Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,174
- 17,635
Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) imefanya Uchaguzi wa Viongozi wa Kitaifa kwa nafasi za juu, ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi kilichomalizika, Bw. Hamisi Abdallah Livembe, amechaguliwa tena kuendelea kushika nafasi ya Mwenyekiti.
Uchaguzi huo umefanyika tarehe 15 Desemba 2025, katika Ukumbi wa New Generation, Jijini Dodoma, na umehusisha idadi kubwa ya wajumbe kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa zoezi la uchaguzi, Mwenyekiti Livembe alieleza kuwa uchaguzi huo ni halali na unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, ambapo Ibara ya 8.0 inayohusu utaratibu wa upigaji kura na utoaji wa matokeo ilisomwa wazi mbele ya wajumbe wote wa mkutano.
Mwenyekiti Livembe alieleza kuwa zoezi hilo limefanyika kwa mujibu wa Katiba ya JWT, baada ya wajumbe zaidi ya 300 kuridhia mkutano na uchaguzi kuendelea, kufuatia tamko la Msajiri wa Vyama na Jumuiya.
Katika uchaguzi huo, viongozi wafuatao walichaguliwa kushika nyadhifa mbalimbali; Hamisi Abdallah Livembe Mwenyekiti, Omary Hussein Mussa – Makamu Mwenyekiti, Abdallah Salim Mohammed – Katibu Mkuu, Ismail Masoud Matare – Naibu Katibu Mkuu hata hivyo, Uchaguzi huo umefanyika kwa amani na utulivu, na wajumbe wote waliridhia matokeo yaliyopatikana.