Riwaya mpya: Mbwa wa geti

Riwaya mpya: Mbwa wa geti

Mbwa wa geti

Sehemu ya kumi na sita

Ni wakati anamalizia kufunga na kugeuka ndipo akaona jambo lingine ambalo mwanzo alilitilia shaka.

Huko juu alikuta si dari tena,ilkuwa ni uwazi mkubwa tu uliotosha mtu kutembea na kulikuwa na boksi kadhaa na kulionekana kufanyika shuguli za kuyapaki maboksi yale na hapo akaamua kufungua boksi moja.

Hakuamini macho yake alikutana na mabomu ya c4 yakiwa yamepangwa vizuri na kulikuwa na mabomu mengine ya baruti.

Zedi akazidi kuyafungua maboksi yale na kukutana na silaha nyingi za kila aina,akazitamani baadhi na akachukua bastola mbili na kuzisunda kiunoni hivyo akawa na jumla ya bastola tatu.

Akazidi kuyafungua maboksi yale na kukutana tena na dawa za kulevya zikiwa zimewekwa kwenye mfuko ya chumvi huku juu kukiwa na jina la MZURI.

Hakuwa na muda zaidi wa kukaa kule juu,hivyo haraka akatafuta namna ya kutoka.

Alikutana na sehemu iliokuwa imetengenezwa kama mlango wa dharura na akatumia hiyo sehemu kutoka mle ndani na huko akajikuta anatokea kwenye ngazi zilizoonesha yupo kwenye floor ya juu na kuna ngazi zinashuka chini,hakuzijali.

Akapita kwenye korido pana iliokuwa inatenganisha vyumba kaadhaa vilivyokuwa ni ofisi kimuonekano,huku akishuhudia ukimya wa hali ya juu na nafsin mwake akajua wenyewe wamekimbia baada ya king’ora cha hatari kulia pale ndani.

Hakutaka kushuka ngazi za chini zaidi akaambaa na korido na kutokea upande wa maliwato na huko akatembea kidogo na kukutana na uwazi uliokuwa unampeleka hadi dirishani akalifikia na kulifungua kisha akatazama nje na kuona namna majengo mengine yalivokaa,yalikaa kwa kupeana migongo.

Akatazama kulia na kushoto akaona alichokuwa anakitafuta.

Bomba la kupitisha maji machafu kutoka juu gorofani hadi chini na yeye akafanya jitihada kidogo na kulifikia kisha akalitumia kushuka chini na kutokomea mtaani huku swali likiwa ni nani aliefanya vile ndani ya bank ile,na alifanya kwa malengo gani hakupata majibu na hadi muda huo alikua anavuka barabara na kuita taxi alioomba imrudishe Nairobi West mtaa wa South b dereva akatii bila kujiuliza sana.

Mjini Naivasha wadudu wasioeleweka walikuwa wanashambulia watu na wanyama waliokuwa wakifugwa huko na,serikali ilikuwa imejaribu kwenda kutoa msaada lakini walizidiwa kasi na wadudu wale,watu walikufa na wachache waliofanikiwa kutoroka,huku sumu ya kuuwa wadudu ikimwagwa huko angalau kuzuia shambulizi hilo lakini wadudu wale hawakufa na ndo walizidi kuleta maafa huku wakiwa na kasi ya ajabu.

Mji wa Nairobi ulitangaziwa hali ya hatari na kila mtu hakujua aelekee wapi kwa wakati huo……

Hayo yalisikika kutoka kwenye radio ndani ya taxi huku mtangazaji akiwa ni Leonard mambo mbotela.

Zedi aliekuwa ameegemea kiti na kujilaza yote aliyasikia na hapo ndipo akili yake ikatakiwa kufanya kazi zaid maana aliona hatari ya shambulio lile la wadudu ambao yeye tu ndie alijua wanatoka wapi japo hakujua chanzo ni nini hasa na kwanini watu wale wanataka kuchukua nchi kwa kutumia ukatili wa namna ile.
****

Dereva wa taxi alisimamisha nyuma ya jengo la KRA(KENYA REVENUE AUTHORITY)kisha akaomba ujira wake na Zedi akazama mfukoni na kumpa kisha yeye akashuka na kulitizama jengo lile namna lilivyokuwa refu.

Akapiga mwendo kidogo na kuingia kwenye kiuchochoro kilichikuwa kimetenganisha majengo kadhaa na kisha akanyoosha na kutokea upande wa mbele wa jengo lile na hapo akaingia ndani yake.

Macho yake yakafanya kazi moja tu kusoma vibao vya maelezo ya ofisi na kazi zake na hapo akapata ofisi alioitaka.

Ilikuwa ni ofisi ya usajili wa magari.

Akaelekea moja kwa moja hadi kwenye mlango wa kuingilia ndani ya ofisi ile na kisha akagonga mlango na kama utaratibu usio rasimi ulivyosambaa ndani ya ofisi za waafrika wengi,hakuitikiwa.Na yeye hakungoja kuitikiwa maana aliujua utaratibu huo.

Akakinyonga kitasa na kuzama ndani.

Nyuma ya meza ya ofisi alimkuta kijana wa makamo yapata miaka thelathini na tano hivi,akavua kofia na mawani yake kisha akakaa bila kukaribishwa kwenye kiti kilichokuwa mbele ya meza huku sasa wakiwa wanatazamana na kijana yule ambae hadi muda huo alikuwa ameshaijua sura ya mtu aliekuwa mbele yake.Aliijua kwa sababu ni ahsubuhi hiyo aliposikia matangazo kwenye radio na tv ya kuwa mtu huyo amefanya jaribio la kutaka kulipua jengo la bank ya KCB mjini Nakuru.

Zedi aliona ubabaikaji wa mwenyeji wake,hakutaka kuuliza lolote zaidi ya kile kilichompeleka pale.

“Naomba kufahamu umiliki wa namba hii K369D” alianza kusema Zedi.

“Wewe ni askari?!” aliuliza mwenyeji yule.

Zedi akamtazama na haraka akajua mtu yule anajikaza kuongea ila anamwogopa,hivyo akaamua kutumia udhaifu huo kama silaha Ya kupata kile alichokihitaji

“sihitaji swali lolote naomba kujua umiliki wa gari hii” alizungumza huku akisimama na hapo akaona mtu yule akitetemeka zaidi na kuanza kupekua kwenye komputa yake na punde akawa na majibu

“Anaitwa Jafo kairuki na makazi yake yako Kibera”

Zedi hakutaka kungoja maneno zaidi akatoka ndani ya jengo lile na wakati anatoka tu hata kabla hajavuka barabara ili kufuata kituo cha madereva taxi,akaona gari la polisi likisimama pale kwa kasi na askari wale wakashuka haraka haraka na kuingia ndani na hapo hakutaka kufanya ujinga wowote haraka akakimbia na kupanda taxi ambapo aliomba apelekwe Kibera na dereva akatii haraka wakawa wapo barabarani wakikunja kona ya uwanja wa ndege wa Nairobi west.

Safari yao ilikuwa imewafikisha hadi langata road na kuifuata hiyo barabara hadi walipotokea kwenye makutano ya southern bypass kisha wakakunja kulia na walipofika Uhuru garden Zedi akaomba kusimama hapo ,akalipa na kumruhusu dereva aondoke kisha yeye akaamua kufuata barabara kwa miguu hadi kwenye mahakama ya National housing na macho yake yakavutiwa na harakati za eneo lile.

Akazidi kusogea na kufika karibu na nyumba alioihitaji na kisha akawa kama anaipita hasa baada ya kuona geti lipo wazi na alipopita tu akaona kuna watu wanajadili kitu huku wakitoka nje nae akainama chini na kuyasikia maongezi yao.

“tayari mbinu ya kuwahamisha imefanya kazi na sasa bado nyaraka moja tu,wahi ukaitafute na wambie mbwa weupe wahamishe kule Nakuru west tunapahitaji kufikia hadi kesho ahsubuhi”

Mtoa maelezo akamaliza na kuanza kurudi ndani huku mpewa maelezo akipanda gari iliokuwa pale na kuondoka kwa kasi .

Zedi alihitji kuingia pale ndani na alihitaji kujua chanzo cha mauji yale kila siku na pia alihitaji kujua hao mbwa weupe kazi yao.

Itaendeleapm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom