RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

kudo mimi nasomaga kimya kimya nisije kufa kwa presha ya arosto, za shunie nasomaga kwa sauti yote
 
sehemu ya tatu

Nilipotulia nae akatulia juu ya mti aliodondokea huku ndege wakiruka kuokoa maisha yao, nikageuza ili niendelee na safari yangu nilipokwisha kugeuka nikaanza kukimbia kwa kasi huku nikijua kabisa yule nyoka sitaweza kumwacha.

Mbele yangu palikuwepo na jiwe kubwa na nilipolifikia nikapita upande wa pili nikajibanza kwenye jiwe lile,jaukupita muda nikasikia nyasdi zaeneo lile zikitoa ukulele napunde nikaona sungura akiruka kwa tahadhari na hapo nikasikia majani yakiongeza kupiga kelele huku ukulele wake ukibadili mwelekeo kuelekea kule alikokimbila sungura yule.

Nikashusha pumzi zangu maana nilijua nimesalimika,nikatoka pale nilipokuwa nikaanza kurudi kule njiani lakini sikupiga hata hatua tatu nikakutana na nyoka yule niliekuwa namkimbia akiwa amenyanyua kichwa chake katika namna ya kutaka kutazama nyuma ya lile jiwe nilipokuwa na hapo nikajiuliza kuhusu akili ya nyoka huyu,mbona ana akili kama ya binadamu,amekuwa kama akifundishwa kuwinda hivi na hapo nikawa nimekosa mbinu ya kujiokoa kutoka kwa mnyama yule.

Lakini mnyama yule hakunifanyia shambulio lolote,alibaki akiwa vile vile na nilipojaribu kumtazama nikapata mshangao mwingine juu ya mnyama yule,hakuwa na macho nyoka yule na hapo nikajua kwanini anatumia kutema mate yale machafu lengo ni afuate harufu ya mate yake.

Nilijaribu kuwaza harufu ntakayokuwa nayo mwilini mwangu huku nyoka yule akiwa mbele yangu,nikajaribu kuweka sawa pua zangu ajabu sikuwa na harufu yoyote,na hapo nikaamua tu kutazama nyuma pale kwenye lile jiwe.

Kumbe pale nilipokuwa nimeegemea kulikuwa na mkondo wa maji uliokuwa ukitirika kutokea juu ya jiwe lile na kuingia katika pango lililokuwa chini ya jiwe lile kubwa.

Nikamtazama tena nyoka yule na hapo nikajua anajaribu kunusa harufu ya mate yake na haipati,lakini nitaondokaje pale maana hatua zozote zitamgutua nyoka yule na ataacha kunusa atafuata sauti.

Nikalishusha taratibu begi langu,kisha nikatazama kulia kwangu kulikuwa na mti mkubwa na majani mafupi,nikalirusha begi lile na kitendo cha ajabu nilichopata kukishudia ni shabaha ya nyoka yule katika kurusha mate yake.

Begi kabla halijatua chini tayari yeye alikuwa maekwisha temea mate nalilipokuwa likidondoka yeye alikuwa ameshafunga safari ya kuliendea.

Nikiwa najindaa kutimka pale nikasikia sauti ya kitu kikipita mbele yangu kwa kasi na kutua kichwani kwa yule nyoka na nilipomtazama nikajua kapigwa risasi.

Wakati nyoka yule akigaagaa chini mimi nikawahi kuruka na kulikwapua begi langu lakini kabla hata sijapiga hatua nyingine risasi ikatua miguuni kwangu,hii ikanipa tahadhari kuwa sikutakiwa kufanya lolote wakati ule na lengo la mpigaji lilikuwa ni kunionya nisifane lolote,lakini moyoni mwangu nilikiri kuwa mpigaji yule ambae sikuwa nimemwona alikuwa na shabaha ya ajabu.

Nilijaribu kutazama kila pahali lakini sikuona mpigaji au hata dalili za alipo mpigaji yule.Nikajaribu kutafuta kona risasi ilipotokea lakini ilikuwa ngumu kuelewa kwa sababu mpigaji alipiga kwa kutumia an imposible direction.hii ina maana alipiga akiwa katika mjongeo hivyo risasi ikakosa uelekeo sahihi wa kutokea lakini ikiwa na lengo la kutua mahali palipokusudiwa.

Nikiwa nimezubaa vilevile nikapata kuona kichaka kikijongea na kutulia hapo nikatambua nia askari wa hifadhi ile,na lile ni gari lao maalumu la kuwawinda majangiri na hapo nikatambua mimi ndie nitakuwa jangili,nilipojitazama kuna bunduki ya kisasa ikining’inia kifuani huku kisu kikiwa kiunoni kwangu.

Punde gari lile lilifika na kusimama karibu yangu na wakashuka watu watano,katika wale watano mmoja alikuwa ni mwanamke.

Walikuwa wamevaa mavazi yao ya kijani cha kufifia huku kikiwa kimeiva sana na kutaka kuwa kama na weusi kwa mbali,mikononi walikuwa wamebeba silaha za smg aina ya micro uzi machine gun na viunoni mwao walikuwa wamebeba mikebe ya risasi kubwa zenye kipenyo cha 38mm.

Mmoja akanifuata na aliponifikia akaninyanganya silaha ile na kisha akabeba kisu changu na begi langu na kuvitupia pembeni na wakati akifanya yale yote yakiendelea wenzie walikuwa wamenielekezea silaha zao.

Sikutaka kuendelea kubaki mikononi mwao lakini nilipopiga hesabau zangu nikagundua kuna mtu kati yao hayupo pale na ni yule aliepiga risasi,nilitambua haya kwa sababu silaha hizi walizobeba zina uwezo wa kupiga masafa ya mita 300-350 lakini pia ilihitaji mtu mwenye jicho la ajabu kuweza kufanikiwa kuona kichwa kidogo cha nyoka na kukipiga risasi na hata wakati naliona gari hili lilikuwa umbali wa mita kama mia hivi lakini umbali ule na silaha zile ni lazima zingetoa kelele lakini mimi kelele sikuzisikia na siaha zao hazina viwambo vya kuzuia sauti.

Kwa hayo machache nikaona kuna mtu yupo mahali na anafuata hatua zangu kila baada ya sikunde moja hivyo sikutakiwa kufanya ujinga wowote.

“wewe ni mhutu au mtutsi” niligutuliwa na swali hilo kutoka kwa mwanaume yule aliekuwa mbele yangu.

Nikapata kigugumizi kujibu maana nilijua uhasama wa makabila yale na jibu lolote lingenisogeza karibu na kifo au mateso ambayo sikuyatarajia.

“mimi mtanzania” niliamua kuwajibu ukweli na hapo nikaona wakitazamana kisha kama walioambizana jambo Fulani,nikasikia wakizikoki silaha zao na kunielekezea.

“mtanzania unafanya nini huku Burundi?” yule bwana aliniuliza kwa ukali kidogo huku macho yake mekundu yakiwa yananitazama kwa tahadhari kubwa.

Nilipata kigugumizi ningewambia nini watu wale ili wanielewe na hata ningewaelesha bado wangeniuliza naelekea wapi nikiwa na silaha mkononi mwangu.
 
sehemu ya nne

Mtu yule aliongea lugha Fulani ambayo sikuelewa na punde akaja mtu mmoja na kunifunga pingu kisha wakaniamuru niingie ndani ya gari yao,sikuwa mbishi ilibidi nifuate wanachokitaka,lakini kwa kuwa sikujua yajayo baada ya mimi kuingia katika gari lile la ajabu lenye mwonekano sawa na kichaka cha malindo ya porini.

******

Nilijikuta nikiwa katika chumba chenye kiza kiasi huku mwanga ukiwa unatoka kwa mbali na mikono yangu ilikuwa imefungwa juu na kukazwa,hali hiyo ilipelekea mimi nipate maumivu makali kwenye usawa nyama kwapa zangu,nilijaribu kungusha macho mle ndani lakini sikuona kitu cha kunisaidia.

Mawazo yangu yalinirudisha wakati tulipokuwa kwenye lile gari,nakumbuka wakati nilipokuwa nikiingia ndani ya lile gari nilikuta mtu mwingine ambae alikuwa ndie dereva wa gari lile kisha wakafuatia wale niliokuwa nao kule nje.

Kabla gari haijaondoka nikaona mtu akija kwa kasi akiwa ameshika silaha ya kudungulia na alikuwa ameshika simu ya upepo na kulisikika maongezi machache amabayo sikuyaelewa na aliepewa kumaliza kuongea kanitazama kwa jicho kali na kisha nikahisi kama kitu cha baridi kikipiga kwenye paji la uso wangu na hapo nikatopea kwenye usingizi hadi wakati huu nilimejikuta nimewekwa mateka.

Nikiwa bado nahangaika na kumbukukumbu ile mara mlango wa chumba kile nilichowekwa ukafunguliwa na akaingia mwanamke aliekuwa akavaa sare zake za kazi huku kiunoni kukiwa na mkanda alioning’iniza bastola yake ya willismith na mikononi mwake alishika sahani iliokuwa na chakula.

Nikiwa hivyo hivyo nimefungwa alianza kunilisha huku akinitizama kwa jicho la huruma kiasi na nilishindwa kuelewa kwa nini aliamua kuniangalia vile,sikuwa na muda wa kujiuliza kuhusu chakula kile nilikifakamia maana nilikuwa nina njaa kweli.

Askari yule alipohakikisha nimekula vya kutosha alitoka huku akinitizama kwa huruma ya kike nadhani ni vile alivyoona napitia mateso makali pale nilipofungwa.

Maumivu yalinizidi hasa sehemu za kwapani na kweli nilikuwa nimechoka hasa na sikujua kwa nini watu wale waliamua kunifunga pale namna ile na kwa nini hadi muda huo walikuwa hawajaja kuniomba wanacho kitaka kutoka kwangu na kama nilikuwa nimekosa basi walistahili kunishtaki kwa kuingia kinyemela kwenye kambi yao ile.

Kiukweli sikutaka kukamatwa kizembe namna ile na kama ningepelekwa kwenye vyombo husika ningeshtakiwa na kisha kurudishwa nchini Tanzania na kitu ambacho sikutaka kiwepo kabisa sikutaka kurudi huko nilikotoka.

*******


Mbele yangu alisimama mwanaume yule alienipekuwa kule milimani,alinitizama katika namna ya viulizo vile vile,hakusema neon akatoa ishara flani na mara moja akaja askari mwingine na kunifungua pale waliponifunga,na kwa uchovu niliokuwa nao nikajikuta najibwaga hini kama gunia la mkaa huku macho yangu yakiwa yanakimbia kutazama pale lililpokuwa fundo la mnyororo lililokuwa limefungwa mikononi mwangu,bado nilikuwa nimefungwa na mnyororo ulikuwa bado upo mikononi mwangu.

Lengo langu la kutazama si kuona ule mnyororo ni kuona madhara ya fundo lile kwangu na hapo nikaona kweli yale madhara ya wazi kabisa.

Nilikuwa nimevilia damu kuzunguka eneo lile na bado ngozi ya juu ilikuwa inaonekana kuathirika zaidi na hapo labda ndio maana wale wanajeshi waliona ninavyoteseka kutokana na mwonekano wa ngozi yangu.

Nilikuwa ni Alibino,lakini nani angenambia mimi ni Albino nikubali.Nilijiona niko tofauti na hao maalbino kwa kiasi kikubwa,kwanza ngozi yangu ahikuwa inaathirika na mionzi yoyote ile na hata macho yangu yalikuwa imara kabisa japo kwa karibu ungenitazma ungeona macho yangu yako tofauti na ya watu weusi.

Nywele zangu nazo zilikuwa na ubrown na si njano kama Albino wengine,kitu pekee kilichonipa udhaifu hata wa akili yangu kutokana na nilivyo ni kupauka kwa ngozi yangu tu.

Nikiwa bado nipo chini akaja askari mwingine na kuninyanyua kisha akaniweka begani kwake na kuanza kuniburuta kwelekea nje.Tulipofika nje nikakuta kuna kundi kubwa la askari wengine waliokuwa wameshikilia bunduki zao huku wakiwa makini sana na mimi na kila nilipokuwa nikijaitahidi kuwaza kwanini wananifanyia vile sikupata jibu.

Yule askari alienisaidia kusimama na kutembea alinibwaga katikati ya kundi kubwa la askari wale,na punde akanisogelea tena yule askari amabe nilihisi ndie kiongozi wao na kusema na mimi

“wewe mwanaharamu jiokoe mwenyewe kabla hatujakuchabanga risasi za moto”

Katika maisha yangu kama ulitaka kukosana na mimi basi ungeonesha kunidharau kwa namna yoyote ile hasa uweke udhaifu wangu kama silaha ya kunionea.

Baada ya yule kiongozi wao kusema vile nikasikia kama kuna kitu kinaniingia mwilini mwangu na hapo nikapata nguvu ya jabu na kujikuta nimesimama wima bila kutarajia na niliposimama tu wale askari wengine walikaanza kushangilia kwa nguvu huku baadhi yao wakipiga risasi hewani huku kelele za kutiana mzuka zikiwajaa.

Nikaanza kuwahesabu,na idadi yao ilipotimia katika ubongo wangu nikiajimabia kinyonge kabisa “wapo thelathini na nne”

Nikiwa bado nimesimama nikawa napiga hesabu za namna ya kuanza kuwatoka haini hawa ikiwa nimefungwa mikono na mnyoro mzito.lakini ni kama walisikia kilio changu mmoja kati yao akaja na kunifungulia na hapo nikawa huru huku sasa nikiwa napiga hesabu mpya namna ya kulichukua begi langu na kisu changu lakini pia silaha yangu,ambavyo vyote vilikuwa vimewekwa juu ya gari bovu lililokuwa pale kambini kwao.

Nikalitazma tena begi lile nikaona lina umuhimu kuliko hata uhai wangu maana mle ndani kulikuwa na kitu nilichokihitaji kuliko hata chakula,na nikaona nisipoomba hiki kitu basi hawa watu itakuwa ni ngumu kuwatoka kwa sababu walinizunguka na walihitaji nifuate njia ambayo wao wangeona inafaa mi kuipita.

“naombeni mizigo yangu” hatimae niliwambia lakini hata kabla sijajua kama nitakubaliwa au la nikashangaa nipo chini na nilipotazma nikamwona alieniangusha kwa kunizoa mtama maridadi kabisa,nikajiinua na kujikung’uta mikono yangu huku roho yangu ikizidi kujaa chuki na hasira juu ya watu hawa ambao wanjiita wakamilifu huku wenye rangi kama yangu tukiitwa Albino.

“ole wenu nitoke hapa salama”nikajisemea taratibu nafsini mwangu.

Begi lililetwa mbele yangu,lakini kisu na silaha yangu sikupewa na hapo nikajua kwanini hawajanipa silaha yoyote,lakini walichotaka kunifanyia nilikikijua kabisa walitaka kunifanya kama komando kipensi na Deadly pray.

Nikajikuta nikitabasamu huku nikiliweka begi langu mgongoni na kuwapa pole askari wale wa msituni walionichukulia kidhaifu kama ngozi yangu ilivyo,na sikuwashangaa maana askari hawa wa hifadhi au wanyama pori walikuwa na sifa moja karibia katika kila nchi ya Afrika,kutesa,kuua na kunyanyasa kila raia waliemkuta katika himaya zao.

Nikaamriwa kuanza kuondoka huku wakinitazma na wengine wakishangilia kwa vifijo na risasi hewani lakini hilo halikunitisha wala kuniogopesha maana sauti yam tutu kwangu ndio furaha yangu na hilo nililitambua bayana na bunduki kwangu ilikuwa ni kama manati tu na kuua kwangu ilikuwa ni kama kula tu sikosei windo langu,kwa hiyo hawa askari hawakunijua kabisa ni kibaya ni wao kuniita MWANAHARAMU.




asalaaam kudo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom