kidi kudi
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 2,510
- 2,163
- Thread starter
- #21
Sehemu ya 15
Bila kuchelewa alimpa taarifa hizo Geofrey
ambaye alichukulia jambo hilo kama la
kawaida na aliamini siku ambayo angerudi
Tanzania mambo yote yangekuwa sawa.
Magreth alikuwa amejiwekea utaratibu wa
kumtembele gerezani kila mwisho wa wiki
jambo lililompa sana faraja. Geofrey naye
tayari alianza kuingiwa na mshtuko wa moyo
juu ya Magreth kutokana na ishara za wazi
alizozipata lakini aliona jambo hilo haliku
wezekana kwa yeye kuwa na uhusiano na
mrembo huyo. Siku zote alimchukulia kama
msichana mwenye huruma na aliamini
hakuna jambo ambalo lingeweza kutokea
kuhusiana na hisia zake. Muda ulikwenda na
hatimaye Geofrey alibakiwa na wiki mbili za
kutumikia adhabu yake, hakuamini hata
kidogo kuwa angeliacha gereza hilo na kuwa
huru. Furaha yake iliongezeka zaidi kutokana
na ahadi ambayo Magreth alishampa ya
kufanikisha safari yake kurudi Tanzania.
Zilibaki siku mbili, hatimaye moja na
mwishoe siku ya Jumapili majira ya saa nane
alipewa nguo za kuvaa alizoelezwa aliletewa
na mtu aliyefika gerezani hapo kumchukua.
Geofrey hakujiuliza maswali mengi akiamini
nguo hizo zilitoka kwa Magreth aliingia katika
chumba cha kubadilishia nguo na kuanza
kuvaa nguo hizo. Lilikuwapo shati moja rangi
nyekundu pia viatu na soksi vilikuwa vya
rangi hiyo pamoja na jinzi moja iliyovutia
kwa muonekano. Geofrey alivivaa na kuanza
kutembea akitoka katika chumba hicho askari
magereza walishtuka na kuanza kumshangilia
kwa mwonekano mzuri aliokuwa nao. Mkuu
wa gereza alimsifia kwa tabia yake nzuri
aliyokuwa nayo kipindi akiwa gerezani hapo
zaidi kitendo chake cha kuwatetea wanyonge.
Alimaliza akimwambia aliamini toka wakati
huo angekuwa raia mwema na mwishoe
alimhurusu aondoke. Geofrey alianza
kutembea kuelekea geti kuu la gereza hilo
kwa haraka akiwa hajiamini kwani alihisi
angeitwa tena kurudi kifungoni. Mara baada
ya kutoka katika geti hilo kidogo moyo wake
ulitulia lakini alihitaji kuondoka kabisa eneo
hilo. Alikuwa akimwangalia Magreth kama
alikuwapo eneo hilo kumchukua kama
alivyoelezwa na askari magereza.
Alizungusha kichwa kila upande eneo hilo
pasipo kumuona zaidi ya gari lililokuwa na
rangi nyekundu ambalo lilikuwa kando yake
kidogo ambalo vioo vyake havikuhurusu mtu
wa nje kuona ndani. Akiwa anatafakari juu ya
jambo la kufanya alishtushwa mlango wa
gari hilo uliokuwa ukifunguliwa, alielekeza
macho yake ili aone mtu ambaye angeshuka.
Alishuhudia mguu wa mwanamke ukiwa na
kiatu rangi nyekundu ukitoka kabla ya mtu
huyo kutoka kabisa. Mshtuko wake
uliongezeka zaidi baada ya kuona mtu huyo
alikuwa Magreth, alikuwa amevaa vitu vyenye
rangi nyekundu toka chini hadi juu. Alikuwa
na gauni la kuvutia na zaidi mkononi pia
alikuwa na maua ya rangi hiyo, alianza
kutembea akielekea eneo ambalo Geofrey
alikuwa amesimama. Mara baada ya
kumfikia alimkubatia kabla ya kusikika pole
sana Geoffur .. ahsante lakini zaidi
nashukuru kwa kunijali muda wote nikiwa
jela Alijibu Geofrey ambaye mapigo yake ya
moyo yalimwenda mbio hakuelewa jambo
lililoendelea siku hiyo lakini rangi nyekundu
ndiyo ilimpa shaka zaidi. Aliongozwa mpaka
kwenye gari hilo lililokuwa Range Rover, kabla
ya kuondoka kwao Geofrey aliamua kuuliza
jambo lililomtatiza ingawaje lilimpa hisia za
ushindi moyoni mwake.
kwa nini kila kitu kina rangi hii.. aliuliza
Geofrey baada ya kushindwa kujizuia,
Magreth alicheka kidogo kabla ya kumgeukia
akimtizama usoni Geoffur leo ni tarehe kumi
na nne mwezi wa pili siku ya wapendanao
duniani, naamini tunapendana alimjibu
jambo lililomfanya Geofrey acheke kwa furaha
ingawaje hakujibu kitu ila aliona kama vile
alikuwa amelala masikini na kuamka mfalme.
Tayari alijipa aslimia mia za kuwa na
Magreth mpaka mwisho wa maisha yake.
Waliongoza mpaka hoteli ya kifahari
iliyokuwapo katika jimbo hilo la Biloku na
huko ndipo uhusiano wao ulianza rasmi
baada ya ahadi nyingi walizowekeana. Siku
iliyofuata Magreth alianza kumtafutia Geofrey
hati ya kusafiria kurudi Tanzania.
Mara baada ya taratibu zote kukamilika
alimsindikiza Geofrey uwanja wa ndege tayari
kwa safari kurudi Tanzania, alimweleza
angerudi pia mara baada ya masomo yake
ya mwaka mmoja uliobakia. Magreth alikuwa
akilia kwani alihisi huo ndiyo ulikuwa kama
mwisho wa yeye kuonana na Geofrey, mara
baada ya kuagana alikuwa amempa namba
ya simu na fedha za kutosha akiwa
amemweleza mara baada ya kufika Tanzania
amjulishe. Safari hiyo ilianza na mwishoe
walifika Tanzania wakiwa wamepita
Uingereza, Ethiopia na nchi nyingine. Geofrey
bila kupoteza muda alikodi teski na
alimweleza dereva ampeleke eneo lililokuwa
na kampuni ya JAJHO, halikuwa jambo gumu
kwa dereva huyo kwani alidai kampuni hiyo
ilikuwa kubwa sana wakati huo. Alihitaji
kufikia katika kampuni hiyo kwani bado
Geofrey kumbukumbu alikuwa nazo juu ya
kampuni hiyo aliyoiacha akiwa anaelekea
Marekani na ilikuwa chini ya umiliki wa baba
yake na wenzie wanne.
Hatimaye walifika katika foleni ya magari
iliyokuwapo maeneo ya posta akiwa
ameelezwa walikaribia kufika katika eneo
lililokuwa na ofisi hizo za kampuni ya
JAJHO. Alikumbuka kumtaarifu Magreth
kuwa tayari alikuwa amefika Tanzania,
wakati huo alikuwa amekaa upande wa
mbele wa teski hiyo akiwa na dereva na kioo
cha gari kilikuwa wazi. Alichukua simu yake
na kumpigia mara baada ya kuita mara moja
ilipokelewa nimeshafiaka Tanzania na niko
nae .. kabla hajamalizia sentesi hiyo mara
baada ya kusalimiana kwao kibaka mmoja
aliinyan`ganya simu hiyo kwa nguvu na
kuondoka kwa kasi eneo hilo la foleni na
tayari magari yalikuwa yamehurusiwa.
Geofrey alichanganyikiwa ghafla juu ya tukio
hilo zaidi hakuwa na namba ya mawasiliano
ya Magreth ambayo ilihifadhiwa kwenye simu
hiyo. Baada ya jitihada za haraka za kuipata
simu hiyo kushindikana aliamua kukubaliana
na tukio hilo na alimhurusu dereva waendelee
na safari akiwa na imani kuwa angeitafuta
namba hiyo. Mara baada ya kufika eneo hilo
aliongozwa mpaka kwenye ofisi ya mmiliki
mkuu wa kampuni hiyo aliyekuwa na hisa
nyingi, aliamini alikuwa anaenda kuonana na
baba yake.
Mara baada ya kuingia katika ofisi hiyo
alikutana na sura tofauti na baba yake ila
kumbukumbu zake zilimjia kwa mbali juu ya
mtu huyo.
samahani namuulizia James Kibudo
Alisikika Geofrey mara baada ya kuketi, mtu
huyo alishtuka kidogo kabla ya kumuuliza
unamuulizia kama nani katika kampuni hii
alijibu mtu huyo kama mmoja wa wamiliki
wa kampuni hii alijibu sikiliza kijana James
Kibudo alifilisika miaka mingi iliyopita na
hayupo kwenye orodha ya wamiliki wa wa
kampuni hii, alituuzia hata jina lake ndiyo
maana hatujabadili jina la kampuni hii ya
JAJHO tukihofia soko letu mtaani, zaidi
alikutwa ameuuawa nch kabla hajamalizia
kuongea Geofrey alikurupuka na kumvamia
akitaka kujua vizuri sentesi ya mwisho
iliyohusu mauaji.
Walinzi kadhaa waliitwa ofisini hapo na
kumkamata zaidi mtu huyo aliyekuwa bosi
aliyejitambulisha kama Jackson aliwaita
wamiliki wenzie Amos, Hamis na Onesmo ili
wamhoji mtu huyo. Geofrey baada ya kutulia
kidogo alijieleza vizuri na mwishoe watu hao
walimpa taarifa za kuuawa kwa baba na
mama yake miaka kumi iliyopita na mdogo
wake Robert walidai hawakujua eneo
alilokuwapo na imani yao ilikuwa alikuwapo
Marekani.
Walimweleza juu ya taarifa walizokuwa nazo
juu ya kifo chake baada ya ajali ya ndege
iliyotokea nchini Guyana. Baada ya maelezo
hayo Geofrey akiwa na majonzi aliaga na
kuondoka eneo hilo la ofisi za JAJHO,
mawazo yake yalikuwa ni kuhakikisha
anaenda Kenya na kushuhudia kabuli la baba
na mama yake.Jackson na wamiliki wenzie
waliitana na kushangilia juu ya tukio hilo la
maelezo ya kifo cha James na mkewe
waliyoyatoa kwa mwanaye na waliamini siri
yao isingevuja.
Alielekea katika nyumba moja ya kulala
wageni maeneo hayo ya Posta na muda wote
alikuwa akilia juu ya tukio hilo alillolisikia,
siku iliyofuata alianza safari akielekea Kenya
kwa lengo la kwenda kuliona kabuli la baba
na mama yake. Mara baada ya kufika jijini
Nairobi aliongoza katika kituo kikuu cha polisi
cha jiji hilo na kuomba kuonyeshwa makabuli
hayo. Tayari alishaelezwa awali na mr.
Jackson kuwa askari wa kituo hicho
wangemsaidia kwani walihusika kwa kiasi
kikubwa na mazishi ya wazazi wake.
ITAENDELEAAA....