Upande wa geti kuu kulikuwa na kulisikika kishindo kikubwa na punde zikafuatia risasi mfululizo
kuingia ndani huku sasa na mabomu ya mkono yakianza kutupwa.
Walinzi wengine wakikimbia kuelekea kule getinI ili kuongeza nguvu na wengine watatu wakakimbia
kuingia ndani nami nikajitosa kuingia nao.
Huku ndani nilikutana na walinzi wa kike wakiwa wapo kila kona na bunduki zao na kwa kuwa ramani
ya nyumba ile niliifahamu hivyo nikajua kabisa huko juu kwenye gorofa atakuwepo Jeba.
Walinzi walikuwa kama nane hivi waliokuwa chini ama ground na bila kuwauliza haraka nikapita
kuzipanda ngazi lakini nikakutana na pingamizi walikataa nielekee huko na bila kujiuliza nikaanzisha
mapigano kwa kila alieoonekana kunikwamisha huku visu vidogo vikinipa msaada mkubwa
kuwadhibiti wadada wale waliionekana wajuvi wa mambo yale ya mapigano .
Nilikuwa nikielekea juu gorofani nikakutana na mdada alieshiba kwa kimazoezi kama mwanaume
akanipa teke murua kifuani na kunirudisha chini kisha kabla sijasimama nikakutana na teke la mbavu
na wakati akiunguruma ili anishindilie tena nikawahi kusimamia magoti na kisha nikakinga mikono na
teke lake likaishiwa kasi ya kunidhuru.
Yule Dada akiwa anaendelea kuunguruma kama kasa jike akiliwa uroda na dume,akaruka juu kwa
mtindo wa Tailand kiki,lakini kabla hajatua chini nikamshudia akipaa zaidi hewani huku akitoa yowe
la uchungu na aliprudi chini hakuwa mtu tena bali alikuwa ni marehemu.
Nikatizama mlangoni sikuona mtu ila kulikuwa na vishindo vya watu waliokuwa wakija pale ndani
haraka nikasimama na kuokota bastola yangu nikakimbia kuelekea kule juu nilikoamini ndiko aliko
Jeba.nilipofika huko nikakutana na korido tupu na ukimya wa hali ya juu nikajua tayari Jeba
ameshatoroka na walinzi wake.
“Jitahidi uiwahi chemba b mzigo waelekea huko”nilimtarifu Kefa kupitia kifaa kilichokuwa
kimepachikwa vyema sikioni kwangu naeakanijibu kisha akanitaarifu niwahi kutoka nilipo maana
kuna kundi kubwa la Wamoro linaingia ndani na nje wameua walinzi wote.
Baada ya kupata taarifa ile haraka nikaanza kuangaza kila kona ya korido za kule gorofani maana
katika kumbukumbu zangu niliamini kabisa moja ya korido kuna sehemu ya kupita na kutokea nje
kwa kupitia hiyo chemba ni sehemu utakayao dodondokea ndiko kwenye sehemu ya kuingilia
kwenye chemba itakayokupeleka mlango b au mlango wa dharura.
Risasi moja ililia kwenye ground,hivyo nikajua tayari Wamoro wameshaingia pale ndani hivyo nifanye
haraka kabla hawajanikuta kule juu.
Nikazipitia korido mbili bila mafanikio na katika korido ya tatu nikakuta mlango wa dharura upo wazi
haraka nikajitosa huko na nilipokwisha kuingia tu nikaufunga mlango ule kisha nikabaki peke yangu
ndani ya kikorido kile chenye mlango,ajabu sikuona sehemu ya kupitia japo niliamini kabisa hapa ndo
penyewe lakini sikujua ni wapi nastahili kupitia.
Wakati nikizunguka zunguka kwenye kile kikorido nikapata kuona kitu kama ufunguo umedondoka
naikaufikia na kuokota na nikipokwisha kuokota nikautizama lakini sikuwa na maana nao nikautupa
chini,wakati unatua chini nikasikia tofauti ya mtuo ule hivyo haraka nikainama ulipoanguka na
kufunua zulia zito lilioluwa Pale.
Kulikuwa na mlango wa chini na haukuwa umefungwa,haraka nikaufungua na kuufuata kwelekea
chini na hatimae nikajikuta natokea nyuma ya jengo lile,lakini wakati nafika chini tu nikakuta kuna
watu wengine wawili waliokuwa wamejivika skafu wakijaribu kufungua mlango ulionesha unapitisha
kitu.
Bila kujiuliza nikawanyeshea risasi na wakati wanaenda chini tayari nilikuwa nimefika kwenye kilango
kile cha chemba,nikaangaza kwenye kiua kimoja kilichokuwa kimewekwa pale mahususi kwa ajili ya
dharura na katika kukumbuka kwangu kutoka kwenye chemba ile hadi kwenye kiua kile kuna hatua
kumi.
Kutoka pale nilipo nikazipiga hatua kumi kwenda kushoto na kweli nikakifikia kiua hicho na
nilipokipekeua nilikuta kuna kitu mfano wa switch lakini ilikuwa imeharibiwa hivyo haikuwa na kazi
tena.
Ku…..nikajikuta natukana tusi zito la nguoni na kurudi tena kwenye kichemba kile lakini hakukua na
pahali pa kufungulia maana kulikuwa na mlango wa aina ya kuhama na si milango ya kupachika.
Akili yangu ikakumbuka kitu haraka nikarudi tena kwenye kiua kile na kitendo bila kusita nikakifikia
kiswichi kile nikatizma kwa makini,nikapata nilichokuwa nakihitaji.
Nikazichuna waya mbili zilizokuwa zinapeleka umeme kwenye switch ile na kisha nikazigusanisha
waya zile, sikutaka kusubiri majibu ya kuona shoti pale nikakimbia tena kurudi kwenye chemba ile na
hapo nikakuta akili yangu imefanya kazi,uwazi ulikuwa umepatikana na sikuwa na namna zaidi ya
kujitosa huko ndani kabla kimlango kile hakijajifunga tena.
*****
Kama ungelibahatika kuingia mle ndani usingeweza kujua kama ile ni njia ya dharura,kulikuwa na taa
zinawaka na pia kulikuwa na upana wa kutosha tu palitengenezwa safi na kupambwa kwa nakishi
nyingi kama vile ni sehemu ya kuishi watu.
Nikazidi kusonga mbele huku nikijitahidi kuwa ndani ya muda ili Jeba asinitoroke.
Ni wakati nikiwa katikati ya njia ile nikapata kusikia kishindo kwa mbele,lakini kishindo kile kilikuwa si
kishindo kidogo kilikuwa ni kishindo kikubwa mithili ya kudondoka kwa ukuta.
Nikaichukua bastola yangu na kuindoa usalama huku sasa nikijaribu kuwa makini na njia ile.
Hatua zangu zilianza kuwa nzito na kishindo kile nikawa sikisikii tena.
Nikiwa naamini kabisa nipo karibu na mlango wa nje nikapata kukutana na jambo la kushangaza
,kulikuwa kuna njia mbili mbele yangu,huku njia zote zikionekana si njia tena bali ni eneo kubwa
lililogawanya vyumba vingi.
Njia moja ilikuwa inapita kulia na nyingine kushoto,nikapiga hesabu za kuotea ni wapi hasa
patanifikisha nje,nikaona inaeza kuwa ni njia ya kulia nikaifuata.
Nilikuwa natembelea ncha ya kiatu changu,huku sasa nikiwa nashudia milango mingi ya vioo ikiwa
upande ule na haraka nikakumbuka milango hii yaeza kuwa ni ya maabara za chini ya ardhi
Nikazidi kusonga lakini sikuwa nimefanikiwa walau kukutana na pahali pa kutokea zaidi nikajikuta
nikianza kuzunguka ndani ya maabara ile na sikuona wapi pa kutokea.
Ndani ya majokofua makubwa nilipata kusuhudia viumbe wengi wa ajabu wakiwa wamehifadhiwa
mle,kulikuwa na nyoka,nge,nyegere na wengineo.