vinneboy
JF-Expert Member
- Aug 12, 2015
- 478
- 436
- Thread starter
- #61
SLAVE SEX(mtumwa wa ngono)……(12)
MTUNZI…..EMMANUEL F. KWAY
Contact…..+255718 862176
AGE….(18+)
ILIPOISHIA.
“Nipishe nina safari,unanichelewesha bwana, toka
mbele yangu NICKSON”
Gloria aliongea kwa ukali na kuyafanya mapigo ya
moyo ya Nickson yazidi kwenda kwa kasi na
jambo hilo kumshangaza sana Nickson na kudhani
wenda anaota ndoto!
SONGA NAYO.
Butwaa alilopigwa Nickson halikuwa na kipimo
chake,alimtizama mke wake mara mbilimbili
aliyekuwa mbele yake akisema kuwa anampotezea
muda tena kwa ukali,alihisi mgongo wake
umepigwa na ubaridi,alihema ndani kwa ndani na
mapigo ya moyo yakamdunda akiwa haamini yale
anayoyasikia kutoka kwa Gloria.
“Sogea basi,au?”
Gloria alizidi kusema, safari hii alisimama na
kuanza kumuangalia mume wake kuanzia juu
utosini mpaka kwenye miguu kwa dharau,hakutofa
utishwa na mtu anayetizama kinyesi!
“Gloria”
“Ndio jina langu,unasemaje?”
“Embuu kaa kidogo tuongee”
“Labda nikirudi”
“Kwani unaenda wapi mke wangu?”
“Sio lazima ujue lakini tambua kuwa nina
safari,tena ya maana”
“Gloria,tafadhali baki na mimi”
“Nickson embu nipite basi,unanichelewesha,kaa
kando”
Katika maneno aliyoongea Gloria hakukua na
masihala ndani yake,ulitokea mzozo mkubwa sana
kwa sababu Nickson hakuwa tayari kumruhusu
Mke wake atoke nje isitoshe hakujua ni wapi
anaenda mbali na hilo pia alikuwa ni mgeni wa jiji
hilo.
Dakika moja baadaye simu ya Gloria ikaita na
kuitoa mfukoni huku akitabasamu na kuiweka
sikioni ili kuongea na upande wa pili wa simu.
“Ndio….natoka nje hapa..kwahiyo tukutane wapi?…
hapo Airpot?. Sio kwako tena?..sasa mimi
sipafahamu, itakuaje?nikodi gari eeh.ahsante
baba,aya sawa.Namimi pia”Gloria akakata simu
baada ya kuhitimisha mazungumzo yake na
Pedeshee Kway.
“Umeona hii simu,naomba nipite sasa”
“Ni nani huyo?”
“Huyu wewe hakuhusu,unachotakiwa kukifanya
wewe hapa ni kunipisha nipite sasa hivi,nitaachwa
na ndege”
“Ndege?”
“Nickson ,usinipotezee muda hapa”
Katika purukushani, Nickson akasukumizwa kwa
nguvu kando na Gloria akatoka nje,moja kwa moja
akaingia ndani ya taxi moja wapo kati ya nyingi
zilizokuwa nje.
“Dada wapi?”
Dereva taxi aliuliza baada ya kumpokea mizigo
mteja wake.
“Airpot”
“Hapo wekundu wawili sista”
“Wekundu wawili ni nini?”
“Elfu ishirini”
“Sawa twende”
Dereva akaingia kwenye usukani safari ikaanza
mara moja.
Nickson alivyotoka nje alimshuhudia mke wake
yupo ndani ya taxi na ikawa imeshaondoka,ha
kutaka kukubali japokuwa moyo ulimuuma
mno,alirudi ndani kwa kasi ya mwewe na kubeba
funguo za gari,ilikuwa ni lazima afukuzie taxi na
azuie safari aliyotaka kuifanya Gloria.
Mkanda kama wa video ulitiririka ndani ya
kompyuta yake ya kichwani akarudi mpaka kijijini
Mwika alivyokuwa na Gloria wakiwa wenye furaha
kisha kufunga ndoa wakiishi wakiwa wenye amani
tele ndani ya ndoa yao.
Aliwaza jinsi alivyomtoa Gloria kijijini kwa wakati
huo alikuwa bado anavaa magagulo akamfundisha
kuvaa vizuri nguo za dukani,lakini leo hii ana
mjibu ovyo kwa dharau,hiyo ikawa haitoshi
akakumbuka jinsi Gloria alivyokuwa amevalia
kimini kilichoonesha mapaja yake nje,Nickson
akapata uchungu zaidi,akazidi kukanyaga mafuta
na gari ikaongeza kasi,katika maongezi aliyoyasikia
kwa mke wake katika simu alisikia neno ‘AIRPORT’
alilijua eneo hilo japokuwa kwa wakati huo
hakuiona Taxi aliyokuwemo mke wake,
ilibidi anyooshe mpaka Airpot na kupaki gari katika
maegesho ya magari akashuka na kuanza
kuangalia huku na kule akimtafuta mke
wake,Gloria.
*****
Pedeshee Kway alikuwa amefika tayari uwanja wa
ndege Mwalimu Nyerere na haikuchukua muda
mfupi wakawasiliana na Gloria, wakaonana.
“Baby safari bado?”
Gloria aliuliza akiwa katikati ya mikono ya
Pedeshee Kway.
“Bado kama dakika hamsini Fulani hivi”Pedeshee
Kway akajibu huku wakianza kutembea.
“Nitafurahi sana niki fika huko ala….”
“Gloriaaa!”
Gloria hakuweza kumalizia sentensi anayotaka
kuongea akakatishwa na mtu aliyekuwa akimuita
jina lake,sauti hiyo aliweza kuitambua ilikuwa ya
Nickson,Mume wake.Akageuka kwa mikogo ya
kisistaduu!
“Unasemaje?”
Namna alivyomjibu Nickson,ilikuwa ni kama
anamjibu mtu wa kawaida kwake, sababu bado
alikuwa amegandana na Pedeshee Kway aliyekuwa
kimnya anamtizama Nickson kuanzia chini mpaka
juu.
“Gloria,nini nimekufanya lakini?mbona unakuwa
hauna shukrani mama angu,tafadhali
usiniache,nakupenda Gloria wangu,nakupenda sana
tafadhali rudi nyumbani,japo chukua hata sekunde
mbili tu ukumbuke wapi nilipokutoa”
Nickson aliongea kwa uchungu,picha aliyoiona
mbele yake ilizidi kumtia wivu zaidi,alishaelewa
tayari hana chake.
“Ha!Haa!Haaaa!,eti nikumbuke nilipotoka wewe
mpumbavu nini,tena uache kuniimbia ngonjera
hapa”
“Gloria usiseme ivyo,mimi nakupenda bado”
“Wewe utampenda nani sasa hivi? Hata ivyo
sijakutambulisha huyu ndiye mwanaume wangu”
“Mwanaume wako kivipi?”
“Kusoma hujui hata picha huoni? Wa wapi wewe!”
Kipindi hicho cha malumbano ya Gloria na Nickson
yakiwa yanaendelea Pedeshee Kway yeye alikaa
kimnya alikuwa ni kama anayeangalia maigizo ya
jukwaani.
Alivyoangalia saa yake ya mkononi aliona ni dakika
thelathini teyari zimekatika,hakutaka tena
kuendelea kupoteza muda,akamshika Gloria kiuno
na kumvuta .Ghafla Nickson akamshika Mkono
Pedeshee Kway ili asiweze kuondoka.
“Kijana! hunijui,sikujui,hatujuani…!”
Pedeshee Kway akageuka akisema huku sura yake
ikiwa imejikunja.
“Jaribu kuwa na ustaarabu kidogo,usijitafutie
matatizo ya kujitakia,UNANICHAFUA”
“Anco tafadhali usinifanyie hivyo”
Nickson akasema kwa uchungu.
“Embu kwanza niachie,hivi nyie vijana mtaacha lini
kuvuta bangi?wewe unamfahamu huyu binti?”
“Ndio ni mke wangu”
“Wapi ameandikwa kuwa ni mke wako?”
“Ni mke wangu Anco”
“Embuu kaa mbali,unanuka jasho! Una uwezo wa
kuwa na mke kama huyu wewe?potea mara moja
usije ukajitafutia mabalaa bwana mdogo”
“Gloria ala…”
Nickson hakuamini macho yake na kusita kuongea
baada ya kuangalia kidoleni kwa Gloria na kutoona
pete ya ndoa,hapo ndipo alichanganyikiwa
zaidi,alimuachia Pedeshee Kway na kuanza
kumvuta Gloria.
“Nickson niachie nakwambia”
“Mke wangu tafadhali,usinifanyie ivy…o nipo chini
ya miguu yako,bado nakupenda kwa dhati.Anco
naomba uniachi..e mke wangu,niurumie nimemtoa
mb…….ali.”
Nickson alishindwa kuyazuia machozi yake
yaliyokuwa tayari yameshaanza kulowanisha
mashavu yake,badala ya Gloria kuuzunika yeye
alicheka.
“Ha!Haaaa!Haaaaaa sasa unalia nini?kisa
naondoka?tafuta mwanamke mwingine Nickson,
mimi sio type yako kwa sasa hivi,achia ngazi”
Gloria aliongea maneno ya dharau huku akitaka
kumtoa Nickson mikononi mwake aliyekuwa bado
analia machozi kama mtoto mdogo.
“Baby,huyu mvuta bangi bado unampenda kwani?”
Pedeshee Kway alimuuliza Gloria.
“Nimpende kwa lipi?”
“Basi nisubiri nakuja”
Baada ya Pedeshee Kway kuondoka.Ghafla Nickson
akaona maaskari sio chini ya kumi wamemfikia na
kumzoa huku wakiwa wameishika suruali yake kwa
nyuma wakimsukuma mbele yaani Tanganyika jeki!
“Jamani nini nimefanya mimi?Yule ni mke wangu”
Nickson alijaribu kuongea huku miguu yake ikiwa
inaelea juu juu.
“Aroo twende,unareta habari za bangi hapa,songa
mbere wewe,utaeleza ukifika kituoni”
Askari mmoja wa kikurya aliyefahamika kwa jina la
Mwita alisema.
“Jamani sio ivy…”
Nickson hakumalizia sentensi yake akatulizwa na
ukofi mkali wa uso na kutupwa ndani ya diffenda
ya polisi.
BILA KUSAHAU KWAMBA HADITHI HII INAPATIKANA
YOTE WATSAP NA INBOX KWA MALIPO YA TSHS
3000/- KWA MWEZI mawasiliano namba +255718
862176.
Sasa unaweza kusoma hadithi za mtunzi kway
insta@storzyakway
ITAENDELEA.