RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

Nilizidi kusogea mbele zaid na huko nikachoka sasa baada ya kukuta kuna kona na kona ile iilkuwa ni
kuzunguka na kurudi nilikotoka.
Nikasimama kupisha umakini wa akili yangu ufanye kazi ni wapi hasa nilistahili kupita kule nilikotoka
au hapa nilipo?
Nikiwa nimetulia tu masikio yangu yakapata kuhisi mburuzo wa kitu na sauti ya ajabu.
Nikarudi nyuma haraka na kujibanza kwenye kona ya jokofu moja,ambalo lilikuwa limemhifadhi
chatu aliekuwa akimla panya wakati huo.
Mjongeo ule ukazidi kusogea,hivyo nikatoa uso wangu kidogo ili nitizame kule kulikotoka sauti ile .
Mwili wangu ukafa ganzi baada ya kushudia kiumbe wa ajabu akiwa kasimama na shoka mkononi
,huku mavazi yake yakiwa chakavu na yamegandiana damu,nywele zake zilikuwa ndefu na
timtim,uso wake ndio ulioniogopesha zaidi,sura yake haikuonekana kama binadamu wa kawaida na
ili angalau unielewa vizuri basi kumbuka sura za watu waliocheza filamu ya wrong turn waeza
nielewa.
Sauti nyingine tena ikasikika nyuma yangu nikageuka,loh nilikuwa katikati ya watu wale wa ajabu
lakini huyu wa nyuma alikuwa wa ajabu zaidi mbali ya sura yake kuwa mbaya lakini alikuwa na umbo
kubwa mfano wa mcheza mieleka Great khali.
Huyu Great Khali alikuwa ameniona na hapo nikasikia akipiga makelele ya gadhabu na kuanza
kunifuata kwa mwendo wa haraka huku mguu wake wa kushoto akiuburuza,nikatamani kukimbilia
kwa huyu mwenye shoka lakini alikuwa ameniogopesha zaidi baada ya kuona akinyanyua shoka lake
baada ya kusikia makelele ya Great khali upande ule mwingine nikibidi nijiosogeze nyuma kidogo ya
pale nilipokuwa hivyo kupelekea nikawa naonekana kwa wote wawili na sikuwa na pa kukimbilia
maana ili nitoke pale basi nipite kwa Great Khali ama nipite kwa huyu mwenye shoka.
Nikiwa napiga hesabu za kujiokoa na hapo nikapata kuona kwenye lile jokofu la chatu,chatu yule
alikuwa ameanza kuijipigiza kwenye vioo vya jokofu lile hivyo kuweka ufa kwenye vioo na muda
wowote angelitoka pale,hakika ganzi iliingia mwilini bila kupenda.
Nilitupa risasi kadhaa kumfikia Great khali lakini ni kama zilikuwa zinamkuna tu alizidi kusogea na
hapo nikajua kabisa wale sio watu wa kawaida hawafi kwa risasi.
Mkono wangu ukakimbilia kwenye soksi ya kushoto huko ukarudi na kisu kidogo kilichotosha
mikononi na mahesabu yangu yakahamia kwa mtu mwenye shoka aliekuwa kushoto kwangu maana
kidogo hakuwa wa umbo kubwa kama mwingine hivyo na Mimi nikaanza kukimbia huku namfuata
na nyuma yangu alifuata Great kali aliekuwa anapiga makelele ya ajabu na uchu wa kunishambulia.
Nilikuwa nakaribia kugongana na mtu yule haraka nikapiga magoti chini na kwa Msaada wa
marumaru za kuteleza nikajikuta nasererka kama mchezaji Icard akishangilia goli uwanjani na kisu
changu kikapenya kwenye goti la kulia la jitu lile na haraka nilipotulia na lenyewe tena likawa
limepigwa kikumbo na Great khali hivyo likadondoka chini kwa nguvu na kumfanya Great asimame
kumuangalia mwenzake na kwa hasira likaunguruma kama Simba na kuzidi kunifuata kwa kasi zaidi
ya mwanzo lakini umbo lake likawa kikwazo cha kufanikiwa kunikamata kwa urahisi maana kila
lilipokuwa linarusha mikono nainama na kulikwepa huku kisu changu kikifanya kazi moja tu kuchana
maungo ya jitu lile la kutisha.
