Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

Akamuona mtu ambaye hakutaraji kumuona pale. Bastola ikawa tayari mkononi mwake, akaanza kuipiga hatua moja baada ya nyingine kuelekea kule alipoelekea yule mtu. Kilikuwa kitu cha kushangaza kumuona Carl Jack akiwa katika eneo lile. Carl Jack aliemtoroka muda mfupi uliopita pale Landmark ubungo. Akaanza kumfuata kwa nyuma kwa tahadhari kubwa, akatembea na kutembea, milipuko haikumshtua tena, akauvuka Ukuta wa jengo mmoja kubwa, akatokeza katika kichochoro ambacho hakuwa na Imani kuwa kingetokea kwa mbele. Wakati anaingia katika kichochoro kile akahisi kitu, kitu ambacho alipenda sana kukiheshimu. Hisia zake zilimwambia hakuwa peke yake. Hisia zilimwambia kuna watu wanaofuatilia kila alipokanyaga. Akataka kuziamini Hisia, hisia ambazo hazikuwahi Kumuangusha. Akageuza Shingo kwa Chati kutizama alipotoka. Hapo akatabasamu baada ya kuwaona watu wasiozidi watatu wakiwa Nyuma yake. Hapo ndipo alipoamua kufanya kile ambacho alitakiwa kufanya. Sekunde ya kwanza alionekana akiingia katika uchochoro ule, na Sekunde ya pili alikuwa nyuma ya watu wale waliokuwa wakimfuatila. Kwa mwendo wa kinyonga na kasi ya kuruka mfano wa chui akamkamata Mmoja kisha kumnyonga Shingo. Mtu yule akatambarajika na kutulia. Akamlaza chini kisha akaendelea na safari ya kumtafuta wa pili. Haikuwa shida kumkamata wa pili.

Akafanya kama alivyofanya mwanzo, mpaka anawamaliza hakuwa ameshtukiwa. Wakati anakimaliza kile kichochoro ili kutokea mtaa wa pili, akasikia kama sauti Dhaifu ya mtu anayemfahamu ikimuita. Kilikuwa kitu kilichomshangaza na kumfanya atulie kama sekunde mbili kusikiliza kwa umakini. Punde sauti ile ile ikarudia tena kumuita, Hapo ndipo alipotambua kuwa aliyekuwa anamuita hakuwa Mwingine Bali Ummu. Lakini udhaifu wa Sauti yake ulimpa mashaka Mohamedi, mashaka ambayo yalijenga maswali Lukuki Kichwani kwake. Alimjua Ummu na aliujua Ushupavu wake. Lakini kwa nini anamuita katika sauti hii ya ukataji tamaa? Akageuka kuifuata sauti ilipotokea. Hatua kumi mbele akakutana na kitu ambacho kilimshtua. Akahisi mwili wake ukipata ganzi na kuhisi kutetemeka. Mbele ya Macho Yake alikuwa akishuhudia Tukio la kutisha na kuogopesha. Tukio ambalo lilimuacha Mohamed Katika machozi. Machozi yakautawala uso wake, muda mfupi Mohamed alikua akiangusha Machozi. Mbele yake ulikuwa umelala mwili wa Mpiganaji mwenzake Ummu Sammy Ukiwa katikati Ya Dimbwi la Damu. Utumbo ulikuwa Nje Huku kifua chake kikiwa hakitazamiki. Hakuonyesha kuwa haukuwa na Uhai, akausogelea na kuuinamia kisha kuinua upande wa kichwani. Alikuwa akiangaliana na kitu cha kutisha kama sio kushtua. Kitu ambacho hata uwe jasiri Vipi huwezi kuvumilia. Akaukuta uhai wa Ummu ukiwa kwa mbali, alikuwa akipumua katika hatua ya Mwisho. Mudy akatamani Kuongea kitu lakini sauti haikuweza kutoka. Akashuhudia Ummu Sammy Akiilaza Shingo pembeni na muda ule ule akatulia.. Alikuwa amekufa mikononi kwa Mohamedi. Chozi likaendelea kudondoka pale alipokuwa akiutingisha mwili wa Ummu. Aliendelea kuutingisha huku akiita Jina lakini bado ukweli haukubadilika, Ummu alikuwa ameshafariki Dunia. Muddy Akamlaza chini kisha kwa Upendo akalibusu paji La Uso la Ummu. Akainuka huku bastola mbili zikiwa mikononi. Kifo cha Ummu hakukitarajia. Sasa ulikuwa ni Muda wa kupambana. Muda wa Kumtafuta Carl Jack. Alijua alikuwa Yeye, alikuwa yeye aliyemuua Ummu. Akaapa na Kujiapiza kuwa lazima alipe kwa kila aliyehusika na Mauaji ya Ummu Sammy.

******

Wakati mapambano yakiendelea kupambano Moto, Upande wa ule Ujumbe wa mkutano ulikuwa umefanikiwa kutoroka na kuingia katika ndege moja ya kijasusi na Safari Ya kukimbia Nchi ikianza. Walikuwa wameshakubali kushulindwa kwa Wakati ule. Na walikuwa wakiondoka Nchini kwenda kujipanga. Walikuwa wamefanikiwa kutoroka kwa kusaidiwa na Majasusi Wa CIA NA KGB. wakaiacha Anga ya Tanzania wakiwa katika Hofu kubwa. Hofu ambayo ilikuwa miongoni mwa vitu ambavyo vilimsumbua kila Mjumbe. Ingawa walikuwa ndani ya dege la kivita lakini bado hawakujiamini. Bado waliendelea kuogopa kuingia mikononi Mwa Serikali. Dege likapotelea huku nyuma likimuacha Mohamed katika maumivu makali. Alishampoteza Ummu na mpaka M*da huo hakuwa anajua Wapi Jenipher alipo. Wakati akiendelea kutembea hapa na kuingia pale akaisikia Simu ya Marehemu Neema ikitoa mlio kuonyesha kuwa kuna ujumbe Umeingia. Akaitoa simu mfukoni na kuufungua Ujumbe. Akakutana na Lugha ile ile ya kijasusi, huu ulikuwa Ujumbe kutoka kwa Mtu mwingine. Huyu Aliseviwa kama Badest Man. Ulikuwa ujumbe wa kumtaarifu Neema wapi alipo. Kwa kuwa Mudy aliitambua Lugha ambayo hutumiwa na majasusi wengi, akaamua kumjibu kuwa anamfuata hapo hapo hotelini. Moyoni Akatabasamu baada ya kujua kuwa majasusi wengi hawaJui kwamba Neema Mtobwa Alikuwa ameshauawa, Hivyo akapanga kuitumia Simu ili kumpata Carl Jack ambaye amehusika kuiondia Roho ya Ummu. Safari ikaanza
 
Back
Top Bottom