Riwaya: Mke wa Rais

Endeleaa baba kukiwashaaa
 
TE="Blaki Womani, post: 17523457, member: 38228"]Nimesoma hapo kwenye DIMBWI LA DAMU nikamkumbuka nameless girl 😀
Upo Na mumewe hapa kwahiyo usishangae,nimeachiwa na mkwe wangu BEN MTOBWA[/QUOTE]

urithi mzuri huo.......toeni kitabu pamoja na wife kitakuwa bomba sana
 
Story nzuri ibra
 
Mudy jamaan sijui atatoka
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 47

Mudy akatabasamu, kisha akainuka na kuongoza kuelekea alipoambiwa. Alikuwa akitembea bila wasiwasi wowote.. Licha ya kujua kuwa anafuatiliwa lakini bado aliupa ubongo wake Utulivu.. Utulivu ambao aliuhitaji sana katika kazi yake ya Hatari. Akauvuka mlango wa kuelekea ndani Ya hoteli ile.. Alipouvuka akaongoza moja kwa moja mpaka sehemu husika.. Alianza kuhesabu chumba kimoja baada ya kingine. Alipokifikia Chumba namba 14 B akakipita kama hakuwa na umuhimu nacho. Akaendelea na Safari kuelekea upande Mwingine.. Wakati akiumaliza upande wa chumba kile, akahisi kusikia vishindo vya mtu.. Hakujipa kazi Ya kugeuka bali aliongoza kama hakuhisi kitu. Kila alipokuwa Akisonga ndivyo vile vishindo vilivyozidi kusikika.. Mudy Akageuka kwa Silika Ya Aina Yake bastola ikiwa tayari Mkononi kulipua.. Macho yake yakagota kwenye mguu wa mtu uliyokuwa ukipotelea kwenye kona.. Mguu ambao alihisi ulikuwa wa mwanamke.. Akarudi na kuendelea na safari.. Tayari kengere ya Hatari zilikuwa zikigonga ovyo katika kichwa chake.. Alitambua uwepo wa mtu sehemu Husika.. Alijua kuhusu kufuatwa kwake na uwepo wa mtu nyuma yake.. Licha Ya kulifahamu Hilo hakuwa na Wasiwasi.. Hakuwa na wasiwasi kwa kuwa alikuwa akitembea huku akijuwa kuwa kulikuwa na watu au Mtu akimfuatilia kutoka mahala fulani..

Mwisho wa safari yake ilikuwa ni katika Vyoo vya Hoteli Ile.. Akaviendea Vyoo vya wanaume.. Akakichagua kimoja na kuingia ndani. Baada ya kuhakikisha hapakuwa na Mtu, akazichomoa bastola Zake mbili na kuziangalia.. Punde akaisikia miguu ya mtu ikisogea pale nje ya Vyoo... Akatega sikio Zaidi.. Bado Mtu Yule aliendelea kusimama pale nje... Mudy akajiandaa kwa Hadaa.. Akaufungua mlango kwa kasi Ya Ajabu huku bastola Mkononi. Lakini kile ambacho alikitarajia hakukiona.. Nje hapakuwa na mtu wala kiumbe Chochote.. Akashangaa kwanza na akili kuhama kwa umbali fulani.. Alikuwa akichezewa mchezo.. Alikuwa akichezewa na mtu ambaye alikuwa na uhakika alimfahamu yeye.. Ni wakati akiwa amezubaa akitizama Mbele Akahisi uwepo wa Mtu mbele Yake.. Akageuka tena kwa Kasi.. Lakini mara hii Hakufanya alichotegemea... Akiwa amegeuka akiwa ameshikilia Bastola Mkononi akajikuta akikutana na Mapigo mawili ambayo Yalitua mkononi kwa Mudy, Bastola Zote Zikaanguka Chini.. Mudy akajiweka sawa Tayari kwa mapambano, mapambano Ambayo hakujua anapambana na Yupi... Akainua macho Yake kumwangalia kiumbe anayetaka kupambana naye.. Macho Yake yakakutana na macho Ya mwanamke.. Alikuwa mwanamke haswa kwa muonekano.. Lakini Macho yao yalipokutana na kuangaliana kwa muda kila mmoja akamsoma Mwenzake.. Kila mtu aliisoma fani Ya mwenzake kupitia Macho Yake.. Kila mmoja alimtambua mwenzake kuwa yu mwalimu katika mapambano ya kutumia mikono na ni mtaalamu katika mapambano Ya kutumia Silaha.

Mudy Alikuwa akitazamana na Revina Michael.. Mwanadada kutoka Shirika la Kijasusi la Rwanda.. Alikuwa ni Mtulivu akimuangalia Mohamedi katika namna ya kumlazimisha kukisoma kitu katika Macho Yake.. Naam, Mudy akakisoma na kukiona kile kilichondani Yake. Hakuogopa wala kuhofia.. Alichokifanya ni kutabasamu.. Tabasamu ambalo lilikuwa kipimo cha mwisho Cha hasira. Kilichofuatia hapo yalikuwa mapigano, mapigano ambayo yalikuwa na ufundi wa hali ya Juu.. Kila mmoja alikuwa akionyesha yeye ni nani katika medani Ya sanaa ya kimapigano.. Zikapita dakika mbili kila mmoja akiwa hajaruhusu kuguswa na Mwenzake.. Mudy hakuwa Mjinga wa kutumia kila alichonacho.. Alichokifanya ni kuchanganya mapigo fulani ya Kirusi na Kimarekani ambayo yalionyesha kupanguliwa kiustadi na Mwanadada Yule.. Akaona Muda wake Ukipotea Bure.. Akabadilisha mapigo na kuanza kutumia Martial Combart.. Yalikuwa mapigo Yenye mchanganyiko wa kijeshi hasa yakitumiwa sana na Makomandoo wa Kirusi, kimarekani na hata Majasusi Wa CIA na wale wa FBI... Ni Mapigo matano Yaliyoweza kumlevya na kumuangusha REVINA MICHAEL..akabaki akitweta pale Chini akimuangalia Mohamedi..

Ni wakati Huo wakitizamana mvua ya Risasi ikavurumishwa kuelekea pale walipo.. Mudy alikuwa amechupa huku na Revina alikuwa amechupa kule.. Hapo ndipo Mudy aliposhuhudia Shabaha na Utaalam Kutoka kwa mwanadada Yule.. Alikuwa akirusha risasi kwa utaalamu wa kipekee, alikuwa akirusha Risasi akizunguka hewani.. Na hata Alipokuja kutua Chini hapakuonekana kuwa na binadamu Aliye hai.. Wote walikuwa wapo chini wametambarajika katikati Ya madimbwi Ya damu... Mohamedi akatabasamu na kumpa Dole Gumba, Revina naye akafanya hivyo... Wote wakainuka na Kuondoka katika Namna ya kila mmoja na Njia Yake. Mudy hakutaka kurudi pale Hotelini bali aliondoka kupitia Mlango wa Nyuma huku Revina Akirudi Chumbani kwake kwa maandalizi fulani ambayo alitaka kuyafanya kabla Hajaondoka kwenda Kwao Rwanda Ndani Ya Siku Inayofuata. Ulikuwa Muda wa Mapambano, Ulikuwa Muda ambao alitamani Kumwambia Mohamedi Ukweli Wote.. Muda ambao alitamani kurudi kwao Rwanda.. Akafungua mlango wa Chumba chake na kuzama ndani. Mbele ya Macho yake akawaona watu wawili
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 48

Akaufungua mlango na kuzama ndani.. Macho yake yakakutana na watu wawili waliokaa kitandani.. Walikuwa mwanaume na mwanamke.. Wote wakimtizama huku mikono yao ikiwa imekamatia bastola.. Revina akaonyesha kutokuwa na mashaka, akaingia kisha kuufunga mlango kwa ndani. Hakuonyesha kuogopa wala kuhofia.. Hofu kwake haikuwepo kabisa. Tabasamu tamu la mtoto wa kinywaranda liliupamba uso wke kana kwamba limetengenezwa mahususi. Akatembea kwa mwendo waKe wa kawaida.. Alionekana kuufurahia ugeni uliyomtembelea Chumbani kwake katika mtindo wa kumfumania. Bado watu wale walikuwa wakimtizama. Bado walikuwa wakiusoma uso na Macho Ya Revina.. Kile ambacho walidhani watakiona kwenye macho yake ndicho ambacho walikutana nacho. Macho yake mazuri kwa kuyatizama hayakuficha kuonyesha kuwa yeye alikuwa ni nani katika Dunia hii.. Hayakuficha kuuonyesha utaalam wake na pia hayakuficha kuwaambia watu wanaomchunguza kuwa yeye hakuwa mtu Wa kuogopa. Revina Akasogea tena na Tena.. Akawafikia karibu watu wale.. Wakajitahidi kutizamana hapa na pale.. Punde mlango ukasukumwa kwa nguvu mtu mmoja akaingia akipiga sarakasi na kuwahi kuizima taa.. Chumba chote kikawa giza.. Kila mmoja alikuwa ameruka na kuangukia upande Wake..

Ukimya wa Ajabu ukajitokeza ndani ya Chumba kile.. Ukimya ambao haukuwapa watu hata nafasi ya kupumua. Kila mmoja alikuwa sehemu yake, alikuwa akiwaza kuondoka pale.. Uingiaji wa kiumbe kile ulioendana na tukio la kuzimwa kwa taa za chumbani kilimduwaza kila mmoja huku Revina akionekana kuduwaa Zaidi. Alijua Mudy alishatoweka katika eneo lile, sasa ni nani aliyeingia chumbani mwake Ukiondoa watu wawili waliokuwemo mwanzo? Ni swali lake hilo ambalo lilimpa Hamu ya kumjua kiumbe Aliyeingia pale ndani.. Lakini hakujua njia gani atumie kumfikia mtu Huyo.. Akaona avute Subira, Subira Ambayo mwisho wake Ungekuwa kuondoka pale. Bado akiwa kwenye lindi la mawazo Huku macho yake yakiangaza kuitafuta nafasi yakuondoka pale. Akausikia mlango ukisukumwa.. Punde akamuona mtu mfano wa kivuli akiingia.. Uingiaji wa Mtu huyu wa pili kulimburudisha Sana Revina.. Uingiaji ambao hakuwahi kuuona hapo kabla. Ingawa kulikuwa na giza na uingiaji wake kuwa mfano wa kivuli, lakini katika macho Ya Revina alimtambua mtu Yule kwa Mapema Sana.. Alimtambua kutokana na kutambua kuwa hakuna mwingine Mtaalam Zaidi Yake.. Alikuwa Mohamedi, Alikuwa Mudy Akiwa amerudi kivingine. Hakuonekana kuwa na papara wala kuhofia kitu. Alionyesha kuingia kanakwamba anaingia Chumbani kwake. Kwanini aingie mfano huu na watu waliopo humu ndani wasimshuti? Kwa nini Arudi hapa Chumbani kwangu wakati Alishaondoka? Wakati akiwaza hilo kukatokea kile ambacho kiliendelea kumsisimua na Kumshangaza.. Mudy Akamuita Revina Kisha kumuita Jenifer.. Hapo ndipo alipogundua kuwa Mohamedi alikuwa na Watu wengine tofauti wanaomsaidia bila kujulikana. Hapo ndipo alipojua kwa nini alipoingia mwanzo watu wale hawakuonyesha matamanio Ya kupambana.. Wakati akiendelea kushangazwa na kinachotokea , taa ikawashwa na Chumba chote kuwa Cheupe. Revina akajikuta Akitizamana na Watu wanne.

Alikuwa Mudy, Jenifer, na Vijana wengine wawili ambao walikuwa ni wasaidizi waliotumwa na Rais kuja kumsaidia Mohamedi. Kati Ya hawa vijana wawili mmoja alikuwa ni Yule aliyekuwa akizozana na Jenifer katika Ukumbu fulani katika kutengeneza mazingira Ya Kumuondoa Mohamed, alipozungukwa na Maadui.

Baada ya wote kutambuana na kupeana mikono.. Wakatakiwa wotoke pale bila kuonekana. Wa kwanza kutoka alikuwa MOHAMED akifuatiwa na Kijana wake.. Akafuatia Jenifer na Mwisho kabisa Alikuwa Revina Na kijana Mwingine.

******

wakati Mohamed Akiondoka katika Hoteli hii pamoja na watu wake, upande wa pili kulikuwa na kikao kizito katika Hoteli fulani katikati ya Jijini la Arusha. Ulikuwa mkutano Uliohudhuriwa na Watu wate wazito katika masuala yao. Mkutano ulikuwa chini ya ulinzi mkali kupindukia. Hakukuwa na mtu yoyote kupita na Hata ulipopita ni lazima uwe Umepekuliwa na wapekuaji kuridhika. Kila aliyekuwa akipita alikuwa ni lazima akaguliwe na kuhojiwa.

Vigogo wengi waliopo kwenye mpango wa kupanga mapinduzi walikuwa kimya katika ukumbi huku kila mmoja akifikiria la kwake katika Moyo Wake. Wengine walikuwa katika Hofu kubwa kutokana na kilichokuwa kikifanywa na Mohamedi. Na Wengine walikuwa katika taharuki hasa kutokana na Mohamedi Kuwaua wenzao ndani Ya Makao Makuu Ya Polisi Mkoa Wa Arusha. Ukumbi ulikuwa Umetulia kila mmoja akimsubiria Mkuu wao. Punde wakasikia sauti Za Viatu virefu Vikiingia. Kila mjumbe akageuza shingo Kuangalia mlangoni.. Wote wakamuona Mwanamke Mrembo akiingia.. Hakuwa Yeye tu, bali alikuwa Amefuatana Mwanamke Mwingine Mrembo Kupindukia. Mmoja walimtambua kuwa ni Mmoja wao, Lakini Mwingine Hawakumtambua. Wote wakamkazia Macho kumwangalia msichana Yule mgeni katika kikao chao.. Kila mmoja alionyesha kuwa na Shauku Ya Kumjua na Kumtambua Mgeni Yule.
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 49

Wajumbe wote wakageuza shingo zao kumtizama mwanadada yule akiingia pale ukumbini. Wote walionekana kujenga maswali katika vichwa vyao.. Hawakuwahi kutambulishwa wala kuambiwa Uwepo wa Mtu huyu.. Mtu ambaye ameingia katika kikao kile kiliosheheni viongozi waandamizi Wa Serikali.. Msichana ambaye hakuonyesha uhatari Wowote katika kumuangalia kwao. Kwanini ameletwa hapa? Na kwanini hatuwahi kuambiwa uwepo wake? Huyu ni nani? Yalikuwa maswali mfululizo yaliosumbua vichwa vya Wajumbe wa Kikao kile. Kila mmoja alikuwa na Shauku ya kumtambua na kumjua alikuwa nani katika kikao hiki nyeti kama Kile. Majibu Yote yalikuwa yakimsubiri mwenyekiti Wa Kikao.. Punde kidogo Mwenye kiti akaingia ukumbini.. Wajumbe wote wakasimama katika kuonyesha heshima kwa kiongozi Wao, lakini mtu mmoja hakuwa amenyanyuka na hakuwa akipiga makofi wala kusalimia kama Wajumbe wengine.. Huyu Alikuwa amekaa akitabasamu.. Na hata wajumbe wote walipokaa bado hakuonyesha kujali. Mwenyekiti akatembea kwa Mwendo wake wa kikakamavu.. Mwendo ambao aliupenda sana tokea alipokuwa Afisa wa ngazi Za Juu katika Jeshi la Wananchi.. Alikuwa mwanajeshi aliyefikia Cheo Cha Uluteni General.. Cheo ambacho kilimfanya kuwa Chini Ya Mkuu Wa Majeshi. Alipofika sehemu alipokaa yule mwanamke, Wakatizamana kwa Muda kisha Wajumbe wote wakashuhudia Mwanamke Yule Akisimama na kutoa Heshima ya kijeshi kisha kukaa tena.

Lilikuwa tukio lililowaburudisha Wajumbe wengi, ile shauku ya kumjua Huyu ni nani ikaongezeka. Kila mmoja alikuwa akiusubiri Utambulisho wa Mwanadada Yule kuliko hata walivyo usubiri Mkutano wao. Baada ya Utaratibu Wote kuwekwa sawa, mwenyekiti alisimama na kuanza kuelezea kila kitu kuhusu kilichotokea Huku akianza na Utamburisho.

'''Ndugu Zangu wajumbe wa kikao hiki. Nadhani kila mmoja anajua kwanini tumeamua kukutana hapa kwa muda huu. Nadhani kila Mmoja anatambua ni Ipi mipango Yetu iliyotufanya Wote tukutane hapa usiku Huu. Lakini kabla Sijaanza kuelezea kile kilichotokea hapa Arusha, kwanza naomba nimtambulishe kwenu Mpiganaji Wetu. Najua Wengini hamumjui mwanadada Huyu lakini hilo sio tatizo.. Huyu mwanadada Anaitwa Revina Michael. Ni mwanadada kutoka katika Shirika la Kijasusi la Rwanda. Huyu ni mwanamke mwenye record katika mapambano Ya kutumia Silaha, mikono na hata Yale ya Ana kwa ana. Ameshiriki mission nyingi za ukombozi wa afrika na Hata kufikia kutunukiwa Tuzo Ya Ushujaa na mshindi wa Tuzo Ya Nobel Kwa Afrika Askofu Desmond Tutu. Kwahiyo nadhani Huyu atakuwa bega kwa bega katika kusaidiana na Vijana wetu kuhakikisha kuwa Mohamed hafiki popote na Lengo letu la kuipindua Serikali hii linafanikiwa.

Tukiachana na Suala la mwanadada Huyu ambaye naweza kumuita shujaa Wa Afrika. Kingine kilichotukutanisha hapa ni kuzungumzia kuhusu mipango Yetu na Wapi ambapo tumefikia kwa nchi wahisani kutuongezea pesa Zaidi ili tuweze kufanyakazi Yetu Vizuri. Wote tunatambua kuwa Tupo katikati ya Mipango Yetu na nchi Nyingi za Ulaya Zimeonyesha kutuunga mkono katika mpango huu. Kwa kutambua hili, kila mjumbe ambaye Ni Kiongozi katika Serikali hii anatakiwa kuwa makini na kunusa kila neno ambalo litaonyesha kuwa na ukakasi katika Safari Hii Ya kimapambano.

Natambua wote tupo katika nia moja, nguvu moja na lenge moja.. Nilazima tusimame tupambane. Ni lazima tuhakikishe Mohamedi Anazuiwa na Kufutiliwa Mbali katika Uso wa dunia Hii.. Ahsanteni kwa kunisikiliza. Nawatakia Mapambano mema na Mipango thabiti katika kulipigania Hili.'' Alimaliza mwanaume Yule kisha akasimama na Kuanza kutoka Nje.

*****
wakati Viongozi wale wakiwa katika kikao katikati Ya Mji wa Arusha.. Huku Upande Wa Pili Mohamed Alikuwa yupo hatua kadhaa kutoka Jengo ambalo lilikuwa likifanyikia Kikao kile. Alikuwa amesimama Sehemu ambayo ilikuwa vigumu kuonekana na mtu kutokana na mavazi ambayo amevaa.. Sauti Kutoka ndani Ya kikao kile alikuwa akiisikia kwa ukaribu zaidi kutokana Na Revina Kuingia Kikaoni Akiwa na vinasa Sauti vidogo mfano wa sindano za kushonea nguo. Sauti ya muongeaji mkuu katika kikao kile haikuwa ngeni masikioni Mwake. Ilikuwa Sauti ambayo alikuwa akiisikia kila siku.. Sauti ya KiongozI Ambaye alikuwa na Dhamana kubwa Katika nchi.. Ilikuwa Sauti Ya Waziri Mkuu. Mohamedi bado hakutaka kuliamini lile.. Akataka kupata Uthibitisho kutoka kwa Jasusi Mwenzake:. Jasusi ambaye alionekana kukubaliwa upande wa pili. Kuisikia Sauti Ya Waziri Mkuu Katika kikao chenye malengo ya hatari kama kile, kilimpa hamu Mohamedi ya kukutana na Waziri mkuu kwa Njia Yoyote. Akaondoka katika Eneo lile katika Uondokaji wa Aina yake.. Alitembea kama babu wa miaka themanini.. Alikuwa amekamata Mkongoja huku Akionekana kutembea kwa Shida kubwa.. Wajumbe wachache Waliokuwa wakitoka hawa kumtupia macho na Hata kama wangemtupia bado Wasingemtambua kutokana na Mavazi Yake. Akaendelea kutembea katika Aina ile ile.. Wakati anataka kuupita uchochoro fulani, akajikuta akivamiwa na WATU, Ghafla Akausikia Ubaridi Wa Mdomo Wa Bastola Ukimgusa kichwani.. TULIA MPUUZI WEWE!
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 50

Akahisi kitu cha baridi kikimgusa kwenye paji lake la uso.. Ulikuwa mdomo wa bastola. Akasikia sauti nzito ikinguruma kutoka nyuma kwake.. TULIA MPUUZI WEWE..

Mohamedi akatulia, alitulia katika namna ya kumpa nafasi aliyemshikia bastola aamini kuwa Hakukuwa na madhara. Ndicho kilichotokea... Watu wale waliamini hakuwa mtu hatari kwao kwa kule kujilegeza na kutii kwake.. Wakalegeza mikono yao.. Wakajisahau kuwa waliambiwa wasimuamini mtu katika Eneo hilo. Wakasahau kuwa waliambiwa wamshuti kila mtu ambaye atapita eneo lile. Wakamuacha kumpa nafasi, walijua ni mzee asiye na madhara.. Hakuwajua kuwa walikuwa wakicheza na kifo.. Hawakujua kuwa walikuwa wakicheza na mdomo wa Mauti.. Hawakujua kuwa Alikuwa Mohamedi, Mohamedi anayesakwa na kutafutwa na kamati ya mapinduzi.. Wakamuweka sawa kutaka kuhoji kwa nini yuko pale.. Hawakuipata nafasi hiyo, hawakupata muda wa kuwa tayari.. Wote walishangaa walipomuona mzee akipaa hewani mithili Ya chui, mshangao wao hawakuumaliza.. Wakajikuta wote wakipiga mweleka baada ya mapigo kadhaa kutoka kwa Mohamedi Kuwaingia sawia.. Hawakuweza kuamka kwa wakati kila mmoja alikuwa chini akiugulia maumivu.. Maumivu ya pigo moja takatifu kutoka kwa Mohamedi.. Hakuwapata nafasi hiyo.. Bastola yake ikakohoa mara nne.. Kikohozi ambacho kiliondoa roho za watu.. Alipomaliza kazi Hakusubiri washtuke, alichokifanya nikuondoke Eneo la tukio kwa kupitia njia ambazo Zisingekuwa Rahisi kugundulika. Akatokomea Mtaani huku akiwa na furaha ya kugundua nani alikuwa nani Nyuma ya Mauaji ya mke Wa Rais na Mpango wa kufanya mapinduzi..

Kwa mara ya kwanza alikuwa amepiga hatua kubwa sana.. Akatabasamu na kucheka kisha kutoweka kabisa tayari kwa maandalizi ya kazi Ya kufa na kupona.

******
wakati Mohamedi akipambana huku, Jenifer na kijana kutoka makao makuu DIDAS RUGIMBANA walikuwa katika mitaa ya jiji la Arusha wakiitafuta Nyumba yenye namba ambazo walipewa na Kepteni George kabla ya Kuuawa. Walikuwa wakitembea huku na huko kama wafanyavyo wapenzi.. Walikuwa wakishikana viuno na wakati mwingine hata kushikana mikono na kubusiana. Kila aliyewaona ama kukutana nao alihisi ni wapenzi.. Wapenzi ambao wanapendana sana. Licha ya kile ambacho walikuwa wakikifanya, lakini bado macho Yao hayakuchoka kutizama kila Jengo lililopo mbele yao.. Wakiwa umbali mfupi kutoka Ulipo ukumbi wa Triple A macho Yao yakakiona kitu ambacho walikuwa wakikitafuta. Ilikuwa Nyumba yenye namba husika. Lilikuwa jumba kubwa sana, jumba ambalo lilizungushiwa ukuta mkubwa ulionakshiwa na Marumaru zenye mfano wa Madini Ya Tanzanite. Ukiondoa hilo, jumba lote lilikuwa limepandwa miti mirefu ambayo ilisababisha uwepo wa Giza Nje ya Jumba lile na ndani Yake.

Nje hapakuonekana na mlinzi au walinzi wa aina yoyote.. Sehemu yote ilikuwa kimya kupindukia. Sehemu yote hapakuonyesha dalili ya kuwepo kwa watu na hata kuishi kwa watu sehemu ile. Jenifer na Rugimbana wakaendelea kuliangalia jumba lile kwa namna ya kutokuwa na Hofu huku wakati Mwingine wakiendelea kukifanya kile walichokuwa wanakifanya ili kuwapoteza Maboya watu ambao wangewahisi ama kuwashtukia. Wakiwa wamelipita jumba lile wakiendelea na safari Yao, mara waKayaona magari Mawili yakitoka katika Jumba lile na kuwapita kwa Mwendo wa kasi Huku ndani Yake wakionekana Watu kibao ambao kwa kuwaangalia tu mavazi Yao, ungejua tu wale ni Special Force.. Lakini Kwa nini wametoka katika jumba lile? Wanahusika vipi na Jumba Hili? Ni mawazo Yaliyopita katika vichwa vyao na kusababisha kupatwa na Hamu kubwa ya kukijua kile ambacho George alikiona mpaka kufikia kuwatuma Wao... Jenifer Akamuangalia Rugimbana kwa Mara Moja, Rugimbana naye Akafanya Hivyo.. Punde kila Mmoja akaingia Upande wake.. Wote walikuwa wakirudi katika jumba lile... Jumba ambalo lilionyesha kuwa na Siri kubwa. Kila mmoja alikuwa ameishikilia bastola yake Mkononi.. Wakati Jenifer akinyata kuelekea kwenye Uzio Wa Jumba lile, kwa mbali Macho yake yakawaona watu wawili wakiwa wamelala Chini.

Ulalaji wao haukuonyesha uhai kabisa.. Akawasogelea watu wale kwa tahadhali Kubwa.. Alipowafikia alishangaa akiwaona wakivuja damu huku wakiwa na matundu Ya Risasi vichwani mwao.. Jenifer akainama na kuugusa mwili wa Marehemu mmoja.. Akaukuta mwili ukiwa Wa Moto Kuonyesha kuwa Muuaji hakuwa mbali na Sehemu Ile. Akaongeza Umakini na kuzidi kutambaa kuelekea kule.. Hatua kumi mbele alikutana na Maiti Wengine wawili.. Hawa walionekana kuvunjwa Shingo. Hisia kuwa Mohamed ndio aliyeifanya kazi ile Zikaanza kumjia Jenifer.. Aliutambua Uuaji wa Mohamed.. Lakini hakuwa na uhakika wa hilo. Akaongeza Umakini huku akiendelea kutembea Nyuma ya Uzia Wa lile Jumba. Mbele kidogo akamuona mtu.. Mtu ambaye alimfahamu sana... Mtu ambaye alikuwa akiuruka ukuta wa jumba Lile.. Ukuta ambao ulionekana kuwa na Nyaya Nyingi na Hatari Sana Za Umeme.. Hakuwa Mwingine Bali alikuwa Mohamedi.. Tabasamu likachanua Usoni kwa Jenifer hasa pale aliposhuhudia maiti Nyingi Zikiwa Zimelaliana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…