Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

Hawakujua kuwa Neema ameshakufa na hawakuwa na habari katika hilo. Ilikuwa safari ya kuelekea Johnesburg hotel sinza. Kila kitu katika mwili na akili yake vilikuwa kwenye utimamu. Utimamu wa kuamua kile ambacho alitaka kukifanya. Bastola zilikuwa sehemu mbali mbali katika mavazi yake. Aliutumia muda mfupi kuondoka katika ya jiji kuelekea Sinza. Hakutaka kumuacha mtu katika mission hii. Kila mtu ambaye angemuhisi basi nilazima angeondoka. Jiji lilikuwa kimya kutokana na kilekilichokuwa kikiendelea. Alipita sehemu ngumu zenye mapambano makali. Hapo Moyo wake ukarudi katika kuamini kuwa Jenipher bado alikuwa akipambana. Jenipher bado alikuwa akiipigania Tanzania Yake. Hakuhitaji kuchelewa, alikuwa na kisasi na Carl Jack. Kisasi cha kumuua Ummu Sammy kinyama. Muda mfupi baadae alikuwa akishuka sinza umbali wa mita mia mbili kutoka ilipo hotel. Akatembea kwa Miguu bila wasiwasi. Kutokana na Eneo lote kuwa kimya hakuuona wasiwasi. Alitembea kana kwamba hakuna chochote. Alipoingia ndani ya Hoteli akalakiwa na tabasamu mwanana kutoka kwa mhudumu wa hoteli Ile. Tabasamu ambalo alilijibu kwa tabasamu kabla hajamuuliza kuhusu ujio wake pale.

Kwa kuwa alikuwa na maelezo yote kuhusu alipo Badest Man hakuchelewa kuruhusiwa. Akazikwea ngazi kwa umakini mkubwa. Mikono yake myepesi ilikuwa tayari kuzifikia silaha zake kwa nukta moja. Akamaliza kukwea ngazi kisha akaingia sehemu ambayo kulikuwa na Korido ndefu. Hapo umakini ukaongezeka. Akaongoza mpaka kilipo Chumba Alichoambiwa ndimo alimo Badest. Akasimama hatua tano Nyuma kisha kutizama kulia na kushoto alipoona hakuna Hatari Yoyote akaamua kurudi mapokezi kwanza. Alitaka kurudi mapokezi ili aonekane ametoka ili iwe rahisi Kurudi Kwa kupitia njia nyingine. Hilo likafanikiwa, Muda Mfupi alikuwa nyuma ya Ua wa Hotel akitizama jinsi ya Kuingia ndani. Akiwa hapo akitizama huku na kule ndipo alipoona kivuli kama cha mtu kikizunguka Eneo fulani katika uzio wa Jengo lile. Wakati akiongeza umakini akamuona mtu mwingine akiruka uzio wa Hotel na kuangukia ndani. Mohamed akatulia, alikuwa ametulia huku mkono wake ukishuka paka sehemu ilipo bastola yake. Bado watu wale walionekana kutulia hata baada ya kutua. Mohamed naye hakutaka kuwahi katika hilo. Akaupa moyo wake subira katika kukabiliana na kilicho mbele yake. Punde akauona mlango wa Siri Wa hotel ile kufunguliwa. Kufunguliwa kwa Mlango ule kukafuatiwa na Mwanamke kutokeza. Mwanamke aliyekamatia Bastola mkononi. Alikuwa ni mwanamke yule aliyemkuta mapokezi, alikuwa ni mwanamke yule mhudumu wa hoteli. Akatulia kwa muda akiangalia kile ambacho kinataka kufanyika. Hakujua kuwa ndani kulikuwa na mtu ambaye kuuawa kwake kilikuwa kitu cha kawaida. Watu wale wakaongea machache bila kutambua uwepo wa Mohamed. Hata pale mlango ulifunguliwa zaidi na watu wale kuingia ndani, bado Mohamed aliendelea kutulia kwa kuwa wakati yupo pale alikiona kivuli cha mtu. Mtu ambaye aliendelea kutulia pale hata baada ya watu wengine kuingia ndani wakitumia mlango wa uani. Akataka kumjua alikuwa nani. Punde akamuona Kijana wa kizungu akitokea katikati ya giza totoro na kuruka katika namna ya kipekee na kuingia ndani ya Hoteli. Ulikuwa urukaji uliosisimua na kuamsha Moyo wa mapigano. Urukaji ambao hutumiwa zaidi na watu ambao ni hatari. Mohammed akatabasamu, hatua ya pili alikuwa akiuparamia uzio na kutua ndani bila kutoa kishindo wala ukelele. Kutua hapo akaongoza mpaka nyuma ya vyumba vya hoteli hiyo. Hapo akasikia minong'ono, minong'one kutoka ndani chumba kimoja, punde akaisikia sauti, sauti za mahaba zikihanikiza katika chumba kimoja wapo. Watu walikuwa katika kile ambacho kilimshangaza Mohammed. Nchi ilikuwa katika hatari huku milipuko ikitanda katika jiji zima lakini watu hawakuwa wakiogopa, watu hawakuhofia, walikuwa wakiiburudisha Miili yao, Walikuwa wakiiburusha katika namna ambayo ilikuwa Ya kipekee. Hawakuogopa milipuko wala Risasi. Mwanamke alikuwa akihanikiza katika aina ambayo hata uwe mgumu vipi lazima ungesimama na kutega sikio. Alikuwa akilia kama ameonewa, alikuwa akilia kanakwamba anaadhibiwa. Mohammed hakusumbuliwa na hilo, akalipita Dirisha na kusonga mbele, hatua nne mbele akasikia minong'ono mingine, minong'ono ambayo ilikuwa tofauti na pale mwanzo. Hii ilikuwa Minong'one ambayo haikusikika kabisa, wakati Muddy Akiendelea kusikiliza kwa Umakini akahisi kama miguu ya mtu kutokea ndani ikielekea nyuma alipo. Vishindo vya mtu huyu vikamfanya ajiandae kwa pigo la Maana. Vishindo vya miguu bado vizidi kusogea, muddy akahesabu hatua baada ya Hatua, Lakini kinyume cha alivyotarajia vile vishindo vikakoma. Kukoma kwa vishindo kukaongeza umakini, umakini katika kufanya kile ambacho kilipaswa kufanya. Punde akamuona mwanadada Yule wa mapokezi akitokea, lakini kabla hajaamua kipi Cha kufanya, tukio la kutisha likatokea mbele ya Macho yake pale alipokiona kichwa cha binti kikisambaratika na Ubongo kusambaa sehemu Yote. Risasi ilikuwa imefanyakazi Yake, tena mbele ya Macho ya Mohammed.. HALI ILITISHAAA
 
nilipenda mnipe muda ili kuandaa vipande vingi zaidi. Huku kuitana humu tutasoma kipande kimoja kila siku. Natambua kiu yenu lakini mtakapo nipa muda basi jioni nitakuja na VIPANDE VINGI. Pia tutambue kuwa kuna wakati lazima niende kuhangaika kwahiyo tuvumiliane
 
nilipenda mnipe muda ili kuandaa vipande vingi zaidi. Huku kuitana humu tutasoma kipande kimoja kila siku. Natambua kiu yenu lakini mtakapo nipa muda basi jioni nitakuja na VIPANDE VINGI. Pia tutambue kuwa kuna wakati lazima niende kuhangaika kwahiyo tuvumiliane
Poa ibraa wacha tuvumulie wanajukwaaa tuvumilee bibiye shunie kuwa mpolee na ww biibiye sohwa kuwa mpolee tufanye subira ilopitilizaaa
 
Hongera sana,Japo umenikwamisha kufanya happa kazi ,ila poa tu liwalo na liwe ,Twenzetuuuu
 
nilipenda mnipe muda ili kuandaa vipande vingi zaidi. Huku kuitana humu tutasoma kipande kimoja kila siku. Natambua kiu yenu lakini mtakapo nipa muda basi jioni nitakuja na VIPANDE VINGI. Pia tutambue kuwa kuna wakati
lazima niende kuhangaika kwahiyo tuvumiliane

Sawa mkuu
 
MKE WA RAIS

Ilikuwa ni mbele ya macho ya Mohamed. Mwanamke yule akaanguka chini ubongo ukiwa umetapakaa kila sehemu. Hapa kusikika mlio wa risasi wala hapakuwa na kelele. Palikuwa kimya kanakwamba hapa kuwa na watu sehemu ile ya hotel. Hata yule mwanamke ambaye alikuwa akihanikiza alikuwa kimya, hapakuwa na hata mnong'ono. Sehemu yote ilikuwa imezizima. Haikuwa Ishara nzuri kwa mpiganaji wa aina yake. Hakutaka kuchelewa mauaji zaidi ya fanyike. Akajibinua samosoti na nakuangia ndani ya Jengo. Kutua chini kukaambatana na kukaribishwa na maiti za watu wawili waliolala katika dimbwi la damu huku wamechinjwa vichwa. Ulikuwa ni wakati mgumu, wakati ambao ulihitaji mapambano ya kweli. Kichwa chake kilivurugika katika maswali, kwanza kuuawa mke wa Rais, pili mawaziri kadhaa akiwemo waziri mkuu. Likaja la ndege za kivita kuharibu makazi. Sasa alikuwa akiangalia miili ya watu waliochinjwa. Kuna nini katika hili, kuna nini katika kifo hiki cha mke wa rais? Alifanyaje? Aliwakosea kipi? Alikuwa mmoja kati ya wanamapinduzi? Hapana kuna kitu hakipo sawa. Ulikuwa ni muda wa kukitafuta hicho kitu ambacho kilifichwa.

Bastola mkononi katika giza totoro na ukimya wa hali ya juu, harufu ya damu ilisikika katika matundu ya pua. Kila alipokuwa akipiga hatua ndivyo alivyozidi kukutana na Unyama huo. Mbele kidogo akakiona tena kivuli, kivuli cha Badest Man. Akajiandaa latika kile ambacho kingetokea, kile ambacho alikitegemea. Hakufanikiwa katika kuupa Uhuru mwili wake. Akashangaa kumuona mtu akimjia katika aina mbalimbali ya mapigo, mapigo ambayo yalikuwa yakichanganywa na kuonekana kama ni kitu kipya machoni kwa Mohammed. Akajikuta akiruhusu Mapigo kadhaa kuingia katika mwili wake na kumtupa Chini. Hakuchelewa kuinuka, lakini hata alipoinuka akajikuta mateke manne kutoka kwa Badest Man Yakimtupa Chini kwa mara ya pili. Sasa Mohammed aliamua kumkabili kiume. Ngumi zikapigwa kwa kila aina ya Ufundi na ujuzi, kila mmoja alitumia kila kitu alichotoka nacho huko alipokuwa. Wote walikuwa wakienda pamoja pale walipokuwa wakitupa mateke. Hata walipokuwa kwenye makonde kila mmoja alikuwa mtamu katika hilo. Wakawa saresare, wakawa kama mapacha katika kufanana, hawakufanana kwa Sura, rangi wala tabia. Hawa walikuwa wakifanana katika kupigana. Mapigo Yao yalikuwa katika usawa.

Kila mmoja alikuwa ameshangazwa na hilo, nikatika kuangaliana likatokea la Kutokea. Hapakuonekana kuwepo kwa mtu mwingine lakini kilichoshangaza ni pale Mohammed alipomuona Badest Man akianguka kama mzigo huku damu zikionekana kumtoka kwa Wingi. Wakati Mohammed akiwa hajajua kipi afuate akamuona mtu akitokea katika giza totoro. Akitokea mfano wa kivuli kutokana na mavazi
yake aliovaa. Akainua uso kutazama vizuri. Akajikuta akitizamana na Jenipher. Wakakumbatiana kwa Nguvu kila mmoja akionyesha kutokuamini macho yake. Nikatika kumbatio hilo Mohammed alipoamua kumwambia ukweli kwamba Ummu Sammy Hawakuwa naye tena. Hakuna kingine walichokiongea, kila mmoja alikuwa na Uchungu. Muda mfupi walikuwa ameshaachiana na walishaondoka katika Eneo lile. Ulikuwa usiku mgumu sana kwao, ulikuwa usiku ambao haukuwa na Raha. Kila mmoja alikuwa kimya akifikiria kila kitu. Kitu kimoja ambacho walijivunia ni kitendo Cha Mohamedi kuichukua simu ya Neema. Kila mawasiliano kutoka kwa watu wake yalikuwa yakiingia moja kwa moja. Hilo liliwasaidia kujua kuwa watu ambao waliingia nchini katika kukamilisha Kazi hii walikuwa majasusi Kumi. Hawa wote walifanya mawasiliano na Neema Kabla ya kuingia na hata baada ya kuingia. Kila kitu kilionyesha kutendeka kwa amri kutoka kwenye namba ambayo haikuandikwa jina zaidi ya Herufi VP. Kila walichokiona kilikuwa kimefanywa kwa Amri Ya mtu huyo akimtumia Neema kwa Ukaribu. Hilo ndilo likawapa hamu Mohamed na Jenipher, walichoamua nikuipiga ile namba kwa kupitia namba ile ile ya Neema. Licha ya kuamua hilo lakini Ugumu ulikuja pale ambapo hawakujua mawasiliano yao yalikuwa yakifanywa kwa Aina gani na kwa mtindo Upi. Hawakuta kuharibu wala hawakutaka kukurupuka.

Saa tisa Usiku iliwakuta kivukoni wakielekea kigamboni wakiwa hawatazamiki. Kwa kuwa watu hawakuwa wengi kwenye pantoni waliingia na kwenda kukaa pembeni kabisa kuruhusu kumuona kila mtu ambaye alikuwa akiingia ndani ya Kivuko. Kila mmoja macho yake yalikuwa yakifanyakazi, kila mmoja macho yake yalikuwa yakimuangalia kila aingiaye. Punde wakakiona kitu ambacho kiliwavutia, kitu ambacho kiliisisimua miili yao. Macho yao yaligota kwa watu wawili waliokuwa wakiingia ndani ya kivuko. Licha ya watu wale kujibadilisha sana lakini hawakuweza kupotea machoni kwa Mohamed. Mwanaume aliyekuwa akiingia alikuwa ni CARL JACK jasusi kutoka CIA akiwa sambamba na mwanamke ambaye Muda mfupi uliyopita Alimuona Sinza katika Hotel Moja.
 
Back
Top Bottom