Jitu lile lililokuwa limedondoka chini nalo likasimama na tayari yalikuwa yote mawili na yalikuwa
yakinitizama kama Simba atazamae windo.

Lile nililolifananisha na Great Khali likaunguruma tena na kuja kwa kasi kunivamia lakini nikainama
chini na likapita na mimi nikawa nimefika kwa lile lilokuwa na shoka na nikalipitia tena na kisu mguu
ule ule wa kulia na nikasimama lakini sikuwa sehemu salama maana macho yangu yalipata kuona
chatu akichoropoka kwenye jokofu alilofungiwa na akawa akija kule tuliko kwa kasi ya umeme.
Sikutaka kufia kinywani kwa chatu yule,nikalipita jitu lile na kuangukia miguu ni kwa Great na harak
nikamchana na kisu tena kwenye guu lake la kushoto na nikapitiliza hadi upande wa pili na
nilipogeuka tayari chatu yule alikuwa amejiviringa mwilini mwa mtu yule aliekuwa na shoka na Great
kali akabaki akishangaa nikatumia upenyo huo kukimbia eneo lile na kurudi kule kwenye njia panda
ili sasa nipite njia ya kushoto lakini kama nilikuwa najua huko ndo salama nilikuwa nakosea sana.
Nilikuwa nakimbia huku natizama nyuma na tayari nilikuwa nakaribia kufika kulipo na njia Panda ile
na hapo bila kutarajia kuna kitu kikadondoka mbele yangu.
Alikuwa ni mtu aliekuwa kasimama mbele yangu lakini mtu huyu alikuwa mweusi kama kapakwa
mkaa na weusi wake ulikuwa wa kungaa sana,na nilipomtizama usoni hofu ikaujaa mwili.
Macho ya mtu huyu yalikuwa yanawaka kama mkaa wa moto na pua yake ilikuwa ndefu zaidi hata ya
ile ya Mr Bean,mikono yake alikuwa amefuga kucha ndefu mithili ya jini shumireta,hakika nilikuwa
katika wakati mwingine mgumu lakini ajabu iliokuwa inanitesa ni vile alivyodondoka mbele yangu
kama popo.
Mtu yule wa ajabu alikuwa amesimam mbele yangu kimya bila kufanya lolote lakini niliamini kabisa
ananitazama mimi
“Jeba anafanya biashara ya kutengeneza watu wa ajabu!”nilijisemea na kisha nikakitazama kisu
changu mkononi lilikuwa tumaini langu pekee.
Nijitikisa kama ninaetaka kufanya shambulizi na hapo nikaona kitu cha ajabu kutoka kwa mtu
yule,akapaa kwenda juu kwa kasi ya ajabu Kama vile Deepaklipa na akawa akinijia kwa kasi ya
umeme nikawahi Kuhama kutoka nilipokuwa na kujibana ukutani na mtu yule akajipigiza chini kwa
nguvu na kutoa kishindo kikubwa,lakini hakubaki hapo hapo akajinyanyua haraka na kubaki
aknitizama kwa gadhabu.
Bila kutarajia mtu yule akapaa tena na kuja kama vile mwewe na mimi nikajikunja kuelekea nyuma
na akapita juu yangu na niliposimama ili nigeuke tayari alikuwa amefika tena hivyo ikabidi nilale chini
na haraka nikasimama na nilipotizama kule aliko nikaona Great kali akija kwa kasi huku akiburuta
mguu wake na hapo nikajua tayari nimekwisha mbele ya viumbe hawa wa ajabu amboa sasa
nilliamini kabisa watakuwa ni walinzi wa eneo hili maana wanashirikiana kuniadhibu.
Nikiwa napiga hesabu za kuwatoka nyuma yangu nikasikia kishindo cha miguu ya watu ikija
inakimbia na punde wakawa wamefika pale.
Walikuwa watu sita na bunduki zao mkononi na skafu shingoni,haraka bila kuniuliza wakataka
kunizunguka ila kwa walichokiona mbele yangu wakatahamaki na kuanza kurusha rusasi hovyo na
hapo nikaona si kiumbe yule mwenye macho kama kaa la moto au kiumbe huyu niliemfananisha na
Great kali aliedhurika na risasi zile zaidi walizidi kutufuata kwa kasi na nilipoona vile ikabidi nikimbiae
na kuwaachia msala ule na ikabidi nisonge mbele na njia ile .
Kwa mbali nikawa nayasikia makelele ya watu wakishambuliwa na Great kali na mwenzie nijisemea

Usisahau kupitia hapa na kisha komenti ili nikutag kila inapotoka tayari sehemu ya kwanza imetoka
RIWAYA MPYA :MBWA WA GETI.
 
“Ngoma ya wakubwa watoto hawakeshi shubamit” kisha nikazidi kusonga na kwa mbele nikaziona
ngazi zikipandisha juu nafsi yangu ilijaa matumaini ya kutokeza nje lakini sikujua kama nitampata
Jeba.
*****
Tayari nilikuwa nipo nje ya chemba ile ya ajabu na watu nilkuwa sijui pa kuanzia ili nimfikie Jeba
ambae sikujua hata unyoya wake ulikoelekea.
“Wahi barabarani ameondoka saivi” ilikuwa sauti ya Kefa ikivuma masikioni pangu,na kisha nikasikia
honi ikipigwa upande wa mashariki kutoka pale nilipkuwa haraka nikaelekea huko.
Nilikuta Vogue nyeusi imesimama barabarani na Kefa akiwa ndani yake bila kuuliza nikaidandia na
Safari ikaanza.
“Nimefika tu nao ndo wanaondoka hapa” alinambia kefa,sikumjibu nikakaa kimya na kumwacha
aitawale barabara usiku ule.
Haukuwa mwendo wa kitoto na kwa mbali tulianza kuona taa za gari,Kefa akaongeza mwendo na
lakini wakati tunawakaribia wakaanza kuvurumisha risasi kutufikia ikabidi niiname na kefa atumie
ujuzi wake kuendesha
“unabunduki humu” nikamuuliza Kefa na bila kunijibu akatumia mkono wa kushoto kunipa micro
UZIHV ya kisasa kabisa nikatabasamu upele ulipata mkunaji.
Nikaikoki na japo ilikuwa inayumba gari yetu nikatuliza akili na kuamini nipo strait kisha nikanyanyua
bunduki ile na kwa kutumia uwazi wa kioo cha mbele kilichopasuka nikalenga usawa wa nyuma
ambapo niliamini dereva wa gari ile mbele atakuwa amekaa na kisha nikaachia risasi tatu kwa
mkupuo na nikamwambia Kefa apunguze mwendo ili kutega nione kama hesabu imefanikiwa .
Kama nilivyotarajia tulianza kuona gari inayumba na kufuatiwa na kishindo kikubwa cha kuanguka
kwa gari na hatukuchukua hata sekunde tukazima breki kwenye gari iliokuwa inazungusha tairi huku
ikiwa imebinuka kama kobe.
Haraka tukapekua lile gari na kukuta walinzi kama watano wa Jeba na Jeba mwenyewe ambae
alikuwa yuko hoi pembeni ya Dereva,na nikabaki nikimtizama hasa baada ya kukumbuka vile
alivyokuwa akiyatizama mateso yangu,
“oya mzigo huu hapa twenzetu maboya wasitukute”alinambia Kefa.
Nikasimama na bila kujiuliza nikamwagia risasi Jeba na huo ndo ukawa mwisho wa kiumbe yule na
kisha nikapiga tank la mafuta la gari ile na kisha tukadandia Vogue na kuondoka huku tukiacha
mlipuko mkubwa nyuma yetu.
******
Tulikuwa tumekwisha kulipekuwa lile koba tulilokuwa tumpora Jeba,na tulipata nyaraka kadhaa
lakini miongoni mwa nyaraka zile kulikuwa na mjengo mzima wa nyumba ya kifahari aliokuwa akiishi
Mobotu sese seko miaka hiyo ndani ya msitu wa Gbadolite,lakini ramani na jengo hili haikuwa
tofauti na mchoro ulioko kwenye paja langu na paja la Disuza.
Nikachukua kalamu na karatasi nikaanza kuchora na kulingana na kumbukumbu ya mchoro wa
Disuza na mchoro wangu nikapata ramani sawa na ile iliokuwa kwenye karatasi zile na hivyo nikajua
tulikuwa na mji wa dhalimu Mobutu mwilini mwetu, lakini nilipokagua na kwingine nikakuta karatasi
nyingi zimeandikwa kwa lugha ya mafumbo huku baadhi ya sehemu zikiwa zimeandikwa neno
BOSS,tulipojaribu angalau kujua maana tukashindwa kabisa na hapo Kefa akaja na jipya.
“Mtu wa mwisho wa kutufumbulia hili yupo gerezani na yatupasa tuzame huko mapema
iwezekanavyo na mtu huyo niliwahi kukuonesha na jina lake anaitwa Gambo.”
Nilimtizama Kefa bila kusema neno kisha nikaenda kitandani na kujilaza huku yeye nikimwacha
akinakili vyema michoro ile na kuipeleka kwenye mfumo wa kompyuta ili aitume ikulu kwa njia ya
MMs.
****
Ahsubuhi Kefa alinisindikiza hadi katiakati ya mtaa wa Megra na huko nilihitajika kufanya jambo ili
niingie mikononi mwa polisi.
Niliamua tu makusudi kukwapua kapu la mtu na kuanza kukimbia haikuchukua muda mrefu nikaingia
mikononi mwa dola na huko nikahukumiwa kesho yake kwa kesi ya uporaji na nilihukiumiwa miezi
miwili.
Ilikuwa ni rahisi mimi kuingia kwenye gereza nililolitaka kwa sababu magereza yote pale jijini
yalikuwa na fujo za wafungwa na hayakuingilika hivyo gereza moja tu ndilo lilikuwa na amani na
ndiko nilipelekwa huko.
Nilianza maisha nikiwa ni mfungwa mwenye vazi maalumu kwa sababu nilikuwa na kifungo kidogo
na ndani ya siku moja sikuwa nimefanikiwa kumuona Gambo.
******
Ilikuwa ni muda wa siku kama tatu hivi nilizokuwa nimekaa pale gerezani na ulikuwa ni muda wa
chakula wafungwa tukiwa tumekaa sehemu moja tukila ndipo nilipopata kuona kitu
kilichonistua,nilimwona Kisuti akiwa ni miongoni mwa wafungwa na nguo yake ilikuwa ni ya
wafungwa wa muda mrefu,nikanyanyuka ili nimfuate lakini askari mmoja akawahi kunizuia
nisanyanyuke na hata Kisuti mwenyewe alikuwa amenitia machoni.
Kila mmoja alikuwa bize na kufanya alichokuwa anakifanya kwenye uwanja mpana uliokuwa ndani
ya lile gereza,kuna waliokuwa wanacheza mpira wa kikapu,wengine mpira wa kamba na pia kuna
wengine walikuwa wakinyanyua vyuma hapa na wengine walikuwa wanafundishana ngumi za boxing
lakini si wote waliokuwa wanashiriki michezo ile nikiwemo mimi tulikaa mbali na wengine lakini mimi
nilikaa mbali wote na macho yangu yalikuwa na kazi moja tu kuhakikisha namtia machoni Gambo
lakini sikuwa nimefanikiwa.
“ulinitia Shaka sana wakati umetekwa na Jeba” niliisikia sauti ikiunguruma nyuma alikuwa ni Kisuti.
Imekuwaje hadi upo humu,nilimtupia swali bwana Kisuti
“Wakati unatekwa nilipata taarifa na haraka nikafanya maarifa ili nikuokoe lakini sikufanikiwa japo
kuikanyaga geti la nyumba ya Jeba na nikawa nimezingirwa na kundi kubwa la askari ambao sikujua
walitokea wapi na waliponikagua kwenye buti ya gari niliokuwa natumia kulikutwa maiti ya
mwanamke ndo maana niko hapa” yalikuwa maelezo machache kutoka kwa kisuti lakini yalikuwa na
maana pia
Unataka kusema kuna mtu ndani ya kundi alivujisha siri yako? Nilimuliza
 
Hii story imefikia patamu ongeza dose mkuu Kudoo!
 
JF ilizima tulitegemea baada ya kurudi hewani atashusha vitu kwa fujo ila ni kinyume chake.
Wasiliana na mimi ili uipate yote kwa mtindo wa PDF kuna watu si waungwana wanakopi kisha wanapaste kwa majina yao na kujipatia fedha
Hivyo anaehitaji utanitafuta hapa 0758573660 au utaniwhatsaap 0658564341
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom