seheme ya sita
Nilikuwa nimetulia tuli juu ya tawi la mti huku nikijitahidi kuweka sawa akili yangu na mwiliuweze kukabiliana na myumbo wa tawi lile.
Nikiwa pale pale juu ya mti nikapata kuona askari kama kum hivi waliokuwa kwa miguu wakijongea kwa mbio kuja eneo lile nilipoziacha zile maiti za watu wale tofauti na nyuma yao kulikuwa nalile gari lao lenye kufanana na kichaka.
Ajabu walipofika kwa ile maiti yenye sare zao wakaibeba na kuingiza kwenye gari lao huku wakionekana wazi kusononeka juu ya jmbo Fulani na niliwaona wakijadiliana kuhusu jambo Fulani na kisha wakaanza tena kufuauta uelekeo niliokujia lakini hawakufika mbali tayri walikuwa wameshaiona ile maiti ya mtu yule mwenye asili ya kisomali.
Walionekana dhahiri kabisa wakishangaa maiti ile kuepo pale na walionekana kabisa wakianza kuingiwa na uoga juu ya jambo lile,nikashangaa kwanini watu wale waingiwe na woga baada ya kuinona maiti ile na yule mtu kama hana mahusiaono na askari wale mtu yule ni nani na kwanini tangu jana wanaonekana wakinifuata mimi kila niendapo wana nitakia nini wasomali hawa,ila hapakuwa na wakunijibu katikakati yam situ ule mnene.
Pale nilipokuwa sikutaka watu wale wenye dharau na wanowinda maisdha yangu waendeelee kujadiri jambo kwa mapana zaidi na hapo nikaikoki vizuri ile silaha ya kudungulia kisha nikaiset eyepiece kayika namna y kuweza kuwaona vyema na hapo nikaachia risasi kutoka kwenye ile sniper riffle 348 sauer na hapo ikaleta matokeo chanya na mtu mmoja kati yao alikuwa chini huku ubongo wake ukitapakaa huku na huko na kuwaacha wenzie wakihaha kujua risasi imetokea wapi.
Nilitabasamu baada ya kuona watu wanaojiita zwazima wakiogopa risasi na hapo nikajiambia “watanikoma” kisha nikatema mate chini kuonesjha kweli mimi ndie yule brown matata nilielitikisa jeshi la watu huko Tanzania sembuse hawa kanyaboya.
Nikafyatua tena risasi nyingine na hapo nikashuhudia akienda chini mtu mwingine na askari waliobaki wote wakkimbilia nyuma ya gari kwa ajili ya kujikinga na mimi nikazidi kubaki palepale juu mti huku nikiwa kimya kabisa na begi langu mgongoni.
*****
Askari wale wa hifadhi ile ya Iyumbi waliendelea kutulia palepale huku wakijaribu kujua adui yao niko wapi.
Nikiwa bado niko palepale nikaisikia sauti ya kitu juu kidogo ya kichwa change na hapo sikuchelea kujua huyo ni nyoka na mimi ikabidi nitulie vilevile bila kutikisika huku uvumilivu wakati wa hatari niliofundishwa jeshini ukiwa umenitwawala vyema kabisa.
Nyoka ailizidi kunitambaa mgongoni mwangu huku akiweka vituo kadhaa kama anaewinda kitu hivi na mimi nikajitahidi kuibana pumzi yangu isisikikike kwa mnyama yule alie juu ya mgongo wangu huku sasa wakti huo kichwa chake kikiwa kipo miguuni pangu na tubo lake likiwa juu ya begi langu na mkia wake ulikuwa bado upo kichwani pangu.
Nilipotizama kule kwa wale askari wa hifadhi nikaona wameongezeka tena na wakati huu walikuwa zaidi ya ishirini na walionekana wakijadili jambo na watatu kati yao nikaona wanaanza kuja na kijia kile nilichopita kuja kwenye mti huu na hapo hofu yangu ikaongezeka na nikajua kosa moja tu litanipeleka kuzimu nab ado nyoka yule alikuwa bado yupo mgongoni kwangu akisikilizia nisichokijua.
Akili ilinituma nifyatue tena risasi lakini nakajua mtikisiko wowote ule ni lazima nyoka yule aliemgongoni kwangu angefanya shambulizi tu,hapo ikabidi nitulie tu huku sasa watu wale wakizidi kusogea karibu namti ule niliojuu yake.
Walifika hadi pale chini ya mti ule na hapo nikamsikia nyoka yule akijivuta kwa nguvu kisha nikamsikia akitema kitu kwelekea kue chini na hapo nikashudia mmoja ya askari wale akitahamaki na kupiga kelele kisha wkaanza kukimbia kurudi kule waliko wenzao lakini nyoka yule nae akajirusha na kudondoka chini kisha akaanza kufukuzana nao nanhpo na mimi nikapata ahueni ya moyo lakini sikuta kuacha kuona nyoka yule atakacho kifanya kwa lile windo lake na nilitaka kujua kwa nini nyoka yule ambae hafananinii kuwa na madhara anapenda kuwinda watu lakini maswali yangu yalipata majibu haraka ni baada ya nyoka yule kumfikia askari yule kisha akamtanga kwa mbele na kunyanyua kichwa chake huku tayari mkia wake ukiwa umeanza kumzunguka askari yule, nilichokishuhudia sijapata kuona hata kitabu kimeandika kuhusu aina ile ya nyoka.
Alianza kujitunisha kuanzia chini kidogo ya kichwa chake na akanza kuwa kma puto na ukubwa wake ukaanza kuongezeka kila alivokuwa akijitunisha lakini kabla hajafanya alichokusudia akapigwa risasi na mtu yule alienipiga mtama wakati nikiwa kabini kwao na hiyo ndo ikawa ponapona ya askari yule amabe muda huo alikuwa ameshalowa kwa jasho.
Nikiwa palepale nikazidi kuwatazama askari wale wakizidi kujadili lakini tena sikutaka kuaacha hivihivi nikaachia risasi ikatua kwenye paji lauso wa mmoja wao tena nikaona mtafaruku kila mmoja akijaribu kuokoa roho yake na mimi tabasamu likazidi kuupamba uso wangu maana nilizihitaji hekaheka kama zile katika maisha yngu na nilipenda zaidi kuona mtu akipata taabu yakuokoa uhai wake kisa mimi waneniita haramu huku wengine wakiniita mlemavu na wengine wakiniita mkosi na mimi nasema mtazika kila nikitaka na mtalia kila ikisikika sauti yam tutu wa bunduki yangu.
*******
MZIGO HUU UTAKUWA TAYARI KUANZIA KESHO HIVYO WALE WASIOPENDA KUNGOJA TUWASLIANE KWA
0758573660
0658564341
0624155629
ASALAAAM KUDO