Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

MWANDISHI IBRAHIM MASIMBA

*******
Alishuka akiwa peke yake baada ya kuachana na Sohwa, akaongoza kuelekea hotelini huku kichwa chake kikiwaza wapi alipo Mudy. Kilikuwa kitu kigumu sana kwa Mudy kutokuonana naye kwa muda wa siku mbili. Hili likampa shaka na wasiwasi mkubwa juu ya usalama wa Mudy. Akalazimisha hisia zake kuamini kwamba Mudy Yupo salama, lakini moyoni kulijaa mashaka. Akatembea usiku ule akiwa na ile Disc mkononi. Hakuuona umuhimu wa kulala usiku ule wakati kuna mtu muhimu kwake hajua wapi alipo. Alichokifanya nikuamua kwenda chumbani kwake ilikufanya mawasiliano na Mudy. Alijua kwa vyovyote walitakiwa kuianza kazi mapema sana. Muda mfupi alikuwa akiipanda lifti ya hoteli kuelekea chunbani kwake. Sekunde Hamsini Lift ikasimama, akashuka na kuongoza kuelekea chumbani. Sehemu yote ilikuwa imetulia sana kuonyesha kuwa hapakuwa na watu kwa wakati ule. Akazivuta hatua kwa uangalifu, masikio yake yalikuwa huru kusikia chochote. Akauvuka ukumbi ambao nao haukuonyesha uwepo wa watu kutokana na ukimya. Hilo likaanza kumpa wasiwasi, akaongeza tahadhari, akaufikia wa chumba chake, akachomoa kadi maalum yakufungulia, mlango ukamtii na kukiruhusu kichwa chake kupita kisha macho kufanyakazi ya kuchungulia kwa chati. Hapakuwa na hatari lakini aligundua kuwa alitembelewa na Mtu, mtu ambaye ni mjuzi kupindukia kutokana na aina ya upekuaji uliofanywa chumbani kwake. Viti vilipekuliwa na kurudishwa kwa aina ile ile, aina ambayo kama ni kwa mtu wakawaida asingeweza kugundua chochote kile. Akaingia kabisa na kuufunga mlango kwa ndani kisha kwenda kujibwaga kwenye kiti kikubwa. Hakutaka kuchelewa kufanya kile ambacho alitaka kukifanya. Alichokifanya nikuiwasha computer yake kisha kuingiza Ile disc muda mfupi akayaona maandishi makubwa tena yalioandikwa kwa Lugha ya Kiswahili. MPANGO OVU.. akaendelea kutizama akiangalia kwa makini kile ambacho kilikuwemo ndani ya Disc. Wakati hilo likiendelea akahisi hakuwa peke yake, akahisi uwepo wa mtu, mtu ambaye alikuwa ndani ya chumba kile. Mkono wake ukashuka chini kuikamata bastola yake. Kengele ya Hatari ikakigonga kichwa chake. Akatulia akijiandaa kwa utayari wa mapambano, utayari wa kujilinda dhidi ya mtu yoyote. Akatulia kama hakuwa na wasiwasi, kama hakushtukia uwepo wa mtu huyo. Punde akahisi michakato ya Viatu, harafu akauona mlango ukicheza, baada ya hapo akauona mlango ukifunguliwa taratibu na kwa utaalam wa hali ya Juu. Jennifer akahama kwa sekunde na kujilaza nyuma ya kiti bila kutoa kishindo chochote. Macho yalikuwa mlangoni na hata mdomo wa bastola ukitizama huko. Akawaona watu watatu wakiingia kwa utulivu kanakwamba wanaingia chumbani kwao. Walikuwa wanaume wawili wa kizungu na mwanamke mmoja ambaye alikuwa ni mweusi.

Baada ya kuingia kila mmoja akajitenga akiangalia kipi ni kipi na nini ni nini. Wakati wakiliangalia hilo likatokea nyingine ambalo liliendelea kumshangaza Jenipher, na haikuwa kwake tu, bali hata kwa wale watu waligwaya na kukubaika. Hakuna alieamini kama ndani kulikuwa na mtu mwingine, tena akiwa umbali wa hatua tano kutoka sehemu ambayo alikuwepo Jenipher.

"Bastard! ? Ilikuwa sauti ya kukubaika kutoka kwa watu wale.. "bastard!" Jenipher naye akaita huku akiinuka Kuelekea pale waliposimama watu wale. Mwanaharamu hakuwajibu, bado aliwatizama huku akitabasamu. Halikuwa tabasamu la urafiki, harikuwa tabasamu la heri. Lilikuwa tabasamu la kiume, tabasamu ambalo kila mmoja alijua kipi ambacho kingetokea pale. Ni hapo walipokuwa wakitizamana taa zikazimwa, kisha kufuatiwa na milio ya Risasi ambayo haikudumu hata kwa dakika moja, ukimya wa ajabu ukatamalaki. Hapakuwa na dalili ya uwepo wa mtu ambaye alikuwa hai. Hapakuwa na mtu ambaye alikuwa akipumua wala kuwepo kwa mtu eneo lile. Taa zikawashwa tena, chumba kikawa cheupe. Wakajikuta wakitizamana uso kwa uso Kati ya Jenipher na Bastard huku chini yake pakiwa na miili ya watu watatu wakiwa maiti, tena wakiwa wameuawa katika staili ile ile ya kuvunjwa shingo.

"Bastard! ? Akaropoka Jane.

"Yeah am bastard" hakuitika yule mwanaume, bali sauti ilitokea nyuma yao, tena sauti ya mwanamke.. Jenipher hakugeuka, hakugeuka kwa kuwa hakuwa mgeni wa sauti ile, haikuwa sauti ngeni Masikioni. Ilikuwa sauti ya mtu ambaye aliwahi kuwa naye kwenye tukio moja ambalo liliitingisha Tanzania. TUKIO ambalo limepachikwa jina la NITAKUFA NA WEWE. Alikuwa Neema Habibu.

********

Alitaka kukumbuka nini kilitokea. Mara ya mwisho alikumbuka kupokea sms kutoka kwa Sohwa akimwambia kuwa lazima awepo sehemu fulani katika muda fulani. Akakumbuka kuwa aliondoka pale akiwa na mkoba ambao ulikuwa na vitu vya kazi. Kufikia hapo kumbukumbu yake ikaanza kurudi taratibu. Akakumbuka alipowaona watu wakishuka kutoka kwenye gari. Kufikia hapo akalikumbuka tukio la kuchomwa na kitu mfano wa sindano ubavuni. Hakukumbuka tena kilichoendelea baada ya hapo. Akainuka pale kitandani na kuanza kutembea mle chumbani. Cha kwanza kukumbuka ilikuwa simu yake ambayo haikuwa imewashwa tokea usiku wa jana. Hapo akahisi kwamba lazima atakuwa ametafutwa, lazima Jenifer atakuwa amemtafuta. Akaiwasha simu kisha akasubiri kwa muda.. Punde Ujumbe mfupi wa maneno ukaanza kuingia. Akaanza kuufungua ujumbe wa kwanza ambao ulitumwa kupitia Whatsapp na namba ambayo ilikuwa ngeni machoni mwake. Akaufungua huku akiwa makini kuangalia alichotumiwa. Akakutana na picha ambayo hakutegemea kukutana nayo. Ilikuwa picha iliokionyesha kichwa cha Sohwa kikiwa hakina kiwiliwili. SOHWA ALIKUWA AMECHINJWA NA KUTENGANISHA KICHWA..

CHOZI LA KIUME LIKASHUKA..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom