RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000

Riwaya ya Kijasusi: SAUTI YAKE MASIKIONI MWANGU
Mwandishi: KELVIN KAGAMBO
Imeletwa Kwenu na:
PSEUDEPIGRAPHAS

SEHEMU YA 1


“..... na sasa ni zamu yako. Sali sala za mwisho tufunge mkataba.”

“Lakini braza Jisu haya yote yanatoka wapi? Kosa langu nini?”

“Unaleta dharau sio? Hujui kosa lako au unauliza kutafuta faida? Sikia Mkuki, mimi sio Jisu yule unayemfahamu, halafu hii kazi ni lazima itimie, lazima nikuue.” Akazungumza kwa msisitizo mwanaume huyo aitwaye Jisu; mrefu, mweusi mwenye mwili wa mazoezi; upara kichwani na sharafa nene zilizoungana kidevuni kutokea chini ya kila sikio lake.


Kisha akaikamata barabara bastola iliyokuwa mkononi mwake, akamuelekezea Mkuki ambaye kwa muda huo alikuwa amepiga magoti mbele ya Jisu. Akavuta pumzi zake kwa kuhesabu moja mpaka tatu ili kujiongezea ujasiri. Akatumbukiza kidole cha shahada cha mkono wake kwenye ‘trigga’ ya bastola kisha akaanza kubofya taratibu.

“Paaaaa!” Mlio mkubwa wa risasi ulisikika nama hiyo, lakini kabla hata shambulio hilo halijafanikiwa Mkuki alikurupuka kutoka usingizini na kuikata ndoto ile mbaya yenye kutisha.

Akaketi kitandani huku akitweta na kutokwa jasho mithili ya mtu aliyelowa mvua ya manyunyu. Akajipa sekunde kadhaa kuirejesha akili yake duniani na alipofanikiwa katika hilo alishusha pumzi ndefu ya kushukuru kwamba lile halikuwa tukio halisi.

Ghafla akashituka; aligundua kitu kipya ambacho hakikuwa cha kawaida—aling’amua kwamba alikuwa kwenye chumba asichokifahamu kabisa, yaani hakuwahi kuwa hapo kabla.

Kilikuwa ni chumba chenye ukubwa wa chumba cha kawaida cha kulala, kuta zote za chumba hicho zilipakwa chokaa huku kitanda na meza ndogo vikiwa ni vitu pekee vilivyomo ndani.

‘Niko wapi?’ Likawa ni swali la kwanza kugonga kichwani mwa Mkuki. Hapo akajipa muda kuvuta kumbukumbu ya kila alichopitia kabla ya kuwa pale chumbani na hakika ubongo wake ulimsitiri, alikumbuka kila kitu.

Alikumbuka watu wawili aliokuwa nao mara ya mwisho, akakumbuka ajali mbaya aliyoipata akiwa na watu hao, pia alikumbuka kwamba ajali ile ilisababishwa na mlipuko mkubwa wa bomu.

‘Au nimesaidiwa?’ akajiuliza Mkuki ‘Lakini ngonja, ngoja nione.’ Akajipa moyo wa kusubiri na hamasa ya kufanya udadisi.

Basi akateremka kutoka pale kitandani; alihisi maumivu mwilini lakini hayakumzuia kutembea kuelekea mlangoni. Lakini kabla hata hajafikia lengo mlango ulifunguliwa, akaingia mwanamke mmoja aliyekuwa akiimba kwa sauti ya juu iliyoashiria uhuru mkubwa alionao, lakini ghafla mwanamke huyo aliacha kuimba mara tu alipomuona Mkuki.

Alikuwa ni mwanamke wa ki-Asia, msichana mfupi, mwembamba, mweupe mwenye nyelwe ndefu na nyingi zilizoficha uso wake wote ingawa hilo halikumzuia kuona mbele.

“Umeamka?” Akauliza mwanamke huyo, lakini kwa lugha ambayo Mkuki hakuilewa, lugha yenye kufanana kabisa na Kichina.

“We ni nani?” Mkuki naye akamtupia swali kwa lugha adhimu ya Kiswahili huku akirudi nyuma taratibu.

“Tulia. Kaa kitandani.” Yakamtoka kwa upole yule msichana, tena kwa lugha ile ile yenye kukanganya masikioni mwa Mkuki.

“Wewe nani na niko wapi hapa?”

“Tulia. Rudi kitandani. Bado hujapona, utajitonesha.” Akasema msichana huyo lakini kwa sababu ya mgongano wa lugha kati yao ilikuwa ni kama anatwanga maji kwenye kinu.

Akanyamaza kidogo yule msichana, akamtazama Mkuki kana kwamba kuna kitu alikuwa akifikiria juu yake kisha akapaza sauti kumuita mtu ambaye bila shaka hakuwa mbali na chumba kile.

“Babaaaa....” Aliita hivyo na sauti ya kiume kutoka nje ikamuitikia.
“Njoo. Amaeamka.” Akasema binti.

Punde mlango ukafunguliwa, akaingia mzee ambaye kwa mtazamo wa haraka Mkuki alijiridhisha kwamba babu huyo alikuwa ni Mchina. Alikuwa ni mzee wa kati ya miaka 60 na 70; mfupi, mwembamba, mweupe, mwenye mvi kichwa kizima na macho madogodogo ya kuvimba.

“Umeamka?” Akauliza mzee huyo kwa lugha ile ile iliyokuwa ikitumiwa na yule msichana, kisha kabla ya kupewa jibu alimfuata Mkuki, akamshika mkono na kumchukua hadi kitandani, akamkalisha.

“Unajisikiaje?” Akauliza yule mzee lakini kwa jinsi ambavyo Mkuki alikuwa akimtazama akagundua fika kwamba kulikuwa na kikwazo cha lugha kati yao.

“Hunielewi? Huzungumzi Kithaiwan?” Akamuuliza lakini bado aliambulia jibu la ukimya.

Akamgeukia yule msichana. “Haelewi.” Akamwambia. Kisha akamgeukia tena Mkuki. “Unaitwa nani?” Akamuuliza; hapa akijitahidi kutumia na vitendo kutafsiri swali lake.

Mkuki akamuelewa lakini pia tayari alishagundua kwamba watu wale hawakuwa na lengo baya juu yake.

“Mkuki. Naitwa Mkuki.” Akajibu.

“Nani?.”

“Mkuki.” Akajibu kwa msisitizo.

“Mkuki?” Akauliza yule mzee kuthibitisha.

“Ndiyo.” Akajibu huku akitingisha kichwa kukubali.

“Ooooh! Mimi ni Wong,” akajitambulisha yule mzee na kuongozea. “Na yule ni Mei Lee.” Akamtambulisha na yule msichana.

“Sisi tumekuokota ufukweni. Tumekusaidia. Unaweza kutuambia unatokea wapi?” Akahoji yule mzee lakini Mkuki alibaki akitumbua macho tu kama ishara ya kwamba hakuwa akimulewa, labda tu pale alipojitambulisha yeye pamoja na yule msichana.

“Baba? Hakuelewi. Tumpe muda.” Akazungumza yule msichana ambaye muda wote sura yake ilikuwa imefunikwa kwa nywele zake ngingi na ndefu.

“Sawa. Simama. Twende.” Akasema yule mzee aliyejitambulisha kwa jina moja la Wong huku akisindikiza sentesi yake kwa vitendo, Mkuki akamuelewa, akasimama na kuanza kumfuata kuelekea nje.

**************************************
Mkuki Salum Goigoi ndilo jina lake halisi, kijana aliyezaliwa na kukulia nchini Tanzania. Hadi mwaka huo 1998 alikuwa na umri wa miaka 23 duniani ingawa haikuwa rahisi kugundua hilo kwa kumtazama; alikuwa akionekana mkubwa zaidi na amekomaa kwelikweli.

Ni mwembamba wa kukonda, mrefu, mweusi mwenye uso wa duara wenye kufanyiza upole fulani unapomtazama; ingawa si kweli kwamba amejaaliwa haiba hiyo.

Kichwa chake kilibeba kumbukumbu za yote yanayomuhusu; yaani alipotoka; kilichotokea; yeye ni nani na mengineyo lakini juu ya yote hayo alinuwia kutowaambia wenyeji wake ukweli wowote na hii ni kwa sababu alikuwa anataka kukwepa kurejeshwa nchini Tanzania.

Hapo alikuwa nchini Thaiwan; taifa dogo ambalo ardhi yake yote ni kisiwa. Nchi ambayo ipo barani Asia, katikati ya China na taifa la Taiwan.
Wathaiwan walikuwa wakifanana kwa kiasi kikubwa sana na Wachina; kimuenekano, kitamaduni na hata itikadi. Wenyeji wa Mkuki walikuwa wakiishi Mkoa wa Shenghei katika kijiji kiitwacho Chensuua; kijiji ambacho wakazi wake walikuwa wakiishi kwa kutegemea shughuli za uvuvi kwa kiasi kikubwa.

Basi kwa siku chache za awali Mkuki aliishi na wenyeji wake kama mtu asiyekumbuka lolote; alijitengenezea mazingira hayo ili wenyeji wake wasipate sababu ya kumrejesha alipotoka; lengo lake ilikuwa ni kulowea palepale.

Kwa siku tano tu za awali alitambulishwa kwa vijana wenzake; kazi hiyo aliifanywa na mzee Wong ili kumsaidia Mkuki kujifunza jinsi ya kuishi kwa kuendana na taratibu zao za maisha ikiwemo kuifahamu lugha kwa urahisi na mambo mengine.

Katika hilo Mkuki alipata changamoto kubwa ya ubaguzi; yaani ingawa vijana walimkubali wakati anatambulishwa kwao lakini hawakutaka kuwa karibu naye—hilo lilifanywa nyuma ya mzee Wong, walimbagua Mkuki kwa sababu ya rangi.

Lakini Maufeng aliamua kuwa tofauti ya vijana wote wa kijijini Chensua—huyu yeye alikuwa ni mvualana wa Kithaiwan ambaye ni pekee aliyekubali kujenga ukaribu na Mkuki ingawa pia kulikuwa na sababu iliyomsukuma kufanya hivyo.

Maufeng yeye alikuwa na matatizo ya akili yanayompelekea kuwa mwendawazimu kabisa kwa kipindi fulani, hivyo vijana wengi walimtenga pia ingawa tatizo lake halikuwa likitokea mara kwa mara.

Maufeng akawa ni mtu wa tatu muhimu kwa ajili ya maisha ya mkuki pale ugenini, yaani ukiwajumuisha mzee Wong na binti yake Mei Lee.

******************************

Wiki mbili za Mkuki ndani ya Thaiwan zilikatika. Sasa taratibu alionekana kuanza kuifahamu lugha ingawa si kwa kiasi kikubwa, na msaada wa nguvu aliupata kutoka kwa Maufeng na mzee Wong, lakini Mei Lee—yule binti wa mzee Wong hakuwa katika orodha hiyo.

Ukweli ni kwamba Mei Lee hakuwa ni msichana wa kawaida; alikuwa ni mpole na kimya kupita maelezo na ili kuthubitisha hiko fikiria suala hili, kwamba tangu Mkuki aanze kuishi kwao hawajawahi kukaa pamoja na kupiga soga ingawa wote walikuwa ni vijana wanaorandana umri. Wala Mei Lee hakuwa na rafiki, jambo pekee alilokuwa akilifanya muda mwingi ni kuimba nyimbo zake mwenyewe na hakika alikukuwa ni mwanamuziki mzuri aliyejaaliwa sauti murua.

Yote tisa; kubwa zaidi ni kwamba kwa kipindi chote hicho cha wiki mbili cha Mkuki kuwa pale hakuwahi kuona sura ya binti huyo, muda wote aliifunika kwa nywele zake kama mtu anayeficha kitu fulani.
Sauti dada Original1 cover.jpg
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000
SEHEMU YA 2

ILIPOISHIA....
Tuliona jinsi ambavyo Mkuki ameanza kuyazoea mazingira nchini Thaiwan. Lakini pia jinsi ambavyo ameishi kwa kipindi kirefu cha zaidi ya wiki mbili bila kuwahi kuiona sura ya Mei Lee....

SHUKA NAYO....
Kuna kipindi Mkuki alitamani sana kuuliza juu ya suala hilo la kuficha uso kwa nywele lakini hakuona hekima ndani yake; yaani angeazaje kuuliza kwa mfano?.

Hata hivyo baadae alipata mbadala wa hilo, alionelea ni vyema amuulize rafiki yake Maufeng kama anataka kujua ukweli, na alifanya hivyo kwenye mazungumzo yao ya kawaida.
“Kwanini Mei Lee anaficha uso kwa nywele?” Alitumbukiza swali la hivyo katikati ya mazungumzo yao.
“Kwanini unaniuliza?” Maufeng akahoji.
“Nataka kujua au kumjua.”
“Unataka kumjua au unataka kunijua mimi kupita Mei Lee?”
“Sijakuelewa.”
“Namaanisha ni vyema ungeenda ukamuuliza mwenyewe.”
“Nitaanzia wapi? Hajawahi hata kukaa na mimi kuongea.”
“Wewe umewahi kukaa naye?”
“Hapana.”
“Kwanini?”
“Anaonekana hapendi ukaribu.”
“Labda na yeye anona huna ukaribu.”
“Hapana... sawa kama ni hivyo mbona hana hata rafiki?”
“Sio lazima kuwa na rafiki. Kama wote wanaokuzunguka hawajatimia vigezo vya kuwa rafiki zako kwanini uwe mnafiki?” akajibu Maufeng na kuuliza swali ambalo lilimfanya Mkuki atulie wakati likiingia ndani, kichwani taratibu.
Akaendelea Maufeng.
“Mimi namjua Mei Lee. Nimewahi kumuona na nina uwezo wa kuwa na jibu la kila swali lako kuhusu yeye. Lakini ukimuuliza mwenyewe utajua mengi zaidi. Jenga ukaribu naye kama kweli unatamani kumfahamu.".
******************************
Sasa Mkuki akajipa mtihani mpya, alinuwia na kujihakikishia kwamba ni lazima afahamu kwanini Mei Lee alikuwa akifunika uso wake kwa nywele lakini pia kujenga ukaribu naye zaidi kama ingewezekana.
Akiwa mbioni kuelekea lengo alilojiwekea, mzee Wong alimletea habari mpya. Alikuwa amemtafutia mtu wa kumfundisha uvuvi ili aweze kupata shughuli itakayomsaidia kujimudu kwa kipindi chote ambacho ataendelea kuwa pale hadi hapo kumbukumbu kuhusu nyumbani kwao zitakapomejea.
“Mtu atakayekufundisha ni mvuvi mzuri tu. Atakueleza na bila shaka utelewa ndani ya muda mfupi.” Alisema Mzee Wong na kuongeza, “Unajua sitaki ukae bure tu, nataka ujichanganye zaidi na vijana wenzako. Hii itasaidia hata kwenye kuiweka sawa afya ya ubongo wako.”
Basi baada ya mazungumzo hayo Mkuki alikutanishwa mara moja na mtu aliyepewa jukumu la kumfundisha na wakafikia makubaliano ya kwamba kesho asubuhi aanze.
Jioni ya siku hiyo alikutana na rafiki yake Maufeng na kumueleza mpango ule; swahiba wake alimuunga sana mkono huku akimuahdi kwamba mara baada ya kufuzu mafunzo hayo yasiyo rasmi wataungana na kuanza kufanya uvuvi pamoja.
Asubuhi ya mafunzo Mkuki aliamka mapema sana kwa ajili ya kujiandaa na yote hiyo ni kwa sababu alikuwa na nia ya dhati ya kufanya jambo lile. Nia aliyokuwa nayo ilitengenzwa na ile siri yake; siri ya kwamba alikukuwa akikumbuka kila kitu kuhusu wapi ametoka. Aliamini kwamba endapo atakuwa na shughuli maalum ya kufanya itakuwa ni rahisi kwake kuendelea kuishi hapo wakati akaiendelea kupanga mipango yake fulani fulani taratibu.
Ingawa uvuvi haukuwa ni shuhuli nyepesi lakini Mkuki alielewa kwa muda mfupi mno; ndani ya wiki mbili tu alikuwa amekwiva kiasi cha kuweza kufanya shughuli hiyo mwenyewe bila usimamizi. Uzuri ni kwamba alikuwa akifundshwa kwa vitendo halisi, yaani alifunzwa kwa mtindo wa kufanya kazi kama msaidizi wa mwalimu wake.
Baada ya kuhitimu mafunzo hayo aliungana na swahiba wake Maufeng katika mchakato wa kutafuta mtumbwi mdogo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi. Halikuwa zoezi jepesi lakini kupitia msaada wa mzee Wong walifanikiwa. Walipata mtunbwi wa kukodi;ingawa awali waliuchukua bila kulipia kwa makubaliano ya kwamba pindi watakapovua na kuuza samaki watalipa pesa hiyo.
Kazi ilianza mara moja na kwa siku za awali ilionyesha mafanikio kwa kiasi cha kuwapatia pesa za kulipia mtumbwi na kujikimu nyumbani.
******************************
Mkuki alitimiza miezi miwili ya kuishi nchini Thaiwan, na sasa yeye akawa ndiye muhudumu mkuu wafamilia. Alileta chakula nyumbani sanjari na mahitaji mengine muhimu na jambo hili lilimtengenezea ukaribu kidogo na Mei Lee kwa sababu ilibidi msichana huyo amuongeleshe Mkuki pindi anapohitaji pesa kwa ajili ya mahitaji madogomadogo ya nyumbani.
Naye Mkuki alijitahidi kutoichezea nafasi hiyo, alihakikisha kwamba ukaribu wake na Mei Lee unajengeka ingawa tamati hakufanikiwa kama ambabvyo alitamani; yaani ni sawa ukaribu kiasi fulani ulikuwepo lakini si kwa ukaribu wa kina kama ambavyo yeye alikuwa akihitaji.
Ilibidi sasa aombe msaada kwa rafiki yake Maufeng kwa sababu aliamini jamaa huyo alikuwa akimfahamu vyema Mei Lee kwahiyo ingekuwa ni rahisi kwake kumpa ushauri wa mbinu za kutumia ili kuukuza ukaribu wake na msichana huyo na hatimaye afanikiwe kufahamu kuhusu kufunika uso wake kwa nywele.
“Labda umnunulie zawadi, anaweza akalainika, akawa rafiki yako.” Alishauri Maufeng.
“Zawadi gani sasa itafaa?” Mkuki akauliza.
Maufeng akacheka kidogo kabla yay kujibu, “Una maswali ya kijinga sana. Zawadi kwa ajili ya Mei Lee unaniuliza mimi!”
“Lakini we ndo uliyenishauri kuhusu zawadi.”
“Ndiyo. Mimi ninachofahamu ni kwamba binadamu wote tunapenda zawadi; linapokuja suala la zawadi gani hilo ni jambo binafsi.” Akafafanua Maufeng na kuongoza. “Lakini unaweza kumnunulia cheni, cheni za jedi. Ni nzuri, wanawake wengi wanazipenda.” Akasema.
Cheni za jedi zilikuwa ni miongoni mwa vitu vyenye gharama ya kawaida ambavyo wanawake wengi wa Kithaiwan hasa waishio vijijini walikuwa wakivipenda. Zilikuwa ni cheni zinazotengenezwa kwa kutumia madini ya Jedi na mchanganyiko wa mawe mengine yenye kufanana na dhahabu kwa mbali.
Basi Mkuki alifanyia kazi ushauri aliopewa; alichanga pesa kwa siku mbili tatu na zilipotimia akaenda kwenye soko dogo linalotumiwa na vijiji zaidi ya vitatu vya eneo hilo, na akanunua cheni yay Jedi kwa ajili ya kumpa Mei Lee.
Sasa mtihani ukabaki kuwa ni jinsi gani ambavyo ataikabdhi zawadi hiyo; katika hili pia aliomba msaada kwa Maufeng.
“Si umchukue muende ufukweni na umpe mkiwa huko.” Akashauri Maufeng.
“Nitamwambiaje sasa?”
Akacheka Maufeng. “Umeeanza na maswali yako ya kijinga. Unamuomba Mei Lee sio mimi. Nenda kamuukize mwenyewe.”
“Lakini we ndo umenishauri.“
“Kwahiyo?”
“Unatakiwa unielezee vizuri.”
“Sasa nikueleezee nini? Mimi sikufindishi jinsi ya kutengeneza ukaribu na mwanamke. Nashauri tu.” Akasema Maufeng na kuongozea. “Lakini sioni ugumu. Mfuate na umuombe mkatembee. Sio lazima iwe leo.”
“Ni ngumu sana.” akasema Mkuki.
“Basi unaweza ukaacha. Kwani ni lazima ujue kwanini anaficha sura?”
Akacheka kidogo Mkuki. “Mimi mwanaume. Najua ni vigumu lakini nitafanikiwa.” Akasema Mkuki na ikawa hivyo.
Jioni ya siku hiyo alimfuata Mei Lee nyuma ya nyumba ambapo alikuwepo huko akiimba. Huo ndio utaratibu wake kila jioni, kama si kwenda kuimba ufukweni basi hujichimbia nyuma ya nyumba, sehemu yenye bustani ndogo anayoitunza Mei Lee mwenyewe, na huko huupa moyo, roho na nafasi yake burudani tamu ya kujiimba nyimbo zake na za wasanii wengine anazozipenda.
Basi Mkuki alikwenda na kusimama nyuma ya pale alipokuwa ameketi Mei Lee; binti hakuwa akifahamu kuhusu ugeni huo, aliendelea kuimba kwa kujiachia kana kwamba alikuwa peke yake. Mkuki alimsikiliza hadi alipomaliza, kisha akafungua kinywa kumsemesha. “Unaimba vizuri sana.” Akazungumza huku akipiga makofi taratibu.
Mei Lee akageuka, akamuona Mkuki, akatazama chini kwa aibu.
“Unaimba vizuri mno.” Akasema tena Mkuki.
“Asante.” Akajibu Mei Lee kwa sauti ya chini sana ingawa Mkuki aliisikia.
“Unajua Mei Lee, wewe ni miongoni mwa waimbaji wachache duniani wenye sauti nzuri za asili. Hata nimeanza kupata wasiwasi juu ya ubinadamu wako, inawezekana wewe ni mmoja wa malaika watakaoipamba paradiso kwa nyimbo zao nzuri baada ya maisha ya dunia kufika ukomo.” akasema Mkuki huku akimsogelea Mei Lee.
Akaendelea.
“Natamani siku moja kila mtu athibitishe kwa sikio lake hiki ninachokwambia,” akamfikia. “Unaimba vizuri.” Akazidi kumpamba. Yote hiyo ilikuwa ni gia ya kumuingia, kutafuta jinsi ya atakavyompa zawadi lakini pia atakavyoomba kufahamua juu ya suala la uso na nywele.
Mei Lee alitazama chini muda wote, soni ilimtawala na hiyo ndiyo hulka yake; yeye ni msichana mwenye aibu kupita maelezo.
Mkuki akaketi pembeni ya pale alipokuwa ameketi Mei Lee, ilikuwa ni juu la benchi dogo lililotengenezwa katikati ya bustani ile nzuri iliyopandwa nyuma ya nyumba. Tena Mkuki alijitahidi kuwa jasiri wa aina yake kiasi kwamba asingeshindwa kuzungunza chochote kile kumwambia dada yake huyo—na hata walipokuwa wameketi walikuwa karibu karibu sana.
“Hatujawahi kukaa pamoja kama hivi,” akasema Mkuki; halikuwa swali lakini aliacha ukimya uchukue nafasi kana kwamba alikuwa akisuburi neno kutoka kwa mwenzie.
Alipoona kimya akaendelea
“Inashangaza kiasi fulani. Unajua sisi ni ndugu sasa. Nadhani Tulitakiwa tuwe karibu tangu siku ya kwanza kufahamiana.” Akasema lakini bado mazungumzo yao yalionenkana ni ya upande mmoja. Mkuki akaamua kitu, akaamua kumshirikisha kwa mtindo wa kumuuliza maswali.
“Unapenda sana kuimba. Nani alikufundisha?”
“Kuimba?”
“Ndio. Nani aliyekufundisha kuimba.”
Mei Lee akajichekesha kidogo. “Mwenyewe tu.” Akajibu.
“Mwenyewe!?”
“Ndio.”
“Inawezekana vipi?”
“Sijui ni vipi inawezekana lakini imewezekana kwangu. Sijawahi kufundishwa na mtu yeyote. Niligundua tu kwamba muziki ni rafiki wa karibu zaidi ambaye naweza kumkabidhi maisha yangu na akanipa furaha muda wote.” Akajibu kwa kirefu na hiyo ni kwa sababu aliulizwa juu ya kitu anachokipenda.
Muziki ni kila kitu katika maisha ya Mei Lee, ni rafiki, mpenzi, nyumba ya amani, bahari ya furaha na mwenzi wa uhai wake. Ni rahisi kumnyima vyote na bado akajihisi binadamu, lakini si kumnyima fursa ya kuimba muziki. Na sauti yake ilikuwa ni kama kinubi, sauti tamu yenye uwezo wa kusimamisha mapigo ya moyo kwa kila mwenye nao, sauti ambayo kamwe huwezi kuisimulia kwa maandishi wala lugha ya picha isipokuwa tu kwa kuisikiliza mwenyewe kwa masikio yako; yaani hata kama wataalamu wa lugha wataamua kukaa chini kutafuta msamiati wa kuielezea sauti ya Mei Lee amini kwamba hawatafanikiwa kupata neno moja lenye kutosha kuidadavua.
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000
SEHEMU YA 3


ILIPOISHIA....
Tuliona jinsi ambavyo Mkuki ameanza kuyazoea mazingira nchini Thaiwan. Lakini pia jinsi ambavyo ameishi kwa kipindi kirefu cha zaidi ya wiki mbili bila kuwahi kuiona sura ya Mei Lee....

SHUKA NAYO....
Kuna kipindi Mkuki alitamani sana kuuliza juu ya suala hilo la kuficha uso kwa nywele lakini hakuona hekima ndani yake; yaani angeazaje kuuliza kwa mfano?.

Hata hivyo baadae alipata mbadala wa hilo, alionelea ni vyema amuulize rafiki yake Maufeng kama anataka kujua ukweli, na alifanya hivyo kwenye mazungumzo yao ya kawaida.
“Kwanini Mei Lee anaficha uso kwa nywele?” Alitumbukiza swali la hivyo katikati ya mazungumzo yao.
“Kwanini unaniuliza?” Maufeng akahoji.
“Nataka kujua au kumjua.”
“Unataka kumjua au unataka kunijua mimi kupita Mei Lee?”
“Sijakuelewa.”
“Namaanisha ni vyema ungeenda ukamuuliza mwenyewe.”
“Nitaanzia wapi? Hajawahi hata kukaa na mimi kuongea.”
“Wewe umewahi kukaa naye?”
“Hapana.”
“Kwanini?”
“Anaonekana hapendi ukaribu.”
“Labda na yeye anona huna ukaribu.”
“Hapana... sawa kama ni hivyo mbona hana hata rafiki?”
“Sio lazima kuwa na rafiki. Kama wote wanaokuzunguka hawajatimia vigezo vya kuwa rafiki zako kwanini uwe mnafiki?” akajibu Maufeng na kuuliza swali ambalo lilimfanya Mkuki atulie wakati likiingia ndani, kichwani taratibu.
Akaendelea Maufeng.
“Mimi namjua Mei Lee. Nimewahi kumuona na nina uwezo wa kuwa na jibu la kila swali lako kuhusu yeye. Lakini ukimuuliza mwenyewe utajua mengi zaidi. Jenga ukaribu naye kama kweli unatamani kumfahamu.".
******************************
Sasa Mkuki akajipa mtihani mpya, alinuwia na kujihakikishia kwamba ni lazima afahamu kwanini Mei Lee alikuwa akifunika uso wake kwa nywele lakini pia kujenga ukaribu naye zaidi kama ingewezekana.
Akiwa mbioni kuelekea lengo alilojiwekea, mzee Wong alimletea habari mpya. Alikuwa amemtafutia mtu wa kumfundisha uvuvi ili aweze kupata shughuli itakayomsaidia kujimudu kwa kipindi chote ambacho ataendelea kuwa pale hadi hapo kumbukumbu kuhusu nyumbani kwao zitakapomejea.
“Mtu atakayekufundisha ni mvuvi mzuri tu. Atakueleza na bila shaka utelewa ndani ya muda mfupi.” Alisema Mzee Wong na kuongeza, “Unajua sitaki ukae bure tu, nataka ujichanganye zaidi na vijana wenzako. Hii itasaidia hata kwenye kuiweka sawa afya ya ubongo wako.”
Basi baada ya mazungumzo hayo Mkuki alikutanishwa mara moja na mtu aliyepewa jukumu la kumfundisha na wakafikia makubaliano ya kwamba kesho asubuhi aanze.
Jioni ya siku hiyo alikutana na rafiki yake Maufeng na kumueleza mpango ule; swahiba wake alimuunga sana mkono huku akimuahdi kwamba mara baada ya kufuzu mafunzo hayo yasiyo rasmi wataungana na kuanza kufanya uvuvi pamoja.
Asubuhi ya mafunzo Mkuki aliamka mapema sana kwa ajili ya kujiandaa na yote hiyo ni kwa sababu alikuwa na nia ya dhati ya kufanya jambo lile. Nia aliyokuwa nayo ilitengenzwa na ile siri yake; siri ya kwamba alikukuwa akikumbuka kila kitu kuhusu wapi ametoka. Aliamini kwamba endapo atakuwa na shughuli maalum ya kufanya itakuwa ni rahisi kwake kuendelea kuishi hapo wakati akaiendelea kupanga mipango yake fulani fulani taratibu.
Ingawa uvuvi haukuwa ni shuhuli nyepesi lakini Mkuki alielewa kwa muda mfupi mno; ndani ya wiki mbili tu alikuwa amekwiva kiasi cha kuweza kufanya shughuli hiyo mwenyewe bila usimamizi. Uzuri ni kwamba alikuwa akifundshwa kwa vitendo halisi, yaani alifunzwa kwa mtindo wa kufanya kazi kama msaidizi wa mwalimu wake.
Baada ya kuhitimu mafunzo hayo aliungana na swahiba wake Maufeng katika mchakato wa kutafuta mtumbwi mdogo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi. Halikuwa zoezi jepesi lakini kupitia msaada wa mzee Wong walifanikiwa. Walipata mtunbwi wa kukodi;ingawa awali waliuchukua bila kulipia kwa makubaliano ya kwamba pindi watakapovua na kuuza samaki watalipa pesa hiyo.
Kazi ilianza mara moja na kwa siku za awali ilionyesha mafanikio kwa kiasi cha kuwapatia pesa za kulipia mtumbwi na kujikimu nyumbani.
******************************
Mkuki alitimiza miezi miwili ya kuishi nchini Thaiwan, na sasa yeye akawa ndiye muhudumu mkuu wafamilia. Alileta chakula nyumbani sanjari na mahitaji mengine muhimu na jambo hili lilimtengenezea ukaribu kidogo na Mei Lee kwa sababu ilibidi msichana huyo amuongeleshe Mkuki pindi anapohitaji pesa kwa ajili ya mahitaji madogomadogo ya nyumbani.
Naye Mkuki alijitahidi kutoichezea nafasi hiyo, alihakikisha kwamba ukaribu wake na Mei Lee unajengeka ingawa tamati hakufanikiwa kama ambabvyo alitamani; yaani ni sawa ukaribu kiasi fulani ulikuwepo lakini si kwa ukaribu wa kina kama ambavyo yeye alikuwa akihitaji.
Ilibidi sasa aombe msaada kwa rafiki yake Maufeng kwa sababu aliamini jamaa huyo alikuwa akimfahamu vyema Mei Lee kwahiyo ingekuwa ni rahisi kwake kumpa ushauri wa mbinu za kutumia ili kuukuza ukaribu wake na msichana huyo na hatimaye afanikiwe kufahamu kuhusu kufunika uso wake kwa nywele.
“Labda umnunulie zawadi, anaweza akalainika, akawa rafiki yako.” Alishauri Maufeng.
“Zawadi gani sasa itafaa?” Mkuki akauliza.
Maufeng akacheka kidogo kabla yay kujibu, “Una maswali ya kijinga sana. Zawadi kwa ajili ya Mei Lee unaniuliza mimi!”
“Lakini we ndo uliyenishauri kuhusu zawadi.”
“Ndiyo. Mimi ninachofahamu ni kwamba binadamu wote tunapenda zawadi; linapokuja suala la zawadi gani hilo ni jambo binafsi.” Akafafanua Maufeng na kuongoza. “Lakini unaweza kumnunulia cheni, cheni za jedi. Ni nzuri, wanawake wengi wanazipenda.” Akasema.
Cheni za jedi zilikuwa ni miongoni mwa vitu vyenye gharama ya kawaida ambavyo wanawake wengi wa Kithaiwan hasa waishio vijijini walikuwa wakivipenda. Zilikuwa ni cheni zinazotengenezwa kwa kutumia madini ya Jedi na mchanganyiko wa mawe mengine yenye kufanana na dhahabu kwa mbali.
Basi Mkuki alifanyia kazi ushauri aliopewa; alichanga pesa kwa siku mbili tatu na zilipotimia akaenda kwenye soko dogo linalotumiwa na vijiji zaidi ya vitatu vya eneo hilo, na akanunua cheni yay Jedi kwa ajili ya kumpa Mei Lee.
Sasa mtihani ukabaki kuwa ni jinsi gani ambavyo ataikabdhi zawadi hiyo; katika hili pia aliomba msaada kwa Maufeng.
“Si umchukue muende ufukweni na umpe mkiwa huko.” Akashauri Maufeng.
“Nitamwambiaje sasa?”
Akacheka Maufeng. “Umeeanza na maswali yako ya kijinga. Unamuomba Mei Lee sio mimi. Nenda kamuukize mwenyewe.”
“Lakini we ndo umenishauri.“
“Kwahiyo?”
“Unatakiwa unielezee vizuri.”
“Sasa nikueleezee nini? Mimi sikufindishi jinsi ya kutengeneza ukaribu na mwanamke. Nashauri tu.” Akasema Maufeng na kuongozea. “Lakini sioni ugumu. Mfuate na umuombe mkatembee. Sio lazima iwe leo.”
“Ni ngumu sana.” akasema Mkuki.
“Basi unaweza ukaacha. Kwani ni lazima ujue kwanini anaficha sura?”
Akacheka kidogo Mkuki. “Mimi mwanaume. Najua ni vigumu lakini nitafanikiwa.” Akasema Mkuki na ikawa hivyo.
Jioni ya siku hiyo alimfuata Mei Lee nyuma ya nyumba ambapo alikuwepo huko akiimba. Huo ndio utaratibu wake kila jioni, kama si kwenda kuimba ufukweni basi hujichimbia nyuma ya nyumba, sehemu yenye bustani ndogo anayoitunza Mei Lee mwenyewe, na huko huupa moyo, roho na nafasi yake burudani tamu ya kujiimba nyimbo zake na za wasanii wengine anazozipenda.
Basi Mkuki alikwenda na kusimama nyuma ya pale alipokuwa ameketi Mei Lee; binti hakuwa akifahamu kuhusu ugeni huo, aliendelea kuimba kwa kujiachia kana kwamba alikuwa peke yake. Mkuki alimsikiliza hadi alipomaliza, kisha akafungua kinywa kumsemesha. “Unaimba vizuri sana.” Akazungumza huku akipiga makofi taratibu.
Mei Lee akageuka, akamuona Mkuki, akatazama chini kwa aibu.
“Unaimba vizuri mno.” Akasema tena Mkuki.
“Asante.” Akajibu Mei Lee kwa sauti ya chini sana ingawa Mkuki aliisikia.
“Unajua Mei Lee, wewe ni miongoni mwa waimbaji wachache duniani wenye sauti nzuri za asili. Hata nimeanza kupata wasiwasi juu ya ubinadamu wako, inawezekana wewe ni mmoja wa malaika watakaoipamba paradiso kwa nyimbo zao nzuri baada ya maisha ya dunia kufika ukomo.” akasema Mkuki huku akimsogelea Mei Lee.
Akaendelea.
“Natamani siku moja kila mtu athibitishe kwa sikio lake hiki ninachokwambia,” akamfikia. “Unaimba vizuri.” Akazidi kumpamba. Yote hiyo ilikuwa ni gia ya kumuingia, kutafuta jinsi ya atakavyompa zawadi lakini pia atakavyoomba kufahamua juu ya suala la uso na nywele.
Mei Lee alitazama chini muda wote, soni ilimtawala na hiyo ndiyo hulka yake; yeye ni msichana mwenye aibu kupita maelezo.
Mkuki akaketi pembeni ya pale alipokuwa ameketi Mei Lee, ilikuwa ni juu la benchi dogo lililotengenezwa katikati ya bustani ile nzuri iliyopandwa nyuma ya nyumba. Tena Mkuki alijitahidi kuwa jasiri wa aina yake kiasi kwamba asingeshindwa kuzungunza chochote kile kumwambia dada yake huyo—na hata walipokuwa wameketi walikuwa karibu karibu sana.
“Hatujawahi kukaa pamoja kama hivi,” akasema Mkuki; halikuwa swali lakini aliacha ukimya uchukue nafasi kana kwamba alikuwa akisuburi neno kutoka kwa mwenzie.
Alipoona kimya akaendelea
“Inashangaza kiasi fulani. Unajua sisi ni ndugu sasa. Nadhani Tulitakiwa tuwe karibu tangu siku ya kwanza kufahamiana.” Akasema lakini bado mazungumzo yao yalionenkana ni ya upande mmoja. Mkuki akaamua kitu, akaamua kumshirikisha kwa mtindo wa kumuuliza maswali.
“Unapenda sana kuimba. Nani alikufundisha?”
“Kuimba?”
“Ndio. Nani aliyekufundisha kuimba.”
Mei Lee akajichekesha kidogo. “Mwenyewe tu.” Akajibu.
“Mwenyewe!?”
“Ndio.”
“Inawezekana vipi?”
“Sijui ni vipi inawezekana lakini imewezekana kwangu. Sijawahi kufundishwa na mtu yeyote. Niligundua tu kwamba muziki ni rafiki wa karibu zaidi ambaye naweza kumkabidhi maisha yangu na akanipa furaha muda wote.” Akajibu kwa kirefu na hiyo ni kwa sababu aliulizwa juu ya kitu anachokipenda.
Muziki ni kila kitu katika maisha ya Mei Lee, ni rafiki, mpenzi, nyumba ya amani, bahari ya furaha na mwenzi wa uhai wake. Ni rahisi kumnyima vyote na bado akajihisi binadamu, lakini si kumnyima fursa ya kuimba muziki. Na sauti yake ilikuwa ni kama kinubi, sauti tamu yenye uwezo wa kusimamisha mapigo ya moyo kwa kila mwenye nao, sauti ambayo kamwe huwezi kuisimulia kwa maandishi wala lugha ya picha isipokuwa tu kwa kuisikiliza mwenyewe kwa masikio yako; yaani hata kama wataalamu wa lugha wataamua kukaa chini kutafuta msamiati wa kuielezea sauti ya Mei Lee amini kwamba hawatafanikiwa kupata neno moja lenye kutosha kuidadavua.

**************************
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000
SEHEMU YA 4


ILIPOISHIA...
Tuliona Maufeng akimshauri Mkuki watoroke kwenda kutafuta maisha kisiwani Jiaju, ambapo tayari mzee Wong alishampiga marufuku kwenda. Je , ni maamuzi gani atakayochukua Mkuki?
ENDELEA....
kuki alifikiria kidogo, akamtazama Maufeng machoni na kuona ni jinsi gani rafiki yake alikuwa na kiu ya kufanya kile wanachokizungumzia. Akarudi kwa upande wake, akashaurina na moyo wake kwa sekunde chache kabla ya kuja na jibu moja thabiti la ‘sawa, tutakwenda.’
*******************************
Kwenda kisiwani Jiaju ulikuwa ni mpango uliopangwa kutimia, hivyo mara bara baada ya Mkuki na Maufeng kuweka akiba ya fedha watakazokwenda kuzitumia kukodia boti walipanga siku ya kutoroka.
Ilikuwa ni Jumanne jioni, walifanya harakati hizo bila kugundulika na mtu yeyote. Walipanda boti ndogo iliyokuwa ikielekea huko Jiaju na walifika kesho yake asubuhi.
Fujo za soko la samaki kisiwani Jiaju liliwapa picha halisi ya jinsi eneo hilo linavyohitajii watu wachangamfu. Kila waliyemuona alikuwa ‘bize’ na mambo yake. Watu walipita huku na huko, mgongano ulikuwa ni mkubwa sana hata Mkuki alijikuta akifananisha eneo hilo na Kariakoo Mtaa wa Kongo .
Walichukua chumba katika nyumba moja ya kulala wageni kisiwani hapo ambayo ilikuwa ikihudumiwa na mwanamke mnene kweli kweli aitwaye Faye—na sasa wakaanza maisha mapya yenye matuamini makubwa ya kufanikiwa na kurejea nyumbani na pesa mzomzo; pesa nyingi kweli kweli.
Mpango wao nambari moja ilikuwa ni kutafuta mtumbwi wa kukodi ambao wangeutumia kwa kufanyia kazi kwa kipindi cha siku thelathini na kurejea nyumbani, waliamini kwa muda huo watakuwa wamehifadhi pesa nyingi kwa ajili ya kufanyia mambo mengine mbali na uvuvi pindi watakaporejea kijijini Chensua.
Ili kupata boti ya kukodi walihitaji dalali wa kuwasaidia kutafuta, na ili kumpata dalali walihitaji mtu wa kuwaunganisha kwa mmoja ambaye atawatafutia boti nzuri kwa ajili ya kazi, na ili kufanikisha hilo ilibidi wajenge ukaribu na Faye—yule mwanamke bonge muhudumu wa ‘gesti’ waliyofikia.
Ilikuwa rahisi zaidi kwa wao kuwa karibu na Faye kupitia Maufeng kwa sababu kwa pale kisiwani Mkuki alikuwa akionekana ni kama kitu cha ajabu na hilo lilijitokeza tangu siku ya kwanza walipowasili. Wathaiwan wengi hakuwahi kupata kumuona binadamu mwenye ngozi yenye rangi kama Mkuki, yeye alikuwa ni mtu mweusi wa kwanza kufika kisiwani Jiaju na wa kwanza kukumbana na ubaguzi wa rangi kisiwani hapo.
Basi Maufeng akaanzisha ukaribu na dada huyo. Alimfuata pale mapokezi, akamsalimu.
“Umechokaa kukaa ndani?” Aliuliza Faye baada ya salamu.
“Hapana. Ila nimependa kuja kukaa na wewe malaika.” Akasema Maufeng, hapa akijtahidi kutumia maneno mazuri ya kumvutia Faye.
Faye akacheka kabla ya kujibu. “Kumbe ni muongeaji.”
“Kwanini?”
“Basi tu. Sura yako inaonesha ni mkimya.” Akasema na kuongeza. “Utakaa hapa mpaka lini?”
“Bado sijajua. Wewe unapenda niondoke lini?”
Akacheka kidogo Faye na kujibu. “Usiondoke”
“Basi nitafanya hivyo.” Akasema Maufeng.
“Kwani umekuja kwa ajili gani? Kununua samaki?”
“Nimekuja kuvua. Lakini bado kuna mambo yananikwamisha.” Akajibu Maufeng lakini kabla hajaendelea akaingia mteja ndani, Faye akainuka na kwenda kumuhudumia kisha akarudi kuendelea na maongezi na Maufeng.
“Enhee. Umesema kuna mambo yanakukwamisha? Mambo gani?”
“Nataka mtumbwi wa kukodi.”
“Mbona iko mingi sana hapa, tena ya gharama tofauti. Naweza nikakuonganisha na dalali.” Akasema Faye bila kujua kwamba alikuwa akielekea kwenye hitaji lilimsogeza Maufeng karibu yake.
“Nitafurahi sana.”
“Basi usijali. Jioni nitakukutanisha naye.” Akasame Faye na mazungumzo mengine yakashika hatamu huku akipewa ofa ya kinywaji na Maufeng.
Jioni; mkuki na Maufeng walikuwa ndani, mlango wa chumba chao ulibishwa hodi, Maufeng akainuka kwenda kufungua. Alikuwa ni Faye, alikuja kwa lengo la kumuita Maufeng ili akutane na dalali wa mitumbwi.
“Sawa, tunakuja.”
“Mnakuja!? Wewe na nani? Na yule mwenzako mweusi.” Faye akahoji lakini kwa sauti ya kunong’ona ili Mkuki asisikie.
“Ndiyo. Kuna tatizo?”
“Hapana lakini.... Au sawa, njoo naye.” Akasema Faye kisha akarejea mapokezi ambapo dalali alikuwepo.
Maufeng akamchukua Mkuki na wakaongozana hadi mapokezi, hawakumuona mtu yeyote eneo hilo zaidi ya Faye mwenyewe.
“Yuko wapi?” Akauliza Maufeng.
“Yule pale,” Faye akaelekeza huku akimnyoshea kidole mwanaume mmoja aliyeketi kwenye viti vya baa ndogo iliyopo kwenye gesti hiyo. “Twendeni.” akaongeza kisha akazunguka kutoka mapokezi na kuongoza njia kuelekea alipokuwa ameketi mwanaume yule.
Wakamfikia.
“Taro?” Faye akamuita kwa jina mwanaume huyo. Taro akainua kichwa kuwatamaza.
Alikuwa ni mwaname wa mwenye asili ya Kijapani, mkubwa kiumri kwa miaka kumi au zaidi ukimlinganisha na kina Mkuki. Mwanamume mnene kiasi, mwenye nywele nyingi nyeusi za kulazwa kwa nyuma na macho ya kuvimba ya Kijapani.
Alimtazama sana Mkuki kama mtu anayeshangaa muujiza fulani.
“Nini hiki?” Akauliza Taro.
“Ndo watu niliokwambia wanataka boti ya kukodi.” Akajibu Faye.
“Huyu na huyu?” Akahoji Taro.
“Ndiyo. Kwani vipi?” Akadakia Maufeng, aliamua kufanya hivyo kwa sababu aliona chembechembe za kibaguzi kwenye maswali ya Taro.
“Kwani vipi? Nashangaa. Sijawahi kuona mtu mwenye upendo kama wewe. Mtu anayefuga nyani na anamtanbulisha nyani wake kama mshirika mwenzake.” Akadhihaki Taro kisha akatoa cheko kubwa la kishenzi.
“Sawa. Naona ni vyema tungeendelea kuzungumzia sababu ya kuwa hapa.” Akasema Maufeng, wakati huo Mkuki akijitahidi kujituliza, kujizuia asikwazike na kejeli za aina ile.
Taro akaendelea kucheka. “Hatuwezi kuendelea. Inabidi kwanza unionyeshe kibali cha kumiliki mnyama pori, na kibali cha daktari kuthibitisha kwamba nyani wako hawezi kutusababishia madhara ya kiafya sisi binadamu.” Akasema lakini kabla hata hajamaliza Mkuki alimrukia, akamkwida, akamnyanyua kutoka kwenye kiti alichokuwa ameketi na kumpiga kichwa matata kwenye midomo hata akachanika, akatokwa damu.
Maufeng na Faye wakawa waamuzi, wakawatenganisha ili Mkuki asiendele kimuadhibu Taro.
“Nitakuua. Nitakuua.” Akasema kwa sauti ya juu Mkuki huku akiwa ni mwenye ghadhabu kwelikweli. Kwa bahati mbaya sauti ilitua kwenye masikio ya askari polisi watatu waliokuwa wakikatiza eneo hilo wakiongozwa na kamanda Su Lee—askari wa kike ambaye ni mmoja wa maaskari polisi viongozi wa kituo cha pekee cha polisi kilichopo kisiwani hapo.
Maaskari wakawasogelea na kitu cha kwanza kukiona ilikuwa ni Mkuki, na aliwashangaza kiasi kwamba badala ya Su Lee kuhoji kuhusu kilichowapelekea pale alianza kuuliza kuhusu Mkuki.
“Nini hiki?” Akahoji Afande Su Lee huku akinyoosha kifimbo chake cha kiaskari kumuelekea Mkuki.
“Ni mshenzi afande. Anataka kuniua. Amenijeruhi hapa.” Akasema Taro huku akionesha jeraha lake mdomi.
Afande Su Lee akamsogelea Mkuki—alikuwa ni mwanamke wa shoka, mwanamke asiyefanana na wanawake wengi. Alikuwa na mwili wa mazoezi kama mwanaume, mrefu tofauti na walivyo Wathaiwan wengi. Sura yake pia ilikuwa ni ya ugwadu kweli kweli, ni kama mtu anayekunywa chai moto kwenye kikombe cha plastiki; kwa kifupi Afande Su Lee hakuwa na haiba ya kike kabisa.
“Wewe ni nani?” Akahoji Afande huku akimuinamia Mkuki.
“Afande ulikuwa ni ugomvi wa kawaida tu, ugomvi wa kibiashara. Mimi na mwenzangu hapa tunataka kukodi boti kwa.....” akadakia Maufeng lakini Su Lee alimkatisha kabla hajamaliza.
“Kelele.”
Maufeng akapiga kimya, Su Lee akamgeukia Mkuki.
“Ni mgeni hapa? Mimi naitwa Inspekta Su Lee, na nina taarifa nyingi kuhusu nyani kama wewe. Leo nakupa nafasi ya upendeleo, lakini tukikutana siku nyingine katika tukio la namna sitakuacha.” Akasema, kisha bila kupoteza muda akachukua watu wake, wakaondoka na hiyo ilikuwa ni kama ‘zali la mentali’ kwa sababu hakuna mtu aliyewahi kuingia kwenye anga za Inspekta Su Lee na akapona kirahisi namna ile—huenda lile lilitokea kwa sababu za msingi ambazo alizifahamu Inspekta mwenyewe.
Baada ya Inspekta Su Lee kutokomea na watu wake mazungumzo kuhusu boti ya kukodi yakaendelea.
“Vipi? Tunapata boti au mpaka jeraha lipone?” Akauliza kwa kejeli Maufeng.
“Mnataka boti gani?” Akaukiza Taro na Maufeng akataja aina ya boti wanayoitaka.
“Kwa siku ngapi?” Akauliza.
“Siku thelathini.” Akajibu Maufeng.
“Zipo,” akasema Taro na kutaja bei ambayo ilikuwa ni sawa na kiasi ambacho kina Mkuki walikuaa nacho.
******************************
Kazi ilianza mara moja baada ya kupata boti, waliingia baharinii kila usiku na asubuhi walirudi na lundo la samaki kama ilivyo kwa wavuvi wengine. Waliuza samaki wote waliokuwa wakipata na pesa waalitumia kiasi kidogo na kilichobaki walihifadhi kwa ajili ya mpango wao.
Hata hivyo mfumo wa maisha pale kisiwani haukuwa rahisi kwa Mkuki, aliandamwa na ubaguzi wa daraja la juu sana ingawa mwenyewe aljitahidi kuwa mvunilivu. Alifanikiwa katika hiko kutokana na roho ya kutafuta akiyokuwa nayo. Alijua anachotafuta, alifahamu hitaji lake kwahiyo hakuwa na sababu ya kuziruhusu hisia za kibaguzi za watu wengine zimkwamishe.
Upande wa Maufeng mambo yalikuwa ni burudani, maisha ya pale kisiwani yalikuwa murua sana kwake kiasi kwamba hadi alipata mpenzi. Alianzisha uhusiano na mrembo ‘kibonge’ Faye ingawa uhusiano wao haukuwa na dalili ya kwamba ungefika mbali.
Sio tu uhusiano, pia Maufeng alitengeneza marafiki wengi wapya lakni ubaya ni kwamba hawakuwa marafiki wema, wengi walikuwa ni wavuvi wapenda pombe na uasherati mwingine uliojaa kisiwani pale na hii ilipelekea hata Maufeng naye akafunzwa ujinga huo; yaani nguvu ya marafiki hao ikamchukua kabisa Maufeng na sasa hata yeye akaanza kujaribu kutumia vileo na tamati akaja kuwa ni mlevi mbwa kiasi kwamba hata akawa kero kwa watu waliomfundisha.
Sasa pombe ikawa ni sehemu ya maisha yake, ikamuendesha barabara hata akafikia hatua ya kuomba kuwa kila wanapopata pesa yeye na Mkuki wagawane ‘pasu kwa pasu’, kila mmoja afe na chake jambo ambalo Mkuki alikataa katakata.
************************************
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000
SEHEMU YA 5
ILIPOISHIA...
Tuliona mgogoro mkubwa kuhusu kugawana pesa umeibuka kati ya Mkuki na Maufeng; Je nini kilijiri baada ya hapo.

SHUKA NAYO...
“Hapana. Utachukua pesa kidogo kwa ajili ya hizo pombe zako. Mpango wetu wa kuweka pesa uko pale pale.” Alieleza Mkuki kupinga suala la kugawana pesa, alijua kuwa baadae lingemsababishia matatizo, angeonekana kamnyonya au kumdhulumu mshirika wake.

Hata hivyo tabia ya ulevi ilimzidi nguvu Maufeng kiasi kwamba sasa akawa hata kula hataki. Akafunga ndoa rasmi na pombe, yeye akawa pombe na pombe ikawa yeye.
Mkuki alijitahidi sana kumuonya, kumrudisha kwenye reli lakini hakufanikiwa—tayari walishakuwa sio watu wa kufanana tena, ulevi ulififsha urafiki wao kwa kiasi kikubwa mno.
********************************
Ni mwanaume gani pale kisiwani angethubutu kuwa na mwanamke wa aina ya Su Lee, mwanamke mwenye kila åkigezo cha kuitwa jike dume, kuanzia umbile, sura na hata tabia. Hivyo ndivyo ambavyo Su Lee alikosa wanaume. Mbali na kukosa wanaume alikuwa na siri kubwa moyoni, siri aliyoitengeneza mwenyewe kutokana na fikra ambazo zilizaliwa kupitia mitazamo ya watu mbalimbali aliyowahi kuisikia na kuifuatilia.
Aliwahi kuishi katika mapenzi, lakini kwa kipindi chote hicho hakuwahi kupata mwanaume aliyewahi kumridhisha katika tendo na hii ni kwa mujibu na nafsi yake mwenyewe.
Kwanini alikuwa haridhiki? Su Lee yeye alijijengea imani kwamba ili ufurahie tendo ni lazima ukutane na mwanaume mwenye uume mkubwa; ubaya katika hili ni kwamba, wanaume wengi wa Thaiwan walikuwa na maumbile madogo yenye kuwatosha watu wasio na mtazamo kama wake. Na hii ndiyo sababu hakutaka hata kumkamata Mkuki siku ile kwa kuwa moja ya taarifa alizowahi kusikia kuhusu watu weusi ni kwamba wana madubwasha makubwa ndani ya suruali zao, hivyo aliamini siku moja Mkuki atamsaidia kukata kiu aliyonayo.
Basi mpango nambari moja wa Su Lee ulikuwa ni kumtafuta Mkuki na kumueleza ukweli ingawa hilo halikuwa jambo jepesi kwa kuwa alitaka lifanyike kwa siri. Akapanga mkakati, akajiahidi kwamba atamtafuta yule rafiki yake kwanza, yaani Maufeng, kisha kupitia huyo atajenga ukaribu na Mkuki na tangu hapo itakuwa rahisi kutimiziwa hitaji lake.
Usiku mmoja alitoka kwenda kwenye gesti wanamoishi kina Mkuki, hiyo ilikuwa ni sehemu ya kutimiza mpango wake. Alikuwa amevalia kiraia, sketi ndefu na blauzi. Alikwenda moja kwa moja hadi kaunta ambapo alimuulizia Maufeng.
“Hayupo afande. Amefanya kosa gani?” Alijibu na kuuliza Faye.
“Hakuna tatizo. Nilikuwa na shida na mmoja kati yao.”
“Hata yule mwenzake? Yule mweusi”
“Ndiyo.”
“Yule yupo ndani. Nimuite.”
“Sawa.”
“Nimwambiaje?”
“Kawaida tu. Mwambie namuhitaji.” Akaelekeza Inspekta Su Lee.
Basi Faye akazunguka na kutoka pale kaunta, akaelekea kwenye kordo ya vyumba na ndani ya sekunde sitini alirudi akiongozana na Mkuki.
“Habari yako?” ikamtoka sabahi Inspekta Su Lee huku akimpa mkono Mkuki na kutabasamu pia. Kile kilichokuwa kikiendelea ilikuwa ni kama ndoto kwa Faye ambaye alikuwa akimfahamu uzuri Inspekta, tangu amjue hakuwahi kumuona akitabasamu hata siku moja, ile ilikuwa ni kama uchuro.
Mkuki akampa mkono pia, wakashikana.
“Salama.” Akaitikia ile salamu na kuongeza. “Nimeambiwa unanitafuta?”
“Ndiyo. Ninashida na nyinyi, mwenzako yuko wapi?”
“Ametoka.”
“Basi hata wewe peke yako unaweza kunisaidia. Tunaweza kuondoka pamoja?” Akauilza Afande Su Lee.
Mkuki alifikiria kidogo. “Sasa hivi?” akauliza.
“Ndiyo.” Inspekta akajibu, basi Mkuki akakubali, kisha akaingia ndani kwenda kubadilisha nguo kwa sababu alikuwa amevalia isivyotakikana, na punde alikuja akiwa ndani ya fulana, suruali nyeusi na viatu vya wazi vya kufanana na malapa.
Baada ya pale wakaondoka pamoja, Inspekta Su Lee na Mkuki. Inpsekta alimuongoza Mkuki hadi ufukweni, eneo ambalo likikuwa tulivu sana na sahihi kwa mazungumzo mazito ya namna ile. Wakiwa huko, alimueleza kila kitu tena kwa kujiamini, aliweka bayana shida yake na jinsi ambavyo angependa Mkuki amsaidie; alihitaji mtu wa kumkuna.
Sasa ukawa ni wasaa wa Mkuki kutoa majibu, ilikuwa ni nyakati ngumu kweli kweli. Yeye kama mwanaume alitakiwa atoe kauli moja thabiti ambayo ama ni ya kukataa au kukubali. Nafsini hakuwa na hitaji na Inspekta Su Lee, hii ni sawa na kusema kwamba hata kama atakubali kuwa msaada kwa Inspekta itakuwa ni kwa sababu za nje ya upendo, si kwamba atakuwa amefanya hilo kwa matakwa yake.
Lakini hata hivyo Mkuki alikuwa na sifa moja kubwa, sifa ya kujiamini. Yeye hakuwa mwoga-mwoga, alikuwa ni mtu mwenye msimamo hasa linapokuja suala zima la kusimamia mtazamo wake; yaani anapodhani kwamba jibu la jambo fulani ni hapana basi husimama katika hapana yake na kuiwekea msingi wa hoja ngumu na imara.
“Nimekuelewa Inspketa, lakini bahati mbaya mimi nimeoa. Ni mume wa mtu.” Alieleza Mkuki baada ya kufikiria kwa muda kidogo.
“Sio tatizo…..” alieleza Inspekta Su Lee. Alimbembeleza sana Mkuki lakini mwanamume aliendelea kusimama imara palepale kwenye ‘hapana’ yake bila kutetereka, bila kutetemeka na tamati ya mazungumzo ilikuwa ni kuondoka ilihali Inspekta akiwa ameshindwa kufanikiwa kutimiza azimio lake.
***************************
Mvutano mkubwa uliibuka kati Mkuki na Maufeng. Siku za kurejea nyumbani zilikuwa zimetimia, walitakiwa kesho ya siku hiyo waondoke lakini sasa Maufeng alikuja na wazo jipya lililokwenda kinyume na makubaliano yao. Yeye alitaka wagawane nusu kwa nusu ya pesa walizohifadhi kwa kipindi chote, kisha Mkuki aondoke mwenyewe na kumuacha Maufeng palepale kisiwani Jiaju.
”Haiwezekani Maufeng. Siwezi kukupa nusu ya pesa na nikakuacha hapa. Turudi nyumbani tukagawane huko kisha utarudi huku kama umepapenda.” Alipinga Mkuki.
Mvutano ulishika kasi kweli kweli, kelele za nataka ‘pesa zangu’ kutoka kwa Maufeng zilipaa hadi nje ya chumba kiasi kwamba ziliwakera hata wateja wengine. Mkuki aliendelea kusimamia maamuzi yake hata mwishowe Maufeng akanyoosha mikono juu, akakubali; akaomba kiasi kidogo cha pesa kwa ajili ya kwenda baa usiku huo ili kesho asubuhi waondoke kurejea kijijini Chensua.
Basi alikwenda kuongezea ulevi kwenye baa moja ambayo si watu wengi walikuwa wakiipenda; ilikuwa karibu na ufukwe, eneo ambalo lilikuwa kimya sana ukilinganisha na maeneo mengine ya kisiwani hapo. Akafika na kuagiza ‘ulabu’, akaketi kwenye meza na kuanza taratibu kupata kinywaji.
Punde wakaingia wanaume watatu na wanawake wawili, wakaketi kwenye meza ya karibu na pale alipokuwa Maufeng, wakaagiza na kundelea kunywa huku wakipiga soga na kucheka kwa furaha, walionekana kuwa ni marafiki wa karibu sana na wale wanawake walikuwa ni wapenzi wao.
Baada ya chupa mbili za bia iliyochanganywa na pombe kali Maufeng alinyanyuka ghafla, akajinyoosha huku akipiga kelele kubwa kana kwamba aliyepandwa na mashetani. Punde akanyamaza, akaanza kucheza taratibu huku akiwasogelea wale watu watano waliongia pale baa na kuketi karibu yake.
Akawafikia.
“Mbona mko na wanawake wazuri?” Akauliza Maufeng. Wale watu wakamtazama bila kumjibu, walimdharau ya kwamba alikuwa ni mlevi ambaye tayari pombe ilishamtawala kichwani mwake; lakini kumbe haikuwa hivyo; kilichomnyanyua Maufeng na kumsogeza pale hazikuwa pombe, bali ni lile tatizo lake la akili ambalo humtokea mara chache.
“Nawauliza mbona mnakuja na wanawake wazuri na wote mnakaa nao peke yenu?”
“Vipi kwani. Hebu jichunge, starehe yako isiwe kero kwetu.”
“Unasemaje. Nakukera? Sasa naondoka naye huyu.” Akasema Maufeng huku akimshika mkono mwanamke mmoja kati ya wale wawili na kuanza kumvuta.
Kitendo bila kuchelewa wale wanaume watatu wote wakasimama, mmoja akauachanisha mkono wa Maufeng na wa yule mwanamke kisha akamsukumia huko, Maufeng akaanguka chini kama kiroba cha viazi mbatata kilichoachiwa na mchuuzi.
Akasimama, akaanza kuwafuata tena, hapa akiwa amekunja ngumi kwa lengo moja tu, kupambana nao. Uwendazimu wake wa msimu ulikuwa ukimuendesha mno, na laiti kama wale watu wangefahamu tatizo lake wangeondoka na kumuacha.
Basi mmoja kati yale wanaume akata kumfundisha adabu, naye akakunja ngumi na kukaa mkao wa tayari kupigana.
Ghafla Maufeng akarusha teke huku akipepesuka kwa ulevi, jamaa akainama kukwepa, akajizungusha mara mbili na kutokea upande kushoto mwa Maufeng, akampiga ngumi konzi eneo la mbavuni, kisha akamchapa na ubapa wa kiganja cha mkono chini kidogo ya kichogo—hayo yalikiwa ni mapigo ya Kong-fu.
Basi Maufeng akapepesuka na kwenda kuangukia juu ya meza ya wale majamaa hata chupa zenye vinywaji zikapasuka na kumjeruhi.
Yule mwanaume akajiweka sawa akimsubiria aamke ili aendelee kumshushia kasheshe lakini ajabu ni kwamba zilipita sekunde kadhaa bila dalili yoyote ya Mauufeng kuamka.
“Vipi?” Wakaulizana wenyewe kwa wenyewe.
“Hebu muangalie.” Mwingine akashauri.

Basi mmoja akamsogelea na kumgeuza na papo hapo ndipo aligundua kuwa Maufeng amezimika. Akataka kujua kuwa alikuwa amepoteza fahamu au amekata roho kabisa, akamuwekea mkono shingoni kujua mwenendo wa mwili wake. Akagundua kitu, akawageukia wenzake kuwatazama. “Hamna kitu.” Akawapasha habari kisha akasimama haraka haraka. “Tuondokeni.” Akawaambia kisha kwa pamoja walitoka baa hapo mbio mbio na kuacha mwili wa Maufeng pale juu ya meza.
***************************
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000
SEHEMU YA 6


ILIPOISHIA....
Tuliona Maufeng amefanya fuj kule baa, amepigwa mpaka kupoteza maisha; wakati huo huo kesho yake asubuhi walitakiwa wafunge safari ya kurejea kijijini yeye pamoja na Mkuki.
Nini kiliendelea?
SHUKA NAYO....
Asubuhi ya safari Mkuki aliamka, hakumuona Maufeng kurejea nyumbani lakini hakutaka hilo likwamishe safari yake. Alipanga kwamba atachukua pesa zote na kurejea nyumbani, lakini ataacha ujumbe na pesa kidogo kwa Faye ili kwamba mwenzake atakaporejea ajue kinachoendelea pamoja na kupata nauli ya kumuwezesha kurejea kijijini Chensua.
Basi baada ya kujiandaa akatia pesa zote katika begi lake la mgongoni, kisha juu ya pesa akaweka nguo chache alizokuwa nazo, Akafunga begi, akasimama na kuanza kuondoka.
Kabla hata hajafika mlangoni kuna mtu alibisha hodi. Mkuki akafungua huku akiomba Mungu mtu huyo awe ni Maufeng ili waondoke pamoja. Lakini mambo yalikwenda kinyume, badala ya kumuona rafiki yake macho yake yalikutana na sura ngumu ya Inspekta Su Lee pamoja na askari wengine watatu wa kiume.
“Inspekta!? Karibu.” Akasema Mkuki huku akitabasamu.
“Unaenda wapi?” Akauliza Inspekta huku akijitahidi kuifanya ile sura yake ya ugwadu kuwa chachu zaidi.
Akajiumauma kabla ya kujibu Mkuki. “Nyumbani.”
“Peke yako?” Akauliza Su Lee.
“Aaah! Hapa... Ndiyo.”
“Ni ndiyo au hapana?”
“Ndiyo. Naondoka peke yangu.”
“Mwenzako?”
“Atakuja yeye peke yake pia.”
“Yuko wapi? Kwanini aje peke yake.”
“Aliondoka jana usiku lakini....” hakumaliza Mkuki. Inspekta Su Lee akatoa agizo la kukamatwa kwa Mkuki mara moja.
“Tazama na begi lake kuthibitisha alichokisema Faye.” Akasema Inspekta Su Lee kuwambia askari wake, Mkuki alichanganyikiwa, hakuwelewa kilichokuwa kinaendelea.
Iko hivi; baada ya Maufeng kuuawa kule baa, wamiliki walitaka kukwepa dhahama kwa sababu hawakuwa wakiwafahamu wale wauaji, hivyo ili kufanikisha hilo waliuchukua mwili wa Maufeng na kwenda kuutupa ufukweni ambapo ulionekana asubuhi na watu wakatoa taarifa polisi.
Baada ya Inspekta Su Lee na watu wake kufuatilia walikwenda kwenye 'gesti' alipokuwa akiishi Maufeng, na walizungumza na Faye kwanza kama muhudumu ambaye pia alikuwa ni mpenzi wa Maufeng. Walimueleza hali halisi kwamba Maufeng ameuawa, na wanamfikiria Mkuki kama mshukiwa nambari moja wa tukio hilo.
Hapo Faye alitiririka akiwathibitishia kwamba ni lazima Mkuki alihusika katika tukio lile.
“Jana usiku walikuwa wanagombania pesa. Itakuwa amemuua ili aondoke na pesa zote peke yake.” Faye aliwaeleza polisi namna hiyo, hapa akisimulia ugomvi uliotokea usiku wa jana kabla ya Maufeng hajachukua pesa kidogo na kwenda baa ambapo umauti ulimkuta.
Basi afande mmoja akachukua begi la Mkuki, akafungua na kuanza kutoa nguo moja baada nyingine na mwishoni, baada ya kutoa nguo zote alikumbana na maburungutu ya pesa.
“Ni kweli. Kuna pesa.” Akataarifu askari huyo na hiyo ilitosha kuwa sababu kamili ya kuondoka na Mkuki kwa tuhuma za kwamba alimuu Maufeng ili atoroke na pesa zote.
Tayari kila kitu kilianza kuingia giza tangu hapo, ni wazi kwamba kwa jinsi hali ilivyokuwa ilikuwa ni ngumu sana kwa yeye kuchomoka katika hatari ile—ushahidi wa kimazingira ulimbana; lakini pia uhasama alioutengeneza dhidi ya Inspekta Su Lee, ile ya kumkatalia kuwa mwandani wake ilikuwa ni miongoni mwa mambo ambayo pengine yatamfanya akose kabisa msaada.
*****************************
Mlango wa selo ulifunguliwa, akaingia askari mmoja aliyekonda kweli kweli, mwenye sura nyembamba yenye kuchekesha kuitazama, yenye masharubu ya dharau yaliyokaa kama kuti la mnazi juu ya mdomo wake.
Alikuwa amemfuata Mkuki, akamchukua, na kumpeleka kwenye chumba cha mahojiano. Akamkalisha kwenye kiti, kisha askari akatoka nje na punde akaingia Inspekta Su Lee na kikombe kidogo cha udongo chenye kahawa.
Akaketi kwenye kiti kingine cha mbele ya pale alipiokuwa Mkuki, wakawa wanatazamana uso kwa uso.
Inspekta akapiga funda moja la kahawa moto, kisha akakiweka kikombe juu ya meza iliyokuwa katikati yao, akamtazama usoni Mkuki kisha yakamtoka maneno; “Giza sio zuri, lakini ni sehemu nzuri ya kuziona nyota.” Akasema Inspekta.
Akaendelea.
“Upo gizani, sio kwa sababu uteketee, bali ili uweze kuziona nyota, kuzijua, na kujiweka karibu nazo. Nahisi nimekujua vizuri kwa muda mfupi nilopata kukaa pamoja nawe, najua huwezi kumuua Maufeng, huwezi kumuua mtu yotote. Huna roho hiyo.”
Akanywa kahawa Inspekta na kuendelea.
“Lakini ni nani atakayekuwa tayari kukuamini? Na hata kama yupo, Je, atakuwa na nguvu ya kuiaminisha dunia kuwa hujamuua rafiki yako? Kama hakuna anayeweza basi hakuna cha kukuondoa gizani, lazima upotelee humu isipokuwa kama utaamua kubadilika, kama utaamua kubadilisha mawazo yako, kama utaacha kufikiria kutafuta njia ya kutoka gizani, badala yake ukaamua kuzitazama nyota na kujiweka karibu nazo.”
“Mimi ni nyota Mkuki, na unanihitaji utake usitake.” Akasema Inspekta kisha akasimama, akaendelea kuzungumza. “Sikia, kesho asubuhi tutakupeleka mahakamani, ni nje ya hapa kisiwani. Na kama utapandishwa kizimbani basi habari zako zote zitaishia hapo, utapotelea gerezani. Mtu pekee mwenye uwezo wa kukuokoa ni mimi, lakini ili nikusaidie inabidi ukubali na uhaidi kunipa kile nikichokuomba.”
Akamuinamia.
“Nadhani tumeelewana. Nakurudisha ndani, jioni nitakuja kwa ajili ya kusikikiza maamuzi yako ya mwisho. Kuishi gizani au karibu na Nyota.” Akasema Inspekta Su Lee na mazungumzo yakaishia hapo, akaondoka wakati Mkuki alichukuliwa kurejeshwa selo.
Aliingia selo akiwa na mawazo maradufu ya ilivyokuwa awali. Mwanzo, kabla hajazungumza na Inspekta Su Lee alikuwa akifikiria jinsi gani atajikwamua katika dhahama hilo, lakini sasa alikuwa akifikiria jinsi atakavyokwakumuka na kwenda kuanza sekeseke jipya la kumuhudumia kingono Inspekta Su Lee.
Alikuwa katikati ya mtihani mzito lakini mwepesi, kwa sababu kwa upande wake kama mwanaume, suala la kuwa mtumwa wa ngono wa mwanamke halikuwa ni tatizo kubwa sana ukilinganisha na lile la kwenda kuozea jela.
Alitumia muda mwingi sana kujiuliza maswali lukuki ya msingi kwa ajili ya kuhakikisha anapata jawabu sahihi juu ya ule mtihani mzito anaoukabili. Nafsi yake ilimshauri kuwa asikubali kuozea jela wakati akili nayo ilimkumbusha kuwa hatopoteza chochote kuwa uraini hata kama atakuwa akitumikishwa na Su Lee. Maswali ya aina hii yalimsaidia kupata jibu moja lililosahihi kwa upande wake, kwamba atakubali kutimiza hitaji la Inspketa Su Lee ili tu aendelee kuwa uraini wakati akiendelea kupanga mipango mingine hata ya kutoroka kurejea kijijini Chensua kwa mzee Wong na Mei Lee.
Jioni Inspekta alikuja kama alivyoahidi, akaomba aletewe mtu wake kwa ajili ya mazungumzo. Mkuki alipokuja wala hawakuzungushana, mtoto wa kiume alitoa kauli iliyothabiti ya kwamba yuko tayari kufanya kama ambavyo Inspekta aliomba ilimardi tu asitupwe gerezani.
*******************************
Asubuhi watuhumiwa wengine walichukuliwa kwa ajili ya kupelekwa mjini, mahakani lakini si mkuki. Inspekta alifanya awezavyo na akaondoka naye nyumbani kwake anapoishi.
“Karibu.” Alimkaribisha ndani mara baada ya kufungua mlango. Mkuki akapita na kuketi kwenye kochi sebuleni.
Ilikuwa ni nyumba ya chumba na sebule ndogo; basi Inspekta Su Lee akaingia chumbani na alipotoka alikuwa amevalia kigauni kifupi na chepesi cha kulalia, lakini niamini mimi kwamba bado hakuwa akivutia hata kama aliacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake.
“Naenda kuoga. Nakuja.” Akasema, kisha akatoka nje kuelekea bafuni.
Kuachwa peke yake kulisisimua lile wazo la kutoroka ambalo Mkuki alikuwa nalo tangu alipofanya maamuzi ya kukubali ombi la Inspekta. Palepale akapiga hesabu matata za kufanikisha zoezi hilo, lakini jambo lililomkwamisha ni wapi ambapo atakimbilia ikiwa kisiwa cha Jiaju kilikuwa ni kidogo sana na Inspekta Su Lee alikuwa na mkono mrefu wa kipolisi, kwamba kama ataamua kumtafuta haitokwisha hata siku moja atakuwa ameshamtia mikononi.
“Nenda tu. Hayo mengine yatajulikana mbele kwa mbele.” Nafsi yake ilimpa ushauri wa kijasiri namna hiyo. Akaupokea, akasimama, akanyata taratibu na kutoka nje, Akatazama hali ilivyo na alipoona kuna utulivu wa kutosha alitimua mbio barabara bila kutazama nyuma.
Alishika njia ya kuelekea lilipo soko, na ni kama alikuwa akiongozana na malaika wa mafanikio, alifika sokoni bila hata kuwa akifuatiliwa nyuma na Su Lee. Alijibanza sehemu moja pale sokoni, karibu na eneo ambalo boti nyingi kutoka China na sehemu nyinginezo zilikuwa zikipakia samaki. Aliona jinsi shughuli ilivyokuwa ikiendelea, aliona jinsi watu wanavyoingia na kutoka kwenye boti hizo wakipakia maboksi ya palastiki yaliyojaa samaki.
Haraka akapata wazo, akaona ili kumkimbia Su Lee, ni vyema akaingia kwenye moja ya boti hizo, na akaondoka nazo zinapoelekea, kisha akiwa huko akatafuta njia ya kurejea kijijini Chensua kwa mzee Wong na Mei Lee.
JE MKUKI ATAFANIKIWA KATIKA MPANGO WAKE.
*****************************
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000
SEHEMU YA 7


ILIPOISHIA...
Tuliona Mkuki ametolewa chini ya polisi kwa msaada wa Inspekta Suu Lee ili wawe wapenzi. Lakini baada ya Mkuki kufikishwa nyumbani kwa Inspekta Suu Lee anawaza kutoroka. Je atafanikiwa?

TIRIRIKA....

Alifanya kama alivyofikiria; alinyata taratibu hadi kwenye boti moja wapo ya zile zinazopakia maboksi ya samaki, akaingia huku akiamini hakuna mtu yeyote yule aliyemuona, na huko akatafuta mahala pazuri pa kujificha na palipotulia zaidi.
Akiwa bado ndani ya boti ametulia, alimuona Inspekta Su Lee na kundi la maaskari takriban watano wakiingia pale sokoni. Akajibanza zaidi huku akichungulia na kuona jinsi waliyokuwa wakimtafuta kwa kumuulizia kwa watu huku wakiangaza huku na huko. Hapa sasa ndipo Mkuki alijikuta akigeuka kuwa mtumishi mzuri wa Mungu, alisali sala zote, aliomba na dua za kila namna ilimradi tu asiingie mikononi mwa Inspekta Su Lee kwa mara nyingine.
Lakini huenda Mungu aliyemuomba hakutaka Mkuki afanikiwe, kwani akiwa pale alimuona Inspekta Su Lee akizungumza na jamaa mmoja, bila shaka alikuwa akimuuliza kama amemuona Mkuki maeneo hayo na jamaa akaonekana akieleeza kwa mikono kuelekewa kule kule kwenye boti aliyokuwemo Mkuki.
Basi Inspekta Su Lee akaachana mtu huyo, kisha taratibu akaanza kuelekea kule kwenye boti. Moyo wa Mkuki ulidunda mara nane zaidi ya kawaida, ni kama ulifungwa turbo kwa ndani. Alihisi joto kali mtoto wa kiume, jasho jembamba lilimiminika hata akawa kama chupa ya bia iliyochomolewa katika friji yenye ubaridi wa kiasi cha kugandisha, alihisi haja pia, tena zote mbili, kubwa na ndogo, na hii kubwa ilikuwa ni ya uharo tu. Alijua kama endapo Inspekta Su Lee atamdaka kwa mara nyingine, kamwe hatopata muawana kutoka kwa mtu yeyote yule; atahukumiwa kwa kosa la mauaji, kosa la kuwatoroka polisi na makosa mengineyo ambayo Inspekta huyo ataamua kumpa.
Inspekta akakaribia kwenye boti, hapa sasa Mkuki akamsikia akizungumza na kiongozi aliyekuwa akisimamia upakiaji wa maboksi ya samaki katika boti hiyo, akamsikia akisema kwamba kuna mtu wanamtafuta, na ameonekana ameingia kwenye boti hiyo.
“Sawa. Unaweza kumtafuta.” Kiongozi akamjibu Inspekta, naye mwanamama akaingia huku akitazama kwa kupeleleza kona zote muhimu.
Mkuki alikuwa akitazama, alijituliza pale huku akitetemeka kwa uwoga. Basi Inspekta akasogea upande ule ule aliokuwamno Mkuki, akasimama mbele ya palepale alipojificha Mkuki, na ni kama alihisi kitu maeneo hayo. Akageuka, akatazama pale alipojilaza Mkuki, palikuwa na giza, ilikuwa si rahisi kuona bila ya kuinama na kuchungulia; basi naye Inspekta akaanza kuinama ili one vizuri.
“Inspekta?” ghafla alisikika mtu akiita kutoka nje ya boti, Inspekta Su Lee akaacha kutaka kuendelea kuchungulia ile sehemu, akasimama, akatazama kule alipoitwa, akamuona mmoja wa askari wake akimpungia mkono kwa ishara ya kwamba aende, kuna kitu wameona.
Inspekta akatoka ndani ya boti kwenda, huko kulikuwa na mvuvi mmoja waliyemkamata na madawa ya kulevya mengi kweli kweli hivyo ilibidi nguvu ihamie huko sasa ingawa Inspekta hakutaka kupoteza muda mwingi katika hilo; alikuwa akimtaka Mkuki tu amfunze adabu.
Basi wakati wao wanaendelea kujadili, shughuli ya kupakia mizigo kwenye boti aliyokuwemo Mkuki ilifika tamati. Nahodha wa chombo hicho akapokea maagizo kutoka kwa kiongozi kwamba awashe mashine na safari ianze mara moja, na hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Mkuki alishukuru sana pale boti ilipoanza kuacha soko la samaki la kiswani Jiaju na kutokomea baharini; hakuwa akifahamu boti inakwenda wapi lakini alichoshukuru ni kwamba alinusurika kuangamia.
Boti ilikuwa ikilekea China katika jiji kubwa na maarufu la Hong Kong. Ilikuwa ni safari ya takriban kilomita 2000 kutoka kisiwani Jiaju. Wakiwa wanakaribia Mkuki alianza kuona majengo marefu ya jiji hilo. Alihisi furaha kubwa moyoni kwa kila kitu, sura ya jiji la Hong Kong ilimfanya apate matumaini mapya ya maisha hata akajikuta anafutilia mbali wazo lake la kurejea kwenye nchi ndogo na maskini aliyotoka—hii ni sawa na kusema kwamba alifutilia mbali wazo la kurudi kwa kina Mei Lee.
Alidhamiria kuanzisha maisha hapo na kiu ya kuona hilo linafanikiwa ilimfanya hata akapata taswira ya jinsi mambo yatakayokwenda; alijiona jinsi akiomba ajira, anakubaliwa, anaanza kazi, anapata ujira wake, anatumia ujira kidogo na kiasi kinachobaki anahifadhi kwa ajili ya kwenda kukuza maisha pindi atakaporejea Tanzania kwao.
Boti aliyoipanda ilisogelea pwani ya mjini Hong Kong, ikaegeshwa kwenye eneo la bandari ndogo ambapo yalikuwepo magari kwa ajili ya kubeba samaki walioletwa na boti hiyo. Hapo Mkuki akachomoka bila kuonekana, ilikuwa ni kazi rahisi sana, na hakutaka kupoteza muda pale bandari, akaingia moja kwa moja mtaani.
Kwa mara ya kwanza kuwa China aligundua kitu; aling’amua kuwa hiyo ilikuwa ni ardhi ya fursa kwa jinsi ambavyo muingiliiano wa watu ulivyokuwa mkubwa. Aliona raia wakipishana huku na huko, kila mmoja akiwa na habari zake, na hakuonekana hata mmoja aliyekuwa akimjali yeye wala mwingine—hiii ikimpa imani ya kwamba labda hata ile kadhia ya ubaguzi itapungua.
Basi alijichanganya mtaani kama raia wengine wa kawaida, hakuna aliyegundua kwamba alikuwa ni mgeni ambaye hakuwa na kibali cha kuishi ndani ya China. Alizunguka akikatiza mitaa mbalimbali ya mji huo, ilipita mtaa wa Shengh ambao unaungana na barabara kubwa iitwayo Mao, huko akapitapita na kutokea kwenye barabara nyingine iitwayo Huan, ambayo ilimuongoza hadi kwenye chochoro moja ambayo iliundwa na majengo mawili kulia na kushoto; jengo moja likikiwa ni ofisi za kampuni iitwayo Huan Express inayomiliki boti za abiria, na jengo lilingine lilikuwa ni mgahawa mkubwa uitwao Chensee.
Jengo la mgahawa lilikuwa na mlango nyuma, kule kichochoroni ambako Mkuki alikuwa anapita. Basi karibu na hapo mlangoni aliwaona vijana sita wenye asili ya kiafrika, walikuwa wakibeba maboksi ya samaki kutoka kwenye gari na kuyaingiza ndani ya mgahawa.
Matumaini ya Mkuki yakaongezeka zaidi, akajiaminisha kwamba wale Waafirka wenzake ni lazima watampa msaada wa aina yoyote ile, ama kazi au mahala pa kulala.
Haraka akawafuata, alipokaribia wakamuona, walikuwa wamepumzika kubeba maboksi japo kwa dakika moja.
Akawafikia.
“Habari zenu?” Akawasilimu kwa lugha ya Kithaiwan, lugha ambayo ilikuwa ni sawa na Kichina tu.
Wakamuitikia kwa pamoja. Akaendelea. “Ndugu zangu nina shida, sijui naweza nikapata msaada kutoka kwenu?.”
“Ongea tu.” Mmoja akamjibu.
“Mimi naitwa Mkuki, nimeingia leo hapa China. Hizi mnavyoniona sina hata sehemu ya kulala, na sina ndugu wala simfahamu mtu yeyote hapa Hong Kong, naombeni mnisaidie hifadhi kwa siku mbili tatu.” Akajieleza lakini badala ya wale watu kumjibu walianza kuinuka mmoja baada ya mwingine na kuanza kubeba maboksi ya samaki na kuingiza ndani.
Mkuki alibaki ameduwaa, hakutegemea mapokeo ya aina ile kutoka kwa watu ambao alikuwa akifanana nao asili. Walimuacha peke yake kwa mtindo wa kumdharau sana kana kwamba aliongea pumba tupu.
Punde mmoja wa wao akarudi kwa ajili ga kuchukua boksi lingine, hakumsemehsa Mkuki kana kwamba hakuwa akimuona pale alilosimama.
“Ndugu yangu.” Mkuki akaamua kumuita, yule mwanaume akaacha kubeba boksi akamgeukia.
Mkuki akaendelea. “Naomba nisaidie Kaka. Sisi ni kitu kimoja.”
“Umetokea wapi?’ Akauliza.
“Nimetokea Thaiwan.”
“Kwahiyo wewe ni Mthaiwan?”
“Hapana. Yaani nilikuwa naishi huko, lakini mimi ni Mtanzania.” Akafafanua.
“Mtanzania? Sawa. Lakini sikia nikwambie, China kuna maisha magumu sana tofauti na unavyofikiria, sio rahisi kupata msaada kwa mtindo wako unaoutumia. Labda cha kukusaidia nikuitie Mtanzania mwenzako ndo mnaweza mkaelewana, ila binafsi sina cha kukusaidia.”
“Wewe ni wapi kwani?” Akauliza Mkuki.
“Kwani unataka kugundua nini? Sioni faida ya wewe kujua asili yangu, cha msingi ni uniambie kama nikuitie Mtanzania mwenzako au niache.”
“Sawa. Niitie.” Akasema Mkuki,
Basi yule jamaa akabeba boksi la samaki, akaingia mgahawani akimuacha Mkuki akisubiri mrejesho wa kile alichoahidiwa.
Jamaa yeye alikuwa ni mtu kutoka Ghana; yeye pamoja na wale wenzake walikuwa ni vibarua wa kazi mbalimbali hapo mgahawani; walibeba maboksi, walioosha vyombo na kadhalka—walitoka kwenye ardhi za mama zao kwa ajili hiyo ya kutafuta maisha nchini China.
Basi punde yule jamaa akarejea akiwa mikono mitupu, alikujua kuchukua boksi moja ambalo liliasalia kwenge gari pamoja na kumpa mrejesho Mkuki juu ya kile walichokubaliana.
“Anakuja.” Akawambia Mkuki juu kwa juu, yaani hata hakusimama, alizungumza huku akienda kwenye gari, akachukua boksi la samaki ambalo lilikuwa la mwisho kwenye gari, akaingia nalo mgahawani akimuacha mkuki amesimama pale pale.
Sekunde sitini baadae ule mlango wa mgahawa ukafinguliwa, akatoka mwanaume mrefu, mnene, mweupe mwenye nywele zilizopunguzwa kawaida na hata ndevu pia. Alikuwa amevalia eproni jeupe kama wale waliokuwa wakibeba maboksi lakini la kwake liliuwa limechafuka zaidi.
Mkuki hakumuona sura na hata yule jamaa hakumuona Mkuki kwa sababu alitoka kinyumenyume akiwa anazungumza na mtu aliyekuwa ndani.
Mkuki akajiweka sawa, akajipanga barabara kwa ajili ya kuzunguma na Mtanzania mwenzake huku akimaini kwamba kwa hatua hiyo aliyofikia msaada utakuwa ni kiti cha lazima.
Yule jamaa akamaliza kuzungumza, akageuza uso wake alipokuwa Mkuki lakini ghafla aliacha kutembea, akamtazama Mkuki kwa kumtumbulia macho kana kwamba amemuona mtu waliyepotezana kitambo kirefu.
“Mkuki?” Jamaa akaita kwa sauti yenye mirindimo iliyoashiria kutoamini kile anachokiona.
“Meja!?” Mkuki naye akalipa mapigo kwa mtindo ule ule.
Basi hapo kilifanyika kitendo ambacho si cha kawaida; Meja alimkimbilia Mkuki na kumkumbatia huku akilia tena machozi kabisa kama mtoto mdogo na hata kwa Mkuki ilikuwa hivyo hivyo.
********************************
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000
SEHEMU YA 8


ILIPOISHIA...
Tuliona Mkuki amefika China, na kwa bahati amekutana na mtu anayemfahamu. Je nini Kiliendelea.

SHUKA NAYO.....
“Mkuki umepona ndugu yangu? Siamini, siamini kaka.” Alisema jamaa yule ambaye Mkuki alimuita kwa jina moja la Meja.
Mkuki alishindwa hata kuzungumza, aliendele kuangua kilio kama mtu aliyechanganyikia, akawa anamuachia kidogo Meja, anamtazama usoni kisha anamvuta wanakumbatiana tena.
Baadae waliachana, kila mmoja akjifuta machozi, Meja akamtaka Mkuki wasogee karibu na ile gari iliyokuwa na maboksi ya samaki, wakasimama hapo kwa kuigemea.
“Mkuki ujue siamini kama ni wewe? Uliponaje?”
“Ni stori ndefu Meja, nadhani tutapata muda nitakusimulia vizuri. Nashukuru Mungu nimepona.”
“Dah! Kwahiyo ulijuaje niko hapa?”
“Hata nilikuwa sifahamu kama nitakukuta hapa. Mi nilikuja natafuta kazi.”
“Kwahiyo unaishi maeneo gani?”
Akajichekesha kidogo Mkuki kabla ya kujibu. “Hata sijui nikujibu nini. Mimi sina hata pakulala Meja, ndo kwanza nimeingia leo hapa China.”
“Kwahiyo ulikuaa unaishi wapi sasa?” akauliza Meja, na yeye hupenda kutumia sana neno 'kwahiyo' kwenye mazungumzo yake.
“Nitakwambia tutapotulia. We unaishi wapi?”
“Niko hapo nyuma, panaitwa Huanzou. Nimepanga, naishi na mwanamke na tuna mtoto mmoja wa kiume anaitwa Jisu, nimeamua kumpa jina la muasisi wa hii safari yetu aisee.” Akaeleza Meja.
“Dah! Hongera. Na hapa ndo kazini?”
“Ndiyo. Naosha-osha vyombo bwana, lakini nashukuru Mungu mkono unaenda kinywani.” Akasema na kuongeza. “Sasa sikia Mkuki, inabidi mi nirudi ndani nikakimbize. Ngoja nikuletee kitu ukae hapa unisubiri, namaliza kazi muda si mrefu tunaondoka pamoja nyumbani.” Akasema Meja kisha akaingia ndani na punde akatoka akiwa na kreti tupu, akampa Mkuki akalie halafu yeye akarudi tena ndani.
Mkuki alikaa pale nje asiamini kilichotokea; aliona ni kama muujiza ama ngekewa, na alishindwa kabisa kujizua kumshukuru Mungu kwa kumuongoza hata kukutana na msaada wa uhakika namna ile.
Meja alikuwa ni rafiki yake, mshikaji wake na kaka yake wa hiari pia. Kiumri Mkuki alikuwa mdogo kwa Meja, alizidiwa miaka takriban sita ingawa alionekana ni mkubwa kutokana na maisha magumu aliyopitia.
Aliendelea kuwa pale huku akikumbuka jinsi ambavyo alipata kujuana na Meja; walivyokutana kwa mara ya kwanza na jinsi walivyokuza urafiki wao.
Aliikumbuka siku ile, ilikuwa ni Jumamosi jioni, alitoka nyumbani kuelekea kwenye Uwanja wa Mpira wa miguu wa Shule ya Msingi ya Tandale ‘A’ iliyopo huko Tandale ambapo wote wawili, Meja na Mkuki walizaliwa na kukulia. Alikwenda kutazama mechi iliyozikutanisha timu mbili kutoka Tandale; Mafisi FC kutoka Tandale Sokoni na Wakali wa Danta kutoka Tandale Bondeni.
Mkuki alifika na kusimama pembeni mwa uwanja akiegemea ukuta wa jengo moja la madarasa ya shule ya msingi Tandale. Pembeni yake kulikuwepo na kundi la vijana wapatao nane wakivuta bangi; ni kawaida kwenye viwanja vya mpira vya shule nyingi Tanzania, kila jioni vijana wa kihuni hujumuika huko na kuvuta bangi haswa zinapochezeka mechi za timu za mitaani namna hiyo.
Miongoni mwa lile kundi la vijana nane alikuwepo Meja, alikuwepo na Jisu pia ambaye yeye ndiye aliyekuwa ‘Pusha’, yaani aliyekuwa akiwauzia wenzie bangi.
Basi Mkuki alifanya kazi mbili akiwa pale aliposimama, macho yake yalitazama kabumbu wakati masikio yalisikiza mazungumzo ya wale wavuta bangi wa karibu yake.
Mada kubwa waliyokuwa wakiijadili ilikuwa ni kuzamia nchini Afrika ya Kusini kwenda kutafuta maisha, na Jisu alitawala mazungumzo yao; alionekana kuijua mno Afrika kusini kwa jinsi ambavyo aliielezea. Aliwasimulia wenzie jinsi ambavyo watu huzamia meli, wanavyoishi baada ya kufika Afrika Kusini, wanavyotafuta pesa na mambo mengine mengi.
Stori zile zilimvuti sana Mkuki hata akajikuta akihamisha akili yake yote upande ule badala ya kutazama kabumbu. Yeye alikuwa ni miongoni mwa vijana wengi wa Kitanzania wasiokuwa na kazi wala kibarua rasmi cha kuwaingiza kipato cha kuendesha maisha yao, kiasi kwamba nafsi zao ziliingiwa giza na imani mbovu ya kwamba ni rahisi sana kufanikiwa kimaisha kama utapata fursa ya kufanya kazi yoyote ile katika mataifa yaliyoendelea.
“Mimi nilikuwa naishi Pritoria, yaani kule ndo pesa nje nje. Ukiwa mjanja mjanja mbona shega tu, unapiga sana pesa.” Mkuki alimsikia Jisu akizungumza namna hiyo; hakuwa akimfahamu hata kwa jina lakini kwa yale mazungumzo yake aligundua kwamba jamaa huyo alishawahi kuishi Afrika Kusini.
Basi Mkuki aliendelea kuwasikiliza akiwa palepale huku nafsi ikimsukuma kutamani kupata nafasi japo mara moja ya kuishi Afrika kusini ili apate pesa zile alizokuwa akizisimulia Jisu, ili aweze kujikimu yeye sanjari na kuwasaidia wazazi wake ambao walikuwa wazee wasiokuwa na msaada licha ya kwamba walikuwa na watoto tisa kujumuisha na Mkuki.
Basi wakiwa bado palepale uwanjani, ghafla Mkuki aliona watu wakikimbia hovyo kuja upande aliokuwa amesimama yeye, kisha papo hapo akawaona wahuni nao wamesiamama na kuanza kutimua mbio huku wakipishana taarifa kwamba kulikuwa na kundi la maaskari polisi limevamia uwanjani hapo kwa ajili ya kuwakamata wavuta bangi.
Ni kweli, askari hao walikuja kwa lengo la kuwanasa wavuta bangi lakini kutokana na hali ilivyo hata waliokwenda kutazama mpira tu walikimbia kwa kuhofia kukamwatwa na kuchanganywa na kundi ambalo hawakuwa miongoni mwao—basi ikawa ni patashika nguo kuchanika, watu walikimbia huku na huko na kutimua vumbi si kidogo.
Basi Mkuki alikuwa ni miongoni mwa wasiovuta bangi lakini wakakimbia kujiepusha na dhahama. Alitoka mbio kulelekea upande ambao haukuwa na polisi wengi na ni watu wachache tu waliopita huko. Mbele yake alimuona Meja akikimbia sambamba na Jisu, yule muuza bangi aliyekuwa akitoa simulizi nyingi kuhusu Afrika Kusini.
Mkononi Jisu alikuwa ameshikilia mfuko wa nailoni uliokuwa umejazwa bangi za biashara, alihakikisha ameukamatia kwa uhodari ili usije ukadondoka na akapata hasara kubwa. Lakini akiwa bado kwenye mbio ghafla kandambili yake aliyokuwa amevaa ikakatika, mkanda ukamnasisha na kupelekea anaanguke chini kama mzigo. Alibingilika huko Jisu, wakati mfuko wake wa bangi uliangukia mbali na yeye. Akajitahidi kuinuka mara moja, akatazama umbali wa zilipo bangi zake akilinganisha na umbali wa askari polisi, na kwa hesabu za haraka akagundua kuwa kama atathubutu kusema azifuate bangi hizo basi askari watamfikia na kumtia mbaroni.
Akapiga moyo konde, akaonelea ni vyema kama atajinusuru yeye kuliko kukamatwa na kutupwa selo ambako ili kutoka angetakiwa atoe rushwa ya kiasi kikubwa cha pesa ukilinganisha na thamani ya zile bangi zake.
Akakambia, akauacha mzigo.
Mkuki aliuona mfuko ule, alipoufukia akauokota, kisha akendelea na safari yake lakini kwa bahati mbaya askari polisi mmoja alimuona, hivyo akaanza kumfukuza yeye kama yeye.
Mkuki aligundua ugeni huo uliokuwa nyuma yake, na hapo sasa akanuwia kwamba atakimbia mpaka mwisho wa pumzi yake ili asinase mikononi mwa askari wale wachapakazi lakini wapendwa rushwa, kwani laiti kama watamkamata, hatotoka nyuma ya nondo hadi pale atakapotoa hongo ya kiasi kikubwa cha pesa.
Basi mbio za Mkuki na polisi zilihamia hadi mtaani, Mkuki alikatiza chochoro hizi na zile ili kumpoteza afande huyo lakini bado askari alikuwa nyuma yake, bila shaka hata yeye alinuwia kwamba ni lazima amkamate tu—ilikuwa ni mshikemshike.
Basi Mkuki alipita chochoro mbili tatu na alipotazama nyuma akagundua kuwa amempoteza kidogo yule askari. Hakuona sababu ya kuendelea kukimbia zaidi, hapo aliamua kuingia kwenye ua wa nyumba moja ili apate kujificha. Ubaya ni kwamba ua wa nyumba aliyoingia ulikuwa mtupu, haukuwa na sehemu ya kujificha. Akapiga hesabu za haraka, akagundua kwamba kama atathubutu kutoka nje na kuendelea kukimbia ni lazima yule afande atamkuta na kumtia mbaroni, hivyo ilikuwa ni lazima atafute pahala salama pa kujificha ndani ya nyumba ile ile.
Akapata wazo ndani ya sekunde chache; akaona itakuwa vyema na salama zaidi kwake kama ataingia kwenye choo cha nyumba hiyo na kujituliza kimya hadi pale atakapohakikisha hali imetulia.
Akafanya hivyo, akasogelea choo cha nyumba hiyo, akafunua pazia la kiroba lililokuwa likining’inia mlangoni, akaingia ndani, akajituliza tuli.
Akiwa huko alimsikia yule askari akipita, akasikia kama amekwenda mbele kisha akarejea, na akamsikia akimuuliza mtu kama alimuona kijana fulani akikimbia na mfuko, hakusikia jibu lakini punde kidogo baadae alisikia ukimya tu.
Mkuki alikaa mle chooni hadi alipojihakikishia kwa imani kwamba hali imetulia kabisa, akatoka akiwa na ule mfuko wenye bangi bila kuonekana na akashika njia ya nyumbani kwao moja kwa moja.
Alifika nyumbani, akaingia ndani kabisa na kujifungia chumbani, akauweka ule mfuko kitandani, akaufungua na kuzitamzama zile bangi. Zilikuwa ni nyingi sana hata akaingiwa na hesabu za haraka kuziuza na kupata kiasi kikubwa sana cha pesa.
Basi baada ya pale akafunga mfuko, akauficha uvunguni mwa kitanda na kutoka kwa ajili ya kwenda mtaani kutafuta mteja wa kununua zile bangi.
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000
SEHEMU YA 9


ILIPOISHIA...
Tuliona Mkuki amefanikiwa kumtoroka Inspekta Su Lee na ametorokea China. Huko akakutana na Mtu anayemfahamu; Na sasa ngoja na sisi ni nan huyu, walifahamiana vipi?
SHUKA NAYO.....
Lakini siku zote biashara chafu hufanywa na watu wazoefu, na hii ilipelekea Mkuki ashidwe kabisa kupata mteja wa kununua zile bangi kwa takriban siku saba kwa sababu hakuwa akifahamina na wateja na aliogopa kumuuliza kila mtu kwa sababu ile ilikuwa ni biashara haramu. Sasa akachoka na biashara hiyo isiyouzika, na wazo pekee alilokuwa nalo ni kuurejesha ule mzigo kwa mwenyewe.

Basi alichokifanya ni kwenda kule kule uwanjani akiamini atamkuta Jisu na amrudishie mzigo wake. Lakini mambo yalikuwa tofauti, siku aliyokwenda hakumkuta Jisu ingawa katika angalia angalia yake alimuona Meja; alikumbuka kwamba jamaa huyo na yule muuza bangi walikuwa pamoja.
Akamfuata, akamsalimu.
“Poa dogo. Nambie.” Akajibu Meja.
“Braza kuna Ishu hapa. Tunaweza kusogea kwa pale tuongee?”
“Aina noma.” Meja akainuka. Wakasogea kwa pembeni.
“Enhee, sema dogo.”
“Braza unakumbuka siku zile polisi walivyokuja hapa?” Akauliza Mkuki.
“Lini? Unasemea hii juzi? Maana hapa polisi ni kama nyumbani kwao mdogo wangu.”
“Ndiyo, juzi kulivyokuwa na mechi ya Mafisi na Wakali wa Danta.”
“Ndio. Nakumbuka. Imekuweje?”
“Wakati mnakimbia yule braza mwingine, yule mweusi hivi mwenye ndevu za timbalendi, alidondosha mfuko wake. Mimi niliukota.”
Meja akashituka. “Ule mfuko wa bangi!?” Akauliza.
“Ndiyo.”
“Uko wapi?”
“Nyumbani.”
“Uko vile vile, hujaugusa?”
“Ndiyo.”
“Kudadadeki! Tunaweza kwenda kuuchukua sasa hivi?”
“Sawa tu.”
“Twenzetu. Halafu nitakupeleka kwa mwenyewe. Lazima akutie vitu mdogo wangu, lazima upate ganji. Unajua ule mzigo ndo ulikuwa kila kitu kwa jamaa, biashara yake yote iko pale. Tangu upotee amekuwa mgonjwa, hata hapa graundini hatokei. Twenzetu.” Akaeleza Meja kisha akamchukua Mkuki wakaanza safari.
“Oyaa. Wapi hiyo?” Wenzake wakamauuliza.
“Nakuja wanangu. Dogo anamchongo hapa, ngoja nikausimamie.” Akawajkbu na wakatokomea huko yeye na Mkuki.
Walifika nyumbani kwa kina Mkuki, Meja akasuburi nje, Mkuki akaingia ndani na punde akatoka akiwa na ule mfuko. Meja akauchukua kwanza, akaufungua kuthaminisha kisha aliporidhika wakaondoka.
Safari yao ilifika tamati alipokuwa akiishi Jisu, yeye alikuwa amepanga chumba kimoja maeneo ya huko huko Tandale.
“Hapa ndo gheto kwa jamaa.” Akasema Meja huku akibisha hodi.
“Nani?” Jisu aliuliza kutokea ndani, sauti yake ilisikika ya kama mgonjwa.
“Meja hapa.”
“Poa. Tulia, nakuja.” Akajibu Jisu, kisha sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa.
“Vipi?” Akauliza Jisu akiwa amesimama katikati ya mlango wa chumba chake.
“Umemuona huyu dogo? Ni ninja mmoja hatari sana. Tuingie ndani nikupe mchongo mzima.” Akasema Meja.
Basi Jisu akaingia ndani, Meja akaufata kisha Mkuki akawa wa mwisho.
“Rudishia mlango dogo.” Jisu akamwambia Mkuki, naye akafanya hivyo.
“Kaa chini dogo ninja. Hapo.” akasema Meja kumuelekeza Mkuki, naye akafanya hivyo. Akatulia kwenye kiti karibu na alipokuwa ameketi Meja.
Chumba cha Jisu kilikuwa ni gheto kweli kweli, kulikuwamo na kitanda kidogo cha futi tatu kwa sita chenye godoro lililolegea mithili ya ulimi wa mbwa, maboksi makubwa matatu ambayo alikuwa akiyatumia kama kabati kuhifadhia nguo na makorokoro mengine. Kulikuwepo ma meza ndogo pia pamoja na kiti cha kutosha watu watatu ambacho Meja na Mkuki walikalia.
“Sasa Jisu, huyu dogo ana mchongo. Hivi unaitwa nani dogo.” Akaanzisha mazungumzo Meja.
“Mimi? Naitwa Mkuki.”
“Umesikia kwanza hilo jina? Dogo ni mkuki kweli. Anachoma kinomanoma,” akapamba Meja, alikuwa ni mtu wa maneno mengi kweli kweli kwa kipindi kile.
Akaendelea.
“Sasa umeona huu mfuko? Una bangi zako uzoangusha juzi. Kumbe dogo alichumpa, akaziokota, akayoyoma nazo. Kwahiyo leo kaja kukucheki graundini hajakukuta.”
Kitendo cha Meja kueleza kwamba bangi zimeokotwa kilimfanya Jisu ashindwe kujizuia kufurahi, alijikuta akicheka kwa furaha mno kiasi kwamba hata Mkuki akagundua kuwa jamaa huyo alikuwa na meno meusi kutokana na uvutaji wa sigara wa kiasi kikubwa.
“Ziko vizuri?” Akauliza Jisu huku akicheka.
“Yaani kama zilivyokuwa. Dogo kanambia hajazigusa. Au siyo dogo?”
“Ndiyo.”
“Umesikia. Ndo maana namuita huyu dogo Ninja. Dogo mpe mzigo wake.” Akasema Meja, hapo Mkuki akajisogeza kidogo karibu na Jisu, akanyoosha mkono kumkabidhi ule mfuko.
Jisu akaupokea, akaufungua na kutazama; mara akaachia tabasamu zito.
“Dogo we ni Ninja. Nimeamini.” Akasema Jisu na kuongeza na swali. “Unaishi wapi?”
“Bondeni kule.” Akajibu Mkuki.
“Anakaa karibu na kwa kina Supa.” Meja akatoa ufafanuzi zaidi.
“Basi poa mdogo wangu. Kwa hiki ulichokifanya lazima nikutoe. Sema hapa sina kitu. Baadae nitakutafuta basi ili tugawane umaskini.” Akasema Jisu akimaanisha lazima ampe zawadi Mkuki kwa kile alichokifanya.
Hivyo ndivyo Mkuki alivyofahamiana na Meja kabla ya kwenda kukutana naye China, na tangu siku ile walikuwa ni maswahiba wakufa na kuzikana. Mkuki akawa ni mmoja wao sasa, akajifunza yote yaliyomfanya afanane na kina Meja. Alianza kunywa pombe, kuvuta sigara na hata bangi pia. Aliongozana nao kila mahali na sasa Meja na Jisu ndiyo ikawa ‘kampani’ yake ingawa walikuwa wamemzidi sana umri.
***********************************
Akiwa bado pale pale kwenge mgahawa Meja alikuja akiwa amebadilisha nguo, amevaa nguo zake binafsi.
“Sasa. Twenzetu.” Akamwambia Mkuki.
“Ushamaliza kazi?”
“Hapana. Nimeomba ruhusa tu. Ningesema nikae hadi muda wa kutoka ungenisubiri sana.” Akafafanua Meja kisha safari ya kuelekea nyumbani kwake ikaanza.
Walikwenda kwa miguu tu, hapakuwa mbali sana kutoka ofisini kwa Meja kiasi kwamba labda wangehitaji usafiri; ilikuwa ni kama mwendo wa nusu saa kwa waendaeo kwa miguu.
Njiani walipiga soga na kuulizana mambo mbalimbali hasa kuhusu jinsi ambavyo walifika China.
“We uliponaje?” Aliuliza Meja.
“Yaani kaka hata sielewi. Nadhani ni Mungu tu ameamua kuniacha hai. Yaani ulivyotokea ule mlipuko sikuelewa kilichoendelea. Nikaja kushtukia naamka kwenye sehemu ambayo hata siiijui, ni Thaiwan huko, kuna mzee aliniokota ufukweni ndo nikaishi kwake muda wote....” akaeleza Mkuki, hapa akisimulia maisha yake yote ya kwa mzee Wong lakini akijitahidi kufupisha baadhi ya mambo.
“Ndo nikadandaia boti, ndo imenileta hapa China.” Akamaliza kusimulia Mkuki. “Wewe ilikuwaje?” Akaamuuliza Meja.
“Mimi ile ngoma ilivyolipuka tu nikaangukia baharini, nikajitahidi kuogelea kama dakika kumi fulani, nikaja kupewa msaada na Wachina fulani hivi walikuwa na boti. Kuja China wakataka kunipelekea ubalozini, nikawapiga chenga, nikaingia zangu mtaani, nikaanzisha harakati zangu, mambo ndo kama hivi unavyoniona.” Akasema Meja.
Pengine stori zao walizielewa wenyewe lakini ukweli ni kwamba Meja na Mkuki walifika hapa walipo leo baada ya kuzamia meli ili wakatafute maisha bora nchi za Ulaya-- kwa kipindi hicho, miaka ya 1990 kurudi nyuma, kuzamia ughabibuni kwa kutumia meli za mizigo ulikuwa ni mchezo kabambe kwa vijana.
Walifanikiwa kukaa kwa siku tatu tu ndani ya meli hiyo iliyokuwa ikieleka nchini Ireland na siku ya nne wakakamatwa na walinzi wa meli. Walinzi wa meli hiyo walikuwa na adhabu moja kubwa kwa ajili ya wazamiaji wanaowakamata. Huwachukua na kuwafungua kwenye msalaba wa chuma walioutengeneza maalum kwa ajili ya kazi hiyo kisha hushindana kuwapiga risasi za kichwa huku wakiwekeana dau; mchezo huu waliuuita “Headshot betting”, yaani ‘kamali ya kulenga kichwa’
Matumaini ya kina Mkuki kuishi Ulaya yalianza kupotea tangu walivyotiwa mbaroni; wote walifahamu huo ndio utakuwa mwisho wa uhai wao, na baada ya kuuliwa watatupwa baharini na kuwa chakula cha samaki.
Basi wakwanza kupandishwa pale msalabani alikuwa ni Jisu, alichukuliwa na askari wawili huku mwenyewe akijitahidi kuwa mpole, alijua kwamba hakukuwa na muawana katika hilo, kifo kilikuwa ni jambo la lazima kwa pale walipofikia.
Wakampandisha, wakamfunga mikono na miguu ili asichimoke, basi akawa ananing’ia pale msalabani kama Yesu wa kwenye filamu.
Askari mmoja akachukua bastola ndogo waliyokuwa wakiitumia, akasogea mbele ya wote, kwenye eneo ambalo mtu anayelenga anatakiwa kusimama. Akanyanyua bastola kumuelekezea Jisu pale juu huku lengo lake likiwa ni kumpiga risasi ya kichwa ili akombe dau waliloliweka askari wote wanaoshiriki mchezo huo.
“Paaa.” Mara Mlio wa risasi ukasikika, hapo Mkuki, Meja na wote walishuhudia damu zikiruka kutoka kichwani mwa Jisu; basi Askari wakaanza kushangilia kana kwamba kile kinachotendeka kilikiwa ni cha kufurahisha mno.
Risasi ile ilimpata Jisu kichwani kama ilivyotakikana, na si kumpata tu bali ilitwaa kabisa uhai wake—Alikufa na kuacha ndoto zote za kutafuta maisha ughaibuni zikining’inia pale juu, msalabani.
Mkuki na Meja walizidi kuchanganyikiwa? Walilia kama watoto wadogo huku wakiwasihi na kuwaomba wale askari waachie ingawa hakuna hata mmoja aliyewajali, wote akili zao zikikuwa kwenye pesa za kamali ile ya kishenzi waliyokuwa wakiicheza.
Baada ya mshindi wa kwanza kupata kitita chake cha pesa dau jingine likachangwa, kisha baada ya hapo askari watatu wakaenda kumfungua Jisu pale msalabani na mwili wake ukatupwa baharini papo hapo ili awe chakula cha samaki. Kisha wakaja walipo Mkuki na Meja, na sasa ikawa ni zamu ya Mkuki.
Wakamchukua, wakamvuta kuelekea msalabani. Yeye hakuwa mtulivu kama alivyokuwa Jisu, aliwasumbua kwa kukukuruka huku na huko lakini walimmudu kwa sababu walikuwa ni watu watatu, wakakamavu na walimpiga pia.
Wakamfikisha msalabani akiwa hoi kwa kipigo cha muda mfupi tu. Wakampandisha msalabani na kumning’iniza kama ilivyokuwa kwa Jisu. Alikiona kifo, aliisikia sauti ya umauti, akanusa harufu ya kaburi na mguso wa kunyofolewa roho pia aliupata. Alijuta kufahamiana na kina Meja, alijuta kuwa mmoja wao kwenye safari ya kwenda kutafuta maisha bora ughaibuni. Alijutia kila kitu.
Basi baada ya kutundikwa askari mmoja akachukua ile bastola yao, akasogea pale ambapo anayelenga husimama, akanyanyua bastola yake kumlenga Mkuki; mwenyewe Mkuki alifumba macho ili asione chochote kitakachoendelea, alizungumza na Mungu wake pia na kumuomba msamaha wa kila jambo baya alilowahi kulifanya ili atakapofika huko Akhera apokelewe kwa ukarimu.
Ghafla mlio wa risasi ulisikika, hata Mkuki mwenyewe aliusikia, akajua kwamba hiyo ni risasi aliyotumiwa kwa ajili ya kutolewa uhai wake. Lakini ajabu ni kwamba zilipita sekunde tano akiwa hai—hapo akagundua kwamba mlengeji alimkosa.
Akafungua macho Mkuki, lakini alichokiona kilimstaajabisha mno. Alimuona yule askari aliyekuwa akimlenga amelala chini akitokwa damu huku ile bastola yake ikiwa pembeni.
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000
SEHEMU YA 10


ILIPOISHIA...
Tuliona Jisu ameshauawa kwa kupigwa risasi ya kichwa, na sasa ni zama ya Mkuki. Je atauawa au atanusurika. Na kama atanusirika atanusurika vipi?

SHUKA NAYO...
Ghafla milio ya risasi nyingi zaidi ikaanza kurindima, hapo sasa wale walinzi walionekana kukimbia huku na huko kama wendawazimu.
Meli ilikuwa imevamiwa na kundi kubwa na maarufu la maharamia watekaji meli ambao walikuwa wakijijta “New generations Pirates” ; yaani “Maharamia wa Kizazi Kipya”. Kundi hilo lilikuwa na Makao Makuu yake nchini Somalia, lilikuwa limesheheni vijana wengi wa kiafrika waliopata mafunzo ya kijeshi na uharamia.
Wenyewe huteka meli kwa oda maalum kutoka mataifa makubwa yenye mvutano hasa wa kibaishara; kwa mfano Taifa la China linaweza kuwatuma wakateke meli ya Marekani lakini haya hufanyika kwa usiri mkubwa, wanaofahamu huwa ni viongozi wa juu wa kundi.
Siku hiyo walipata oda ya utekaji meli hiyo kutoka kwa nchi ya Korea Kaskazini, na lengo kuu ilikuwa ni kutwaa madini ya Uranium ambayo hutumika kutengenezea mabomu ya Nyukilia, na inasemekana kwamba, mzigo huo ulikuwa ni wa taifa la Marekani bali waliwatumia Ireland kama daganganya toto ya mataifa mengine kwa sababu kwa kipindi hiko dunia ndiyo ilikuwa mbioni kuzisimamisha imara juhudi za kupiga vita utengenezaji wa mabomu ya nyukilia ambapo kimsingi taifa la Marekani ndiyo lilikuwa kinara la kuhakikisha hilo linafanikiwa.
Basi mapambano yalikuwa ni makubwa mno, meli ikageuka kuwa uwanja wa vita. Walinzi wa meli walishambuliwa mno, na walishindwa kabisa kuwazuia maharamia hao kwa sababu walikuwa wengi sana. Ilikuwa ni vita ya dakika kumi tu na tayari meli ilikuwa chini ya maharamia hao, na sasa wakawa wanaongoza kuelekea Korea Kaskazini badala Ireland.
Baada ya hali ya utulivu kuchukua nafasi ndipo sasa Mkuki na Meja walipewa msaada na wale maharamia huku wakiamrishwa kuwa miongoni mwao. Ilibidi wakubaliane nao tu kwa sababu walichokuwa wanakihitaji kwa muda ule ilikuwa ni uhai.
*******************************
Taarifa ya kutekwa kwa meli ya Ireland iliifikia serikali ya Marekani. Haraka kilifanyika kikao cha dharura cha viongozi wa juu wa serikali hiyo na wakayajadili madhara makubwa ya endapo madini yale yatawafikiwa mahasimu wao Korea Kaskazini.
Tamati waliamua kwamba ni lazima meli ile isambaratishwe mapema kabla mzigo haujafikishwa Korea na hivyo ndivyo ambavyo ilifanyika. Serikali ya Marekani, kupitia jeshi lake waliachia kombora la masafa marefu lililokwenda kubutua meli yote hiyo, na kwa kipindi hicho meli ilikuwa karibu kabisa na Thaiwan ambapo Mkuki aliishi na mzee Wong na Mei Lee.
Basi meli yote ilisambaratishwa na bomu lile, mahariamia karibu wote waliuawa na kuishia baharini lakini Mungu aliamua kufanya miujiza yake kwa Mkuki na Meja.
Mkuki yeye alipoteza fahamu mara baada ya bomu kuisambaratisha meli, lakini maji ya bahari yakamchukua hadi kwenye fukwe za Thaiwan ambapo mzee Wong alimuokota na kumsaidia kumpa matibabu.
Meja yeye aliogela kwa muda mefu kidogo hadi alipata msaada kutoka kwa Wachina waliokuwa karibu na meli ile, na hivyo ndivyo walivyookoka.
*************************************
Walifika kwenye jengo alilokuwa akiishi Meja, jengo la ghorofa saba na yeye Meja alikuwa akiishi ghorofa ya nne. Lifti ya jengo hilo ilikuwa imeharibika, hivyo walipanda juu kwa kutumua ngazi tu.
Dakika chache wakafika mbele ya mlango wa nyumba yake, Meja akatoa funguo mfukoni, akafungua mlango wakaingia.
“Karibu.” Akasema Meja kumwambia Mkuki ambaye mara baada ya kuingia alijikuta akishindwa hata kuketi chini kwa kushangaa.
Meja alikuwa akiishi mahala pazuri mno, kiasi kwamba Mkuki aliona kama Mungu alikosea sana kwa kutokumuumba yeye kuwa Meja. Aliingiwa na wivu usioelezeka, alitamani kila kitu kilochokuwa mle ndani hata akajilaumu mwenyewe kwanini alikawia kuja China na kuendelea kuishi kule Thaiwan vijijini.
Nyumba ya Meja ilikuwa na vyumba vitatu vya kulala, sebule, jiko na stoo ndogo. Hapo sebuleni palivutia mno, ‘fanicha’ za gharama na za kisasa zilikuwepo, vifaa vya umeme kama vile televisheni kubwa na ya kisasa, redio, kiyoyozi na kadhalika, vyote vilikuwemo hapo. Hakika Mkuki alishindwa kulizuia bumbuwazi lake.
“Keti basi.” Meja akamwambia.
“Dah! Meja hongera sana. Una maisha mazuri mno.”
“Kawaida tu Mkuki. Kaa chini basi.” Akasema Meja.
Mkuki akakaa chini huku bado akiwa katika hali ile ile ya bumbuwazi, wivu na tamaa.
“Nakuletea juisi.” Akauliza Meja.
“Sawa. Sawa tu Meja.” Akasema.
Meja akaenda jikoni, huko ndipo lilipokuwa friji. Punde akarejea akiwa na glasi kubwa yenye juisi, akamkabidhi Mkuki naye akaketi.
“Najua hujala. Lakini inabidi tumsubiri mke wangu aje kukupikia.” Akasema Meja.
Mkuki akatabasamu kidogo. “Ndo Nilitaka nikuuliize. Ulinambia una mke na mtoto lakini siwaoni.” Akasema.
“Ndo hivyo. Watarudi. Tuna duka la kuuza maua mbele mbele huko. Kwahiyo mke wangu ndo anauza.”
“Duka lenu wenyewe!?”
“Ndiyo.”
Mkuki akaguna huku akitingisha kichwa kama anayejilaumu. “Kaka shikamoo. Nimekukubali. Saluti kwako.”
“Asante.”
“Wanarudi saa ngapi?”
“Jioni. Nadhani baada ya masaaa mawili watakuwa hapa.” Akaeleza Meja.
Baada ya pale stori zikashika hatamu huku Meja akimuhahidi Mkuki kwamba atamtafutia kazi ili naye ajikimu kimaisha na ikiwezekana kuanzisha maisha yake kama yeye.
Saa moja na nusu baadae mke wa Meja alirudi nyumbani. Alifungua mlango bila kubisha hodi, mtoto wao akatangulia kuingia, na alipomuona baba yake tu alimkimbilka na kukumbatia. Akamsalimu kwa Kichina; hiyo ndiyo lugha waliyokuwa wakiitumia katika mazungumzo ya kila siku.
Mke akaingia pia, akasimama mlangoni kwanza akimtazama Mkuki, hakutarajia kukuta mgeni nyumbani.
Alikuwa ni mwanamke wa Kiafrika, mnene mwenye umbo la kibantu, mweusi haswa na mrefu, hakuwa na sura ya kuvutia sana lakini alitazamika na kutambulika kuwa ni mwanamke; yeye alikuwa ni mtu kutoka Ghana, na kwa majina alikuwa akiitwa Onyuletwa Ojuku.
“Karibu.” Akasema Onyuletwa kumwambia Mkuki kwa Kichina.
“Asante.” Akajibu Mkuki.
Yule mwanamke akapita moja kwa moja hadi jikoni, akaweka mzigo aliyokuwa ameibeba kisha akarudi sebuleni, akaketi karibu na mume wake.
“Salama!?” Mume akamuuliza.
“Safi tu.” Mke akajibu.
“Sawa. Sasa tuna mgeni hapa. Huyu bwana anaitwa Mkuki, ni rafiki yangu sana, na ni miongoni mwa wale wenzangu niliokwambia tulikuwa pamoja kwenye meli, kwahiyo tulikuwa tunaishi pamoja Tanzania.”
“Sawa. Karibu shemeji.”
“Asante sana.”
“Mkuki. Huyu ndo mke wangu, ndo sababu ya mimi kuja china, ningebaki Tanzania ningekutana naye wapi?” Akatambukisha kwa mtindo wa masihara Meja na wote wakacheka. Kisha mtoto naye akaambiwa amuite Mkuki Baba mdogo na baada ya hapo Meja akamuomba mke wake apike chakula kitamu kwa ajili ya mgeni.
**********************************
Kitu kimoja kuhusu Mkuki hakikuwekwa wazi kwa mke wa Meja, hawakumueleza kwamba Mkuki hataondoka, ataendelea kukaa nao kwa muda fulani.
Meja alificha suala hilo kwa sababu alijua madhara yake. Yeye na mke walikuwa na makubaliano hawatakuwa na familia ya kuzidi watu watatu, yaani wao pamoja na mtoto wao mmoja.
Ilipofika jioni Onyuletwa alimuita mumewe chumbani na kuhoji kulikoni, mbona mgeni hana dalili za kuondoka.
**********************************
Kitu kimoja kuhusu Mkuki hakikuwekwa wazi kwa mke wa Meja, hawakumueleza kwamba Mkuki hataondoka, ataendelea kukaa nao kwa muda fulani.
Meja alificha suala hilo kwa sababu alijua madhara yake. Yeye na mke walikuwa na makubaliano hawatakuwa na familia ya kuzidi watu watatu, yaani wao pamoja na mtoto wao mmoja.
Ilipofika jioni Onyuletwa alimuita mumewe chumbani na kuhoji kulikoni, mbona mgeni hana dalili za kuondoka.
“Nilisahau tu kukwambia. Mkuki hana sehemu ya kuishi? Kwahiyo tutakaa naye kwa siku kadhaa wakati mimi nikiwa namtafutia kazi, akiwa vizuri ataondoka.” Alimueleza.
“Hapana. Hiyo nimekataa Meja. Hatuna uwezo wa kumudu familia kubwa namna hiyo, na tulishakubaliana.”
“Najua lakini hatuna namna. Kwahiyo inabidi tumsaidie tu.”
“Hatuwezi Meja. Fanya uwezavyo aondoke kesho.”
“Mke wangu hatuwezi kufanya hivyo. Mkuki amenisaidia sana. Pengine bila yeye nisingekuwa saa, aliniokoa kwenye kifo.” Akasema Meja; hapa akimdanganya mke wake ili kumshawishi kumsadia Mkuki.
“Hiyo siyo sababu Meja. Rafiki siyo Mungu hata akuokoe na kifo. Mimi na wewe tukikubaliana kuhusu kubana matumizi ya pesa, sasa leo anakuja mtu tena bila taarifa eti tuishi nae, ina maana tuongeze matumizi? Hapana Meja. Mwambie tu aende. Hatuwezi kuwa na maendeleo tunayoyatafuta kwa mtindo huo.”
“Nimekwambia ni kwa muda mfupi. Tatizo nini? Kwahiyo unataka nimfukuze rafiki yangu? Ndugu yangu?.”
“Najua unatumia uanaume wako kwenda kinyume na makubaliano lakini ufahamu kwamba hilo halitusaidii Meja, linatudidimiza.”
“Kwahiyo?”
“Anakaa kwa muda gani?”
“Wiki mbili mpaka tatu. Hatozidisha hapo.”
“Sawa. Lakini naomba zisipite, utanichukia Meja.”
“Usijali mke wangu.” Akasema Meja na wakayamaliza namna hiyo yeye na mke na tangu hapo Mkuki akaishi pale rasmi.
*****************************
Wiki moja baadae Mkuki akapata kibarua pale pale alipokuwa akifanya Meja; alikuwa ni mbeba maboksi ya vyakula kama vile samaki kutoka na mazagazaga mengineyo kutoka sokoni.
Mambo yalikwenda vizuri, maendeleo yalionekana, kwani kabla hata hajatia mkokoni mshahara wake wa wiki ya kwanza alikuwa ameshaanza kuonja marupurupu ya kazi hiyo aliyoyapata kwa njia za ujanja ujanja kama vile kuuza baadhi ya vyakula anavyobeba na kadhalika.
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000
SEHEMU YA 11


ILIPOISHIA...

Tuliona Mkuki amepata msaada wa kuishi nchini China kutoka kwa rafiki yake Meja; na sasa hata ametafutiwa kazi na ameshaanza kufanya.

JIPE RAHA....

Mpango nambari moja ulikuwa ni kupata pesa ya kumuwezesha kuhama pale kwa Meja, akaishi peke yake ili awe huru zaidi kujipangia mambo.
Wiki mbili zilifika akiwa bado kwa Meja, na siku hiyo ya kumi na nne ilikuwa ni siku ambayo iliyafanya maisha yake kuwa na taswira nyingine mpya kabisa tofauti na mipango yake.
Siku hiyo muda wa kumaliza kazi ulifika, alijimwagia maji na kujiandaa kurejea nyumbani. Meja alipumzika siku hiyo, kwahiyo safari ya nyumbani ilimuhusu peke yake tofauti na siku nyingine ambazo huongozana wakati wa kuja na kuondoka.
Lakini kabla hata hajaondoka mfanyakazi mwenzake alimfata na kumpa ujumbe wa kwamba kuna mtu anamuita—mgeni wake.
“Ni nani?”
“Sijui. Yupo nje hapo.”
“Yukoje? Ni mwanamke au mwanaume?”
“Unaonaje ungeenda kumuona ili hayo maswali unayoniuliza yasiwe na umuhimu tena?” Akasema mleta taarifa.
Basi Mkuki akiwa tayari kwa ajili ya kuondoka akaendea mbele kwenye mlango wa wateja kuingia mgahawani. Hakuona mtu hata alipotoka, alitazama huku na huko, na kote kulikiwa kweupe. Akasogea kwa mbele kidogo, eneo lililokuwa na maegesho ya magari kwa ajili ya wateja wa mgahawa lakini pia hakuona mtu.
“Mkuki.” Mara alisikia sauti ya kike ikiita kutoka nyuma yake, sauti anayoifahamu tena si kidogo, sauti anayopenda kusikia, sauti yenye kuyapendeza masikio yake, sauti yenye nguvu ya kuponya, yenye uwezo wa kuligeuza donda kuwa kovu, na kuvo kufutika kabisa, yenye kujaza kilogramu za furaha ndani ya nafsi, sauti yenye kuubembeleza moyo na kuituliza roho, ikatuliwa mwanana.
Akageuka Mkuki, na hapo macho yake yakatua kwa mwanamke anayenfahamu pia, tena anayemfahu mno, kupita maelezo. Alikuwa amesimama umbali mfupi kutoka pale alipo alipo.
“Mei Lee!?” Mkuki akaita kana mwamba haamini alichokuwa anakiona.
Mei Lee hakudiriki kumjibu, badala yake alijichoropoa mbio kutoka pale alipo kulekea kwa mkuki, alipomfikia akajirusha na kumkumbatia kwa kujing’ang’aniza mno huku akitoa kilio cha kugugumia, kilio cha kike.
Mkuki naye hakutaka kumuachia, alimkumbatia vile vile huku akimbembeleza hadi sasa wakawa ni kama maigizo kwa baadhi ya wateja waliokuwa wakiingia na kutoka mgahawani.
Dada alilia si kisogo, tena kilio kikavu, kilio kitupu, wala hakutoa sauti kuzungumza neno hata moja.
Basi baada ya kumbato refu Mkuki akamtaka Mei Lee watoke eneo lile, akamchukua hadi kwenye mgahawa mdogo uliopo karibu na mgahawa anaofanyia kazi Mkuki, alimpeleka huko kwa ajili kuzungumza. Waliagiza kahawa, kinywaji muhimu na cha gharama nchini China, na baada ya kuhudumiwa uwanja ukawa wao sasa.
Mkuki alikuwa ametingwa na kizungumkuti, hakujua aanze kuuliza swali lipi kati ya, Kwanini uko hapa? Umefikaje hapa? Au umejuaje niko hapa?; yote yalikuwa ni maswali ambayo yangemsaidia kukata kiu yake ya kufahamu kinachodendelea.
Pia, kabla ya kuendelea Mkuki alimuomba Mei Lee aachie wazi uso wake kwa sababu kwa upande wake hakukuwa na umuhimu wa kuufunika kwa nywele namna ile.


“Kwanini uko hapa?” Aliamua kuanza na swali hilo, lakini hakuuliza kwa sauti ya kibabe kana kwamba alikuwa akimlaumu kuwa pale, bali alizungumza naye taratibu na kwa upendo kama afanyavyo siku zote.
Badala ya kujibu Mei Lee alianza kulia kilio kizito cha kugugumia kiasi kwamba Mkuki akapata kibarua cha kumbembeleza; binti aliacha kulia alipoamua mwenyewe dakika chache baadae.
“Niambie Mei Lee. Kwanini uko hapa?” Akauliza tena Mkuki.
“Ulitukimbia?” Akauliza kwa upole Mei Lee badala ya kujibu swali.
“Hapana…” akajibu Mkuki, kisha akafikiria kidogo jinsi ambavyo angeyapanga maneno na kumuelezea Mei kilicchotokea japo kwa ufupi. “Sikuwakimbia, na wala si mpango wangu kuwa hapa China. Yote ni kwa sababu ya matatizo makubwa yaliyonikuta kule kisiwani.” Akaeleza.
“Na Maufeng?” akauliza tena Mei Lee. Mkuki akatulia kidogo, akamtazama usoni Mei Lee, na macho yao yalipogongana mtoto wa kiume akatazama chini kwa unyonge kana kwamba alikuwa na hatia juu ya kile alichoulizwa.
“Sielewe ni nini kimempata, nilishangaa tu niko nyumbani, askari wanakuja, wananikamata, wanasema nimemuua.” Akaelezea Mkuki.
“Hukumuua?”
“Hapana. Siwezi kufaunya hivyo Mei Lee. Maufeng alikuwa ni rafiki yangu muhimu na hata wewe unajua.”
“Sawa. Na ulipanga kurudi lini nyumbani?”
“Mipango ikikaa sawa. Lakini kwa sababu nimekuona tunaweza tukarudi hata sasa hivi” alizungumza Mkuki, ingawa hilo la kurejea halikuwa likitoka moyoni, alilisema kwa sababu ilipenda kuona Mei Lee akifurahi, na alijua hilo litamfurahisha.
“Turudi? Tutaishi wapi?” akauliza Mei Lee, hapa sauti yake ikisika kama yenye mirindimo ya kilio kwa ndani.
“Nyumbani, kwa mzee Wong, au wewe unatakaje?” akauliza Mkuki huku sasa akimatazama Mei Lee usoni kwa macho makavu. Mei Lee naye alimtazama bila aibu, ikawa ni macho dhidi ya macho, na ndani ya sekunde chache tu macho ya Mei Lee yakaanza kutiririsha mifereji ya machozi.
“Mei Lee, nyamaza. Mimi si nipo hapa mbele yako, unalia nini sasa?”
“Baba amekufa Mkuki, wamemuua.” Yakamtoka Mei Lee.
Papo hapo Mkuki alibadilika ghafla, aliganda mithili ya mtu aliyetumbukizwa ndani ya jokofu lenye baridi kali sana, hakutaka kukataa kile alichokisikia lakini haikuwa rahisi kukikubali. Ilikuwa ni kama taarifa yenye uchuro, haikumpendeza kabisa.
Mei Lee alilia, ni kama yeye ndiye ambaye alipewa taarifa ile mbaya. Ilibidi Mkuki acheze nafasi yake ya kiume, alinyanyuka kutoka kwenye kiti chake na kwenda kumbembeleza msichana, yaani ni kama walikuwa kwenye maombolezo.
Mei Lee akatulia kidogo, lakini bado kwikwi za kilio zilisikika. Hali ilipokuwa shwari kwa kiasi fulani Mkuki alimtaka binti amuelezee ilivyokuwa.
“Walikuwa wanakutafuta wewe. Wakamkamata ili awaonyeshe ulipo.”
“Mimi!? Nani aliyekuwa akinitafuta? Kwanini?”
“Familia ya kina Maufeng. Wanasema uliimua ndugu yao, walitaka kukua pia” akaeleza Mei Lee.
Mkuki akahisi ganzi mwili mzima kwa taarifa ile, hakutarajia kutokea jambo la aina hiyo hata kidogo. Alijiona ni mkosefu aliyepitiliza, kumsababishia kifo mtu asiye na hatia ambaye awali alimuonya juu ya safari yake ya kwenda kisiwani Jiaju kutafuta pesa nyingi. Alihisi ametenda dhambi kubwa mno, dhambi isiyostahili toba, dhambi yenye kukumbukwa. Alitamani dunia ifikie mwisho kwa sababu alijihisi ni mwenye gundu lisilotakata hata kwa kuoga makombe, kila alichokigusa kilinuka harufu ya uozo, harufu mbaya mno. Au kama si dunia kufika tamati basi alitamani muda urejee nyuma, ajikute nyumbani kwao Tandale na atafute kibarua kingine cha kufanya na si kujichanganya na kujidanganya kwenda kusaka maisha bora ughaibuni kiasi cha kuwasababishia wengine matatizo makubwa namna hii.
Mzee Wong aliuliwa na ndugu wa Maufeng ambao baada ya mtoto wao kuuwawa kule kisiwani taarifa ziliwafikia kwamba ameuawa na Mkuki, lakini Mkuki huyohuyo alitoroka gerezani na kutokomea kusikojulikana. Hivyo familia ikivamia nyumbani kwa mzee Wong wakimtaka awaonyeshe wapi alipokimbilia Mkuki. Kwa kuwa mzee Wong hakuwa akifahamu lolote kuhusu Mkuki, wale watu walimchukulia kama anaficha hivyo wakamuua yeye na walitaka kumuua na Mei Lee ila yeye alifamikiwa kuwatoroka na kukimbia.
Mei Lee akafanya alichokijua, akapanda boti iendeayo China kutoka Thaiwan na kufika hapo Hong Kong ambapo alikutana Mkuki; haya yote aliyasimulia Mei Lee.
“Umejuaje kama niko hapa?”
“Nilikuwa nakuona hapa kila siku kwa siku tatu sasa.”
“Kwanini huku nishitua.”
“Nilikuwa naogopa.” Akaeleaza Mei Lee.
“Kwahiyo ulikuwa unalala wapi siku zote hizo?”
“Nje.” Akasema Mei
Basi wakaongea mengi hata wakajisahau, giza likaingia na kuwakuta bado wako palepale na hapo sasa mkuki ndipo akakumbuka kama kuna suala la akurudi nyumbani. Akamtaka Mei Lee waondoke, huku akimuomba aendelee kuacha wazi uso wake kama ambavyo alimtaka afanye mara baada ya kukutana.
Waliondoka pamoja hadi nyumbani kwa Meja; alipokuwa akiishi Mkuki. Eneo lilikuwa kimya mno kwa sababu ulikuwa ni muda wa usiku ambao watu wengi walikuwa ndani mwao.
Walipandisha moja kwa moja hadi ghorofani, huku Mkuki alijipanga kweli kweli jinsi ya atakavyomtambulisha Mei Lee na kueleza kwamba itabidi alale naye pale.
Walifika mlangoni, Mkuki akabisha hodi, wakiwa hapo waliona taa zimewashwa ndani, kisha punde kidogo mlango ukafunguliwa, alikuwa ni Meja aliyefungua—akaonana na Mkuki.
“Vipi? Mbona mpaka saa hizi?” Akauliza kwa kiswahili Meja huku sura yake ikionekana yenye chukizo; hakuwa amefurahishwa na jambo lile.
“Kuna ishu ya dharura ilijitokeza.” Akajibu Mkuki; hapo mgeni wake akiwa bado hajaonwa na Meja.
“Poa. Ingia” akasema Meja akitangulia ndani.
Mkuki akamtolea ishara Mei Lee ya kwamba amfuate kisha akaingia ndani; Mei Lee pia akaingia, hapo sasa ndipo Meja alipomuona.
Sura ya Mei Lee iliulipua moyo wa Meja, alishituka sana na laiti kama angemuona bintu huyo bila kuwepo kwa rafiki yake Mkuki basi huenda angetoka mbio huku akipiga mayowe ya uomba msaada wa kwamba amekutana na zimwi lenye kuitisha.

“Nani huyu?” Akauliza Meja kwa Kiswahili.
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000
HAYA MAMBO YANAZIDI KUNOGA 🔥 🔥 🔥
TUMEFIKIA KATIKATI MWA SIMULIZI HII YA KIJASUSI.....

SIMULIZI INA SEHEMU 22 TU.........

TUKUTANE TENA KESHO
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000

Simulizi Zinazorushwa na Pseudepigraphas

1. Simulizi: Kurudi Kwa Moza
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Kurudi Kwa Moza

2. Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad
Bonyeza hapa chini kusoma
Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

3.Simulizi: Nini maana ya mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Nini maana ya mapenzi


4. Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi

5. Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma

Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

💥💥💥NEW 💥 💥 💥

6. RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu
Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu

7. NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma

NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000
SEHEMU YA 12


ILIPOISHIA...

Tuliona Mkuki amekutana na Mei Lee na sasa amemchukua kwenda kuishi naye nyumbani kwa Meja.Je Meja na Mke wake watakubali?

SHUKA NAYO

“Nani huyu?” Akauliza Meja kwa Kiswahili.
Mkuki hakujibu mara moja, alitengeneza kimya cha sekunde tano, “Ni stori ndefu Meja. Nadhani kesho tutaongea vizuri.” Akasema.
Meja akamtazama, taswira ya hasira iliuchafua uso wake lakini hakutaka kuzibadilsiha hasira hizo kuwa maneno; alijua pengine angezungumza maneno mabaya yasiyofaa kumwambia rafiki yake huyo kipenzi.
“Ina maana atalala hapa?” Akauliza Meja.
“Ndiyo. Lakini ni....”
“Basi. Usiendelee. Usiku mwema. Usisahau kuzima taa.” Akasema Meja kisha akaelekea chumbani kwake akimuacha Mkuki na Mei Lee pale sebuleni. Aliondoka kwa hasira mno.
“Twende.” Mkuki akamwambia Mei Lee huku akitangulia kwenye kordo ya vyumba vya kulala, alipofika kwenye swichi akazima taa, halafu akafungua mlango wa chumba chake wakaingia ndani. Akawasha taa ya chumbani.
“Karibu.” Akamwambia mgeni wake huku akimuoneshea ishara ya kwamba aketi kitandani; Mei Lee akafanya hivyo na Mkuki mwenyewe akaketi kitandani pia pembeni kidogo ya pale alipokuwa Mei Lee.
Chumba kikawa kimya kwa zaidi ya sekunde theleathini, hakuna aliyethubutu kumsemesha mwenzake wala kujikohoza, wote walikuwa kama mabubu; kama watu ambao ndiyo mara ya kwanza wanakutana.
“Una usingizi sio?” Mkuki akavunja ukimya kwa swali. Mei Lee akaitikia ndiyo kwa kutingisha kichwa tu.
“Basi utalala hapa.” Akasema Mkuki akimaanisha atala kitandani.
“Na wewe?” Mei Lee akauliza.
Mkuki akamtazama kidogo kabala ya kumjibu. “Popote.”Akasema huku akitabasamu.
“Hapa pia?” Akauliza Mei Lee akimaanisha kwamba na Mkuki pia atalala kitandani.
“Ndiyo.” Akajibu kwa kujiamini Mkuki na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Walilala kitanda kimoja lakini kwa mtindo wa mzungu wa nne. Tena walilala kwa utilivu bila yeyote kati yao kufanya ghadhabu ya aina yoyote kwa mwenzie, walilala kama kaka na dada wa kuzaliwa tumbo moja tu.
*********************************
Asubuhi waliamshwa na hodi za fujo zilizokuwa zikigongwa mlangoni mwa chumba chao, Mkuki akaamka, akatazama nje kupitia dirishani akagundua kumekucha, kisha akateremka kitandani, akaenda mbiombio mlangoni kufungua mlango.
Hapo akamuona mke wa Meja akiwa amefura kweli kweli....
“Yuko wapi huyo malaya wako? Naomba mtoke nyumbani kwangu sasa hivi.” Akabatwa mke wa Meja tena kwa kichina kiasi kwamba hata Mei Lee alisikia na kuelewa.
Mkuki akabaki ameduwaa pale mlangoni asijue cha kufanya, kwamba amjibu au afuate ile amri aliyopewa ya kuondoka.
“Naongea na wewe hunielewi? Nyumbani kwangu sio gesti, hii ni nyumba ya kuishi, ufuska mkafanyie huko mbele.” Akawaka. Alikuwa ni mwanamke kutoka Ghana, na kwa taarifa tu ni kwamba wanawake wengi kutoka Afrika Magharibi ni wazuri kwenye kuchonga mdomo.
Mkuki akaamua kumtolea uvivu.
“Usinipelekeshe. Na nina uwezo wa kutoondoka nikitaka.” Akasema.
“Unasemaje? Hunijui eeh? Ngoja sasa.” akasema yule mwanamke kisha akamsukumia pembeni Mkuki ili aingie ndani kwenda kumtoa kimabavu Mei Lee.
Basi papo hapo Mkuki akashituka, kumbe haikuwa kweli, ilikuwa ni ndoto ambayo pengine ilizaliwa na mawazo yake mwenyewe.
Mei Lee alikuwa bado amelala, yeye Mkuki akaamka, akasogea dirishani, akakunja pazia na kugundua kuwa tayari kumekucha. Akiwa bado pale dirishani alisikia hodi, akashituka kidogo kwa sababu kila kitu kilikwenda kama ndotoni.
Hodi ikaendelea.
Mkuki akaenda mlangoni kufungua. Akamuona Meja, ndiye aliyekuwa akibisha hodi.
“Uko poa?” Meja akamuuliza kwa kiswahili.
“Ndiyo. Za kuamka.”
“Safi tu. Shemeji vipi?”
Mkuki akajichekesha kidogo. “Sio shemeji yako bhana.”
“Kumbe?”
“Ni dada yangu tu.”
Meja akacheka. “Una dada mchina? Poa. Njoo tuzungumze.” Akamwambia.
Mkuki akatoka, akafunga mlango akamfuta Meja aliyekuwa anaelekea sebuleni, walipofika wakaketi kwenye viti.
“Nataka tuongee moja kwa moja bila konakona Mkuki. Ni hivi, ulichokifanya jana sijakilewa kabisa.”
“Kipi?”
“Kuhusu mgeni wako. Umerudi usiku halafu na mtu, we unaionaje hiyo braza.”
“Haijatulia.”
“Umeona eeh! Sasa mke wangu bado hajajua kama kuna mgeni, na ameshaenda dukani, kwahiyo jitahidi kutofanya hivi tena.” Alisema Meja. Yeye alifikiria kwamba Mei Lee ni mpenzi wa Mkuki, hivyo atakuwa amekuja tu na asubuhi hiyo ataondoka.
Mkuki aligundua ule mkanganyiko aliousababisha, sasa akawa anapanga jinsi atakavyofikisha taarifa kwa Meja kwamba Mei Lee hana pakulala, hivyo lengo la kuja nae pale ni waishi pamoja.
“Sasa mimi natangulia. Utanikuta kazini.” Akasema Meja, kisha akasimama tayari kwa safari lakini kabla hajapiga hata hatua moja akauliza. “Na ile usoni mwake ni nini? Aliunguaga na moto?”
“Hapana. Ndo aivyozaliwa.” Akajibu Mkuki na kuongeza. “Lakini Meja kuna jambo naomba tuzungumze.”
“Kwahiyo nikae?”
“Ndiyo.”Akasema Mkuki, Meja akakaa palepale alipoinuka.
“Utanisamehe kama nitakukwaza kaka, lakini ukweli ni kwamba nahitaji msaada wako katika hili kama ambavyo umesaidia mahala pa kulala, mahala pakuishi.” Akasema Mkuki na kuendelea. “Unakumbuka nilvyokusimulia kuhusu nilivyosaidiwa na mzee mmoja na binti yake kule Thaiwan?”
“Ndio.” Meja akajibu.
“Basi yule binti ni huyu.”
“Kuna kitu sijaelewa.” Akasema Meja na kuendelea. “Unakumbuka ulichonisimulia kuhusu safari yako kutoka Thaiwan hadi hapa?”
“Ndiyo nakumbuka.”
“Ulinambia umetoroka, na hawajui uko wapi. Sasa amejuaje uko hapa? yaani mmekutana vipi yaani?”
“Iko hivi Meja; baada ya mimi kutoroka huyu msichana na baba yake wakavamiwa na ile familia ya yule jamaa niliyekwenda naye kisiwani.....” akasema Mkuki na hapo akasimulia kila kilichotokea kama ambavyo alisimuliwa na Mei Lee.
“... kwahiyo alitorokea huku. Yaani ni kama Mungu ameamua kutukutanisha tena.” Akamalizia kuelezea Mkuki.
“Naomba niseme kitu nilichokielewa kabla hujamaliza.” Akasema Meja.
“Sawa.”
“Unamaanisha huyu binti pia hana sehemu ya kukaa. Unataka tuishi naye hapa, sio?”
Mkuki akatulia kidogo, jibu la swali lile lilikuwa gumu zaidi ya chuma. “Ndiyo. Lakini ni kwa muda tu. Nikihama nitaondoka naye.”
“Kudadeki! Hiyo haiwezekani broo. Tena naomba usinielewe vibaya, usije ukafikiria kwamba mimi sitaki kukusaidia lakini ukweli ni kwamba msaada unaouhitaji kwa wakati huu ni mgumu sana. Mimi siwezi.”
“Naelewa Meja lakini unajua wewe ndiye ndugu yangu hapa China, sina mwingine wa kunisaidia.”
“Naelewa kila kitu Mkuki, nimeamua tu kukwambia ukweli. Unajua hata wewe kuwa hapa ni kutokana na ubishi wangu tu, mke wangu alikuwa hataki kabisa kwa sababu tulishakubaliana kwamba familia yetu ni mwisho watu watatu tu, mgeni akija siku tatu anaondoka. Maisha ya China ni magumu sana Mkuki, kila kitu kinahitaji pesa. Na si mimi si mke wangu sote tuko ugenini, sote tumekuja kutafuta maisha kisha tutarejea nyumbani, sasa kama tutaishi tukiwasaidia wengine ni lini tutatimiza lengo lililotuleta China. Nielewe. Wewe ni mshikaji wangu, ni mdogo wangu, sitaki kukupangia kuhusu maisha yako, namaanisha sitaki kukushawishi eti labda umtelekeze huyo demu, ila kama unataka kumsaidia tafuta njia nyingine lakini kwa hapa nyumbani hapana.” Akasema Meja.
“Sawa. Nimekuelewa.” Akaitikia kwa unyonge Mkuki.
Basi Meja akasimama, akaongoza hadi mlangoni, akafungua mlango lakini kabla hajatoka akamgekia Mkuki. “Nisamehe dogo kama nitakuwa nimekukosea.” akasema kisha akatoka na kufunga mlango.
Mkuki alibaki ameduwaa asijue la kufanya, hakuwa na pesa ya kusema labda akampangie Mei Lee chumba hotelini na wala hakuwa na ujasiri wa kuweza kumtelekeza msichana huyo. Alihisi yeye ndiyo chanzo cha matatizo yote, hivyo alikuwa na jukumu la kumuangalia Mei Lee kwa jicho la karibu.
Hapo ndipo Mkuki alipotamani ardhi ipasuke, litokezee shimo kubwa mno, atumbukie humo kisha ardhi ijifunge ili watakaobaki watamfute miaka nenda rudi na wasimpate. Alijihisi amebeba mzigo mkubwa sana, yaani kama konokono mwenye gramu 9 aliyetishwa jumba la kobe lenye kilo 12, ni msigo mzito hakika.
Alihisi na kizunguzungu, alihisi kutoelewa na zaidi alijuta kwanini alidiriki kuikimbia ardhi ya nyumbani alipozaliwa mama yake yake kwa sababu za kipuuzi. Hakika alichanganyikiwa na kuna muda alitamani hata kunywa sumu, afe, akapumzike.
“Uko sawa.” Mara akasikia sauti ya Mei Lee ikimuuliza hivyo kutokea nyuma ya pale alipoketi.
Akageuka, akamuona amesimama.
“Aah! Umeamka?” Akauliza Mkuki badala ya kujibu swali aliloulizwa.
“Ndiyo.”
“Basi jiandae tuondoke.”
“Tunaenda wapi?" Akaukiza Mei Lee. Mkuki akaonekana kutulia kidogo akitafakari jibu la swali lile kwa sababu ukweli ni kwamba hakuwa akijua wapi atakwenda naye baada ya pale.
“Aaah. Jiandae tu twende.” Akajibu kwa kifupi tu Mkuki.
Mei Lee akamtazama kwa sekunde kadhaa na kuna kitu akagundua, akamsogelea na kuketi pembeni yake, akamshika mkono na kuuminyaminya kana kwamba hawakuwa kaka na dada; walikuwa ni wapenzi.
“Wamekataa mimi kuishi hapa?” Akauliza taratibu Mei Lee.
Mkuki akashituka kidogo, hakutarajia swali lile kwa sababu aliamini wakati anazungumza na Meja, Mei Lee alikuwa amelala, lakini pia hata kama alikuwa macho, asingeelewa chochote kwa sababu walizungumza kwa kiswahili.
“Hapana. Hapana. Hawajakataa.” Akasema.
“Najua wamekataa. Sikia. Mimi nitarudi kuishi nilipokuwa naishi awali, wewe endelea kuishi hapa. Sitaki kuwa tatizo katika maisha yako Mkuki.” Akasema Mei Lee. Yalikuwa ni maneno machache lakini makali kama miiba, yakapenya na kuingia ndani mwa Mkuki, yakasambaa kila kwenye mshipa wa damu na kwenye neva zote, yakausugua na moyo wake kama msasa na hapo akashindwa kujizuia kutokwa chozi mtoto wa kiume.
Mei Lee naye alikuwa ni nani hata asiambukizike huzuni ile, naye akaanza kulia pia. Vilio vya kimya kimya vikatawala ndani pale, ni mifereji ya machozi machoni ndiyo iliyozungumza tu—hakika walilia sana.
Sasa Mkuki akaamua kuchukua jukumu la kiume, akaanza kunyamaza, kisha akamsogeza Mei Lee na kumkumbatia, na kumlaza kifuani mwake huku akimpigapiga mgongoni taratibu.
Lakini ghafla mlango ulifunguliwa, akaingia Mke wa Meja na akawakuta Mkuki na Mei Lee katika hali ile ile. Ubongo wake ulipokea alichokiona ndani ya nusu sekunde tu, na papo hapo ukampa jibu kwamba Mkuki aliingiza mwanamke ndani baada ya kuachwa mwenyewe nyumbani.
“Mungu wangu!” Akang'aka, papo hapo Mkuki na Mei Lee wakaachiana na kumtazama.
*****************************
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
2,004
2,000
SEHEMU YA 13


ILIPOISHIA...
Tuliona Mkuki amekutana na Mei Lee, amempeleka nyumbani kwa Meja, wakalala huko, lakini asubuhi Meja akamtaka aondoke kwamba nyumbani kwake hakuna nafasi ya kukaa Mei Lee.
Akiwa kwenye sintofahamu, Mkuki na Mei Lee, Inyuletwa anawakuta wakiwa wamekumbatiana.
SOMA KILICHOENDELEA...

“Nini hiki unafanya? Nauliza ni uchafu gani huu unafanya ndani ya nyumba yangu? Hapana haiwezekani.” Akawaka. Akatoa simu yake, akabofyabofya kumpigia mume wake.

“Shemeji naomba nikueleweshe....” akataka kujitetea Mkuki lakini wapi,
“Sitaki kusikia chochote kutokwa kwako. Sitaki kuongea na wewe. Hunijui sikujui.” Akasema Onyuletwa, alikuwa ameshikwa na jazba kweli kweli.
Simu ikapokelewa.
“Meja naomba njoo nyumbani sasa hivi.” Akasema kisha akaa kimya kusikiliza upande wa pili.
Akaendelea.
“Nimekwambia njoo nyumbani sasa hivi, kama huwezi hutonikuta. Nafunga mizigo yangu naondoka na mwanangu nakuachia nyumba.”
Akasikiliza upande wa pili.
“Nimekwambia njoo. Siwezi kuvumilia huu uchafu siwezi. Kumbe nyinyi Watanzania ni wafuska namna hii, hapana. Najuta kukujua, najuta kuishi na wewe. Naondoka Meja.” Akabatwa Onyuletwa kisha akata simu.
Hakutaka kuzungunza na Mkuki hata kidogo, akaenda chumbani kwake akimuacha Mkuki na Mei Lee pale sebuleni wamepigwa bumbuwazi kama wachawi waliokutwa wakicheza cheketucheketu.
Punde Onyuletwa akatoka na begi moja la nguo akaliweka sebuleni, akarudi chumbani tena na dakika tano baadae akatoka na begi lingine, hakumsemesha mtu, alikuwa amenuna na kukunja sura kweli kweli.
Mara ya tatu akatoka na begi lingine na akarudi tena ndani na papo hapo mlango ukafunguliwa, Meja akaingia, alipomuona Mkuki na Mei Lee tu akagundua kwamba mke wake aliwakuta na akahisi kwamba huenda Mkuki aliingiza mwanamke huyo baada ya wao kutoka.
Akanyamaza Meja, akasimama palepale mlangoni akimtazama Mkuki na Mei Lee kana kwamba hata yeye ilikuwa ni mara ya kwanza kuwatia machoni. Hakutaka mke wake afahamu kwamba anayo taarifa kuhusu huyo mgeni wa Mkuki, alielewa kwamba hilo lingefanya mke wake amuone 'kilaza' wa mbingu ya saba.
Punde mke wake akaja sebuleni akiwa begi dogo. Akamuona mume wake.
“Meja? Umemleta huyu ili afanye huu ufuska kwenye nyumba yangu? Sasa mimi naondoka, nawaachia nyumba, siwezi kukaa na mshenzi wa hivi. Hebu mtazame mwanamke mwenyewe kwanza, sura ya ajabu kama....” hakumalizia, Meja akamkatishaa.
“Basi mke wangu.” Alisema Meja kisha akamgeukia Mkuki. “Kaka ndo nini hiki unafanya? Unaingizaje mwanamke ndani ya nyumba yangu bila kunitaarifu?” Akauliza Meja. Mkuki akamuelewa kwamba alikuwa anajitoa kwenye ‘msala’.
“Meja naomba watoe watu wako sasa hivi. Sitaki kuwaona na kama itakuwa haiwezekani mimi nionodoke na mwanangu.” Akasema.
Sasa agizo hilo ndilo lilimtoa kijasho chembachemba Meja; mtihani aliopewa na mke wake ulikuwa ni mzito zaidi ya ule wa utaamua yupi kati ya simba na chui ukiwa na bastola yenye risasi moja tu.
Shida ilikuwa ni kwamba Mkuki alikuwa ni rafiki yake tena kipenzi wakati mke wake pia alikuwa ni muhimu kwake kama ambavyo Mei Lee alikuwa muhimu kwa Mkuki. Onyuletwa ndiye aliyemasaidia Meja kupata kazi pale anapofanya, kabla ya kuwa na uhusiano naye Meja alikuwa si lolote si chochote, hana kazi, ni kama goigoi anyetangatanga mtaani tu.
“Mke wangu, naomba tulizungumze hili.”
“Sitaki kuongea chochote Meja. SITAKI. SITAKI. Unawondoa ama niondoke?”
Meja akatulia kidogo, hapa akiupa nafasi ubungo wake uchakate jibu la kutoa juu ya lile swali aliloulizwa, bila shaka alihitaji ujasiri katika kutoa jibu hilo.
“Mkuki.” Akaita Meja. Mkuki akamtazama usoni kama ishara ya kwamba anamsikiliza. “Nenda kaka.” Akazungumza kwa kiswahili Meja. Aliumia sana moyoni, hakutaka kuzungumza vile, yale hayakuwa maamuzi yake, bali alisukumwa na matakwa ya mke wake. Ilikuwa ni lazima amsikilize ili kuiokoa ndoa yake, kuokoa familia yake na kumnusuru mtoto wake na madhara ya kulelewa na mzazi mmoja.
Basi Mkuki akasimama bila kusema neno
Akaenda moja kwa moja hadi chumbani na punde akatoka akiwa na begi dogo lenye nguo, ni nguo zake alizonunuliwa akiwa pale kwa Meja.
“Twende.” Akamwambia Mei Lee. Binti akasimama na kumfuata.
Mkuki akafungua mlango walipoufikia, akampisha Mei Lee atangulie kutoka kisha naye akafuata, lakini kabla hajarudisha, akamgeukia Meja na kumtazama kwa jicho ambalo ni kama alikuwa akimlaani kwa kile alichomfanyia, alimtazma hivyo kwa sekunde kumi kisha akafunga mlango, akaondoka.


********************************
Walifika nje, kwa pamoja, Mkuki na Mei Lee walitembea bila kusemeshana. Kila mmoja aliogopa kwa sababu wote wawili walikuwa wanajiona wakosefu na kwamba ndio chanzo cha yale yanayoendelea.
Mkuki alihisi bila yeye Mei Lee asingukuwa pale China akidhalilika kiasi kile wakati Mei Lee naye alijiona ndiyo sababu ya Mkuki kutimuliwa kama mbwa pale alipokuwa akiishi kwa kufadhiliwa.
Lakini Mei Lee alifurukutwa mno moyoni, alihisi kuna ulazima wa kuzungumza chochote juu ya kile kilichotokea, hata kuomba msamaha ikibidi.
“Mkuki?” Aliita Mei Lee katikati ya safari, Mkuki akamtazama kuashiria kwamba anamsikiliza.
“Samahani...” akasema.
“Usiseme. Hakuna ukichokosea. Mimi ndiye nastahili kukuomba msamaha.”
“Hakuna ulichokosea, ni mimi.”
Mkuki akajitabasamisha kidogo. “Basi si wewe si mimi, sote hatuna kosa, hatustahili kuombana msamaha,” akasema Mkuki kisha akapiga kimya kidogo akimtamza Mei Lee usoni huku wakiendelea kitembea.
Akaendelea kuzungunza Mkuki.
“Nadhani kilichotokea ni kama kukohoa. Kinaonekana si kitendo kizuri machoni mwa watu lakini huwezi kikuzia. Mimi na wewe hatuwezi kukizuia, ilikuwa ni lazima kitokee.”
Mei Lee akatabasamu, alifurahishwa na kauli za Mkuki, zilimfanya ajihisi mwepesi, asiye na mzigo wowote moyoni.
“Tunakwenda wapi?” Akauliza.
Mkuki akatabasamu kidogo kabla ya kumjibu. “Popote Mungu atakapotupeleka.”
Mei Lee akacheka.
“Lakini natakiwa niende kazini. Ninakwenda kukuacha sehemu kisha tutaonana jioni nikitoka.” akasema Mkuki.
Safari iliendelea huku sasa hali ya hewa ikionekana si rafiki kwa matembezi ya kawaida—yaani kulikuwa na dalili zote za kunyesha mvua kubwa. Wakapita mitaa miwili, wakatokea kwenye mtaa mwingine uitwao Cheynun Temple. Mtaa huu ulikuwa na barabara ndogo yenye kupita magari machache.
Basi wakiwa pembezoni mwa barabara walimuona bibi mmoja akivuka barabara mbele yao, alikuwa ni mzee kweli kweli na hata mwendo wake ulithibitisha hilo. Lakini mbele ya bibi huyo waliona gari ndogo ikija kwa kasi kana kwamba ilikuwa ikiendeshwa na mwendawazimu.
Mkuki alihisi jambo, alifikiria kwamba huenda gari lile litafika alipo bibi kabla ya kuvuka na kama ni hivyo basi ni wazi kwamba litamgonga.
Basi ghafla Mkuki akatimua mbio kuelekea alipo bibi hata alimshitua Mei Lee naye akataka kukimbia bila kujua kwanini mwenzake alifanya hivyo. Lengo la Mkuki ilikuwa ni kumfikia yule bibi na kumuoka na ajali iliyokuwa karibu kumkumba.
Kabla Mkuki hajamfikia bibi gari lilikuwa limeshamkaribia bibi na hapo Mkuki akagundua kuwa njia pekee iliyobaki ya kumnusuru kikongwe yule na umauti ni kujirusha na kumsukumia pembeni.
Hata bibi mwenyewe aliliona gari, lakini hakuwa na cha kufanya zaidi ya kufumba mambo asishuhudie jinsi atakavyozolewa juu juu na gari lile liendelo kasi sana.
Basi kabla gari halijamkumba bibi, Mkuki alijirusha, akamsukuma bibi na wote wawili wakaangukia pembeni mwa barabara, gari ikapita kwa kasi na ikawa imewakosa.
Bibi alichunika kidogo, lakini ni heri majeraha kuliko umauti.
Mkuki akasimama, akamuinua na bibi na wakati huo Mei Lee naye ndiyo alikuwa anafika pale.
“Mmeumia? Bibi umeumia?”
“Hapa tu.” Akajibu bibi huku akionesha kiwiko cha mkono wake wa kulia ambacho kilikuwa na mchubuko. Kisha akamgeukia Mkuki ambaye alikuwa karibu yake, akamtazama kana kwamba ni bubu asiye na maneno yoyote ya kumwambia, kisha ghafla bibi akajichoropoa, akamkumbatia Mkuki huku akilia kwa furaha.
“Asante mjukuu wangu. Asante sana.” Akasema.
Kabla hata Mkuki hajajibu radi likarindima, na mvua ya rasharasha ikaanza kunyesha; iliwanyeshea.
Mkuki akajitoa kwenye kumbato la bibi. “Unaenda wapi bibi?” Akamuuliza.
“Nyumbani.”
“Ni wapi?”
“Hapo mtaa wa nyuma.”
“Basi twende tukupeleke haraka kabla mvua haijawa kubwa.” Akasema Mkuki na hicho ndicho kilichoafanyika. Walimchukua bibi wakampeleka hadi kwake. Hapakuwa mbali na pale, ilikuwa ni mtaa wa nyuma tu.
Bibi huyu alikuwa akiishi kwenye jengo nambari 11 la mtaa huo. Jengo la ghorofa nane, wakati yeye alikuwa akiishi ghorofa ya sita. Walipanda lifti, bibi akatangulia kwa msaada wa kushikwa mkono na Mei Lee hadi mbele ya mlango wa chumba anachoishi bibi huyo.
Bibi akachukua funguo kutoka katika pochi yake ndogo, akampa Mkuki amsaidie kufungua, Mkuki akafanya hivyo kisha bibi akatangulia kuingia ndani, Mei Lee akafuata na Mkuki akawa wa mwisho.
Bibi alikuwa akiishi kwenye nyumba ya hadhi kubwa kweli kweli, sebule yake ilikuwa na fanicha tena za kisasa na ilipendeza mno.
“Karibuni.” Yakamtoka.
“Asante bibi. Tunaomba twende.” Akasema Mkuki.
“Haraka kiasi hicho? Kaeni niwapatie kahawa wanangu.”
“Hapana bibi. Siku nyingine tutakauja, tunawahi kazini.”
“Hata kama. Kazi ni bora lakini si bora zaidi ya kupokea shukurani.” Akasema bibi.
“Siku nyingine bibi.”
“Kweli!? Mnafanya wapi kazi?”
“Kwenye mgahawa wa Huan.”
“Nyote wawili?”
“Ndiyo.” Akaongopa Mkuki.
“Kweli?” akahoji bibi kana kwamba kuna kitu alikuwa akifahamu.
“Ndiyo, lakini leo mwenzangu anapumzika. Naenda mimi peke yangu.” Akasema Mkuki, aligundua ile hali ya utambuzi aliyokuwa nayo bibi, kwahiyo alijitahidi kuendana na kasi yake.
“Anhaa! Basi naona itakuwa vyema kama huyu binti atabaki hapa na mimi hadi utakaporudi kazini…..” akasema bibi lakini Mkuki alimkatisha.
“Hapana bibi…..” Bibi akamkatisha pia.
“Mjukuu wangu? Mwanangu? Niko mwenyewe hapa nyumbani, sina mtu wa kuzungumza naye. Naomba mnisaidie katika hili pia kama ambavyo mlinisaidia kule barabarani.” Akasema bibi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom