Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

OTE="ABBYA, post: 19244621, member: 358994"]Pole mkuu,[/QUOTE]
Ahsante sana mkuu
 
MKE WA RAIS

Mwandishi Ibrahim Masimba

* *******
Mlango ukagongwa, Mudy akatulia, ukagongwa tena kwa mara ya pili, bado Mudy bado hakuinuka wala kuchukua hatua yoyote. Mkono wake ulikuwa ukielekea sehemu alipoihifadhi silaha yake. Macho yalikuwa yakiutizama mlango, na masikio yakawa tayari kusikia kile ambacho hakikuwa rahisi kuonekana kwa macho. UKIMYA. . yeah ukimya wa ajabu ukatokea, hakusikia vishindo vya miguu wala michakato. Bado ukimya ulichukua nafasi yake, bado ukimya kanakwamba hapakuwa na mtu aliegonga mlango ukatokea. KWA NINI UKIMYA? Hakutaka kuliamini wala kulikubali hilo, sekunde ya kwanza na yapili zilimkuta akiwa pembeni ya mlango sikio likiwa mkabara kusikiliza chochote. Lakini haikuwa hivyo, hakusikia chochote, licha ya mlango kugongwa muda mfupi uliopita, lakini sekunde hii palikuwa na ukimya, ukimya ambao haukuwa wakawaida. Nani aligonga mlango? Alihitaji nini? Kama alihitaji kitu kwa nini hakuendelea? Yalikuwa maswali yaliyokisumbua kichwa chake, maswali ambayo ilikuwa lazima ayapatie majibu. Sikuzote kwenye ujasusi hutakiwi kudharau kitu ama kuwa na majibu mepesi katika jambo zito kama lile. Akaamua kurudi pale pale alipokuwa amekaaa. Hakarudi kukaa kujisahau, bali alikuwa amekaa akihisi lolote linaweza kutokea. Safari hii akaichukua simu ya Marehemu Sohwa na kuanza kuipitia. Alianzia kwenye ujumbe mfupi kwa mara ya pili. Akaamua kuuchunguza kila ujumbe, alikuwa akisoma huku macho na akili yake vikiwa mlangoni. Kulikuwa na meseji nyingi ambazo zilitumwa kwa lugha ya kirusi, lugha ambayo haikuwa tatizo kwake. Kati ya namba za watumaji ujumbe kulikuwa na namba moja ambayo Mudy aliitilia mashaka. Namba ile ilionyesha kuwa ni ya mtu ambaye ndie aliekuwa kinara wa kuwasiliana na marehemu Sohwa. Aliitizama tena ile namba kisha akainakili pembeni kama alivyofanya pale mwanzo, kisha akaizima na kuitupia kitandani. Akakivuta kile kifaa chake na kukitumbukiza kwenye laptop yake, muda mfupi picha zikatokea. Hazikuwa picha kama picha bali ilikuwa video, video ambayo ilimuonyesha Sohwa akiingia chumbani kwake. Ikamuonyesha akiyavua mavazi yake na kuingia bafuni. Baada ya Sohwa kuingia bafuni na kuurudisha mlango, punde akaonekana mtu akiingia, huyu alikuwa mzungu na alionekana kuwa ni mtu wa mazoezi. Baada ya mzungu yule kuingia ndani akamuona naye akielekea bafuni ambako alikuwepo Sohwa. Muda mfupi baadae ikasikika miguno ambayo iliashiria watu wale (sohwa na yule Mzungu) walikuwa wakifanya mapenzi. Miguno iliendelea kwa muda mpaka pale waliporudi chumbani na kuendelea na tendo lile ambalo lilikuwa likitendeka katika mtindo wa kihuni (hard style)

Ulionekana ulikuwa mchezo ambao waliuzoea kutokana na kuonekana wote kuwa ni wazoefu katika mtindo ule. Katika kufanyika kwa tendo hilo ndipo tukio la kutisha likatokea. Wakati Sohwa ameinama kwa kukishika kitanda Huku mzungu yule akiwa nyuma akiendelea na kitendo kile, akamuona mzungu Yule akichukua kisu kubwa kutoka nyuma ya kiti ambacho kilikuwa ndani ya chumba. Baada ya kuhakikisha amekishika kisu kwa ufasaha, akakishika kichwa cha Sohwa kupitia nywele zake ndefu.. sekunde tano mbele mudy alishuhudia kichwa cha Sohwa Akikanguka pembeni Huku kiwiliwili kikikurupuka na kuruka huku na huko. Yalikuwa mauaji ya kinyama sana kwa mtu anayemfahamu. Ni uchungu sana kumpoteza mtu kama Sohwa Richardson. Mwanamke ambaye kamwe hakutaka kuona nchi fulani akionewa. Licha ya Kuwa mmoja kati ya majasusi wa FSB (zamani KGB) Hakusita kumsaidia Mudy katika missions nyingi. Alikumbuka mara ya kwanza kukutana naye ilikuwa ni kule Afghanistan wakati huo Muddy akiwa ni Mmoja ya wapelelezi kutoka Africa waliombwa na FSB kusaidia kumrudisha Urusi Jasusi alieasi na kutorokea nchini humo. Machozi yalikuwa yamelowesha meza. Alichokifanya ni kuizima laptop, kisha akakichukua kifaa chake na kukificha sehemu yake maalum. Akakiangalia kile chumba kwa muda, akatabasamu, harikuwa tabasamu la furaha. Muda mfupi alikuwa akikiacha kile chumba kwa kupitia dirishani na kutua upande wa pili. Alichepuka na kuacha hoteli ile kichwani kwake asijue wapi anaelekea. Kila alipokuwa akitembea tukio la kuuawa kwa Sohwa lilikuwa likijirudia kichwani mwake. Akaona ni wakati wakwenda kuua, ni wakati wa kwenda kumsaka mtu yule aliemuona akimuua. Hakutaka kurudi kule alipowaacha Mwanaharamu na Wenzake. Kisasi cha kumuua aliemuua Sohwa kilikuwa cha kwanza kwake. Hakutaka kumshirikisha katika kisasi mtu yoyote.

*******
Alishuka kwenye tax na kuchepuka mpaka upande wa pili wa barabara. Akaongoza akitembea kama mtu wa kawaida mpaka sehemu moja ambayo palikuwa na huduma ya Internet. Akaingia ndani na kuomba kupewa sehemu ya pembeni kidogo. Alichokifanya nikuichukua namba ambayo alihisi ni ya muuaji wa sohwa. Akaiandika kwenye kompyuta kisha akaandika na maneno kadhaa.. ndani ya Dakika Mbili maneno yaliosomeka Victoria Base yakatokea mbele ya kompyuta.

"Victoria Base? Swali la kwanza alilojiuliza. Hakusubiri kulipata jibu, alichokifanya nikuinuka na kutoka nje kabisa ya Jengo lile. Wakati anatoka kwa mbali macho yake yakamuona mtu, mtu ambaye hakujua uwepo wake maeneo yale. hakuwa mwingine bali yule Msichana wa kule Hotelini. Msichana ambaye Muddy Hakujua alikuwa ni nani na kwa nini yuko pale. Hapo akaipqta hamu ya kumpata ili amsaidie katika kuijua kambi ya victoria.. Akatembea kuelekea kule alipo..
 
MKE WA RAIS

Mwandishi: Ibrahim Masimba
*********

Alihitaji kumtumia msichana yule, alihitaji kumtumia katika kuijua kambi iitwayo victoria. Aliuhitaji msaada wa mwanamke yule. Lakini angemuamini vipi mwanamke ambaye anahisi anamfuatilia yeye. Ugongwaji wa mlango kule hotelini na kule kumuona pale kulimpa hisia tofauti. Hisia ambazo hakupenda kuzidharau. Huyu ni mmoja wao na ananifuatilia mimi. Yalikuwa maneno aliyoyatamka wakati akiivuka barabara kuelekea upande wa zinapopaki tax. Alitembea akiangalia eneo lote kwa jicho la tatu, alitizama kuhakikisha kuwa hakuna mtu yoyote anayemfuatilia. Akaifikia tax na kuingia pasipokutoa salamu. Muda huo huo dereva naye akaingia pasipo kutoa salamu. Dereva akaiwasha gari na kukanyaga mafuta. Gari ikaanza kutembea kwa mwendo wa kawaida. Wakati huo ilikuwa yapata majira ya saa tatu na nusu usiku. Gari ikatembea pasipo abiria kusema wapi anapoelekea. Hilo lilikuwa aina ya tabia nyingine, hakuwahi kupakia abiria mkorofi kama huyu. Akageuka kutizama nyuma alipokaa abiria wake akitegemea kuulizwa chochote, lakini akapigwa na mshangao ambao hakuutegemea, licha ya kumuona mtu akiingia ndani ya gari yake lakini kwa wakati huu alishangaa zaidi baada ya kutokumuona mtu. Kusema kweli hilo hakuwa amelitegemea. Hakuwa amejiandaa kwa tukio hilo. Akabaki kuduwaa. Punde akaliona gari aina ya marcedes Benz likimpita kisha likasimama kwa mbele. Kabla hajajua nini cha kufanya akawaona watu watatu wenye silaha wakiisogelea gari yake. Hawakuwa watu wa utani na hawakuonyesha umasihara. Watu wale wakaifikia gari yake kisha bila kuuliza mdomo wa bastola ukaelekezwa kwake, harafu wale wawili wakaufungua mlango wa nyuma kwa kasi bastola mkononi. Lakini mshangao uliompata dereva mara ya kwanza,ndio mshtuko ambao waliupata hawa watu. Walipoteza umakini kwa sekunde karibia kumi wakishangazwa na kutoweka kwa mtu wao katika mazingira tatanishi. Bastola tatu zikaelekezwa kichwani kwa dereva akitakiwa kusema wapi alipo mtu ambaye aliingia ndani ya gari. Lakini hata yeye alikuwa ameshangazwa na uyeyukaji wa abiria wake, abiria alieingia bila salamu na kuketi siti ya abiria, kisha kuyeyuka mfano wa kivuri. Angejibu nini? Jibu angelitoa wapi? Akaendelea kutetemeka huku midomo ya bastola tatu ikimtizama. Hapakuwa na masihara tena, lakini hata swali liliporudiwa hakuwa na majibu. Kidole cha mmoja kati yao kikashuka taratibu kwenye kitufe cha kuruhusu risasi.. lakini kabla hajafyatua wakaisikia sauti, sauti kutoka nyuma yao, sauti ambayo iliwagutusha na kuendelea kupoteza umakini. Ilikuwa sauti ya Muddy, tena ikitokea nyuma yao. Wote wakageuka kwa pamoja, wote wakageuka huku bastola zimetangulia, lakini walikuwa wamechelewa, kwani hawakuipata nafasi hiyo, hawakuipata nafasi ya kufyatua.. punde walikuwa wakianguka chini kila mmoja akivuja damu. Risasi kutoka kwenye bastola yenye kiwambo cha kuzuia mlio zilitosha kuwamaliza watu wale. Muddy hakuchelewa wala hakutaka kuwapekua, akaingia ndani ya tax ile ile akiamulu dereva Ampeleke VICTORIA BASE.

Kuitaja Victoria Base kukaleta mshtuko machoni kwa dereva yule, mshtuko ambao ulikuwa wazi machoni mwake. Hilo likamvutia Muddy, likamvutia kwa kuwa alihisi sasa amepata mtu wa kumpeleka.

"Boss huko ni hatari haparuhusiwi kufika mtu yoyote wala gari." Hatimaye aliongea dereva kwa sauti yenye woga ndani yake.

"Endesha gari, mimi na wewe tutakuwa watu wa kwanza kufika huko." Akajibu Mudy pasipokuonyesha masihara.

"Boss unaongea kwa kuwa hupajui huko. Hivi umeshawahi kuwasikia CIA na Hata KGB? Akajibu dereva yule huku akimuangalia Mohamed.

Kufikia hapo Mudy akatambua kuwa mtu alienae alikuwa mtu sahihi kwake. Alikuwa mtu sahihi wa kumpeleka Victoria Base ama Kumueleza ukweli kuhusu sehemu hiyo.

"Hapana siwajui na wasikia tu. Lakini kwa nini hiyo sehemu iogopewe hivyo kunakitu gani?" Akauliza Muddy huku akijifanya hajui kitu.

" wewe ni nani kwanza? Maana nilichokishuhudia pale nyuma tulipopita ni hatari. Nahisi hata wewe unaweza kuwa jasusi wa CIA, MOSSAD ama FSB."akajibu mtu yule.

"Mimi ni mtu wa kawaida sana. Natamani kufika huko kwa kuwa nashangaa watu wengi wanaogopa kufika huko." Akajibu Mohammed akionyesha ni mtu wa kawaida kabisa.

""Unadhani huko nyuma watu walikuwa wakiogopa? Siku hizi tu ndio watu wanaogopa hasa baa.....kabla hajaimalizia kauli ile Muddy akashangaa kuiona damu ikiruka... Dereva alikuwa amepigwa Risasi kupitia kwenye kioo. Gari akaanza kuyumba huku na huko, muddy hakuwa mpuuzi, akaufungua mlango na chupa akiangukia kando ya barabara. Muda mfupi baada ya kuruka akaiona gari ikienda kugonga ukingo wa barabara, kisha kulipuka.

Muddy aliiangalia gari ikiwaka moto, kisha akaamua kuondoka. Alihitaji kufika Victoria Base lakini kwanza alihitaji kwenda kuonana na mwanamke yule, mwanamke ambaye alihisi alikuwa nyuma ya matukio yote. Alihitaji kurudi pale hotelini, kurudi kwa njia nyingine na akiwa mwingine kabisa. Alihitaji kumjua yule mwanamke, na alitaka kuijua victoria Base.. akageuka kuelekea huko, huku maneno ya dereva Tax yakimpa mwanga ingawa aliuawa kabla ya kuyamalizia
 
Back
Top Bottom