Riwaya: Salamu kutoka kuzimu

Riwaya: Salamu kutoka kuzimu

Status
Not open for further replies.
Msiuane, hata mpiganaji amegoma. Kwa wale wapenzi tembeleeni Mpiganaji kila mara
 
Hizo bei umetoa wapi? Kwa nini vitabu ni adimu? Kama nimemuunga ndugu yangu alioko mbali na miji jf ili ajifunze kupitia Ben Mtobwa itakuaje? Huoni hii ni njia ya kutangaza tuu Kama magari ya mikoani wanavyotuwekea bongo muvis tunaenjoi na wengine tusio na umeme kwetu?
Pia Kama mmekosa wanunuzi ni kutokana na kukosa mbinu za kibiashara. Sie wadau 16 tuu wa riwaya si wa kuwafanya mbabaiiiiike kiivo.
Mpiganaji Blog na yeye nimeota ni muuza vitabu ndo maana anaweka namba yake kila akituletea kurasa kadhaa.
Ntamaholo yeye anasaidiana na wadau wengine Kama jimena, kidikudi, willy gamba1 na wengineo "kutangaza" tuu.
 
Last edited:
. ntamaholo na KudiKudi mtakuwa mfano wa wanaojinufaisha kazi za watu ndani ya mitandao ya kijamii. Pengine ni nyinyi pia mnaomiliki blogu hizo zinazotoa hadithi hizo .
Mkuu ukiwa unatoa shutuma na uhakika uwe nao, la sivyo huko mahakamani unapopasema hata mi napajua. Huwa sipendi kujihusisha na malumbano na mtu nisiemfahamu kwahiyo itoshe tu kusema yatosha na naomba nisitajwe kwenye malumbano yenu
 
Mi nipo dar temeke, chang'ombe tcc zaman kwa sasa cds.nahitaji sana vitabu vya joram
 
Hizo bei umetoa wapi? Kwa nini vitabu ni adimu? Kama nimemuunga ndugu yangu alioko mbali na miji jf ili ajifunze kupitia Ben Mtobwa itakuaje? Huoni hii ni njia ya kutangaza tuu Kama magari ya mikoani wanavyotuwekea bongo muvis tunaenjoi na wengine tusio na umeme kwetu?
Pia Kama mmekosa wanunuzi ni kutokana na kukosa mbinu za kibiashara. Sie wadau 16 tuu wa riwaya si wa kuwafanya mbabaiiiiike kiivo.
Mpiganaji Blog na yeye nimeota ni muuza vitabu ndo maana anaweka namba yake kila akituletea kurasa kadhaa.
Ntamaholo yeye anasaidiana na wadau wengine Kama jimena, kidikudi, willy gamba1 na wengineo "kutangaza" tuu.
Angeomba akapata ruhusa isingekua mbaya. Tunachoongelea ni kuchukua kitu kwa mtu bila idhini na kukifanya vile utakavyo. Swala sio kukimbiza wateja. Mbona mgumu kuelewa wewe.
 
My father is dead and l am wearing his shoes. Kuna kipindi aliwahi kufanya msako wa watu wa aina hii.
Pole sana kwa kumpoteza baba may he continue R.I.P. Ila kwa niaba ya wadau wenzangu Kina barige ntamaholo kidi kudi na wote ambao huwa wanasaidia kuzileta hapa, tunaomba ridhaa/ Idhini ya kuzisoma hapa, au hata kama ni wewe mwenyewe uwe unatuletea hadithi hizi hapa. Wapenzi wake ni wengi, na labda ndio njia pekee kwa sisi wengine kumuenzi ndugu Mtobwa.
Wengine tuko mbali sana na kuja huko ni mara moja baada ya miaka kadhaa, na wala hatuwezi kuvipata kwa urahisi.
Tunaomba sana kama hiyo haitaathiri soko la vitabu basi tupe ridhaa yako. Maana hii ni aina moja wapo ya matangazo pia japo najua vina uwezo wa kujiuza hata bila matangazo.
 
ninachopinga ni kitabu cha baba kinapotolewa as if hakina anayekisimamia. Nothing more.
 
Sasa mkuu tushauriane hapa. Nini kifanyike? Mi nimeomba ridhaa yako tu ila bado sijajua kama umekubali au la
 
SURA YA SABA II
Neema aliposhutuka kutoka katika usingizi mzito, alijikuta amelala kitandani akiwa uchi, kando Proper alikuwa amemkumbatia kwa mkono mmoja huku mkono mwingine ukizichezea chuchu zake. Lakini pia ulimi wa Proper ulikuwa katika kinywa cha Neema. Neema alishituka na kujivuta kando kwa nguvu huku akitamka maneno ambayo hayakusikika kikamilifu. Hata hivyo hakufaulu kujitoa katika mikono yenye nguvu ya Proper ambayo ilizidi kumbana.
"Bado kidogo mpenzi", Proper alisema, "Tutafanya mara moja zaidi kisha nitakuruhusu utakwenda zako", Sauti ilifuatiwa na kicheko ambacho katika masikio ya Neema kilijaa jeuri na kebehi.
"Nini kinatokea hapa?" Neema alifanikiwa kuuliza swali, huku mshangao ukimtoka na aibu ikianza kumwingia.
"Tunafanya mapenzi, ndio maana nikasema bado kidogo halafu nikuruhusu uondoke zako", Proper alimjibu Neema.
"Mapenzi!" Neema alihoji huku akifoka. "Nitakushitaki", Neema alifanikiwa kumwambia Proper.
"Kwa nani?".
"Umeninajisi. Umenitenda pasi hiari yangu. Siwezi kuvumilia upuuzi huu, nitahakikisha unafika kwenye vyombo vya sheria", Neema alisisitiza.
Kicheko kingine kikamtoka Proper. "Usiwe kama mtoto mdogo", alisema Proper akiendelea kucheka, "Nani atakuelewa? Zaidi, nani atakuamini? Ulivyo mrembo kila mmoja ataamini kuwa unatosha kabisa kumfanya Profesa yeyote mwenye hisia asahau majukumu yake kwa muda ili afanye mapenzi na wewe. Nani atakanusha nikisema kuwa jana tulikutana mitaani tukaahidiana uje leo na umekuja? Au kuna yeyote aliyeniona nikikuvuta huko nje na kukuleta hapa ndani?"
Maneno hayo yalimwingia Neema. Hakuona uwezekano wowote wa kuifanya hatia ya mtu huyu idhihirike . Lakini alikuwa na hofu moyoni. Si hofu ya kufanya mapenzi bila kukusudia. Hofu yake ilitokana na kutofahamu kitu gani kilimfanya apoteze fahamu na kuvuliwa mavazi na ... Pia hofu ilimzidi kwa kutokuwa na hakika na yote yaliyofanyika baada ya kupoteza fahamu. Ilikuwa kama ndoto ya kitambo anayokumbuka kwa shida. Ilikuwa kana kwamba ananusa harufu iliyomfanya apoteze fahamu. Pia, alikumbuka kuwa alimsikia mtu huyo alipokuwa akimhoji kuhusu kifo cha Joram Kiango, naye akiropoka kila kitu alichofahamu. Alimweleza juu ya yule mwanamke mwenye sura mbaya ambaye aliileta picha yake. Kisha alikumbuka kuwa alinyweshwa kitu fulani na kuambiwa, "Hiyo itakufanya usafiri leo hadi aliko mpenzi wako Joram. Usisahau kumsalimu. Baada ya hapo ndipo nguo zilipovuliwa. Akaletwa kitandani ambako...
"Pamoja na kufanya mapenzi", Profesa Kimara, au Proper alikuwa akiendelea, "Nitakulipa vema, Sina mkono wa birika , hususan kwa mabinti awzuri kama wewe. Umenifanya nimsahau mke wangu aliyefariki miaka kumi iliyopita". Alisema huku akiushughulisha mkono wake kutambaa kutoka katika matiti ya Neema hadi tumboni mwake, mkono huo ukateleza hadi katikati ya miguu ya Neema.
Neema akausukuma mkono huo kando na kujiinua kwa nguvu. "Sijapata kumwona mtu mshenzi kama wewe", alifoka kwa hasira akiyaendea mavazi yake yaliyokuwa juu ya kochi.
"Kwanini mpenzi? Nipe nafasi nyingine uone jinsi nilivyo mstaarabu katika suala zima la mapenzi. Tafadhali. Mara moja tu halafu utakwenda zako...".
Sauti ilikuwa ya mapenzi. Ni tabasamu lake ambalo lilibeba kitu kingine kabisa. Kitu kisicho karibu na mapenzi hata kidogo. Kitu ambacho kilikuwa kinyume kabisa na mapenzi na mahaba. Jambo ambalo lilimuongezea hasira Neema. Alizivaa nguo zake haraka haraka, Akautwaa mfuko wake na kuanza kutoka.
"Siku yoyote ukijisikia tena kufanya mapenzi unakaribishwa". Proper alisema huku akifungua pochi lake na kutoa kiasi cha pesa.
"Sihitaji chochote kutoka kwako", Neema alifoka huku akitoka.
Alipofika kituo cha basi alifungua mkoba wake kuangalia. Kila kitu kilikuwa sawa isipokuwa bastola yake! Hakujua cha kufanya.
Alipofika nyumbani, Neema aliketi juu ya sofa akajaribu kufikiri, mara akahisi hana nguvu za kufikiri lolote. Alichokitaraji ni pumziko tu. Mara akausikia usingizi mzito ukimnyemelea. Kitanda alikiona mbali. Akajinyoosha juu ya kochi usingizi mzito ukamchukua.
Ulikuwa usingizi wa aina yake. Ulimchukua moja kwa moja na kumtoa katika dunia hii na kumpeleka katika dunia nyingine. Dunia yenye kiza kizito. Dunia isiyo na hisia.
Unono alipoingia alimkuta Neema katika usingizi huo. Awali hakufahamu kinachotokea. Akapoteza dakika kadhaa akilihusudu kwa wivu umbo zuri la Neema ambalo lililala kifudifudi juu ya kochi. Kisha akapoteza dakika zingine kadhaa akijaribu kumwamusha kwa kumsukuma. Mara akaiona damu nzito iliyokuwa ikimtoka Neema midomoni na puani, Ulimi ulivyoponyoka kutoka kinywani na kuduwaa nje, upande mmoja. Akayaona macho yalivyotoka nje. Kila kitu kilitangaza mauti ya Neema.
"Amekufa", Unono alifoka huku akiruka kurudi nyuma.
Kifo. Unono alikifahamu sana. Alikifahamu sana toka wazazi wake wote wawili walipokufa kwa ajali ya gari wakati huo akiwa na umri wa miaka mitano tu. Alikifahamu kifo miaka minne baadaye wakati shangazi yake aliyekuwa mlezi wake wa pekee, alipofariki kwa kipindupindu. Naam, alikifahamu kifo na madhara yake. Lakini hakupata kuwa karibu na kifo kiasi hiki. Hakuwahi kumugusa mtu aliyekata roho na kumsukasuka. Hivyo, alipouondoa mkono wake juu ya mwili wa Neema, aligeuka na kuanza kutoka nje mbio, huku akipiga kelele.
Hakwenda mbali kabla ya kutokea gari yenye dereva mwenye haraka zake, ambayo ilimgonga Unono na kumwua pale pale.
Watu walioshuhudia ajali hiyo, hasa baada ya kumuona alivyokuwa akikimbia hovyo barabarani, na kumuona alivyokuwa, waliamini mara moja kuwa alikuwa 'Mwendawazimu mmoja' amegongwa na gari na kufa. ******************************
Miongoni mwa watu walioshuhudia ajali hii ni Proper. Kama watu wengine yeye pia ajali hii ilimsikitisha. Tofauti ni kwamba yeye hakusikitika kwa kuona maisha ya binadamu yakiteketea ghafla katika hali ya kutisha kama hiyo, la. Kwanza hakuna jambo lolote lililomsisimua katika maisha yake zaidi ya kumuona mtu akikata roho. Hakuna mchezo alioupenda au kuujua zaidi ya kuua ama kushuhudia kifo.
Proper alisikitika kukosa fursa na kuzungumza na Unono ili kujua yote anayofahamu juu yake na wapi alikopata picha ambayo Neema aliizungumzia wakati alipomhoji baada ya kumlewesha kwa dawa zake. Aliamua kummalizia Neema, baada ya kuona kuwa hakujua lolote lingine la haja. Ndiyo akamnywesha sumu ile maalumu ambayo ilikusudiwa kumuua Neema kwa utulivu, baada ya muda fulani. Kisha alimfuata kwa hila hadi hapa ambapo alijificha katika uchochoro akimsubiri Unono. Alifanikiwa kumwona wakati anaingia ndani na alivyotoka mbio. Kabla hajaanza kumfuata, ilitokea gari na kumgonga kwa bahati mbaya.
Proper alifanikiwa kujisokomeza katikati ya umati wa watu waliojaa hapo barabarani. Akiwa kajibadili kimavazi na kitabia, hakuwa yule profesa Kimara tena, bali mmoja wa watu kadhaa wa mkitaani na hakuna yeyote ambaye angeweza kumshuku. Hivyo hakuna aliyemwona akiinama na kuokota mkoba wa marehemu na kwenda kando ambako aliufungua na kupekuwa ndani. Ndani ya mkoba huo hakukuwa na chochote alichohitaji. Aliutupa mkoba huo chini na kupishana na watu waliokuwa wakielekea kwenye tukio hilo la ajali, akaelekea nyumbani kwa Neema.
Hakuna aliyemwona akiingia. Alisimama kando ya kitanda akitabasamu kwa 'uzuri' wa kazi yake. Neema alikuwa amekufa kwa namna aliyotaka. Yeyote ambaye angeingia na kumtazama haraka haraka angedhani yuko usingizini. Hata hivyo Proper hakuridhika kikamilifu. Akambeba na kumlaza juu ya kitanda na kumfunika kwa shuka hadi usoni. Kisha akafanya msako wa haraka haraka. Alikuwa akiitafuta ile picha aliyosema Neema. Hakuiona. Akalazimika kuondoka
Mlangoni alikutana na jirani mmoja wa Neema ambaye alimtazama kwa macho ya kuuliza japo hakuuliza chochote.
"Nilikuwa mgeni wa huyu dada lakini naona amelala", Proper alieleza.
"Amelala?" jirani huyo alihoji akijaribu kuchungulia ndani. alipoona mwili wa Neema umetulia kitandani aliamini. "Naona tumwache alale. Shoga yetu lapatwa na msiba mkubwa".
Akiufahamu umbeya wa wanawake wa Dar es Salaam, Proper hakusubiri kumsikiliza. Alifanya haraka kurejea nyumbani kwake ambako aliendelea kuandaa mpango wake. Kisha akaipitia tena taarifa yake ambayo alikwisha iandaa kwa ajili ya kuipeperusha nje. Aliirekebisha taarifa hiyo hapa na pale, kisha akavuta mtambo wake wa kupeperusha habari na kuufungua. Kisha aliufunga na kusubiri muda wa majibu. Aliyahofia majibu hayo lakini hakujali. Maadamu alikuwa kadhamiria. Lolote lisingemfanya ashindwe kuutekeleza.
Kidogo hofu ilikuwa ikimwingia kwa kufikiri wapi yule marehemu aliyegongwa na gari aliipata picha yake na vipi picha hiyo isipatikane ingawa alikuwa ameitafuta kwa umakini. Kuna jambo la kutisha linamnyemelea? Wapi? alijiuliza.
Hakuna vipi angeweza kuacha mwanya wa kupatikana kwa urahisi. Mambo mengi ama yote aliyotaka yafanyike kikamilifu alikuwa akiyafanya mwenyewe, japo alikuwa na watu wengi chini yake ambao wanalipwa vyema na wamekamilika kimauaji. Wote hao yeye anawafahamu lakini hakuna yeyote anayemfahamu. Yeyote anayedhani kuwa anamfahamu basi alikuwa akijidanganya kwani Proper unayeongea naye leo si Proper wa kesho. Kadhalika vifo vyote vilivyotokea alivitekeleza mwenyewe kiufundi zaidi ya alivyofundishwa. Alimuua Waridi kikatili, ili polisi waamini kuwa ni mwendawazimu mwingine ambaye anaipenda sana kazi ya kuua watu wasiokuwa na hatia. Joram amekufa kwa bomu, Neema alikuwa msiri wa Joram! Yeyote aliyemuua Joram asingesita kumuua Neema. Zaidi, Neema kafa kwa sumu ile ile iliyokusudiwa kumuua Joram. Katika hali kama hiyo, nani angefanya nini kumtia hatiani kwa urahisi? Polisi? Wao wasingeenda mbali na ukweli. Joram aliyekuwa na uwezo wa kunusa chochote sasa yuko kuzimu.
Hata hivyo Proper alihisi kama uovu fulani uliojificha kando ukimnyemelea. Kama angeipata ile picha... Kama yule mwanamke asingepatwa na ajali... angeweza kujisikia salama zaidi. Aliifukuza hofu kwa kujiliza kwa moja ya sigara zake kali, ambazo huzivuta kwa nadra sana. Kisha akaitazama saa yake. Alipoona imepungua dakika moja ili kupata majibu yataarifa yake, aliubonyeza mtambo wake. Karatasi yenye maandishi ikajitokeza. Akaichukua na kuanza kuisoma.
...Utapewa majibu rasmi kesho muda kama huu... taarifa hiyo ilieleza, akaisoma tena kisha akaichana, mabaki akayatia katika mtambo mwingine wa kusaga karatasi hata ikawa kama majivu.
Hakujua jibu rasmi litakuwa lipi na lilimhusu vipi. Alichotuma yeye halikuwa swali wala ombi. Ilikuwa taarifa ambayo watake wasitake ingefanyika. "Wapuuzi", aliwaza. Akawatoa akilini na kuanza kuandaa mkutano mwingine baina yake na washirika wake. Washirika ambao kiasi fulani hawakuwa zaidi ya mateka wake.
 
Barige, tumekatazwa kuzitumia riwaya hizi, kuzitoa huko zinakoandaliwa kuzileta JF. Nameless girl amekataza, na anapanga kutushtaki.

Naomba tusiendelee kuzileta hapa, kama vipi tusome hukohuko Mpiganaji na kukaa kimya, labda Mpiganaji ana mkataba na nameless nasi inaonekana tunawachafulia.

Namtafta invisible aifutilie mbali thread hii
 
da! Nimekuelewa sana kaka.tuko pamoja.asante kwa kumwaga simulizi
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom