JENIPHER
SEHEMU YA 019
******
Ilikuwa lazima wafike, ilikuwa lazima waende katika misitu ya katanga kurudi na watafiti waliotekwa. Ilikuwa kazi ngumu kuifikia misitu hiyo bila kupitia Mjini. Hakukuwa na njia ya gari ama baiskeli ya kuwapeleka huko pale watakapoingia katika nchi ya rwanda. Lakini ilikuwa lazima wafike, ilikuwa lazima watembea ama kutumia usafiri kufika huko. Hapa kuwa salama na hapakuwa sehemu sahihi katika kutembea. Hilo lilikuwa changamoto kwa watu hawa. Ilikuwa lazima waende. Walikuwa wamekaa watatu katika chumba kimoja wakiitizama ramani ya kuwafikisha huko. Kila mmoja kichwa kilikuwa kikimuuma akitafuta jinsi ya kufanikisha azma yao. Kazi waliopewa na taifa ilikuwa kubwa sana, kazi ya kurudi na watafiti wao, kazi ya kurudi na wanasayansi. Kila mmoja aliijua hali ya kiusalama katika nchi ya kongo, kila mmoja alitambua hatari ambayo wangekutana nayo endapo wangeanza kwenda kinshasa. Walitaka kutumia msitu kwa msitu katika kufika huko. Jenipher, Masimba pamoja na Muddy bado walikuwa wamejifungia katika chumba hicho kila mmoja akiichora ramani katika kichwa chake. Ilikuwa safari ya kufa na kupona, safari ya kifo mkononi, safari ambayo ilibeba matumaini yote ya wanasayansi waliotekwa. Ilikuwa ni lazima wote waanze ndani ya misitu.. hilo likapita na kilichobakia ilikuwa ni safari. Wana usalama wengine wawili tayari walikuwa wameshatangulia katika nchi ya congo katika kufanya kile kinachojulikana kama kuisafisha njia. Hawa walipelekwa katika kunusa kile ambacho kingewasaidia wanausalama kuingia nchini humo pasipo kuwepo kwa matatizo. Walihakikisha wananusa katika kila sehemu kuhakikisha kwamba mission ile inafanikiwa katika wakati ambao umepangwa. Kila kitu kilikuwa tayari kwa safari, kila kitu kiliandaliwa ikiwa ni pamoja na watu wakuwapokea katika nchi ya rwanda. Tayari kulikuwa na watu waliowekwa tayari kwa kuwapeleka mpaka katika mpaka wa rwanda na nchi ya Congo. Hayo yote yalifanywa na Spy ambao walipandikizwa katika jeshi la rwanda kwa sababu ya kusaidia pale yatakapotokea mahitaji ama uhitaji wa taarifa Muhimu sana. Yote hiyo ilikuwa ni kulifanya taifa la Tanzania liwe katika usalama. Wakati sisi tukiwa tumelala huku tukila raha, kuna watu katika Tanzania hii wakihatarisha maisha yao. Wakati sisi tukipiga kelele na porojo katika vitu visivyo na msingi, kuna watu ambao maisha yao wameyaweka rehani kwa sababu ya watanzania. Wapo katika mipaka na vikosi vya waasi wakichukua hili na kuchukua lile yote ikiwa ni kwa sababu ya nchi hii.. Kuna watu ambao huitwa Spy katika kitengo fulani nyeti katika nchi hii. Watu hao ndio wanaotufanya Watanzania tuwe na amani. Watu hawa asilimia tisini ya maisha yao ni kifo. Wapo ambao wapo katika kikundi cha Al shababy, wapi ambao wapo katika mataifa yote makubwa wakichukua taarifa sababu ya usalama wetu. Hawa hawalali kwa sababu ya Tanzania. Na kazi yao kubwa ni kuhakikisha tunaishi kwa amani.
Hawa ndio watu ambao walitengeneza njia katika mission na hata katika ziara za viongozi wa nchi. Kila uchwao Tanzania tukiwa na amani tambua hawa wamehusika kwa asilimia mia. Hivyo suala la kufanikisha watu hawa kufika misitu ya katanga ni lazima waifanye wao kazi.
******
Waliingia katika nchi ya rwanda kila mtu kwa njia yake na kwa wakati wake. Wote walikuwa na taarifa moja ya kukutana kwao katika mpaka wa nchi hizo mbili. Kwahiyo nilazima kila mmoja apitie katika njia tofauti ili kutokuhisiwa kuwa ni wamoja katika safari hiyo. Wa kwanza kufika huko alikuwa Jenipher akiwa sambamba na vijana wengine wawili ambao hawa walihakikisha kuwa hakuna chochote kibaya kingeweza kumtokea Jenipher. Waliwasili hapo majira ya jioni wakiwa katika usafiri wa kawaida. Walipofika hapo wakamuacha Jenipher atangulie eneo hilo wao wakimfuata kwa nyuma. Hakuwa Jenipher pekee katika mwili wake, bali alikuwa Jenipher sambamba na watoto wake watatu katika maeneo tofauti ya mwili wake. Umbo lake lilimvutia kila mwanaume ambaye alimtizama, hiyo ilikuwa ni silaha muhimu sana kwake. Silaha ambayo kwa kitaalam huitwa pussypower kutokana na mara nyingi wanausalama wengi wa kike kutumia miili yao ilikupata habari sehemu fulani. Alitembea akiuacha mwili wake ujitingishe, wanaume wengi wakinyarwanda walikuwa wakimtizama katika namna tatu tofauti. Wapo ambao walimtizama kwa matamanio ya kumpata, kuna ambao walimtizama kwa woga wakidhani ni mwanausalama. Wengine walimtizama kwa kuwa alikuwa akivutia kutizama. Hilo likampa Jenipher nguvu ya kuendelea kutembea kwa mwendo ule. Ilikuwa ni lazima wapite hapo na kuingia katika nchi ya congo, ni lazima waitafute njia ambayo ingewapitisha hapo. Akaona ni muda wa kuutumia mwili wake. Muda wa kutafuta mbinu ya kufika katanga pasipo kutokea kwa rabsha zozote zile. Akaifikia meza ambayo haikuwa na mtu akajibweteka katika sehemu hiyo ambayo palikuwa na wamama wanaouza chakula. Muda mfupi akafuatwa na mwanadada mrefu, mzuri wakinyarwandwa. Huyu alikuwa msichana mzuri kama walivyo wasichana wengi wa rwanda.
"Habari yako?" Alisalimia mwanadada yule kwa kiswahili kibovu.
Kusalimiwa katika Lugha ya kiswahili kulimshtua sana Jenipher. Lakini ulikuwa mshtuko wake pekee yake, mshtuko ambao haukufika hata machoni kwa msichana huyo.
'"Nzuri tu, umejuaje kama mimi najua hii lugha? Akajibu Jenipher huku akimuangalia mwanamke yule. "Kuna mtu pale ndio ameniambia kuwa nikuulize una kula nini!" Alijibu mnyarwanda yule huku akinyoosha kidole kumuonyesha Jenipher. Jenipher akageuza macho yake, akajikuta akimuona mtu ambaye hakumuona wakati anaingia hapo. Alikuwa akiangaliana na Masimba. Alikuwa tofauti na masimba yule alietoka Tanzania. Huyu alikuwa amebadilika zaudi na zaidi. Tabasamu likachanua usoni kwake. Lakini wakati anacheka akamuona mwanamke mwingine wa kinyarwanda akisogea pale alipokaa masimba. Tofauti ya huyu na yule, yule alikuwa na sare za jeshi la rwanda lakini uzuri walikuwa wakifanana. Akili ya Jenipher ikafanyakazi kwa haraka sana, huyu alikuwa mmoja kati yao. Huyu alikuwa mmoja kati ya spying anayefanya kazi ndani ya Jeshi la Rwanda. Alikuwa pale kwa kazi maalumu ya kuhakishasha wanavuka na kuingia salama katika nchi ya Congo.
ITAENDELEA
HATA HII UKIITAKA UTAIPATA KUANZIA MWANZO WAKE.