Riwaya: Nitakupata tu

Dah pumzika kwa aman bro hii story nilikuwa sijaanza kuisoma niltaka iishe kwanza Mungu akuondelee adhabu ya kabri mkuu
 








 
NITAKUPATA TU


SEHEMU YA 094
Masimba akifuatana na Mwanaharamu walikuwa wamepakiza mwili wa Veronika kwenye gari waliyokuja nayo huku wakihakikisha wamemfunga Teddy vizuri na kumuweka kwenye buti kisha wakaondoka eneo hilo nakuelekea maeneo ya nje ya jiji la Dar es salaam.
***********
Wakati Vero akielekea kwenda kwa mzee Raymond hakujua kuwa tayari Teddy alikuwa amenusa na kufahamu wapi walipokuwa watoto wa masimba, akiwa na lengo moja tu la kuhakikisha kuwa anamuua Masimba, ndipo alipopigiwa simu na makao makuu ya ujasusi kutoka nchi ya marekani,kumtaarifu kuhusu ni wapi walipo watoto wa Masimba na kuhusu Mzee Raymond na uhusika Wake na kundi hatari la Mafia duniani na uhusika wake katika kuhakikisha kuwa wanaiyaribu mipango yote ya Marekani na kuhakikisha inapatikana betri kwa kila hali.
Teddy alipopata taarifa zote ndipo alipo wai kwenda kwa Mzee Raymond na kumchoma Sindano ya sumu maeneo ya shingo na Mzee kufariki hapo hapo. Kisha kwakutumia uzoefu alio upata nchini Syria na mafunzo ya kijajusi aliyopata Kwa hisani ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania alifanikiwa kuwahamisha watoto na kuwapeleka kwenye nyumba kubwa iliyopo maeneo ya Masaki karibu na Double tree hotel kisha yeye kurudi na kumsubiri Masimba hakujua kuwa Veronika ndiye angetokea
***********
Gari iliendeshwa taratibu huku kila mmoja akiwa mwenye hudhuni akifikiria kuhusu kifo cha Veronika, "Mwanaharamu"Masimba alimwita na kumstua na kumtoa katika dimbwi la Mawazo, Angalia kwenye saiti mila, hamadi gari nne zilikuwa zikija Kwa kasi kuwafuata wakina Masimba, ikabidi Masimba akanyage mafuta na kuongeza mwendo... Itaendelea
 
hongera mkuu.. ila pengo la Ibra naona halizibiki
 
KWA NIABA YA FAMILIA YA MZEE Masimba WA HANDENI MKOANI TANGA, TUNAPENDA KUTOA SHUKRANI ZETU ZA DHATI KWENU WAPENDWA WETU AMBAO MLIKUWA NASI KTK KIPINDI IKI KIGUMU CHA MAJONZI YA KUONDOKEWA NA MTOTO WETU MPENDWA MAREHEMU Ibrahim Haji Islam ( MASIMBA ) ALIE FARIKI JUZI TAR.4/07/2017 SAA MBILI UCKU KTK HOSPITAL YA TEMEKE DAR-ES-SALAAM,NA KUZIKWA LEO TAR.6/07/2017 VIBAONI HANDENI MKOANI TANGA,SHUKRANI ZETU ZA DHATI ZIWAFIKIE MADAKTARI NA MANESI WA HOSPITAL YA TEMEKE WALIO AKIKISHA WANAPIGANIA UHAI WA Ibrahim LAKINI KWA UWEZO WAKE MUNGU IKASHINDIKANA,PIA TUNA WASHUKURU WATU WOTE WA KIGAMBONI ALIPO KUWA ANA ISHI MAREHEMU KWA MSAADA WAO WA HALI NA MALI KUAKISHA TUNA MALIZA HILI SWALA ZITO KWETU,PIA TUNA WASHUKURU MARAFIKI WOTE AMBAO WALIO KUWA WANAISHI NA MAREHEMU KWA KUJITOLEA KWA NAMNA MOJA AU NYENGINE,ASWA SHUKRANI ZETU ZIWAFIKIE WALE WOTE WALIO TUSAIDIA KTK UPANDE WA HELA HILI TUFANI KISHE PALE PALIPO NA MAPUNGUFU YA PESA,NA PIA TUNA WASHUKURU WALE WALIO PIGA SIMU NA KUTUPA POLE PAMOJA KUTOA MAWAZO YAO,KWANI TUNA THAMINI MAWAZO YENU NA KUTAMBUA UMUHIMU WENU KWA MTOTO WETU MASIMBA, KWA UFUPI ATUWEZI KUTAJA MTU MMOJA MMOJA ZAIDI YA KUWASHUKURU WOTE,HILA JUMAMOSI TUTA MALIZA TATU NA KUPITISHA KISOMO MOJA KWA MOJA, TUNA RUDIA TENA ASANTENI SAANA KWANI TUMEJIFUNZA KUWA MTOTO WETU ALIKUWA NANYI VIZURI KTK MAISHA YENU YA KILA SIKU,NDIO MAANA ASILIMIA YA WATU WENGI MLIGUSWA NA KIFO CHAKE MPAKA WENGINE WALIFIKIA KUTOAMINI KAMA MASIMBA AMEFARIKI KWELI? HILA TUNA PENDA KUSEMA KAZI YA MUNGU AINA MAKOSA,KIKUBWA NI KUMUOMBEA DUA HILI APUMZIKE KWA AMANI, ASANTENI SANA NA ATUNA CHA KUWALIPA HILA MUNGU NDIO ATAKAO WALIPA HAPA DUNIANI MPAKA HAELA.....by haji mvula
 
Mwenyezi mpumzishe kwa Amani mja wako na umsamehe dhambi zake,
Hakika kifo cha IBRA kimetugusa wengi na tunashindwa jinsi YA kuisapoti hata familia ya marehemu,
 
Nashauri km itawezekana kwa wale tuliokuwa tuna soma riwaya zake kuchangishana ili kuwasaidia hata wanae iwe mchango wetu kwake
Busara tupu hapa umeandika juzi kati niliandika kuhusu jambo hili kiasi kuonyesha thlimthamini akiwa hai na pia tunamuenzi japo kwa pesa kidogo ni jambo jema.
 
Nashauri km itawezekana kwa wale tuliokuwa tuna soma riwaya zake kuchangishana ili kuwasaidia hata wanae iwe mchango wetu kwake
ni jambo jema. nashauri liratibiwe vizuri kuepuka yale ya wala rambirambi wa Arusha
 
Hatareeee sanaaaa nzuriii
 
Daah nimekuja kusoma riwaya nifurahi nimegeuka na moyo kutoa machozi Rest In Peace Ibra
 
Nilianza kuisoma hii riwaya wiki hii nikijua itafika mwisho kumbe mwandishi wetu kipenzi anatutoka hivi hivi so sad IMENIUMA SANA! Ulazwe mahali pema peponi Ibrahim Masimba sisi tupo nyuma yako.
 
daaaaaa!!!!,inauma saaana aseee, Mungu mpunzishe kwa amani ndugu yetu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…