Riwaya magnum22

Riwaya magnum22

Kulubule
Uraibu wa Magnum 22 unanimaliza, haya maumivu nayoyapata si yakitoto mkuu!
Weka sehemu inayofuata mkuu watu tumalize wikend vyema!
 
Amata ga imba. Mojawapo wa waandishi wa riwaya nao wapenda sanaa...mojawapo ya riwaya zake pendwa kwangu..

Harmunaputra. Mji wa kale uliopotea

Msitu wa solondo

Romeo & julieth
Dracula
Escrow
Na nyingine kibaoooo tu. Riwaya zake.

Baada ya kucomment. Ngoja sasa nianze kusomaa hiibriwaya tafadhari. Mleta riwaya hii. Utume yoteee usiiache bila kuisha. Kama MJUKUU WA CHIFU anavyofanya.
 
Jamani hii riwaya mm kila muda naingia kuona kama imewekwa lakini naona kimya tu toka jana
 
Nilimtafta asubuhi Kulubule akadai yuko site na hana bundle akaniahidi jioni atatupia kigongo kinachofuata! Hvyo tumvumilie tu ila nadhani kuanzia mda huu na kuendelea anaweza kutupa mzigo!
 
Basi ngoja tuvute subira mkuu!...
 
MAGNUM 22

Sehemu 21

ADDIS ABABA – ETHIOPIA
SIKU HII TOFAUTI NA SIKU nyingine zote, pambazuko lake lilikuwa na mikiki mikiki mingi, wapo ambao hata hawakujali nini kinatukia siku hiyo, wengine hawakupata hata lepe la usingizi kwa kile ambacho walijua kinaweza kutokea, na hawakupenda kitokee, hawa hawakuwa wengine zaidi ya wanausalama wa taifa hilo na nchi nyingine za Afrika.
Vikao vilivyofululiza kwenye taasisi mbali mbali vilikuwa vikizungumzia swala hili; kikao cha kamati kuu ya AU pamoja na usalama wa viongozi hao kufuatia mauaji yliyotokea Angola, Ivory Coast na kukoswakoswa kwa mwenyekiti wa umoja huo, rais wa Gambia alipokuwa katika moja ya vikao vidogo vya umoja huo jijini Dar es salaam. Katika moja ya agenda ambazo zingezungumziwa katika kikao hiki cha kamati kuu, ni pamoja na kulifikisha katika muafaka swala la kuimega Somalia na kuwa mataifa mawili kama ambavyo watu fulani walitaka, na kwa kushinikiza hilo waliamua kufanya mauaji ya viongozi wa umoja huo.
Katika kikao hiki, kulitegemewa ugeni mkubwa wa tajiri mkubwa Afrika Bwana Jaffer Bakhari, aliyekuwa akitajwa na kila chombo cha habari duniani kuwa ni chanzo cha machafuko huko Somalia na mauaji ya viongozi wa Afrika. Katika kikao hiki alitakiwa kufika kwani agenda mojawapo ilimhusu yeye na Somalia yake.
Katika moja ya majengo nyeti ya serikali Mtaa wa Eritrea, kikao cha baraza la usalama la AU kilikuwa kikimaliza mkutano wake alfajiri hiyo.
“Ulinzi utatakiwa uwe mkali sana kama tulivyoamua, na wapelelezi wetu wahakikishe wanaiweka Addis katikati. Hawa washenzi hawatakiwi kupenya sehemu yoyote ile kuingia ndani ya jiji hili kwa maana madhara yao tunayajua…” alizungumza mwenyekiti wa baraza hilo wakati akifunga kikao.
“Samahani mwenyekiti, kama sijasahau, mjumbe wa Tanzania alisema wao wataendelea na sakata la kumsaka huyu au hawa wauaji kwa sababu walifanya tukio hilo ndani ya ardhi yao, swali ni je, huoni kuwa kama watafika hapa watavuruga upelelezi wetu?”
“Yule bibi aikuumize kichwa, hana lolote si yeye wala idara yake, nashangaa sana kwa nini AU iliwaamini kiasi hicho, lakini sasa wameona, wameshindwa…”
“Mwenyekiti, mpaka sasa tunajua Tanzania na idara yake imefikia wapi katika uchunguzi huu? Si ajabu wakawa mbele kuliko sisi, mimi nafikiri tyumhusishe mpelelezi mmoja wan chi hiyo kutoka idara yao ya kijasusi ili aungane na hawa wetu, tukifanya hivi tutafaulu…”
“Hakuna kitu kama hicho mjumbe! Mpaka sasa ninavyokwambia, mpelelezi wao wanaomtegemea amekwishakufa lakini wamefanya siri, na amekufa katika sakata hili hili,” akajibu kwa kumkata kauli mjumbe huyo. Wajumbe wa kikao hicho wakatazamana na kubaki na alama za kushangaa na kujiuliza; moja kiongozi wao kajuaje kama mpelelezi wa Tanzania amekufa? Na kwa nini wao hawana ripoti kama hiyo? Kwa sababu wao walichokuwa wakijua tu ni kwamba, idara ya ujasusi ya Tanzania imeshindwa kufanya kazi kwa wakati na kuwasilisha taarifa kwa muda muafaka, basi. Kwa ukimya ule mwenyekiti wa baraza akagundua kuwa amekosea kwa kusema hivyo.
“Sawa sawa wajumbe, tutaliongea hili katika kikao chetu cha jioni na mtapta jibu kama Tanzania itahusika au la,” akajaribu kuliweka sawa jambo hilo.
Hawa nao wakamaliza kikao chao na kutawanyika kadiri ya majukumu yao.
Mpaka kufikia saa tatu asubuhi hakuna hata mwanausalama mmoja aliyegundua uwapo wa Martin Gupter na kundi lake katika jiji hilo. Ijapowa upekuzi wa kina kwa kila mgeni ulifanyika lakini haukuza matunda.
“Wameogopa kuja!” mmoja wa makachero akamwambia mwenzake.
“Wanajua wakija watajichimbia kaburi,” mwingine akaitikia. Tayari Addis Ababa ilikuwa na pilikapilika nyingi siku hiyo kwa kuwa ni saa chache tu zilizofuata mgeni wa kwanza angefika katika nchi hiyo, hivyo tayari vijana walipangwa, dori kwa kutumia magari na helikopta zilikuwa zikifanyika.
* * *
Kutoka Sierra Leone, Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lungi, Kamanda Amata alifanikiwa kuabiri ndege ya saa saba usiku ya sirika la AIATA. Wakati wa safari yote hiyo alikuwa akiwaza tu ni jinsi gani atamtia mkononi Martin na kundi lake. Alijuwa wazi kuwa kuna timu iliyoundwa kwa ajili ya upelelezi wa watu hao, lakini yeye aliamua kutokuwaacha, bali kuhakikisha anawatia mbaroni au anawapoteza kwa mkono wake.
Saa mbili kamili asubuhi, ndege hiyo akakanyaga ardhi ya Addis’ kwa madaha na kuingia katika egesho lake, kisha wageni wakaruhusiwa kuingia katika jiji hilo. Miongoni mwa wageni waliofika asubuhi hiyo alikuwamo Kamanda Amata, akiwa ndani ya jinzi mpauko, shati la drafti nyekundu na nyeusi na kichwani mwake kofia kubwa ya pama, miwani ya kumkinga dhidi ya miale mikali ya jua ilitulia vyema machoni pake aghalabu ndevu bandia zilimfanya afanane na cowboy mmoja hivi. Kifuani mwake alining’iniza kamera ya kisasa kabisa, kama ungemtazama usingefikiria zaidi bali ungejua tu kuwa ni mwandishi wa gazeti fulani la kimataifa. Kwa uzoefu wa kazi yake aliweza kuwana makachero wengi uwanjani hapo, lakini wao hawakuweza kumgundua kirahisi labda kwa sababu hawakuwa na mpango naye. Nusu saa baade alikuwa katika hoteli kubwa ya Blue Moon, katikati ya jiji hilo. Hakutaka makuu zaidi ya kutulia kimya chumbani kwake na kupanga hili na lile kwa maana alikuwa akijua wazi kuwa viongozi wanaotegemewa wataingia nchini hapo siku hiyo na mkutano huo utachukua nafasi siku inayofuata.
* * *
‘Hakikisheni mnawatia mbaroni, wao watatu na wengine wapo hapahapa tunaendelea kuwalinda, mambo yakiwa tiki tu tunawapiga pingu. Msiwe na wasiwasi na mimi, mimi naendelea poa kabisa na naweza nikatoka hospitali muda wowote kutoka sasa. Chiba na Gina mfike Addis haraka iwezekanavyo, nafikiri kaka yenu keshafika huko, nendeni mkafanye yale mnayopaswa kutenda.’
Chiba wa Chiba alikuwa akikumbuka maneno ya bosi wake, Madam S, mara walipokuwa wakiagana katika hospitali ya jeshi ya Lugalo. Mwanamama huyu hatari kabisa katika medani za kiusalama alilazwa hospitalini hapo siku tatu nyuma baada ya kupata ajali mbaya ya gari katika makutano ya Barabara ya Morogoro na Bibi Titi. Mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa Amata kuwa ‘wanawatafuta’ wapo Ethiopia, akaamua kuongeza kikosi katika jiji hilo, hivyo TSA 2 na TSA 5 waliingia kazini.
“Tumefika!” Chiba akamwambia Gina. Gina akatupa jicho dirishani na macho yake yakapendezeshwa na mandhari ya kuvutia ya Jiji la Addis Ababa.
“Ni mara yangu ya kwanza kufika hapa,” Gina akamwambia Chiba.
“Safi sana nitakupeleka ukale injera,” akamtania. Injera ni chakula cha kienyeji katika nchi hiyo kama ilivyo kwetu ugali. Mara sauti ya kike ikawataka kufunga mikanda nao wakafanya hivyo tayari kwa kutua. Akaitazama saa yake, ikamwambia kuwa tayari imetimu saa sita mchana. Wakiwa katika harakati hizo wakapata tangazo lingine la dharura ya kuwa watasalia angani kama dakika arobaini na tano hivi ili kupisha ndege za marais wa Gambia na Afrika Kusini kutua.
“Kumekucha!” Gina akasema.
“Kwa vipi?”
“Sipati picha rafiki zetu jinsi wanavyohaha sasa kwa mapokezi hayo,” akasema akimaanisha wanausalama wa nchi hiyo. Baada ya saa moja hivi ndege ile ikatua katika uwanja huo mkubwa kabisa wa Bole.
“Kazi ya kwanza!” Gina akamuuliza Chiba mara baada ya kutoka nje ya uwanja huo.
“Kuweka mipango yetu sawa, tunatakiwa kufika katika shamba la kanisa la Orthodox, mambo yetu yote yatakuwa huko,” Chiba akamwambia Gina, na wakiwa katika mazungumzo hayo, gari moja, Toyota Pickup likasimama umbali wa kurusha jiwe tu utoka wao waliposimama. Ndani ya gari hilo kulikuwa na mwanaume mmoja aliyevali kanzu jeusi na msalaba mkubwa kifuani mwake, akafungua mlango na kutoka nje. Alipowaona tu Gina na Chiba, akainama kama ishara ya kuwasalimu nao wakafanya hivyo hivyo, moja kwa moja wakajua kuwa huyo ni mwenyeji wao wakaongozana na kuingia garini.
“Karibuni Addis!” yule bwana akawakaribisha huku tayari akikamata barabara ya kuelekea nje ya mji, “Naitwa Archemedius, kutoka Orthodox Church,” akajitambulisha.
“Asante sana,” nao wakajibu na kujitambulisha kisha mazungumzo mengine yakafuatia ambayo zaidi yalikuwa na kufahamiana na kujuliana hali. Baada ya mwendo wa takribani saa moja na nusu hivi, waijikuta nje ya mji. Yule bwana akaiacha barabara kubwa na kuchukua ile ya vumbi yenye mashimo na machanganyiko wa mawe na udongo. Kilomita moja mbele wakaingia kwenye wigo wenye kanisa kubwa sana mbele yao, gari likatembea taratibu mpaka ndani ya kijumba kimojawapo. Wakateremka na kuchukua mikoba yao kisha wakamfuata yule mwenyeji wao. Wakapita kando ya kanisa hilo na kukutana na ukuta upande wa nyuma, wakauzunguka mpaka upande wa pili ambapo palikuwa na mlango mdogo wa chuma. Yule kasisi akabofya sehemu fulani ya ukuta na sekunde kumi tu zilizofuata kijimlango kile kikafunguka, wakaingia ndani.
Ulikuwa ni uwa mkubwa sana, wenye maua mengi ya kupendeza, kwa harakaharaka utavutiwa na ukimya wake, hapakuonekana mtu, bali vipepeo tu vilivyokuwa vinaruka huku na huko. Archimedius, akawafikisha kwenye moja ya milango mingi na kuufungua, wakaingia na kujikuta kwenye kijichumba kidogo. Chiba akatazama harakaharaka na kugundua kuwa ilikuwa ni lifti, ikawateremsha chini kama mita kumi na mbili hivi, wakatoka na kupita koridoni mpaka katika chumba kingine.
“Karibuni sana!” Archimedius akawakaribisha kwa mara ya pili wakiwa wanajibwaga kwenye makochi ya kisasa kabisa yenye vono ya kuvutia, “Jisikieni mpo nyumbani, Madam S ndiye aliyeuagiza tuwafikishe hapa na kuwapa sehemu ya kuratibu kazi zenu, hivyo mpo sehemu salama sana. Hii sehemu watu hawaijui na wala hawajawahi kufika, kama mnavyoona ni kanisa ambalo hutumika kila jumapili na huko juu kuna monastery kubwa ya kimisionari ya Orthodox ya Mtakatifu Ilarius,” akawaeleza.
“Hapa tulipokaa kuna vyumba vitatu, hili siyo jokofu ni mlango wa chumba, ukibonyeza namba 0-7-7-3, utaingia chumbani,” akachukua rimoti mezani na kubofya namba hizo, kweli, ule mlango ukafunguka na ndani yake kulikuwa na kitanda kikubwa, meza ya kujiremba, na kabati moja la nguo, kiti kimoja na meza ya kusomea.
“Lakini ukikose na kubonya namba nyingine yoyote ile, utafungua jokofu na si chumba,” akafunga ule mlango na kubofya tarakimu nyingine hapo ukafunguka mlango ule ule lakini mara hii vilionekana vinywaji na matunda na vyakula anuai.
“Du! Hii nimeikubali!” Gina akajikuta anamwambia Chiba, naye akatikisa kichwa kuonesha hiyo ni ‘kali ya mwaka’. Yule kijana akawatazama Gina na Chiba na kuendelea kuwapa maelekezo, “Na chumba kingine ni upande huu, hilo hapo si kabati la vyombo, ni chumba na namba yake ni 7-3-2-0, kama mwanzo, ukikosea utakutana na mabakuli na vijiko. Na cha tatu ni hiki huku kwenye shelfu la vitabu namba yake ni 6-7-0-5. Kwa hiyo mkariri hizo namba, mambo yenu yote mtayafanyia hapa ndani, hakuna atakayewasumbua hata mimi tukiachana hapa hamtaniona tena, baada ya hapa njooni niwaoneshe jambo la mwisho,” akawachukua na kutoka nao kwenye ile korido, wakaifuata na kuingia kwenye lango kubwa, huko kulikuwa na eneo wazi kubwa lililoegeshwa magari mengi sana katika mpangilio wa kupendeza.
“Hapa ni maegesho, mkitaka kwenda mjini, mtachukua gari hapa mnayoipenda, funguo zipo ndani na ukifuata hiyo mishale itakutoa nje ya mpaka mjini, nimemaliza!” Archimedeus akamaliza kuwapa maelekezo na kurudi nao ndani.
“Samahani nilisahau jambo, mkimpata mwenzenu, mtamleta hapa, kazi yenu haitakiwi kupangwa nje ya chumba hiki, kwa maelekezo niliyopewa,” akamaliza na kupeana nao mikono kisha wakaachana. Gina na Chiba wakarudi ndani ya kile chumba na kuufunga mlango, kila mmoja akajaribu rimoti kufungua chumba chake na kuingia. Kila chumba kilikamilika, choo, bafu ndani na jiko dogo la kahawa au chai lilikuwepo.
Chiba akarudi sebuleni na kuwasha luninga kubwa iliyowekwa ukutani, macho yake yakakutana na matangazo ya moja kwa moja kutoka kituo cha televisheni cha EBC. Hakikuwa kingine ni mapokezi ya marais waliokuwa wakimiminika katika jiji hilo.
* * *
Hoteli ya BLUE MOON
Kamanda Amata bado alikuwa ametulia kimya katika chumba chake hicho, huku mezani kukiwa na chupa kubwa ya pombe aina ya Covousier ikiishia tumboni mwake taratibu, makwapani mwake alikuwa amening’iniza bastola mbili, mja upande huu na nyingine upande mwingine. Kwa ujumla alikuwa tayari kwa kazi lakini bado akili yake haikuwa katika umoja mzuri na mwili wake. Katika meza hiyo hiyo, alikuwa ameweka kijitabu kidogo cha kumbukumbu, si chake bali kile alichokichukua kwa marehemu Innocent na karatasi nyingine ile aliyoichukua kule Waterloo ndani ya jumba ‘Silent Rock Villa’. Ukiachana na mkono ulioshika bilauri iliyojaa pombe nusu, alikuwa amekamata simu upande mwingine akibofya namba ambazo amezikuta zimeandikwa ndani ya karatasi ile. Katika hisia zake, kwa vyovyote, alijuwa wazi kuwa wenye namba hizo watakuwa na uhusiano na Gupter na kundi lake ama wa kikazi au wa kidugu.
Nitajitambulishaje? Akajiuliza mara baada ya kuiweka simu sikioni na kusikia ikiita upande wa pili. Simu yake hii ilikuwa ni ile ambayo ni vigumu sana kuitambua uelekeo ilipo.
“Hello!” upande wa pili ikaitikia.
“Bole International Airport, reception, habari za kazi!” Amata akajikuta akitamka kuwa simu hiyo inatoka katika meza ya mapokezi ya Uwanja wa ndege wa Bole.
“Kuna mtu hapa ni mgeni wako ametupatia namba hii ili uje umpokee, amefika takribani saa tatu zilizopita, tafadhali fika mapokezi umchukue!” Amata akasema huku ahajui nini atafanya kama aliyempigia simu atakubali wito huo.
“Ok, got’ya!” upande wa pili ukajibu na simu ikakatika.
“Bingo!” Amata akajikuta anasema kwa sauti, akainuka na kujitupia koti lake ili kuficha ile ‘miguu ya kuku’, akainuka na kuitia ile simu mfukoni, akachukua vitu kadhaa ikiwemo kile kijitabu cha kumbukumbu ambacho hakukiacha hata nukta moja tangu akipate kwa maana hakuwa amemaliza kazi yake. Akafungua mlango na kutoka nje, akashuka chini kabisa ya hotei hiyo na kuzielekea taksi, moja wapo ya hizo ikamchukua na kumkimbiza uwanja wa ndege.
* * *
Katika kitongoji cha Aleltu, nje ya jiji la Addis kilomita takribani hamsini na tatu kutoka mjini kati, ndiko Martin Gupter na kundi lake waliweka makazi ya muda ambayo kwa mipango yao, hayo yalikuwa makazi ya saa tisini na sita tu. Mwendo wa nusu saa tu ungeweza kufika katikati ya jiji hilo kama ungeendesha gari kwa mwendo kasi wa kilomita 100 kwa saa.
Martin Gupter aliteremsha kikombe chake cha kahawa huku macho yake yakiwa kwenye dirisha kubwa yakisanifu mandhari ya nje ya nyumba hiyo. Nyumba hiy, Amanda alikuwa ameikodi kwa juma moja tu kwa ajili ya kufanyia kazi yao, alikwishaihakikishia usalama, kwa kuwa ni mara nyingi wageni wan je huitumia kwa kuikodi kama wao. Ikiwa ni moja ya mbinu za kujificha kwa kivuli cha watalii ndani ya jiji hilo maarufu kabisa Afrika. Kwa mbali katika barabara ya vumbi aliliona gari likija kasi upande huo, akachukua darubini yake na kutazama. Ni gari ambalo haikumchukua muda kulijua.
“Amanda amefika!” akamwambia Fredy, kisha wakatoka nje kumlaki, dakika moja baadae wote wakawa tayari wameketi kuizunguka meza moja ya duara sebuleni hapo.
“Tupe habari za mjini!” Martin akaanzisha mazungumzo.
“Huko ni moto asee, kama nilivyowaambia jana, wageni wetu wameshaanza kufika, na wote tayari ninajua wapi wanafikia, isitoshe hata wana uinzi kiasi gani…”
“Wanapenyeka?” Fredy akadakiza swali.
“Itabidi wapenyeke, hakuna jinsi,” Amanda akasisitiza huku akijimiminia kahawa, na alipomaliza na kupiga funda moja akakitua kile kikombe.
“Mmepata taarifa yoyote kutoka kwa mteja wetu?” Amanda akatupa swali maana anajua kuwa taarifa nyeti za kazi huwa zinafika moja kwa moja kwa Martin na si mtu mwingine yeyote.
“Yes! Ujumbe wote utafika jioni ya leo, utakuwa na watu sita akiwamo Fadick Al Habib, na ndiye kiongozi wa msafara, mzee mwenyewe hawezi kufika wala wenzake. Maagizo ni yale yale, mkutano wa AU na hawa jamaa utakuwa saa tisa alasiri jioni, wakikubaliana basi kazi imekwisha, wasipokubaliana tunatakiwa tuendelee na operesheni yetu. Sasa endapo itatubidi tuendelee na operesheni, ndiyo tupange sasa…!” Martin akawaeleza.
“Sawa, baada ya kikao cha kesho, usiku kutakuwa na tafrija katika hoteli ya kifahari ya Golden Tulip, na hawa wageni wote watakuwepo,” Amanda akatoa maelekezo.
“Nimekuelewa, sasa baada ya kazi ya kesho sote tunatakiwa tukutane na Jaffer kule Riyadh kwa bakshisi za mwisho…” Martin akawaambia na kila mmoja akatabasamu.
“Sasa nafikiri ni muda muafaka kutoka, cha muhimu ni kujiweka sawa, tusitambulike, tukaikague hoteli hiyo, na ile atakayofikia mwenyekiti wao kisha tutazame na mengine ii siku ya kesho tuwe tayari,” Martin akamaliza kwa kuwaambia hilo na kila mmoja akaanza kujiandaa kwa jinsi anavyojua yeye ili mradi tu wakiwa huko mjini basi wasigundulike kirahisi.
* * *
Uwanja wa ndege wa BOLE
Kamanda Amata akawasili katika uwanja huo, akaiacha ile taksi baada ya kumaliza kulipia huduma hiyo, akavuta hatua na kuyapita maegesho mpaka kwenye sakafu ya uwanja huo. Macho yake yalikuwa yakipepesa harakaharaka na kutazama huku na huko, ni hapo ndipo ailipokutana macho kwa macho na mtu asiyemtaraji; kijana jamali, mweusi wa wastani mwenye tambo haswa la kipiganaji ambalo lilifichwa na nguo nadhifu, suti ya kisasa ambayo isingeweza kumpa wasiwasi mtu yeyote amtazamaye.
Drunken Hamidou, mpelelezi kutoka jumuia ya ECOWAS, akamsalimu kwa macho pasi na kumkaribia kwa maana alijua kwa nini mtu huyo yuko hapo. Almwona wazi kuwa kijana huyo alitamani kumkaribia na kumsalimia, kwa jinsi alivyopigwa na mshangao lakini Amata hakuruhusu hilo kwani yeye alikuwa na kazi yake binafsi. Akamwacha na kukaribia meza ya mapokezi ambako kwa ndani kulikuwa na watu wawili na nje kulikuwa na mtu mwingine ambaye kulionekana kama kuna mabishano kati yao. Akili ya Amata ikafanya kazi haraka na kujua kwa vyovyote alichokitaraji ndicho kinatokea. Naye akawasili palepale mezani na kujifanya akiongea na mhudumu mwingine kuuliza maswali ambayo hayana jibu la kiurahisi. Huku akisikiliza mazungumzo ya watu wale wawili wakibishana, huyu wan je akisema kuwa amepigiwa simu na amekuja kumfata mgeni wake, na huyu wandani akipinga kuwa hawajapiga kwa mtu yeyote kuhusu huo ugeni. Mwishowe yule kijana mwenye asili ya Uzungu uliyochakaa akaondoka akitukana matusi. Kamanda Amata akamalizana haraka na mhudumu huyo na kuondoka, lengo lake halikuwa jingine zaidi ya kumfuatilia mtu huyo. Akamtazama akielekea katika maegesho, huku akiongea kwa simu yake na kusimama nje ya Range Rover moja ya gharama sana. Kamanda Amata akajifanya kama anafunga kamba ya kiatu chake ili kumpa nafasi kijana huyo kumaliza mazungumzo yake.
Kijana yule hakuwa na hili wala lile, aliposhusha simu yake, na kuitia mfukoni, akageuka kukamata mlango wa gari ndipo akajikuta ana kwa ana na domo la bastola, mtu aliyekamata mashine hiyo hakuwahi kumwona hata siku moja tangu azaliwe.
“Uphhhhhhh!!!!!” akashusha pumzi na kijasho chembamba kikaanza kumtiririka.
“Ingia!” Amata akamwambia kwa kiingereza.
“Wewe ni nani…?”
“…Get in!!” akamwambia tena huku tayari akiwa keshaondoa kilinda usalama cha bastola hiyo. Yule kijana akafungua mlango na kuingia na Amata akaingia mlango wa nyuma yake na kuketi, mara hii akamwekea mtutu wa bastola kwenye mbavu zake upande wa nyuma.
“Drive!” akamwamuru.
“Tunaenda wapi?” yule kijana akauliza.
“Nyumbani kwako!” akamjibu.
“Nyumbani kwangu?” akauliza, “Mi sina nyumba, kama unataka gari chukua!!!” yule kijana akaongea kwa kitetemeshi huku akimpa funguo Amata.
“HEYYYY!!!!” Amata akang’aka, na yule bwana akabaki kimya kabisa.
“Bosi wako ni nani?” akamtupia swali.
“Mr. Bbaattolloommiinno!!” akajibu huku akitetemeka.
“Nina shida na yeye, nipeleke!” akamwamuru.
“Ssaawwaa!!” akajibu na kuwasha gari, Amata akatulia kimya akimwangalia kijana huyo akiendesha kwenye barabara za Addis kuelekea huko atakako. Kijana yule ambaye kwa kumwangalia na kumsikia lafudhi yake tu ungejua kuwa ni Mtaliano aliendesha gari kwa takribani dakika kumi hivi na kuufikia Mtaa wa Lorenzo Tiezaz, hapo akaachana na barabara ya kwanza na kuingia kwenye mtaa huo mpaka katika jumba moja kubwa lenye wigo mkubwa sana wa michongoma.
“Ni hapa!” yule kijana akamwambia Amata.
“Sikiliza, mimi ndiye mgeni wake ambaye ulitakiwa kunifikisha kwake, na nimefika uwanja wa ndege kwa saa nyingi sana, sasa nipeleke nionane naye,” akamwambia na dakika hiyo hiyo lango likafunguka na lile gari likapotelea ndani ya kasri hilo. Mbele ya jumba hilo, alisimama mwanadada mrembo wa kizungu, akisubiri gari hilo kuegeshwa.
“Umefika, na huyo mwanadada atakufikisha kwa Bwana Mkubwa!” yule kijana akamwambia Amata.
“Asante, unisubiri hapa ili unirudishe, sawa?”
“Sawa!”
Amata akashuka na kupeana mikono na yule mwanadada, kisha akaongozwa ndani ya jumba hilo mpaka kwenye chumba kimoja cha gharama sana, akaingia na kukaribishwa na mzee wa makamo, mnene, aiyejaa kwenye kiti alichokikalia.
“Karibu sana!” akakaribishwa huku yule mwanadada akimimina kinywaji kikali bilaurini.
“Asante sana! Nimeshakaribia,” Amata akajibu na kujituliza kitini.
“Nimepata simu kuwa wewe ni mgeni wangu,na mimi sikutegemea ugeni siku ya leo,” yule bwana akamwambia Amata.
“Ndiyo, na mimi ndiye niliyepiga simu, si kweli kwamba ilipigwa kutoka uwanja wandege,” akamwambia.
Maneno hayo yakamfanya yule bwana ashtuke kidogo, maana hakuelewa imekuwaje hata mgeni huyu apige simu na kufika mahala hapo. Akamtazama mzungu yule, Mtaliano mwenye nywele nyeupe zilizomwagika mabegani kama za Sir Newton Isaac.
Hawa ndiyo mabaki ya Wataliano walioua ndugu zetu Waethiopia miaka ileee! Amata akawaza, akijaribu kuirudia historia ya watu hao walipoingia katika nchi hiyo na kufanya mauaji mabaya kabisa ya ‘weusi’ zaidi ya elfu ishirini au thelathini.
“Enhe, nipe ujumbe wangu kijana maana huwa sina muda mrefu wa kuzungumza na watu hasa wasio na miadi kama wewe!” akaongea kwa dharau huku akiweka mtemba wake kinywani na kupiga pafu kama tatu hivi na kuruhusu moshi mzito ukijaze chumba hicho kupitia tundu za pua yake kubwa.
“Tunaweza kubaki wawili?” Amata akamuuliza.
“Bila shaka!” akajibu na kumwamuru mwanadada yule atoke, naye akafanya hivyo.
Kamanda Amata hakuzungumza, akachomo picha tatu mfukoni mwake na kumwekea mezani. Yule mzee akazitazama kwa makini, kana kwamba kajua ni nini ambacho mgeni wake huyo atasema. Akachukua tena mtemba wake na kuuweka kinywani, akapiga pafu kadhaa na kuushusha kisha akakung’uta jivu kwenye kibweta chake. Kwa mkono mwingine akaichukua picha ya mwanamke, Amanda, akaiweka kando.
“Namjua huyu!” akamwambia Amata. Moyo wa Amata ukapiga samasoti, akahema kwa nguvu, “Vipi una shida naye?” yule bwana akauliza na kumgutua Amata kwenye lindi la mawazo.
“Unamjuaje? Ninamhitaji kwa hali na mali,”
“Huyu ni mteja wangu, nimemwona si mara nyingi, bali alikuja hapa kukodi nyumba ya kuishi kwa muda wa wiki moja hivi…”
“Una nyumba za kukodi?”
“Si! Si! Nyingi sana, nimezijenga mashambanai huko,” akaeleza.
“Nahitaji kukutana naye, nipe maelekezo,” Amata akamwambia.
“No! siwezi kukupa maelezo yoyote ya mteja wangu, ni kinyume na baishara hii,” Balomino akajibu.
“Utanipa au hutonipa?” Amata akamuuliza.
“Nikupe wewe kama nani?” yule Mtaliano akauliza huku akijiweka vyema kitini, Amata akaigundua hila yake, kwa wepesi sana akainuka pale alipo na kumbana yule mzee kitini, kisha akachomo bastola kutoka kiunoni mwake, akarudi na kujibwaga katika kiti chake huku akiwa kamnyoshea mtaliano huyo domo la Berreta 87, bastola ya kizamani ya miaka ya ’76 huko Italia na wengine huuita ‘Series 81’.
“Niambiye hiyo nyumba ipo wapi?” akamuuliza, yule bwana kijasho kilikuwa kikimwagika.
“Aleltu!” akajibu na mara mguu wake ukakanyaga kitufe fulani chini ya meza. Amata akajua mambo yashaharibika, sekunde yoyote wangemvamia hapo, akatazama huku na huku.
“Hah! Hah! Hah! Hah! Aaaaaa!” yule tajiri akacheka cheko baya sana lililomuuzi Amata, akageuka na pigo moja zito akamzimisha kisha akafungua mlango, alipotaka tu kutoka akakutana na watu kama wane hivi wanakuja wakikimbia na bunduki mikononi. Akageuka na kurudi kwenye dirisha kubwa, huku mlangoni akiwa kasukumia kochi kubwa, akatazama huku na huko na kulifungua dirisha lile, akatoka na kutua nje.
Kumwacha hai si jambo zuri ataniharibia kazi! Akawaza na kuchukua ile bastola mkononi, akafyatua risasi moja iliyotua moyoni na kummaliza. Akaambaa ambaa na ukuta mpaka dirisha la tatu hivi, akalikuta lipo wazi, akachungulia ndani akamkuta mwanamke mmoja akiendelea na kazi kwenye kompyuta, akalikamata na kuingia ndani akatua bila kusikika. Akauendea mlango, na hapo ndipo yule mwanamke alipogundua kuwa hayupo peke yake, akapiga kelele lakini Amata akamuwahi na kumbana kinywa.
“Nipe ramani ya kufika Aleltu, kwenye nyumba za bosi wako,” akamwambia na kumwachia. Yule mwanamke akapekua na kumpa kitabu kimoja kikubwa tu lakini kinachoweza kuingia katika mfuko wa ndani wa koti lake.
“Nisindikize mpaka nje ya jingo,” akamwambia, na yule mwanamke akafanya hivyo, wakapita pamoja kwenye korido kana kwamba ni moja ya wateja wa tajiri huyo. Alipofika nje, akaagana na mwanamke huyo na kuingia kwenye gari lile lile lakini mara hii halikuwa na dereva ila funguo ilikuwa ikining’inia. Kamanda Amata, akaingia ndani na kutia injini moto, mashine ikaunguruma, akatingiza gia ya kwanza na kuondoka kwa fujo. Katika lango la kutokea nje mlinzi alizuia gari hilo lisitoke lakini mwenyewe hakuwa na budi kutoka barabarani baada ya kuona hakuna dalili za kusimama. Amata akagonga geti na gari lile likaharibika vibaya huku likiacha lango wazi. Akaendelea kuendesha kwa mwendo wa kasi mpaka sehemu alipoona panafaa, akasimama na kuteremka, akaliacha gari hilo na kuingia kwenye kichaka cha miti, akapotelea zake kwa mwendo wa miguu.
* * *
Chiba alikuwa mezani kimya huku kompyuta yake ikiendelea na kazi ya kutafuta mambo mbalimbali ikiwemo kuingia katika mitandao mbalimbali, lakini licha ya yote hayo alikuwa akijaribu kumtafuta Kamanda Amata kama anaweza kupata ishara yoyote. Wakati huo Gina hakuwepo humo ndani, yeye alijitoma mitaani kutafuta hili na lile ili baadaye wakijumuisha tafutishi zao waweze kupata kipi ni kipi. Chiba na Gina hawakuwa na muda mrefu wa kujua nini cha kufanya, kazi kubwa kwao ilikuwa ni kutegua kitendawili cha kama Martin Gupter na kundi lake wapo ndani ya Addis au la. Mpaka dakika hiyo kila ambako mashushushu wan chi hiyo walikuwa wametega kuwanasa, hawakuwaona.
“Sidhani kama wamefika” – labda ni maneno ambayo wanausalama wengi ambao wamejawa uvivu wa kiupelelezi. Sifa ya kuwa mpelelezi hasa kwenye kiwango cha espionage, lazima uwe na milango sita ya fahamu yaani umzidi mwanadamu wa kawaida. Wakati wao wanafuata wanayoambiwa na wakubwa wao tayari TSA walikuwa Addis na Kamanda Amata yupo hatua mbili mbele kuwatia mkononi washenzi hao.
Simu ya Gina ikaita, akainyakua kutoka kwenye mkoba wake, akaitazama kwenye kioo, kisha akasonga kando pasipo na watu na kuiweka sikioni.
“Uelekeo wapi?” sauti ya Chiba ikasikika kutoka upande wa pili.
“Katikati ya Mtaa wa Mauritius!”
“Kuna lolote?” akauliza.
“Upande huu hamna jipya, nimejaribu pia kupita HQ ya AU nako bado inaonekana hakuna jibu jipya, baadhi ya watu wanaofananishwa na Gupter wamewekwa tunduni, kiujumla hali ni tete,” Gina akaeleza.
“Vipi upande wako?” akamtupia swali.
“Huku habari ni nzuri, nimepata uelekeo wa Kamanda Ama….”
“Yeeeessss nambie yuko wapi?” Gina akamkatisha Chiba kwa furaha.
“Namuona karibu na Mtaa wa D.A.R Sahara, akielekea katikati ya mji,” Chiba akamuelekeza Gina, naye akawasha kifaa chake mfano wa simu ya mkononi na kuiweka juu ya kioo ramani ya Addis Ababa, akautafuta mtaa mtaa huo na kuupata kisha akatafuta barabara ya kufika kutoka pale alipo, akapata umbali ni k.m 9. Akaingia garini na kuwasha, kisha akingiza gari barabarani na kuufuata Mtaa wa Mauritius, akauacha ule wa Tanzania na kukunja kuchukua Barabara ya Ethio China.
Kwenye kompyuta ya Chiba aliweza kuwaona wote wawili na alijaribu kumuelekeza Gina jinsi ya kumkuta Amata, lakini baadae akashangaa kuona Gina amesimama mahali kwa muda mrefu sana. Akampigia simu na kujibiwa kuwa alikuwa amekamatwa na askari wa Barabarani kwa kuwa aliingia barabara kuu kimakosa. Chiba alijikuta akishikwa na hasira kwa kuwa muda ulikuwa ukipotea. Baada kama ya dakika thelathini hivi simu yake ikaita, akaipokea na kuzungumza machache na Gina.
“Sasa nenda hoteli ya Blue Moon ameingia hapo! Nafikiri ndipo alipofikia, ukimpata hakikisha unamhamishia huku,” Chibna akampa maelekezo Gina.
“Copy!” Gina akajibu na kukata simu.
 
