yeye aliomuona Leehom kuwa ni mwanamume mkarimu sana mwenye lengo la kumsaidia kumvusha daraja la maisha—kutoka umasikini uliomlea kwenda utajiri anaouota.
Kutoka pale studio lilipokuwa likifanyika zoezi la uchukuaji picha za tangazo hadi nyumbani kwa Leehom ilikuwa ni safari ya dakika kumi na tano tu; jumba jipya la Leehom lilikuwa huko Henshuu, kitongoji ambacho kilikuwa ni makazi ya wanasiasa wakubwa, wasanii maarufu nchini China na wafanyabiashara mamilionea—binti alipelekwa huko. Nakwambia alichanganyikiwa na kila jumba alilokuwa akiliona, hata akashikwa na wasiwasi ya kwamba inawezekana ile ilikuwa ni safari ya kuelekea paradiso.
Punde gari yao ikasimama mbele jumba la Leehom; jumba kubwa la kifahari lililojengwa kwa mtindo unaowapendeza matajiri wengi nchini China. Jumba hilo lilivutia mno, liliupendeza moyo wa Mei Lee na hata macho pia kiasi kwamba alihisi kutamani kuwa mmiliki wa kasri lile kwa namna yoyote ile—hata kwa kupewa kama zawadi.
Basi baada ya pale lango kubwa la jumba hilo likafunguliwa, Leehom akaingiza gari yake ndani na kwenda kuituliza kwenye maegesho maalumu, kisha akateremka, akazunguka na kwenda kumfungulia mlango Mei Lee pia.
“Tumefika.” Akamwambia huku akiachia tabasamu kubwa.
Binti akateremka polepole huku bado akiendelea kushangaa huku na huko, Leehom akafunga mlango kisha akamshika mkono na kumuongoza kuelekea ndani zaidi ya jumba lile.
Walipoingia ndani ndo Mei Lee alizidi kupata wazimu, sebule ya jumba lile ilikuwa ni zuri hakika, ilikuwa na kila kitu chenye kupendeza macho na kumfanya mgeni ajihisi mwenye thamani kubwa kuwa pale.
“Karibu. Keti hapa.” Alisema Leehom kumwambia Mei Lee huku akimulekeza kwa mkono ni wapi pa kuketi. Binti akafanya kama alivyoombwa, akaketi taratibu huku bado akiigeza shingo yake huku na huko ili ayaridhishe macho.
Leehom naye akaketi, kisha baada ya pale alifanya npango wa wote wawili kupata kinywaji laini kwa ajili ya kusindikiza mazungunzo yao—alimuagiza kijakazi wake kuhakikisha hilo linfanikiwa.
Basi baada ya kuletewa vinywaji yalizungumzwa mengi sana siku ile lakini Leehom hakudiriki kuweka wazi hisia zake kwa Mei Lee. Alitaka kutumia vitendo tupu, au kama ni maneno basi yawe mwishoni sana, kipindi ambacho binti atakuwa tayari amegundua kila kitu kupitia matendo yake. Alikuwa akimpenda, tena mapenzi kweli, sio kumtamani au kumchezea, lengo lake lilikuwa ni kumuoa mara moja pindi tu binti atakapomuelewa na kumkubali.
Usiku uliingia, hapo ndipo Leehom aliamua kumchukua Mei Lee kwa ajili ya kumrejesha nyumbani. Walitoka hadi nje, hadi kwenye maegesho ya magari. Huko akachukua pikipiki kubwa ambalo alipanga kulitumia siku hiyo. Basi mwanamume akapanda, binti akapanda nyuma pia na kumshika kiuno Leehom huku akimlalia kidogo kwa mgongoni; si kwamba alidhamiria kufanya hivyo isipokuwa pikipiki lenyewe lilimlazimisha kwa jinsi ambavyo sehemu ya nyuma ya ilivyokuwa imeinuka—hapo wote wawili walikuwa wamevalia kofia ngumu kichwani.
Safari ikaanza, Leehom aliendesha kwa kasi kubwa sana kama ambavyo ilikuwa kawaida yake. Yeye alikuwa ni chizi wa vyombo vya moto, alipenda magari mazuri ya michezo na mapikipiki pia na ndiyo maana alikuwa akimiliki mashine hizo nyingi huku akizitumia kwa kuzibadilisha mara kwa mara.
Mwendo alioendesha ulifupisha mno safari, walifika nje ya hoteli aliyokuwa akiishi Mei lee na Mkuki, akasimamisha hapo na binti akateremka, kisha akavua na Helmet na kumkabidhi Leehom. Mwanamume akaipokea huku akimtazama jicho kavu Mei Lee, uso kwa uso bila kupepesa.
“Vipi?” Akauliza Leehom.
“Vipi vipi?” Akauliza Mei Lee huku akitabsamu.
“Kuna kitu nakiona... machoni mwako.”
“Kitu gani?”
Akashusha pumzi Leehom kabla ya kuzungumza. “Macho yako yanambia unataka niseme nilichokibeba moyoni.”
Akacheka kidogo Mei Lee. “Tufanye ni kweli.... Haya nataka kusikia ulichokibeba moyoni.” Akazungumza Mei Lee; yeye kila kitu alichukulia masihara kwa sababu walishazoeshana kutaniana namna hiyo.
“Natamani kukubusu kabla sijaondoka.” Akasema Leehom kwa kujiamini. Mei Lee akamtazma usoni asiamini kile alichokisikia, na si kile alichokisikia tu, bali kwa jinsi ambavyo Leehom alikizungumza kwa utulivu na hisia.
Hapo kimya kikachukua nafasi, kimya cha zaidi ya sekunde kumi. Si Mei Lee si Leehom, wote walivipa likizo vinywa vyao huku wakitazama machoni.
“Naweza?” Akaamua kuuliza Leehom, lakini binti hakumjibu.
Basi alichoamua ni kuteremka kwenye pikipiki, akaweka ‘helement’ yake aliyokuwa ameishika mkononi kwenye mkono wa kushoto wa ‘motosaiko’ hiyo kisha akapiga hatua mbili kumuelekea Mei Lee—wakawa umbali mdogo sana. Akamshika mikono yote miwili, akamtazama usoni kwa jicho lililonena, jicho lililozungumza yaliyomoyoni mwake hasa kuhusu lile ombi lake la kumbusu kabla ya kuondoka.
Basi taratibu Leehom alianza kujisogeza karibu na Mei Lee ili ambusu kinywani, binti aliishia kufumba macho tu, aliishiwa nguvu, alishindwa kupinga lolote juu ya kila kilichokuwa kinaendelea ingawa alikuwa akifahamu kwamba lile halikuwa ni jambo la kiungwana.
Lakini kabla hata ya Leehom hajafanikisha lengo alisukumwa ghafla na kuangukia huko; alikuwa ni Mkuki aliyefanya hivyo, kumbe alishuhudia kila kitu tangu Leehom na Mei Lee wanafika pale hotelini, alikuwa juu kwenye chumba chao, hivyo alitazama sinema nzima kupitia dirishani na sasa ndiyo alishuka chini kuja kuharibu mchezo
**************************************
 
SEHEMU YA 20

ILIPOISHIA...
Tuliona Mei Lee anarudishwa na Leehom kutoka kwenye kupiga picha za video za tangazo lakini akiwa amechelewa sana. Wanapofika Leehom anaomba kumbusu, lakini ghafla Mkuki anavamia na kuanzsha songombingo.

ILIKUWAJE...

Lakini huyu hakuwa Mkuki mtulivu yule unayemfahamu, alikuwa ni mkuki mwenye roho ya mbogo. Alikuja akiwa ni mwenye hasira na ghadhabu kweli kweli ya kuweza hata kuua mtu, hasira ambayo ilianzia ndani tumboni kwenye bandama na kupanda mpaka kooni—angeweza kufanya lolote kwa hali ile.
Basi kwa hasira hizo hizo alisogea karibu na pikipiki la Leehom, akalisukuma kwa mguu wake na likaanguka chini hata kioo cha pembeni (Side Mirror) kikavunjika; wakati huo Leehom ndiyo alikuwa akiamka pale chini alipoangukia baada ya kusukumwa.
Leehom akafanikiwa kunyanyuka kabisa, akasimama akijitazama mwili kwa mtindo wa kujikagua, kisha akajipangusa vumbi au chochote kile alichoona kinafaa kupanguswa kutoka mwilini mwake na baada ya hapo akaanza kumfuta taratibu Mkuki pale alipokuwa, na kwa jinsi alivyokuwa anakwenda Leehom, ilionekana waziwazi kwamba mpambano mkubwa ungeibuka kati yao.
Mkuki naye akajiweka tayari kwa lolote, alifahamu kwamba kama mwanaume alistahili kupigana mpaka hatua ya mwisho ili kuthibitisha uanaume wake. Hakutakaa kuwa mnyonge, aliamini katika msemo wa mtaani usemao ‘Pesa huna, nguvu huna, hata mkwara?’
Basi Leehom alizidi kumfuata Mkuki, lakini kabla hata hajamfikia, Mei Lee alichomoka pale alipokuwa na kwenda kusimama katikati yake yao akinyoosha mikono kama ishara ya kuwazuia. Leehom akawa muelewa, hakutaka kufanya kinyume na jinsi ambavyo Mei Lee alitaka na huenda alikubali kwa urahisi hivyo ili labda Mei Lee amuone kwamba ni mwanamume muelewa; Mkuki yeye bado alikuwa ni kama mbogo mwenye uwendawazimu, alifura kweli kweli huku akiropokwa maneno ya ovyo ambayo yalimkera hata Mei Lee pia.
“…usije ukafikiri mimi ni mjinga. Naweza nikakunyoosha hata kama upo kwenye ardhi ya mama yako.” Akabwata Mkuki.
“Kuninyoosha!? Unaweza? Unaweza nikuruhusu ufanye sasa hivi?” akauliza kwa dharau Leehom, tena polepole kana kwamba hawakuwa wakigombana.
“Sishindwi. Sina ninachoogopa kutoka kwako. Sijali kuhusu pesa zako wala umaarufu wako.”
“Unaigiza kijiamini sana, lakini kwa taarifa yako tu ni kwamba umewasha moto ambao hautazimika kwa namna yoyote ile.”
“Kuzimika? Hata mimi najua kwamba hautazimika kwa sababu kabla ya wewe kuuzima nitakuwa nimeshakuzima.” Akazidisha jeuri Mkuki.
Leehom akacheka kabla ya kujibu tena, “Hii vita unayoinzisha ni nyepesi sana, inatabarika mno, najua siwezi kushindwa kuwa mshindi ninapotupwa ulingo mmoja na nguruwe wa aina yako.”
“Washindi hawaongeiongei, wanashinda.” Akasema Mkuki, kisha kabla hata ya Leehom hajatoa neno la kumjibu Mei Lee akaingilia kati; si kwa kuzungumza, bali alimshika mkono Mkuki na kumuongoza kurudi hotelini—wakaondoka hivyo wakimuacha Leehom akiwatizama tu.
***************************
Ndani hakukukalika; Mkuki alihitaji majibu yaliyonyooka juu ya kile alichoshuhudia, na ingawa binti alimjibu lakini kilichosemwa aliona ni kama porojo za kumlanghai tu.
Aliongea maneno mengi sana mkuki juu ya lile tukio, hata mengine yalikuwa ni mbaya kuyasikia lakini tamati alikuwa mpole; aliamua kumsahamehe Mei Lee kwa sababu alikuwa akimfahamu uzuri, alijua kwamba hata kama alikuwa anafanya jambo mbaya ilikuwa ni kutokana na vishawishi, hivyo alimtaka kuwekeza nguvu nyingi kwenye mazoezi kwa ajili ya fainali ya shindano badala ya kupoteza muda mwingi akiwa karibu na Leehom.
Lakini asubuhi ya siku ya tukio lile magazeti yote yaliandika habari za ugomvi mkubwa kati ya Leehom na Mkuki ambao chanzo chake kilifahamika haraka kwamba walikuwa wakigombania mwananamke; yaani Mei Lee. Tena habari hiyo haikwenda kavu, bali na picha za tukio zilizopigwa kwa utaalamu wa hali ya juu huku picha ambayo ilitumika sana ikionyesha wakati ule Leehom aliposukumwa na Mkuki. Picha zote zilipigwa na mtu mmoja isipokuwa aliziuza kwa kila gazeti na alipata pesa nyingi sana kwa kuwa Leehom alikuwa ni mtu maarufu mno pale China.
Ile ikawa ni ‘skendo’ kubwa sana na huenda ilikuwa na madhara kwa watu wote watatu lakini hilo halikuwa rahisi kuonekana kwa mtu mwenye upeo wa kawaida. Watu wengi walidhani kwamba taarifa ile ililenga kumchafua Leehom kwa sababu tayari yeye alikuwa ni nembo ya Taifa la China.
Hata hivyo ni kama ilikuwa kweli, habari zile ilimuumiza sana Leehom kwa sababu baada ya kusambaa huku na huko kuna baadhi ya makampuni aliyokuwa akifanya nayo kazi kama balozi yalimpiga chini mara moja kwa madai kwamba kwa kile alichokifanya kilikuwa ni hatari kwa taswira ya makampuni hayo. Hapo sasa ndipo Leehom akaketi chini, meza moja na watu wake wa kazi ili kuangalia jinsi ya kutafuta utatuzi wa haraka wa sauala hilo kabla mambo hayajaoza kabisa.
***********************************
Usiku wa deni hauchelewi kucha, siku ya fainali ya yale mashindano iliwadia kana kwamba ni kufumba na kufumbua tu. Mashabiki waliolipa viingilio vikubwa walijazana ukumbini huku wengi wakiwa ni wapenzi wa dhati wa Mei Lee na muziki wake; na hii ilikuwa ni wazi kwamba binti alikuwa anakwenda kutwaa ushindi utakaobadilisha maisha yake kuanzia siku hiyo.
Mkuki alikuwepo pia ukumbini pamoja na adui yake Leehom; tena Leehom yeye alikuwepo hapo kama mgeni maalimu wa shindano ambaye ndiye atakayekuwa na jukumu la kumtangaza mshindi mara baada ya washiriki wote, akiwemo Mei Lee watakapotumia kete zao kwa kuimba kwa mara ya mwisho. Hata hivyo suala hilo la Leehom kumtangaza mshindi lilishapingwa na baadhi ya wataalamu wa mambo ya burudani wakidai kwamba litapunguza mvuto wa shindano kwa kuwa tayari Leehom alishaonekana kuwa na mtafaruku na baadhi ya mshiriki ambaye kwa namna moja ama nyingine anaonekana kuwa na dalili zote za kutawazwa mshindi. Lakini kila kitu kilishindikana kubadilishwa kwa sababu mgogoro wa Leehom na Mei Lee uliibua kipindi cha mwisho kuelekea fainali ya shindano hivyo mambo yaliachwa yaendelee kama yalivyopangwa.
Basi hakukuwa na cha kupoteza muda, mshiriki mmoja baada ya mwingine kati ya wale watano waliosalia alipanda jukwaani na kujaribu kuwashawishi mashabiki kwa mara ya mwisho kwamba alikuwa na uwezo mkubwa zaidi na alistahili kushinda.
Kila mshiriki alipewa fursa ya kuimba nyimbo tatu kwa siku hiyo, lakini ni kwa mtindo wa kuimba moja na kumpisha mshiriki mwingine hadi pale wote watakapotimiza hivyo vibao vitatu.
Kila Mei Lee alipopanda jukwwani shagwe zilitawala ukumbini, watu walisimama na kufatisha kila alichokiimba kuashiria ni jinsi gani alikuwa akiwakosha. Masaa mawili baadae kila msanii akawa ameshaimba nyimbo mbili na sasa ikawa ni zamu ya kutumia kete yao ya mwisho—kuimba wimbo wa tatu.
Wote wakaimba, na tamati ilikuwa ni zamu ya Mei Lee na alipanga kuimba wimbo aliouimba mara ya kwanza alipokuwa akitafuta nafasi ya kushiriki katika shindano hilo, wimbo alioutunga maalum kwa ajili ya Mkuki; wimbo wenye kubeba hisia nzito za mahaba alizonazo juu ya mwanaume huyo; wimbo uitwao RANGI YA HUBA.
Mashairi yake yalimkuna kila mtu pale ukumbini lakini sanasana ni kwa jinsi ambavyo mwenyewe aliimba, aliyatamka kwa ufundi maneno ya kwenye kila mstari wa shairi hilo kiasi kwamba masikio ya wote yalipenda kile kitu bila kuchoka. Mioyo ya mashabiki pale ukumbini ilitetemeshwa, walisikia raha mno kumsikia Mei Lee, ni kama sauti yake ilivujiza asali na maziwa masikioni mwao. Walitamani shindano lisiishe, na pia walitamani liwe shindano la mshiriki mmoja ambaye ni Mei Lee ili awaimbie yeye muda wote na si vinginenvyo.
Baada ya Mei Lee kumaliza kuimba hadhira ilitulizwa na maneno ya kuchombeza ya mshehereshaji wa onyesho lile, kisha Jaji Mkuu akapewa nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya majaji wenzake wawili na baada ya hapo mshehereshaji akamkaribisha mgeni maalum; Leehom kwa ajili ya kuja kumtangaza mshindi wa shindano.
Huo ulikuwa ndio wasaa mahususi kwa ajili ya kuthibitisha umahiri wa Mei lee na jinsi ambavyo alifanikiwa kuziteka roho za mashabiki kwa sababu iko wazi kwamba atakayetangazwa kuwa mshindi pale atatafsiriwa kama mtu aliyekuwa bora kwa kuimba zaidi ya washiriki wote. Na ilikuwa ni Mei Lee kwa sababu mpka hatua ya mwisho, kabla ya fainali kura zilionesha kwamba anaongoza, isipokuwa inapofikia siku ya fainali kura huwa ni siri, haziwekwi wazi tena hadi pale anapotangazwa mshindi.

**********************
 
SEHEMU YA 21


ILIPOISHIA...
Siku ya fainali imefika, washiriki wote akiwemo Mei Lee wamesharusha karata zao za mwisho, wameimba nyimbo tatu kila mmoja. Na sasa ni muda wa kutajwa mshindi, na kazi hiyo ya kumtaja mshindi inafanywa na Leehom.
ENDELEA....
Basi Leehom akapanda jukwani kuungana na washiriki wote watano, majaji na mshehereshaji, huku mkononi akiwa na karatasi yenye jina la washindi watatu kati ya wale watano pamoja na kipaza sauti. Alikuwa amevalia nadhifu mno siku hiyo—suti matata iliyobuniwa na mbunifu wa mavazi maarufu nchini humo aitwae Xiaomi. Watu walimshangilia mara tu alipopanda jukwaani kwa sababu hata yeye alikiwu ni kipenzi cha wapenda muziki wa nchini China, tena walimpenda zaidi ya ambavyo wanampenda Mei Lee sasa hivi.

“Habarini za jioni.” Akasalimu na baada ya kujibiwa akaendelea kwa ujumla, “Leo ni siku kubwa sana, siku kubwa kwa sisi kushuhudia ushindi wa wenzetu hawa walioshiriki shindano, lakini ni siku kubwa kwao kwa shuhudia ushindi walioupigania miaka nenda rudi. Kama ningetaka nisitumie maneno ningesema leo ni siku ya fainali, na maana ya fainali ni kumjua mshindi.
Kimsingi wote watano ni washindi, lakini kwa bahati ni kwamba karatasi niliyoishika hapa mkononi ina nafasi ya majina matatu tu. Kwanini nasema hivi? Nasema hivi kumaanisha kwamba hata kama wewe mshiriki mmoja hutatajwa humu bado una nafasi ya kutimiza ndoto zako kwa sababu hata mimi sikupitia mashindano ya hivi, lakini leo nina nafasi niliyokuwa nikiiota kuwa nayo.
Kama nilivyokwishasema, nina majina ya watu watatu hapa mkononi ambao ni mshindi wa kwanza, wa pili na watatu, na nitamtaja mshindi wa tatu, kisha wa pili na wa kwanza. Lakini kabla sijaanza kutaja nataka nikumbushe kitu kimoja kwamba; WASHINDI HAWAONGEI, WANASHIDA.” Akazungumza Leehom na watu wakashangilia kana kwamba walipenda sana kile alichokizungumza.
Basi Leehom akaanza kutaja majina, akaanza na mshindi wa tatu kama alivyofafanua mwanzo na hapo akaja mvulana aliyeshika nafasi hiyo. Watu wakamshangilia kwa kiasi chake wakati anatoka alipokuwa amesimama na washiriki wenzake pale jukwaani na kusogea karibu na majaji kwenda kupokea anachostahili—alipiga picha kadhaa na Leehom, na majaji wote ambao pia walikuwa pale jukwaani kisha zawadi atakayopata ikatangazwa hadharani kisha akasimama palepale jukwaani, karibu na majaji.
Kisha wapili pia akatajwa, mashabiki wakaangua shangwe kubwa ingawa hazikufikia kiasi cha ambavyo huwa wanamshangilia Mei Lee japo zilizidi shangwe alizopata mshindi wa tatu. Mshiriki huyu naye alikuwa ni mvulana, akasogea kwa majaji na kufanyiwa kama ilivyokuwa kwa mshindi wa tatu—yaani kupiga picha kisha mwishowe zawadi yake kutangazwa hadharani kisha akasimama karibu na majaji pia.
Sasa homa ikawavaa mashabiki ulipofika muda wa kumfahamu mshindi wa kwanza wa shidano hilo; kwa sababu nafasi ilibaki moja wakati bado Mei Lee na mtu aliyekuwana akimfuata kwa kura walikuwa hawajatajwa. Hii ni sawa na kusema kwamba, mmoja kati yao ni lazima atatoka kapa.
Leehom akapewa ruhusa ya kuendelea.
“Mshindi wa shindano letu kwa mwaka huu ni....” akazungumza Leehom, kisha akapiga kimya akiwatazama mashabiki kana kwamba alikuwa akiwauliza ‘mnanfahamu?’
Akaendelea.
“Mshindi ni…. Liu Kang.” Akasema kwa sauti kubwa na hapo ziliibuka shangwe za watu waliokuwa wakimkubali Liu Kang huku mashabiki wengine hasa wanaompenda Mei Lee wakishindwa kuamini kile kilichotokea—inakuwaje mshiriki ambaye alikuwa akionekana kukubalika zaidi amekosa hata nafasi ya tatu.
Zogo kubwa lilizuka papo hapo bila kuchelewa, mashabiki wa Mei Lee walianzsha fujo wakilaani vikali na kupinga matokeo yale kwa madai kwamba yalichakachuliwa. Fujo zikapamba moto kiasi kwamba sasa watu walianza kupigana kwa kurushiana chupa na kadhalikaka. Ilikuwa ni mshikeshike kweli kweli ambao pengine hakuna hata aliyetarajia, lakini kwa sababu waliuanzisha basi shetani naye akakamatia katikati yao.
Ilibidi askari wapewe taarifa wakati huo tayari walinzi wa kawaida walianza kutumia nguvu kutuliza zile ghasia na pia kuwalinda watu waliokuwa pale jukwani ili wasidhurike na walifanikiwa katika hilo kwa kuwatorosha majaji wote, washindi wa kwanza hadi wa tatu na Leehom pia ambaye kimsingi ndiye alikuwa amepaniwa zaidi na mashabiki wa Mei Lee .
Mkuki hakujihusisha na gomvi lolote kule alipokuwa, alitulia akiugulia maumivu yaliyosababishwa na kile kilichotokea. Roho ilimuuma sana kwa sababu alifahamu fika kwamba yale hayakuwa matokeo halisi kwa maana ya kwamba lazima kuna mchezo mchafu utakuwa umefanyika na bila shaka mpango huo uliratibiwa na Leehom kama sehemu ya vita aliyoitangaza mara baada ya kuibuka kwa mgogoro wao. Alipoteza matumaini hata alijikuta akijuta kuwa mjinga kiasi cha kukubali kuacha kazi yake kwenye mgahawa kule Hong kong ili amlete Mei lee kuja kushiriki shindano la kishenzi namna hii, shindano lisilozingatia misingi ya haki kabisa—na hapa sasa ndiyo alizidi kujiona ni mtu wa ‘fungu la kukosa’.
Mei Lee yeye ndiyo alishindwa hata kujizuia, alilia sana kwa sababu alikuwa na imani sawasawa na Mkuki. Aliamini kwamba ule ushindi ulikuwa wake, na si wa Liu Kang kama ilivyotangazwa, isipokuwa kile kilichotokea ilikuwa ni dhuluma iliyofanywa na Leehom akishirikiana na waratibu wa shindano hilo. Basi akiwa bado palepale jukwaani ghafla alianza kuhisi kizunguzungu; aliona ni kama dunia inarukaruka hivi, inakwenda mrama. Taratibu giza likaanza kuivaa nuru ya macho yake, miguu ikapoteza nguvu na uwezo wa kusimama na punde akaanguka chini kama mzigo, akazimika.

********************************
 
SEHEMU YA 22 ......... MWISHO

ILIPOISHIA...
Mei Lee yeye ndiyo alishindwa hata kujizuia, alilia sana kwa sababu alikuwa na imani sawasawa na Mkuki. Aliamini kwamba ule ushindi ulikuwa wake, na si wa Liu Kang kama ilivyotangazwa, isipokuwa kile kilichotokea ilikuwa ni dhuluma iliyofanywa na Leehom akishirikiana na waratibu wa shindano hilo. Basi akiwa bado palepale jukwaani ghafla alianza kuhisi kizunguzungu; aliona ni kama dunia inarukaruka hivi, inakwenda mrama. Taratibu giza likaanza kuivaa nuru ya macho yake, miguu ikapoteza nguvu na uwezo wa kusimama na punde akaanguka chini kama mzigo, akazimika.
SHUKA NAYO TARATIIIBUUU...
Fahamu zilimrejea Mei Lee saa tatu baadae na alipozinduka tu alijikuta amelazwa kitandani ndani ya chumba cha hospitali. Pembeni yake alikuwepo Leehom, ambaye mara tu alipogundua kuwa Mei Lee amerejewa na fahamu alimsogelea.

“Vipi? Unajisikiaje?”
“Mkuki. Mkuki yuko wapi?” Akauliza Mei Lee.
“Tulia kwanza, kila kiti kuhusu Mkuki utafahamu baadae.”
“Hapana. Sitaki. Nataka kumuona Mkuki sasa hivi.”
“Tulia kwanza.”
“Sitaki...” akasema Mei Lee huku akionesha kwa vitendo kwamba kweli alikuwa hataki kutulia; akataka kuinuka pale kitandani lakini Leehom alimzuia kabla hajafanya hivyo.
“Ngoja. Tulia. Mkuki huyupo.” Akasema Leehom huku akimtuliza Mei Lee kwa kumzuia asiinuke.
“Yuko wapi?”
“Amekamatwa.”
“Amekamatwa? Kwa Kosa gani"? Akahoji kwa mshangao Mei Lee.
Leehom akatulia kidogo kabla ya kijibu. “Kumbe alikuwa akiishi hapa bila kibali, na si unajua kuwa yeye si mchina wala Mthaiwan.” Akasema na hapo ndipo alizidi kumchanganya zaidi Mei Lee na nusura apoteze fahamu kwa mara nyingine.
Alichofikiria kwa haraka ni kwamba mara baada ya taarifa ile asingeweza tena kumuona Mkuki kwa sababu kwa kosa ambalo Leehom alimueleza ni wazi kuwa uhamiaji wangemrudisha Mkuki nchini kwao tu.
Kile alichokisema Leehom kilikuwa ni kweli tupu, lakini hata hivyo kila kitu kilikuwa ni mpango wake yeye mwenyewe kama sehemu ya kuhakikisha anashinda ile vita aliyoitangaza dhidi ya Mkuki. Aligundua kuwa si rahisi kwa Mkuki kuwa na kibali na hii kutokana na historia ya Mkuki aliyoipata kutoka kwa Mei Lee mwenyewe; alimsimulia kipindi kile walichokuwa na ukaribu. Leehom akatumia upungufu huo, akatoa taarifa uhamiaji na wao wakaishuhulikia mapema taarifa hiyo kwahiyo walipomkamata Mkuki walimchukua na kumfanyia mahojiano ambapo alieleza kila kitu, kwamba yeye alikuwa ni Mtanzania na hata alifikaje China. Hii ilikuwa ni sawa na kusema kwamba baada ya taarifa hiyo uhamiaji walifanya mawasiliano na ubalozi wa Tanzania nchini China ambao walifanya mpango wa kumrejesha nyumbani na hilo lilifanikiwa-- Mkuki alirejeshwa kwao.
“Nadhani watakuwa wameshamrejesha kwao” alieleza Leehom kumwambia Mei Lee ambaye kwa muda huo alikuwa ameshikwa na uchungu usiosemekana, uchungu ambao hakuna msamiati kutoka kwenye lugha yoyote ile yenye kuweza kuelezea. Aliona dunia na kila kilichomo ndani yake vimekosa kumjali, alihisi kuonewa na alitabiri jinsi ambavyo ataishi maisha ya masumbuko bila ya uwepo wa karibu wa Mkuki; mwanamume ambaye kwa mtazamo wake Mei Lee alikuwa ni mwenye vigezo vyote vya kuitwa SHUJAA. Mwanaume ambaye alimfanya aishi upande wa raha wa dunia, akampa kila kitu ilihali hakuwa na kitu, mwanaume aliyemfundisha mapenzi, aliyemfundisha kupenda na kupendwa, mwanaume alimuonyesha RANGI YA HUBA.
Alifikiria mengi akiwa pale lakini tamati alinyanyua kinywa chake na kuzungumza sentensi moja yenye maneno mawili tu ambayo ilikuwa ni swali kwa Leehom.
“Kwahiyo umeshinda?” Aliuliza hivyo Mei Lee.
“Kushinda nini?” Leehom akahoji. Hakuwa amelielewa swali kwa sababu lilikuja tofauti kulinganisha na mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea.
“Vita. Vita yako dhidi ya Mkuki.”
“Hapana. Sikuwa na vita naye. Nilishamsamehe.”
“Sawa. Naomba mniruhusu kutoka hapa.”
“Kutoka uende wapi? Afya yako bado haijatengemaa Mei Lee.”
“Niko vizuri.”
“Bado.”
“Lakini ni mimi. Mimi ndiye nahusika, ndiye nafahamu kuhusu Afya yangu, unasemaje siko vizuri wakati mwenyewe najiona niko sawa? Nataka kuondoka.” Akafoka Mei Lee lakini Leehom hakutaka kuonekana mwepesi, hakutaka kukubali kirahisi kila kilichosemwa na msichana huyo.
“Kwenda wapi?”
“Mbali. Mbali na wewe shetani, mshindi wa vita kwa njia za haramu.” Akang'aka kwa maneno makali namna hiyo ambayo yalimfanya Leehom apoe akimtazama Mei Lee kwa hasira za ndani kwa ndani.
“Lakini hupaswi kuzungumza hayo Mei Lee. Unatakiwa ufahamu hisia zangu. Unielewe. Nakupenda.” Akaropoka Leehom lakini Mei Lee aliishia kumtazama tu, wakatazamana kwa zaidi ya sekunde kumi kisha msichana akafungua kinywa chake kuzungumza sentensi fupi yenye maneno matatu tu.
“Nina mimba ya Mkuki.” alizungumza Mei Lee tena hapa akiwa na uso wenye kumaanisha kile alichokizungumza. Taarifa ile ilimuacha kinywa wazi Leehom ambaye alifanya hila zote ili kumpata Mei Lee. Alikuwa akimpenda sana lakini je ni kweli angeweza kuendelea kumpenda hata kama mwanamke huyo atakuwa na ujauzito wa Mkuki kama alivyoeleza.
Akandelea kuzungumza Mei Lee.
“Najua nia yako Leehom. Nafahamu kila kitu unachowaza kuhusu mimi. Najua umempoteza Mkuki ili nihamie katika dunia yako, lakini ukweli haitawezekana. Umemuondosha mtu mwenye moyo wangu, kwahiyo hata nikisema nikupende nitatumia akili. Nitakupenda kwa ujanja ujanja. Ahadi ulizokuwa ukinipa za kunisaidia kutimiza ndoto zangu si ngeni, yote hayo Mkuki alishayafanya, kwahiyo nguvu unazotumia ni kazi bure. Ni sawa na kumwaga sukari katikati ya bahari ili maji chumvi yafanane ladha na asali.”
Leehom aliganda kama sanamu, maneno ya Mei Lee yalimchoma mno kwa sababu alikuwa na matarajio makubwa juu ya msichana huyo na ndiyo maana alifanya figisu zote za kuhakikisha anampoteza Mkuki.
Basi baada ya pale Mei Lee alilazimisha kuondoka na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Hakurejea Thaiwan, alibaki pale pale China na aliendesha maisha yake kwa kuimba nyimbo mtaani ambapo wapita njia walimtunza sarafu ambazo alizichannganya na kupata pesa ya kutosha kumsukuma kimaisha. Lakini alifanya hivyo kwa wiki moja tu, baadae alipata mtu wa kumshika mkono, akamsaidia kurekodi nyimbo nyingi na alifanikiwa sana kimuziki ndani ya muda mfupi tu kwa sababu tayari alikuwa na kundi kubwa la mashabiki aliowavuna katika lile shindano la kusaka vipaji lilikuja kuharibiwa na hila za Leehom.
Mei Lee sasa akawa ni miongoni mwa wasanii wakubwa nchini China, wasanii wa kutumainiwa na taratibu akaanza kufika ‘level’ za Leehom. Alimfikia kabisa na akawa ni mpinzani wake mkubwa mno na hiyo ikaandika historia kubwa katika tasnia ya muziki nchini China.
Kuhusu mimba ya Mkuki ilikuwa ni kweli kabisa na Mei Lee aligundua hilo muda mrefu isipokuwa aliliweka akiba, alipanga kumwambia Mkuki siku ya fainali, baada ya yeye kutangazwa mshindi kwa sababu alikuwa na imani kubwa katika hilo.
Basi aliulea ujauzito huo lakini kwa masikitiko makubwa sana kwa sababu alijua kuwa mtoto wake atazaliwa, na hatokuja kumjua baba yake kwa sababu hata yeye hakuwa akijua alipo kwa kuwa kwa kipindi chote walichoishi na Mkuki hakuwai kufahamu mpenzi wake anatiokea wapi; si unakumbuka Mkuki alikuwa anaficha kila kitu kwa madai kwamba hana kumbukumbu yoyote ya anapotokea.
Kuna wakati Mei Lee alijaribu kufuatilia lakini alishindwa kabisa kupata jibu la uhakika, na hapo ndipo alipokata tamaa kabisa na kuamua kumshukuru Mungu tu kwa kila kilichotokea huku akijitahidi kumuombea sana mwanaume huyo huko alipo.


************************************
“Nilirudishwa nyumbani na kuendelea na maisha ya kifukara yaleyale niliyoyakimbia, hakuna kitu kilichobadilika, sanasana mambo yalizidi kuwa magumu, kwa sababu kwanza nilikuwa kama mgeni, sijui fursa ziko wapi na pia nilikuwa sina maisha ya amani kabisa kabisa. Watu wananidhihaki kwamba nilizamia lakini nimerudi sina kitu, lakini ndo ukweli, kwahiyo sina sababu ya kuwachukia, labda nijichukie mimi na maamuzi yangu niliyoyafanya.” Anaeleza mzee Mkuki Salum Goigoi. Hapa akiwa katika kituo cha redio akifanyiwa mahojiano ya moja kwa moja juu ya ile safari ya maisha aliyopitia-- hii ni baada ya miaka takribani 20 tangu kutokea kwa tukio lile.
“Bado unaikumbuka sura ya Mei Lee? Yaani unaweza kutuambia alikuwa anaonekanaje?” mtangazaji anamuuliza.
“Hapana, sio rahisi kukumbuka kiasi cha kuweza kumuelezea alikuwaje; lakini kwa kifupi alikuwa ni mzuri, mrembo. Isipokuwa kitu kimoja kutoka kwake ndo siwezi kukisahau.”
“Kitu gani?”
“Sauti yake. Sauti ya Mei Lee bado ipo masikioni mwangu. Nikilala, nikiamka, nikitembea, popote huwa naisikia. Mungu alinipa tuzo kumpata yule mwanamke.” Anashindwa kuendelea kuzungumza mzee Mkuki, anahisi uchungu sana, na kooni ni kama amemeza chuma cha moto kinachoteremka taratibu kwenda tumboni. Anaanza kulia kwa kugugumia.
“Okey. Msikilizaji mzee Mkuki anashindwa kuendelea kuzungumza. Naomba tupate mapumziko mafupi kutoka kwa mdhamini, ili na yeye apate muda wa kutulia, tutakoporejea ataendelea kutueleza mengi zaidi kuhusu hii safari ya maisha aliyopitia. Tutarejea.”
******************************

MWISHO

MWISHO WA MSIMU WA KWANZA WA RIWAYA YA SAUTI YAKE MASIKIONI MWANGU; JIANDAE KWA MSIMU WA PILI AMBAO UTAKUJA NA MAJIBU YA MASWALI YAKO YOTE ULIYOBAKI NAYO. UTAFAHAMU MAISHA YA MUZIKI NA UMAARUFU YA MEI LEE, UTAFAHAMU KUHUSU MIMBA YAKE NA HATA KUHUSU MTOTO IKIWA ALIZALIWA AU LAA! NA JE KAMA ALIZALIWA VIPI KUHUSU BABA YAKE, ATAISHI MIAKA YOTE BILA KUMFAHAMU? NA KAMA ATAMFAHAMU ATAKUWA ALIPITIA NJIA GANI KUFANIKISHA HILO.
 
ASANTE KWA KUTUUNGA MKONO SISI PAMOJA NA MWANDISHI/MTUNZI WA RIWAYA.


Riwaya hii imeletwa kwenu na BURE SERIES
 
Simulizi Zinazorushwa na BURE SERIES

1. Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Kurudi Kwa Moza

2. Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad
Bonyeza hapa chini kusoma
Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

3.Simulizi: Nini maana ya mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Nini maana ya mapenzi

4. Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi

5. Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

6. RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu
Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu

7. NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)

🔥 🔥 🔥 NEW🔥🔥🔥

8. RIWAYA: Mume Gaidi

Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Mume Gaidi

9. STORY: Sitaki Tena

Bonyeza hapa chini kusoma
STORY: Sitaki Tena

10. Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)

Bonyeza hapa chini kusoma
Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom