RIWAYA: Mtumwa wa Ngono

RIWAYA: Mtumwa wa Ngono

SLAVE SEX(mtumwa wa ngono)……(15)
MTUNZI….EMMANUEL F. KWAY
Contact…+255718 862176
AGE….(18+)
ILIPOISHIA.
Hayo ndiyo maneno aliyoongea Pedeshee Kway
huku kioo cha gari kikipanda juu,hakutania alitoa
gari kwa kasi na kumuacha Gloria akiwa hospitalini
asijue wapi aelekee kwa sababu alikuwa bado
mgeni wa jiji la Afrika kusini.
SONGA NAYO.
Jambo lililokuwa limemtokea Gloria bado
hakuliamini kama lilikuwa ndoto au kweli,hata siku
moja hakuamini kuwa Pedeshee Kway angemgeuka
kiasi hicho na kumuacha kwasababu ya mimba
aliyokuwa nayo,ghafla akajiangalia tumboni na
kuchukizwa na mtoto aliyembeba,alimuona ndiye
aliyetia dosari katika maisha yake ya raha
mustarehe.Alitamani kitu kinachotokea kisiwe cha
ukweli bali ndoto ili ashtuke.Ni kweli alilishuhudia
Landcruiser V8 linatoka nje ya geti likikunja kona
na kutokomea, hapo ndipo aliposhtuka kama mtu
aliyetoka usingizini,aliweka mikono yake kichwani
na kujikuta akilengwa na machozi hofu
ilimtanda,hapo ndipo picha ya mume wake Nickson
ikamjia kichwani na kujiona jinsi gani alivyokuwa
mwanamke mpumbavu.
Gloria alijutia na kutamani siku zirudi nyuma lakini
haikuwezekana alikuwa ameshachelewa, alitamani
arudi nyumbani haraka ili akamuombe msamaha
Nickson ili warudiane ingawa hakuamini kama
angesamehewa kutokana na unyama aliomfanyia
wa kumuweka kituo cha polisi.
“Lazima nimuombe msamaha Nickson wangu”
Aliwaza Gloria huku akiwa amekaa chini.Wakati
tukio zima linatokea la kuachwa na Pedeshee Kway
na gari kuna Mzee Mmoja aliliona na alitaka kujua
nini hatma yake.Alisogea karibu na Gloria kwa
huruma na kumshika bega la kulia.
“Hallo”
Mzee huyo Mweusi tii alimsalimia Gloria,huku
akimtizama usoni.
“Sorry for what happened”(samahani kwa
yaliyotokea)
Mzee huyo alisema huku akizidi kumsogelea Gloria
karibu nayeye akajikuta amechuchumaa.
“Am Mr.Zuma”
Alijitambulisha Mzee huyo lakini Gloria hakusema
lolote.
“Can you speak zulu?so that you tell me”(Unaweza
kuongea kizulu ili uniambie)
“No tafadhali go”
Gloria akachanganya kiswahili na kuongea kwa
hasira na kwa wakati huo hakutaka kuongea na
mtu yoyote Yule,alichokuwa anafikiria kichwani
kwake ni kuitoa mimba ya mtoto huyo,aliamini
kuwa ndiye aliyemzibia sterehe yake aliyoonjeshwa
kidogo.
Ghafla akasimama na kurejea hospitalini ili
kuzungumza na daktari juu ya kutoa mimba,kwa
kiingereza kibovu alichokua anazungumza
kilieleweka.
“Why are you aborting?”
Daktari alimuuliza tena swali Gloria kwa mara
nyingine,akitaka kujua ni kwanini anataka kuitoa
mimba kubwa kama hiyo.
“Because me mmhhh, I hate children is me and
Father of the the children don’t like me,okay”
Gloria alizidi kuunga unga na kuvuta maneno ya
kiingereza akijaribu kuyaunga na gundi ili
afanikiwe.Lakini daktari alimuelewa japo kwa shida.
“Are you sure?” (Una uhakika)
“Yes,Yes my doctor”
Gloria akajibu kwa ujasiri kwa bahati nzuri alikuwa
anapochi na ndani yake alikuwa na Dollar elfu
mbili, hiyo aliamini ingetosha kabisa kuuwa kiumbe
chake kilichokuwa tumboni kilichomsababishia
asitishiwe huduma.
Dokta akatoka nje baadaye alirudi na vifaa vya
kazi.Jambo la kutoa mimba katika nchi ya Afrika
Kusini lilipigwa vita na jambo hilo lilikuwa ni kosa
la jinai,lakini kutokana na tamaa ya pesa Dokta
Vunga akajikuta amepatwa na tamaa.
Dola elfu moja ikamfanya atake kuuwa mtoto
aliyefikisha miezi mitano tumboni.Ghafla baada ya
Gloria kupanda kitandani akaingia mwanaume
mweusi.
“Vipi bwana mbona unaingia bila utaratibu?,hapa
sio chooni”
Dokta Vunga akauliza kwa Jazba.Gloria akageuka
na kuona sura ya mzee aliyekutana naye muda
mfupi uliopita.
“Naomba jambo unalotaka kulifanya uliache mara
moja,.kwa sababu nitakushtaki sasa hivi”
“Jambo gani?”
“Unajifanya hujui,unataka kumfanyia nini huyu
Mwanamke aliyelala hapo kitandani?”
“Nampima tu Malaria naomba utoke nje”
Mabishano hayo yalifanyika kwa lugha ya kizulu.
“Unampima Malaria na mikasi?sasa subiri nipige
simu polisi ili….”
“Ngoja kwanza basi”
Dokta Vunga aliogopa mno kusikia habari za
polisi,alihisi kinyesi kinambana, Mwanamke
aliyelala juu ya kitanda ameipanua miguu yake
alikuwa mbioni kwenda kufanya kitendo cha kuuwa
mtoto tumboni.
Ilibidi aghairi ghafla baada ya kusikia neno
polisi,akakumbuka ndugu zake na wadogo zake
waliokuwa wakimtegemea na aliamini kitendo cha
kushtakiwa kingemfanya afungwe kama sio
kunyongwa.
“Nachotaka mimi huyo binti umuache kama alivyo”
“Hilo?hilo ondoa shaka”
Dokta Vunga akabadilisha msimamo
wake.Mr.Zuma alijikuta anaingiwa na huruma na
kutaka kujua nini chanzo cha Mwanamke huyo
kutaka kuuwa kiumbe kisicho na hatia,akamshawi
shi watoke hospitali ili watafute sehemu
waongee.Gloria kwa shingo upande akainuka na
wote wakatoka nje mpaka kwenye gari la kifahari
Lamborghin,lilikuwa gari la kisasa Mr.Zuma
akawasha gari hilo na kuligeuza huku akianza
kumzoea Gloria taratibu.
“Tell me,why are you crying?”(Nambie kwanini
unalia)
Mr.Zuma akamuuliza Gloria ambaye badala ya
kujibu akazidi kulia zaidi,hii ikamfanya Mr.Zuma
azidi kutaka kujua kiundani,picha ya mwanaume
aliyekuwa anamfokea na kuondoka na Landcruiser
v8 ikamjia kichwani.
“Who was that Man,is he your husband?”(Yule
mwanaume ni nani,ni mumeo)
Mr.Zuma alizidi kuuliza wakiwa wanazidi kusonga
mbele.wakapita barabara ya Kuelekea Stellenbosch
wakanyoosha wakafika mpaka paar,gari lilizidi
kutembea kwa kasi, urefu wa kilomita nyingi
mpaka wakafika Hermanus,wakaacha lami na
kuingia kwenye barabara iliyochongwa vizuri ikiwa
na majani mazuri pembeni yake,urefu wa mita mia
mbili arobaini gari la kifahari likasimama nje ya
geti kubwa.
Mr.Zuma akatoa Rimoti na kubonyeza, lango
likajifungua lenyewe.Gloria alistaajabu mno,hasa
baada ya kuona mbele yake jumba kubwa kupita
kiasi, nje kulisheheni magari tofauti ya
kifahari,Kichwani kwake alikuwa ana vitu vingi sana
anavifikiria,vitu alivyokuwa anaviona
vilimchanganya akili yake akabaki na kazi ya
kugeuza shingo yake,kwa mbali kidogo aliona kuna
uwanja mkubwa kiasi huku ndani yake wakiwemo
Farasi weupe wanatembea huku na kule.
“Welcome home”(Karibu nyumbani)
Mr.Zuma alizungumza na kushuka garini
akamfungulia Gloria mlango wote wakashuka na
kutembea,namna alivyopokelewa Mr.Zuma alizidi
kustaajabu ghafla akajihisi yupo peponi,lilikuwa ni
jumba kubwa la kisasa.Wakaingia wote ndani
wakakaribishwa kwenye kiti na wafanyakazi wa
ndani baada ya muda mfupi Juisi ililetwa.Mr.Zuma
akawa ana kazi ya kumsaili Gloria akimuhoji
maswali mawili matatu,alifurahi mno alivyojua ni
mtanzania.
“Bongo,nilishawahi ishi kule ujue,nimekaa Tabata
pale jijini Dar es salaam,Arusha sakina nimekaa
sana, Moshi Marangu,nikaendaga mpaka mulima
Kilimanjaro,nikapanda mpaka juu Kibo na
Mawenzi”
Mr.Zuma alizungumza Kiswahili, Gloria
akashangazwa.Na wakaanza kuongea.
“Hukuniambia ilikuwaje,pale hospitalini,Yule jamaa
ni nani? Mumeo?”
“Ndio,ni mume wangu kaikataa hii mimba na
isingekuwa wewe ningesha muuwa huyu mtoto”
Gloria hakuona haya yoyote, aliyoongea hayakuwa
na ukweli hata kidogo.
“Usijali kabisa,mimi nitakusaidia”
“Sawa,nitashukuru”
Hapo ndipo mazoea yakawa yameanza.Uzuri wa
Gloria ulizidi maradufu siku hadi siku,kila alipopita
mbele yake Mr.Zuma alibaki akishindwa kuelewa ni
kitu gani akifanye,katika maisha yake ni kweli
hakuwahi kuona mwanamke mzuri kama Gloria.
Uzuri wa Gloria uliunyanyasa Moyo wa
Mr.Zuma.Pamoja na kusaidiwa na Mr.Zuma na
kupewa msaada lakini hakuacha kumkumbuka
Mume wake Nickson na alitamani kurudi Tanzania
dakika hiyo hiyo ili akamuombe msamaha mume
wake,alijiona mkosaji na alistaili moto wa
Sheteni.Siku hiyo usiku Mr.Zuma alirudi akiwa
amelewa chakali, akangia chumbani kwa Gloria na
kuufungua mlango akamkuta amelala.
Gloria akashtuka kutoka usingizini na kuwasha
switch ya kitandani.
“Vipi?”
“Viiiipi Nini,tulia ivyo ivyoooo”
Mr.Zuma alivua nguo zake na kumsogelea Gloria
karibu akimlazimisha kufanya naye ngono huku
akimuhaidi angempa pesa nyingi endapo atakubali
tendo hilo litokee.
“kiasi gani?”
Gloria aliuliza kwa sauti ya puani huku
akirembua,udenda ulimtoka.
“Dollar elfu kumi”
“Ni ndogo mbona”
Gloria akatingisha kiberiti.
“Dollar laki tano”
Moyo wa Gloria ukapiga paa! Dola laki tano
hazikuwa ndogo kwake japokuwa hakuelewa ni
kiasi gani cha pesa endapo akizibadilisha, bila
kuuliza akajikuta anamsogelea Mr.Zuma na kuutoa
ulimi wake nje,ndimi zao zikagusana wakaanza
kulana denda.
BILA KUSAHAU KWAMBA HADITHI HII INAPATIKANA
YOTE WATSAP NA INBOX KWA TSHS 3000/- KWA
MWEZI.mawasiliano namba 0718 862176.
(BADO SHINDANO LINAENDELEA LA STORY ZA
KWAY SHINDA PESA KWA MAELEZO ZAIDI INGIA
KWENYE UKURASA WA STORY ZA KWAY ILI UPATE
MAELEKEZO)
Sasa unaweza kusoma hadithi za mtunzi kway
insta@storyzakway
ITAENDELEA.
 
SLAVE SEX(mtumwa wa ngono)………(16)
MTUNZI…..EMMANUEL F. KWAY
Contact….+255718 862176
AGE….(18+)
ILIPOISHIA.
Moyo wa Gloria ukapiga paa! Dola elfu tano
hazikuwa ndogo kwake japokuwa hakuelewa ni
kiasi cha pesa akizibadilisha, bila kuuliza akajikuta
anamsogelea Mr.Zuma na kuutoa ulimi wake
nje,ndimi zao zikagusana wakaanza kulana denda.
SONGA NAYO.
Dolla laki tano ilikuwa imehaidiwa kutolewa endapo
tu Gloria atakubali kulala na Mr.Zuma,zilikuwa ni
pesa nyingi mno kwake, kwa hesabu za haraka
haraka ilikuwa sio chini ya milioni sabini na tano
za kitanzania,kwake kupanua miguu na kufanya
ngono ilikuwa kazi ndogo,akavua nguo zake huku
akiendelea kupigana mabusu ya ndimi na Mr.Zuma
aliyekuwa teyari yupo sayari nyingine, haelewi ni
kitu gani kinaendelea ulimwenguni,damu yake
ilimwenda mbio akashusha suruali yake ya Jinsi
kama umeme na kuipanua miguu ya Gloria,
hakujali kumuandaa, kwake ilikuwa ni mwendo wa
kijeshi.
Haraka akaingiza karoti yake na kuanza kufanya
tendo baya la kuzini.
Pesa ikawa imenunua penzi la Gloria,Mpaka
Mr.Zuma anamaliza mzunguko wake wa kwanza
hakuamini, alitamani aanze tena upya, lakini
alikuwa yupo hoi bin taaban!hakujali kuwa
anafanya ngono na mwanamke aliyekuwa mjamzito
ili mradi amekidhi haja zake, hayo hayakumuhusu
na halikuwa swala lake,huo ndio ukawa mchezo
wake kila akirudi usiku, alihitaji penzi kutoka kwa
Gloria na akapewa mara moja kwa mihadi ya
kumpatia pesa nyingi.
Gloria akawa mtumwa wa Ngono!Lakini mbali na
hapo alipakumbuka nyumbani Tanzania na mara
kwa mara alimgusia Mr.Zuma juu ya yeye kurejea
Tanzania.
“Usijali wiki ijayo utaenda,nitakufanyia mipango ya
pasipoti mpya ili urudi Tanzania”
Alisema Mr.Zuma siku hiyo asubuhi wakiwa wote
kitandani,tumbo la Gloria lilishaanza kuwa kubwa
teyari na likatokeza mbele, akawa kama wamama
wengine wapatapo ujauzito.
“Nitafurahi sana,na nikijifungua tu,nakuhakikishia
nitakupa mapenzi ambayo hukuwahi kupata katika
maisha yako yote,utajuta kunifahamu nakwambia”
Gloria alijitapa mbele ya Bwana Zuma.
“Nitafurahi kusikia ivyo,mimi nakupenda kweli
ujue,ujifungue tu mapema ili nijilie vyangu,wao
wanasema vya nini, sisi tunajiuliza tutavipata lini”
kuishi kwa Zuma muda mwingi Tanzania
kulimfanya ajue mipasho ya kibongo!
“Hee,kumbe nawewe una maneno!”
“Ukisusa sisi twala,na ukijifungua tu uniambie ili
nije huko kukuona kichuna wangu”
“Hilo ondoa shaka”
“Nakupenda Gloria”
“Mimi pia Zuma”
Kila mtu alimtamkia maneno matamu
mwenzake,Zuma alimpenda kweli Gloria na alitaka
aishi naye hata ikiwezekana amlee mtoto atakaye
zaa.Penzi la mchezo mchezo likawa limezaa mizizi
ndani ya moyo wa Mr.Zuma, akakolea na
mwanamke huyu mzuri wa kichaga, na alielewa
kuwa yupo kwenye matatizo ya kuachwa na Mume
wake,na hivyo ndivyo alivyoambiwa na
Gloria,kumbe ulikuwa ni uwongo mtupu!
Hatimaye wiki moja ikakatika Mr.Zuma akawa
tayari amemfanyia mipango ya pasipoti na
kumkatia Tiketi inayoondoka siku ya Jumamosi
saa kumi ya Jioni.Gloria alionekana ni mtu
mwenye uzuni siku hiyo ya Alhamisi
alivyokabidhiwa hati ya kusafiria vikiambatanishwa
na tiketi ya ndege.
“Mbona umekuwa mnyonge kiasi hicho mpenzi
wangu?”
Mr.Zuma akajitosa kuuliza swali.
“Nimekuzoea sana,sijui nitaishi vipi bila ya wewe”
“Mimi ni wako mbona,ondoa shaka na nipo tayari
hata kukuoa”
“Kweli?”
“Ndio”
“Siamini kwa kweli”
“Niamini nayo sema,kwanini usiniamini au
unanichukuliaje,unanichukulia mimi yoyoo sana
tatizo lako”
“Sio ivyo Baby”
“Kumbe nini sasa?amini ninayo kwambia
nakupenda kweli,na ukijifungua tu mimi nitaarifu ili
nije Tanzania”
“Sawa nitafanya ivyo”
Gloria alishamsahau tena Nickson, raha alizokuwa
akipewa kama malkia ziliweza kumbadili akili yake,
akasahau tayari maumivu yote yaliyompata katika
maisha yake,alimuona Mr.Zuma ndiye kama
Mungu wake wa pili.
“Kumbe kuna watu wana uwezo kiasi hiki hapa
duniani,Kway, Kwaaay umeula wa chuya,ulidhani
umenikomoa,shenzi wewe”
Hayo yalimiminika kichwani Kwa Gloria akiwa
anatizama Jumba kubwa la kifahari,kila
alichokitizama kilikuwa ni kitu cha Thamani
kwake.Siku hiyo Jioni ilipofika Mr.Zuma
akamchukua wakaenda kushangaa jiji la
Capetown,jiji liilikuwa zuri na ndiyo likamfanya
Gloria apagawe zaidi.Mr.Zuma alimpitisha Gloria
kwenye ma’casino’ ya wacheza uchi.
Huko alikutanishwa na matajiri wakubwa wa nchi
hiyo yaani ‘mataikun’ wa mji.Usiku wa siku hiyo
Gloria akapewa sigara avute kidogo.
“Mimi siwezi sijawahi kuvuta sigara katika maisha
yangu, naogopa sana”
“Vuta watakuona mshamba,weka mdomoni kama
hivi alafu toa moshi nje”
Gloria akapewa maelekezo akajaribu, kwa mara ya
kwanza akakohoa mfululizo baada ya kuvuta Moshi
mwingi ambao ulimpalia,akaambiwa ajaribu tena
na tena, mwishowe akaweza. nayeye akawa
miongoni mwa gari Moshi!
Sigara na pombe zikanyweka siku hiyo,Gloria
hakujali kuwa ilikuwa ni hatari kwa kiumbe
alichokuwa nacho tumboni,yeye aliona ni sawa
kwake,ilimradi tu Mr.Zuma afurahi,baada ya kulewa
wote walibebana mpaka ndani ya gari aina ya
Escelard lililokuwa la Mr.Zuma,wakaingia na safari
ya kurudi nyumbani ikaanza,ulikuwa ni usiku
mzito,hakuna walichokuwa wakifanya ndani ya gari
zaidi ya kunyonyana ndimi zao na kufanya
matendo machafu,mpaka wanafika wakamalizia
haja zao kitandani kisha kulala.
****
Ni kweli Gloria alitakiwa kusafiri siku ya Jumamosi
na ndiyo maana alikuwa teyari ameshawasili
uwanja mkubwa wa ndege akiwa kushoto na
Mr.Zuma,Gloria alionekana kukosa raha ya maisha.
“Bila kusahau ukijifungua tu naomba tuwasiliane”
“Sawa mpenzi”
Waliagana mara ya mwisho mwisho huku
wakipigana mabusu ya mdomoni,Gloria alikuwa
teyari ametengeneza pesa ya kutosha,
alishafunguliwa akaunti ya bank na Mr.Zuma na
ndipo alipoziweka pesa zake humo.
***
“Nenda wewe ushapigwa nyuma,hauna uwanauwe
wowote ule, sitaki kuamini kuwa nafanya kazi na
mabwabwa,hiyo kazi ya kupakuliwa umeanza lini?
Eti..”
Bosi Magugu alikuwa akiongea maneno ya shombo
na yasiyo faa mbele ya Nickson tena kwa sauti
kubwa mbele ya wafanyakazi wengine.
Nickson aliumia moyo, swala la yeye kufanyiwa
kitendo kibaya cha kuingiliwa kimwili hakuelewa
bosi wake alilijua vipi,ukizingatia hakupenda iwe
ivyo.Alichukia zaidi hasa bosi wake alivyokuwa
akimuita bonge la shoga.
“Nakuuliza wewe bonge la shoga anti
Nickson,umefikia wapi na ile kesi?”
“Tayari bosi,imeshapelekwa mahakamani na
anaisimamia Angelina Masawe”
“wewe ilikushinda kwani?”
“Hapana”
“Kaza sauti shoga,mimi usinilegezee sauti mimi
situmiagi mlango wa nyuma”
Nickson alijikaza,japokuwa maneno hayo yalipita
kwenye pina ya masikio yake na kuuchoma moyo
wake, siku zote alimlaumu Gloria kwa mambo
yote,licha ya hayo alimuachia Mungu, kwake
alihesabia kama changamoto ambazo zinakuja na
kuondoka.
“Haikunishinda bosi,bali alisema nimuachie
tukakubaliana ndiyo ikawa vile”
“Sawa unaweza ukaenda,lakini kama ukijisikia
namna gani uje basi nikupe huduma”
Hilo ndilo neno la kejeli alilosema Bosi wake
Magugu.
Nickson alikuwa mpole alikuwa hana tabia za
kumjibu mtu vibaya hata kama ungemtukana
vipi,watu walimshangaa na kumshauri aache kazi
lakini yeye alikataa,maisha hayo yakaendelea kama
kawaida, Nickson akiendelea kudhalilishwa kila
kukicha,lakini hata siku moja hakufanya malipizo.
Siku hiyo ya Jumamosi hakukuwa na kazi ivyo
walihaidiana na rafiki yake kipenzi Tito watoke
kidogo waweze kuongea mambo mawili matatu.
“Oyaa we Nickson”
Tito aliita baada ya kufika nje mlangoni kwa
Nickson, asubuhi.
“Tito”
Nickson aliitikia akiwa ndani.
“Vipi umelala?”
“Nilale wapi rafiki yangu karibu ndani basi,unywe
hata chai”
Aliongea baada ya kufungua mlango.
“Mimi sio mkaaji jiandae basi,twenzetu kwa mfojo
hapo tukapate supu kidogo na mbili tatu baridi”
“Poa,ingia basi ndani,ukiwa unanisubiri hapa nioge
chap,twenzetu”
“Poa usiwaze”
Nickson akaingia ndani na kujimwagia
maji,alivyotoka alikuwa amevaa tshirt ya kaki na
suruali nyeusi,wakaingia ndani ya gari la Tito na
safari ya kwenda kwenye baa ya mfojo aliyekuwa
maarufu kwa kuchoma nyama ikaanza,watu
walitoka Mbagala,Kimara hata Yombo ili kuja kwa
mfojo mchoma nyama.
Japokuwa ilikuwa asubuhi lakini palichanganya
watu walikuwa wamejazana madirishani wakitaka
supu asubuhi.
“Nickson nisubiri hapa,nikaagize supu”
“Poa mimi utanikuta”
NUSU SAA BAADAYE kila mtu alikuwa na
mchemsho wa supu na nyama choma.Wakaagiza
pombe na kuanza kushushia.
“wewe dada embu njoo na kisichana kimoja”
Haraka muhudumu akaleta kichupa kidogo cha
konyagi.
“Tito,leo umepania”
“Leo ni kugambeka tu”
“Wacha bwana”
“Nataka leo tulewe mpaka basi,kwani kesho kuna
kazi?”
“Hapana”
“Kumbe nini?”
“Kanisani kesho”
“Kwenda zako,hakuna cha kanisani hapa,tunarudi
asubuhi”
Pombe zililetwa ikawa kata mti panda mti na kweli
pombe zilianza kupanda kichwani.
“Nicki eeeeeeee”
“Vipi Jembeeeee”
“Embu niaaambiee tatizo ni kiitu gani,mbona Bosi
anakuleteaa gozigoziii kiasi hicho,samahani lakiniiii
kama nitakuwa nakuudhiii,kama hutojali,just tell
me my friend!.au nakoseaaa? kama nakosea
Mungu anirehemu aaah anisamehee,Wewe ni rafiki
yangu mkubwaaa saaaana,Embu niambie ukweli
wa moyonii,ili nijue nikushauri vipi,sijalewa hapa
lakini nipo kamili gado”
Tito aliongea kwa sauti ya kilevi pombe zikiwa
tayari kichwani, hata kwa Nickson habari ilikuwa
hiyo hiyo nayeye amelewa,walikuwa wamesha
kunywa kiasi kikubwa cha pombe kali
walizochanganya na bia.Nickson akamuangalia
rafiki yake kwa kitambo,lakini badala ya kuadithia
Nickson alianza kulia machozi.
“Tii….to ina…niuma sa……naaaaaaaa!”
BILA KUSAHAU KWAMBA HADITHI HII INAPATIKANA
YOTE WATSAP NA INBOX TSHS 3000/- KWA
MWEZI .mawasiliano namba +255718 862176.
(SHARE HADITHI HII KWA WATU HAMSINI NA
UPATE OFA YA KUINGIA KWENYE MAGROUP
YANGU YA HADITHI FREE OF CHARGE)
Sasa unaweza kusoma hadithi za mtunzi kway
insta@storyzakway
ITAENDELEA.
 
SLAVE SEX(mtumwa wa ngono)……(17)
MTUNZI….EMMANUEL F. KWAY
Contact….+255718 862176
AGE….(18+)
ILIPOISHIA.
walikuwa wamesha kunywa kiasi kikubwa cha
pombe kali walizochanganya na bia.Nickson
akamuangalia rafiki yake kwa kitambo,lakini badala
ya kuadithia Nickson alianza kulia machozi.
“Tii….to ina…niuma sa……naaaaaaaa!”
SONGA NAYO.
Yalikuwa ni maumivu yasiyoweza kuelezeka
kiwepesi,Moyo wake ukawa kama umechomwa na
mkuki wenye moto,akamkumbuka Gloria
alivyokuwa amebeba mkungu wa ndizi huko
Mashambani kijijini Mwika,akamtizama Tito na
kufuta machozi yake akitumia kiganja
chake,akavuta pumzi na kuanza kumuhadithia kila
kitu tangu alivyoenda kijijini na kurudi na
Gloria,kila kitu alikiweka bayana.
Historia yake ilitumia kama dakika arobaini nzima
sababu ya kulia kwake.Tito alijaribu kumbembeleza
swaiba wake asilie machozi.
“Em…bu nishauri..kitu gani nikifanye rafiki yangu?”
Nickson aliuliza baada ya kumaliza kuhadithia
huku akibubujikwa na machozi.Tito alimuonea
huruma mpaka machozi yakamlenga, akavuta
picha kama ingekuwa yeye angefanya nini,simulizi
ya Nickson ili mpandisha hasira akahema juu kifua
chake kikawa kinapanda na kushuka.
“Bosi anaishiiii wapi kwani?Anaishi waaaapi huyo
Mamake zakeeeeeee,Nickson niambie nikaue
haiwezekani akutese mimiii nipo haii blood fool”
Tito huku akijipiga piga kifua chake alisema,
alivyotaka kusimama Nickson akamshika mkono
na kumrudisha chini, kitini.
“Kaaa jembee,kaaa ndiyo maana sikutaka
kukwambia nilijua tu utaharibu,funika kombe
mwanaharamu apite,naomba usijaribu kufanya
chochote”
“Huyo Malaya unampenda kwanza?”
“Malaya gani?”
“Gloria”
“Gloria sio Malaya”
“wewe fala nini?kumbe nani,Gloria Malayaaa
tu,hana maana piga chini huyo demu asikupe
stress”
“Kumbuka ni mke wangu,nimekula nae kiapoo
kanisanii”
“Bogasi wewe,Eti mke wangu,ona alichokufanyia
mpaka akuuwe sio?,wewe mshkaji wangu isitoshe
bado nataka uishi bado kijana mzuri,wanawake
kibao wapo,leo nataka twende sehemu ukajionee
mwenyewe”
“Acha tu Tito”
“Psiiii psiiiiii wewe muhuduumuuu,wewe
muhudumuuuuuuuuuu”
Tito akapaza sauti na muhudumu akafika.
“Mbona nakuita muda wotee huo hauji,ulikuwa
unashikwa shikwaaa au?”
“Hapana sikusikia,Niwaongeze vinywaji?”
“Leta kreti la bia moja hapaaaaaa,uliweke hapa
pembeni”
“Bia gani na gani?”
“Kama unavyotuona nusu kwa nusu,fanya upesi
fanya upesi”
Sekunde tano hazikupita Kreti la bia likawekwa
kandokando yao,ni kweli siku hiyo walikunywa
kupita kiasi,mpaka baadhi ya wateja
wakawashangaa, mpaka inafika saa moja jioni
walikuwa bwiii!,tilalila.
“Sasa hapaaaaa,Embu tuwashe gari twende
Mandela Club mabibo mwisho twenzeetu
babakeee”
Tito alisimama huku akiyumba huku na kule, hatua
moja mbele kumi nyuma,akamuinua Nickson
wakaingia ndani ya gari.
Tito akaingia kilevi safari ya kwenda mabibo
kuruka majoka ikaanza.Saa mbili na dakika tano
wakawa wamefika mabibo mwisho,wakapaki gari
pembezoni mwa grocery,hapo wakashuka.
“Sasa hapaaa Nickson subiriii hapaaaaaa,nimpi
gieeee Simu mchepuko wangu Neema,huku ndiyo
najificha na na na na sitaki aje mwenyewe aje na
rafiki yake,mzuri huyo wapoo hapo juu mabibo
hostel,ukimwangalia vizuri kama Wema
sepetu,mtoto mweeupeeee ana chooo hiko, huyo
ninaye taka kukupa sasa”
Tito aliongea huku akiyumba kilevi na mikono yake
akaiweka nyuma kumaanisha kuwa msichana
atakayekuja na Neema ana makalio
makubwa.Wakatafuta kiti wakakaa.
“Titooo,mimi siongezi haapa nilipo nipo Topu
topuuuuu yaaani,lakini ninampenda Gloria”
“Acha ufala,usiniletee za kuleta, leo lazima
uondoke na mzigooooo haiwezekani”
Tito alimshawishi wakaendelea na pombe huku
akiendelea kupiga simu.Namna alivyokuwa
anaongea na simu kana kwamba alikuwa anaongea
na mtu aliyekuwa amesimama naye mita mia
tano,aliongea kwa sauti ya juu.
“wewe Neema,nimekwambia tuupoo hapa kaaribu
na Mandela Club,kwenye baa ya Nzota,pale kwa
siku zote,alafuuu nisikilize sasa kwa makini uje na
Yule rafiki yako Pendoo…ndio Pendo Jonas,nipo na
Nickson Shayoooo,.Ndio atalala uje ujeee fanya
upesi,chukua hata boda boda mpenzi
wangu,nakupendaaaa mwaaa mwaaaaa”
Tito akamaliza kuongea na kurudi kwenye kiti
ambapo walizidi kupiga stori na nyama choma ya
mbuzi ikaagizwa,nusu saa baadaye Pembeni yake
walisimama Neema na msichana mwingine
mrembo kupita kiasi,urefu wa msichana huyo na
weupe ulimfanya ang’ae,macho madogo kama ya
kichina yalibeba mashavu makubwa kiasi, midomo
yake ilikuwa laini na mipana na ilikuwa imepakwa
rangi nyekundu.Nickson alimkazia macho akizidi
kumkagua kwa juu na kila idara.
“Ah,Wema sepetuuu!”
Tito akaita baada ya kugeuka, ni kweli msichana
huyu mrembo alifanana na mcheza filamu wa
kibongo Wema sepetu, hata miili yao, usingebisha
ungeambiwa kuwa ni ndugu yake,chuo cha UDSM
alifahamika kwa jina hilo.
“Kaeni sasa,karibuniiiiiii Neeeema mpenzi”
Bila aibu yoyote Tito alimsogelea Neema na
kuanza kumla denda hapo hapo, Pendo na Nickson
wakabaki kuangaliana.
“Sasaaa Nickson sijawahi kukutambuliiiisha my
friend,huyu unayemuonaaa hapa ndiye
anayenipunguzia stress,wife akizingua
kidogoooo,wala siongei nakuja kwa Neema wangu
mambo yanakwishaaaaaa,wala siwaziii sijuiii
nini….wife yupooo aaaaaah yanini,maishaaa
yenyewe mafupi haya,kuna msemo unasema
usinipe stress am still young!”
Mazungumzo yao hayakuwa mengine zaidi ya Tito
kumpigia debe Pendo, alikuwa kuwadi siku
hiyo,kila alichoongea Tito Neema alitia neno lake.
“Pendo au Wema sepetu what ever,huyuuuu rafiki
yangu,he is my buddy,he is my friend.Nakwambia
yaani ukimuoneaa huyu mimi nauaa mtu,sasa
pendoo embu muongee vizuriiii basi mama”
“Kweli shoga angu,chakalika,leo wawili wawili”
Neema akamuunga mkono bwana ake!
Ilivyofika saa tano usiku walichukuana na kuvuka
barabara mpaka upande wa pili, hapo wakalipia na
kuingia Mandela club.
Mziki ulikuwa unatumbuizwa, siku hiyo alikuwa Dj
Maarufu aliyeitwa ‘Dj Choka’ na kufanya watu
wajae ukumbini,wasanii mbali mbali kama
Professor Jay na A.Y walikuwepo pia ndani ya club
hiyo,watu walirindima wakiserebuka ikawa
mshikemshike.Wasichana warembo walikuwepo,hii
ilimchanganya akili Nickson akamuona Gloria
hakuna kitu kabisa.
“Kumbe kuna watoto wazuuuuri namna hii kuliko
hata Gloriaaa,ebwana weeee duniani hapa kuna
warembo”
Nickson aliwaza huku akiingia taratibu ,Pendo
Jonas au wema Sepetu kama walivyozoea kumuita
nayeye alikuwa nyuma yake wanaongozana mpaka
kaunta, wakaagiza pombe kali.
Disco lilichanganya wakati wa kuingia kati ukafika
Pendo akamshika mkono Nickson,alishaambiwa
kuwa Nickson ana pesa, hivyo kwake alikuwa
amepata buzi la kumchuna!
Walifika kati na kuanza kucheza mziki wa pamoja
jinsi walivyokuwa wakicheza walikuwa ni watu
kama waliokuwa wamefahamiana masaa sabini na
mbili yaliyopita, kumbe walikutana siku hiyo
hiyo.Kwa makusudi Pendo alikuwa akikatikia
mwiko wa Nickson na akawa anapitisha mkono
wake na kuushika.Nickson taratibu akaanza
kupandwa na midadi.Hilo pendo aliligundua.
“Nicksooon”
Pendo aliita akiwa sikioni mwa Nickson.
“Niambie chauremboooo,unajua sana
kucheza,wewe ni mjamaica nini?”
Nickson akaweka utani,pendo akacheka meno yake
yaliyojipanga na meupe yakaonekana uzuri wake
ukachanua.
“Tunaweza tukaenda nje kidogoo”
“Kufanya nini tena?”
“Nina mazungumzo nawewe Nickson”
“Sasa si uniambie hapahapa”
“Hapana sio hapa,kuna kelele”
“Sawa,tweenzetu”
Wote wakavutana, Pendo akapitisha mkono wake
kiunoni mwa Nickson wakatoka nje,kitendo cha
kufika gizani kama umeme Nickson akavutwa
mpaka mdomoni mwa pendo,wakaanza kulana
denda,kutokana na Pombe nyingi alizokunywa
Nickson hakuweza kufanya lolote alitoa
ushirikiano,pendo akazidi kucheza na ndimi ya
Nickson akapitisha mkono wake mpaka kwenye
zipu na kutoa tango la Nickson lililokuwa teyari
limekakamaa.Hisia zake zilikuwa mbali, ghafla
akaiona sura ya Gloria mbele yake.
“Nakupenda,nakupenda sana kwaniniiii ulinifanyia
ivyo lakiniiiiiiii Mke wangu?”
Nickson aliongea huku akizidi kupata raha za
ajabu,akidhani pendo ndiyo Gloria.
“Mimi,nakupenda pia Nickson”
“Tafadhali usiniache”
Pendo akapiga magoti na kuliweka Tango la
Nickson mdomoni huku akilinyonya kama
koni,macho ya Nickson yakabadilika rangi,nayeye
hakufanya makosa akapitisha mkono wake juu ya
maziwa ya Pendo akaanza kuyachezea na
kuyapekecha taratibu sana.
“Oyaaaa Nicksoniiiiiiii,eeeh samahaaaniii jamani”
Tito ndiyo aliyewashtua kutoka katika dimbwi la
raha,Pendo akawa ameona aibu akafunga blauzi
yake haraka na kuangalia chini.
“Vipiii Mzee?”
Nickson akauliza.
“Basi,endeleeni”
“Mimi nirudishe nyumbaniiiii bwana”
“Sio sasa hivi,wewe endelea tu,au mkachukue
room”
“Titooo eeeh nimechooka nirudishe tafadhali”
Nickson akang’ang’ania arudishwe,hapo hakukuwa
na kipingamizi,wakaingia ndani ya gari na safari
ikaanza,wote walikuwa chakali.
Nusu saa baadaye walikuwa wapo Segerea
majumba sita,Nickson akashuka na kuwaaga
wenzake akaingia ndani.
Kitu cha kwanza alivyofungua mlango alishtuka
baada ya kuona taa zimewashwa,akasita kutembea
baada ya kuhisi kama kuna mtu anatokea
chumbani,akawa amejiandaa kwa kukimbia
akidhani wenda ni majambazi.
“Gloriaaaaaaa”
Nickson aliita kwa sauti, alibaki ameganda haamini
mtu aliyemuona mbele yake.
 
Nahisi ningerudi nilikotoka......
 
Mwanamke hana hayaaa kabisa..... Karudi tena kwa Nickson?
 
SLAVE SEX(mtumwa wa ngono)…….(18)
MTUNZI….EMMANUEL F. KWAY
Contact…+255718 862176
ILIPOISHIA.
“Gloriaaaaaaa”
Nickson aliita kwa sauti, alibaki ameganda haamini
mtu aliyemuona mbele yake.
SONGA NAYO.
“Gloria ni wewe kweeliii au naota ndoto jamaniii?
Gloriaaa ni wewe mama ulikuwa wapi mke wangu?
nilibaki mpweke sana,maisha bila wewe siwezi
nimekozea tafadhali usiniache mwenyewe”
Nickson alikuwa akiongea Mwenyewe huku
akimsogelea Gloria na kumkumbatia, lakini yeye
Gloria hakuonesha ushirikiano wa aina yoyote ile
alibaki tu amenyamaza.
“Au itakuwa pombe,naomba unisamehe mimii leo
nimechelewa kurudi,nilikuwa na marafiki
zangu,sikuweza kukaa mwenyewe ndani bila wewe
mke wangu,ndio maaanaaa nikachelewa leo, na ni
leo tu basi”
“Sawa”
Hatimaye Gloria akajibu na kutabasamu,kitu kama
roho ya huruma vikamuingia ndani ya moyo wake,
akamuhurumia Nickson jinsi alivyokuwa akiomba
msamaha huku machozi yakimlenga machoni.
“Za hapa?”
“Hapa nzuri tu"
"mtoto huyo ajambo?”
“Huyu ajambo,za siku nyingi nilikumisi sana”
“Hata mimi”
“Twende basi ndani”
“Sawa lakini nilihangaika kweli kupata
funguo,nisingeangalia kwenye maua leo
usingenikuta hapa”
“Uzuri umefika salama”
Nickson hakutaka kujua ni wapi Mke wake
alipotoka,kitendo cha kurudi kwake kilimfanya awe
na furaha isiyo kifani,tofauti na fikra za Gloria
hakurudi nyumbani kwa mapenzi yake bali
kujifungua mtoto, mimba yake ndiyo iliyomrudisha
nyumbani ajifungue na kuondoka akaendelee kula
maisha na Mr.Zuma huko Afrika kusini,hakutaka
kabisa kubaki Dar es saalam,akiuita mji wa
kimaskini.
“Alafu mbona huku chumbani kuchafu namna hii
Nickson?”
Aliuliza Gloria baada ya kupiga jicho chini.
“Mimi nitawezaje kufanya usafi mke wangu?”
“Nawewe umeshaanza kuwa mchafu bwana
aaaah,unashindwa hata kupangusa pangusa
meza,embu angalia mavumbi pale,angalia nguo
zilivyokuwa shagala bagala,mimi sitaki wachafu”
“Hee Gloria leo unaniambia ivyo?”
“Umezidi bwana,nakwambia ukweli”
Nickson hakutaka kuongea zaidi,kilichomuuma
tena ni jinsi Gloria alivyokuwa ana ongea huku
akiwa anabenua mdomo wake kama wanawake wa
Kiswahili,aliumia zaidi!
Asubuhi kulivyokucha Nickson akawa wa kwanza
kuamka, akaenda jikoni akandaa chai na kuiweka
mezani kwa kuwa ilikuwa siku ya Jumapili, alioga
haraka haraka na kuvaa tayari kwa kwenda
kanisani kuabudu,japokuwa alichukia misa ya pili
lakini hakuwa na jinsi.
“Gloria chai ipo mezani,mimi naenda kanisani,baki
salama”
Alisema Nickson na haraka kutembea mpaka
kwenye gari lake mpaka kanisani kwao usharika wa
K.K.K.T karibu kabisa na anapoishi,nia na
dhumuni lingine la kwenda kanisani lilikuwa ni
kuiombea ndoa yake,ilibidi amuombee Gloria na
alihaidi kuwa endapo misa ikiisha atanyoosha
mpaka ofisini kwa mchungaji na kumueleza shida
zake.
Ni kweli saa nane kasoro ya mchana misa ikawa
imeisha,Nickson akanyoosha mpaka ofisini kwa
mchungaji.
“Bwana asifiwe”
Nickson akasalimia baada ya kufika ofisini.
“Milele Amina”
“Mchungaji, mimi nimekuja hapa nina matatizo
makubwa sana na ndoa yangu,acha nisipoteze
muda,ndoa yangu haijafikisha hata mwaka
nadhani, lakini imekuwa inavisa sana”
Nickson alianza kujielezea, lakini kadri alivyozidi
kuelezea machozi yalikuwa yakimlenga mwishowe
akajikuta analia bila kutegemea,ki ukweli
alimpenda Sana Gloria na Mchungaji aliyekuwa
mbele yake aliamini kuwa ndiye atakuwa msaada
wake na wala sio kitu kingine.
Mchungaji huyo aliyefahamika kwa Jina la
Mchungaji Patrick, alikuwa kimnya anamtizama
muumini wake jinsi anavyolia.
“Kijana”
“Naaam Baba mchungaji”
“Tatizo lako limekwisha kuanzia sasa,hilo pepo
baya sana,tutalikemea katika JINA LA YESU WA
NAZARETH ALIYE HAI,je upo tayari Mr.Nickson
Shayo?”
“Ndio Mchungaji nipo tayari hata sasa hivi”
“Simama tusali”
Nickson akatiii na maombi yakaaanza
maramoja,mchungaji alikemea huku akitaja mara
nyingi ndoa ya Nickson Shayo iweze kufunguliwa.
“BABA WA MAJESHI,BABA WA MAJESHI,NAOMBA
UWEZE KUIFUNGUA NDOA YA NICKSON,BABA
ULISEMA TULIITE JINA LAKO NAWE
UTAITIKA,NAOMBA MAPEPO YASHINDWE KATIKA
JINA YA MWANAO YESU KRISTO,KATIKA JINA LA
YESU FUNGUA NDOA YA NICKSON SHAYO NA
GLORIA,AMEN”
Mchungaji Patrick alimaliza na wote wakafungua
macho,Moyo wa Nickson ulihisi furaha sana
aliamini kuwa Mungu angetenda miujiza na hilo
ndilo aliambiwa na mchungaji kabla ya kutoka
ofisini kwake.
Akaingia kwenye gari lake na kuondoka kurejea
nyumbani kwake,ambapo alimkuta Gloria yupo
kwenye kochi Seblen anaangalia Televisheni,Siku
hiyo wakaongea kama kawaida Gloria hakuonesha
dharau yotote ile,Nickson akaanza kuweka
matumaini juu ya mchungaji Patrick,
akaamini huyo ndiye kila kitu na ni mtumishi wa
Mungu,na alitaka siku moja amuambie Gloria juu
ya kuhudhuria kanisani.
“Gloria”
“Abee”
“Jumapili inayokuja naomba twende kanisani”
“Kanisani?”
“Ndio”
“Kufanya nini?”
“Kumuomba Mungu na pia kumuombea mtoto
wetu awe na afya,si unajua lakini tumuweke
mikononi mwa Mungu baba”
“Mhhhh”
“Mbona umeguna?”
“Hapana,sina shida nitaenda kanisani”
“Nashukuru sana,kesho utaanza kliniki”
Maongezi hayo yalifanyika siku hiyo usiku wakiwa
meza ya chakula,walikula vizuri na kwenda
chumbani,huko hakuna mazungumzo yoyote yale
yaliyoendelea zaidi ya kila mtu kulala.
Ni kweli siku iliyofuata Nickson Shayo akamuandaa
mkewe kwa ajili ya kwenda hospitalini,wakafika na
kupewa dawa,akamrudisha nayeye akaanza safari
ya kwenda kazini,ratiba zikaendelea kama
kawaida,Nickson akarejewa na furaha upya,na
akaanza kunawiri kama kawaida.
“Driii driiiii driiii”
Siku hiyo akiwa ofisini kwake simu yake ya
mkononi ikaita, na namba zilikuwa ngeni.
“Baby?”
Nickson akashtuka na kuitoa simu sikioni ili
kuangalia namba kwa umakini,sauti haikuwa ya
Gloria.
“Wewe nani?”
“Jamani mara hii ushanisahau,mimi pendo”
“Pendo gani?”
“Pendo jamani,rafiki yake Neema,tulikutana
Mandela Club tukacheza mziki wote”
“Niambie Pendo,vipi?”
“Nimekumisi”
“Ahsante”
“Vipi naweza nikakuona leo?”
“Hapana”
“Lini nitakuona?”
“Hautoweza kuniona tena,mimi na wewe biashara
yetu iliishia kule kule,kwahiyo tafadhali”
“Kwanini sasa?”
“Mimi ni mume wa mtu,na siku ile ilitokea tu
bahati mbaya,kwaheri”
Nickson alikata simu,hakutaka mazoea kabisa na
msichana huyo Pendo,.alishaamua kupendana na
Mke wake Gloria na huyo ndiye aliamini kuwa ndio
chaguo lake kutoka kwa Mungu,na ndiyo ivyo hata
mchungaji Patrick humwambia kila siku.
***
“Mke wangu,hizo ndio nguo gani umevaa tena?”
“Si nguo kama nguo zingine,kwani zipoje?”
“Tunaenda kanisani kumbuka”
“Kwani inahusu nini?”
“Ndio uvae kinguo kifupi namna hiyo?”
“Joto bwana”
“Nakuomba,hatukai kanisani sana,vaa lile dera
lako,isitoshe ndio itakuwa vizuri na hiyo mimba
uliyokuwa nayo”
“Basi siendi kanisani”
“Mke wangu Gloria,mbona unakuwa ivyo?nipo
chini ya miguu yako,nilimuhaidi Mchungaji Patrick
kuwa nitaenda nawewe”
“Sawa,tunawahi kurudi lakini”
“Ndio”
Gloria akarudi na kubadili nguo,ambapo alivaa dera
na kitambaa kichwani wakaongozana mpaka
kanisani,Mchungaji Patrick alikuwa teyari yupo
kanisani anahubiri neno la Mungu,wakaingia mtu
na mke wake na kuketi viti vya nyuma kutokana
na umati wa watu uliofurika siku hiyo ya Jumapili.
BILA KUSAHAU KWAMBA HADITHI HII INAPATIKANA
YOTE WATSAP NA INBOX KWA MALIPO YA TSHS
3000/- KWA MWEZI, mawasiliano namba +255718
862176.(BADO KINYANG'ANYIRO CHA STORY ZA
KWAY SHINDA PESA KINAENDELEA, KUWA
MSHINDI NYAKUA KITITA CHA SHILINGI LAKI MOJA
TASLIM)
Sasa unaweza kusoma hadithi za mtunzi kway
insta@storyzakway
ITAENDELEA.
 
Nckson kwel amempnd mke wak jpo hlo lmke halna shkran
 
Back
Top Bottom