MAGNUM 22

Sehemu 22

Hoteli ya Blue Moon
Kamanda Amata alijibwaga kitini, akakitoa kile kitabu alichopewa na yule mwanamke, akakiweka mezani kisha akijimiminia pombe katika bilauri yake na kupiga mafunda mawili tu, ikaisha, akjimiminia tena na kupiga funda moja kisha akitua mezani. Baada ya ukimya wa sekunde kadhaa akiwa katika kutafakari jambo, akapeleka mkono na kutaka kuchukua kile kitabu. Mbisho wa hodi ukamshtua, akachomoa bastola yake na kuiweka tayari. Hodi ile ikarudiwa tena.
Jinsi ilivyokuwa ikigongwa, haikuwa ngeni masikioni mwake kwani kati idara ya TSA kila mmoja alikuwa na jinsi ya kugonga hodi au kengele ya mlangoni. Ijapokuwa alijua kuwa hiyo ni code ya Gina, Amata hakutaka kukubaliana na moyo wake.
Trust no one! Akajisemea moyoni huku akiinuka taratibu na bastola yake mkononi, akauendea mlango na kukinyonga kitasa taratibu. Akaufungua mlango huku yeye akibaki nyuma yake.
“TSA 5!” Gina akatamka kabla ya kuingia ndani. Kamanda Amata akajitokeza baada ya kusikia sauti tamu ya msichana ampendaye. Wakakumbatiana kwa nguvu na kupeana mabusu motomoto, hata sekunde kumi hazikupita wakaangushiana kitandani na kupeana mahaba mazito waliyoyamisi kwa siku nyingi. Saa nzima ya pilika pilika za kitandani ilipokwisha, wakasindikizana maliwatoni na kujiweka sawa, kisha wakarudi tena chumbani.
“Mmefika lini?” Amata akamuuliza. Hili ndilo lilikuwa swali la kwanza la Amata kwa Gina tangu wakutane saa moja iliyopita.
“Leo hii mida kama ya saa nne au tano hivi,” akajibu.
“Umejuaje kama niko hapa?”
“Nipo na Chiba…”
“Aaaa basi hapo lazima mnipate. Sasa inabidi tutafute pa kuweka kambi maana mambo tayari yameiva, mi nimeshaliamsha dude,” Amata akamwambia Gina.
“Kinachotakiwa ni wewe kufunga kilicho chako hapa na kunifuata, tayari tumepata kambi ambayo Madam S alikwishaiandaa kwa siri…”
“Iko wapi?” Amata akauliza.
“Just do kile nimekwambia!”
“Sawa Kiongozi,” Amata akajibu na kuanza kuweka vizuri vikorokoro vyake, dakika kumi baadae alikuwa tayari kwa safari. Katika meza ya mapokezi akahakikisha ameipia kila kitu na hakujibu hata swali moja la mhudumu. Wakaingia garini na Gina akashika njia na kutokomea mjini.
“Vipi, hatuna msindikizaji?” Gina akauliza.
“Tupo peke yetu tu,” Amata akajibu huku akirudisha macho yake kutoka nyuma kuja mbele. Mwendo nusu saa uliwafikisha katika jingo lile lile upande wa maegesho. Gina akaegesha gari na kuteremka akifuatiwa na Amata, wakachukua mizigo na kupita katika njia ile aliyoelekezwa na Archimedeus.
“Karibu sana Kamanda!” Chiba akamkaribisha katika sebule ile waliyokabidhiwa.
“Asante sana, nashukuru kwa kuwa mmekuja, vipi bibi anaendeleaje?” Amata akauliza.
“Nimewasiliana naye si muda mrefu, yuko poa na ameruhusiwa kurudi nyumbani,” Chiba akaeleza huku akiweka kando mkoba wa Amata alioutwaa toka mabegani pake pindi tu alipompokea.
“Hatuna budi kuanza kazi mara moja kwani muda unakimbia,” Chiba akasema na Amata akaafiki kwa kichwa, “mpaka sasa duru zote zinaonekana zikiamini kuwa Gupter hayupo nchini hapa…”
“Ni hatari sana kwa sababu watalegeza ulinzi wakati mshenzi huyu na timu yake wamejaa tele ndani ya Addis!” Amata akamkatisha na kumjibu. Gina na Chiba wakashtuka kidogo.
“Yupo?” Chiba akauliza.
“Kabla ya yote mmekagua hiki kiapartment, kusije kuwa kuna watotot wanatusikiliza tu!” Amata akawaambia akimaanisha kama kuna vinasa sauti vya siri.
“Aaaaa Kamanda, hilo ni jukumu la kwanza, unaona kifaa hiki hapa…?”
“Yap!”
“Hiki ni kifaa kipya kabisa, hapa kilipo kikigundua tu kuwa tunasikilizwa kitapiga kelele; kwa ukimya wake ujue mambo shwari,” Chiba akamwambia.
“Ok! Gupter na washenzi wake wameingia hapa masaa ishirini na nne hivi au arobaini na nane labda…”
“Una uhakika?” Gina akauliza.
“Huwa sibahatishi mama! Mi nimefika hapa nikitokea Sierra, pale nilipata namba ya mtu wa huku ambaye nahisi Gupter alikuwa akiwasiliana naye…”
“Yupo wapi tumtaiti mapema?” Chiba akawahi kuuliza.
“Umechelewa Chiba, ndiyo maana kuna TSA 1 na TSA2, wewe ni 2, kwa maana hiyo 1 alishafanya kazi na huyu mshenzi tayari anahemea kuzimu,” Amata akaeleza.
“Umemuua?” Gina akauliza.
“Hakukuwa na jinsi kwa maana ningemwacha hai angeweza kuwapa taarifa ‘kina Guter kuwa nawasaka, hivyo mpaka sasa hata wao hawajui kuwa nipo, ukizingatia wanaamini kuwa mimi ni mfu na ninaoza tu kwenye kaburi la pamoja…” Amata akaeleza.
“Nakuamini Kamanda, lazima uoneshe heshima ya cheo chako,” Chiba akamsifia.
“Sasa ipo hivi, yule Mtaliano ni tajiri wa kukodisha majumba ya kuishi na ana nyumba zake huko mashambani, na kati ya nyumba hizi moja wapo kwapangisha kina Gupter…”
“Wapi huko?” Gina akadakiza swali.
“Aleltu!”
“Aleltu, Aleltu, Aleltu!!!”
“Huwezi kupajua bwana,” Amata akamwambia Gina huku akiweka mezani kile kitabu cha ramani, akakifungua na wote kwa pamoja wakaanza kuisoma ramani hiyo ya Jiji la Addis na viunga vyake. Wakati Gina na Amata wakisoma, Chiba alikuwa akitafuta katika mtandao, eneo lilipo, namba za nyumba na wamiliki.
“Batlomino Augusto!” akatamka baada ya kupata tafutishi za kutosha, “Hapa kuna nyumba namba na mtaa,” akaeleza Chiba.
“Twendeni tukavamie tumalize mchezo!” Gina akapendekeza.
“Mmmmmh Gina kila mara namkwambia, ‘don’t put your best foot forward’. Adui kama huyu si bwege kama waliokula pesa za EPA, wakati mwingine mwache adui hata anywe chain a wewe ukiwa unamwangalia tu kwa sababu huo si wakati mzuri wa kufanya uvamizi,” Amata akamwambia Gina.
“Unamaanisha nini, tumwache mpaka afanye mauaji mengine hapo kesho?” Gina akaongea kwa uchungu.
“Si hivyo, ili kumtia mbaroni muuaji mwenye taaluma kama huyu inabidi kwanza umsome aina yake ya kuua; anavizia? Anadhamiria? Au anafanyaje… Gupter lazima tumstadi kwa muda mrefu…”
“Hatuna muda Amata, time is now!” Gina akang’aka.
“Sikiliza Gina, wenzako tulishaanza kumstadi huyu mjinga miezi miwili ilopita, na tumegundua kwamba, mauaji aliyotaka kuyafanya Dar es salaama ndiyo atakayoyafanya hapa, nikiwa na maana kuwa, atatekeleza mauaji baada ya kikao, huo ndiyo mpango,” Amata akasema.
“Sasa tufanyaje, tuwasake tuwatait usiku huu au tufanyeje?” Chiba akauliza.
“Hawa lazima watembelewe usiku huu huu, na kukiwakuta hatakiwi kuachwa mtu, ni kuwatia tunduni tu!” Amata akasisitiza. Akaitazama saa yake, tayari ilikuwa ni saa nane inaenda tisa za alasiri.
* * *
Hoteli ya Golden Tulip – Addis Ababa
Kama ni ulinzi basi hapa ulikuwa umeimarishwa, kila aliyekuwa akiingia ndani ya hoteli hii alikuwa akipekuliwa vilivyo. Mitambo ya kisasa ilifungwa pande tafauti za hoteli hiyo kuanzia juu mpaka chini na kuhakikisha hata akipita mende anaonekana. Alasiri hiyo Martin Gupter aliegesha gari katika eneo la kuegeshea la hoteli hiyo. Ndani ya gari lake alikuwa yeye na Fredy huku wakimwacha Amanda akiwasili na gari lingine.
“Lazima tuujaribu ulinzi!” Guter akasema.
“Huo ni mchezo wa hatari sana kaka,” Fredy akamwambia.
“Sikiliza, mimi kwangu ni mchezo wa kawaida sana kwa sababu nimeshafanya kazi hiyo kwa miaka mingi, najua nini na nini cha kufanya na nijikute ndani ya hoteli…” akasema.
“Ok! Jaribu…. Unataka kuingia?”
“Yeah! Nataka kuingia na kunya bia moja, we nisubiri hapa,” Gupter akamwambia Fredy na kushuka, moja kwa moja akauendea mlango wa hoteli hiyo ambao mbele yake kulikuwa na askari kama wane hivi wakiwajibika huku na huko, kumkagua huyu na yule.
Sasa hii ni hoteli tu kwa ajili ya chakula cha jioni, huko wanakolala kuna ulinzi gani! Guter akawaza wakati akipandisha ngazi za kuingia ndani.
“Hey man! Stop for inspection please!” askari mmoja alimuomba asimame kwa ukaguzi, Gupter akafanya hivyo. Akapekuliwa kila kona ya mwili wake, na upande mmoja wa koti akakutwa na bastola, ikachomolewa.
“We ni mgeni wa hoteli hii?” akaulizwa.
“No, ila mara kadhaa hupenda kuja kupata kinywaji kidogo au kucheza poker,” Gupter akajibu.
“Sawa, sasa hutoruhusiwa kuingia na hii silaha, ni hatari kwa sasa, utaiacha hapa, na kuichukua ukitoka,” yule askari akamwambia. Wakati Gupter akimsikiliza, kulikuwa na askari mwingine akimtolea macho kijana huyu wa kizungu mwenye mustachi wa wastani na ndevu za kuote kwa mbali na sura yake ni kama iliwahi kuungua miaka mingi nyuma. Gupter alimwona askari huyu akahisi labda amemgundua, akapiga moyo konde.
“Ok, waweza kuendelea na safari yako,” akaruhusiwa. Hatua kama kumi mbele akasikia sauti ikimwita.
“Hey man!!!” askari yule yule wa kwanza akamwita tena.
Ohoooo huku kuitana mara mbili kuna jambo! Gupter akawaza na kugeuka kiuvivu kidogo.
“Wallet yako hii,” akaambiwa. Kumbe wakati anasachiwa alikuwa ameweka waleti mezani na kuisahau hapo.
“Asante sana!” akashukuru na kuichukua kisha akaingia zake ndani.
Kutoka katika maegesho, Amanda akashusha darubini yake na kushusha pumzi ndefu, akaiweka kando na kutulia kwa sekunde kadhaa. Akafungua mlango na kushuka, akaufunga kwa mguu nyuma yake na kuvuta hatua kuelekea kwenye vibanda vya kuuza mambo ya utamaduni, huko akapoteza kama saa nzima hivi akinunua hiki na kuangalia kile, lakini yote hayo yalikuwa geresha tu, lengo kuu lilikuwa ni kupata habari mbili tatu kutoka kwa wananchi hao.
Baada ya saa moja kupita, Martin Gupter akatoka kwenye mlango ule ule na kuchukua bastola yake, kisha akavuta hatua na kulielekea gari la Amanda akaingia na kuketi.
“Vipi?” Amanda akauliza.
“Ulinzi mwepesi sana kwa mtu kama mimi, nitaingia na kufanya yangu pindi ikibidi na nikitakiwa kufanya hivyo. Twende sasa tukaonane na Fadick,” akamwambia Amanda.
“Unapajua alipo?”
“Ndiyo maana nikakwambia twende,” Gupter akajibu na mwanamke huyo akaliondoa gari na mita chache nyuma akafuatwa na Fredy.
Drunken Hamidou
Mara alipotoka uwanja wa ndege, kijana huyu mpelelezi machachri wa jumuia ya ECOWAS akafika katika chumba cha siri ambacho yeye na wenzake wawili walioteuliwa kuunda timu ya kipelelezi ya kumsaka muuaji wa viongozi wa Afrika hukutana na kuweka mezani tafutishi zao. Kama ilivyo ada kwao, muda huo kila mmoja alfika kwa njia yake na kukutana ndani ya chumba hiki cha siri katika moja ya ofisi za jingo kubwa la mikutano na ofisi la Umoja wa Afrika.
“Kazi ni ngumu, viongozi wote wamefika salama, sasa sihida ni kuhakikisha huyu jamaa kweli hajaingia nchini?” mmoj wao kutoka jumuia ya SADC akawaambia wenzake.
“Tunapiga ngumi kichakani, kumbukeni mshenzi huyu naye ni kachero kama sisi hivyo anajua mbinu zote tunazotumia, nimehakikisha ulinzi mkali upo katika hoteli ambayo Mwenyekiti wa atafikia…” mwingine akasema.
“Nimemwona Amata Ric!” Drunken Hamidou akawaambia swahiba zake. Kila mmoja akashtuka na kumtazama kijana huyo, “Amata!? Wa TISS” akauliza yulle wa SADC.
“Ndiyo, alikuja uwanja wa ndege, akaenda mapokezi na baada ya dakika chache akatoka kwa mwendo wa kasi kidogo akaingia kwenye gari aina ya Range Rover na kuondoka,” akawaambia.
“Umemfananisha! Inasemekana Amata ametoweka na habari ambazo ninazo ni kuwa Idara ya usalama wa Taifa ya Tanzania, inaficha habari hii kwa aibu kwa kuwa walijinasibu kuwa wataimaliza kazi hii kwa siku chache,” mwingine akaongea kwa kujiamini kabisa.
“Narudia, nimemwona Amata Ric, na kama yeye yuko hapa basi Gupter yupo hapa, tuwe makini… Amata si mtu wa kutoweka ovyo, kama kweli alitoweka basi alitoweka kikazi, na sasa ameibukia Addis… pendekezo langu mimi tutumie dakika chache kumsaka kwa njia zote, na tukimpata tufanye kazi pamoja, kwa vyovyote yuko mbele kuliko sisi, si ajabu anamjua hata demu wa Gupter anaishi wapi…” Drunken akawaambia wenzake, ukimya ukajidai kati yao, hakuwa aliyeongea lolote.
“Hapana, hata kamati yenyewe itatushangaa, tunaacha kutegua kitendawili na kumtafuta Amata…”
Baada ya kikao hicho kifupi kukamilika, wakatawanyika, lakini kama kazi yao ili, siri hufanyika kwa siri na siri huwa siri ya siri. Kila mmoja alifika kwa mkuu wake kwa siri na kumpa taarifa aliyokuwa nayo kutokana na kazi yake ya siku hiyo.
Ni huyu Drunken Hamidou ndiye aliyetoa taarifa kwa mkuu wake na ikasambaa katika kamati ya usalama ya umoja huo kuwa Amata yupo Addis. Haikuwa rahisi kueleweka kwa wadau wa kamati hiyo, habari hii iliwachanganya kiasi na swali likawa, je TSA wapo Addis? Mwenyekiti wa baraza hilo, hakufurahishwa hata kidogo na habari hiyo, akauliza mara kadhaa kama ni kweli wana uhakika aliyeonekana ni huyo au kivuli chake, akahakikishiwa kuwa ni yeye.
Katika kikao cha jioni hiyo, wadau wa baraza la usalama walikuwa na mjadala mzito sana kuhusu jambo hilo.
“Mimi, nikiongea kama mwenyekiti, mwenye mamlaka, nasema hivi, haitakiwi kwa idara yoyote ya usalama, kutoka popote pale, kuingilia mchakato huu wa kumnasa Gupter bila kibali chetu. Na kwa kanuni hii natoa amri na itekelezwe mara moja, huyu kijana wa TSA, nani sijui…”
“…Amata!”
“Yes! Amata, akamatwe na kuwekwa ndani ili kupisha kazi yetu ifanyike kwa umakini,” akamaliza kusema na ukimya ukatawala. Hakuna mjumbe yeyote aliyejibu au kuweka neno lolote. Hoja chache zikaendelea na baadae kikao hicho kikavunjwa ikiwa bado mwenyekiti wa baraza hilo la usalama la muda akitaka Amata akamatwe. Mara baada ya kumaliza kikao, mwenyekiti yule akatoka na kuwaacha wajumbe wake, akaingia gari ni kuelekea katikati ya mji, ndani ya jengo fulani ambalo kwalo alikutana na watu wengine watatu.
“Nahitaji mnifanyie kazi moja tu,” akawaambia.
“Ipi mkuu?”
“Kuna huyu mpelelezi wa Tanzania, inasemekana yupo hapa Addis, huyu anaweza kutuharibia kazi yetu, hivyo akamatwe awekwe ndani haraka kabla ya giza hili alijaisha,” akawaambia. Wale vijana wakatazamana kwa sekunde kadhaa kisha mmoja wao akahoji.
“Mkuu, kwa nini tusimjumuishe huyo mtu katika timu yetu? Maana mpaka sasa huyu Gupter anatuumiza vichwa, sisi hapa tuna tetesi tu kuwa anaweza kuwa nchini…”
“Mmejuaje?” akahoji.
“Mpaka sasa tunafuatilia ndege ya jana ambayo ilipata hitilafu, tunahisi hawa jamaa wameingia nchini kwa kutumia njia hiyo, yaani kushuka kwa miamvuli,” mmoja wa wale vijana akaeleza. Maelezo haya yakamfanya huyu mzee kuduwaa, hakuwahi kufikiri kitu kama hicho kichwani mwake.
“Any way, vyovyote vile, nataka huyu bwana akamatwe, mkishamkamata, tutamhoji kama ana habari yoyote juu ya mtu au watu hawa,”mwenyekiti akawaambia na kuwaaga pasi na kuruhusu swali lolote.
* * *
Ujumbe kutoka Oman, uliotumwa na Jaffer Bakhari uliwasili Addis Ababa ukiongozwa na Fadicky Al Habib. Ingawa baraza la usalama la muda lilikwishamtuhumu mtu huyu kama kiongozi wa mauaji haya, bado hawakuweza kumkamata kama wengi walivyotaka. Walijua amefika na watu wengine kama kumi hivi lakini kwa sheria za kimataifa hawakuweza kuwagusa watu hao.
“Kesho ni mwisho, wakikubali, itakuwa sherehe kwetu kuikomboa nchi yetu, wakikataa basi wataendeea kushuhudia mauaji na vita visivyokwisha,” wengine wakaitika na kuunga mkono.
Watu hawa walijipanga kwa hoja nzito dhidi ya Umoja wa Afrika, wakidhamiria kuipata ardhi ya mama zao.
“Na huyu mwenyekiti ndiye anayatunyima ardhi ile, hastahili kuishi, na kesho aongozwe na dhamira yake akubali ombi letu,” akawaambia.
Akiwa katika kuongea huko, simu yake ikaita, akaitazama na kuona namba ambayo alikwishapewa kuwa itampigia. Akainuka na kuingia katika chumba maalumu ambacho hakiruhusu sauti kutoka nje.
“Yes Shooter!” akaitikia simu hiyo.
“Tupo!” sauti ya pili ikasema.
“Mpango ni kama ulivyoambiwa, haujabadilika, ikiwa positive, utafanya ulivyoambiwa na ikiwa negative utajua wewe unamalizaje mchezo,” Fadicky akamwambia mtu wa upande wa pili.
“Unafikiri kuna kikwazo? Mbegu zetu tumezipanda kila mahali na zinamea vyema, over and out!” Fadick akasema.
“Hakuna kikwazo, kila tundu linapenyeka, over and out!” sauti ya upande wa pili ikajibu.
“Uno trabajo!”
Simu ikakatika.
* * *
Martin Gupter, akashusha simu sikioni na kubaki kimya huku akitafuna bubble gum kinywani mwake. Kwa taratibu sana, akafungua mlango na kukanyaga ardhi yenye vumbi, ya kijiji hiko cha Alertu. Akavuta hatua na kuingia ndani ya nyumba hiyo, giza lilikuwa limetawala ndani mwote. Fredy na Amanda walikuwa wamebaki mjini wakiendelea kupanga hiki na kile kwa kificho kikubwa ili wasijulikane. Ni Martin Gupter pekee alikuwa amerudi muda huo akiwategemea wenzi wake usiku wa baadae wa siku hiyo. Hatua zake chache zikamfikisha chumbani, na hapa ndipo moyo wake ulipolipuka kama kombora. Juu ya kitanda chake alikuta vitu viwili ambavyo hakutegemea; bunduki kubwa ‘Magnum 22’ na ua waridi.
Nani kaweka vitu hivi? Akajiuliza, hakupata jibu. Moyowe ukadunda kwa nguvu na hofu, akavuta hatua na kukikaribia kabisa kitanda kile, macho yake yakatua vyema katika bunduki ile, kilichomshangaza zaidi ni kuwa ilikuwa ile ile ya kwake. Bunduki aina ya Magnum 22 Riffle, na juu yake imefungwa hadubini ile ile. Martin Gupter, mikono ikamtetemeka, kijasho chembamba kikamtiririka, hakuelewa kama anaota au yu macho. Akatzama huku na huko, huku akichomoa bastola yake kutoka kiunoni na kuikamata barabara kabisa. Kutoka hapo akaanza kupita chumba kimoja kimoja kuangalia kama adui yake yupo ndani ya nyumba yake hiyo, la. Martin Gupter, kila alipojaribu kufikiria juu ya hilo, alijikuta yupo njia panda, akajitupa kitini na kuinua simu yake, na kuwataka Amanda na Fredy kurudi.
Robo saa baadae, wawili hawa wakaingia katika nyumba hiyo, tayari ilikuwa usiku wa saa tatu na nusu hivi kadiri ya saa iliyoning’inizwa ukutani.
“Martin!!” Amanda akaita na kumfanya kijana huyo kugutuka kama aliyepigwa shoti ya umeme, “Vipi, mbona umetutaka kurudi mapema ilhali bado tulikuwa kazini?” Amanda akasema.
“Kila kitu kimerudi, ndugu zangu hapa kazi ni ngumu!” akamjibu.
“Kivipi? Sikuelewi!” Fredy akadakiza.
Martin akainuka kitiki na kuwapa ishara ya kuwa wamfuate, nao wakafanya hivyo, wakafika chumbani kwa Martin na kujikuta wakipigwa butwaa. Fredy akamgeukia Martin na kumwambia, “They are here!” (wapo hapa).
“Yes! Na hii sasa ni hatari, jamani uamuzi wangu ni huu, hatuna budi kuhama hili eneo haraka, maana adui yetu keshajua wapi tulipo,” Martin akasema.
Amanda akatulia kimya bila kujibu neno lolote, akili yake ilikuwa bado ikijaribu kuyapanga mambo.
“Ina maana TSA wapo hapa?” akarudia swali ambalo alishaliuliza kwanza.
“Kwani ni nani alikuwa nabunduki hii? Si ilitoka mikononi mwangu tukiwa Tanzania, kwa mara ya kwanza katika maisha yangu!” Martin akasema.
“Sawa, tuhame na tuhamie tusipopajua lakini kama tumefanikiwa kumuua namba moja wao, hawa wengine hawatatusumbua kabisa,” Amanda akasema na Fredy akatikisa kichwa huku akitoa mkoba wake kabatini.
“Jamani, sikilizeni, kule Free Town tulipomkamata yule bwege, kumbuka tulimwekea nini kitandani… si ua waridi?” Fredy akawakumbusha kwa maneno hayo. Ukimya wa sekunde kadhaa ukapita katikati yao, Amanda akamtazama kijana huyo kwa macho ya kidadisi, “Unataka kusemaje?” akauliza.
“Yule mjinga hajafa! Kwa sababu nani awape ujumbe kama huu wenzake? Hamuoni kwamba kataka kujitambulisha kuwa yupo hapa, yaani mzima wa afya…” Fredy akasema.
“Katokaje mle ndani, mle hatoki mtu labda kama hana mwili,” Martin akamjibu.
“Hajafa, na yupo hapa, kwanza Battlomino ameuawa leo, vipi kama ni yeye kampa ramani ya tulipo,” Fredy akazidi kudadavu mambo.
“Tuondokeni!” Martin akazidi kusisitiza, akaichukua ile bunduki na kulitia lile ua katika kopo la takataka, “Tukapige kambi Etonto,” akasema akiwa tayari mkoba begani.
“Etonto?” Amanda akauliza.
“Ndiyo, Etonto… kesho tutakuja mjini kwa tukio moja tu, kuua au kunywa soda!” Gupter akamjibu na kutoka nje, dakika tano baadae wawili hao nao wakatoka na kuingia garini, wakaondoka zao na kuiacha nyumba hiyo kama walivyoikuta.
“Simwelewi huyu jamaa, kama ni yeye kweli, basi si mtu wa kawaida,” Fredy akasema huku akiendesha gari kwa kasi.
“Huyu ni shetani! Tena shetani asiye na mkia,” Amanda akajibu.
“Sasa awe shetani asiwe shetani, kesho nikimtia machoni tu, nitamuua kwa bunduki hii hii, mtoto wa kahaba yule!” Martin akaongea kwa hasira.
“Nimekumbuka!” Amanda akasema na kumpa ishara Fredy asimame, “Ni vipi kama hiyo bunduki imewekwa GPS na inmfanya adui atufuatilie kirahisi?” akasema. Martin akaitazama ile bunduki na kuigeuzageuza, akafungua mlango wa gari na kutoka nje, akaitupa kwenye vichaka na kurudi garini.
“Umeitupa?”
“Nimeificha!”
Fredy akarudisha gari barabarani na kuendelea na safari.
* * *
Chiba akaegesha gari jirani kabisa na kichaka kile kile ambacho Martin aliitupa ile bunduki muda mchache uliopita. Gina akashuka na kufuatiwa na Kamanda Amata, wakaingia kichakani na kuichukua ile bunduki kisha wakarudi garini.
“Wana bahati sana, wameshtukia njama,” Amata akasema.
“Kwa hiyo!!” Chiba akauliza.
“Turudi mjini, tukajipange upya, kesho lazima tuwatie nguvuni kabla hawajaleta madhara,” Amata akajibu huku gari likigeuzwa na kurudi mjini.
Baada ya kama nusu saa hivi, wakawasili mjini na Chiba aliendesha gari kwa mwendo wa wastani huku mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea.
“Chiba!” Amata akaita.
“Sema!” Chiba akaitikia.
“Nahisi tuna kampani nyuma yetu, nimeangalia kwa muda mrefu sana, kuna magari mawili yanatufuatilia, kila mmoja ajiweke tayari maana hatujui kama ni marafiki au maadui,” Amata akawaambia huku akiiweka bastola yake vyema, tayari kwa lolote litakalotokea, Amanda naye akafanya hivyo hivyo na kumkabidhi Chiba bastola huku yeye akiweka yake wake tayari.
“Tayari?” Chiba akauliza.
“Ndiyo, weka gari pembeni na asishuke mtu tuone!” amata akatoa maelekezo na Chiba akafuata. Akaegesha gari kando ya barabara. Amata alikuwa sahihi kabisa kwani mara baada ya kusimama, yale magari nayo yakasimama moja nyuma na jingine mbele huku wao wakiwa katikati. Vijana kama sita hivi wakateremka, kati yao, wawili wakasogelea gari walilokuwamo TSA na kugonga kioo cha mbele. Chiba akashusha kioo robo tu ili kusikiliza nini kitazungumzwa.
Wale mabwana wakatoa vitambulisho na kujitambulisha kuwa wametoka ofisi maalumu ya usalama ya AU. Chiba naye akato kitambulisho chake halisi kabisa cha TSA na kuwaonesha na Gina akafanya vivyo hivyo na Amata pia baada ya kushusha kioo mpaka chini.
“Tuna shida na Amata Ric, shida ya kikazi, tumepata taarifa kuwa yuko hapa na tumefurahi kwa kuwa tumemuona!” mmoja wao akasema. Gina na Chiba wakatazamana kisha wakamtazama Amata.
“Ngoja niwasikilize,” Amata akasema na wenzake wakamruhusu, akateremka garini na kuitia bastola yake katika kikoba chake, wakasimama pembeni kama mita nne hivi kutoka walipoegesha magari yao.
“TSA! Tumepata taarifa kuwa u hapa, na kwa sababu wewe ni mwanausalama kama sisi, mkurugenzi wetu wa idara ya AU anahitaji kukuona kwa mazungumzo ya kikazi,” mmoja wa wale vijana akamwambia Amata kwa kiingereza chenye lafudhi ya kihabeshi. Kamanda Amata akatulia kimya kama sekunde kumi hivi kisha akavuta hatua kurudi katika gari, akawaambia wenzake jambo hilo.
“No! tunaenda wote, sisi tutaamini vipi juu ya hilo? Vipi kama ni njama, je?” Gina akauliza.
“Mchezo wetu ni ule ule…” Amata akasema.
“Aaaakh! Ok, code gani?” Gina akauliza.
“300.1R” akamjibu na kuondoka. Wale vijana wakaongozana nae na kuingia kwenye gari lao kisha yote mawili yakaingia barabarani na kuondoka kwa kasi, si kwa mwendo waliokuja nao. Chiba naye akaingiza gari barabarani na kutokomea mjini, Gina akajiegemeza kitini huku mkono mmoja ukiwa umeegemezwa kwenye dirisha na kiganja kichwani.
“Code 300.1R” Gina akarudia kodi hiyo aliyopewa na Amata ambayo ni moja kati ya kodi nyingi wanazotumia kwa ajili ya kazi zao, ikiwa na manaa kwamba 300 ni masaa matatu kamili, .1 ni sekunde ya kwanza baada ya masaa hayo matatu na R ni Rescue, yaani ikifika masaa matatu bila taarifa yoyote kutoka kwa Amata basi sekunde ya kwanza ikigonga waanze mikakati ya kumuokoa, tayari atakuwa matatizoni.
* * *
Ndani ya gari lile, Amata aliketi kiti cha nyuma katikati kushoto na kulia kukiwa na wale vijana. Dereva amaye alificha macho yake kwa miwani ya giza japokuwa ni usiku alikuwa ametingwa na kazi yake wala hakujali jambo jingine lolote.
“Lini umefika Addis?” kijana wa upande wa kushoto akauliza.
“Miezi mitatu ilopita!” Amata akajibu.
“Miezi mitatu!?” yule jamaa akajiuliza na kushangaa.
“Ee, miezi mitatu…” akajibu na kubaki kimya. Lile gari likapenya mitaa kadhaa na kuibukia upande mwingine mji. Baada ya mwendo wa takribani dakika hamsini hivi wakaingia kwenye jingo moja kubwa na lile gari likateremka chini jingo hilo. Ndani tu ya jingo hilo, lile gari lilitembea kama dakika kumi na tano hivi na mwisho likaegeshwa sehemu fulani ambapo palikuwa kama stoo ka jinsi makorokoro yalivyozagaa huku na huko.
“Tumefika!” yule kijana akamwambia Amata.
“Mkurugenzi yuko wapi?” Amata akauliza.
“We teremka atakuja tu,” akajibiwa.
Kengele za hatari kichwani mwa Amata zikagonga, “Sishuki mpaka mkurugenzi afike maana ndiye anayenihitaji si ninyi,” akawajibu kijeuri.
“Asee, usitake tutumie njia za kisovieti…” kijana mwingine mwenye mwili mkubwa uliojaa nyama akasema huku akisogelea gari lile.
“Kwa hiyo si mkurugenzi anayenihitaji, mmeniteka sivyo, yaani wanausalama mnamteka mwanausalama! Haya tumieni njia mnayotaka kunishusha…” akajibu kijeuri huku akiwa bado kaketi kitini na mkanda ukiwa umezunguka kiunoni mwake. Yule bwana akasogea mpaka pale na kuwahi kuufyatua mkanda wa kiti, Amata akasogea pembeni na kumpa wakati mgumu jamaa yule, mara akaona mlango wa upande huo nao ukifunguliwa na mtu mwingine. Akafanya kama anatoka na yule bwana akampokea kwa konde moja zito tumboni, Amata akajikunja kwa maumivu na kurudi ndani ya gari. Jamaa aliyempiga ngumi akaingia mkono kumshika, Amata akakamkata mlango na kuubamiza kwa nguvu, akambana vidole na yule jamaa akapiga yowe la uchungu. Upande wa pili yule bonge alimdaka Amata na kumvuata nje, akambaga chini lakini Amata akawahi kusimama, kabla hajajiandaa akajikuta akipokea mapigo mazito kutoka kwa bonge huyo kisha na virungu kadhaa vikatua mwilini mwake na kumbakisha akiwa hoi sakafuni.
“Unajifanya mjanja kwenye ardhi ya watu!” yule bonge akamwambia Amata.
Haikupita hata dakika ishirini, Marcedec Benzi moja jeusi likaingia na kufuatiwa na Nissan Patrol short Chassis nalo jeusi pia, yakasimama na taa zake zikiwa full zikimmulika Amata usoni.
“Hah! Hah! Hah! Hah! Aaaaaah, umefufuka siyo?” sauti nzito ya mtu ambaye hakuweza kumwona vizuri ilisikika, “sikiliza kijana, hizi kazi si za kufanya kama ufanyavyo wewe, kukuepushia haya, ulishauawa wewe kule Waterloo, kwa nini hukutulia ufe?” akamuuliza. Kamanda Amata akainua uso wake kwa taabu kidogo na kumtazama huyo asemaye, hakumwona sura ila kitambulisho alichokuwa amekivaa kilimtambulisha kwa kusomeka MARILEKC FikrMARYAM. Jina tu tayari lilimpa habari kamili Amata, alilijua kwa sababu ni huyu ndiye aliyeteuliwa kuongoza kamati ya dharula ya usalama ya AU iliyokuwa na jukumu la kumsaka muuaji wa viongozi wa Afrika ambayo iliweka makao yake katika Jiji la Dar es salaam. Ni huyu, mtu wa ngazi ya juu sana katika idara ya usalama ya Umoja wan chi za Afrika, raia wa Elitrea mwenye unasaba wa karibu na Uethiopia.
“Marilekc FikrMaryam! Kumbe ni wewe… unyeihujumu Afrika na watu wake…” Amata akasema. Mzee huyo akahisi ganzi mwili mzima kwa maana jina lake daima huwa halitambuliki, akajipapasa kifuani na kukuta kitambulisho kikiwa kinaning’inia. Kwa sekunde chache, sura ikaonesha uzee mara mbili ya ule aliyokuwa nao. Marilekc akamtazama Amata pale chini na kujikuta mate yakimkauka, akameza funda kubwa na kusimama wima, kwa mkono wake wa kulia akakivua kile kitambulisho na kukitia mfukoni.
“Make him uncomfortable…” akawaamuru wale vijana nao wakaanza kumsulubu Kamanda kwa zamu. Walipiga kila mmoja kwa jinsi yake, aliyetumia mateke sawa, aliyechukua fimbo sawa, mwenye gongo twende. Dakika tano za kipigo zilimwacha Amata akiwa hoi pasi na kujitetea.
“Mwacheni!” akaamuru, na wale vijana wakamwacha na kusimama kando. Marilekc akachutama na kumtazama Amata, “unajua nini kuhusu muuaji wa viongozi wa Afrika?” akamuuliza.
“Ni-ni-ni-ttta-ju-a ni-ni, wa-ka-ti mi-mi si-hu-si-ki?” Amata akajibu kwa taabu kidogo.
“Wewe unajua, na hapa Addis umekuja kufanya nini?”
“Ni-me-ku-ja kumlinda –ra-i-s wa-ngu!” akajibu na kujinyoosha kidogo. Marilekc akawatazama vijana wake, akawaona wapo ngangari wakisubiri amri ya mkubwa wao, akarudisha macho kwa Amata.
“Nataka unipe tafutishi zote za sakata hili…” akamwambia.
“Sina!” Amata akajibu kwa neno moja tu.
“Huna!? Na zile ulizochukua Angola…”
“Anhaaa wewe ni mmoja wa-o,” Amata akasema, mara akajikuta akipokea teke moja zito usoni lililomtupia upande wa pili, damu zikamtiririka puani, akakohoa na kujaribu kujiinua, mara yule bonge akampiga teke jingine la tumboni na kumbwaga kando.
“Ni-ninyi ni wa-na-u-sssa-la-ma au ma-ja-mbazi?” akauliza.
Marilekc akasogea na kuchutama kwa mara nyingine, “Nakuuliza kwa mara ya tatu, zi wapi tafutishi za mpango huu wa mauaji ya viongozi?”
“Zipo Tanzania, wasiliana na Madam Sellina, atakupatia mpaka nilipoishia…” Amata akajibu, mara hii kwa ukakamavu kidogo.
“Sikiliza we bwege, mimi nina akili, mimi ni mwenyekiti wa kamati ya usalama, kukukamata na kukuweka hapa ni moja ya mbinu za kutaka kusaidia uchunguzi dhidi ya mauaji haya, najua wewe unajua, lakini tulipoiondoa idara yenu katika hili, tulimaanisha kuwa mnatakiwa kuwasilisha tafutishi zote mikononi mwetu…”
“…ndiyo maana mkamtengenezea ajali Madam Sellina, mlidhani mtamuua? Hajafa, hajafa, yupo hai na hivi tunavyoongea, usiku huu anatua Addis…”
“SHUT UP!!!! SON OF BITCH!” Malirekc akang’aka na kumrukia Amata, hapo ndipo alipofanya kosa ambalo alilijutia. Kamanda Amata akaviringika upande wa pili na kumshuhudia mtu mzima huyo akitua sakafuni kwenye makolokolo na uchafu, akachomoa bastola na kuifyatua, Amata akapiga sarakasi na risasi ile ikaingia moja kwa moja kwenye tenki la mafuta katika gari iliyoegeshwa jirani. Mlipuko mzito ukatokea, lile gari likabiringishwa hewani na kujipigiza juu kisha likarudi chini, mara gari lingine nalo likadaka moto.
“Ita fayaaaa!!!” kelele zikasikika, huku vijana wa Marilekc wakitawanyika kumsaka Amata asiwapotete.
“Hakikisheni hatoroki,” Malirekc akawaambia huku akijiondoa eneo lile na ving’ora vya polisi vikisikika nje.
Kamanda Amata baada ya kuruka sarakasi ile akaangukia upande wa pili lakini kutokana na maumivu aliyokuwa nayo akajikuta anashindwa hata kujisogeza. Akiwa katika kuhangaika akasikia bunduki zinazoondolewa usalama, akatulia tuli na kuweka mikono yake kisogoni huku akiwa kalala kifudifudi. Vijana wa Marilekc kutoka idara nyeti ya usalama ya AU wakamzunguka wakiwa na shot gun na wengine bastola.
“Arrest him!” (mkamateni) Malireck akatoa amri na Amata akatiwa pingu na kusombwa mpaka kwenye gari moja jeusi, akasukumiwa ndani na kufungiwa. Ving’ora vya magari ya polisi vikatulia na kubaki vimulimuli vikipendezesha eneo lile kwa taa zake za rangirangi na magari ya faya yalikwishawasili na kuanza kazi yao mara moja. Malireck akaonesha kitambulisho chake na kupigiwa saluti za heshima, kisha kwa ishara ya mkono akawaamuru vijana wake wamtoe Amata na kumkabidhi kwa wale polisi.
“Make naye huyu, asihojiwe na wala asichanganywe na mtuhumiwa yeyote, tutakuja wenyewe kumhoji, ni mmoja wa watu tunawatafuta kwa kuhatarisha usalama wa Afrika!,” akawaambia wale askari, nao wakamchukua na kumtia garini kisha wakaondoka naye kwenda kumhifadhi.
 
MAGNUM 22

Sehemu 21

ADDIS ABABA – ETHIOPIA
SIKU HII TOFAUTI NA SIKU nyingine zote, pambazuko lake lilikuwa na mikiki mikiki mingi, wapo ambao hata hawakujali nini kinatukia siku hiyo, wengine hawakupata hata lepe la usingizi kwa kile ambacho walijua kinaweza kutokea, na hawakupenda kitokee, hawa hawakuwa wengine zaidi ya wanausalama wa taifa hilo na nchi nyingine za Afrika.
Vikao vilivyofululiza kwenye taasisi mbali mbali vilikuwa vikizungumzia swala hili; kikao cha kamati kuu ya AU pamoja na usalama wa viongozi hao kufuatia mauaji yliyotokea Angola, Ivory Coast na kukoswakoswa kwa mwenyekiti wa umoja huo, rais wa Gambia alipokuwa katika moja ya vikao vidogo vya umoja huo jijini Dar es salaam. Katika moja ya agenda ambazo zingezungumziwa katika kikao hiki cha kamati kuu, ni pamoja na kulifikisha katika muafaka swala la kuimega Somalia na kuwa mataifa mawili kama ambavyo watu fulani walitaka, na kwa kushinikiza hilo waliamua kufanya mauaji ya viongozi wa umoja huo.
Katika kikao hiki, kulitegemewa ugeni mkubwa wa tajiri mkubwa Afrika Bwana Jaffer Bakhari, aliyekuwa akitajwa na kila chombo cha habari duniani kuwa ni chanzo cha machafuko huko Somalia na mauaji ya viongozi wa Afrika. Katika kikao hiki alitakiwa kufika kwani agenda mojawapo ilimhusu yeye na Somalia yake.
Katika moja ya majengo nyeti ya serikali Mtaa wa Eritrea, kikao cha baraza la usalama la AU kilikuwa kikimaliza mkutano wake alfajiri hiyo.
“Ulinzi utatakiwa uwe mkali sana kama tulivyoamua, na wapelelezi wetu wahakikishe wanaiweka Addis katikati. Hawa washenzi hawatakiwi kupenya sehemu yoyote ile kuingia ndani ya jiji hili kwa maana madhara yao tunayajua…” alizungumza mwenyekiti wa baraza hilo wakati akifunga kikao.
“Samahani mwenyekiti, kama sijasahau, mjumbe wa Tanzania alisema wao wataendelea na sakata la kumsaka huyu au hawa wauaji kwa sababu walifanya tukio hilo ndani ya ardhi yao, swali ni je, huoni kuwa kama watafika hapa watavuruga upelelezi wetu?”
“Yule bibi aikuumize kichwa, hana lolote si yeye wala idara yake, nashangaa sana kwa nini AU iliwaamini kiasi hicho, lakini sasa wameona, wameshindwa…”
“Mwenyekiti, mpaka sasa tunajua Tanzania na idara yake imefikia wapi katika uchunguzi huu? Si ajabu wakawa mbele kuliko sisi, mimi nafikiri tyumhusishe mpelelezi mmoja wan chi hiyo kutoka idara yao ya kijasusi ili aungane na hawa wetu, tukifanya hivi tutafaulu…”
“Hakuna kitu kama hicho mjumbe! Mpaka sasa ninavyokwambia, mpelelezi wao wanaomtegemea amekwishakufa lakini wamefanya siri, na amekufa katika sakata hili hili,” akajibu kwa kumkata kauli mjumbe huyo. Wajumbe wa kikao hicho wakatazamana na kubaki na alama za kushangaa na kujiuliza; moja kiongozi wao kajuaje kama mpelelezi wa Tanzania amekufa? Na kwa nini wao hawana ripoti kama hiyo? Kwa sababu wao walichokuwa wakijua tu ni kwamba, idara ya ujasusi ya Tanzania imeshindwa kufanya kazi kwa wakati na kuwasilisha taarifa kwa muda muafaka, basi. Kwa ukimya ule mwenyekiti wa baraza akagundua kuwa amekosea kwa kusema hivyo.
“Sawa sawa wajumbe, tutaliongea hili katika kikao chetu cha jioni na mtapta jibu kama Tanzania itahusika au la,” akajaribu kuliweka sawa jambo hilo.
Hawa nao wakamaliza kikao chao na kutawanyika kadiri ya majukumu yao.
Mpaka kufikia saa tatu asubuhi hakuna hata mwanausalama mmoja aliyegundua uwapo wa Martin Gupter na kundi lake katika jiji hilo. Ijapowa upekuzi wa kina kwa kila mgeni ulifanyika lakini haukuza matunda.
“Wameogopa kuja!” mmoja wa makachero akamwambia mwenzake.
“Wanajua wakija watajichimbia kaburi,” mwingine akaitikia. Tayari Addis Ababa ilikuwa na pilikapilika nyingi siku hiyo kwa kuwa ni saa chache tu zilizofuata mgeni wa kwanza angefika katika nchi hiyo, hivyo tayari vijana walipangwa, dori kwa kutumia magari na helikopta zilikuwa zikifanyika.
* * *
Kutoka Sierra Leone, Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lungi, Kamanda Amata alifanikiwa kuabiri ndege ya saa saba usiku ya sirika la AIATA. Wakati wa safari yote hiyo alikuwa akiwaza tu ni jinsi gani atamtia mkononi Martin na kundi lake. Alijuwa wazi kuwa kuna timu iliyoundwa kwa ajili ya upelelezi wa watu hao, lakini yeye aliamua kutokuwaacha, bali kuhakikisha anawatia mbaroni au anawapoteza kwa mkono wake.
Saa mbili kamili asubuhi, ndege hiyo akakanyaga ardhi ya Addis’ kwa madaha na kuingia katika egesho lake, kisha wageni wakaruhusiwa kuingia katika jiji hilo. Miongoni mwa wageni waliofika asubuhi hiyo alikuwamo Kamanda Amata, akiwa ndani ya jinzi mpauko, shati la drafti nyekundu na nyeusi na kichwani mwake kofia kubwa ya pama, miwani ya kumkinga dhidi ya miale mikali ya jua ilitulia vyema machoni pake aghalabu ndevu bandia zilimfanya afanane na cowboy mmoja hivi. Kifuani mwake alining’iniza kamera ya kisasa kabisa, kama ungemtazama usingefikiria zaidi bali ungejua tu kuwa ni mwandishi wa gazeti fulani la kimataifa. Kwa uzoefu wa kazi yake aliweza kuwana makachero wengi uwanjani hapo, lakini wao hawakuweza kumgundua kirahisi labda kwa sababu hawakuwa na mpango naye. Nusu saa baade alikuwa katika hoteli kubwa ya Blue Moon, katikati ya jiji hilo. Hakutaka makuu zaidi ya kutulia kimya chumbani kwake na kupanga hili na lile kwa maana alikuwa akijua wazi kuwa viongozi wanaotegemewa wataingia nchini hapo siku hiyo na mkutano huo utachukua nafasi siku inayofuata.
* * *
‘Hakikisheni mnawatia mbaroni, wao watatu na wengine wapo hapahapa tunaendelea kuwalinda, mambo yakiwa tiki tu tunawapiga pingu. Msiwe na wasiwasi na mimi, mimi naendelea poa kabisa na naweza nikatoka hospitali muda wowote kutoka sasa. Chiba na Gina mfike Addis haraka iwezekanavyo, nafikiri kaka yenu keshafika huko, nendeni mkafanye yale mnayopaswa kutenda.’
Chiba wa Chiba alikuwa akikumbuka maneno ya bosi wake, Madam S, mara walipokuwa wakiagana katika hospitali ya jeshi ya Lugalo. Mwanamama huyu hatari kabisa katika medani za kiusalama alilazwa hospitalini hapo siku tatu nyuma baada ya kupata ajali mbaya ya gari katika makutano ya Barabara ya Morogoro na Bibi Titi. Mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa Amata kuwa ‘wanawatafuta’ wapo Ethiopia, akaamua kuongeza kikosi katika jiji hilo, hivyo TSA 2 na TSA 5 waliingia kazini.
“Tumefika!” Chiba akamwambia Gina. Gina akatupa jicho dirishani na macho yake yakapendezeshwa na mandhari ya kuvutia ya Jiji la Addis Ababa.
“Ni mara yangu ya kwanza kufika hapa,” Gina akamwambia Chiba.
“Safi sana nitakupeleka ukale injera,” akamtania. Injera ni chakula cha kienyeji katika nchi hiyo kama ilivyo kwetu ugali. Mara sauti ya kike ikawataka kufunga mikanda nao wakafanya hivyo tayari kwa kutua. Akaitazama saa yake, ikamwambia kuwa tayari imetimu saa sita mchana. Wakiwa katika harakati hizo wakapata tangazo lingine la dharura ya kuwa watasalia angani kama dakika arobaini na tano hivi ili kupisha ndege za marais wa Gambia na Afrika Kusini kutua.
“Kumekucha!” Gina akasema.
“Kwa vipi?”
“Sipati picha rafiki zetu jinsi wanavyohaha sasa kwa mapokezi hayo,” akasema akimaanisha wanausalama wa nchi hiyo. Baada ya saa moja hivi ndege ile ikatua katika uwanja huo mkubwa kabisa wa Bole.
“Kazi ya kwanza!” Gina akamuuliza Chiba mara baada ya kutoka nje ya uwanja huo.
“Kuweka mipango yetu sawa, tunatakiwa kufika katika shamba la kanisa la Orthodox, mambo yetu yote yatakuwa huko,” Chiba akamwambia Gina, na wakiwa katika mazungumzo hayo, gari moja, Toyota Pickup likasimama umbali wa kurusha jiwe tu utoka wao waliposimama. Ndani ya gari hilo kulikuwa na mwanaume mmoja aliyevali kanzu jeusi na msalaba mkubwa kifuani mwake, akafungua mlango na kutoka nje. Alipowaona tu Gina na Chiba, akainama kama ishara ya kuwasalimu nao wakafanya hivyo hivyo, moja kwa moja wakajua kuwa huyo ni mwenyeji wao wakaongozana na kuingia garini.
“Karibuni Addis!” yule bwana akawakaribisha huku tayari akikamata barabara ya kuelekea nje ya mji, “Naitwa Archemedius, kutoka Orthodox Church,” akajitambulisha.
“Asante sana,” nao wakajibu na kujitambulisha kisha mazungumzo mengine yakafuatia ambayo zaidi yalikuwa na kufahamiana na kujuliana hali. Baada ya mwendo wa takribani saa moja na nusu hivi, waijikuta nje ya mji. Yule bwana akaiacha barabara kubwa na kuchukua ile ya vumbi yenye mashimo na machanganyiko wa mawe na udongo. Kilomita moja mbele wakaingia kwenye wigo wenye kanisa kubwa sana mbele yao, gari likatembea taratibu mpaka ndani ya kijumba kimojawapo. Wakateremka na kuchukua mikoba yao kisha wakamfuata yule mwenyeji wao. Wakapita kando ya kanisa hilo na kukutana na ukuta upande wa nyuma, wakauzunguka mpaka upande wa pili ambapo palikuwa na mlango mdogo wa chuma. Yule kasisi akabofya sehemu fulani ya ukuta na sekunde kumi tu zilizofuata kijimlango kile kikafunguka, wakaingia ndani.
Ulikuwa ni uwa mkubwa sana, wenye maua mengi ya kupendeza, kwa harakaharaka utavutiwa na ukimya wake, hapakuonekana mtu, bali vipepeo tu vilivyokuwa vinaruka huku na huko. Archimedius, akawafikisha kwenye moja ya milango mingi na kuufungua, wakaingia na kujikuta kwenye kijichumba kidogo. Chiba akatazama harakaharaka na kugundua kuwa ilikuwa ni lifti, ikawateremsha chini kama mita kumi na mbili hivi, wakatoka na kupita koridoni mpaka katika chumba kingine.
“Karibuni sana!” Archimedius akawakaribisha kwa mara ya pili wakiwa wanajibwaga kwenye makochi ya kisasa kabisa yenye vono ya kuvutia, “Jisikieni mpo nyumbani, Madam S ndiye aliyeuagiza tuwafikishe hapa na kuwapa sehemu ya kuratibu kazi zenu, hivyo mpo sehemu salama sana. Hii sehemu watu hawaijui na wala hawajawahi kufika, kama mnavyoona ni kanisa ambalo hutumika kila jumapili na huko juu kuna monastery kubwa ya kimisionari ya Orthodox ya Mtakatifu Ilarius,” akawaeleza.
“Hapa tulipokaa kuna vyumba vitatu, hili siyo jokofu ni mlango wa chumba, ukibonyeza namba 0-7-7-3, utaingia chumbani,” akachukua rimoti mezani na kubofya namba hizo, kweli, ule mlango ukafunguka na ndani yake kulikuwa na kitanda kikubwa, meza ya kujiremba, na kabati moja la nguo, kiti kimoja na meza ya kusomea.
“Lakini ukikose na kubonya namba nyingine yoyote ile, utafungua jokofu na si chumba,” akafunga ule mlango na kubofya tarakimu nyingine hapo ukafunguka mlango ule ule lakini mara hii vilionekana vinywaji na matunda na vyakula anuai.
“Du! Hii nimeikubali!” Gina akajikuta anamwambia Chiba, naye akatikisa kichwa kuonesha hiyo ni ‘kali ya mwaka’. Yule kijana akawatazama Gina na Chiba na kuendelea kuwapa maelekezo, “Na chumba kingine ni upande huu, hilo hapo si kabati la vyombo, ni chumba na namba yake ni 7-3-2-0, kama mwanzo, ukikosea utakutana na mabakuli na vijiko. Na cha tatu ni hiki huku kwenye shelfu la vitabu namba yake ni 6-7-0-5. Kwa hiyo mkariri hizo namba, mambo yenu yote mtayafanyia hapa ndani, hakuna atakayewasumbua hata mimi tukiachana hapa hamtaniona tena, baada ya hapa njooni niwaoneshe jambo la mwisho,” akawachukua na kutoka nao kwenye ile korido, wakaifuata na kuingia kwenye lango kubwa, huko kulikuwa na eneo wazi kubwa lililoegeshwa magari mengi sana katika mpangilio wa kupendeza.
“Hapa ni maegesho, mkitaka kwenda mjini, mtachukua gari hapa mnayoipenda, funguo zipo ndani na ukifuata hiyo mishale itakutoa nje ya mpaka mjini, nimemaliza!” Archimedeus akamaliza kuwapa maelekezo na kurudi nao ndani.
“Samahani nilisahau jambo, mkimpata mwenzenu, mtamleta hapa, kazi yenu haitakiwi kupangwa nje ya chumba hiki, kwa maelekezo niliyopewa,” akamaliza na kupeana nao mikono kisha wakaachana. Gina na Chiba wakarudi ndani ya kile chumba na kuufunga mlango, kila mmoja akajaribu rimoti kufungua chumba chake na kuingia. Kila chumba kilikamilika, choo, bafu ndani na jiko dogo la kahawa au chai lilikuwepo.
Chiba akarudi sebuleni na kuwasha luninga kubwa iliyowekwa ukutani, macho yake yakakutana na matangazo ya moja kwa moja kutoka kituo cha televisheni cha EBC. Hakikuwa kingine ni mapokezi ya marais waliokuwa wakimiminika katika jiji hilo.
* * *
Hoteli ya BLUE MOON
Kamanda Amata bado alikuwa ametulia kimya katika chumba chake hicho, huku mezani kukiwa na chupa kubwa ya pombe aina ya Covousier ikiishia tumboni mwake taratibu, makwapani mwake alikuwa amening’iniza bastola mbili, mja upande huu na nyingine upande mwingine. Kwa ujumla alikuwa tayari kwa kazi lakini bado akili yake haikuwa katika umoja mzuri na mwili wake. Katika meza hiyo hiyo, alikuwa ameweka kijitabu kidogo cha kumbukumbu, si chake bali kile alichokichukua kwa marehemu Innocent na karatasi nyingine ile aliyoichukua kule Waterloo ndani ya jumba ‘Silent Rock Villa’. Ukiachana na mkono ulioshika bilauri iliyojaa pombe nusu, alikuwa amekamata simu upande mwingine akibofya namba ambazo amezikuta zimeandikwa ndani ya karatasi ile. Katika hisia zake, kwa vyovyote, alijuwa wazi kuwa wenye namba hizo watakuwa na uhusiano na Gupter na kundi lake ama wa kikazi au wa kidugu.
Nitajitambulishaje? Akajiuliza mara baada ya kuiweka simu sikioni na kusikia ikiita upande wa pili. Simu yake hii ilikuwa ni ile ambayo ni vigumu sana kuitambua uelekeo ilipo.
“Hello!” upande wa pili ikaitikia.
“Bole International Airport, reception, habari za kazi!” Amata akajikuta akitamka kuwa simu hiyo inatoka katika meza ya mapokezi ya Uwanja wa ndege wa Bole.
“Kuna mtu hapa ni mgeni wako ametupatia namba hii ili uje umpokee, amefika takribani saa tatu zilizopita, tafadhali fika mapokezi umchukue!” Amata akasema huku ahajui nini atafanya kama aliyempigia simu atakubali wito huo.
“Ok, got’ya!” upande wa pili ukajibu na simu ikakatika.
“Bingo!” Amata akajikuta anasema kwa sauti, akainuka na kujitupia koti lake ili kuficha ile ‘miguu ya kuku’, akainuka na kuitia ile simu mfukoni, akachukua vitu kadhaa ikiwemo kile kijitabu cha kumbukumbu ambacho hakukiacha hata nukta moja tangu akipate kwa maana hakuwa amemaliza kazi yake. Akafungua mlango na kutoka nje, akashuka chini kabisa ya hotei hiyo na kuzielekea taksi, moja wapo ya hizo ikamchukua na kumkimbiza uwanja wa ndege.
* * *
Katika kitongoji cha Aleltu, nje ya jiji la Addis kilomita takribani hamsini na tatu kutoka mjini kati, ndiko Martin Gupter na kundi lake waliweka makazi ya muda ambayo kwa mipango yao, hayo yalikuwa makazi ya saa tisini na sita tu. Mwendo wa nusu saa tu ungeweza kufika katikati ya jiji hilo kama ungeendesha gari kwa mwendo kasi wa kilomita 100 kwa saa.
Martin Gupter aliteremsha kikombe chake cha kahawa huku macho yake yakiwa kwenye dirisha kubwa yakisanifu mandhari ya nje ya nyumba hiyo. Nyumba hiy, Amanda alikuwa ameikodi kwa juma moja tu kwa ajili ya kufanyia kazi yao, alikwishaihakikishia usalama, kwa kuwa ni mara nyingi wageni wan je huitumia kwa kuikodi kama wao. Ikiwa ni moja ya mbinu za kujificha kwa kivuli cha watalii ndani ya jiji hilo maarufu kabisa Afrika. Kwa mbali katika barabara ya vumbi aliliona gari likija kasi upande huo, akachukua darubini yake na kutazama. Ni gari ambalo haikumchukua muda kulijua.
“Amanda amefika!” akamwambia Fredy, kisha wakatoka nje kumlaki, dakika moja baadae wote wakawa tayari wameketi kuizunguka meza moja ya duara sebuleni hapo.
“Tupe habari za mjini!” Martin akaanzisha mazungumzo.
“Huko ni moto asee, kama nilivyowaambia jana, wageni wetu wameshaanza kufika, na wote tayari ninajua wapi wanafikia, isitoshe hata wana uinzi kiasi gani…”
“Wanapenyeka?” Fredy akadakiza swali.
“Itabidi wapenyeke, hakuna jinsi,” Amanda akasisitiza huku akijimiminia kahawa, na alipomaliza na kupiga funda moja akakitua kile kikombe.
“Mmepata taarifa yoyote kutoka kwa mteja wetu?” Amanda akatupa swali maana anajua kuwa taarifa nyeti za kazi huwa zinafika moja kwa moja kwa Martin na si mtu mwingine yeyote.
“Yes! Ujumbe wote utafika jioni ya leo, utakuwa na watu sita akiwamo Fadick Al Habib, na ndiye kiongozi wa msafara, mzee mwenyewe hawezi kufika wala wenzake. Maagizo ni yale yale, mkutano wa AU na hawa jamaa utakuwa saa tisa alasiri jioni, wakikubaliana basi kazi imekwisha, wasipokubaliana tunatakiwa tuendelee na operesheni yetu. Sasa endapo itatubidi tuendelee na operesheni, ndiyo tupange sasa…!” Martin akawaeleza.
“Sawa, baada ya kikao cha kesho, usiku kutakuwa na tafrija katika hoteli ya kifahari ya Golden Tulip, na hawa wageni wote watakuwepo,” Amanda akatoa maelekezo.
“Nimekuelewa, sasa baada ya kazi ya kesho sote tunatakiwa tukutane na Jaffer kule Riyadh kwa bakshisi za mwisho…” Martin akawaambia na kila mmoja akatabasamu.
“Sasa nafikiri ni muda muafaka kutoka, cha muhimu ni kujiweka sawa, tusitambulike, tukaikague hoteli hiyo, na ile atakayofikia mwenyekiti wao kisha tutazame na mengine ii siku ya kesho tuwe tayari,” Martin akamaliza kwa kuwaambia hilo na kila mmoja akaanza kujiandaa kwa jinsi anavyojua yeye ili mradi tu wakiwa huko mjini basi wasigundulike kirahisi.
* * *
Uwanja wa ndege wa BOLE
Kamanda Amata akawasili katika uwanja huo, akaiacha ile taksi baada ya kumaliza kulipia huduma hiyo, akavuta hatua na kuyapita maegesho mpaka kwenye sakafu ya uwanja huo. Macho yake yalikuwa yakipepesa harakaharaka na kutazama huku na huko, ni hapo ndipo ailipokutana macho kwa macho na mtu asiyemtaraji; kijana jamali, mweusi wa wastani mwenye tambo haswa la kipiganaji ambalo lilifichwa na nguo nadhifu, suti ya kisasa ambayo isingeweza kumpa wasiwasi mtu yeyote amtazamaye.
Drunken Hamidou, mpelelezi kutoka jumuia ya ECOWAS, akamsalimu kwa macho pasi na kumkaribia kwa maana alijua kwa nini mtu huyo yuko hapo. Almwona wazi kuwa kijana huyo alitamani kumkaribia na kumsalimia, kwa jinsi alivyopigwa na mshangao lakini Amata hakuruhusu hilo kwani yeye alikuwa na kazi yake binafsi. Akamwacha na kukaribia meza ya mapokezi ambako kwa ndani kulikuwa na watu wawili na nje kulikuwa na mtu mwingine ambaye kulionekana kama kuna mabishano kati yao. Akili ya Amata ikafanya kazi haraka na kujua kwa vyovyote alichokitaraji ndicho kinatokea. Naye akawasili palepale mezani na kujifanya akiongea na mhudumu mwingine kuuliza maswali ambayo hayana jibu la kiurahisi. Huku akisikiliza mazungumzo ya watu wale wawili wakibishana, huyu wan je akisema kuwa amepigiwa simu na amekuja kumfata mgeni wake, na huyu wandani akipinga kuwa hawajapiga kwa mtu yeyote kuhusu huo ugeni. Mwishowe yule kijana mwenye asili ya Uzungu uliyochakaa akaondoka akitukana matusi. Kamanda Amata akamalizana haraka na mhudumu huyo na kuondoka, lengo lake halikuwa jingine zaidi ya kumfuatilia mtu huyo. Akamtazama akielekea katika maegesho, huku akiongea kwa simu yake na kusimama nje ya Range Rover moja ya gharama sana. Kamanda Amata akajifanya kama anafunga kamba ya kiatu chake ili kumpa nafasi kijana huyo kumaliza mazungumzo yake.
Kijana yule hakuwa na hili wala lile, aliposhusha simu yake, na kuitia mfukoni, akageuka kukamata mlango wa gari ndipo akajikuta ana kwa ana na domo la bastola, mtu aliyekamata mashine hiyo hakuwahi kumwona hata siku moja tangu azaliwe.
“Uphhhhhhh!!!!!” akashusha pumzi na kijasho chembamba kikaanza kumtiririka.
“Ingia!” Amata akamwambia kwa kiingereza.
“Wewe ni nani…?”
“…Get in!!” akamwambia tena huku tayari akiwa keshaondoa kilinda usalama cha bastola hiyo. Yule kijana akafungua mlango na kuingia na Amata akaingia mlango wa nyuma yake na kuketi, mara hii akamwekea mtutu wa bastola kwenye mbavu zake upande wa nyuma.
“Drive!” akamwamuru.
“Tunaenda wapi?” yule kijana akauliza.
“Nyumbani kwako!” akamjibu.
“Nyumbani kwangu?” akauliza, “Mi sina nyumba, kama unataka gari chukua!!!” yule kijana akaongea kwa kitetemeshi huku akimpa funguo Amata.
“HEYYYY!!!!” Amata akang’aka, na yule bwana akabaki kimya kabisa.
“Bosi wako ni nani?” akamtupia swali.
“Mr. Bbaattolloommiinno!!” akajibu huku akitetemeka.
“Nina shida na yeye, nipeleke!” akamwamuru.
“Ssaawwaa!!” akajibu na kuwasha gari, Amata akatulia kimya akimwangalia kijana huyo akiendesha kwenye barabara za Addis kuelekea huko atakako. Kijana yule ambaye kwa kumwangalia na kumsikia lafudhi yake tu ungejua kuwa ni Mtaliano aliendesha gari kwa takribani dakika kumi hivi na kuufikia Mtaa wa Lorenzo Tiezaz, hapo akaachana na barabara ya kwanza na kuingia kwenye mtaa huo mpaka katika jumba moja kubwa lenye wigo mkubwa sana wa michongoma.
“Ni hapa!” yule kijana akamwambia Amata.
“Sikiliza, mimi ndiye mgeni wake ambaye ulitakiwa kunifikisha kwake, na nimefika uwanja wa ndege kwa saa nyingi sana, sasa nipeleke nionane naye,” akamwambia na dakika hiyo hiyo lango likafunguka na lile gari likapotelea ndani ya kasri hilo. Mbele ya jumba hilo, alisimama mwanadada mrembo wa kizungu, akisubiri gari hilo kuegeshwa.
“Umefika, na huyo mwanadada atakufikisha kwa Bwana Mkubwa!” yule kijana akamwambia Amata.
“Asante, unisubiri hapa ili unirudishe, sawa?”
“Sawa!”
Amata akashuka na kupeana mikono na yule mwanadada, kisha akaongozwa ndani ya jumba hilo mpaka kwenye chumba kimoja cha gharama sana, akaingia na kukaribishwa na mzee wa makamo, mnene, aiyejaa kwenye kiti alichokikalia.
“Karibu sana!” akakaribishwa huku yule mwanadada akimimina kinywaji kikali bilaurini.
“Asante sana! Nimeshakaribia,” Amata akajibu na kujituliza kitini.
“Nimepata simu kuwa wewe ni mgeni wangu,na mimi sikutegemea ugeni siku ya leo,” yule bwana akamwambia Amata.
“Ndiyo, na mimi ndiye niliyepiga simu, si kweli kwamba ilipigwa kutoka uwanja wandege,” akamwambia.
Maneno hayo yakamfanya yule bwana ashtuke kidogo, maana hakuelewa imekuwaje hata mgeni huyu apige simu na kufika mahala hapo. Akamtazama mzungu yule, Mtaliano mwenye nywele nyeupe zilizomwagika mabegani kama za Sir Newton Isaac.
Hawa ndiyo mabaki ya Wataliano walioua ndugu zetu Waethiopia miaka ileee! Amata akawaza, akijaribu kuirudia historia ya watu hao walipoingia katika nchi hiyo na kufanya mauaji mabaya kabisa ya ‘weusi’ zaidi ya elfu ishirini au thelathini.
“Enhe, nipe ujumbe wangu kijana maana huwa sina muda mrefu wa kuzungumza na watu hasa wasio na miadi kama wewe!” akaongea kwa dharau huku akiweka mtemba wake kinywani na kupiga pafu kama tatu hivi na kuruhusu moshi mzito ukijaze chumba hicho kupitia tundu za pua yake kubwa.
“Tunaweza kubaki wawili?” Amata akamuuliza.
“Bila shaka!” akajibu na kumwamuru mwanadada yule atoke, naye akafanya hivyo.
Kamanda Amata hakuzungumza, akachomo picha tatu mfukoni mwake na kumwekea mezani. Yule mzee akazitazama kwa makini, kana kwamba kajua ni nini ambacho mgeni wake huyo atasema. Akachukua tena mtemba wake na kuuweka kinywani, akapiga pafu kadhaa na kuushusha kisha akakung’uta jivu kwenye kibweta chake. Kwa mkono mwingine akaichukua picha ya mwanamke, Amanda, akaiweka kando.
“Namjua huyu!” akamwambia Amata. Moyo wa Amata ukapiga samasoti, akahema kwa nguvu, “Vipi una shida naye?” yule bwana akauliza na kumgutua Amata kwenye lindi la mawazo.
“Unamjuaje? Ninamhitaji kwa hali na mali,”
“Huyu ni mteja wangu, nimemwona si mara nyingi, bali alikuja hapa kukodi nyumba ya kuishi kwa muda wa wiki moja hivi…”
“Una nyumba za kukodi?”
“Si! Si! Nyingi sana, nimezijenga mashambanai huko,” akaeleza.
“Nahitaji kukutana naye, nipe maelekezo,” Amata akamwambia.
“No! siwezi kukupa maelezo yoyote ya mteja wangu, ni kinyume na baishara hii,” Balomino akajibu.
“Utanipa au hutonipa?” Amata akamuuliza.
“Nikupe wewe kama nani?” yule Mtaliano akauliza huku akijiweka vyema kitini, Amata akaigundua hila yake, kwa wepesi sana akainuka pale alipo na kumbana yule mzee kitini, kisha akachomo bastola kutoka kiunoni mwake, akarudi na kujibwaga katika kiti chake huku akiwa kamnyoshea mtaliano huyo domo la Berreta 87, bastola ya kizamani ya miaka ya ’76 huko Italia na wengine huuita ‘Series 81’.
“Niambiye hiyo nyumba ipo wapi?” akamuuliza, yule bwana kijasho kilikuwa kikimwagika.
“Aleltu!” akajibu na mara mguu wake ukakanyaga kitufe fulani chini ya meza. Amata akajua mambo yashaharibika, sekunde yoyote wangemvamia hapo, akatazama huku na huku.
“Hah! Hah! Hah! Hah! Aaaaaa!” yule tajiri akacheka cheko baya sana lililomuuzi Amata, akageuka na pigo moja zito akamzimisha kisha akafungua mlango, alipotaka tu kutoka akakutana na watu kama wane hivi wanakuja wakikimbia na bunduki mikononi. Akageuka na kurudi kwenye dirisha kubwa, huku mlangoni akiwa kasukumia kochi kubwa, akatazama huku na huko na kulifungua dirisha lile, akatoka na kutua nje.
Kumwacha hai si jambo zuri ataniharibia kazi! Akawaza na kuchukua ile bastola mkononi, akafyatua risasi moja iliyotua moyoni na kummaliza. Akaambaa ambaa na ukuta mpaka dirisha la tatu hivi, akalikuta lipo wazi, akachungulia ndani akamkuta mwanamke mmoja akiendelea na kazi kwenye kompyuta, akalikamata na kuingia ndani akatua bila kusikika. Akauendea mlango, na hapo ndipo yule mwanamke alipogundua kuwa hayupo peke yake, akapiga kelele lakini Amata akamuwahi na kumbana kinywa.
“Nipe ramani ya kufika Aleltu, kwenye nyumba za bosi wako,” akamwambia na kumwachia. Yule mwanamke akapekua na kumpa kitabu kimoja kikubwa tu lakini kinachoweza kuingia katika mfuko wa ndani wa koti lake.
“Nisindikize mpaka nje ya jingo,” akamwambia, na yule mwanamke akafanya hivyo, wakapita pamoja kwenye korido kana kwamba ni moja ya wateja wa tajiri huyo. Alipofika nje, akaagana na mwanamke huyo na kuingia kwenye gari lile lile lakini mara hii halikuwa na dereva ila funguo ilikuwa ikining’inia. Kamanda Amata, akaingia ndani na kutia injini moto, mashine ikaunguruma, akatingiza gia ya kwanza na kuondoka kwa fujo. Katika lango la kutokea nje mlinzi alizuia gari hilo lisitoke lakini mwenyewe hakuwa na budi kutoka barabarani baada ya kuona hakuna dalili za kusimama. Amata akagonga geti na gari lile likaharibika vibaya huku likiacha lango wazi. Akaendelea kuendesha kwa mwendo wa kasi mpaka sehemu alipoona panafaa, akasimama na kuteremka, akaliacha gari hilo na kuingia kwenye kichaka cha miti, akapotelea zake kwa mwendo wa miguu.
* * *
Chiba alikuwa mezani kimya huku kompyuta yake ikiendelea na kazi ya kutafuta mambo mbalimbali ikiwemo kuingia katika mitandao mbalimbali, lakini licha ya yote hayo alikuwa akijaribu kumtafuta Kamanda Amata kama anaweza kupata ishara yoyote. Wakati huo Gina hakuwepo humo ndani, yeye alijitoma mitaani kutafuta hili na lile ili baadaye wakijumuisha tafutishi zao waweze kupata kipi ni kipi. Chiba na Gina hawakuwa na muda mrefu wa kujua nini cha kufanya, kazi kubwa kwao ilikuwa ni kutegua kitendawili cha kama Martin Gupter na kundi lake wapo ndani ya Addis au la. Mpaka dakika hiyo kila ambako mashushushu wan chi hiyo walikuwa wametega kuwanasa, hawakuwaona.
“Sidhani kama wamefika” – labda ni maneno ambayo wanausalama wengi ambao wamejawa uvivu wa kiupelelezi. Sifa ya kuwa mpelelezi hasa kwenye kiwango cha espionage, lazima uwe na milango sita ya fahamu yaani umzidi mwanadamu wa kawaida. Wakati wao wanafuata wanayoambiwa na wakubwa wao tayari TSA walikuwa Addis na Kamanda Amata yupo hatua mbili mbele kuwatia mkononi washenzi hao.
Simu ya Gina ikaita, akainyakua kutoka kwenye mkoba wake, akaitazama kwenye kioo, kisha akasonga kando pasipo na watu na kuiweka sikioni.
“Uelekeo wapi?” sauti ya Chiba ikasikika kutoka upande wa pili.
“Katikati ya Mtaa wa Mauritius!”
“Kuna lolote?” akauliza.
“Upande huu hamna jipya, nimejaribu pia kupita HQ ya AU nako bado inaonekana hakuna jibu jipya, baadhi ya watu wanaofananishwa na Gupter wamewekwa tunduni, kiujumla hali ni tete,” Gina akaeleza.
“Vipi upande wako?” akamtupia swali.
“Huku habari ni nzuri, nimepata uelekeo wa Kamanda Ama….”
“Yeeeessss nambie yuko wapi?” Gina akamkatisha Chiba kwa furaha.
“Namuona karibu na Mtaa wa D.A.R Sahara, akielekea katikati ya mji,” Chiba akamuelekeza Gina, naye akawasha kifaa chake mfano wa simu ya mkononi na kuiweka juu ya kioo ramani ya Addis Ababa, akautafuta mtaa mtaa huo na kuupata kisha akatafuta barabara ya kufika kutoka pale alipo, akapata umbali ni k.m 9. Akaingia garini na kuwasha, kisha akingiza gari barabarani na kuufuata Mtaa wa Mauritius, akauacha ule wa Tanzania na kukunja kuchukua Barabara ya Ethio China.
Kwenye kompyuta ya Chiba aliweza kuwaona wote wawili na alijaribu kumuelekeza Gina jinsi ya kumkuta Amata, lakini baadae akashangaa kuona Gina amesimama mahali kwa muda mrefu sana. Akampigia simu na kujibiwa kuwa alikuwa amekamatwa na askari wa Barabarani kwa kuwa aliingia barabara kuu kimakosa. Chiba alijikuta akishikwa na hasira kwa kuwa muda ulikuwa ukipotea. Baada kama ya dakika thelathini hivi simu yake ikaita, akaipokea na kuzungumza machache na Gina.
“Sasa nenda hoteli ya Blue Moon ameingia hapo! Nafikiri ndipo alipofikia, ukimpata hakikisha unamhamishia huku,” Chibna akampa maelekezo Gina.
“Copy!” Gina akajibu na kukata simu.
Asanteh mkuu
Ila ukituongezea kwa leo hii dozi itapendeza zaidi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom