Madhara anayoyapitia kiongozi muuaji

Madhara anayoyapitia kiongozi muuaji

Izato

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2019
Posts
5,311
Reaction score
11,414
Kuna madhara makubwa anayoyapatia kiongozi mwenye hatia ya mauaji hata kama ana mamlaka makubwa juu ya wananchi wake. Kuuwa ni dhambi kubwa kwa hiyo basi kuna madhara makubwa ya kisheria, kijamii, na kiroho ama kisaikolojia.

Madhara ya Kisheria
1. Kufunguliwa kesi ya jinai mahakamani.
2. Rekodi ya jinai ya muaji itabakia maisha yote ya muuaji.

Madhara ya Kijamii
1. Kutengwa na jamii kwa kuwa watu watakuogopa na kuepuka kushirikiana na muuaji.
2. Kupoteza heshima mbele ya jamii.
3. Familia za wahanga daima hutafuta fursa ya kulipiza kisasi kwa muuaji

Madhara ya Kiroho na Kisaikolojia
1. Dhamiri inakusuta, kutopata usingizi. Kumbukumbu mbaya zitamfuatilia muuaji mchana na usiku, huku ukajihisi hatia moyoni mwake.
2. Hofu, wasiwasi au kuteseka moyoni.
3. Wauaji hupata "depression" ambayo hupelekea kutamani kujiua na hata kuishia kujiua kabisa
4. Kujitenga na Mungu
Mwanzo 4:10-11
Sauti ya damu ya ndugu yako inanena kutoka katika ardhi. Dhambi inamtenganisha muuaji na Mungu wake kwa Imani yoyote Ile aliyokuwa nayo.
5. Laana ya damu inamuandama na kizazi chake chote
Methali 28:17
Mtu aliyezongwa na hatia ya damu ya mtu, atakimbilia shimoni; mtu asimshike.

Kwa kawaida muuaji huwa anapata hasira za mara kwa mara kutokana kuandamwa na mawazo ya hatia ya mauaji. Kuuwa hakutatui tatizo badala yake inamletea muuaji matatizo zaidi.
 
Hapo madhara ya kiroho na kisaikolojia tukizingatia kifungu (4) kujitenga na Mungu hii inategemea huyo kiongozi anamuabudu Mungu yupi.

Maana miungu wengine kadiri anavyomwaga damu ndivyo anavyozidi kumkaribia that's why hata kuna baadhi ya waumini wenzake utakuta wanamuunga mkono.
 
Zomeazomea pale ilipotajwa awamu ya 6 na Mwana FA inadhihirisha Samia anapitia magumu huku akifarijiwa na wanafiki waliomzunguka. Muuaji lazima akinywe kikombe cha maovu yake.
 
Tunaona sasa Jumuiya ya Commonwealth nayo imekuja na maelekezo yanayohitaji utekelezaji la sivyo utawala wa huyu kiongozi muuaji utazidi kutengwa na jumuiya ya kimataifa..

Kila siku sura inazidi kumshuka kwa aibu na hofu, huku akiwa amezungukwa na kundi la wanafiki wakimfariji. Siku si nyingi atajikuta yupo peke yake.
 
Kuna madhara makubwa anayoyapatia kiongozi mwenye hatia ya mauaji hata kama ana mamlaka makubwa juu ya wananchi wake. Kuuwa ni dhambi kubwa kwa hiyo basi kuna madhara makubwa ya kisheria, kijamii, na kiroho ama kisaikolojia.

Madhara ya Kisheria
1. Kufunguliwa kesi ya jinai mahakamani.
2. Rekodi ya jinai ya muaji itabakia maisha yote ya muuaji.

Madhara ya Kijamii
1. Kutengwa na jamii kwa kuwa watu watakuogopa na kuepuka kushirikiana na muuaji.
2. Kupoteza heshima mbele ya jamii.
3. Familia za wahanga daima hutafuta fursa ya kulipiza kisasi kwa muuaji

Madhara ya Kiroho na Kisaikolojia
1. Dhamiri inakusuta, kutopata usingizi. Kumbukumbu mbaya zitamfuatilia muuaji mchana na usiku, huku ukajihisi hatia moyoni mwake.
2. Hofu, wasiwasi au kuteseka moyoni.
3. Wauaji hupata "depression" ambayo hupelekea kutamani kujiua na hata kuishia kujiua kabisa
4. Kujitenga na Mungu
Mwanzo 4:10-11
Sauti ya damu ya ndugu yako inanena kutoka katika ardhi. Dhambi inamtenganisha muuaji na Mungu wake kwa Imani yoyote Ile aliyokuwa nayo.
5. Laana ya damu inamuandama na kizazi chake chote
Methali 28:17
Mtu aliyezongwa na hatia ya damu ya mtu, atakimbilia shimoni; mtu asimshike.

Kwa kawaida muuaji huwa anapata hasira za mara kwa mara kutokana kuandamwa na mawazo ya hatia ya mauaji. Kuuwa hakutatui tatizo badala yake inamletea muuaji matatizo zaidi.
FACT!
 
Back
Top Bottom