RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu

SEHEMU YA 22 ......... MWISHO

ILIPOISHIA...
Mei Lee yeye ndiyo alishindwa hata kujizuia, alilia sana kwa sababu alikuwa na imani sawasawa na Mkuki. Aliamini kwamba ule ushindi ulikuwa wake, na si wa Liu Kang kama ilivyotangazwa, isipokuwa kile kilichotokea ilikuwa ni dhuluma iliyofanywa na Leehom akishirikiana na waratibu wa shindano hilo. Basi akiwa bado palepale jukwaani ghafla alianza kuhisi kizunguzungu; aliona ni kama dunia inarukaruka hivi, inakwenda mrama. Taratibu giza likaanza kuivaa nuru ya macho yake, miguu ikapoteza nguvu na uwezo wa kusimama na punde akaanguka chini kama mzigo, akazimika.
SHUKA NAYO TARATIIIBUUU...
Fahamu zilimrejea Mei Lee saa tatu baadae na alipozinduka tu alijikuta amelazwa kitandani ndani ya chumba cha hospitali. Pembeni yake alikuwepo Leehom, ambaye mara tu alipogundua kuwa Mei Lee amerejewa na fahamu alimsogelea.

“Vipi? Unajisikiaje?”
“Mkuki. Mkuki yuko wapi?” Akauliza Mei Lee.
“Tulia kwanza, kila kiti kuhusu Mkuki utafahamu baadae.”
“Hapana. Sitaki. Nataka kumuona Mkuki sasa hivi.”
“Tulia kwanza.”
“Sitaki...” akasema Mei Lee huku akionesha kwa vitendo kwamba kweli alikuwa hataki kutulia; akataka kuinuka pale kitandani lakini Leehom alimzuia kabla hajafanya hivyo.
“Ngoja. Tulia. Mkuki huyupo.” Akasema Leehom huku akimtuliza Mei Lee kwa kumzuia asiinuke.
“Yuko wapi?”
“Amekamatwa.”
“Amekamatwa? Kwa Kosa gani"? Akahoji kwa mshangao Mei Lee.
Leehom akatulia kidogo kabla ya kijibu. “Kumbe alikuwa akiishi hapa bila kibali, na si unajua kuwa yeye si mchina wala Mthaiwan.” Akasema na hapo ndipo alizidi kumchanganya zaidi Mei Lee na nusura apoteze fahamu kwa mara nyingine.
Alichofikiria kwa haraka ni kwamba mara baada ya taarifa ile asingeweza tena kumuona Mkuki kwa sababu kwa kosa ambalo Leehom alimueleza ni wazi kuwa uhamiaji wangemrudisha Mkuki nchini kwao tu.
Kile alichokisema Leehom kilikuwa ni kweli tupu, lakini hata hivyo kila kitu kilikuwa ni mpango wake yeye mwenyewe kama sehemu ya kuhakikisha anashinda ile vita aliyoitangaza dhidi ya Mkuki. Aligundua kuwa si rahisi kwa Mkuki kuwa na kibali na hii kutokana na historia ya Mkuki aliyoipata kutoka kwa Mei Lee mwenyewe; alimsimulia kipindi kile walichokuwa na ukaribu. Leehom akatumia upungufu huo, akatoa taarifa uhamiaji na wao wakaishuhulikia mapema taarifa hiyo kwahiyo walipomkamata Mkuki walimchukua na kumfanyia mahojiano ambapo alieleza kila kitu, kwamba yeye alikuwa ni Mtanzania na hata alifikaje China. Hii ilikuwa ni sawa na kusema kwamba baada ya taarifa hiyo uhamiaji walifanya mawasiliano na ubalozi wa Tanzania nchini China ambao walifanya mpango wa kumrejesha nyumbani na hilo lilifanikiwa-- Mkuki alirejeshwa kwao.
“Nadhani watakuwa wameshamrejesha kwao” alieleza Leehom kumwambia Mei Lee ambaye kwa muda huo alikuwa ameshikwa na uchungu usiosemekana, uchungu ambao hakuna msamiati kutoka kwenye lugha yoyote ile yenye kuweza kuelezea. Aliona dunia na kila kilichomo ndani yake vimekosa kumjali, alihisi kuonewa na alitabiri jinsi ambavyo ataishi maisha ya masumbuko bila ya uwepo wa karibu wa Mkuki; mwanamume ambaye kwa mtazamo wake Mei Lee alikuwa ni mwenye vigezo vyote vya kuitwa SHUJAA. Mwanaume ambaye alimfanya aishi upande wa raha wa dunia, akampa kila kitu ilihali hakuwa na kitu, mwanaume aliyemfundisha mapenzi, aliyemfundisha kupenda na kupendwa, mwanaume alimuonyesha RANGI YA HUBA.
Alifikiria mengi akiwa pale lakini tamati alinyanyua kinywa chake na kuzungumza sentensi moja yenye maneno mawili tu ambayo ilikuwa ni swali kwa Leehom.
“Kwahiyo umeshinda?” Aliuliza hivyo Mei Lee.
“Kushinda nini?” Leehom akahoji. Hakuwa amelielewa swali kwa sababu lilikuja tofauti kulinganisha na mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea.
“Vita. Vita yako dhidi ya Mkuki.”
“Hapana. Sikuwa na vita naye. Nilishamsamehe.”
“Sawa. Naomba mniruhusu kutoka hapa.”
“Kutoka uende wapi? Afya yako bado haijatengemaa Mei Lee.”
“Niko vizuri.”
“Bado.”
“Lakini ni mimi. Mimi ndiye nahusika, ndiye nafahamu kuhusu Afya yangu, unasemaje siko vizuri wakati mwenyewe najiona niko sawa? Nataka kuondoka.” Akafoka Mei Lee lakini Leehom hakutaka kuonekana mwepesi, hakutaka kukubali kirahisi kila kilichosemwa na msichana huyo.
“Kwenda wapi?”
“Mbali. Mbali na wewe shetani, mshindi wa vita kwa njia za haramu.” Akang'aka kwa maneno makali namna hiyo ambayo yalimfanya Leehom apoe akimtazama Mei Lee kwa hasira za ndani kwa ndani.
“Lakini hupaswi kuzungumza hayo Mei Lee. Unatakiwa ufahamu hisia zangu. Unielewe. Nakupenda.” Akaropoka Leehom lakini Mei Lee aliishia kumtazama tu, wakatazamana kwa zaidi ya sekunde kumi kisha msichana akafungua kinywa chake kuzungumza sentensi fupi yenye maneno matatu tu.
“Nina mimba ya Mkuki.” alizungumza Mei Lee tena hapa akiwa na uso wenye kumaanisha kile alichokizungumza. Taarifa ile ilimuacha kinywa wazi Leehom ambaye alifanya hila zote ili kumpata Mei Lee. Alikuwa akimpenda sana lakini je ni kweli angeweza kuendelea kumpenda hata kama mwanamke huyo atakuwa na ujauzito wa Mkuki kama alivyoeleza.
Akandelea kuzungumza Mei Lee.
“Najua nia yako Leehom. Nafahamu kila kitu unachowaza kuhusu mimi. Najua umempoteza Mkuki ili nihamie katika dunia yako, lakini ukweli haitawezekana. Umemuondosha mtu mwenye moyo wangu, kwahiyo hata nikisema nikupende nitatumia akili. Nitakupenda kwa ujanja ujanja. Ahadi ulizokuwa ukinipa za kunisaidia kutimiza ndoto zangu si ngeni, yote hayo Mkuki alishayafanya, kwahiyo nguvu unazotumia ni kazi bure. Ni sawa na kumwaga sukari katikati ya bahari ili maji chumvi yafanane ladha na asali.”
Leehom aliganda kama sanamu, maneno ya Mei Lee yalimchoma mno kwa sababu alikuwa na matarajio makubwa juu ya msichana huyo na ndiyo maana alifanya figisu zote za kuhakikisha anampoteza Mkuki.
Basi baada ya pale Mei Lee alilazimisha kuondoka na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Hakurejea Thaiwan, alibaki pale pale China na aliendesha maisha yake kwa kuimba nyimbo mtaani ambapo wapita njia walimtunza sarafu ambazo alizichannganya na kupata pesa ya kutosha kumsukuma kimaisha. Lakini alifanya hivyo kwa wiki moja tu, baadae alipata mtu wa kumshika mkono, akamsaidia kurekodi nyimbo nyingi na alifanikiwa sana kimuziki ndani ya muda mfupi tu kwa sababu tayari alikuwa na kundi kubwa la mashabiki aliowavuna katika lile shindano la kusaka vipaji lilikuja kuharibiwa na hila za Leehom.
Mei Lee sasa akawa ni miongoni mwa wasanii wakubwa nchini China, wasanii wa kutumainiwa na taratibu akaanza kufika ‘level’ za Leehom. Alimfikia kabisa na akawa ni mpinzani wake mkubwa mno na hiyo ikaandika historia kubwa katika tasnia ya muziki nchini China.
Kuhusu mimba ya Mkuki ilikuwa ni kweli kabisa na Mei Lee aligundua hilo muda mrefu isipokuwa aliliweka akiba, alipanga kumwambia Mkuki siku ya fainali, baada ya yeye kutangazwa mshindi kwa sababu alikuwa na imani kubwa katika hilo.
Basi aliulea ujauzito huo lakini kwa masikitiko makubwa sana kwa sababu alijua kuwa mtoto wake atazaliwa, na hatokuja kumjua baba yake kwa sababu hata yeye hakuwa akijua alipo kwa kuwa kwa kipindi chote walichoishi na Mkuki hakuwai kufahamu mpenzi wake anatiokea wapi; si unakumbuka Mkuki alikuwa anaficha kila kitu kwa madai kwamba hana kumbukumbu yoyote ya anapotokea.
Kuna wakati Mei Lee alijaribu kufuatilia lakini alishindwa kabisa kupata jibu la uhakika, na hapo ndipo alipokata tamaa kabisa na kuamua kumshukuru Mungu tu kwa kila kilichotokea huku akijitahidi kumuombea sana mwanaume huyo huko alipo.


************************************
“Nilirudishwa nyumbani na kuendelea na maisha ya kifukara yaleyale niliyoyakimbia, hakuna kitu kilichobadilika, sanasana mambo yalizidi kuwa magumu, kwa sababu kwanza nilikuwa kama mgeni, sijui fursa ziko wapi na pia nilikuwa sina maisha ya amani kabisa kabisa. Watu wananidhihaki kwamba nilizamia lakini nimerudi sina kitu, lakini ndo ukweli, kwahiyo sina sababu ya kuwachukia, labda nijichukie mimi na maamuzi yangu niliyoyafanya.” Anaeleza mzee Mkuki Salum Goigoi. Hapa akiwa katika kituo cha redio akifanyiwa mahojiano ya moja kwa moja juu ya ile safari ya maisha aliyopitia-- hii ni baada ya miaka takribani 20 tangu kutokea kwa tukio lile.
“Bado unaikumbuka sura ya Mei Lee? Yaani unaweza kutuambia alikuwa anaonekanaje?” mtangazaji anamuuliza.
“Hapana, sio rahisi kukumbuka kiasi cha kuweza kumuelezea alikuwaje; lakini kwa kifupi alikuwa ni mzuri, mrembo. Isipokuwa kitu kimoja kutoka kwake ndo siwezi kukisahau.”
“Kitu gani?”
“Sauti yake. Sauti ya Mei Lee bado ipo masikioni mwangu. Nikilala, nikiamka, nikitembea, popote huwa naisikia. Mungu alinipa tuzo kumpata yule mwanamke.” Anashindwa kuendelea kuzungumza mzee Mkuki, anahisi uchungu sana, na kooni ni kama amemeza chuma cha moto kinachoteremka taratibu kwenda tumboni. Anaanza kulia kwa kugugumia.
“Okey. Msikilizaji mzee Mkuki anashindwa kuendelea kuzungumza. Naomba tupate mapumziko mafupi kutoka kwa mdhamini, ili na yeye apate muda wa kutulia, tutakoporejea ataendelea kutueleza mengi zaidi kuhusu hii safari ya maisha aliyopitia. Tutarejea.”
******************************

MWISHO

MWISHO WA MSIMU WA KWANZA WA RIWAYA YA SAUTI YAKE MASIKIONI MWANGU; JIANDAE KWA MSIMU WA PILI AMBAO UTAKUJA NA MAJIBU YA MASWALI YAKO YOTE ULIYOBAKI NAYO. UTAFAHAMU MAISHA YA MUZIKI NA UMAARUFU YA MEI LEE, UTAFAHAMU KUHUSU MIMBA YAKE NA HATA KUHUSU MTOTO IKIWA ALIZALIWA AU LAA! NA JE KAMA ALIZALIWA VIPI KUHUSU BABA YAKE, ATAISHI MIAKA YOTE BILA KUMFAHAMU? NA KAMA ATAMFAHAMU ATAKUWA ALIPITIA NJIA GANI KUFANIKISHA HILO.

Safi sana... Bonge la story...

Chapter Closed...



Cc: mahondaw
 
Riwaya ya Kijasusi: SAUTI YAKE MASIKIONI MWANGU
Mwandishi: KELVIN KAGAMBO
Imeletwa Kwenu na: BURE SERIES


SEHEMU YA 1

“..... na sasa ni zamu yako. Sali sala za mwisho tufunge mkataba.”

“Lakini braza Jisu haya yote yanatoka wapi? Kosa langu nini?”

“Unaleta dharau sio? Hujui kosa lako au unauliza kutafuta faida? Sikia Mkuki, mimi sio Jisu yule unayemfahamu, halafu hii kazi ni lazima itimie, lazima nikuue.” Akazungumza kwa msisitizo mwanaume huyo aitwaye Jisu; mrefu, mweusi mwenye mwili wa mazoezi; upara kichwani na sharafa nene zilizoungana kidevuni kutokea chini ya kila sikio lake.


Kisha akaikamata barabara bastola iliyokuwa mkononi mwake, akamuelekezea Mkuki ambaye kwa muda huo alikuwa amepiga magoti mbele ya Jisu. Akavuta pumzi zake kwa kuhesabu moja mpaka tatu ili kujiongezea ujasiri. Akatumbukiza kidole cha shahada cha mkono wake kwenye ‘trigga’ ya bastola kisha akaanza kubofya taratibu.

“Paaaaa!” Mlio mkubwa wa risasi ulisikika nama hiyo, lakini kabla hata shambulio hilo halijafanikiwa Mkuki alikurupuka kutoka usingizini na kuikata ndoto ile mbaya yenye kutisha.

Akaketi kitandani huku akitweta na kutokwa jasho mithili ya mtu aliyelowa mvua ya manyunyu. Akajipa sekunde kadhaa kuirejesha akili yake duniani na alipofanikiwa katika hilo alishusha pumzi ndefu ya kushukuru kwamba lile halikuwa tukio halisi.

Ghafla akashituka; aligundua kitu kipya ambacho hakikuwa cha kawaida—aling’amua kwamba alikuwa kwenye chumba asichokifahamu kabisa, yaani hakuwahi kuwa hapo kabla.

Kilikuwa ni chumba chenye ukubwa wa chumba cha kawaida cha kulala, kuta zote za chumba hicho zilipakwa chokaa huku kitanda na meza ndogo vikiwa ni vitu pekee vilivyomo ndani.

‘Niko wapi?’ Likawa ni swali la kwanza kugonga kichwani mwa Mkuki. Hapo akajipa muda kuvuta kumbukumbu ya kila alichopitia kabla ya kuwa pale chumbani na hakika ubongo wake ulimsitiri, alikumbuka kila kitu.

Alikumbuka watu wawili aliokuwa nao mara ya mwisho, akakumbuka ajali mbaya aliyoipata akiwa na watu hao, pia alikumbuka kwamba ajali ile ilisababishwa na mlipuko mkubwa wa bomu.

‘Au nimesaidiwa?’ akajiuliza Mkuki ‘Lakini ngonja, ngoja nione.’ Akajipa moyo wa kusubiri na hamasa ya kufanya udadisi.

Basi akateremka kutoka pale kitandani; alihisi maumivu mwilini lakini hayakumzuia kutembea kuelekea mlangoni. Lakini kabla hata hajafikia lengo mlango ulifunguliwa, akaingia mwanamke mmoja aliyekuwa akiimba kwa sauti ya juu iliyoashiria uhuru mkubwa alionao, lakini ghafla mwanamke huyo aliacha kuimba mara tu alipomuona Mkuki.

Alikuwa ni mwanamke wa ki-Asia, msichana mfupi, mwembamba, mweupe mwenye nyelwe ndefu na nyingi zilizoficha uso wake wote ingawa hilo halikumzuia kuona mbele.

“Umeamka?” Akauliza mwanamke huyo, lakini kwa lugha ambayo Mkuki hakuilewa, lugha yenye kufanana kabisa na Kichina.

“We ni nani?” Mkuki naye akamtupia swali kwa lugha adhimu ya Kiswahili huku akirudi nyuma taratibu.

“Tulia. Kaa kitandani.” Yakamtoka kwa upole yule msichana, tena kwa lugha ile ile yenye kukanganya masikioni mwa Mkuki.

“Wewe nani na niko wapi hapa?”

“Tulia. Rudi kitandani. Bado hujapona, utajitonesha.” Akasema msichana huyo lakini kwa sababu ya mgongano wa lugha kati yao ilikuwa ni kama anatwanga maji kwenye kinu.

Akanyamaza kidogo yule msichana, akamtazama Mkuki kana kwamba kuna kitu alikuwa akifikiria juu yake kisha akapaza sauti kumuita mtu ambaye bila shaka hakuwa mbali na chumba kile.

“Babaaaa....” Aliita hivyo na sauti ya kiume kutoka nje ikamuitikia.
“Njoo. Amaeamka.” Akasema binti.

Punde mlango ukafunguliwa, akaingia mzee ambaye kwa mtazamo wa haraka Mkuki alijiridhisha kwamba babu huyo alikuwa ni Mchina. Alikuwa ni mzee wa kati ya miaka 60 na 70; mfupi, mwembamba, mweupe, mwenye mvi kichwa kizima na macho madogodogo ya kuvimba.

“Umeamka?” Akauliza mzee huyo kwa lugha ile ile iliyokuwa ikitumiwa na yule msichana, kisha kabla ya kupewa jibu alimfuata Mkuki, akamshika mkono na kumchukua hadi kitandani, akamkalisha.

“Unajisikiaje?” Akauliza yule mzee lakini kwa jinsi ambavyo Mkuki alikuwa akimtazama akagundua fika kwamba kulikuwa na kikwazo cha lugha kati yao.

“Hunielewi? Huzungumzi Kithaiwan?” Akamuuliza lakini bado aliambulia jibu la ukimya.

Akamgeukia yule msichana. “Haelewi.” Akamwambia. Kisha akamgeukia tena Mkuki. “Unaitwa nani?” Akamuuliza; hapa akijitahidi kutumia na vitendo kutafsiri swali lake.

Mkuki akamuelewa lakini pia tayari alishagundua kwamba watu wale hawakuwa na lengo baya juu yake.

“Mkuki. Naitwa Mkuki.” Akajibu.

“Nani?.”

“Mkuki.” Akajibu kwa msisitizo.

“Mkuki?” Akauliza yule mzee kuthibitisha.

“Ndiyo.” Akajibu huku akitingisha kichwa kukubali.

“Ooooh! Mimi ni Wong,” akajitambulisha yule mzee na kuongozea. “Na yule ni Mei Lee.” Akamtambulisha na yule msichana.

“Sisi tumekuokota ufukweni. Tumekusaidia. Unaweza kutuambia unatokea wapi?” Akahoji yule mzee lakini Mkuki alibaki akitumbua macho tu kama ishara ya kwamba hakuwa akimulewa, labda tu pale alipojitambulisha yeye pamoja na yule msichana.

“Baba? Hakuelewi. Tumpe muda.” Akazungumza yule msichana ambaye muda wote sura yake ilikuwa imefunikwa kwa nywele zake ngingi na ndefu.

“Sawa. Simama. Twende.” Akasema yule mzee aliyejitambulisha kwa jina moja la Wong huku akisindikiza sentesi yake kwa vitendo, Mkuki akamuelewa, akasimama na kuanza kumfuata kuelekea nje.

**************************************
Mkuki Salum Goigoi ndilo jina lake halisi, kijana aliyezaliwa na kukulia nchini Tanzania. Hadi mwaka huo 1998 alikuwa na umri wa miaka 23 duniani ingawa haikuwa rahisi kugundua hilo kwa kumtazama; alikuwa akionekana mkubwa zaidi na amekomaa kwelikweli.

Ni mwembamba wa kukonda, mrefu, mweusi mwenye uso wa duara wenye kufanyiza upole fulani unapomtazama; ingawa si kweli kwamba amejaaliwa haiba hiyo.

Kichwa chake kilibeba kumbukumbu za yote yanayomuhusu; yaani alipotoka; kilichotokea; yeye ni nani na mengineyo lakini juu ya yote hayo alinuwia kutowaambia wenyeji wake ukweli wowote na hii ni kwa sababu alikuwa anataka kukwepa kurejeshwa nchini Tanzania.

Hapo alikuwa nchini Thaiwan; taifa dogo ambalo ardhi yake yote ni kisiwa. Nchi ambayo ipo barani Asia, katikati ya China na taifa la Taiwan.
Wathaiwan walikuwa wakifanana kwa kiasi kikubwa sana na Wachina; kimuenekano, kitamaduni na hata itikadi. Wenyeji wa Mkuki walikuwa wakiishi Mkoa wa Shenghei katika kijiji kiitwacho Chensuua; kijiji ambacho wakazi wake walikuwa wakiishi kwa kutegemea shughuli za uvuvi kwa kiasi kikubwa.

Basi kwa siku chache za awali Mkuki aliishi na wenyeji wake kama mtu asiyekumbuka lolote; alijitengenezea mazingira hayo ili wenyeji wake wasipate sababu ya kumrejesha alipotoka; lengo lake ilikuwa ni kulowea palepale.

Kwa siku tano tu za awali alitambulishwa kwa vijana wenzake; kazi hiyo aliifanywa na mzee Wong ili kumsaidia Mkuki kujifunza jinsi ya kuishi kwa kuendana na taratibu zao za maisha ikiwemo kuifahamu lugha kwa urahisi na mambo mengine.

Katika hilo Mkuki alipata changamoto kubwa ya ubaguzi; yaani ingawa vijana walimkubali wakati anatambulishwa kwao lakini hawakutaka kuwa karibu naye—hilo lilifanywa nyuma ya mzee Wong, walimbagua Mkuki kwa sababu ya rangi.

Lakini Maufeng aliamua kuwa tofauti ya vijana wote wa kijijini Chensua—huyu yeye alikuwa ni mvualana wa Kithaiwan ambaye ni pekee aliyekubali kujenga ukaribu na Mkuki ingawa pia kulikuwa na sababu iliyomsukuma kufanya hivyo.

Maufeng yeye alikuwa na matatizo ya akili yanayompelekea kuwa mwendawazimu kabisa kwa kipindi fulani, hivyo vijana wengi walimtenga pia ingawa tatizo lake halikuwa likitokea mara kwa mara.

Maufeng akawa ni mtu wa tatu muhimu kwa ajili ya maisha ya mkuki pale ugenini, yaani ukiwajumuisha mzee Wong na binti yake Mei Lee.

******************************

Wiki mbili za Mkuki ndani ya Thaiwan zilikatika. Sasa taratibu alionekana kuanza kuifahamu lugha ingawa si kwa kiasi kikubwa, na msaada wa nguvu aliupata kutoka kwa Maufeng na mzee Wong, lakini Mei Lee—yule binti wa mzee Wong hakuwa katika orodha hiyo.

Ukweli ni kwamba Mei Lee hakuwa ni msichana wa kawaida; alikuwa ni mpole na kimya kupita maelezo na ili kuthubitisha hiko fikiria suala hili, kwamba tangu Mkuki aanze kuishi kwao hawajawahi kukaa pamoja na kupiga soga ingawa wote walikuwa ni vijana wanaorandana umri. Wala Mei Lee hakuwa na rafiki, jambo pekee alilokuwa akilifanya muda mwingi ni kuimba nyimbo zake mwenyewe na hakika alikukuwa ni mwanamuziki mzuri aliyejaaliwa sauti murua.

Yote tisa; kubwa zaidi ni kwamba kwa kipindi chote hicho cha wiki mbili cha Mkuki kuwa pale hakuwahi kuona sura ya binti huyo, muda wote aliifunika kwa nywele zake kama mtu anayeficha kitu fulani.
View attachment 1493765
Iko pouwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom