Lumbi9
JF-Expert Member
- Oct 12, 2014
- 8,738
- 12,428
SURA YA SITA
Inspekta Kombora alikuwa mgonjwa
mahututi, ingawa hakuwa tayari kumweleza
daktari wake kuhusu kuumwa kwake wala
hakutaka kujieleza mwenyewe ni maradhi
gani yanamsumbua. Alijiona tu yu hoi bin
taaban, hali ambayo ilimtokea ghafla baada
ya kuviona vile vipande vya mwili wa
binadamu vilivyotawanywa kwa bomu. Lakini
kilichomuuguza zaidi ni kuokotwa zile ndevu
za bandia alizokuwa amevaa Joram Kiango.
Joram kafa! lilikuwa wazo lililomtesa zaidi
ya ukweli Inspekta Kombora. Joram ambaye
jina lake lilikuwa tishio kwa waovu wote
wenye nia mbaya kwa nchi na wananchi
wake! Joram ambaye alikubali kuiweka roho
yake hatarini mara kwa mara kwa lengo la
kuwakabiri maadui wenye nguvu na uwezo
wa kutisha! Joram, kijana mwenye moyo wa
jiwe na mwili wa chuma! Joram amekufa?...
Miaka mingi ilikuwa imepita, kiasi kwamba
Inspekta Kombora hakumbuki siku gani
aliyotokwa na machozi. Leo hii, akiwa peke
yake ofidini, akiitazama meza yake, alihisi
chozi likipenya kwenye vipingamizi vyote na
kuelea juu ya mashavu yake, jambo ambalo
lilimshangaza zaidi. Mshangao ambao
ulimezwa na hasira kali za ghafla. Akaupiga
mkono wake mezani kwa nguvu nyingi na
kuvifanya vifaa kadhaa vilivyokuwa mezani
hapo vidondoke sakafuni. Hakujishughulisha
kuviokota.
"Joeam kafa!... aliendelea kuwaza kwa
machungu.
Mara swali la kutisha likamjia akilini,
Ataitangazia nini dunia iliyoamini kuwa
Joram alikufa siku nyingi, atasema nini
badala ya ule uongo wa kifo
kilichosababishwa na sumu. Dunia
ingemwelewa vipi mzee huyu mwenye
dhamana kubwa serikalini.
Halafu akajikuta akitetemeka ghafla
lilipomjia swali la kutisha zaidi. Nani hawa
wauaji na wanakusudia kufanya nini?
Kwamba, hawa si adui wa mzaha, Hakuwa
na shaka na swali lake hilo. Yeyote
aliyehusika kumwua Joram na hasa
aliyemwua kikatili kiasi kile, hawezi kuwa
mtu wa mzaha hata chembe. Wala hakuwa
mtu anayecheza isipokuwa aliyedhamiria
kufanya jambo baya mno ambalo hakutaka
Joram Kiango aliingilie kama walivyofanya
majuzi kwa kuwavunja uti wa mgongo wale
waroho waliokuwa katika hatua za mwisho
za kupindua nchi na kuiuza kwa mabepari.
Hawa ambao wameshawishika kumwua
Joram kwa bei yoyote ile wanakusudia
kufanya nini?.
Ilimuumiza zaidi kujiona yeye kama mkuu wa
usalama akae kimya wakati akijua kuwa
kuna uovu uliojificha kando ukinyemelea,
wakati huo huo akiwa hajui ni uovu gani na
utatokea upande gani. Alikuwa amekwisha
fanya mengi. Tangu jana wakati akitazama
mabaki ya marehemu wakati yakikusanywa,
alikwisha chukua hatua zote za upelelezi
dhidi ya mauaji hayo. Kikosi cha askari
kilikwisha teuliwa kitambo, kikifuatilia kila
kichochoro ambacho kingeweza kuwafikisha
mbele ya adui, Maswali mengi pia yalikuwa
yakiulizwa. Lakini yawezekana kabisa
maswali hayo yangeweza kuulizwa kwa
miaka bila majibu kupatikana. Mtu pekee
ambaye ama alikuwa na jibu tayari, ama
angeweza kulipata mapema zaidi, sasa
alikuwa marehemu.
Hata hivyo afanye nini? Aendelee kusubiri
mtu au watu hawa wafanye yote
waliyokusudia wakati yeye akiendelea
kustarehe juu ya kiti hiki kama Ofisa wa
Polisi alijiuliza. Afanye nini kuongeza nguvu
ya mkono kuwatafuta maadui hao? Nani
anaweza kuwa na walau fununu ya
kinachotokea?.
Ni katika kujiuliza maswali hayo
alipomkumbuka Katibu Mahsusi ya Joram
Kiango, yule msichana mzuri, Neema Iddy.
Akajilaumu kwa uamzi wake wa kumpinga
msaidizi wake mmoja ambaye alipendekeza
Neema aletwe ili amthibitishie marehemu.
"Ataonyeshwa nini? Huone kama tunaweza
kumpata msichana wa watu ndoto za kutisha
katika maisha yake yote au hata wazimu kwa
kumuonyesha haya mabaki ya mtu aliyekuwa
mwenzi na mpenzi wake?". Kombora alikuwa
amemjibu hivyo askari huyo. "Hapana",
aliongeza. "Mwacheni".
Zaidi ya hayo, nadhani mnakumbuka kuwa
hii ni siri ya watu wachache sana,
watakaowajibika kufahamu aliyefariki ni
Joram Kiango. Wengine wote lazima
waendelee kuamini kuwa alifariki ghafla
kabla ya kifo hiki.
"Sasa aliuona umuhimu mkubwa wa
kumuona Neema. Hivyo bila ya kuaga wapi
aendako, alipanda gari na kuielekeza iliko
ofisi ya Joram.
Aliikuta ofisi hii imefungwa. Akaielekeza
Temeke, ambako aliifahamu jina la mtaa na
namba ya nyumba yake Neema.
******************************
Ilikuwa siku ndefu kwa Neema Iddy. Ingawa
kila siku ni kama siku nyingine lakini siku hii
aliiona hivyo kutokana na ile harara kubwa
iliyomkaria rohoni ikimtia shauku ya
kumwona Joram Kiango na kutaka kufahamu
hicho alichokuwa akikishughulikia safari hii,
hata akaweza kujibadili na kuwa mkongwe
kiasi kile, na kutangazwa uongo kuwa
amekufa. Neema alihisi kuwa mkasa huu bila
shaka ni wa kutisha na wa hatari kuliko yote
iliyotangulia, au sivyo, Joram asingechukua
hashari kiasi kile, wala polisi wasingeafiki
kutangaza uongo. Ilimsikitisha Neema
alipomkumbuka Joram alivyomnyima siri
hiyo kwa madai ya kwamba, ni "Hatari"
kumhusisha.
Siku ya jana nzima, Neema alikuwa
ameshinda katika hali hiyo. Akihesabu
dakika na masaa, akisubiri wakati ambao
ingetanagzwa upya redioni: "Joram yu hai...
Na amesababisha kukamatwa kwa wahujumu
ambao..." Ni hapo alipokuwa akiishia
Neema. Na ni swali hilo ambalo lilikuwa
likimweka roho juu. Hamu ya kujua safari hii
adui ni nani na walikusudia kufanya nini.
Neema alitabasamu, akakumbuka sifa
ambayo Joram aliipata kwa kusuluhisha
mambo magumu magumu. Mara hii, akawaza
atailetea nchi yake gani? Wazo kuwa
angetokea mtu, amshinde Joram, hasa
baada ya kutangazwa kuwa amekufa, kama
walivyotaka wao, swali hili halikuwa na
nafasi katika fikra za Neema. Akawa mtu
ambaye anasikia sifa za wapelelezi hodari
duniani, pamoja na kusoma hadithi za
kubuni juu ya upelelezi, Bado Neema alikuwa
hakumbuki kama alikwisha tokea yeyote
mwingine ambaye alikuwa na mtindo wa
aina ya Joram Kiango. Mtu asiyeogopa wala
kutishiwa, mtu asiyekata tamaa, mtu
anayejua kila anachofanya! Neema alihisi
furaha na faraja kubwa kuona kuwa yeye ni
msichana pekee ambaye amepata fursa ya
kushirikiana na mtu huyu shujaa. Hadhi
iliyoje!.
Ni mawazo hayo yaliyokuwa yakimfanya
Neema atabasamu. Lakini alihitahidi kuificha
tabasamu hilo kwa huzuni ya uongo kila
alipotokea mtu wa kumpa pole kwa kifo cha
'mwajiri' wake. Ilikuwa ni wajibu wake
kujifanya yumo katika msiba.
"AMekufa kijana yule mzuri? Siamini"
angesema kijana mmoja. Neema bila ya
kumtazama ya kumtazama usoni angemjibu
kwa masikitiko.
"Amekufa... ndiyo hali ya dunia.
Kifo cha ghafla! Wamempa sumu.
"Haijajulikana".
"Ama kweli ndege mjanja hunasa kwenye
tundu bovu".
Angeondoka huyo, aje mwingine. Kila mmoja
alisema hili au lile.
Neema aliwasikiliza wote na kuwafanya
waondoke wakiwa wameamini kile ambacho
hawakutaka kukiamini, kuwa Joram Kiango
amefariki.
Neema akiwa katika hali hiyo, tabasamu
rohoni, huzuni moyoni, alisikia gari
likisimama mlangoni mwao na baadaye
mlango wa chumba chake ukagongwa.
Aliingia Inspekta Mkwaju Kombora.
Macho ya Inspekta Kombora yalimfanya
Neema ahisi jambo mara moja kuwa
hakukuwa na habari njema. Neema akiwa si
mgeni kwa Inspekta Kombora baada ya
kuzungumza naye mara kwa mara kuhusu
harakati na mipango ya Joram, Neema
alimjua Inspekta huyu vizuri, alifahamu
wakati gani yuko katika hali mbaya
kimawazo na wakati gani anajisingizia hali
mbaya. Leo ilikuwa dhahiri kuwa kuna kitu
kikubwa kimemkaria rohoni.
"Kuna nini Inspekta?", Neema alihoji baada
ya kumaribisha kiti.
"Joram amekufa!" Inspekta Kombora
alimwambia.
"Najua", Neema alijibu kwa tabasamu.
"Nadhani bado hujanielewa. A-me-ku-fa",
alisisitiza,
Kidogo Neema akashangaa. "Ndiyo mzee!
Nadhani hata wewe unajua. Imebidi ujifanye
hivyo kwa ajili ya watu hawa ambao
wanamtafuta Joram. Muda si mrefu
atafufuka na jambo ambalo naamini
litakusisimua Inspekta".
Kombora akamkatisha kwa kumweleza
kuhusu tukio zima la bomu lililosababisha
kutawanyika kwa viungo vya marehemu.
"Nimeona nitakutia katika msiba na simanzi
iwapo nitakuonyesha mabaki hayo ya Joram.
Ama kweli kilikuwa kifo cha kusikitisha sana
dada yangu. Sikuona kama ungestahili
kumwona mtu uliyempenda sana akiwa
katika hali kama ile".
Ndipo Neema alipopata ukweli wa mambo
ulivyo. Aliduwaa kwa muda, Macho kayatoa
akimtazama Kombora wakati hamuoni.
Neema alihisi damu yake imesimama kabisa
na fikra kukwama. Joram kufa! Fahamu
zilipomrejea, alinong'ona maneno fulani
ambayo Kombora hakuyasikia. Kisha
akaondoka mbio hadi chumbani kwake.
Alifunua mto na kutoa bastola yake ndogo
aliyozawadiwa na Joram katika moja ya
sherehe zake za kuzaliwa. Akaishika imara
na kuitingisha huku akipiga kelele:
"Nitamwua yeyote aliyekuua Joram..."
alifoka Neema, lakini sauti ilitoka
ikinong'ona hata isiyafikie masikio yake
mwenyewe. Alipokumbuka kuwa alikuwa
hamjui mwuaji huyo, aliirejesha silaha hiy
katika maficho yake ya siri na kubaki
ameduwaa katikati ya chumba chake. Kisha
akarejea ukumbini na kuketi chini.
"Samahani Inspekta", Neema alisema
polepole, "Kwa muda mrefu sijapata habari
mbaya ya kuumiza kama hii",
"Si habari ya kupendeza hata kidogo. Mimi
pia imenitia homa. Pole sana".
Baada ya kutafakari kwa muda, Inspekta
Kombora akayarejesha maongezi yake kikazi.
Alimsihi Neema kumweleza chochote
anachofahamu ambacho kingeweza
kupatikana kwa mwuaji au wauaji hao
mapema iwezekanavyo. Hata hivyo Inspekta
Kombora alivunjika moyo baada ya
kugundua kuwa Neema hajui lolote la
maana. Hivyo akaondoka kimya kimya
kurejea ofisini kwake baada ya
kumkumbusha Neema kuwa kifo cha Joram
kiendelee kuaminika kuwa alifariki ghafla
kwa maradhi ambayo hayajafahamika.
Neema alibaki katika hali ile ile ya butwaa,
moyo ukiwa kama uliokufa ganzi na ubongo
kudumaa. Alihisi kama mtu aliyefika
ukingoni katika safari yake ya maisha.
Kwake Joram alikuwa kila kitu. Alikuwa
furaha na faraja katika maisha yake, heri na
neema yake. Hakuona vipi angeweza
kuyahimili maisha bila tabasam la Koram
mbele yake. Hakujua vipi ataweza
kusisimukwa bila harakati za Joram dhidi ya
adui zake.
Mapenzi ya Neema na Joram hayakuwa yale
ya kimwili kati ya msichana na mvulana.
Lakini Neema aliyaona kuwa ni makubwa
zaidi ya uhusiano wa aina hiyo. Makubwa
yaliyojengeka katika misingi mikubwa zaidi.
Ni kweli kuwa zipo nyakati ambazo Neema
alijikuta akimhitaji Joram kimwili kwa tamaa
kali kuliko alivyowahi kuhitaji kitu chochote.
Siku kama hizo alikesha kitandani akisali
kuomba Joram atokee, amkumbatie. Ni kweli
pia kuwa kuna siku ambazo aliwahi kuona
tamaa hiyo ikiwaka katika macho ya Joram
kwa nguvu kiasi kwamba ilitokea kama
mwujiza alipofaulu kutotamka kile ambacho
alitamani kukitamka. Kitu ambacho jibu la
Neema lisingekuwa zaidi. "Sawa tu".
Wote walifanikiwa kuzitawala nafsi zao.
Kama alivyowahi kusema Joram: "Akili
isipoutawala mwili ni sawa na gari kuacha
barabara na matokeo yake hakuna
asiyefahamu", Joram! ambaye sasa ni
marehemu!
Bado haikukubalika kichwani mwa Neema
kuwa Joram amekufa. Ilimrudia akilini siku
ile ambayo alimwona Joram kwa mara ya
kwanza.
Wakati huo Neema akiwa mwandishi wa
habari katika gazeti moja hapa nchini. Siku
hiyo alipata barua kutoka kwa mtu
asiyejulikana, ikimdokeza kuwa mtu mmoja
mkubwa serikalini alikuwa amehusishwa
katika mauaji ya watu watatu ambao maitiza
zao ziliokotwa huko Manzese. Habari hii
ilikuwa imeishitua sana nchi. Neema akiwa
mwandishi anayependa kuripoti habari
kubwa kama hii, aliamua kwenda kutafuta
ukweli na kuandika habari hii kwa undani ili
kuligusa kila jicho la msomaji.
Ilibidi Neema ajifanye kuwa mwanamke
kahaba ili aweze kuingia ndani ya jumba la
kigogo huyo. Huko ndani Neema alifanya kila
mbinu hadi kuteka mawazo ya mtumishi wa
mkubwa huyo wa serikali, ambaye bila
kufahamu aliweza kueleza habari zote za siri
zinazofanywa na kigogo huyo. Neema
alipofanikiwa kuujua udani wa mauaji hayo
alitumia mlango wa uwani kutoka katika
jumba hilo na kurejea ofisini kuwahi nafasi
katika gazeti la kesho. Lakini hakuweza
kufika mbali baada ya kujikuta akiwa katikati
ya watu wanne wenye bastola ambao
walimpiga na kitako kichwani Neema
akapoteza fahamu. Fahamu zilipomrejea
alijikuta yuko baharini, katika jahazi, mmoja
wa majambazi hao akiwa amemshika
kichwani na mwingine miguuni wakijiandaa
wakijiandaa kumtosa majini. Alilia kwa
nguvu zake zote lakini majambazi
hayakuonyesha dalili yoyote ya kumuonea
huruma. Mmoja wao alikuwa akisema kwa
kebehi.
"Kamlilie mama aliyekuzaa na hao bwana
zako waliokutuma kuchunguza mambo
yasiyokuhusu".
"Sikieni, mimi si mpelelezi..." alijaribu
kusema. hakuna aliyemsikia. Wakamwinua
juu na kumchezesha bembea ili wamtupe
kwa urahisi. Neema alikoma kulia. Badala
yake akayafumba macho yake akisubiri kifo.
Ni hapo lilipotokea jambo ambalo hakuna
aliyelitegemea. Mtu aliibuka ghafla kutoka
mahali fulani katika jahazi hilo na
kuwashambulia watu hao kwa mtindo wa
upiganaji ambao Neema aliwahi kuuona
katika michezo ya sinema tu. Dakika chache
baadaye maadui wote walikuwa wamelala
chini wakigalagala kwa maumivu. Mtu huyo
alimwunua Neema na kuanza kumkumbatia
huku akimtazama kwa tabasamu.
"Pole sana mpenzi", alitamka mtu huyo
baada ya kuona mshangao hauyaachi macho
ya Neema.
"Umeyaokoa maisha yangu... Asante sana",
Neema alisema kwa sauti ya unyenyekevu. "U
nani wewe?".
"Naitwa Joram Kiango".
"Joram!", Neema alifoka kwa mshangao.
Alikuwa amepata kusikia jina jilo
likihusishwa sana katika kuwakabiri
majambazi, wahaini na wahalifu wengine.
Alikuwa amelisoma mara kadhaa magazetini.
Lakini hakupata kumtia machoni. Ndio
kwanza akaona hawakukosea sana wale
walioandika kuwa yu kijana mzuri.
Walichosahau ni kutoweka neno 'sana' katika
sifa zake. Kwa keli Neema hakutegemea
kama mtu mwenye tabia zile za kupambana
na maadui wengi ana kwa ana bila hofu
angeweza kuwa hivi; mzuri sana, mtaratibu
sana, macho yenye upole, sauti... "Joram
Kiango!" akaita tena. "Umeniokoa lakini sijui
namna ya kukushukuru".
"Huna haja", Joram alimjibu. "Ni mimi
mwenye haki ya kukushukuru. Siku zote
nilimshuku mkubwa yule kuhusika katika yale
mauaji lakini sikuwa na ushahidi wa kutosha.
Wewe umefanya kazi nzuri Neema.
Umeniwezesha kupata ushahidi mzuri. Hawa
wauaji watasema ukweli watakapofika
mahakamani..."
"Ni wewe uliyeandika ile barua?", Neema
aliropoka ghafla.
"Ndio", Joram alijibu baada ya kutabasamu.
Nadhani utaniwia radhi kwa kukufanya
chambo. Nilikufahamu siku nyingi na kujua
kuwa u msichana shujaa. Nilijua kuwa
ungefanya vizuri, na umefanya vizuri... vitu
vyote viwili ambavyo nilivihitaji unavyo,
ushujaa na uzuri..."
Neema alijikuta akimkumbatia Joram.
Walitulia kwa muda na tena kwa faraja.
walipoachana Joram aliiwasha mashine ya
jahazi na kuiendesha hadi pwani ya bahari
ambapo aliwakabidhi majambazi hao kwa
polisi. Siku chache baadaye mahakama ilitoa
adhabu kali kwa 'mkubwa' huyo kitanzi na
majamazi kufungwa kifungo cha maisha jela.
Neema alipotoka mahakamani alimsaka
Joram bila mafanikio. Ilikuwa baada ya wiki
kadhaa walipokutana bila kutegemea.
Hawakutengana tena.
Na sasa Joram amekufa, Neema aliwaza.
"Yeyote aliyemwua nitahakikisha
anamfuata", Neema alifoka kimya kimya.
"Naapa".